About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Saturday, October 8, 2011

RAIS KIKWETE VURUGU ZA UMEYA SONGEA DKT NCHIMBI AMEKUZALILISHA

                                                Rais Jakaya Mrisho Kikwete

                          DKT Emmanuel Nchimbi aliyeshika kipaza sauti
   Charles Mhagama Diwani wa Kata ya Matogoro ambaye anadaiwa kuwa Chaguo la Dkt Nchimbi katika nafasi ya UMEYA
  
Na Gideon Mwakanosya,Songea
SAKATA la uchaguzi wa Meya Mjini Songea Mkoani Ruvuma lililopelekea kupitishwa kwa Charles Mhagama kuwa Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa utata mkubwa limezidi kuchukua sura mpya ambapo baadhi ya madiwani wa CCM wameanza kususia vikao vinavyoitishwa na Chama chao wilayani humo.
 
Ikumbukwe hivi karibuni katika Manispaa  hiyo kulifanyika uchaguzi wa Meya wa Manispaa hiyo ili kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Meya aliyefariki miezi michache iliyopita marehemu Ally Manya.
 
Lakini kabla sijachambua kwa ufupi na kuchambua jinsi mkutano huo ulivyokuwa nieleze jinsi mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM ulivyokuwa na jinsi ulivyotawaliwa na mizengwe ya kila namna.
 
Baada ya kutangazwa uchaguzi wa kura za maoni ndani ya CCM  madiwani wanane na kada mmoja wa Chama hicho walichukua fomu za kuomba kuteuliwa na Chama hicho ili mmoja kati yao agombee nafasi hiyo akichuana na mgombea atakayechaguliwa na Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA).
 
Licha ya Nchimbi kuhojiwa na Mwandishi wa makala hii kama alikuwa akimtaka  Meya aliyepitishwa kwa kupindua matokeo Charles Mhagama lakini habari zilivuja baada ya habari kusambaa kuwa alisambaza meseji za simu zikitaka madiwani wapitishe Mhagama kuwa Meya wa Manispaa ya Songea.
 
Madiwani na makada wa Chama hicho walionya tabia ya Nchimbi kuwachagulia kiongozi anayemtaka yeye ili afuate matakwa yake lakini Nchimbi alikanusha uvumi wa habari hizo zilizoenea katika viunga vya Mji wa Songea na kuthibitisha kuwa zilikuwa na chembe ya ukweli fulani.
 
Kiongozi mmoja wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Songea ameuambia mtandao huu wa www.stephano mango.blogspot.com kuwa Nchimbi alibanwa kwenye kikao cha kamati ya siasa kilichofanyika Septemba 25 mwaka huu  kuwa yeye ndiye aliyesababisha vurugu zilizotokea kwenye uchaguzi wa Meya uliofanyika kwenye Ukumbi wa SACCOS ya Manispaa 23 Septemba kwa kulazimisha  mtu anayemtaka kuwa ndiye awe Meya.
 
Mmoja wa Madiwani machachari wa Chama hicho Manispaa ya Songea ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini alisema madiwani walibanwa kwenye vikao vya  Chama hicho ili wachague diwani huyo asiyekubalika kuwa ndiye agombee Umeya na vikao vya Chama hicho vikapendekeza jina lake na majina ya madiwani wawili wanawake na kuyakata majina ya madiwani wanaokubalika.
 
Majina yaliyopitishwa na vikao vya Chama hicho ili wakapigiwe kura na madiwani wa CCM ni Mariam Dizumba,Genifrida Haule na Charles Mhagama na katika uchaguzi wao wa CCM  walibanwa ili wamchague Mhagama ili apeperushe bendera ya CCM’anasema diwani huyo’.Anasema kuwa Mariam Dizumba ambaye pia ni mke wa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Songea Mjini Hemedi Dizumba hata kura yake mwenyewe alijinyima hivyo aliambulia sifuri.
 
Anasema kuwa kwa kumuonyeshea au kumkomoa Nchimbi wakaamua kumpigia kura diwani huyo ili wakamuumbue kwenye uchaguzi wa jumla ambao ungevipambanisha Chadema na CCM  kwa kumpigia kura za hapana au maarufu kwa kura za maruhani.

Hata hivyo Katibu wa CCM Songea mjini  Alphonce Siwale alipoulizwa kuhusiana na ushawishi wa Nchimbi wa kumtaka Mhagama awe  Meya alisema kama alituma ujumbe wa simu wa kuwataka madiwani wa CCM kumchagua diwani huyo alisema alifanya hivyo kwa ushawishi wake binafsi.
 
Katika uchaguzi uliofanyika 23 Septemba mwaka huu Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) hakikusimamisha mgombea hivyo kukatokea majadiliano ni jinsi gani uchaguzi utakuwa huru na wa haki kwa kuwa Chadema hawakusimamisha mgombea.
 
Kutokana na hali hiyo ndipo Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Nachoa Zakaria ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi huo alisimama na kutoa ufafanuzi wa kanuni za uchaguzi wa nafasi hiyo na kusema wanatakiwa kupiga kura za ndiyo kama wanamtaka mgombea huyo na ikiwa hawamtaki basi wanatakiwa kupiga kura za hapana.
 
Sipendi nirudie yale yaliyoandikwa na wenzagu lakini napenda kujadili muktadha mzima uliozunguka tukio hilo na ni nani alisababisha kama vile Chemsha bongo ya yai na kifaranga cha kuku nini kilianza.
 
Katika uchaguzi huo ni wazi kabisa kanuni zilivunjwa baada ya kubainika kuwa Charles Mhagama alipigiwa kura za Hapana 14 na za ndiyo 12 na waswahili husema kwa nini tuandikie mate wakati wino upo?hivyo basi kama uchaguzi ule ulikuwa huru na wa haki na kanuni hazikuvunjwa basi kura zingehesabiwa tena kabla ya Naibu Meya kuiba kura na kuziweka kwenye kipima joto chake kidogo na kukificha sehemu zake za siri.
 
Baada ya kupigwa kura na kuhesabiwa hadharani Msimamizi wa uchaguzi Nachoa  alimwonyesha matokea Dizumba ndipo alipotaka kusoma alionyesha mstuko mbele ya madiwani na kumuonyesha Nchimbi ambaye alimuamuru kuyasoma kwa kuyapindua na alipoyasoma madiwani wakataka kura zirudiwe kuhesabiwa kwa madai alichokitangaza hakikuwa na ukweli.
 
Hapo ndipo kulitokea vurumai kubwa na ndipo Naibu Meya huyo alipopigwa  mtama  na diwani wa Kata ya Mjini kupitia Chadema Joseph Fuime na kuanguka chini kisha kuinuka kukimbilia nje na kura alizokwapua na hapo ndipo diwani huyo alipomwendea Nchimbi na kumwambia ni aibu kwake kusimamia wizi wa kura.
 
‘Ni aibu kubwa kwa Waziri kama wewe kusimamia wizi wa kura na hapa huwezi kunifanya chochote kwa kuwa Uwaziri wako ni nje ya ukumbi huu na tukiwa ndani humu wewe ni diwani kama mimi na utambue kuwa Songea wamechoka na tabia yako ya kuwachagulia viongozi’alisema diwani huyo huku akiwa amemkodolea macho Nchimbi ambaye alikuwa akinon’gonezana  jambo na diwani wa  Matarawe James Makene.
 
Wakati akitoka nje ndipo alipopokewa na watu waliokuwa nje ya ukumbi huo ambao walikuwa wakimwimbia Nchimbi mwizi wetu na yeye alionekana akizungukazunguka akichezea simu asijue la kufanya hadi pale alipokuja dereva wake na gari na kumpakia na kisha kuondoka eneo hilo  ambalo lilikuwa lina vurumai kubwa.
 
Baada ya Naibu Meya kutoka nje ya ukumbi alikimbilia kwenye gari moja na kuingia huku akifuatwa na madiwani wawili wa Chadema ambao walikuwa wakimzuia asikimbie na kura,katika sakata hilo Kada wa CCM Hamis Abdalah Ally alitaka kumgonga na gari diwani wa Mfaranyaki(CHADEMA) Salumu Mfamaji ambaye alikuwa mbele ya gari hiyo.Kada huyo wa CCM alifanikiwe kumkimbiza Naibu Meya huyo ili asiweze kupigwa.
 
Baada ya tukio hilo maneno yalizagaa mitaani kwamba Nchimbi ametishia kuwanyang’anya kadi madiwani saba wanaodaiwa kupiga kura za hapana dhidi ya mgombea pekee wa Chama chake,jambo ambalo lilijadiliwa na wachunguzi wa masuala ya siasa kwamba wanawezaje kuwanyang’anya kadi madiwani hao wakati kura ni siri ya mtu na wao wamewajuaje?.
 
