Mzee Samwel Mapunda akimpongeza Mgeni Rasmi Juma Nyumayo mara baada ya kumaliza kuwahutubia katika sherehe za mahafali katika shule ya Msingi Mkombozi na kuwapatia msaada wa mifuko kumi ya Saruji(Cement) na wazazi kuahidi kubebelea mchanga kwa ajili ya kusakafia darasa la Awali shuleni hapo
Kushoto Padre Chinguku akiwaonyesha,Gideon Mwakanosya,Mwandishi Mkongwe wa Magazeti ya Nipashe na guardian na Mjumbe wa Bodi ya Swacco(katikati)kulia ni mzee Samwel Mapunda namna watoto walivyopendeza katika mahafali hiyo
Kulia ni Gideon Mwakanosya akisalimiana na Mjapani ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja kutokana na pilikapilika za kufanikisha mahafali hiyo,pembeni ni wanafunzi wakiwa na hamu ya kuendelea kusherehekea mahafali hayo
Viongozi mbalimbali wakiwa na Mgeni Rasmi Nyumayo katika darasa linalodaiwa kuwa ni la Awali ambalo halijasakafiwa na mgeni Rasmi kutoa mifuko kumi ya Saruji na wazazi kuahidi kutoa mchanga wa kusakafia darasa hilo kwa lengo la kutaka watoto wao wakombolewe na elimu itolewayo Shuleni hapo
Watoto wakitafakari kwa umakini hatima ya elimu yao mara baada ya kupewa Saruji na mchanga utakaotumika kuondoa vumbi katika darasa lao
Watoto wakitamani kucheza kiduku kutokana na furaha kubwa waliyonayo baada ya kusikia kuwa darasa lao litakuwa katika hali stahiki kwa kuendelea kupatiwa elimu kusudiwa
Viongozi wa Serikali ya Kata ya Bombambili wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mgeni rasmi nje ya darasa la Awali ambalo linatarajiwa kukarabatiwa hivi punde
Wa kwanza kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mkombozi Imelda Mbawala akiwa kwenye picha ya pamoja na Mgeni Rasmi na familia ya Kazimguru
Sherehe ikifunguliwa kwa mbwembwe zote kwenye ukumbi wa Chama cha Walimu Mkoa wa Ruvuma,ikiongozwa na Mgeni Rasmi Nyumayo,kushoto ni Diwani wa kata ya Bombambili Kenny Moto akisaidiwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Mjimwema Twalik Mpakasini wa kwanza kushoto
Mwalimu Mstaafu Agnes Nkoma aliyeanza kazi mwaka 1972 na kustaafu utumishi wa UMMA,mei mwaka huu 2011 akipokea zawadi ya utumishi uliotukuka kutoka kwa Mgeni Rasmi Nyumayo katika Mahafali ya Shule ya Mkombozi ambapo amestaafu akiwa Mwalimu Mkuu katika Shule hiyo
Mwalimu Bibi(Notbuluga Mapunda)akimshukuru kwa utumishi wake Mwalimu Agnes Nkoma na kumtakia maisha mema ya kustaafu utumishi wa UMMA
Sherehe yoyote duniani haiwezi kufanikiwa bila kuwepo mziki au burudani,sasa kazi ipo Dj MKongwe ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Bombambili akionyesha umahiri wake wa kusugua Cd na kuchezesha pini za uhakika kwa wazee na vijana(Masharobaro)
Wahitimu wa darasa la Saba katika Shule ya Msingi Mkombozi wakimng'ang'ania Mgeni Rasmi Nyumayo kucheza muziki wa kisasa bila kufahamu kuwa mwenzao alikuwa kijana wa zamani na sasa akitaka kutikisa kichwa na kisigino chini lazima achezewe nyimbo za zamani kama vile Ottu Jazz Band,Sikinde na zingine za aina hiyo bila kusahau TWISTI
Hapo sasa Mgeni Rasmi akiwa na Wazee wenzake akisakata rumba katika mahafali ya aina yake huku akitamani kuvua koti la suti ili aweze kumudu vizuri rumba hilo
Ukosikia kipindi maalumu ndio hicho cha kuongeza vocha ya tumbo ili uweze kupata nguvu za kufanya jambo na uwezo kamilifu wa kufikiri,kwa kweli sherehe hiyo ilikuwa ni ya aina yake kufanyika mjini hapa,tuwashukuru wote waliowezesha mtandao huu wa http://www.stephanomango.blogspot.com/ kufika shuleni hapo na ukumbi ili kuweza kuwaletea wasomaji na wadau wa mtandao huo taarifa na burudani
Saturday, September 3, 2011
Mzee Samwel Mapunda na Mkewe Mwalimu Notbuluga Mapunda(Mwalimu Bibi) hawakubaki nyuma katika Mahafali hayo kwa kumsindikiza mjukuu wao Dickson Mapunda kushikana mkono na Mgeni Rasmi Nyumayo na kupokea uthibitisho wa kuhitimu elimu ya Msingi darasa la Saba mwaka huu 2011
Hapa sasa ni kucheza Kiduku kwenda mbele kwa wahitimu wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Mkombozi ikiwa ni furaha ya kuhitimu na kukabidhiwa cheti na Mgeni Rasmi Nyumayo kwa kudumu katika darasa la kwanza hadi la saba mwaka huu
Usiposhuhudia Mahafali haya unaweza kujilaumu kwa kukosa raha na maneno ya busara na hekima kutoka kwa Mgeni rasmi Nyumayo na hapa ni watoto ambao urefu wake ni wa mashaka wakiwa wanatafuta uwezo wa kuona kinachoendelea
Wageni waalikwa,walimu na wanafunzi wakiwa wanafuatilia mahafali hayo kwa umakini mkubwa
Mgeni Rasmi Juma Nyumayo ambaye ni Mwanaharakati wa masuala ya haki za binadamu akimpa msaada wa fedha ya kununulia Uniformu Mwanafunzi wa darasa la tano Agnes Magagura baada ya kusikia kuwa anashindwa kuendelea na Shule kwa kukosa Uniformu na kuguswa kutoa msaada huo
Mwalimu Mkuu Mstaafu wa Shule ya Mkombozi Agnes Nkoma akishangiliwa na Wanafunzi wake alipokuwa anawaaga na kwenda kuanza maisha mapya ya URAIANI kwa kuwa amestaafu utumishi wa Umma
Hapa sasa ni kucheza Kiduku kwenda mbele kwa wahitimu wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Mkombozi ikiwa ni furaha ya kuhitimu na kukabidhiwa cheti na Mgeni Rasmi Nyumayo kwa kudumu katika darasa la kwanza hadi la saba mwaka huu
Usiposhuhudia Mahafali haya unaweza kujilaumu kwa kukosa raha na maneno ya busara na hekima kutoka kwa Mgeni rasmi Nyumayo na hapa ni watoto ambao urefu wake ni wa mashaka wakiwa wanatafuta uwezo wa kuona kinachoendelea
Wageni waalikwa,walimu na wanafunzi wakiwa wanafuatilia mahafali hayo kwa umakini mkubwa
Mgeni Rasmi Juma Nyumayo ambaye ni Mwanaharakati wa masuala ya haki za binadamu akimpa msaada wa fedha ya kununulia Uniformu Mwanafunzi wa darasa la tano Agnes Magagura baada ya kusikia kuwa anashindwa kuendelea na Shule kwa kukosa Uniformu na kuguswa kutoa msaada huo
Mwalimu Mkuu Mstaafu wa Shule ya Mkombozi Agnes Nkoma akishangiliwa na Wanafunzi wake alipokuwa anawaaga na kwenda kuanza maisha mapya ya URAIANI kwa kuwa amestaafu utumishi wa Umma
Padre Chinguku ambaye ni Mlezi wa Kituo cha Kulea Watoto Waishio katika Mazingira Magumu SWACCO akiendesha maombi kabla ya Mgeni Rasmi ajaanza kuhutubia Wazazi,Wageni Waalikwa,Wanafunzi na Walimu wa Shule ya Msingi Mkombozi wakati wa Mahafali ya Darasa la Saba katika Shule hiyo
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya kwanza ya darasa la saba toka Shule hiyo ianzishwe ,Mhariri Msaidi wa Magazeti ya Elimu na Tujifunze kanda ya Kusini Juma Nyumayo,ambaye alimwakilisha Mhariri Mkuu wa Magazeti hayo Christiani Sikapundwa akiwasalimu wanafunzi na wageni waalikwa kabla hajaanza kuwahutubia,Kushoto ni Diwani wa Kata ya Bombambili kupitia Chadema,Kenny Moto Mpangara,kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo,Immelda Mbawala
Mgeni Rasmi Juma Nyumayo akimkabidhi cheti cha kuhitimu Elimu ya Msingi Mwanafunzi Amina Kazimguru katika mahafali yaliyofanyika jana katika viwanja vya Shule hiyo mjini hapa
RAIA 11 WA PAKSTANI NA BANGRADESHI WAKAMATWA RUVUMA
Na Stephano Mango,Songea
JESHI la Polisi Mkoani Ruvuma linawashikilia watu 11 ambao ni raia wa nchi za Bangradeshi na Pakstani ambao wanadaiwa kuwa wamefukuzwa toka Msumbiji kwa kupigwa mijeredi na kunyang’anywa fedha pamoja na mali walizokuwa nazo na askari wa nchi hiyo.
