About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Thursday, December 29, 2011

WAKUU WA MIKOA INAYOLIMA KOROSHO KUANDAMANA KUMUONA RAIS JAKAYA KIKWETE

Na,Steven Augustino Tunduru

WAKUU wa Mikoa inayolima Korosho  nchini wameahidi kupeleka kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete kero ya ubabaishaji wa bei ya soko la zao hilo ili aweze kulitafutia ufumbuzi wa kudumu zikiwa ni juhudi za kuwawezesha Wakulima kupata matunda ya jasho lao.

Hayao yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma  Saidi Mwambungu wakati akiongea na wadau wa maendeleo waliojitokeza katika kikao cha dharula cha kujadili hatima ya tukio la ubabaisshaji wa soko la Korosho ambalo msimu huu bei yake imeonesha kusuasua kilichofanyika katika ukumbi wa Boma la halmashauri ya Wilaya hiyo mjini hapa .

Sambamba na maamuzi hayo pia Mwambungu na kamati hiyo ikatoka na azimio la kutouza Korosho hizo kwa Makampuni hayo babaishaji vinginevyo wakubali kununua Korosho hizo kwa Bei itakayo kubalika na wakatumia nafasi hiyo kumuomba Meneja wa Benki ya Nmb Omari Mleche kuongeza mkopo kwa vyama vya msingi ili kuwezesha kununua Korosho zote kwa wakulima wakati juhudi za kutafuta Soko la uhakika zikiendelea.

Akifafanua taarifa hiyo Mwambungu alisema kuwa maamuzi hayo yamefikiwa na Wakuu wa Mikoa ya Lindi Ruvuma na Mtwara baada ya kubaini kuwerpo kwa ubabaishaji wa Soko hilo ulio oneshwa na Wanunuzi hao wakubwa Korosho katika Msimu huu hauwezi kufumbiwa macho na Serikali na kuwaacha Wakulima wakiteseka bila msaada wa Serikali yao. 

Awali wakitoa taarifa ya ubabaishaji wa Soko la Mazao hayo Meneja wa Chama Kikuu cha Wakulima wa Korosho TAMCU Ltd  Imani Kalembo na Mwenyekiti wa  Chama hicho Mahamudu Katomondo walisema kuwa  ubabaishaji huo umeonekana katika minada mitatu iliyopita ambapo Makampuni ya Abbas Eport Treding Co.Ltd na Olam Co. Ltd awali wote waliomba kununua chini ya Bei  ya Tsh. 1500 kwa kilo moja hali iliyo onesha kuwa makampuni hayo yana ajenda ya siri ya kutaka chama hicho kishindwe kuwalipa Wakulima wake malipo yao ya awamu ya pili.

Walisema kinacho watia mashaka zaidi viongozi hao na kuwafanya wabaini uwepo wa mchezo mchafu kutoa katika Makampuni hayo ni kitendo cha Makampuni hayo pekee kati ya Makampuni 70 ambayo yalijiandikisha na kuomba kununua Korosho hizo katika Msimu huu wa Mwaka 2011/2012,

Wakizungumzia taarifa ya ununuzi Korosho hizo kutoka kwa wakulima walisema kuwa hadi sasa vyama vya msingi vya ushirika vime kwisha kusanya jumla ya Kilo 4,554334 kati ya Kilo 7,000,000 zinazotarajiwa kununuliwa katika Mismu huu na chama chao.

 Wakitoa maoni yao wabunge wa Wilaya ya Tunduru  Eng. Ramo Makani na Alhaji Mtutura Mtutura waliiomba Serikali kutumia Fedha zilizo idhinishwa katika Bajeti iliyopita kwa ajili ya Matumizi ya dhalula ili zitumike kununula Korosho hizo kutoka kwa Wakulima zikiwa ni juhudi za kuwaondolea adha hiyo.

Nao Madiwani Kazembe said  wa kata ya Ligunga na Burhani Nakanje wa Kata ya Marumba mbali na kuutuhumu uongozi wa Kiwanda cha Kubangulia Korosho kinacho milikiwa na Kampni ya Korosho Africa Ltd kuto kuwa na msaada kwa wakulima wa Wilaya yao waliiomba Serikali kuwa na macho na Wanunuzi hao vinginevyo watawaangusha na kuwafanya wananchi kukosa imani na Serikali yao.

