Nahodha wa timu ya NBC Emmanuel Ntobi akitamba kuwashushia mvua ya magori watani wao wa jadi CRDB
Kikosi cha timu ya NBC kinachopambana na CRDB leo asubuhi
Nembo ya NBC ikiwa imewekwa kwenye uwanja wa Majimaji na kumaanisha kuwa ushindi ni lazima
Kikosi cha timu ya CRDB kinachopambana na NBC leo kwenye uwanja wa Majimaji kikiwa kimetulia na kukwepa kutoa aina yoyote ya tambo na kusubiri dakika tisini uwanjani ndipo watasema jambo
Nahodha wa timu ya NBC Emmanuel Ntobi akitafakari jambo na mke wake Bi Sara kabla ya mechi kuanza katika uwanja wa Majimaji
Saturday, November 19, 2011
MUASISI WA VURUGU NA MISA YA PILI KANISA LA ANGLIKANA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIEZI 12
Askofu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma Dk.Maternus Kapinga
NaThomas Lipuka,Songea.
MUASISI na kiongozi wa wakristo wa dhehebu la misa ya pili wilayani Mbinga mkoani Ruvuma Joseph Lombola amehukumiwa kifungo cha miezi 12 kwa kosa la kufanya vurugu katika kanisa la Anglikana la Kristo Mfalme mjini Mbinga.
Lombola ambaye pia ni katibu wa Tume ya Utumishi ya Walimu (TSD) wilayani Mbinga ametiwa hatiani pamoja na Martin Mawala aliyeachishwa upadre wa kanisa Anglikana kwa kutomtii Askofu wa Dayosisi ya Ruvuma.
Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Mbinga Frank Mahimbali akitoa hukumu alisema ameridhika na upande wa mashitaka kuwa washitakiwa bila uhalali walifanya vurugu wakati ibada ikiendeshwa na padre Andrew Nkomola wa kanisa la Kristo Mfalme mjini Mbinga.
Kutokana na hali hiyo ,mahakama iliwatia hatiani hivi karibuni na kuwahukumu kifungo cha nje cha miezi 12 kila mmoja na kwamba katika kipindi hicho hawatakiwi kufanya kosa la aina yoyote.
Awali mwendesha mashtaka wa polisi Inspekta Isaya alidai washitakiwa hao walitenda makosa hayo Agosti 16 ,2009 katika kanisa hilo ambapo washitakiwa waliingia kanisani na kwenda madhabahuni kisha waliondoa vitambaa,kutupa vitabu vitakatifu na sakramenti takatifu jambo ambalo lilisababisha vurugu kutoka kwa waumini.
Habari zaidi kutoka ndani ya kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma zinadai kuwa Lombola ambaye hivi sasa anatumikia kifungo cha mwaka mmoja ndiye kiongozi wa kikundi cha kidini kinachojiita Wakristo wa Misa ya Pili(SECT) ambacho kinaendesha shughuli zake mkoani Ruvuma bila uhalali wa kisheria kwa kuwa hakina usajiri wowote.
Dhana ya Misa ya Pili imetokana na ibada ya waumini ambao wamejitenga na uaskofu wa kanisa la Anglikana hivyo hawana Askofu na bado walijiita waanglikana, wakalazimisha kufanya ibada zao katika makanisa ya uaskofu wa Ruvuma kwa kuvamia makanisa na kujiita waumini wa misa ya pili.
Askofu wa kanisa Anglikana Dayosisi ya Ruvuma Dk.Maternus Kapinga amesema amani ya kanisa hilo itaimarika zaidi baada ya kufungwa kwa muasisi wa SECT ambaye alikuwa ni muhimili wa kikundi cha Wakristo wa Misa ya Pili ambao kazi yao kubwa ni kulaghai,kuposha,kuharibu kanisa la Mungu na kuvuruga uongozi wa Askofu wa Ruvuma.
Kwa mujibu wa Askofu Kapinga waasisi,viongozi na wafadhili wakuu wa SECT ni wanasiasa,watu walioshindwa huduma takatifu na watu wanaowania vyeo na mali katika kanisa hilo ambao wamejiengua kutoka katika kanisa hilo kwa madai ya kutotaka kumtii Askofu wa Ruvuma wa awamu ya tatu.
Uchunguzi uliofanyika ndani ya Dayosisi hiyo umebaini kuwa kikundi ambacho kinamkataa Askofu na kujiita wakristo wa dhehebu la Misa ya pili ndani ya kanisa hilo ni wale wenye roho inayoongozwa na ukabila, chuki, ulaghai, tamaa, wizi, upinzani, uzushi, kiburi,ukengeufu na faraka.
“Lengo kuu la kikundi hicho ni kumwaga damu isiyo na hatia hasa wakidhamiria kumuondoa Askofu wa Ruvuma kutoa huduma takatifu aliyoitiwa na Mungu,mbinu kuu ambayo wanaitumia ili kutekeleza lengo hilo ni kupotosha na kutowaambia watu ukweli’’,alisema mkristo ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini.
Mkristo huyo anabainisha zaidi kuwa kikundi hicho kinawashawishi watu wawafuate katika kumkataa Askofu wa Ruvuma na kwamba walifanikiwa kuanzisha vikundi katika maeneo ya Mbinga,Songea,Chiulu,Liuli na Puulu, vikundi ambavyo hivi sasa vyote vimekufa na wakristo wametubu na wamerudi kwa Askofu wa kanisa la Mungu.
Viongozi wa SECT ili kutimiza azima yao ya kulivuruga kanisa ,waliamua kuwa ajiri makasisi waliosimamishwa ili wawe viongozi wao wa kiroho.
Makasisi hao walisimamishwa kutoa huduma takatifu katika kanisa hilo baada ya kufanya makosa mabaya yakiwemo kuvunja ndoa, kutokutii mamlaka ya Mungu na kuishi na vimada.
Askofu Dk.Kapinga anasema waumini wa dhehebu la Misa ya Pili wamekuwa wakiigiza ibada zao kanisani na kwamba lengo lao halikuwa kumuabudu Mungu bali ni kuleta fujo ili ulimwengu useme Dayosisi ya Ruvuma ni yenye ni migogoro.
“Watu waliozuiwa kutoa huduma ya ukasisi katika kanisa hilo ,walikaidi amri hii ya Mungu na mamlaka halali ya kanisa,watu hao wakijua kuwa hawana mamlaka ya kasisi,lakini waliwadanganya watu na serikali kwa kuwaibia malipo,mathalani kwa kufungisha ndoa bila kulipia kibali cha kufungisha ndoa’’,alifafanua Askofu Dk.Kapinga.