Akizungumza na mtandao wa http://www.stephanomango.blogspot.com/ Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda amesema kuwa raia hao wa Pakstani na Bangladeshi wamekamatwa jana majira ya saa za asubuhi huko katika kijiji cha Magwamila kilichopo mpakani mwa Msumbiji na Tanzania.
Kamuhanda amewataja waliokamatwa ambao ni raia wa Bangladeshi kuwa ni Shahed Alzam (29), Amar Ahmed (25),Gavan Halifa (40),Mhamed Parvas (23),shojal Meya (28) na Sohal Meya (28), Raia toka Pakstani waliokamatwa amewataja kuwa ni Hassan Bilar (20),Fawad Yasin (20),Mohamed Awadh (20),Aftal Hussein (24) na Hasad Ashar (45).
Amefafanua kuwa watu hao baada ya kukamatwa na kuhojiwa na polisi kwa kushirikiana na Idara ya uhamiaji Mkoani humo wamedai kuwa katikati ya mwezi uliopita waliondoka Pakstan wote kwa pamoja na walisafiri kwa ndege hadi Jijini Dar es Salaam ambako walitafuta usafiri wa basi hadi Mtwara mjini.
Ameeleza zaidi kuwa raia hao wa Nchi za Pakstani na Bangladeshi wakiwa Mtwara mjini walifanikiwa kupata usafiri kwa kutumia magari hadi Msumbiji lakini lengo lao kubwa ni kuelekea Afrika Kusini kutafuta maisha ambako wamedai kuwa waliambiwa na wenzao ambao wako Afrika kusini kuwa huko maisha ni mazuri.
Amebainisha zaidi kuwa watu hao wakiwa Msumbiji huku wakiwa wanatafuta namna ya kufika Afrika kusini walikamatwa na askari wa Msumbiji kisha walipelekwa mpakani mwa nchi hiyo na Tanzania huku wakiwa wanapigwa mijeredi na baadae wakawatelekeza kwenye Kijiji cha Magwamila ambako walikutwa wakiwa hawana kitu chochote.
Amesema kuwa raia hao wa Bangladeshi na Pakstani kwasasa wameondolewa Magwamila wapo katika Kituo kikuu cha Polisi cha Songea wakati wanafanya utaratibu wa kuwasiliana na idara ya uhamiaji ili iangalie ni namna gani wahamiaji hao haramu watawachukulia hatua .
MWISHO
Friday, September 2, 2011
WACHAWI WAKUTANA KUPANGA KUMUUA MGANGA WA JADI
Frola Ndembo maarufu kwa jina la Binti Ndembo akionyesha miliki yake ambayo inaonekana kuwa tishio kwa waganga wenzake na watu wananao daiwa kuwa ni WACHAWI
Na Joseph Mwambije,Songea
WATU wanaosadikiwa kuwa wachawi wanadaiwa kufanya vikao viwili usiku vya kumuua Mganga mmoja maarufu Mkoani Ruvuma aitwaye Frola Ndembo ambaye hulisaidia jeshi la Polisi kukamata wahalifu wanaokuja kwake kujizindika.
Wachawi hao watatu akiwemo akiwemo binti wa miaka tisa walinaswa na Mganga huyo anayefanyia shughuli zake kwenye kijiji cha Namabengo Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma na kujisalimisha huku wakieleza jinsi shughuli za ushirikina ziavyofanyika.
Mwandishi wa habari hizi wa mtandao wa http://www.stephanomango.blogspot.com/ ,Joseph Mwambije alishuhudia mtoto huyo Loveness Mapunda(jina linahifadhiwa)akijieleza kwenye eneo maaalumu kwa Mganga huyo ambalo huitwa Uwanja wa dhambi ambalo Mshirikina hueleza jinsi anavyofanya ushirikina na kutubu kwenye umati mkubwa wa watu unaokuwa umemzunguka.
Akijieleza katika eneo hilo mtoto huyo ambaye ana maendeleo mazuri darasani alisema uchawi alipewa na Bibi yake ambaye alikuwa pamoja naye kwa mganga huyo alisema yeye na Bibi yake huyo walihudhuria vikao viwili vya Wachawi vya kumuua Mganga huyo lakini hawakuchangia hoja yoyote.
Akisimulia huku akitoa machozi katika Uwanja wa dhambi alisema Bibi yake amemtia muhuri mama yake mzazi kwa ajili ya kumla Krismas ya mwaka huu na kwamba amemuweka yai sehemu za siri jambo linalomfanya aumwe ugonjwa usiojulikana.
Alisema sababu za kufanya kikao hicho ni kutokana na Mganga huyo kuwaumbuanakuwasumbua jambo linalowafanya kushindwakula nyama za watu kwa raha.
Alijieleza kuwa yeye ni mchawi na huwa anakwenda makaburini usiku na Bibi yake na kwamba alipewa uchawi bila kujijua hivyo anapenda Mganga huyo amuondoe uchawi.
Kwa upande wake Mganga huyo maarufu kwa jina la Binti Ndembo alijigamba kwamba Wachawi hawawezi kumuua bali atakufa Mungu atakapopenda na kwamba ataendelea kuwaumbua wachawi na Majambazi na wezi.
WALIMU WA UFUNDI WATAKIWA KUWAJENGEA UWEZO WA KUJITEGEMEA WANAFUNZI
Na Joseph Mwambije,Songea
KAIMU Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Nyanda za juu kusini Susan Magani amewataka wahitimu wa kozi ya CBET kutokuwa na muda wa mchezo kwenye kazi yao ya Ualimu wa Ufundi kwa kuwa inamjengea mtu ujuzi katika maisha yake
Aliitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati akifunga kozi ya kufundisha kwa kutumia mfumo mpya wa Compitance based education and training(CBET) iliyofanyika Peramiho na kushirikisha walimu 36 wa vyuo vya ufundi toka Mikoa ya Ruvuma na Iringa.
Magani alisema kuwa kazi hiyo ni kazi nzito na muhimu kama zilivyo kazi nyingine hivyo ni vyema walimu wanaofundisha vyuo vya ufundi wakatambua jukumu lao la kuwajengea watu ujuzi wa kwenda kujitegemea.
‘Walimu mnaofundisha vyuo vya ufundi mnapaswa kujijua kuwa nyinyi ni watu muhimu mnaohusika katika kumjengea mtu ujuzi wa kujitafutia maisha hivyo mnapaswa kujiendeleza kielimu kwa kuwa kuna mabadiliko ya kiuchumi’alisema Magani.