Siku ya pili baada ya tukio hilo Nchimbi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Songea Mjini na Waziri wa habari utamaduni na michezo alipigiwa simu na mwandishi wa habari wa Gazeti la Majira Joseph Mwambije ili kutaka kujua kama kweli aliwatisha madiwani hao kuwanya’nganya kadi alisema hawezi kufanya hivyo kwa kuwa kanuni na taratibu za Chama hicho anazijua.

Lakini pia alisema kuwa waandishi ni wajinga na wapumbavu kwa kuwa wameandika habari za uongo kuwa yeye amekimbia na sanduku la kura.
 
Septemba 25 mwaka huu aliitisha mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea na kutoa tamko la kukanusha kuwa yeye hakukimbia na sanduku la kura akiyatuhumu magazeti matatu ya kila siku kwa kumuandika habari za kumchafulia jina.
 
Ama kwa hakika Nchimbi amechanganyikiwa na tukio lile limemchanganya pengine na kupunguza kasi yake ya  mbio za Urais wa mwaka 2015 kwani yeye katika tamko lake anayatuhumu magazeti yaliyoandika habari hiyo Septemba 23 lakini ukweli ni kwamba siku hiyo  ndiyo kilifanyika kikao cha Baraza la madiwani na hakuna gazeti lililoandika habari hiyo siku hiyo bali magazeti yaliripoti habari za tukio hilo Septemba 24 mwaka huu.
 
Harakati za Waziri huyo kijana kukanusha tuhuma hizo zitaishia kumuumbua zaidi ikiwa picha za video zitaonyeshwa kwenye  halaiki ya watu kwa kuwa yeye Nchimbi anasema hakuna diwani aliyetoka nje ya ukumbi huo na kura lakini kama hakuna diwani aliyetoka nje ya ukumbi na kura,Mariam  Dizumba kwa nini alitoka ndani ya ukumbi akikimbia na kwanini alipigwa ngwala na kudondoka na kwa nini aliondoka wakati kikao hakijafungwa?
 
Pia katika tamko lake anasema Meya aliyechaguliwa alifunga mkutano lakini ukweli ni kwamba mkutano au kikao hicho hakikufungwa hivyo kiliparaganyika baada ya utaratibu mzima na kanuni za uchaguzi huo kuvurugwa kwa kuwa aliyetakiwa kutangaza matokeo hayo ni Mkurugenzi wa Manispaa na si Naibu Meya ambaye ni mpigakura kwenye uchaguzi huo na pia ana maslahi.
 
Wachambuzi wa masuala ya siasa wanahoji ni kwa nini CCM Songea Mjini imetoa mapendekezo ya  kuwafukuza uanachama madiwani watano kati ya  saba waliopiga kura za hapana dhidi ya Mhagama wakati mwaka 2007 hawakumchukulia hatua Mariam Dizumba ambaye alipiga kura ya hapana kwa Elizabeti Ngongi ambaye alishinda unaibu meya kwenye uchaguzi wa mwaka huo na akaenda mahakamani kuzuia uchaguzi huo.
 
Katika sakata la mwaka huo Manispaa hiyo ilikaa bila Naibu Meya kwa miezi mitano hadi pale nafasi hiyo alipopewa Mariam Dizumba ambaye alishindwa na ndipo akaamua kufuta  kesi sasa  madiwani hao watano na huyu aliyekishtaki Chama chake,Mkurugenzi na Elizabeti Ngongi yupi mwenye kosa kubwa?
 
Anaendelea kusema katika tamko lake’mkutano huu wa  madiwani ulirekodiwa kwa picha za video,mikanda ya picha hizo ipo inaweza kupatikana kwa ushahidi’anasema.Lakini picha hizo za video zinaonyesha akizomewa kwa kuitwa mwizi wa kura na huku akielezwa kuwa ni aibu kwake kusimamia wizi wa kura na kama alionyeshwa picha hizo basi alionyeshwa sehemu tu ya picha za tukio.
 
Lakini ni katika mkutano huo ndipo alipobanwa na waandishi wa habari athibitishe ujinga na upumbavu wao na ikiwa atashindwa kufanya hivyo afute kauli yake na atoe ufafanuzi kuhusu madai yake kwamba habari hizo zimeandikwa na mtu mmoja na kwamba katika tukio hilo amemdhalilisha Rais kwa nini asijiuzulu kwa kumdhalilisha Rais aliyemteua?
 
Nchimbi  alishindwa kuyajibu maswali hayo na kupandwa na jazba na kutoa maelezo ambayo hayahusiani na maswali aliyoulizwa na kushusha heshima yake.
 
Wakati hali ikiwa hivyo Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA)Mkoa wa Ruvuma Joseph Fuime anasema kuwa kwa tukio lile ingekuwa enzi ya Mwalimu Nyerere Nchimbi angejiuzulu.
 
Akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Shule ya msingi mfaranyaki maarufu kama Soko la samaki  Fuime alisema ni aibu kwa Manispaa ya Songea ambayo ni maskini kumchagua Meya aliyedai kuwa ni mwizi aliyehusika na uuzaji wa greda kwa shilingi milioni 18, na ununuzi wa gari bovu la Zimamoto kwa shilingi milioni 350 ambapo  Mhagama alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo alisema greda liliuzwa kwa kufuata sheria zote na kuhusu gari bovu la Zimamoto halimuhusu kwani magari hayo yalinunuliwa saba Nchi nzima.
 
Alisema huo ni mpango wa wabunge kuwaweka watu wao kwenye nafasi za uongozi ili waibe fedha na kwamba walifanya makosa kumchagua Nchimbi na wangemchagua aliyekuwa mgombea wa Chadema Edson  Mbogoro asingewaletea Meya mwizi.’Anamtaka Meya huyo ili ajinufaishe na mimi nasema Charles Mhagama atakuwa Meya wa Mbunge si wa madiwani na akipita mitaani mumzomee Meya huyo’alisema.
 
Alisema hiyo ni aibu kwa Rais aliyemteua na kwamba Chama Chake kimejipanga kuzunguka kata zote 21 kueleza ubaya wa Nchimbi  na mwenendo mzima wa uchaguzi wa Meya na kueleza kuwa Manispaa hiyo haina Meya hivyo baada ya mikutano hiyo watafanya maandamano makubwa ya kupinga uchaguzi huo na kumpinga Meya huyo na kuvigeuza viwanja vya manipsaa hiyo kuwa Tahariri Squere ambavyo vilim’ngoa madarakani aliyekuwa Rais wa Misri Hosni Mubarak.
 
Hivyo basi ili kunusuru vurugu zitakazotokea kwenye maandamano yanayotarajiwa kufanyika ni wazi basi inatakiwa kurudia uchaguzi kwa kuwa uchaguzi uliofanyika ulikiuka utaratibu na CCM wana wasiwasi gani kurudia uchaguzi?Hapa ndipo Intelejensia ya Polisi  inapaswa kufanya kazi kunusuru hali ya hewa  ili yasije yakatokea mauaji  kama yale yaliyotokea Arusha.
 
Mapendekezo ya CCM Wilaya ya Songea kufukuza madiwani waliopiga kura za hapana kwa mgombea wa Chama hicho yamepokelewa na Chama hicho Mkoa wa Ruvuma ili yaweze kutolewa maamuzi na Katibu wa Chama hicho Mkoa huo Emmanuel Mteming'ombe amesema Kamati ya maadili ya Chama hicho imewahoji madiwani hao ambao anasema kwenye Kamati ya siasa Wilaya hawakusikilizwa na kamati ya siasa Mkoa itatoa uamuzi wa kuwafukuza au kutowafukuza.
 
Hata hivyo wachunguzi wa mambo wa siasa wanasema madiwani hao hawatafukuzwa na kamati hiyo kwa kuwa ni kiongozi mmoja pekee na genge lake ndiye anayeshinikiza wafukuzwe na kwamba hawajafanya kosa linalofanya wafukuzwe na  ikiwa watafukuzwa kwa upepo wa siasa Songea upande wa chama hicho si mzuri na kata hizo zinaweza kudondokea upinzani.
 
Hivi karibuni CCM Wilaya ya Songea mjini iliitisha kikao na madiwani wake kwa ajili ya kusafisha hali ya kisiasa ambayo imechafuka lakini hakikuweza kufanyika kutokana na madiwani kukisusia kwa kile kinachodaiwa kuwa ni mgomo wa kudumu kushinikiza kujiuzulu kwa Meya huyo anayedaiwa kupitishwa kwa mizengwe huku nguvu ya kigogo mmoja ikitajwa kuhusika.
 
Lakini pia katika kikao hicho madiwani waliopendekezwa kufukuzwa waliitwa na walifika wakiwa na kadi zao mfukoni tayari kwa kuzikabidhi ikiwa wataambiwa watoke kwenye Chama hicho. 
 