Kikundi cha cha dhehebu la Misa ya pili kilijitokeza hadharani Desemba mwaka 2007 na hadi mwaka 2010 kikundi hicho kilikuwa kimemalizika na Dayosisi ya Ruvuma kuwa katika hali ya amani na utulivu kutokana na juhudi zilizozaa matunda kwa ushirikiano baina ya waumini,uongozi wa kanisa na viongozi wa serikali katika ngazi mbalimbali mkoani Ruvuma.
Takwimu toka ofisi ya Askofu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma zinaonesha kuwa hadi kufikia Oktoba 31 mwaka huu kanisa hilo lina jumla ya waumini 41,000 ambapo dhehebu la Misa ya Pili lina waumini wasiozidi 50(hamsini)
WASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUKUTWA NA PURI 54 ZA BANGI KATA YA MSHANGANO
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda
Na Gideon Mwakanosya, Songea
JESHI la Polisi Mkoani Ruvuma linawashikilia watu watano wakikabiliwa na tuhuma za kukutwa na puri 54 za bangi ambayo ilikuwa ikiuzwa kwenye eneo la Mshangano katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda amesema kuwa tukio hilo lilitokea jana majira ya saa tatu asubuhi huko katika eneo la Mshangano Manispaa ya Songea ambako askari wakiwa doria walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao wakiuza wengine wakinunua bangi.
Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Kessy Mwegela (28) na Jordan Juma (19) wote wakazi wa bombambili,wengine ni John Kanjoroka (26) na Joseph Moyo wote wakazi wa eneo la Mshangano Manispaa ya Songea.
Amesema kuwa watuhumiwa hao baada ya kuona askari Polisi wakiwa wamewazunguka walitafuta njia ya kutaka kukimbia lakini Polisi walifanikiwa kuwatia mbaroni wakiwa na puri 54 kwenye mfuko wa Rambo na nyingine zilikuwa kwenye mifuko yao ya suruali walizokuwa wamevaa.
Amefafanua kuwa watuhumiwa hao kati yao ni wauzaji maarufu wa bangi katika Manispaa ya Songea na wengine ni wavutaji ambao walikuwa wamefika kwenye eneo hilo kwaajili ya kununua bangi.
Kamanda kamuhanda amesema kuwa polisi bado inaendelea kufanya upelelezi zaidi wa tukio hilo na kwamba utakapokamilika watuhumiwa watafikishwa Mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili.
Friday, November 18, 2011
WALIMU WA SAYANSI NA LUGHA WILAYANI NAMTUMBO NI TATIZO SUGU
Na Stephano Mango, Namtumbo
HALMASHAURI ya Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma ambayo ina shule 30 za Sekondari zikiwemo Shule 24 za Serikali na Shule za Binafsi 6 inakabiliwa na tatizo kubwa la upungufu wa Walimu wa masomo ya Sayansi na Lugha na kusababisha Wanafunzi wa Shule hizo kushindwa kumudu masomo ipasavyo wakiwa kwenye Shule hizo.
Akizungumza na Mtandao wa www.stephanomango.blogspot.com jana Ofisini kwake Kaimu Afisa Elimu wa Shule za Sekondari wa Wilaya ya Namtumbo Lydia Herbert alisema kuwa Halmashauri hiyo yenye jumla ya Wanafunzi wa Sekondari 7871 wakiwemo wavulana 4671 na wasichana 3193 ina uhaba mkubwa wa walimu wa Masomo ya Sayansi na Lugha.
Herbert alisema kuwa mpaka sasa Halmashauri hiyo ina walimu 208 wa Shule za Sekondari ambao hawawezi kukidhi haja ya wanafunzi waliopo kwenye Shule za Sekondari Wilayani humo na kwamba kutokana na hali hiyo kuna upungufu wa walimu 32 wa masomo ya sayansi na lugha.
Alieleza zaidi kuwa hali ya miundo mbinu katika shule za Sekondari zilizopo katika Wilaya hiyo ilikuwa inahitajika kuwa na vyumba vya madarasa 285 lakini vyumba vya madarasa vilivyopo kwasasa ni 164 na kufanya kuwepo tatizo kubwa la vyumba vya madarasa kwenye Shule hizo.
Alibainisha zaidi kuwa katika Shule hizo za Sekondari Wilayani humo zinahitajika maabara 115 lakini maabara zilizopo ni 3 tatu ambazo zipo katika Shule mbili za binafsi na Shule moja ya Serikali na walimu wa Shule hizo wanakabiliwa na tatizo kubwa la nyumba za kuishi ambapo nyumba za walimu zinazohitajika ni 384 na nyumba zilizopo ni 84 tu ,.
Alisema katika Shule hizo za Sekondari Wilayani humo kuna changamoto kubwa zinazojitokeza mara kwa mara ambaapo ni utoro wa wanafunzi wa kike na wakiume uliokithiri na mimba za utotoni ambapo wanafunzi 22 walibainika kuwa ni wajawazito katika kipindi cha January hadi October mwaka huu.
Ameitaja mikakati mbalimbali ya kukabiliana na changamoto hizo kuwa ni kuwaelimisha wananchi wa Wilaya ya Namtumbo juu ya umuhimu wa elimu kupitia mikutano ya ndani na ya hadhara ili waweze kuelewa kuwa wazazi wa wanafunzi hao wanapaswa kuchangia ujenzi wa madarasa,madawati na kujenga nyumba z akuishi walimu.
Mikakati mingine ni kuboresha miundo mbinu ya Shule za Sekondari Wilayani humo ili kuwa na Mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia kwa kujenga nyumba za walimu,vyumba vya madarasa pamoja na maabara kwa mwaka wa fedha 2011/2012.
Kaimu Afisa Elimu huyo Herbert ameiomba Serikali kupitia Wizara za Elimu Utamaduni na Ufundi na Wizara ya Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa (TAMISEMI ) kuona umuhimu wa kuwaletea walimu wengi zaidi wa masomo ya sayansi ambao wataweza kuziba mapengo mengi ya walimu katika Shule za Sekondari Wilayani humo
Thursday, November 17, 2011
WANANCHI WATAADHARISHWA UZAGAAJI WA NOTI BANDIA MKOANI RUVUMA
Na Gideon Mwakanosya, Songea
JESHI la polisi Mkoani Ruvuma limewataadharisha wananchi wakiwemo wakulima na wafanyabiashara kuwa makini wanapofanya shughuli zao za kila siku hasa wanapouza mazao au wanaponunua bidhaa za biashara zao kwani katika Mkoa huo noti bandia za shilingi Elfu 5000 na shilingi Elfu 10,000 zimezagaa ambapo kufuatia hali hiyo Polisi imefanikiwa kuwanasa watu wawili wakiwa na noti bandia za shilingi alfu 10 kila mmoja zenye thamani ya shilingi laki 5.