Pia aliwataka walimu wa vyuo vya ufundi kuwa wajasiriamali ili waweze kupambana na makali ya maisha ya sasa ambayo yanaendelea kupanda kila siku na kuwa wajasiriamali wa vitendo na kwamba kwa hali hiyo hata wanafunzi wao wanaweza kuiga ujasiriamali toka kwao.
Alisema kuwa walimu hao waliohitimu mafunzo ya kufundisha kwa kutumia mfumo huo mpya watakuwa na nafasi nzuri ya kuwaeleza wanafunzi watakaokuja kusoma kwenye vyuo vyao.
Akijibu risala ya wahitimu hao ilyotaka walimu wa ufundi toka taasisi za dini na binafsi kuongezewa mishahara,walimu kupata mafuzo ya kopyuta na kiingereza na kufungua maduka ya vitabu vya ufundi alisema maombi yao yatafanyiwa kazi.
Kaimu Mkurugenzi huyo wa VETA alisema suala la upatikanaji wa vitabu wataliingiza kwenye mpango kazi wa miaka mitano na maoni yao yatapelekwa kwenye ngazi za juu kwa ajili ya hatua zaidi
MWISHO
Wednesday, August 31, 2011
BIASHARA YA VIUNGO VYA BINADAMU YAHOFIWA KUANZA RUVUMA
Na Stephano Mango,Songea.
JESHI la polisi mkoaniRuvuma limebaini kuwa mabaki ya mwili wa binadamu yaliyokutwa yamehifadhiwa kwenye mfuko na kutupwa kati kati ya mto Nakawale wilayani Songea hivi karibuni ulikuwa tayari umeshachunwa ngozi na kuchukuliwa mifupa pamoja na kichwa kitendo kilichofanywa na watu wasiojulikana na kisha kutokomea navyo kusikojulikana.
JESHI la polisi mkoani
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda akizungumza na mtandao wa http://www.stephanomango.blogspot.com/ alisema kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 24 mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi katika eneo la Nakawale wilayani Songea ambako Afisa mtendaji wa kijiji hicho alipewa taarifa na wananchi kuwa kuna mwili wa binadamu ukiwa umehifadhiwa kwenye kiloba umeonekana upo kati kati ya mto.
Alisema kuwa Afisa mtendaji huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana baada ya kupata taarifa hiyo alikwenda kwenye eneo la tukio ambako aliwakuta wananchi wamekusanyika kisha alifanya mawasiliano na polisi ambao baadaye walifika kwenye eneo la tukio wakiwa wameongozana na daktari wa serikali kwa ajiri ya uchunguzi.
Aidha alisema kuwa baada ya kufanyika kwa uchunguzi wa mwili huo ilibainika kuwa mwili huo ulikuwa ni wa marehemu Jafar Shabani mkazi wa kijiji hicho huku ukiwa umechunwa ngozi ,mifupa pamoja na kichwa na kubaki nyama na nguo za marehemu huyo zikiwa kando kando ya mto huo ambazo ndizo zilizopelekea wananchi kugundua kuwa aliyeuawa kuwa ni Shaban.
Kamuhanda ameeleza zaidi kuwa polisi baada ya kufanya uchunguzi zaidi walibaini kuwa siku chache kabla ya tukio hilo marehemu huyo alikuwa amegombana na Said Kandemanje(37) ambaye tayari amekamatwa na anahojiwa na polisi kuhusiana na tukio hilo .
Aidha kamuhanda alisema kuwa uchunguzi uliofanywa unaonyesha kuwepo kwa vitendo vya ufukuaji wa makaburi yaliyoko kwenye vijiji vya nchi jirani ya Msumbiji ambako karibu na mpaka wa Tanzania na kuchukua viungo mbali mbali vya binadamu vinavyodaiwa kupelekwa nchi nyingine kwa uuzaji wa mifupa hiyo ya binadamu.
Alisema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kina kuhusiana na matukio hayo ili kuweza kubaini mtandao wa watu wanaofanya vitendo hivyo viovu na kuwafikisha kwenye vyombo vya kisheria kwa hatua zaidi
MWISHO
MWANAFUNZI ASAKWA KWA KUMUUA MJOMBA WAKE TUNDURU
Na Gideon Mwakanosya,Songea.
JESHI la polisi mkoani
Akizungumza mwandishi wa mtandao huu wa http://www.stephanomango.blogspot.com/ ofisini kwake kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma Bw.Michael Kamuhanda alisema kuwa tukio hilo la mauaji limetokea jana majira ya saa 8 usiku wakati wa ugomvi baina ya marehemu ambaye jina lake ni Michael Gabriel(23) mkazi wa kijiji hicho na dada yake Marisela Jamadin(27).
Kamanda Kamuhanda alisema kuwa inadaiwa siku ya tukio hilo katika kijiji hicho cha Mtonya Gabriel aliuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na mtoto wa dada yake huyo Agrey Emmanuel(14) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Mtonya wilayani humo na baada ya kugundua kuwa ameua alikimbia na kutokomea kusikojulikana.
Kamanda Kamuhanda alisema kuwa mwanafunzi huyo Agrey anatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi utakaofanyika nchini kote mwezi ujao na hivyo jeshi la polisi mkoani humu linaendelea kumsaka kuhusiana na tuhuma hizo na uchunguzi unaendelea kuhusiana na tukio hilo na hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa.
Hata hivyo kamada Kamuhanda alisema kuwa chanzo cha ugomvi huo ambao umepelekea Gabriel kuhuwawa na mpwa wake bado hakijajulikana licha ya kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi.
Mwisho.
Tuesday, August 30, 2011
KAMPUNI YA SONGEA NETWORK YAPANIA MAKUBWA KATIKA KILIMO NA ELIMU
Na Thomas Lipuka,Songea
KAMPUNI ya Songea Network Centre na Valongo Network Centre za Mkoani Ruvuma zimeazimia kuimarisha kilimo cha Kahawa,ulezi na Jetropa katika Mkoa wa Ruvuma ili kuwakomboa wananchi wa kipato cha chini kwa kilimo hicho.
Kampuni hizo zimetambulishwa jana rasmi mbele ya Serikali ya Mkoa na kutaja malengo yao katika kuendeleza mazao hayo matatu kwa ustawi wa jamii za watanzania ambao zaidi ya asilimia 80 wanategemea kilimo.
Mkurugenzi wa Kampuni hizo Xaveri Kazimoto Komba ameyataja malengo yao kuwa ni kuendeleza elimu katika Mkoa,kuimarisha kilimo cha ulezi,kahawa na Jetropa,kukuza utamaduni na kuimarisha hali ya Mkoa kwa mazingira ili uoto wa asili usitoweke.
Komba alisema katika kuimarisha kilimo cha kahawa Mkoani Ruvuma tayari ameisha unganisha Mkoa na watafiti wa zao hilo toka Ujerumani ambao kwa kutumia teknolojia za kisasa wataliendeleza zao hilo na kuleta uzalishaji wenye tija ili kukuza kipato cha wakulima wa kahawa Mkoani Ruvuma.
Akiongelea hatua zingine za kuboresha uzalishaji wa zao hilo na mazao mengine yaliyo tajwa amesema hapata kuwepo na tatizo la soko kwani utaratibu umeisha andaliwa wa kununua mazao hayo iwapo yatazalishwa kwa kasi na kutunza ubora wake na soko limeandaliwa.
Akitambulisha mradi wa kuboresha elimu Kazimoto amesema tayari wameisha anzisha Sekondari ya St.Sapiensia ambayo ina kidato cha nne sasa na kuchukua wanafunzi wa dini zote wa kike na wa kiume,shule ambayo iko Parokia ya Mjimwema manispaa ya Songea.
Katika hatua nyingine tayari Songea Network Centre imeisha panda miti zaidi ya 500 ya kivuli matunda na mbao kwa hatua ya kulinda na kuboresha mazingira,miti ambayo imepandwa Songea mjini na Kijiji cha Mbinga Mhalule Tarafa ya Muhukuru.