Wakijibu tuhuma za Kiwanda hicho kuto kuwa na msaada kwa Wakulima wa zao hilo msimamizi wa Kiwanda hicho Dinesh Poojali na Enginia wa Kiwanda hicho Sivan Edayath mbali na kutoa taarifa kuwa kiwanda chao kimefungwa kutokana na kuishiwa Korosho za kubangua walisema kuwa wao hawana maamuzi yoyoyte juu ya ununuzi wa korosho hizo kutoka katika vyama vya ushirika vya msingi vya Wakulima wa Tunduru. 

Mwisho

MTANDAO WA SONNGO WAWAKUTANISHA WANANCHI WA KADA TOFAUTI KATIKA MDAHALO WA KUJADILI KATIBA YA MWAKA 1977


 Mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi zisizo za Kiserikali Wilaya ya Songea Siwaji Gama akifungua mdahalo,wa kwanza kushoto ni Afisa Habari wa Sonngo Endrwe Chatwanga,wa kwanza kulia ni Boniface Bundala, wa pili kulia ni Katibu wa Sonngo Mathew Ngarimanayo
 Washiriki wa mdahalo huo wakiendelea kusikiliza hoja mbalimbali zinazoendelea kuwasilishwa na jopo la wataalamu wa sheria na katiba
 Waandishi wa Habari wakisikiliza majadiliano katika mdahalo huo,kutoka kushoto ni Catherine Nyoni (Tbc) Amon Mtega(Mtanzania) Gideon Mwakanosya(Nipashe) Joseph Mwambije(Majira)

Washiriki wakisikiliza kwa umakini mapitio na uchambuzi wa wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 Jimbo la Songea Mjini

Tuesday, December 27, 2011

WADAU WA MTANDAO HUU WAMWEMELEKA KWENYE KUMBUKIZI ZA KUZALIWA KWA MDAU MWENZAO WA MTANDAO EMMANUEL NTOBI

 Keki iliyotengenezwa kwa ubora wenye viwango stahiki maalumu kwa kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwa Emmanuel Ntobi

Emmanue Ntobi akijiandaa kuwasha baruti huku akishuhudiwa na Mpenzi wake Bi Sarah Mohamed




 Emmanuel Ntobi akimrisha keki ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwake mpenzi wake Bi, Sarah Mohamed
 Emmanuel Ntobi akimrisha keki Mr Ng'aida kwenye sherehe hiyo

 Mdau wa Mtandao huu Stephano Mango akipata keki tamu iliyoandaliwa kwa ajili ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Emmanuel Ntobi wakati wa sherehe hiyo ya aina yake iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Benki ya biashara ya NBC juzi usiku muda mfupi kabla Bwana wetu yesu Kristu ajazaliwa ndio maana Ntobi Emmanuel alibatizwa jina hilo likiwa na maana ya Bwana pamoja nasi 






Wadau mbalimbali wakiendelea kupata chakula na vinywaji vya aina mbalimbali kwenye sherehe hiyo iliyofana