Tahadhali hiyo imetolewa jana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda wakati alipokuwa akiongea na Waandishi wa habari ofisini kwake.
Kamuhanda amewataja wanoshikiliwa na polisi kuwa ni Joseph Kilagi ( 25) na Francis Nkunji (19) wote wakazi wa jijini Dar es salaam ambao walitiwa mbaroni tangu Novemba 13 mwaka huu majira ya saa mbili usiku kwenye kituo kikuu cha mabasi cha Mjini Songea wakiwa wanateremka kwenye basi wakitokea Dar es salaam.
Amesema kuwa askari ambao walikuwa doria kwenye eneo la Kituo cha mabasi waliwakamata watuhumiwa hao wakiwa na noti bandia 50 ambazo kila noti moja ni shilingi elfu 10 zote zikiwa na thamani ya shilingi laki 5.
Amefafanua zaidi kuwa noti hizo bandia zilizokamatwa zina namba AC.0011601 kila moja na kwamba watuhumiwa walipohojiwa na askari hao waliokuwa doria walidai kuwa wametokea Dar es salaam na wamekuja Songea kufanya biashara ya kununua mahindi.
Kamanda Kamuhanda ameeleza kuwa kwasasa hivi polisi inaendelea kufanya upelelezi kuhusiana na tukio hilo na kwamba watuhumiwa hao watafikishwa Mahakami kujibu shtaka linalowakabili mara tu upelelezi utakapokamilika.
Amewataadhalisha wafanyabiashara wa Wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma kuwa wanapofanyabiashara zao kuwa waangalifu pale wanapokutana na noti za shilingi Elfu 5000 na Elfu 10,000ambazo zinadaiwa ndiyo noti bandia zimezagaa kwenye magulio,minada na maeneo mengine ya biashara za jumla na rejareja na kwamba wananchi watakaowagundua watu wenye tabia mbaya ya kusambaza noti bandia watoe taarifa katika kituo chochote cha polisi kilicho karibu.
WASHIRIKI WA MAJADILIANO YA PAMOJA KUHUSU UTAFITI MDOGO WA VYOMBO VYA HABARI RUVUMA WAMALIZA WARSHA YA SIKU MBILI NA KUAZIMIA NJIA BORA YA KUKUSANYA NA KUSAMBAZA TAARIFA KWENYE VIKUNDI NA MITANDAO YA JAMII
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mafunzo husika
Washiriki wakiendelea na mijadala mbalimbali kwenye ukumbi wa warsha
Bi Jenni akiwasirisha mada iliyojadiliwa kwenye kikundi chake wakati wa warsha
Washiriki wakisikiliza mada iliyokuwa inawasilishwa na Mwezeshaji kutoka TGNP Badi Darusi
Washiriki wakiendelea na mijadala mbalimbali kwenye ukumbi wa warsha
Bi Jenni akiwasirisha mada iliyojadiliwa kwenye kikundi chake wakati wa warsha
Washiriki wakisikiliza mada iliyokuwa inawasilishwa na Mwezeshaji kutoka TGNP Badi Darusi
TGNP NA DHANA YA UMUHIMU WA KUANZISHA VITUO VYA TAARIFA KWENYE VIKUNDI NA MITANDAO YA KIJAMII
VITUO VYA TAARIFA NA MAALIFA KATIKA JAMII
Na Stephano Mango,Songea
Ni sehemu maalumu ya kukutana kwa lengo la kujifunza na kuhabarishana masuala mbalimbali yanayohusu jamii zetu kwa faida ya vizazi vilivyopo na vijavyo
KWANINI VITUO HIVYO
-Kuleta chachu ya harakati za ukombozi wa mwanamke wa kimapinduzi katika jamii
-Kusaidia ujenzi wa nguvu za pamoja kwa kutumia kukusanya na kusambaza taarifa
-Kuendesha mijadala ya wazi na kuweka kumbukumbu kuhusu mijadala hiyo
-Kufanya uchambuzi na ufuatiliaji wa masuala au kero zinazoikabili jamii husika na kuchukua hatua za pamoja
LENGO KUU
-Kuwawezesha wanaharakati wa ukombozi wa mwanamke wa kimapinduzi,vikundi,mitandao ya jamii kufikia fursa za kupashana,kubadilishana maarifa na taarifa
-Kuongeza hamasa katika masuala yanayohusu haki za binadamu kwa mlengo wa ukombozi wa mwanamke wa kimapinduzi
MALENGO MAHSUSI YA VITUO
-Kuwa na eneo la vituo vya wanawake,vikundi na kuhamasishana ili kuchukua hatua za pamoja kuleta mabadiliko
-Kukita vuguvugu la ukombozi wa mwanamke wa kimapinduzi katika ngazi ya jamii kwa kuwawezesha wanawake na vikundi vya wanaharakati na mitandao kuweka kumbukumbu na kupashana habari
-Kuboresha na kuimarisha mahusiano na kupashana habari kati ya wanaharakati na vikundi ili kupunguza pengo kati ya wanaofaidi taarifa muhimu na wale ambao hawapati taarifa hizo kwa wakati muafaka
Wednesday, November 16, 2011
Tuesday, November 15, 2011
TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MPANGO KAZI WA ASASI YA RUVUMA ORPHANS ASSOCIATIONS(ROA)
(ROA)
Sokoine Road
Simu: 0754-533 032, 0713-290 473
E-mail: roaruvuma@yahoo.co.uk
TAARIFA YA UTENDAJI KAZI
HALMASHAURI YA MANISPAA YA SONGEA
JULAI HADI SEPTEMBA, 2011
Imeandaliwa na;
Menejinemti ya ROA. Oktoba, 2011
TANZIA TANZIA TANZIA TANZIA TANZIA TANZIA TANZIA TANZIA TANZIA TANZIA TANZIA TANZIA TANZIA TANZIA TANZIA TANZIA TANZIA TANZIA
Mtandao huu unaungana na familia ya Gerson Msigwa kwenye majonzi makubwa ya kuondokewa na ndugu yao mpendwa Pascalina Lukas Msigwa mwenye umri wa miezi 6 aliyefariki dunia jana mchana kwenye Hospital ya mkoa ya Songea na mazishi kufanyika leo kwenye makaburi ya Songambele,Bombambili,Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe,Mungu mwenyezi aiweke roho ya marehemu na marehemu wengine wote mahali pema peponi Amina
Ndugu wa familia ya Marehemu Pascalina Lukas Msigwa wakiwasha michumaa na kuiweka juu ya kabuli lake ikiwa ni ishara ya mwanga wa milele na upendo wao kwake baada ya mazishi yake yaliyofanyika leo mchana katika makaburi ya Songambele Bombambili mjini Songea na kuhudhuriwa na wananchi,viongozi wa vyama mbalimbali na Serikali,Waandishi wa Habari na wafanyabiashara mbalimbali mjini Songea na mkoa jilani wa Njombe