Katibu wa CCM wa Wilaya ya Songea mijini Alphonce Siwale alipohojiwa kuhusu kuitishwa kwa kikao hicho alithibitisha kukiitisha na kusema kuwa kilishindikana kufanyika kutokana na mahudhurio hafifu ya madiwani ambao hawakufika hata nusu.
 
Alisema kuwa madiwani wengi walishindwa kuhudhuria kikao hicho kwa kuwa walikuwa safarini na kwamba kitafanyika tena kitakapopangwa na  kilipaswa kusafisha hali ya hewa iliyochafuka kutokana na uchaguzi wa Meya.
 
Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa anapaswa kumuondoa Nchimbi kwenye nafasi ya Uwaziri wa habari,utamaduni na michezo kwani kwa tukio lile alimdhalilisha   na aibu ile itamfuata Nchimbi kokote atakakokwenda iwe Dares salaam,Dodoma,Mbeya na Songea hivyo basi aibu ya Nchimbi ni aibu ya Kikwete aliyemteua.
  
MWISHO

Friday, October 7, 2011

NI NGUMU KUAMINI,LAKINI ASHIKILIWA NA POLISI KWA KUSABABISHA KIFO AKILAZIMISHA PENZI

Na Mwandishi Wetu, Songea
JESHI la Polisi Mkoani Ruvuma limemtia mbaroni Elly Millinga (33) Mkazi wa Kijiji cha Matiri Wilayani Mbinga kwa tuhuma za kumchoma kisu sehemu za tumboni Mzazi mwenzake Florida Mhaiki (26) Mkazi wa mtaa  wa Masumuni Mbinga mjini ambaye anadaiwa alikataa kufanya nae mapenzi
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Naftan Mantamba alisema kuwa tukio hilo lilitokea Octoba 7 mwaka huu majira ya saa 6.30 huko katika Mtaa wa Masumuni Mbinga mjini.
Mantamba alifafanua kuwa siku hiyo ya tukio Florida alichomwa kisu sehemu za tumboni na mzazi mwenzake Millinga ambaye alifika nyumbani kwa Florida majira ya saa za jioni ya Octoba 6 mwaka huu na kuanza kuongea nae kwa lengo la kumshawishi mzazi mwenzake waendelee kuishi kama mke na mume
Ameeleza zaidi kuwa Millinga pamoja na kutoa ushawishi huo Florida alikataa katakata na kudai kuwa watoto wawili aliozaa nae ameshindwa kuwahudumia hivyo hakuna sababu yeyote ya msingi ya kuridhia kurudiana na Millinga.
Amesema kuwa ilipofika majira ya saa 3 usiku ya Octoba 6 mwaka huu usiku Florida alimweleza mzazi mwenzake Millinga kuwa muda wa kwenda kulala umefika hivyo aliamua kumpatia nafasi ya kulala chumba ambacho kipo uani mwa nyumba kubwa na Millinga alienda kulala.
Amefafanua zaidi kuwa ilipofika saa 6 usiku Millinga aliamka na kwenda hadi kwenye chumba ambako Florida alikuwa amelala na kumtaka amfungulie mlango na baada ya kuingia aliendelea kumsihi Florida ili akubaliane na ombi alilomweleza hapo awali lakini ombi hilo halikuweza kukubalika ndipo Millinga alipoamua kuchukua kisu mfukoni na kumchoma sehemu za tumboni.
Ameeleza zaidi kuwa Florida baada ya kuchomwa kisu na mzazi mwenzake alipiga kelele kwa lengo la kupata msaada majirani walifika kwenye eneo la tukio na kumkuta Florida akiwa kwenye hali mbaya na kwenye chumba chake kulikuwa kumetapakaa damu.
Amesema kuwa majirani walimchukua Florida na kumkimbiza kwenye hospitali ya Serikali ya Mbinga kwa matibabu ambako alifari dunia wakati akiwa anaendelea kupata matibabu na polisi baada ya kupata taarifa ya tukio hilo walikwenda kwenye eneo la tukio na walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa Millinga ambaye kwasasa anaendelea kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo.
MWISHO

Thursday, October 6, 2011

AJINYONGA KWA KUMKATAA MKE MWENZA WILAYANI MBINGA


 Na Gideon Mwakanosya, Songea
MWANAMKE  mmoja Apolonjali Hyera (45) Mkazi wa Kitongoji cha Mapendano kilichopo katika Kijiji cha Mzuzu Wilayani Mbinga amekufa kwa kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani baada ya mume wake kuoa mwanamke mwingine.
Habari zilizopatikana jana mjini hapa ambazo zimethibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Naftani Mantamba zimesema kuwa tukio hilo limetokea Octoba 5 mwaka huu majira ya saa 6 mchana huko katika Kitongoji cha Mapendano kilichopo katika Kijiji cha Mzuzu Wilayani Mbinga.
Mantamba amesema kuwa siku hiyo ya tukio inadaiwa Apolonjali alikutwa akiwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya katani  kwa kujining’iniza juu ya mti kwenye msitu mkubwa wa Kijiji hicho.
Ameeleza zaidi kuwa Apolonjali anadaiwa kuwa aliamua kujinyonga baada ya kumtuhumu mume wake kuamua kuoa mwanamke mwingine wakati yeye ametoka nyumbani kwa wazazi wao na yupo kwaajili yake hivyo alikuwa akijiuliza ni kwanini ameamua kuchukua uamuzi huo.
Amefafanua zaidi kuwa kutokana na kuwepo kwa mvutano huo kati yake na mume wake Kelvin Sesilisi (45) ndiyo aliamua kuchukua uamuzi wa kujiua na kuacha maagizo kuwa ameamua aondoke amuache mwanamke aliyempata
Mantamba amesema kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi ambao umemsababishia Apolonjali kufikia uamuzi wa kujiua kwa kujinyonga kwa kujining’iniza kwenye mti uliopo katikati ya msitu

ANYWA SUMU,AFARIKI BAADA YA KUONYWA KUACHA UASHERATI MBAMBABAY

Na Mwandishi Wetu,Songea
JANETH Mwanjali ni msichana mwenye umri wa miaka 15 mkazi wa mji mdogo wa Mbamba bay uliopo Wilayani Nyasa Mkoa wa Ruvuma amefariki dunia baada ya kunywa dawa ya kuulia panya iliyokuwa imehifadhiwa nyumbani kwa wazazi wake.
Akizungumza na mtandao huu wa http://www.stephanomango.blogspot.com/  Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Naftani Mantamba amesema kuwa tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 4 asubuhi nyumbani kwa wazazi wa Janeth.
Mantamba amesema kuwa siku hiyo kabla ya tukio kutokea  inadaiwa kuwa Janeth aliitwa na mama yake mzazi Anna Kalima ambaye alikuwa akimuonya aache tabia ya kulala kwa wanaume na baadaye ulitokea ugomvi kati yake na mama yake ambaye alikuwa akimtuhumu kuwa anamuonea wivu kisha alikwenda ndani ya nyumba na kutafuta dawa ya kuulia panya ambayo aliinywa.
Amesema kuwa baada ya kuinywa dawa hiyo muda mfupi alianza kubadilika na hali yake ikawa mbaya hivyo mama yake mzazi aliamua kumchukua na kumpeleka hadi Kituo cha afya cha Mbamba bay ambako muda mfupi baadaye alifariki dunia akiendelea kupatiwa matibabu.
Mantamba amesema kuwa Chanzo cha tukio hilo ni kwamba Janeth alikuwa amegombana na mama yake mzazi aliyekuwa akimkanya kuwa aache tabia ya kulala nje kwa wanaume jambo ambalo lilimtia hasirá na kuchukua uamuzi wa kutafuta dawa ya kuulia panya na kunywa kwa lengo la kujiua.
Hata hivyo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mantamba ameeleza kuwa kwasasa Polisi wanaendelea kufanya upelelezi wa kina kuhusiana na tukio hilo licha ya kuwa Upelelezi wa awali umebaini kuwa Janeth alipandwa na hasira wakati anaonywa na mama yake mzazi.