Naye Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Vestina Nguruse ambaye kwa cheo chake ni mshauri wa mipango Mkoa amesema mradi wa kilimo kinachojali watu unaoanzishwa na Songea Network Centre uwe endelevu kwa kuwa mipango yake ni ukombozi kwa watu wa Ruvuma.
Amesema shida kubwa ni soko kwa mazao ya wakulima na bei zisizo za uhakika ambazo hubadilishwa mara kwa mara kutokana na soko la dunia linavyoendelea lakini kutokana na utafiti wa kina uliofanywa na Songea Network Centre bila wasiwasi suala la soko litadhibitiwa kikamilifu.
Nguruse amefafanua kuwa fursa za kuendeleza mazao haya katika Mkoa zipo za kutosha akataja uwepo wa ardhi safi kwa kilimo cha kahawa,ulezi na Jetropa ni nguvu kazi ya kutosha yaani wakulima uwepo wa Bandari ya Mtwara na ujenzi wa barabara inayoendelea toka Mtwara Mbamba bay pia mito na mabonde yenye maji wakati wote kwa kilimo cha umwagiliaji.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa Nguruse aliwaasa viongozi wa mradi kusimamia mradi huo uwe endelevu na utimize azima yake ya kumkomboa mkulima wa Mkoa wa Ruvuma
Wakati huo huo imefahamika kuwa jitihada za kupata soko la uhakika kwa mazao hayo matatu zimeletwa na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Ahamad Ngemara ambaye amefanya jitihada kubwa kwa suala la masoko nchini Ujerumani.
KAIMU MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA ANNA MBOGO
WANANCHI SONGEA WAIFYATUKIA WIZARA YA AFYA
Na Stephano Mango,Songea
WANANCHI wa Vijiji vilivyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuona umuhimu wa kuwaletea watumishi wenye taaluma wakiwemo wauguzi na Waganga kwenye Zahanati na vituo vya Afya ambako kuna Upungufu wa Wataalamu.
Wakizungumza kwa Nyakati tofauti na mtandao wa http://www.stephanomango.blogspot.com/ wananchi hao wameeleza kuwa kwenye baadhi ya Zahanati na Vituo vya Afya vilivyopo Wilayani Songea kuna tatizo kubwa la upungufu wa Wauguzi na Waganga ambao umekuwa ukisababisha kuwepo kero kubwa kwa Wakazi wa Vijiji hivyo.
Hebron Mbilinyi Mkazi wa Kijiji cha Madaba alisema kuwa katika Kituo cha Afya cha Madaba kina wauguzi na waganga wachache na kusababisha kuwepo msongamano mkubwa wa wagonjwa wanaofika kupata tiba kwenye Kituo hicho.
Alisema kuwa huduma inayotolewa kwenye Kituo hicho cha Afya ni duni kwani wakati mwingine wagonjwa ambao wana uwezo kifedha hulazimika kutafuta Hospitali za kulipia ambako hupatiwa matibabu.
Said Hussein Mkazi wa Kijiji cha Muhukuru alisema kuwa Kituo cha Afya cha Muhukuru kimekuwa na tatizo kubwa la kutokuwa na Waganga hasa ikizingatia kuwa kina Mganga mmoja tu ambaye hulazimika kutoa huduma tangu asubuhi na wauguzi waliopo ni wachache hivyo anaiomba Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ione umuhimu wa kuwakumbuka wakazi wa Muhukuru kwa kuwapelekea Wataalamu wenye sifa ambazo zitapunguza kero zilizopo Kijijini hapo ambako kuna umbali wa Kilomita 80 tokea Songea Mjini ambako kuna Hospitali ya Serikali ya Mkoa.
Fadhili Ngonyani Mkazi wa Kijiji cha Liyangweni alieleza zaidi kuwa Huduma inayotolewa katika Zahanati ya Kijiji hicho siyo ya kuridhisha kwasababu Zahanati hiyo ina Wauguzi wachache ambao ndiyo wamekuwa wakitoa huduma badala ya Mganga ambaye hajaletwa tangu muda mrefu hivyo ameitaka Halmashauri ya Wilaya hiyo kuchukua hatua za haraka kutafuta Waganga pamoja na Wauguzi kwenye Zahanati hiyo ili kupunguza kero iliyopo Kijijini hapo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Anna Mbogo aliuambia mtandao huu kuhusiana na kuwepo kwa malalamiko toka kwa Wananchi ya upungufu wa wataalamu kwenye Zahanati na Vituo vya Afya alikiri kuwa Halmashauri yake ina upungufu wa Wataalamu kwenye Zahanati na Vituo na Afya.
Mbogo alisema kuwa Halmashauri hiyo ina Vituo viwili vya Afya ambapo alivitaja kuwa ni Kituo cha Afya cha Muhukuru na Kituo cha Afya cha Madaba ambavyo vyote vina waganga watatu tu badala ya kuwa na waganga wanne kila kimoja.
Alifafanua kuwa Halmashauri hiyo pia ina Zahanati za Vijiji 23 ambazo zina wauguzi na waganga wachache na baadhi ya Zahanati zilizopo hazina waganga na badala yake wauguzi ndiyo wamekuwa wakitoa huduma kwenye Zahanati hizo.
Alizitaja Zahanati ambazo hazina kabisa waganga kuwa ni Liyangweni,Nambendo,Gumbiro na Ngahokola na Kituo cha Afya cha Muhukuru kina mganga na Madaba kuna waganga wawili wakati kila Kituo cha Afya kulipaswa kuwe na waganga wanne na kwenye Zahanati kunapaswa kuwe na waganga wawili.
Alieleza zaidi kuwa kutokana na hali hiyo kwenye vituo vya afya kuna upungufu wa waganga watatu na kwenye Zahanati kuna upungufu wa waganga 29 wakati mahitaji ya waganga kwenye Halmashauri hiyo bado ni kubwa na kusababisha kuwepo Changamoto kubwa ya upungufu mkubwa wa wataalamu wenye sifa wakiwemo wauguzi na waganga jitihada inaendelea kufanywa ya kutafuta waganga na wauguzi wenye sifa kujaza nafasi zenye upungufu kwenye Zahanati
MIKARATUSI NI MITI HATARI KATIKA VYANZO VYA MAJI KWENYE MILIMA YA MATOGORO
Na Thomas Lipuka,Songea
IMEBAINI kuwa ukosefu wa maji kiangazi katika Manispaa ya Songea unachangiwa kwa kiasi kikubwa na aina ya miti ambayo ipo katika misitu ya milima Matogoro ambayo hunyonya maji kwa kiwango kikubwa kwa kipindi cha mwaka.
Afisa maliasili wa Mkoa Ruvuma Enock Buja akizungumza na mtandao wa http://www.stephanomango.blogspot.com/ alisema utafiti uliofanywa na Taasisi inayoshughulikia utafiti wa misitu nchini ijulikanayo kama TAFORMA, imebaini kuwa kuna aina kadhaa ya miti ambayo kwa kiwango kikubwa.
Ameitaja miti hiyo kuwa ni mikaratusi (Camaldulensis) ambayo hunyonya maji kiasi cha milimita 1240 kwa mwaka na mikaratusi aina ya (Microrhea) pia hunyonya maji milimita 1050 kwa mwaka.
Afisa maliasili huyo wa Mkoa amefafanua kuwa ,aina nyingine ya miti inayonyonya maji kwa wingi ni mikaratusi hujulikana kama patula wenye uwezo wa kunyonya maji kiasi cha milimita 665 kwa mwaka.
Katika ufafanuzi Buja amesema miti hiyo yote iliyo tajwa ipo misitu ya milima matogoro ambapo kiasi mingi imeondolewa kwa maji ikiwa kiasi, tu ikiwa na lengo la kuiondoa isilete hatari ya kukosekana kwa maji,kwa wakazi wa Manispaa ya Songea.
Afisa maliasili huyo ameongeza kusema kuwa kiasi kilichotajwa hunyonywa na miti hiyo ambapo kwa mti mmoja na sio kwa uwingi wake katika misitu.