Bibi wa Marehemu Pascalina Lukas Msigwa(Mama Lucy) akiweka ua kwenye kaburi la marehemu ikiwa ni ishara ya upendo
Msemaji wa familia ya Marehemu Pascalina Lukas Msigwa,Gorden Sanga(Sanga One) akiwashukuru ndugu,jamaa na marafiki waliojaribu kunusuru uhai wa marehemu na wale wote waliojitokeza kumsindikiza kwenye makazi ya milele ndugu yao mpendwa
WARSHA YA TGNP YAWAKUTANISHA WADAU MBALIMBALI WA HARAKATI ZA MWANAMKE WA KIMAPINDUZI
MTANDAO WA JINSIA TANZANIA(TGNP) KATIKA UTAFITI MDOGO WA VYOMBO VYA HABARI MWAKA 2011 RUVUMA
Waandishi wa Habari wa Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) Kanda za nyanda za juu Kusini Stephano Mango na Juma Nyumayo wakitambulishana Kiraghabishi kwenye warsha ya majadiliano ya pamoja kuhusu utafiti mdogo wa vyombo vya habari mwaka 2011 iliyofanyika kwenye ukumbi wa Saccos ya Walimu wa Songea Vijijini leo
Mwezeshaji toka TGNP Badi Darusi akieleza maudhui ya warsha hiyo kwa washiriki
Washiriki wa warsha hiyo wakisikiliza mada mbalimbali zilizowasilishwa na Mwezeshaji Badi Darusi
WANAWAKE WATAKIWA KUACHA UWOGA WA KURIPOTI TAARIFA ZA UKATILI WA KIJINSIA
Na Stephano Mango,Songea
WANAWAKE nchini wametakiwa kuacha uwoga wa kutoa taarifa za ukatili wa kijinsia kwenye vyombo vya habari ili kuweza kujenga mazingira ya kukomesha ukatili mbalimbali wa kijinsia uliokithili miongoni mwa jamii za Kitanzania
Wito huo umetolewa jana na Naibu Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mariam Dizumba alipokuwa akichangia mada ya wadau muhimu wa Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) kwenye warsha ya majadiliano ya pamoja kuhusu utafiti mdogo wa vyombo vya habari iliyofanyika kwenye ukumbi wa Saccos ya Walimu wa Songea Vijijini
Dizumba alisema kuwa vyombo vya habari ni wadau muhimu sana katika harakati za ukombozi wa mwanamke wa kimapinduzi hasa wakati huu ambao taifa letu linaelekea kwenye miaka 50 ya uhuru ili kuweza kuzibaini changamoto mbalimbali za wanawake zilizokuwa zinawakabili wanawake miaka hiyo na sasa tuweke mikakati mingine ya kuzikabili changamoto za sasa
Akizungumza kwenye warsha hiyo ya siku mbili Mwanaharakati wa Mtandao wa Jinsia Nyanda za Juu Kusini Juma Nyumayo alisema kuwa vyombo vya habari nchini vimetoa mchango mkubwa sana katika harakati za kuleta usawa ,uwiano wa kijinsia na haki sawa za kijamii ili kuboresha ustawi wao
Nyumayo alisema kuwa kwa muda mrefu sasa vyombo hivyo vimeweza kusambaza taarifa za ujengaji wa vuguvugu la ukombozi wa wanawake wa kimapinduzi hasa wanaoishi pembezoni ili kukuza uwepo na upatikanaji wa habari na maarifa kuhusu harakati za ujenzi wa vuguvugu hilo na kusaidia kujenga mitandao na kuendeleza vuguvugu hilo
Kwa upande wake Mwezeshaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) Badi Darusi alisema kuwa lengo kuu la majadiliano hayo ya siku mbili ni kuelewa ni kwa kiasi gani vyombo vya habari vimeweza kuchangia katika kazi za Tgnp na kusambaza habari kupitia kampeni ya na harakati za ukombozi wa mwanamke wa Kimapinduzi mkoani Ruvuma
Darusi alisema kuwa washiriki watapata fursa ya kuwatambua wadau muhimu wa Tgnp katika ngazi za jamii,fursa na changamoto zao,kuainisha na kuchambua hatua zilizochukuliwa na katika harakati za Tgnp,kupima kiwango cha uelewa wa kuhusu Tgnp na Waandishi wa habari katika dhana ya majadiliano,dodoso,visa mkasa,maswali chokozi,kazi za vikundi na uchambuzi wa pamoja
Mwezeshaji toka TGNP Badi Darusi akieleza maudhui ya warsha hiyo kwa washiriki
Washiriki wa warsha hiyo wakisikiliza mada mbalimbali zilizowasilishwa na Mwezeshaji Badi Darusi
Monday, November 14, 2011
NBC WATAMBA KUICHARAZA BAKORA CRDB KATIKA MECHI YA KIRAFIKI
Nahodha wa Timu ya NBC Emmanuel Ntobi akizungumza na waandishi wa habari
Na Stephano Mango,Songea
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) tawi la Songea wametamba kuwanyeshea mvua ya magori watani wao wa jadi Benki CRDB katika mechi ya kirafiki inayotarajiwa kuchezwa Novemba 20 mwaka huu katika uwanja wa Majimaji
Akizungumza na Waandishi wa habari jana kwenye viwanja vya Makumbusho ya Taifa ya Majiamaji Songea Nahodha wa timu ya NBC Songea Emmanuel Ntobi alisema maandalizi ya mechi hiyo yamekamilika kwani wachezaji wote wana ari nzuri wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya mechi hiyo ya aina yake
Ntobi alisema kuwa lengo mechi hiyo ni kukuza urafiki,ujirani na undugu kati ya taasisi za kifedha na wateja wao kiujumla kwani muda mwingi wamekuwa wakikutana katika shuguli za kibenki tu na kufanya wateja wasifurahi pamoja na wafanyakazi wa taasisi za kibenki
Alisema kuwa lengo jingine ni kujenga afya njema za wafanyakazi wa taasisi hizo za kifedha kwani michezo licha ya kuwaweka watu pamoja pia ni nguzo muhimu ya kujenga afya stahiki kwa binadamu yoyote
Alisema kuwa siku hiyo ni muhimu sana kwa kutengeneza na kudumisha mtandao baina ya wateja na maafisa wa taasisi hizo za benki na kwamba kutakuwa na burudani mbalimbali zitakazoporomoshwa na maafisa wa benki hizo muhimu kibiashara nchini
Alifafanua kuwa mechi hiyo ya kirafiki ni hatua muhimu ya kuendelea na mipango stahiki ya kuboresha shughuli za kibenki na wateja wa taasisi za kifedha ndani ya mkoa na nje ya mkoa ili waweze kufaidi huduma za taasisi hizo kikamilifu na kukuza mahusiano