Wednesday, October 5, 2011

MADIWANI WA CCM SONGEA WASUSIA KIKAO CHA CHAMA CHAO NA WENGINE WAWATUPIA MADONGO VIONGOZI WAO

Na Mwandishi Wetu,Songea
MADIWANI wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Songea Mjini wamesusia kikao kilichoitishwa na viongozi wa Chama hicho Wilaya kwa kile kilichodaiwa ni mgomo wa kudumu kushinikiza kujiuzuru kwa Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Charles Mhagama
Wakizungumza na waandishi wa habari jana kwa nyakati tofauti nje ya Ofisi ya Chama hicho ambapo kikao hicho kilipangwa kufanyika walisema kuwa wameshtushwa na taarifa ya kuitwa kwenye kikao hicho bila kuelezwa ajenda zake wala muda wa kukaa kikao hicho
Walisema kuwa wamefika kwenye kikao hicho wameshindwa kuwaona baadhi ya viongozi wa Chama hicho ambao ndio waliowaita kitendo ambacho kinaonyesha ni dharau dhidi ya madiwani
 Baadhi ya Madiwani hao Christian Matembo wa Kata ya SeedFarm,Kurabest Mgwasa wa Kata ya Msamala na Faustine Mhagama wa Kata ya Mshangano walisema kuwa kiu kubwa ya Madiwani ni kutaka kuona Charles Mhagama ambaye anadaiwa kuwa ni Mstahiki Meya anajiuzuru ili uchaguzi mpya uitishwe kwani kura alizopata wakati wa uchaguzi hazikuwa halali
“Tumechoka kuogopana ndani ya chama kwa kuwaacha wachache wanawaburuze wengi kwa maslahi yaliyojificha kwani hatuwezi kuvumilia vitendo vya uvunjifu wa demokrasia vya kuwatisha madiwani waliotimiza haki yao ya kupiga kura za hapana kwenye uchaguzi wa umeya uliopita hivi karibuni kwa kuwaita ni wasaliti wa chama”alisema Matembo
Alisema kuwa Madiwani wengi wamempigia kura za hapana Charles Mhagama lakini tunashangaa kuona mtu huyo anatembelea gari ya Mstahiki Meya na kufanya kazi kama Meya wakati siku ya kupiga kura uchaguzi ulivurugika na kusababisha madiwani kushikana kutokana na kumkataa Mhagama
Diwani wa Kata ya Mshangano Faustine Mhagama ambaye pia ni Katibu wa Madiwani wote wa Ccm alisema kuwa kitendo cha Viongozi wa Ccm Wilaya cha kupendekeza Madiwani watano wa Chama hicho wavuliwe uanachama ni kuongeza mpasuko ndani ya chama kwani kura walizopiga zilikuwa za siri hivyo kuwahukumu hao ni kuwanyanyasa na kuwanyima haki zao za msingi
Mhagama alisema kuwa kanuni za kudumu za Halmashauri zina eleza kuwa jambo lolote litakalo fanyika kwenye kikao cha Baraza la Madiwani halipaswi kuhojiwa wala kujadiliwa na mamlaka nyingine hivyo Ccm Wilaya ya Songea Mjini kupitia Kamati ya Maadili na y a Siasa kuwahoji Madiwani kwa kile kilichotokea kwenye Baraza ni kukiuka kanuni na kusababisha utendaji wa kosa kwa makusudi na kuendekeza makundi bila sababu ya msingi
“Ili kulinda heshima ya Chama ni Vema Charles Mhagama aridhie kujiuzuru nafasi hiyo ili uchaguzi urudiwe upya badala ya kuwanyanyasa baadhi ya Madiwani wanaodaiwa kupiga kura za hapana na kupelekea Diwani huyo kupitishwa kwa kura za hapana 14 na za ndiyo 12”alisema Mhagama
Alisema kuwa Madiwani wataendelea kususia vikao vitakavyoitishwa na Chama na Halmashauri ya Manispaa ya Songea mpaka uitishwe uchaguzi mwingine ambapo Madiwani watamchagua kiongozi watakaomuona anafaa na sio kulazimishiwa kiongozi
Naye Diwani wa Kata ya Msamala Kurabest Mgwasa alisema kuwa Ccm Wilaya imependekeza Madiwani watano wavuliwe uanachama ambapo hatma yao ipo kwenye ngazi ya Chama hicho Mkoa lakini cha kushangaza Madiwani hao nao wameitwa kwenye kikao hicho jambo ambalo lingeweza kuleta vurugu kubwa
Kwa upande wa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Songea Mjini Alfonce Siwale alikiri kuitisha kikao hicho ambacho kilipaswa  kifanyike jana lakini kilishindikana kutokana na mahudhurio hafifu ya Madiwani ambao hawakufika hata nusu yao
Siwale alisema kuwa kikao hicho kilikuwa na agenda za kutaka kurudisha hali ya hewa sawa kutokana na vurugu za uchaguzi wa umeya uliofanyika Septemba 23 mwaka huu ambao haukumalizika
Alisema kuwa Madiwani wengi wameshindwa kuhudhuria kikao hicho kwa kuwa wapo safarini na hivyo kikao hicho  kimepangwa kufanyika Octoba 11 katika ofisi za Chama hicho na kueleza kuwa Madiwani hao hawana mgomo wowote
Alieleza kuwa Chama hicho kina Madiwani 21 lakini waliofika kwenye kikao hicho walikuwa nane na kufanywa kikao hicho kutofanyika na kwamba kwenye kikao hicho Madiwani waliopendekezwa kufukuzwa na chama ndio waliojitokeza kwa wingi
MWISHO





Tuesday, October 4, 2011

TAKUKURU WAMNASA AFISA MTENDAJI WA KATA WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SONGEA KWA RUSHWA KIDUCHU

Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Shule ya Tanga Expedito Luambano(aliyesimama)
Na Mwandishi Wetu ,Songea
TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Mkoani Ruvuma inamshikilia Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Shule ya Tanga iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya shilingi 20,000 kutoka kwa mwananchi ambaye jina lake limehifadhiwa wa Kata hiyo ambaye alikwenda Ofisini kwake kuomba asaidiwe kulipwa deni toka kwa Mfanyabiashara mmoja ambaye naye jina lake limehifadhiwa.
Akizungumza na mtandao huu wa www.stephanomango.com Ofisini kwake Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Mkoani Ruvuma Daudi Masiko amesema tukio hilo limetokea Octoba 2 mwaka huu majira ya saa za mchana huko kwenye eneo la nane nane Msamala Songea Mjini.
Masiko amemtaja anayeshikiliwa na Takukuru kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya shilingi elfu 20,000 Expedito Luambano (36) ambaye ni Kaimu Afisa Mtendaji wa Shule ya Tanga ambapo amebainisha zaidi kuwa siku chache zilizopita Luambano akiwa Ofisini kwake alifikiwa na mwananchi mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa ambaye alikuwa anataka asaidiwe na Ofisi hiyo ili Mfanyabiashara anayemdai aweze kumlipa deni ambalo ni la muda mrefu.
Amefafanua zaidi kuwa mwananchi huyo akiwa kwenye Ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata hiyo alishawishiwa na Luambano kuwa atafute shilingi elfu 20,000 ili aweze kumsaidia kumsaka Mfanyabiashara huyo anayemdai aweze kulipwa deni .
Ameeleza kuwa mwananchi huyo alikubaliana na maelezo aliyopewa na Luambano kisha alitoka kwenye Ofisi hiyo kwa makubaliano kuwa wangekutana kwenye eneo la nane nane lililopo Msamala kwenye bar iliyopo kwenye eneo hilo.
Amesema kuwa mwananchi huyo baadae alishtuka na kupata wazo kwenda kwenye Ofisi za Takukuru ambako alitoa taarifa na kuwaeleza kwa kina juu ya maelezo aliyopewa na Afisa Mtendaji Luambano ambapo baadae Maafisa wa Takukuru waliweka mtego kisha walimtaka mwananchi huyo awasiliane na Afisa Mtendaji mahali watakapokutana kupeana fedha hizo.
Mkuu wa Takukuru Mkoani Ruvuma Masiko amesema kuwa baada ya mwananchi huyo kufanya mawasiliano na Afisa Mtendaji  Luambano Takukuru ilimpatia fedha shilingi elfu 20,000 na kumtaka ande mahali walipokubaliana kupeana fedha hizo huku maafisa wa Takukuru wakiwa wanamfuatilia kwa karibu na walipofika kwenye eneo la tukio alimkuta Luambano akiwa anamsubiri kwenye bar ambako alimkabidhi fedha hiyo na baada ya muda mfupi maafisa wa Takukuru waliizingira bar hiyo na kumkuta Luambano akiwa na fedha shilingi elfu 20,000 aliyopewa na mwananchi huyo ambaye jina lake limehifadhiwa.
Amefafanua zaidi kuwa Luambano ambaye pia ni Afisa Mtendaji wa Serikali wa Mtaa wa Tanga anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa kwa tuhuma za  kuomba na kupokea rushwa ya shilingi elfu 20,000 ambayo ni kosa chini ya kifungu cha 15 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007
MWISHO