MUUGUZI WA KIJIJI CHA MANGO AJINYONGA KUTOKANA NA WIVU WA KIMAPENZI

                                              
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda
Na Gideon Mwakanosya ,Songea
MUUGUZI wa Zahanati ya kijiji cha Mango kilichopo kata ya Kihagara wilayani Mbinga Bosco Nchimbi (29) amekutwa  kwenye kenchi ya chumba chake akiwa amekufa baada ya kujinyonga  kwa kujitundika  juu ya kenchi kwa kutumia kamba ya katani.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda amesema kuwa tukio hilo limetokea juzi majira ya saa kumi jioni  huko katika kijiji cha Mango , ambapo katekista wa kijiji cha Tumbi  Joseph Nchimbi ndiye aliyegundua   kuwepo kwa tukio la kujinyonga Nchimbi .
Amefafanua kuwa, Inadaiwa siku ya tukio kateksta Nchimbi alikuwa ameenda nyumbani kwa Marehemu  kwa ajili ya kumpa ushauri  baada ya kuwepo malumbano  kati yake na Mwanamke aliyezaa naye mtoto  anayedaiwa kuwa alikuwa akilalamikiwa kuwa ameanza kufanya ngono na wanaume wengine wakati mtoto wao bado ni mchanga.
Kamanda alieleza zaidi kuwa Katekista Nchimbi  baada ya kugundua  tukio hilo  alitoa taarifa kwa uongozi wa serikali ya kijiji cha Mango  ambao nao ulitoa taarifa polisi  na askari polisi walipofika katika eneo la tukio wakiwa wameongoozana na Mganga walikuta mwili wa marehemu  ukiwa unaninginia  .
Kamanda amesema,chanzo cha kujinyonga ni wivu wa mapenzi   kati yake na mwanamke aliyezaa naye ambaye wakati wote alikuwa akimuonya kuacha tabia ya kufanya mapenzi na wanaume ovyo kwani anamuaharibu mtoto  wao mchanga lakini mwanamke huyo aliendelea hali iliyosababisha apandwe na hasira na kuchukua huamuzi huo.
MWISHO.

Monday, December 26, 2011

Nawatakia Sikukuu njema za X-MASS,BOXING DAY,na MWAKA MPYA wa 2012 wenye Baraka na mafanikio makubwa


Nawasalimu wadau wote wa mtandao wa www.stephanomango.blogspot.comkwa kunipa ushirikiano wenu katika kipindi chote cha mwaka 2011

Nawatakia heri sana katika msimu huu wa mwishoni mwa mwaka 2011 na maandalizi mema ya mwaka mpya wa 2012





God is Love

Christmas is all about love

Christmas is thus about God and Love

Love is the key to peace among all mankind

Love is the key to peace and happiness within all creation

Love needs to be practiced - love needs to flow - love needs to make happy

Love starts with your partner, children and family and expands to all world

God bless all mankind

VIONGOZI NCHINI WATAKIWA KUWATUMIKIA WANANCHI ILI KULINDA AMANI YA NCHI

Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Songea Norbert Mtega
 
Na, Augustino Chindiye Tunduru

VIONGOZI wa kuchaguliwa na waliopewa mamlaka ya kulitumikia Taifa wameombwa kuitumikia Jamii kwa uadilifu ili kuendelea kudumisha amani na utulivu vinginevyo kuna hatari ya amani hiyo inayojivuniwa na taifa letu kutoweka.

Rai hiyo imetolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo la TUNDURU- Masasi Castory Msemwa wakati akiongea na waamini waliohudhulia katika Misa takatifu ya kukumbuka kuzaliwa Yesu Kristo ya Noeli iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Xavery mjini hapa.

Akifafanua taarifa hiyo kupitia Mahubiri hayo Askofu Msemwa alisema kuwa pamoja na Viongozi hao kufahamu hayo lakini wamekuwa walafi hali ambayo imekuwa ikiwasukuma kuwatesa Wananchi waliowapa nyadhifa hizo .

Alisema mbali na hali hiyo kuonekana wazi kwa Viongozi wa Serikali lakini pia matukio kama hayo yamekuwa yakiwakumba viongozi wa Dini ambapo wamekuwa wakipenda kujinufasha ili waendeelee kuongeza furaha mioyoni mwao kwa kujipangia marupurupu yao wenyewe bila kuwajali wengine na kuiacha jamii ikiteseka bila misaada yao.

Askofu Msemwa akatumia nafasi hiyo kuhimiza upendo miongoni mwetu na kueleza kuwa endapo upendo utaendelea kutoweka kuna hatari ya amani tunayo jivunia kumomonyoka na kuipeleka nchi yetu pabaya.

Katika hutuba hiyo pia Askofu Msemwa akaikumbusha jamii kuiga mwenendo wa mwasisi wa Taifa la Watanzania Mwenyeheri Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mtumishi wa Mungu Sister Bernadeta wa Jimbo la Perahimo ambaye amekuwa gumzo kubwa kutokana na watu wengi kwenda kuomba katika kaburi lake na kufanikiwa.

Alisema Sister Bernadeta alitangazwa hivi karibuni kuwa mtumishi wa Mungu ukiwa ni mchakato wa kufikia nafasi ya Mwenyeheri na kongeza kuwa mapendo ya kweli katika jamii yao ndiyo yaliyowafanya waendelee kukumbwa na jamii yao .