Nahodha huyo Ntobi alisema kuwa baada ya mechi hiyo kukamilika kutakuwa na programu nyingine mbalimbali za ujrlani mwema ikiwa pamoja na midaharo kuhusu thamani ya shilingi ya Tanzania na kudorora kwa uchumi wake
Alieleza zaidi kuwa katika mechi hiyo ya aina yake mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Meneja wa Kampuni ya Tigo Mkoa wa Ruvuma Wilfred Nestory na kwamba wateja wa taasisi za fedha na wapenzi wa soka wanapaswa kuhudhuria mechi hiyo muhimu
MWISHO
HAYA NDIYO YALIYOJIRI KATIKA UZINDUZI WA MRADI WA KISASA NA WA AINA YAKE WA UPIMAJI WA VIWANJA 18000 KATIKA KATA YA MSHANGANO
Afisa Mtendaji wa kata ya Mshangano Stan Kibiki akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi wa upimaji wa viwanja 18000 wakati wa uzinduzi
Diwani wa Kata ya Mshangano Faustine Mhagama akizungumza siku ya uzinduzi
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ardhi Plan Gombo Samandito akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa mradi wa upimaji wa viwanja 18000 katika kata ya Mshangano
Sehemu ya mradi wa upimaji viwanja 18000 linavyoonekana katika eneo la Beroya kata ya Mshangano
Diwani wa Kata ya Mshangano Faustine Mhagama akizungumza siku ya uzinduzi
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ardhi Plan Gombo Samandito akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa mradi wa upimaji wa viwanja 18000 katika kata ya Mshangano
Sehemu ya mradi wa upimaji viwanja 18000 linavyoonekana katika eneo la Beroya kata ya Mshangano
MRADI WA UPIMAJI VIWANJA 18000 WAZINDURIWA KWA MBWEMBWE MBALIMBALI KATIKA ENEO LA BEROYA KATA YA MSHANGANO
Mgeni Rasmi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati za Huduza za Uchumi na Jamii katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea Genfrida Haule wa tatu toka kushoto ambaye alimwakilisha Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Charles Mhagama akizindua mradi wa upimaji wa viwanja 18000 katika eneo la kata ya Mshangano kwa kutumia Kampuni ya Ardhi Plan huku akishuhudiwa na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali
Mgeni rasmi Genfrida Haule akikagua barabara iliyochimbwa na wananchi wa Kta ya Mshangano ndani ya eneo la mradi wa upimaji wa viwanja huku akisindikizwa na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali katika Manispaa ya Songea
Mgeni Rasmi Genfrida Haule akiwahutubia wananchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa mradi wa kisasa na wa aina yake wa upimaji wa viwanja 18000
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakisikiliza hotuba ya ufunguzi wa mradi wa upimaji wa viwanja iliyokuwa ikitolewa na mgeni rasmi Genfrida Haule
Mgeni rasmi Genfrida Haule akikagua barabara iliyochimbwa na wananchi wa Kta ya Mshangano ndani ya eneo la mradi wa upimaji wa viwanja huku akisindikizwa na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali katika Manispaa ya Songea
Mgeni Rasmi Genfrida Haule akiwahutubia wananchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa mradi wa kisasa na wa aina yake wa upimaji wa viwanja 18000
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakisikiliza hotuba ya ufunguzi wa mradi wa upimaji wa viwanja iliyokuwa ikitolewa na mgeni rasmi Genfrida Haule
Sehemu ya barabara iliyochongwa na wananchi kwa kupata ujira wa kulipwa Tshs 5000 kwa kila mmoja kwenye eneo la mradi
MRADI WA UPIMAJI VIWANJA 18000 SONGEA KUWAKOMBOA WANANCHI KIUCHUMI
Na Stephano Mango,Songea
IMEDHIHIRIKA kuwa tatizo la makazi holela ambalo limeshamiri nchini limetokana na kutokuwa makini katika mipango miji na ukosefu wa wataalamu wa mipango miji wenye ubunifu na kusababisha adha kubwa kwa wananchi kutokana na wananchi kuvamia maeneo mengi na kujenga holela
Na kusababisha maeneo hayo mengi ya aina hiyo kukosa miundombinu ya maji safi na maji taka,barabara na nishati ya umeme na kufanya mikakati mbalimbali ya maendeleo kutofikiwa kikamilifu,jambo ambalo linawezekana kuepukwa ikiwa kila mtu atatimiza wajibu wake kwa kukomesha ujenzi wa makazi holela
Novemba 19 mwaka 2011 nilibahatika kuhudhuria uzinduzi wa mradi wa kisasa na wa aina yake ambao haujawahi kutokea tangu nchi ipate uhuru wake mwaka 1961 wa upimaji wa viwanja 18,000 katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea
Mradi huo umezinduriwa katika kata ya Mshangano yenye mitaa mitano ya Namanyigu,Mitendewawa,Mhumbezi,Chandarua na Mshangano yenye jumla ya kaya 1508 zenye wakazi 7540 ikiwa wanaume 3196 na wanawake 4344
Ambapo wakazi wa kata hiyo kama walivyo wakazi wa kata zingine 20 zilizopo kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Songea wanajishughulisha na kilimo,ufugaji,na biashara ndogondogo katika kujitafutia kipato cha maisha yao,
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa upimaji wa viwanja hivyo alikuwa Mshahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Charles Mhagama ambaye aliwakilishwa na Mwenyekiti wa Kamati za Huduma za Uchumi na Jamii wa Manispaa hiyo Genfrida Haule