Katika utafiti huo imeelezwa kuwa ipo miti mingine kwa mfano mgunga na mvile inayoelekea kutumia maji mengi kuliko mikaratusi iliyotajwa hapo juu.
Amesema baadhi ya mazao ya kilimo mathalani mpunga na miwa nayo hutumia kwa kiwango ambacho karibu sawa ya mikaratusi.
Katika msukumo wa Kitaifa wa kupunguza umaskini MKUKUTA mbinu nyingi zinafikiliwa kutumika katika kufikia azma hiyo bahati mbaya upandaji miti katika vyanzo vya maji haujatiliwa mkazo kwa umakini hasa miti gani ipandwe ili kuondokana na tatizo la miti kunyonya maji.
Ni sahihi kabisa kuvuna miti iliyopo misitu ya milima matogoro kwani miti hiyo ni hatari na ni adui mkubwa wa chanzo kikuu cha maji yatumiayo katika Manispaa ya Songea.
Hivi sasa Taifa limeagiza kuwa kila Wilaya ipande miti zaidi ya 1500 ili kurudisha jotoridi na kuondoa hewa ya ukaa ambayo inatishia Taifa letu kwa tabia mbaya za baadhi ya watu wakatao miti bila kupanda au kwa ajili ya mkaa na shughuli za ujenzi na za kibinadamu.
Hali ya uchomaji moto ni tatizo la pili katika misitu ya milima matogoro mbali ya juhudi za mkoa za kurudishia miti hiyo mwaka hadi mwaka kwa utaratibu wa kupanda miti ya asili ambayo hainyonyi maji kwa wingi jambo hilo juhudi zake linafifishwa na watu waharibifu wanaoendeleza vitendo vya uchomaji moto katika mlima matogoro na misitu yake Mkoani Ruvuma.
MILIONI 215 KUTUMIKA KUNUNULIA MADAWA YA KUULIA WADUDU
Na Stephano Mango,Mbinga
SERIKALI kwa kushirikiana na wadau wa zao la kahawa Wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma imechangisha jumla ya shilingi milioni 215 kwa ajili ya kununulia madawa yatakayotumika kupambana na wadudu waharibifu wa zao hilo .
Katibu tawala wa wilaya hiyo Idd Mponda alisema fedha hizo zimetumika kununulia madawa aina ya SUBA ambayo hutumika kuulia wadudu aina ya vidung’ata ambao wamekuwa wakishambulia miti ya kahawa.
Alisema kuwa jumla ya hekta 48 ya zao hilo zimeshambuliwa na wadudu hao na kusababisha uzalishaji wa kahawa kushuka.
Mponda alisema kufuatia jitihada zilizofanyika kuanzia Julai mwaka jana hadi sasa za kutokomeza wadudu hao mashamba mengi yameonekana kwenda vizuri na kwamba katika msimu wa mwaka 20011/12 uzalishaji unatarajia kuongezeka hadi kufikia tani 9,000.
"Kinachotakiwa kwa wakulima ni kuhakikisha wanazingatia yale wanayoelekezwa na wataalamu wa kilimo na kwamba wajiunge pamoja na kuanzisha mashamba darasa ili iwe rahisi kwa maofisa ugani kuwafikia", alisema Mponda.
Kuhusu wanunuzi wa zao hilo alisema wanapaswa kuzingatia masharti yaliyowekwa na uongozi wa wilaya hiyo na kwamba kwa wale ambao watabainika kutorosha kahawa kwa lengo la kukwepa kulipa ushuru watachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kunyang’anywa leseni ya biashara hiyo.
Pia alisema wakati umefika kwa wakulima wa zao hilo kuwa makini na wafanyabiashara wajanja wanaozunguka vijijini kununua zao hilo kwani baadhi yao wamekuwa wakiwarubuni wakulima kuwa bei ya kahawa imeshuka kwenye soko la dunia ili wanunue zao hilo kwa bei ya chini jambo ambalo sio sahihi.
Monday, August 29, 2011
KAMANDA WA POLISI MKOA WA RUVUMA MICHAEL KAMUHANDA
Na Cresencia Kapinga,Songea
WATU sita wamefariki dunia papo hapo na wengine wawili wamejeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka na kuwaka moto katika kijiji cha Chunya kilichopo wilayani Mbinga mkoani Ruvuma.Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Machael Kamuhanda akizungumza na mtandao wa http://www.stephanomango.blogspot.com/ alisema kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya saa 12 jioni na kwamba miongoni mwa waliofariki miili yao imeuungua vibaya huku maiti hizo zikiwa hazitambuliki.Kamuhanda alisema kuwa tukio hilo limehusisha Gari lenye namba za usajili T 270 BDG Landrover likiwa linaendeshwa na Dereva Stevin Ngoko (32) kupinduka na kuwaka moto na kusababisha vifo vya watu sita papo hapo katika kiji cha Chunya barabara iendayo Mbambabay toka Mbinga.Kamuhanda amewataja waliojeruhiwa katika ajari hiyo kuwa ni Jeremia Masalo (38) mkazi wa nchi jirani ya Msumbiji na Anna Godfrey (3) mkazi wa Mbambabay ambao wote wamelazwa katika Hospitali ya Serikali ya Wilaya ya Mbinga kwa matibabu.Alisema kuwa watu waliokufa majina yao hayajaweza kufahamika kutokana na maiti hizo kutotambulika kwa kuwa zimeungua vibaya na zote zimepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya hiyo.Kamuhanda alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi ambao ulimsababishia dereva wa gari hilo kushindwa kumudu usukani na kwamba jeshi lake linaendesha msako wa kumtafuta dereva wa gari hilo Bw. Ngoko ambaye alitoroka mara tu baada ya kutokea ajali hiyo.
Sunday, August 28, 2011
WANANCHI WAMTAKA MKURUGENZI KUITISHA UCHAGUZI WA SERIKALI YA KIJIJI CHA MKILI
Na Thomas Lipuka,Songea
WANANCHI wa Kijiji cha Mkili Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma wamemtaka Mkurugezi wa Halmashauri Wilaya ya Mbinga kusimamia zoezi la kupata uongozi wa kijiji hicho kwani kijiji hicho kwa muda mrefu kina uongozi wa mda ambapo shughuli zote huendeshwa na Mtendaji wa kijiji, baada ya aliyekuwa Mwenyeketi wa kijiji hicho John Isdori Tilia kusimamishwa uongozi na Serikali yake yote .
Tuhuma zilizopelekea Mwenyekiti huyo na serikali yake yote kusimamishwa uongozi ni pamoja na kutoitisha mikutano ya serikali ya kijiji kutosoma mapato na matumizi ya kijiji kushindwa kusimamia miradi mbalimbali ya kijiji na wakati mwingine kujishughulisha zaidi na mambo ya starehe na kuacha yale yanayohusu maendeleo ya wanakijiji .
Wanakijiji wa Mkili baadhi yao wametaja miradi ambayo ameshindwa kusimamia ni ujenzi wa kibanio cha mfereji wa maji kwa kilimo cha umwagiliaji ambacho kipo katika mto Ndumbi kijijini hapo ,ujenzi unaendelea wakituo cha afya kwa kujenga nyumba nne za waganga na ukarabati wa barabara itokayo bandari ya Mkili hadi Hospitari ya Litembo .
Wakitoa kero zao kupitia mtandao wa http://www.stephanomango.blogspot.com/ baadhi ya wanakijiji hao walisema toka serikali ya kijiji hicho ichaguliwe hawajasomewa taarifa ya mapato na matumizi ambapo shughuli zote huendeshwa na mwenyekiti aliyesimamishwa uongozi na mtendaji bila wanakijiji kuhusishwa.
Wameongeza kuwa kijiji hicho kina bonde la kutosha kwa fursa ya kilimo cha umwagiliaji wa mpunga ambapo tayari Halmashauri ya Mbinga ilishatoa mradi wa umwagiliaji katika kijiji hicho lakini kwa kukosa uongozi bora wa kijiji,kibanio kilisombwa na maji mara mbili jambo ambalo mkandalasi hakufuatiliwa namna alivyojenga kibanio hicho na ubora wake .