MAJAMBAZI WAPORA,WAJERUHI ABIRIA NA KUSABABISHA KIFO CHA MTOTO

Na Mwandishi Wetu,Songea.
JESHI la Polisi Mkoani Ruvuma linawasaka majambazi wawili ambao walivamia gari lililokuwa limebeba abiria 14 kutoka Mbamba bay kwenda Mbinga na kufyatua  risasi tano ambazo ziliwajeruhi watu wawili akiwemo mtoto wa umri wa mwaka mmoja na nusu  ambaye alikuwa amepigwa risasi kwenye mguu wa kushoto akiwa amebebwa na mama yake mzazi kisha majambazi hao walifanikiwa kuwapora abiria fedha Shilingi 930,000 na baadaye walikimbia na kutokomea kusikojulikana.
Akizungumza na mtandao huu wa www.stephanomango.blogspot.com  Ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda amesema kuwa tukio hilo lilitokea Octoba 3 mwaka huu majira ya saa 1.30 asubuhi  huko katika Kijiji cha Ng’ombo kilichopo katika Kata ya Kilosa Wilaya ya Nyasa .
Kamuhanda amesema kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio Dereva wa gari lenye namba za usajili T 554 ASE Toyota Hilux Joseph Hamza (35) akiwa  anaendesha  gari  hilo lililokuwa na abiria 14 waliokuwa wanatoka Mbamba bay kuelekea Mbinga Mjini akiwa katikati ya daraja ghafla aliwaona watu wawili wakiwa wamefunga vitambaa usoni huku wakiwa na Bunduki mbili ambao walilivamia gari hilo kisha walianza kufyatua risasi hewani ambazo ziliwajeruhi abiria wawili .
Amefafanua kuwa watu hao wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi ambao walikuwa na siraha za SMG na SAR  waliwapiga risasi Rehema Haule (11) ambaye alijeruhiwa  vibaya kwenye mguu wa kushoto wakati akiwa amebebwa na mama yake mzazi na Castory Kinunda (31) Mkazi wa Mbamba bay alijeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi na majambazi hao kwenye mkono wa kushoto .
Amebainisha zaidi kuwa  majambazi hao baada ya kufyatua risasi hewani walianza kuwapekua abiria mmoja hadi mwingine ambapo baadae walifanikiwa kuwapora abiria hao shilingi 930,000 na baada ya kuwanyang’anya fedha hizo walikimbia na kutokomea porini .
Alieleza zaidi kuwa majeruhi Rehema baada ya kupigwa  risasi kwenye mguu wa kushoto alikimbizwa katika Hospitali ya Misheni ya Liuli ambako alifariki dunia muda mfupi wakati akiendelea kupata matibabu na majeruhi  Kinunda  kwasasa hivi amelazwa katika hospitali ya Serikali ya Mbinga akiendelea kupata matibabu na hali yake bado ni mbaya.
Kamanda Kamuhanda amesema kuwa Polisi baada ya kupata taarifa ya tukio hilo walienda kwenye eneo la tukio na kuwakuta baadhi ya  abiria ambao walielezea tukio hilo lilivyotokea na kwamba upelelezi wa awali umefanyika ambao umebaini kuwa majambazi hao wametokea Kyela Mkoani Mbeya kwa kupitia Ziwa Nyasa.
MWISHO

VIONGOZI WA DINI WAOMBWA KUWANUSURU WANAFUNZI WA MTONYA NA MAPEPO

Na Augustino Chindiye,Tunduru

SHULE ya Msingi Mtonya Wilayani Tunduru imefungwa kwa muda usiojulikana ili kuwapisha Wazee wa mila,Mapadre na  Mashehe ili wawasaidie kuomba na kuyaondoa Mapepo ambayo yamekuwa yakisababisha Wanafunzi wanaosoma katika Shule hiyo kupatwa na homa ya kuchanganyikiwa na kuanguka wakati wa masomo.

Amri ya kufungwa kwa Shule hiyo imetolewa na Afisa elimu wa Shule za Msingi Mwl. Rashid Mandoa baada ya juhudi za maafisa tabibu kutoka katika Hospitali ya Wilaya ya Tunduru kushindwa kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo.

Mwl. Mandoa aliendelea kufafanua kuwa tatizo la kuanguka na kupoteza fahamu kwa wanafunzi hao limekuwa likiongezeka siku hadi siku ambapo awali idadi ya watoto waliokuwa wakianguka walikuwa ni kati na watoto mmoja na watano lakini hivi sasa tatizo hilo limefikia zaidi ya watoto hamsini kwa siku.

Alisema kufuatia hali hiyo wazazi wa watoto wanaosoma katika shule hiyo walikuwa wakilazimika kufuatana na watoto wao na kupiga kambi pembezoni mwa shule wakiwa na lengo la kuwasaida watoto watakao kumbwa na homa hiyo.

Alisema ingawa Serikali haiamini mambo ya ushirikina lakini idara yake imechukua maamuzi hayo baada ya kubaini kuongezeka kwa matukio hayo na kwamba endepo tatizo hilo litaachiliwa liendelee kuna
hatari ya kushusha kwa taaluma za wanafunzi kutakakosababishwa na kushuka kwa ari ya wanafunzi kutopenda masomo.
Mwisho.

BUNGE LATAKIWA KUHAKIKISHA SUALA LA PENSHENI KWA WAZEE LINAINGIZWA KWENYE BAJETI YA TAIFA

  Mzee huyu ni miongoni mwa watu wanaotakiwa kupewa matibabu bure na pensheni nchini ili aweze kujikimu na maisha yake

Na Augusino Chindiye, Tunduru
BUNGE la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania limeahidi kusimamia na kuhakikisha kuwa mpango wa kuanza kuwalipa pensheni  wazee hapa nchini unaingizwa katika Bajeti ya Bunge lijalo na kuanza kulipwa mapema 2012.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru  Juma Madaha akiwa ananukuu Hotuba iliyokuwa imeandaliwa na Mwenyekiti wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  Jenista Mhagama ambaye alitakiwa kuwa mgeni Rasmi katika maadhimisho ya siku ya Wazee Duniani iliyofanyika katika viwanja vya Baraza la Iddi Mjini Tunduru.

Akifafanua taarifa hiyo Dc,Madaha alisema kuwa Mhagama kwa kushirikiana na Wabunge wenzake wakiwemo wabunge kutoka Mkoa wa Ruvuma ameahidi kutoa msukumo mkubwa na kuhakikisha kuwa mswada wa kuanza kuwalipa Pensheni unatungiwa sheria mapema iwezekanavyo ili wazee wa Tanzania waanze kunufaika na mafao hayo.

Hotuba hiyo iliendelea kueleza kuwa wakati Wabunge hao wakishughulikia tatizo hilo tayari Serikali imeanza kuweka msukumo wa kuendelea kuwahudumia Wazee kote nchini waanze kupata huduma za Matibabu bure kupitia mkakati wa kuwaagiza Waganga wakuu wa Hospitali zote nchini kutenga vyumba maalumu vya kutolea huduma hiyo kwa wazee zikiwa ni juhudi za kuwaondolea kero na foleni.

Alisema Sambamba na kuwepo kwa zoezi hilo pia Hotuba hiyo ilieleza kuwa tayari Serikali pia kupitia Wakuu wa Wilaya kote nchini wamewaagiza watenzaji wa Vijiji kutekeleza agizo la kuwaandikia Wazee barua zitakazo wafanya watambuliwe na kuanza kupatiwa huduma za matibabu bure kuanzia ngazi za Zahanati,Vituo vya afya na Hospitali.

Awali akisoma Risala ya Wazee katika madhimisho hayo Katibu wa Chama cha Wazee wa Wilaya ya Tunduru (HAWATU) Jafari Msonjele alisema kuwa pamoja na kundi hilo kukabiliwa na changamoto nyingi za kimaisha Wazee wengi kote nchini wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kulea kundi kubwa la Watoto yatima ambao wengi wao wameachwa na ndugu,jamaa na Watoto wao waliopoteza maisha kutokana na ugonjwa wa Ukimwi.

Wazee hao pia katika taarifa yao wakagusia changamoto kubwa ya kitaifa inayo wakabiri wazee wenzao wastaafu ambao wamekuwa wakiyumbishwa kwa muda mrefu kulipwa pensheni zao na mashirika ya PPF,PSPF, na LPF na wakatumia nafasi hiyo kuyaomba mashirika hayo kuridhia maombi ya wanachama wake ya kuanza kuwalipa wanachama wake malipo ya mwezi mmoja, Mitatu na Sita bila kupitisha muda wake pamoja na kuangalia uwezekano wa kama kuna nyongeza basi iongezwe kwa wanachama wote  ili kuwapunguzia makali ya maisha.