Akizindua mradi huo wa upimaji viwanja hivyo Haule alisema kuwa Suala la upimaji viwanja ni hatua kubwa ya maendeleo kwa kuwa baada ya upimaji miundombinu ya maji na umeme itakuja na wananchi wameongeza kipato kwa kuweza kukopa na kuendesha miradi kupitia viwanja na nyumba zao huku viwanja vikipandishwa thamani
“Mradi huo utawainua kiuchumi wananchi wa Kata ya Mshangano kwa sababu wataweza kukopaa kupitia makazi yao na kwamba wataweza kuishi katika makazi bora yaliyopimwa na kufanya mji wa Mshangano kuwa wa kisasa zaidi kuliko maeneo mengine ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea”alisema Haule
Akielezea historia ya Mradi huo Afisa Mtendaji wa Kata ya Mshangano Stan Kibiki alisema kuwa mradi huo wa upimaji wa viwanja kwa kutumia Kampuni uliibuliwa na wananchi wenyewe baada ya kuona wanakaa na kuishi katika makazi holela yasiyopimwa kwa muda mrefu
Kibiki alisema kuwa kwa muda wa miaka mingi wananchi wa kata hii wamekuwa wakipeleka maombi Halmashauri ya kuomba kupimiwa maeneo yao bila mafanikio kutokana na Halmashauri kukosa uwezo wa kifedha
“Mwaka 2010 kata yetu ilibahatika kupata mradi wa upimaji wa viwanja ilibahatika kupata mradi wa upimaji viwanja wa Halmashauri lakini bahati mbaya fedha yenyewe ilikuwa kidogo kwani waliweza kupima viwanja 347 katika mtaa wa Namanyigu eneo dogo mashambani hivyo tatizo la wananchi kuishi katika makazi holela lilibaki palepale”alisema Kibiki
Alisema kuwa wananchi kwa kushirikiana na viongozi wao katika kutatua tatizo hili waliamua kutafuta njia mbadala ambayo kwa kutumia sheria namba 8 ya Mipango Miji ya 2007 walitafuta Kampuni ya Ardhi Plan ya Jijini Dar Es Salaam ili iweze kuwapimia viwanja katika maeneo yao
Alieleza kuwa baada ya kuipata Kampuni hiyo makubaliano yakawa malipo ni ardhi kwa ardhi yaani wanapima ardhi wanalipwa ardhi kwa asilimia za kwamba mwananchi anapata 60% ya ardhi iliyopimwa na Kampuni inapata 40% ya ardhi iliyopimwa
Alifafanua kuwa asilimia 40% inayotolewa kwa Kampuni inatumika katika kuandaa michoro ya ubunifu wa mipango Miji (10%),kupima viwanja (10%)kuchonga barabara (10%) na faida ya Kampuni (10%) na kwamba mradi huu hauhusishi malipo ya fidia yoyote hii ni kwa makubaliano ya wananchi wenyewe na itakuwa kwa kusogezana
Afisa huyo alisema kuwa maeneo ya umma kama vile soko,shule,zahanati ,makaburi,stendi,msikiti,kanisa na maeneo ya wazi(open space) yatatolewa bure katika mradi huo na kufanywa kuwa mradi wa kwanza kuibuliwa na wananchi wenyewe kwa kuitumia Kampuni ya Ardhi Plan kupanga mji wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea
Alieleza kuwa gharama za mradi huo zinatolewa na wananchi wenyewe kwa kutoa ardhi badala ya kusubiri Serikali mpaka ipate uwezo wa kifedha ambapo kwa wale wenye maeneo madogo yaani kiwanja kimoja mpaka viwili wanatozwa gharama ya fedha shilingi laki moja(100,000/=) kwa kiwanja kimoja na laki mbili(200,000) kwa viwanja viwili kama gharama za upimaji
Kibiki alisema kuwa mitaa ambayo michoro yake imekamilika ni Mshangano,Namanyigu, na Mitendewawa yenye jumla ya viwanja elfu kumi na nane (18,000/=) ambapo mitaa mingine itafuata baadaye
“Mchoro ambao tayari mawe yameshapandwa ni mchoro namba 9 ujulikanao kama Beroya na sasa wananchi wanaendelea na uchongaji wa barabara mchoro ambao una jumla ya viwanja 800”alisema Kibiki
Alisema kuwa mradi huo umesifiwa na viongozi wengi na wanaharakati mbalimbali wa masuala ya ardhi na maendeleo ya wananchi wanyonge kwani wamefanikiwa kupata maeneo yaliyopimwa na kuthaminiwa kwa ajili ya makazi yao na kuondokana na makazi holela
“Tunaomba wananchi wa maeneo mengine wenye matatizo kama yetu watuunge mkono wafanye kama tulivyofanya sisi kwani watapata maisha bora kwani thamani ya ardhi yao itapanda na kuwa na thamani kubwa”alisema
Alieleza zaidi kuwa huduma za jamii kama maji ya bomba,umeme,barabara na miundombinu mingine itawafikia kama ambavyo wananchi wa kata ya Mshangano wanavyotegemea kupata mara baada ya mradi kukamilika
Kibiki alisema kuwa katika mradi huo wananchi watapata faida nyingi ikiwemo ya ajira kuanzia hatua ya kupima viwanja kwani mchoro mmoja umetoa ajira kwa watu 40 ambao wamekuwa wanalipwa Tshs 4000/= kwa kutwa moja na kwamba kwa michoro 23 itatoa ajira kwa watu 920
Alifafanua kuwa kwenye uchongaji wa barabara mchoro mmoja umetoa ajira kwa watu 80 ambapo kila mmoja analipwa Tshs 5000/= kwa kutwa hivyo michoro 23 itatoa ajira kwa watu 1840 ambapo jumla ya michoro yote 23 wananchi watakao kuwa wamepata ajira kwenye upimaji na kuchonga barabara ni watu 2760 wanawake na wanaume
Alieleza jumla ya fedha watakayokuwa wanapata wananchi wa kata hiyo kwenye upimaji wa viwanja ni 920X4000=3680,000/= na kwenye uchongaji wa barabara 1840x5000=9,200,000/= na kufanya jumla ya fedha yote kuwa ni Tshs 12,880,000/= kwa siku
Alifafanua kuwa wafanyakazi hao watatoka ndani ya kata ya Mshangano ambapo mradi unatekelezwa kwani hiyo inaweza kuwasaidia sana wananchi kujikimu kimaisha na kumudu kununua pembejeo za kilimo katika msimu huu na hivyo kuzalisha mazao kwa wingi
Naye Diwani wa Kata ya Mshangano Faustine Mhagama akizungumza kwenye uzinduzi huo alisema kuwa mti wenye matunda ndio unaopigwa mawe hivyo kwa kuwa mradi huo una manufaa kwa wananchi wake umekuwa ukipigwa sana mawe,lakini hata hivyo anasema atasimamaimara kupigania haki za wananchi wake.