Wamesema kilimo hicho cha umwagiliaji katika bonde lililopo kijijini hapo kingeweza kuwanasua wanakijiji kwa kupata zao la mpunga mara mbili kwa mwaka hivyo wamemwomba mkurugezi wa Wilaya ya Mbinga kuharakisha zoezi la kuwapata viongozi wa serikali ya kijiji ili kuharakisha maendeleoyao .
Walipoulizwa kuhusu tatizo la sumu inayotiwa katika mito inayozunguka kijijini hapo hasa toka eneo milimani walisema vitendo hivyo vya uharibifu vinatendwa na baadhi ya watu kutoka vijiji vya Mahande ,Siasa ,Lundumato,Mkoha,kwa uroho wa kutafuta Samaki ambapo madhara yake huua madhalia yote ya viumbe hai katika mito hiyo ambayo ni Ndumbi ,Mnyamaji,Chipindi,na Luhorochi.
Wanakijiji hao wamempongeza mkurugezi mtendaji wa Halmashauri wa Wilaya ya Mbinga kwa kuwatia moyo ili wafyatue matofari ya nyumba nne za waganga kwa ajili ya kuimarisha na kupanua kituo cha afya cha Mkili pia kwa ahadi ya kupatiwa gari la kusafirisha wagonjwa siku za usoni toka kituo cha afya Mkili hadi Hospitari za Lihili, Mbinga ,Litembo ,Songea na Peramiho.
Aidha wanakijiji hao wameiomba serikali kuwaimarishia mawasiliano ya simu kwa kuwajengea minara ya Voda,Airtel,Tigo na TTCL,mawasiliano ambayo wanayapata kwa shida kwa kupanda juu ya miti ama kwenye vichuguu.
WANANCHI wa Kijiji cha Mkili Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma wamemtaka Mkurugezi wa Halmashauri Wilaya ya Mbinga kusimamia zoezi la kupata uongozi wa kijiji hicho kwani kijiji hicho kwa muda mrefu kina uongozi wa mda ambapo shughuli zote huendeshwa na Mtendaji wa kijiji, baada ya aliyekuwa Mwenyeketi wa kijiji hicho John Isdori Tilia kusimamishwa uongozi na Serikali yake yote .
Tuhuma zilizopelekea Mwenyekiti huyo na serikali yake yote kusimamishwa uongozi ni pamoja na kutoitisha mikutano ya serikali ya kijiji kutosoma mapato na matumizi ya kijiji kushindwa kusimamia miradi mbalimbali ya kijiji na wakati mwingine kujishughulisha zaidi na mambo ya starehe na kuacha yale yanayohusu maendeleo ya wanakijiji .
Wanakijiji wa Mkili baadhi yao wametaja miradi ambayo ameshindwa kusimamia ni ujenzi wa kibanio cha mfereji wa maji kwa kilimo cha umwagiliaji ambacho kipo katika mto Ndumbi kijijini hapo ,ujenzi unaendelea wakituo cha afya kwa kujenga nyumba nne za waganga na ukarabati wa barabara itokayo bandari ya Mkili hadi Hospitari ya Litembo .
Wakitoa kero zao kupitia mtandao wa http://www.stephanomango.blogspot.com/ baadhi ya wanakijiji hao walisema toka serikali ya kijiji hicho ichaguliwe hawajasomewa taarifa ya mapato na matumizi ambapo shughuli zote huendeshwa na mwenyekiti aliyesimamishwa uongozi na mtendaji bila wanakijiji kuhusishwa.
Wameongeza kuwa kijiji hicho kina bonde la kutosha kwa fursa ya kilimo cha umwagiliaji wa mpunga ambapo tayari Halmashauri ya Mbinga ilishatoa mradi wa umwagiliaji katika kijiji hicho lakini kwa kukosa uongozi bora wa kijiji,kibanio kilisombwa na maji mara mbili jambo ambalo mkandalasi hakufuatiliwa namna alivyojenga kibanio hicho na ubora wake .
Wamesema kilimo hicho cha umwagiliaji katika bonde lililopo kijijini hapo kingeweza kuwanasua wanakijiji kwa kupata zao la mpunga mara mbili kwa mwaka hivyo wamemwomba mkurugezi wa Wilaya ya Mbinga kuharakisha zoezi la kuwapata viongozi wa serikali ya kijiji ili kuharakisha maendeleo
Walipoulizwa kuhusu tatizo la sumu inayotiwa katika mito inayozunguka kijijini hapo hasa toka eneo milimani walisema vitendo hivyo vya uharibifu vinatendwa na baadhi ya watu kutoka vijiji vya Mahande ,Siasa ,Lundumato,Mkoha,kwa uroho wa kutafuta Samaki ambapo madhara yake huua madhalia yote ya viumbe hai katika mito hiyo ambayo ni Ndumbi ,Mnyamaji,Chipindi,na Luhorochi.
Wanakijiji hao wamempongeza mkurugezi mtendaji wa Halmashauri wa Wilaya ya Mbinga kwa kuwatia moyo ili wafyatue matofari ya nyumba nne za waganga kwa ajili ya kuimarisha na kupanua kituo cha afya cha Mkili pia kwa ahadi ya kupatiwa gari la kusafirisha wagonjwa siku za usoni toka kituo cha afya Mkili hadi Hospitari za Lihili, Mbinga ,Litembo ,Songea na Peramiho.
Aidha wanakijiji hao wameiomba serikali kuwaimarishia mawasiliano ya simu kwa kuwajengea minara ya Voda,Airtel,Tigo na TTCL,mawasiliano ambayo wanayapata kwa shida kwa kupanda juu ya miti ama kwenye vichuguu.
AFYA ZA WAFANYABIASHARA SOKO KUU SONGEA ZIPO HATARINI KWA KUKUBWA NA MAGONJWA YA MLIPUKO
Na Gideon Mwakanosya,Songea.
WAFANYABIASHARA katika Soko kuu katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoa wa Ruvuma wapo katika hatari kubwa ya kukumbwa na magonjwa ya milipuko kikiwemo Kipindupindu kutokana na miundo mbinu ya maji taka yanayo simamiwa na mamlaka ya Maji safi na Maji taka Songea (SOUWASA) kuwa mibovu pamoja na wauzaji wa nyama ya ng’ombe kwenye mabucha kutiririsha maji machafu wanayosafishia utumbo wa ng’ombe hadi maeneo wanayouzia nyanya,vitunguu na mbogamboga wafanyabiashara wadogo.
Mwandishi wa mtandao wa http://www.stephanomango.blogspot.com/ jana alifanya mazungumzo na baadhi ya wafanyabiashara sokoni hapo ambapo walieleza kuwa miundo mbinu ya maji taka imekuwa ikipasuka na kutiririsha maji kwenye maeneo wanayouzia bidhaa zao na kusababisha adha kubwa kwa wafanyabiashara hao ambao wamekuwa wakilazimika kufanya kazi katika mazingira magumu.
Walisema katika hali ya kushangaza soko hilo lina maafisa afya ambao wamekuwa wakifanya kazi kila siku kwenye eneo hilo ambalo lina mazingira machafu lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa.
Issa Hussen ambaye ni mfanya biashara katika soko hilo alieleza kuwa wafanyabiashara wa mbogamboga ambao wamekuwa wakitandika magunia chini kisha kuweka bidhaa zao kama nyanya, vitunguu wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu kwani kwenye maeneo wanayofanyia biashara hiyo maji yanayotiririshwa toka kwenye ma bucha ya nyama za ng’ombe wanayooshea utumbo wa ng’ombe pamoja na maji taka ambayo yanayo tiririka toka kwenye mtandao wa Souwasa yamekuwa yakipita kwenye eneo hilo wanayofanyia biashara na kuwaletea adha kubwa kwani wanunuzi wamekuwa wakikataa kununua bidhaa zao kutokana na maji machafu kuwa jirani na biashara zao.