Nae Mwenyekiti wa Chama hicho Said Kabora akitoa neno la shukurani wakati wa kufunga maadhimisho hayo pamoja na kulipongeza Bunge kwa kauli hiyo alisema kuwa Wazee bado wanayo imani na serikali yao na wana amini kuwa macho hayo yaliyo ahidiwa kwa vipofu na chombo kinacho wawakilisha katika utoaji wa maamuzi yatatekelezeka na kuwafanya wazee kote nchini kufurahia matunda ya nchi yao. 
  Mwisho

Sunday, October 2, 2011

UCHAGUZI WA UDIWANI KATA YA MATIMIRA CCM WAIBUKA KIDEDEA

                Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Peramiho Anna Mbogo

Na Mwandishi Wetu,Songea
Mtandao huu wa www.stephanomango.blogspot.com umefanikiwa kupata matokeo ya uchaguzi wa Udiwani Kata ya Matimila Wilaya ya Songea Vijijini ambapo Chama cha Mapinduzi(CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)walisimamisha wagombea
Matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika Octoba 2 mwaka huu 2011 ambayo yamethibitishwa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Peramiho ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Songea Vijijini Anna Mbogo ni kuwa mgombea wa nafasi hiyo kutoka CHADEMA ,Eleuterius Kasmir Pili amepata kura 923 na mgombea wa CCM ,Menas Cosmas Komba amepata kura 1386
Kwa matokeo hayo,mtandao huu unaungana na wananchi wote wapenda maendeleo kumpongeza mshindi aliyeibuka kidedea katika uchaguzi huo,pia unatoa pole kwa wale wote waliojeruhiwa kwa namna moja au nyingine katika harakati za uchaguzi huo
Mungu awabariki na kuwapa nguvu wale walioumia kutokana na vurugu zilizojitokeza wakati wa kampeni na wakati wa kusubiri majibu
Mtandao huu una laani vikali nguvu za ziada zilizokuwa zinatumika na vyama vyote viwili ambavyo vilisimamisha wagombea katika uchaguzi huo ulioacha majeruhi zaidi ya 12na kusababisha haki za binadamu kuvurugika na kuchafua demokrasia stahiki
Tunaendelea kuwasiliana na Waandishi wengine waliopo kwenye uchaguzi wa udiwani na ubunge huko Igunga ili tuweze kuwajuza habari za matokeo ya uchaguzi katika maeneo hayo
MWISHO

KAMATI YA MAADILI YA CCM MKOA WA RUVUMA YAWAHOJI MADIWANI WATANO KUHUSU SAKATA LA UMEYA

Na, Mwandishi Wetu,Songea

KAMATI ya Maadili ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma imewahoji Madiwani watano wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea ambao walituhumiwa na Chama hicho Wilaya ya Songea mjini kuwa wamekisaliti chama kwa kumpigia kura za hapana mgombea Umeya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

Kamati hiyo iliyokuwa na wajumbe Corneus Msuya ambaye ni Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Ruvuma,Emmanuel Mteming'ombe ambaye ni Katibu wa CCM mkoa wa Ruvuma,Henriet Ndimbo ambaye ni Katibu wa Uchumi na Fedha wa chama hicho mkoa, na Mama Litunu iliwahoji Madiwani hao ili kujiridhisha na tuhumu walizotuhumiwa nazo na CCM Wilaya ya Songea Mjini

Madiwani ambao wamehojiwa ni Christian Matembo(SeedFarm) Victor Ngongi(Ruvuma)Kurabest Mgwasa(Msamala) Faustine Mhagama(Mshangano) na Genfrida Haule diwani wa Viti Maalum wa chama hicho

Kwa mujibu wa Katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma Emmanuel Mteming'ombe akizungumza na mtandao huu wa http://www.stephanomango.blogspot.com/ alisema kuwa kikao hicho cha Maadili kilikuwa kinawapa fursa ya kujitete madiwani walihotuhumiwa

Mteming'ombe alieleza kuwa kimewahoji madiwani hao na chama kimetafakari tuhuma zao na majibu ambayo wamejitetea,baada ya hapo kitatoa onyo kwa madiwani wote akiwemo na Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Dkt Emmanuel Nchimbi kutokana na utomvu wa nidhamu aliouonyesha katika uchaguzi huo wa Umeya wa Songea mjini

Mtandao huu utaendelea kuwajuza wasomaji wake kila kitu kitakachojili bila kumuonea mtu,kumuogopa kwa wadhifa wake ili kuwawezesha wadau wa mtandao huu kujiridhisha na kutafakari viongozi wao waliopewa dhamana na wananchi walivyokuwa na tabia ya uroho wa madaraka kwa faida yao binafsi huku wakiwaacha wananchi wakiwa maskini wa kutupwa

Saturday, October 1, 2011

MADIWANI WA CCM WAITWA KWENYE KAMATI YA MAADILI YA CHAMA HICHO MKOA WA RUVUMA KUHOJIWA SAKATA LA UMEYA WA MANISPAA YA SONGEA

 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma Corneus Msuya
Katibu wa Ccm Mkoa wa Ruvuma Emmanuel Mteming'ombe

Na Mwandishi Wetu,Songea

MADIWANI wote wa Chama cha Mapinduzi Halmashauri ya Manispaa ya Songea wameitwa kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya Chama hicho Mkoa wa Ruvuma kuhusiana na sakata la uchaguzi wa umeya uliofanyika septemba 23 mwaka huu

Awali Kamati ya siasa ya Halmashauri kuu ya chama hicho wilaya ya Songea Mjini ilipendekeza madiwani watano wa Chma hicho wafukuzwe uwanachama kwa madai kuwa wamekidhalilisha chama katika uchaguzi huo kwa kumpigia mgombea wa nafasi ya Umeya Charles Mhagama kura za ndiyo 14 za hapana n kura 12

Baada ya chama hicho kupendekeza hivyo, kamati ya Siasa ya CCM mkoa wa Ruvuma ilikutana katika kikao chake cha ghafla na kujadili mapendekezo hayo ili kupata muafaka stahiki

Leo chama hicho kimewaita Madiwani wake wote na kuwahoji katika kikao cha maadili,mengi yatakayojili mtandao huu wa http://www.stephanomango.blogspot.com/ utaendelea kukujuza

Friday, September 30, 2011

HATMA YA KUFUKUZWA UWANACHAMA MADIWANI WATANO SONGEA MJINI MIKONONI MWA KAMATI YA SIASA YA HALMASHAURI KUU YA CCM MKOA WA RUVUMA

                       
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Songea Mjini Hemed Dizumba
                        
Katibu wa CCM wilaya ya Songea Alfonce Siwale
Na  Mwandishi Wetu,Songea
CHAMA cha  Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Songea mjini Mkoa wa  Ruvuma  kimetoa mapendekezo ya kuwafukuza uanachama wa chama hicho  madiwani  watano kwa madai ya kukiuka taratibu za chama hicho kwa kupiga kura za hapana kwa mgombea wa umeya Bw. Charles Mhagama anayedaiwa kupitishwa kwa kura za hapana 14 na za ndiyo 12.
Katika kikao cha kamati ya siasa kilichokaa hivi karibuni ambacho kolikuwa na ajenda tatu ikiwemo agenda ya kufungua mkutano,kupata taarifa ya kamati ya maadili ya Ccm Wilaya kuhusu uchaguzi wa Umeya uliofanyika Septemba 23 mwaka huu na kufunga mkutano ambapo Madiwani hao katika kikao cha kwanza cha maadili walitishia kurudisha kadi za chama hicho kutokana na kutoridhishwa na muenendo wa chama hicho unaotokana na kuvurugwa na kigogo mmoja wa ngazi ya Serikalini
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sakata hilo jana ofisini kwake Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Songea Alfonce Siwale alikiri kufanyika kwa vikao hivyo viwili cha maadili na kamati ya siasa na kudai kuwa madiwani wote wa chama hicho walihojiwa kuhusu mwenendo wa uchaguzi wa Umeya
Siwale alisema kuwa baada ya kikao cha maadili kuwahoji madiwani wote ndipo kamati ya siasa ya halmashauri kuu ya wilaya ilipoketi na kujadili kwa kina kilichojili kutoka kwenye kamati ya maadili kuhusiana na uchaguzi huo