Anasema kuwa kwa mradi huo wananchi wamenufaika kwa kuweza kuuza viwanja vyao kwa bei kubwa lakini pia Halmashauri imepunguziwa gharama ya kulipa fidia ambayo mara nyingi imekuwa ikichelewa kulipa au kushindwa kulipa na kuzua malalamiko na migogoro kwa wananchi
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Ardhi Plan inayopima viwanja hivyo Gombo Samandito anasema kuwa Mradi huo ni wa aina yake hapa Nchini na kwamba hakujawahi kuwa na mradi kama ule wa kupima viwanja 18,000 kwa muda mfupi tangu nchi ipate uhuru na kwamba dhamira yao ni kuona wananchi wakiishi katika makazi bora.
Samandito alisema kuwa mradi huo umeisaidia sana Serikali kwani umeipunguza tatizo la kushindwa kupanga mji kutokana na ukosefu wa fedha za kugharamia mipango stahiki ya makazi bora kwani wananchi wa Mshangano wamethubutu kupanga mji kwa gharama zao jambo ambalo halijawahi kutokea kwa wananchi kupima viwanja vingi kiasi hicho kwa gharama zao
Mwandishi wa Makala
Anapatikana Simu 0755-335051/0715-335051/0784-335051/0778-335051
Barua pepe;stephano12mango@yahoo.com
WANANCHI SONGEA KUPIMIWA VIWANJA 18,000 KUONDOKANA NA MAKAZI HOLELA
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ardhi Plan Gombo Samandito akiwaonyeshwa wananchi RAMANI zilizopitishwa na Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya upimaji wa viwanja kata ya Mshangano
Na Joseph Mwambije,Songea
HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma imezindua mradi wa upimaji viwanja zaidi ya 18,000 unaofanywa na Kampuni binafsi ya Ardhi Plan Limited kwenye Kata ya Mshangano baada ya kuibuliwa na wananchi wenyewe baada ya kuona wanaishi katika makazi holela kwa muda mrefu.
Mradi huo umezinduliwa juzi na Meya wa Manispaa ya Songea Charles Mhagama aliyewakilishwa na Mwenyekiti wa huduma za jamii na elimu wa Manispaa hiyo Genifrida Haule aliyekata utepe kuzindua mradi huo.
Akizungumza baada ya kuzindua mradi huo Haule alisema Mradi huo utawainua kiuchumi wananchi wa Kata ya Mshangano kwa sababu wataweza kukopaa kupitia makazi yao na kwamba wataweza kuishi katika makazi bora,
‘Suala la upimaji viwanja ni hatua kubwa ya maendeleo kwa kuwa baada ya upimaji miundombinu ya maji na umeme itakuja na wananchi wameongeza kipato kwa kuweza kukopa na kuendesha miradi kupitia viwanja vyao na nyumba zao huku viwanja vikipandishwa thamani’alisema.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa Mradi huo Afisa Mtendaji wa Kata ya Mshangano Stan Kibiki alisema Kata hiyo ina Kaya 1508 zenye wakazi 7540 na mitaa mitano ya Mshangano,Namanyigu,Chandarua,Mitendewawa na Muhumbezi.
Alisema kuwa wananchi baada ya kuona kwa muda mrefu wanakaa na kuishi katika makazi holela yasiyopimwa wakaamua kuibua Mradi wa upimaji viwanja hasa baada ya kupeleka maombi ya kupimiwa viwanja Halmashauri lakini ilishindwa kuwapimia kwa kile ilichodai kuwa haina fedha.
“Mwaka 2010 Kata yetu ilipata bahati ya kupata mradi wa upimaji viwanja ulioendeshwa na Manispaa ya Songea lakini fedha ilikuwa kidogo na hivyo waliweza kupima viwanja 347 tu katika Mtaa mmoja wa Namanyigu katika eneo dogo na hivyo tatizo la wananchi kuishi katika makazi holela likabaki palepale’alisema katika taarifa hiyo.
Alisema kuwa wananchi katika kutatua tatizo hilo kwa kushirikiana na viongozi wao waliamua kutafuta njia mbadala kwa kutumia sheria namba 8 ya ya mipango miji ya mwaka 2007 walitafuta Kampuni ya Ardhi Plan Limitedya Dares-salaam ili iweze kuwapimia viwanja katika maeneo yao.
Alisema Mitaa ambayo michoro yake imekamlika ni Mshangano,Namanyigu, na Mitendewawa yenye jumla ya viwanja 18,000 na mitaa mingine itafuata baadaye na kufafanua kuwa mchoro namba 9 wa Beroya wenye viwanja 800 umekamilika na kazi ya kuchonga barabara inaendelea.
Afisa Mtendaji huyo alisema mradi huo umesaidia kutoa ajira kwa wananchi kwa kuwa mchoro mmoja umetoa ajira kwa wananchi 40 ambao walikuwa wanalipwa sh. 4000 kwa kutwa na kwamba michoro23 ya mradi huo itatoa ajira 920.
Alisema katika uchongajio barabara mchoro mmoja unatoa ajira kwa watu 80 ambapo kila mmoja analipwea sh. 5000 na kwamba wananchi 2760 wanawake na wanaume watakuwa wamepata ajira katika zoezi la uchongaji wa barabara.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni hiyo inayopima viwanja hivyo Gombo Samandito anasema kuwa Mradi huo ni wa aina yake hapa Nchini na kwamba hakujawahi kuwa na mradi kama ule wa kupima viwanja 18,000 kwa muda mfupi tangu nchi ipate uhuru na kwamba dhamira yao ni kuona wananchi wakiishi katika makazi bora.