Kwa upande wake Afisa masoko wa Halmashauri ya Manispaa hiyo Salum Homera alipoulizwa na mtandao huu kuhusiana na malalamiko ya wafanyabiashara kuhusiana na kukithiri kwa uchafu kwenye soko kuu ambalo limekuwa likitiririsha maji machafu kwenye ambayo yamekuwa yakipita jirani kabisa na maeneo ya biashara zao alikiri kuwepo kwa tatizo hilo lakini alisema kuwa tatizo hilo lipo juu ya uwezo wake.
Homera alisema kuwa Ofisi yake ilisha toa taarifa kwa idara ya Afya na kwamba maafisa afya ndiyo walitakiwa kuona umuhimu wa kudhibiti hali hiyo iliyojitokeza sokoni na kwamba mamlaka ya maji safi na maji taka songea (SOUWASA) nao walishapewa taarifa na waliahidi kufika kufanyia matengenezo mtandao wa maji taka.
Kwa upande wake Afisa afya wa Halmashauri ya Manispaa hiyo Mahundi alipohojiwa na nipashe kuhusiana na kukithiri kwa uchafu katika soko hilo, alieleza kuwa tatizo hilo Ofisi yake ilikuwa bado haijalipata lakini Afisa masoko ndiye alitakiwa kutoa taaarifa ki maandishi kwenye ofisi ya idara ya afya ili tatizo hilo liweze kufanyiwa kazi kirahisi kwani yeye ndiye msimamizi mkuu wa masoko yote ya halamashauri.
Jitihada za mtandao huu za kumpata Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji safi na maji taka (SOUWASA) Fransis Kapongo ziligonga mwamba baada ya kumpigia simu yake ya mkononi zaidi ya mara tatu bila kupatikana na nipashe ilifanya jitihada zaidi ya kuwasiliana na kaimu katibu tawala wa mkoa wa Ruvuma Dr.Anselmo Tarimo na kumuuliza juu ya uchafu uliokithiri sokoni Songea amabye alikiri na kudai kuwa tatizo hilo linalazimika kufanyiwa utaratibu wa haraka ili kulimaliza kuanzia mwanzoni mwa wiki hii ambapo wataalamu wote wa afya watalazimishwa wawepo kwenye soko hilo ili waone ni jins gani wataweka mazingira mazuri sokoni hapo ambayo yatawafanya wafanyabiashar wasikumbwe na magonjwa ya milipuko.
MWEKEZAJI ADAIWA KUPORA ARDHI YA EKARI 5000 KWA WANAKIJIJI LIPOKERA
Wananchi wa kijiji cha Lipokera wakiwaonyesha waandishi wa Habari ardhi yao ambayo wanadai wameporwa na mwekezaji
Wananchi wakionyesha mahindi yao baada ya kuvuna haraka haraka kwa kumuogopa mwekezaji asije akawanyang'anyaNa Thomas Lipuka,Songea.
WAKAZI wa kijiji cha Lipokela wilayani Songea mkoani Ruvuma wanamuomba Waziri wa ardhi,nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka kuwasaidia kuirejea ardhi yao yenye ukubwa wa zaidi ya hekari 5000 iliyochukuliwa kinyemela na mwekezaji.
Wakizungumza na waandishi wa habari katika kijiji hicho baadhi ya wananchi walidai kuwa mwekezaji mwenye asili ya Asia anayefahamika kwa jina moja la Merali tangu mwaka 1985 alipewa ardhi kinyemela bila baraka za wananchi na kusababisha ardhi hiyo kuingia kwenye mgogoro mkubwa.
Wananchi wamedai kuwa mwekezaji huyo alipewa ardhi hiyo katika mazingira ya kifisadi kupitia aliyekuwa mwenyekiti wa kijiji hicho Joseph Komba pamoja na aliyekuwa katibu wake Gervas Mbonde .
Hata hivyo walisema mwekezaji huyo alipewa ardhi kwa maamuzi ya wananchi yenye ukubwa wa hekari 1000 mwaka 1984 na kwamba mwaka 1985 aliomba tena ardhi hekari zaidi ya 5000 ambazo alipewa bila baraka za wananchi na kuleta mgogoro ambao unaendelea hadi sasa.
``Kuanzia mwaka 1985 wananchi wa kijiji cha Lipokela hawakujua kama ardhi yao ya hekari 5000 amepewa mwekezaji hadi mwaka jana takriban miaka 25 ndipo ilipofahamika na kusababisha wananchi zaidi ya 250 wanaolima mashamba pamoja na makazi kwenye eneo hilo kuambiwa kuwa eneo hilo ni mali ya mwekezaji wa kiasia’’,walidai wananchi hao.
Akizungumza kwa niaba ya wenzao Mwenyekiti mstaafu wa kijiji hicho Faustine Komba alibainisha kuwa ardhi hiyo yenye mgogoro ilianza kutumika na wananchi kuanzia mwaka 1993 ambao walipimiwa kihalali na uongozi wa kijiji na kuendelea kuitumia mwaka hadi mwaka bila kutambua kuwa amepewa mwekezaji kinyemela.
Komba alisema mwekezaji alipewa kisheria hekari 1000 tu upande wa kulia mwa barabara ya Songea - Mbinga na kwamba eneo lenye hekari zaidi ya 5000 upande wa kushoto ambazo mwekezaji huyo anadai kupewa kinyemera sio zake kwa kuwa ni mali ya wananchi ambazo walipewa kihalali na serikali ya kijiji.
Uchunguzi ambao umefanywa na wanakijiji wanadai wamebaini kuwa mwekezaji huyo kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa kijiji hivi sasa amekuwa dalali wa kuwauzia ardhi wawekezaji wengine kutoka nchini Afrika kusini na Marekani hivyo wameiomba serikali na hasa waziri wa ardhi kuingilia kati mgogoro huyo.
Wananchi hao wakiwemo Gofrey Lupindu,Agustino Komba,Filbert Kinunda, Vestina Hyera, Bomba Nchimbi wakizungumza kwa uchungu mkubwa ,walidai kuwa hivi sasa pia hawana imani na mwenyekiti wa kijiji aliyopo madarakani John Nchimbi ambaye anadaiwa kumsaidia mwekezaji badala ya kuwasaidia wananchi waliomweka madarakani.
Uchunguzi umebaini kuwa iwapo serikali haitachukua hatua za makusudi katika kutatua mgogoro huo wa ardhi kuna hatari ya kutokea machafuko makubwa kutokana na ukweli kuwa wananchi wa kijiji hicho wamedai hawapo tayari kuona mwekezaji anapora ardhi yao kinyemela na kusababisha wananchi kuwa wakimbizi katika ardhi yao.
Uchunguzi mwingine ambao umefanywa katika kijiji hicho umebaini kuwa mwekezaji huyo ambaye alipewa hekari 1000 na wananchi katika kipindi cha miaka mitatu alifanikiwa kulima hekari 15 tu na kitendo cha kutaka kuchukua hekari nyingine zaidi ya 4000 kinawapa mashaka kuwa kijiji hicho kipo katika hatari ya kuuzwa kwa kisingizio cha uwekezaji.
Afisa ardhi wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Japhet Mungashwa amekiri kwamba mwekezaji huyo amemilikishwa eneo la hekari 5000 kihalali kwa kipindi cha miaka 99 kwa sheria ya ardhi ya mwaka 1923 ambayo inawaruhusu wajumbe wa kijiji kupitisha maamuzi bila kushirikisha maamuzi ya wananchi wote kama ilivyo katika sheria mpya ya ardhi ya mwaka 1999.
Wananchi hao wametoa mwito kwa serikali ya wilaya ya Songea,mkoa wa Ruvuma pamoja na Waziri wa ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi kufika katika kijiji hicho ili kujionea hali halisi ya ardhi ya mashamba na makazi ambayo wameporwa na mwekezaji.