Katibu huyo alieleza kuwa kuna mambo mengi yamejadiliwa kwenye kikao hicho pamoja na mwenendo wa chama baada ya uchaguzi huo wa Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea uliokitia doa chama cha Ccm na kumdharirisha Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Dkt Emmanuel Nchimbi
Alipotakiwa na waandishi wa habari kueleza kilichojadiliwa kwenye kikao hicho,Siwale alieleza  kuwa kanuni za chama hicho zinaeleza kuwa kinachojadiliwa na Kamati ya Siasa ya halmashauri kuu ya Wilaya kinakuwa siri kwani mambo yake mengi yanawasilishwa kwenye Kamati ya Siasa ya chama hicho mkoa ili kiweze kuyajadili na kuyatolea maamuzi hivyo wao ndio wanaweza kutoa taarifa sahihi kwa kile tulichowapelekea kutoka Wilayani
Alipoulizwa kuhusu habari zilizozagaa mitaani kuwa Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Dkt Nchimbi ndiye aliyeshinikiza kurudishwa jina la Diwani wa kata ya Matogoro Charles Mhagama na Madiwani wawili wa Viti Maalum ,alikanusha kuwa sio kweli na kama mtu anaushahidi wa hilo basi ieleweke alifanya hivyo kwa ushawishi wa kawaida wa uchaguzi
Kwa upande wake wa Katibu wa Ccm Mkoa wa Ruvuma Emmanuel Mteming”ombe alipohojiwa na waandishi wa habari kuhusiana na sakata hilo alisema kuwa wamepokea mapendekezo kutoka Ccm Wilaya ya Songea Mjini  ya kuwafukuza madiwani watano wa chama hicho na Kamati ya Siasa ya Ccm Mkoa inaendelea na vikao vyake ili kuweza kufikia hitimisha la sakata hilo
Mteming”ombe alisema kuwa hali ya chama kwa sasa ni tete hivyo maamuzi mengi  yanayofikiwa katika vikao vya chama hicho vinapaswa kuzingatia matakwa ya wananchama wake ili kuweza kurudisha imani kwa wananchi ambao ndio wanaokiangalia chama hicho kwa ukaribu sana
Awali ilidaiwa kuwa madiwani saba wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea wanatarajiwa kunyang”anywa kadi na Chama hicho kutokana na kukisaliti chama hicho kwa kumpigia Diwani wa Kata ya Matogoro Charles Mhagama kura za hapana 12 na za ndio 14 katika uchaguzi wa septemba 23 mwaka 2011 na kuwataja madiwani hao kuwa na kata zao kwenye mabano  Christian Matembo ( SeedFarm),Faustine Mhagama(Mshangano)
Wengine ni Victor Ngongi(Ruvuma)Kurabest Mgwasa(Msamala)Gelard Ndimbo(Ruhuwiko)Wilon Kapinga (Ndilimalitembo)na Genfrida Haule diwani wa Viti Maalum wa Chama hicho
MWISHO

HAYA NDIYO MTANDAO HUU UMEWEZA KUKUSANYA SIKU YA UZINDUZI WA GARI YA DHAHABU ILIYOFANYIKA KWENYE VIWANJA VYA NSSF

 Mtendaji wa TCCIA mkoa wa Ruvuma Philemon Moyo akionyesha gari ya dhahabu iliyotolewa kwa wajasiriamali juzi kwa ushirikiano wa KOICA na TCCIA mkoa wa Ruvuma
 Wakorea wa Kujitolea wakiwa na nyuso za furaha wakati wa hafla ya uzinduzi wa gari ya dhahabu
 Wakorea wa Kujitolea wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa hafla ya uzinduzi wa gari ya dhahabu juzi
 Viongozi wa Korea,TCCIA na Kaimu Mkuuwa Mkoa wa Ruvuma Thomas Oley Sabaya wakizindua gari ya dhahabu kwa kupakia bidhaa za wajasiriamali katika gari hilo
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Thomas Oley Sabaya akimpa zawadi ya Mvinyo Meneja wa Programu ya Wakorea wa Kujitolea Hwang,Jin Yung(Jenne) kushoto ni Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Ruvuma Mays Mkwembe
 Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Ruvuma Mays Mkwembe akizungumzia mfumo wa utafutaji wa Masoko na Uuzaji bidhaa kwa kutumia gari ya dhahabu
Meneja wa Programu ya Wakorea wa Kujitolea Hwang,Jin Yung akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa gari ya dhahabu
Mtaalamu wa Masoko wa Kujitolea Jaehong,Cho akitafsiri hotuba iliyotolewa na Meneja wa Programu ya Wakorea wa Kujitolea Hwang,Jin Yung wakati wa uzinduzi wa gari ya dhahabu

Thursday, September 29, 2011

WAJASIRIAMALI WATAKIWA KUTUMIA FURSA ZILIZOPO KUKUZA SHUGHULI ZAO

                    Na Stephano Mango,Songea
WAJASIRIAMALI wa mkoa wa Ruvuma wametakiwa kutumia rasilimali zilizopo mkoani humo katika shughuli zao ili ziweze kuwasaidia kuondokana na umasikini miongoni mwa jamii zinazowazunguka

Wito huo umetolewa jana kwenye viwanja vya NSSF na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Thomas Oley Sabaya wakati wa uzinduzi wa  mradi wa utafutaji wa masoko na uuzaji wa bidhaa kwa kutumia gari ya dhahabu iliyotolewa kwa wajasiriamali wa mkoa wa Ruvuma kwa ushirikiano wa Chemba ya Wafanyabiashara,Wenye Viwanda na Kilimo(TCCIA) na Wakorea chini ya mradi wa KOICA

Sabaya ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Songea alisema kuwa Mkoa wa Ruvuma una hali ya hewa nzuri ambayo unaweza kuifanyia shughuli yoyote ile ya kijasiliamali hivyo wananchi wanapaswa waitumie fursa hiyo vizuri katika kukuza uchumi wao na wa jamii yote kiujumla

Alisema kuwa imebainika kuwa wajasiliamali ni muhimu sana katika kukuza uchumi endelevu wa nchi lakini wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi ambazo tunapaswa kuziondoa ili waweze kuchangia kikamilifu uchumi wan chi yao

Akizungumza kwenye uzinduzi huo Meneja wa Programu ya Wakorea wa Kujitolea Hwang,Jin Yun(Jenne) alisema kuwa mradi huo ni ushirikiano kati ya KOICA na TCCIA Ruvuma wenye dhumuni la kuimarisha mfumo wa utafutaji wa masoko na uuzaji bidhaa kwa kutumia gari katika mkoa wa Ruvuma

Jin Yung alisema kuwa KOICA kupitia Programu ya Korea ya marafiki wa kujitolea wa dunia ambao husambazwa sehemu mbalimbali husaidia kuijengea uwezo miradi midogo iliyopo kwenye taasisi wanazofanyia kazi

‘Katika mradi huu Serikali ya Jamhuri ya Korea Kusini kupitia Shirika la Kimataifa la maendeleo la Korea(KOICA) imetoa msaada wa dola za Kimarekani 29,550 ambapo TCCIA Mkoa wa Ruvuma imechangia dola za Kimarekani 650 katika kukamilisha mradi huu pia napenda kuushukuru uongozi wa TCCIA kwa ushirikiano wanaoutoa kwa Jaehong Cho kwani bila yeye tusingeweza kufanikisha mradi huu”alisema Jin Yung

Awali Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Ruvuma Mays Mkwembe akitoa utangulizi wa uzinduzi huo alisema kuwa kwa kushirikiana na KOICA tulifanikiwa kuibua mradi huu ambao unazinduriwa ukiwa na lengo la kuwasaidia wajasiliamali katika nyanza ya usafirishaji na uuzaji bidhaa mbalimbali ili ziwafikie wateja kwa urahisi na kwa muda muafaka

Mkwembe alisema kuwa mradi huu utasaidia kutatua changamoto zinazowakabili wajasiriamali kama vile tatizo la usafiri wa bidhaa kwa gharama kubwa pia bila kuwa na gari ya uhakika,tatizo la kutafuta masoko,kuvumisha na kutangaza bidhaa zao

Alifafanua kuwa kazi ya gari la dhahabu itakuwa ni usafirishaji wa bidhaa hadi kwenye soko ambapo muuzaji anahitaji,kuuza bidhaa mbalimbali katika gari,kutangaza na uvumishaji wa bidhaa mahali popote,maonyesho ya bidhaa kupitia gari,kutangaza shughuli mbalimbali za biashara,kukodisha gari kwa shuguli mbalimbali

 Mwenyekiti huyo alisema kuwa taasisi ya TCCIA ilianzishwa mwaka 1998 mkoani Ruvuma ambapo hadi sasa TCCIA iko katika mikoa yote 21 ya Tanzania Bara na kwamba ipo mbele katika kukuza na kuendeleza sekta binafsi katika mkoa wa Ruvuma

Mkwembe alisema kuwa kazi kubwa ya taasisi hiyo ni pamoja na utetezi na ushawishi katika kujenga mazingira vutivu ya kuendeleza sekta binafsi,kujenga mazingira ya mahusiano na majadiliano na Serikali katika kuendeleza dhana ya ubia kati ya sekta binafsi na sekta ya umma

Alizitaja kazi nyingine kuwa ni utoaji wa taarifa za masoko na biashara mbalimbali kwa kupitia kituo cha taarifa,kutoa mafunzo mbalimbali ya kuendeleza biashara na ujasiriamali,utoaji wa hati ya uasili wa bidhaa
MWISHO




 Viongozi wa ngazi mbalimbali wa TCCIA Ruvuma wakifuatilia hotuba zilizokuwa zikitolewa kwenye uzinduzi huo
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Thomas Oley Sabaya akisikiliza hotuba iliyokuwa inatolewa na Meneja wa Programu ya Wakorea wa Kujitolea Hwang,Jin Yung(Jenne)katikati,wa kwanza kushoto ni Mtaalamu wa Masoko wa Kujitolea Jaehong Cho ambaye alikuwa mkalimani wa lugha ya Kikorea kwenda kiswahili
Afisa Biashara Mkoa wa Ruvuma Nehemia Jemes akipita mbele ya kikundi cha ngoma kilichotumbuiza wakati wa uzinduzi wa gari ya dhahabu

UZINDUZI WA MRADI WA UTAFUTAJI WA MASOKO NA UUZAJI BIDHAA NI MKOMBOZI WA WAJASILIAMALI

 Kikundi cha Mletere kikitumbuiza wageni na Wajasiriamali mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi wa gari ya dhahabu jana
 Wageni mbalimbali wakifuatilia kwa umakini hafla hiyo muhimu kwa wajasiliamali jana

Bidhaa ambazo zinazalishwa Tanzania na wajasiliamali wake zikiwa zimepangwa vizuri kwenye shelfu maalumu ili kuwawezesha washiriki kuangaria na kuzinunua ikiwa ni fahari kununua bidhaa zinazotengenezwa na wajasiliamali wa ndani

HALI TETE NDANI YA CCM,VIJANA WA CCM SONGEA WATISHIA KUKIMBILIA UPINZANI


                       Na Joseph Mwambije,Songea

VIJANA wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) Mkoani  Ruvuma wamekitaka Chama hicho  kurejesha nguvu iliyokuwa nayo miaka ya 70 enzi ya Mwalimu Nyerere ya kuwachukulia hatua Viongozi wa Serikali wanaojihusisha na ufisadi vinginevyo watakihama na kwenda Upinzani.
 