Naye Diwani wa Kata hiyo Faustin Mhagama anasema mti wenye matunda ndio unaopigwa mawe hivyo kwa kuwa mradi huo una manufaa kwa wananchi wake umekuwa ukipigwa sana mawe,lakini hata hivyo anasema atasimamaimara kupigania haki za wananchi wake.
Anasema kuwa kwa mradi huo wananchi wamenufaika kwa kuweza kuuza viwanja vyao kwa bei kubwa lakini pia Halmashauri imepunguziwa gharama ya kulipa fidia ambayo mara nyingi imekuwa ikichelewa kulipa au kushindwa kulipa na kuzua malalamiko na migogoro kwa wananchi.
MWISHO
Saturday, November 12, 2011
MAGARI YA ABIRIA YAKWAMA KITUO CHA MABASI KUTOKANA NA MVUA
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Nachoa Zakaria
Na Mwandishi Wetu, Songea
WAKAZI wa Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wakiwemo wamiliki wa mabasi yanayo safirisha abiria wameulalamikia uongozi wa Halmashauri ya Manspaa hiyo kutokana na kushindwa kuzifanyia ukarabati barabara pamoja na kituo kikuu cha mabasi ambacho kimekithili kuwa na ubovu ambao umesababisha kuwepo na mashimo mengi katikati ya kituo hicho na kupelekea magari kukwama wakati mvua zinaendelea kunyesha
Mtandao huu wa stephanomango.blogspot.com ulitembelea kituo hicho cha mabasi kwa lengo la kujionea hali halisi ya ubovu wa miundo mbinu kwenye eneo hilo ambalo lilikuwa limejaa tope wakati mvua zinaendelea kunyesha huku mabasi yaliyosheheni abiria yakiwa yametitia kwenye tope hilo.
Uharibifu huo ambao umechangia kwa kiasi kikubwa kujaa kwa tope na kusababisha wananchi na magari kupita kwa tabu na mengine kukwama kabisa kutokana na utelezi uliotokana na uongozi wa Halmashauri hiyo kuridhia kumwaga kifusi cha udongo wa mfinyaji katikati ya kituo hicho kwa madai kuwa wanafukia mashimo yaliyokithili kwenye eneo hilo jambo ambalo limeonekana kuwa ni kero kubwa kwa wakazi wa Songea wakiwemo abiria na wamiliki wa mabasi .
Hali hiyo ndiyo iliyopelekea watumiaji wa kituo hicho kutoa malalamiko yao kwa Halmashauri ya Manispaa ya Songea wakidai kilio chao cha kutengenezewa stendi hiyo kimekuwa ni cha muda mrefu na kitu cha kushangaza hakuna hatua zozote zinazo chukuliwa kwa ajiri ya kukinusuru kituo hicho ambacho kipo katikati ya Manispaa hiyo
Mmoja wa wakazi wa Manispaa ya Songea Lucas Haule alisema inashangaza kuona kituo hicho ambacho kimekuwa kikilalamikiwa kwa muda mrefu kutokana na miundo mbinu yake kuwa mibovu huku Halmashauri ikitoza ushuru mkubwa kwa magari yanayo ingia kwenye kituo hicho yakiwemo mabasi ya kusafirishia abiria .
Nae mmoja wa watumiaji wa kituo hicho cha mabasi Paulo Ndunguru alisema kuwa anashangazwa kuona kituo hicho kilicho kithiri mashimo kinatengenezwa kiholela bila kufuata utaalamu na kudai kwamba endapo kama ungetumika utaalamu yakinifu tatizo hilo la kukwama kwa magari katikati ya kituo lisingeweza kujitokeza .
Hata hivyo jitihada zilizofanywa na mtandao huu za kumpata mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa hiyo Nachoa Zakaria ziligonga mwamba baada ya kutopatikana ofsini kwake ambapo Katibu muhutasi wake alieleza kuwa Mkurugenzi alikuwa kwenye vikao vya maandalizi ya mapokezi ya mwenge na maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru na kwamba simu yake ya kiganjani alipopigiwa mara tatu iliita bila kupokelewa.
MWISHO
WANANCHI WATWANGANA KUGOMBEA ARDHI WILAYANI TUNDURU
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Madaha
Na Augustino Chindiye,Tunduru
MAPIGANO makali ya kugombea Ardhi ya kulima yamezuka kati ya wakazi wa vijiji vya Semeni Chikomo Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma na kumjeruhi kwa kukata kata kwa Mapanga mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mohamed Abdalah.
Kufuatia tukio hilo majeruhi huyo amelazwa katika Hospitali ya Missioni ya Mbesa baaya ya kujeruhi vibaya sehemu mbali mbali za mwili wake hali iliyo pelekea zaidi ya watu 50 wakazi wa kijiji cha Chikomo Wilayani humo wanatafutwa na Polisi ili waweze kujibu tuhuma hizo zilizotokaka na wananchi wa vijiji hivyo kuanzisha mapigano hayo.
Wakizungumzia tukio hilo kwa nyakati tofauti mbali na kukiri kutokea kwa ugomvi huo madiwani wa Kata za Mtina Mahamudu Katomondo na Kata ya Mbesa , Mohamedi Mtiko kila mmoja wao alitoa lawama kuwa wananchi wa kijiji jirani ndio chanzo cha mgogoro huo.
Upande wa Diwani wa kata ya mtina Katomondo yeye alidai kuwa wananchi wa kijiji cha Chikomo ndio waliofanya makosa ya kuvamia mipaka ya kijiji chake akidai kuwa mpaka unaotenganisha kijiji cha Semeni na Chikomo iliwekwa eneo la ng’ambo ya Mto Lukumbule.
Wakati diwani huyo akitoa madai hayo Diwani wa Kata ya Mbesa Mtiko yeye alidai kuwa na watu watatu waliohusika wakati wa upimaji wa mipaka hiyo mwaka 1978 na wanayo ramani hiyo inayo onesha mipaka ya vijiji hivyo na kwamba ugomvi uliopo kati ya vijiji hivyo umetokana na wananchi wa kijiji cha Semeni kukaidi kulipa ushuru unaotakiwa kutozwa pindi wakulima wanapovuka mipaka na kwenda kulima kijiji jirani.
Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo,Katibu tawala wa Wilaya ya Tunduru Martini Mulwafu mbali na kukiri kuwepo kwa mgogoro huo alisema kuwa ofisi yake imepanga kufanya mazungumzo kati ya viongozi kutoka katika Tarafa, kata na vijiji vinavyohusika na mgogoro huo ili kutafuta ufumbuzi wa kudumu.
Subscribe to:
Posts (Atom)