Sheria ya ardhi ya vijiji namba tano kifungu cha tano ya mwaka 1999 inasema kuwa Halmashauri ya kijiji haitagawa ardhi au kutoa hakimiliki ya kimila bila ya kwanza kupata idhini ya mkutano wa kijiji ambapo katika kifungu cha sita katika sheria hiyo kinaeleza Halmashauri ya kijiji italazimika kutoa taarifa na kuzingatia maoni ya mkutano wa kijiji kuhusu uendeshaji na usimamizi wa ardhi ya kijiji.
Kwa mawasiliano andika lipukakomba@yahoo.com
Saturday, August 27, 2011
Diwani wa Kata ya Mshangano Faustine Mhagama akizungumza na ndugu na jamaa zake akiwa katika Kituo kikuu cha Polisi Songea baada ya kulipoti kituoni hapo akiwa nje kwa dhamana,katikati Joseph Haule ambaye alikuwa ni mtangazaji wa uwepo wa maandamano,kushoto ni dereva wa gari la matangazo ya maandamano Suzo Luoga
POLISI WAMKAMATA DIWANI NA WAZUIA MAANDAMANO SONGEA
Na,Stephano Mango,Songea
JESHI la Polisi mkoani Ruvuma liliwakamata na kuwahoji zaidi ya masaa matatu wakazi wawili wa Kata ya Mshangano na Diwani wa kata hiyo kupitia Chama cha Mapinduzi(CCM)kwa tuhuma za kutangaza maandamano ya amani ya wananchi wa kata hiyo wakidai kupimiwa ardhi yao na Kampuni ya Ardhi Plan na kumtaka Waziri mkuu Mizengo Pinda kuwatimua kazi Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea na Afisa Mipango Miji wa Manispaa hiyo ambao wameonyesha dhahili kutaka kuwadhulumu maeneo yao
Wakazi hao waliokamatwa na polisi ni Suzo Luoga ambaye alikuwa ni dereva wa gari ya matangazo lenye namba za usajili T 295 AJS aina ya Chesar mark II,Joseph Haule ambaye alikuwa mtangazaji na Faustine Mhagama ambaye ni Diwani wa kata hiyo ambao wote walikamatwa wakiwa kwenye gari hilo ambalo lilikuwa linapita kwenye mitaa ya kata hiyo kuwatangazia uwepo wa maandamano makubwa
Mmoja wa watuhumiwa hao Haule ambaye alikuwa mtangazaji alisema kuwa kazi hiyo alipewa na viongozi ambao wenyeviti wa serikali ya mitaa ya Namanyigu,Mshangano na Mitendewawa na kwamba shughuli hiyo ya utangazaji ilisimamiwa kikamilifu na Diwani wa kata lengo kuhakikisha ujumbe unawafikia wakazi wote wa kata hiyo
Naye wa Kata hiyo Mhagama akizungumza na mtandao wa http://www.stephanomango.blogspot.com/ jana alikili kukamatwa na alidai kuwa yeye pamoja na wenzake walikamatwa na Polisi majira ya saa tatu usiku huko katika eneo la Mshangano na waliamriwa kuingia kwenye gari la Polisi wakiwa chini ya ulinzi mkali na kupelekwa kwenye kituo kikubwa cha Polisi
Alisema kuwa mara baada ya kufikishwa kituoni hapo waliamliwa kuvuliwa viatu,mkanda na kuanza kupekuliwa na kasha kuwekwa mahabusu ambapo baadae alifika Kaimu Mkuu wa Polisi wa Wilaya akiwa ameongozana na Askari Kanzu wawili ambao walianza kuwahoji hadi saa tano na nusu usiku ndipo walipoambiwa wawatafute watu wa kuwadhamini ambapo Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea James Makene pamoja na Diwani wa Viti maalum Rehema Milinga walifika kituoni hapo na kuwadhamini
Kwa upande wake Makene ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Matarawe aliuambia mtandao huu kuwa kitendo cha kuwakamata Diwani na wenzake ni uonevu mkubwa na kinyume na utawala bora kwa kuwa Serikali ya Kata ya Mshangano ilipeleka barua ya kuomba kibali cha maandamano toka tarehe 19.8.2011 ambapo mpaka wanakamatwa walikuwa hawajapewa barua wala maelezo ya aina yoyote jambo ambalo liliashiria kukubaliwa ingawa baada ya kuwaweka mahabusu ndipo wakapewa barua ya maelekezo jambo ambalo limeleta utata mkubwa wa uadilifu wa jeshi hilo
Naye Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda alisema kuwa wananchi wa kata ya Mshangano waliomba kibali cha kutaka kufanya maandamano makubwa ya amani lakini katika barua yao ilionyesha mapungufu mengi ikiwa ni pamoja na kutoeleza tarehe,muda na njia ambayo maandamano yatapita
Kamuhada alisema kuwa tayari Serikali ya Kata ilipewa barua ya maelekezo na Jeshi la Polisi yenye kumbukumbu namba.SOA.3.6/65 ya tarehe 25.8.2011 ambayo ilipokelewa na Diwani wa kata hiyo majira ya saa tatu usiku
MWISHO
Katibu Mpya wa Jimbo la Songea Mjini Chadema Masumbuko Paulo
CHADEMA SONGEA WAPATA KATIBU MPYA WA JIMBO
Na,Stephano Mango,Songea
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma kimempata Katibu mpya wa Jimbo la Songea Masumbuko Paulo katika uchaguzi wa wanachama wa chama hicho uliofanyika jana katika Ofisi ya Kata ya Mfaranyaki
Akitangaza matokeo hayo Mwenyekiti wa Jimbo hilo ambaye pia ni Diwani wa kata ya Majengo mjini hapa Idd Abdalah alisema kuwa wanachama waliopiga kura ni 80 ambapo Masumbuko Paulo amepata kura 54,Ajaba Nditi alipata kura 18, Zuber Tindwa alipata kura 8 ambapo Christopha Nyoni alipata kura 0
Abdalah alimtangaza Masumbuko Paulo kuwa ndiye ameibuka mshindi wa kwanza na hivyo kuanzia hapo anakuwa Katibu mpya wa Jimbo hilo na kwamba anatakiwa kuanza kazi mara moja ili kuweza kuendana na kasi ya chama hicho
Awali Mwenyekiti huyo aliwaambia wajumbe kuwa nafasi hiyo ya Ukatibu ilikuwa wazi kutokana na aliyekuwepo katika nafasi hiyo kuiacha na kwenda kufanya kazi kwenye Mashirika yasiyoya kiserikali
Alifafanua zaidi kuwa katika uchaguzi huo Wagombea walikuwa watano ambapo mgombea Said Ligema aliamua kujitoa dakika za mwisho za uchaguzi jambo ambalo viongozi wa Wilaya walikubaliana na uamuzi wake huo
Akiwashukuru wajumbe kwa kumchagua Masumbuko Paulo alisema kuwa imani na dhamana waliyompa ni kubwa sana hivyo atakitumikia chama kwa uadilifu mkubwa ili kiweze kupata ushindi stahiki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na chaguzi zingine zijazo
Masumbuko alisema kuwa Chama kipo katika harakati kubwa za kujiimalisha maeneo ya pembezoni mwa miji na vijijini hivyo kazi hiyo ya kujikita maeneo hayo kwa lengo la kukisambaza chama ni jukumu la wananchama wote wenye mapenzi ya dhati na chama hicho
Akifunga mkutano huo wa uchaguzi Mwenyekiti wa Chama hicho Wilaya ya Songea Peter Mboya alisema kuwa wanachama ndio nguzo stahiki ya chama chochote duniani hivyo ni vema popote pale alipo mwanachama anatakiwa afanye jambo kwa maslahi ya chama
Mboya alisema kuwa muda wa mabadiliko ya kitaifa umefika ambapo chama hicho kinatakiwa kuchukua dhamana ya kuwaongoza watanzania hivyo ni vema tukaonyesha kwa dhata mbele ya wananchi kuwa tunaweza kuwaondoha hapa walipo katika kipindi hiki cha miaka 50 ya uhuru na kuwapeleka katika hali nyingine ya ustawi wa maisha yao
MWISHO
Subscribe to:
Posts (Atom)