Walitishia kukihama Chama hicho hivi karibuni kwenye Mkutano ulioitishwa kwa ajili ya kupata maoni yao ya namna ya kurejesha heshima yake na kujua  kwa nini Vijana wanakichukia Chama hicho kilichoshika dola.
 
Walitoa  kauli za kukitahadharisha Chama hicho mbele ya wajumbe wawili wa Baraza la vijana wa CCM  Taifa  ambao pia ni wajumbe wa kamati ya watu nane inayozunguka Nchi nzima kuchukua maoni ya vijana na kuyafanyia kazi kwa lengo la kurejesha heshima ya Chama hicho.
 
Mmoja wa Vijana hao ambaye anatoka kwenye kundi la vijana wasomi Razalo Komba alisema shida kubwa inayokipata Chama hicho inatokana namna ya watendaji wabovu wa Serikali ambao wanatumia vibaya madaraka yao ndani ya Serikali na kuwatendea vibaya wananchi.
 
Alisema kuwa wapinzani wameijengea chuki inayotokana na Viongozi wa juu wa Serikali kushindwa kutimiza wajibu wao na kufanya mambo kana kwamba hakuna utawala wa sheria hivyo wanajiona wao ni Miungu watu wanaoweza kufanya chochote bila kuguswa.
 
‘Kwa jinsi mambo yanavyokwenda inaonyesha dhahiri kwamba CCM haiwapendi wasomi na udhaifu huo wapinzani wameutumia na kuwateka wasomi na hivi sasa inaungwa mkono na wasomi wengi ambao wana uzalendo na Nchi yao ambao wanaona mambo yanakwenda ndivyo sivyo,kama mambo yatakwenda hivi yanavyokwenda hata mimi nitahamia  Upinzani’alisema.
 
Kijana mwingine  Amoni Mtega alisema Chama hicho kimepoteza mvuto mbele ya watu kwa kuwa kinashindwa kujibu hoja za Wapinzani hivyo akakitaka kujibu hoja hizo tena kwa wakati huku akisisitiza kwamba kwa kushindwa kuzijibu hoja hata kama ni za uongo wananchi wanayaaamini yanayosemwa.
 
Alisema kuwa vijana wamedharauliwa na kunyimwa fursa za maendeleo na ndio sababu wanakimbilia kwenye vyama vya upinzani ambavyo wanaviona kuwa mkombozi wao mpya badala ya Chama cha CCM.
 
Akizungumza mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo Joseph Mkilikiti  alisema maoni hayo watayafikisha kwenye Baraza kuu Taifa ambalo litapeleka kwenye uongozi wa juu wa Chama hicho ili yaweze  kufanyiwa kazi.

Mkutano huo ulitonosha vidonda vya makundi ya uchaguzi wa mwaka jana kati ya kambi za Oliver Mhaiki na ya Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Dkt Emanuel Nchimbi baada ya Vijana  wa kambi ya Nchimbi ambao walitokea upinzani kumsifia Mbunge huyo na kumponda Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa CCM Songea Mjini Vikta Ngonyani ambaye hakuwa kambi ya Mbunge huyo kwamba hajasoma,hafanyi ziara kuwatembelea vijana na kwamba hawezi kukabiliana na siasa za sasa.
 
Akifunga mkutano huo huku akionekana kujibu hoja za vijana hao Mwenyekiti huyo wa vijana wa CCM Songea mjini alisema kuwa inashangazwa na maneno ya vijana hao kuwa bado hawajui taratibu za chama hicho kwani waliingia na kukuta ziara zimeshafanyika  hivyo amewataka watulie iliwajifunze na siku zijazo watapata uongozi ndani ya chama hicho.
 
Alisema vijana hao ndio waliosababishan CCM kupoteza Kata tano za Mjini kwa kuwa Mbunge alikuwa akiwatumia kufanya kampeni na badala ya kuomba kura wao walikuwa wakiwatukana wapiga kura hivyo wapiga kura waliwaadhibu kwa kuwachagua madiwani wa CHADEMA.
       MWISHO.  

CHADEMA KUMPINGA MEYA ANAYEDAIWA KUCHAKACHUA MATOKEO YA KITI HICHO TUKUFU

Na  Joseph Mwambije,Songea
CHAMA cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA)Mkoani Ruvuma kimepanga kufanya maandamano makubwa ya kupinga uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Songea ulio mwezesha Charles Mhagama kuwa Mstahiki Meya anayedaiwa kuchaguliwa kwa kura za ndiyo 12 na za hapana 14 na kuweka kambi kwenye viwanja vya Manispaa.
 
Hayo yamebainishwa juzi na Mwenyekiti wa Chama hicho wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Joseph Fuime wakati akiwahutubia maelfu ya wananchi wa Songea kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya msingi mfaranyaki.
 
Alisema kuwa sababu kubwa ya kufanya maandamano hayo ni kupinga uchaguzi huo uliofanyika bila kufuata taratibu na kwamba licha ya kuwa Halmashauri ya Manispaa Songea kuwa maskini lakini wamemchagua Meya aliyedai kuwa ni mwizi.
 
‘Wamemchagulia Meya aliyehusika na uuzaji wa greda kwa shilingi milioni18,ununuzi wa gari  bovu la Zimamoto kwa shilingi milioni 350 ambalo halifanyi kazi na huu ni mpango wa Wabunge kuweka watu wao ili waibe fedha’alisema na kuongeza
 
‘Mlifanya makosa makubwa kumchagua Nchimbi(Emanuel Nchimbi) na mngemchagua Mbogoro(Edson Mbogoro) kuwa  Mbunge wenu  tusingepata Meya mwizi na kama ingekuwa enzi ya Nyerere Nchimbi angejiuzulu anamtka Meya huyo ili amtumie kujinufaisha na tunatamka kuwa huyo si Meya wa wananchi ni Meya wa Mbunge na atapopita mitaani mumzomee’alisema.
 
Alimshambulia Mbunge wa jimbo la Songea Mjini  Emmanuel Nchimbi kuwa hana nia njema na wananchi wake na kwamba watakuwa tayari kutoa ushahidi kuwa kura ziliibwa na hivyo watapambana kwa kutumia  akili na busara na watashinda.
 
Alisema kuwa kabla ya kufanya maandamano hayo watazunguka kata 21 za Manispa ya Songea kufanya mikutano ya kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwenye  maandamano na kuanda vyakula na taa na kisha kuvigeuza viwanja vya Manispaa kuwa Viwanja vilivyomng’oa  madarakani aliyekuwa Rais wa Misri.
 
Hata hivyo  Bw. Mhagama alipoulizwa kuhusu tuhuma za kuhusika na ununuzi wa gari bovu la Zimamoto,uuzaji wa greda alisema yeye hausiki na tuhuma hizo kwa kuwa magari hayo yalinunuliwa saba Nchi nzima na kwamba greda liliuzwa kwa kufuata sheria zote.
 
Naye  katibu wa Jimbo la Songea Mjini Bw. Masumbuko Paul alisema kuwa Wabunge wa Mkoa wa Ruvuma wamekuwa mzigo kwa wananchi wao kwa kushindwa kuwatatulia matatizo yao kama tatizo kubwa la umeme na ajira kwa wananchi,alisema kuwa siku za CCM kukaa madarakani zinahesabika.
 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Songea Mjini Idd Abdalah alilaani kukihusisha CHADEMA na udini,ukabila  na urangi na kuwataka Waislamu kuondoa dhana hiyo na kuungana kuiondoa CCM madarakani huku akiwapongeza madiwani wa CCM waliopiga kura za hapana kwa Mhagama.
Mwisho