Mwisho

Thursday, December 22, 2011

DIWANI MSTAAFU GOLDEN SANGA (SANGA ONE) ATOA MSAADA WA ELFU HAMSINI KWENYE KIKUNDI CHA SANAA CHA WAZALENDO KWA AJILI YA MAANDALIZI YA UZINDUZI WA FALAMU YAO YA MAJARIBU

 Diwani Mstaafu wa Kata ya Bombambili Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma Golden Sanga maarufu kwa jina la Sanga One akimkabidhi shilingi elfu hamsini(50,000/=) Mwenyekiti wa kundi la sanaa la Wazalendo Abdalah Bin Ahmed kwa jina la kisanii Ramsh,katikati ni Mlezi wa kundi hilo Mama Ndimbo,wa kwanza kushoto ni Mhasibu wa kundi hilo Zainab Nungu kwa jina la kisanii Walda
 Diwani Mstaafu Sanga One akizungumza na kundi la wasanii la Wazalendo mara baada ya kukabidhi msaada wa fedha kwa ajili ya maandalizi ya uzinduzi wa filamu mpya ya kundi hilo,Katikati Mlezi wa kundi hilo Mama Ndimbo,wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa kundi hilo Abdalah Bin Ahmed-Ramsh
 Sanga One akiwa kwenye picha ya pamoja na wasanii wa kundi la Wazalendo mara baada ya kuzungumza nao hivi karibuni kwenye ukumbi wa Better Life Tanzania mjini Songea
Baadhi ya wasanii wa kundi la Wazalendo wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wao

KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI WA HALMASHAURI YA SONGEA CHAANZA ASUBUHI HII KATIKA JENGO LA MAENDELEO

 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Beatrice Msomisi akiwasalimia wajumbe wa Baraza la Madiwani
 Kutoka kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho Jenista Mhagama,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Beatrice Msomisi,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Songea Rajabu Mtiula,Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Andrwe Mhagama
 Madiwani wa Halmashauri ya Songea wakiendelea na kikao chao kilichofanyika kwenye ukumbi wa jengo la Maendeleo(Mnara wa saa)
Wataalamu na wakuu wa idara mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea wakisikiliza kwa umakini hoja mbalimbali zinazoendelea kuwasilishwa kwenye kikao hicho

Wednesday, December 21, 2011

VETA SONGEA YATOA MAFUNZO KWA MADEREVA WA PIKIPIKI 106



Na Gideon Mwakanosya, Songea

MKUU wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu amewahimiza vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha nne Mkoani humo ambao wameshindwa kupata nafasi ya kuendelea na masomo  ya elimu ya kidato cha tano waone umuhimu wa kujiunga na mafunzo ya elimu ya ufundi stadi yanayoendeshwa na VETA SONGEA ambayo yataweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika kukabiliana na tatizo la ajira lililopo hapa nchini.

Ushauri huo umetolewa hivi karibuni na Mkuu wa Mkao wa Ruvuma Said Mwambungu wakati wa maafari ya nne ya wanafunzi walio hitimu mafunzo ya udereva wa magari ya abilia yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo cha elimu na mafunzo ya ufundi stadi(VETA MJINI SONGEA).

Alisema kuwa mafunzo ya ufundi stadi yanayotolewa na VETA SONGEA yameonekana kuwa ni msaada mkubwa kwa wakazi wa maeneo mbalimbali kutoka wilaya za Mbinga, Tunduru, Namtumbo na Songea ambao wengi wao baada ya kuhitimu kozi walizosomea wameweza kupata ajira na wengine wamejiajili wao wenyewe.

Amefafanua kuwa kutokana na hali hiyo serikali Mkoani humo inaendelea kuwahimiza wazazi wa watoto waliomaliza sekondari ambao wameshindwa kuendelea na elimu ya kidato cha tano wawapeleke VETA ambako wataweza kupatiwa elimu ya ufundi stadi ambayo wakihitimu na kufahulu vizuri wataweza kuajiriwa serikalini, kwenye makampuni ya watu binafsi na wengine wataweza kujiajiri wao wenyewe badala ya kuwaacha waendelee kulandalanda mitaani ambako wanaweza kujifunza mambo mabaya.

Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha elimu na ufundi stadi (VETA SONGEA) Gideon Ole Lairumbe  alisema kuwa VETA SONGEA ni chuo cha mafunzo stadi ambacho kinatoa huduma Mkoani Ruvuma ambacho ni moja wapo ya vyuo vilivyopo chini ya mamlaka ya elimu na mafunzo stadi(VETA).

Alisema kuwa kutokana na hali hiyo chuo chake kimeendesha mafunzo ya ufundi stadi kwa kozi mbalimbali ambapo alizitaja kuwa ni udereva wa magari wa madaraja yote, udereva wa pikipiki, saluni, kompyuta, uhazili, ufundi wakutengeneza kompyuta, umeme jua, umeme wa majumbani na ufundi wa magari.

Alibainisha zaidi kuawa kwenye maafari ya 4 ambayo wahitimu 106 wamepata vyeti ni wale waliokuwa wanajifunza udereva wa magari ya abilia ambao waliotokea  wilaya za Tunduru, Mbinga, Namtumbo na Songea ambapo alidai kuwa kwakuwa serikali ina mpango wa kubadirisha leseni za magari ya kubeba abilia VETA SONGEA tayari imetoa mafunzo yakinifu ya udereva wa magari makubwa yakiwemo ya kubeba abilia.

Ole Lairumbe alieleza kuwa pia VETA SONGEA imekuwa ikifanya kazi yakutoa mafunzo ya udereva wa magari na pikipiki kwa kushirikiana na taasisi zote ambazo kwa njia moja au nyingine zina uhusiano na fani hiyo kama vile Polisi, Sumatra, Takukuru, Kikosi cha zima moto na Bima.

Aliongeza kuwa kila mwezi kunakuwa na wahitimu takribani 40 ambo ni wa kozi wa kuendesha udereva wa pikipiki ambapo kwa wilaya ya mbinga VETA SONGEA inaendesha mafunzo ya udereva wa pikipiki kwa kushirikiana na chuo cha maendeleo ya wananchi mbinga (FDC) ambako novemba mwaka huu wanafunzi 56 wamehitimu mafunzo ya kozi ya kuendesha pikipiki na kwa wilaya ya Tunduru VETA SONGEA imekuwa ikiendesha mafunzo kwa kushirikiana idara ya ujenzi ambako wanafunzi 23 walikuwa wanachukua mafunzo ya udereva wa magari madogo na wanafunzi 45 walikuwa wanajifunza uendeshaji pikipiki.

Mkuu huyo wa Chuo cha VETA SONGEA Ole Lairumbe alisema  baada ya serikali kuruhusu pikipiki kutumika kama chombo cha usafiri wa kubebea abilia  jamii hapa nchini imeshuhudia ongezeko la ajali nyingi barabarani jambo ambalo limekuawa likisababisha hasara kubwa kwa serikali kwa kuwahudumia waathirika wa ajari zinazotokana na uendeshaji mbaya wa pikipiki hivyo kutokana na hali hiyo ndiyo maana chuo chake kimejikita kutoa mafunzo ya uendeshaji wa pikipiki.

Na kwamba VETA inaendelea kuwahamasisha wakazi wa maeneo mbalimbali Mkoani humo wakiwemo wa vijiji vya Lituhi, Mbambabay na Kindimba juu amboko VETA imefungua madarasa ya kozi ya kuendesha pikipiki waone umuhimu wa kujifunza sheria za usalama barabarani na namna ya kumudu usukani kuliko kuendesha pikipiki bila ya kuwa na mafunzo ya aina yeyote jambo ambalo linaweza kusababisha ajali mara kwa mara.

Mwisho.

Monday, December 19, 2011

KAPTENI KOMBA AICHARUKIA WIZARA YA UJENZI KWA DHARAU WALIZOZIONYESHA MBELE YA WAPIGA KURA WAKE NYASA

         Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi Kapteni John Komba
Na Gideon Mwakanosya,Nyasa
WANANCHI wa vijiji vya Mwelampya, Mkaya, Ngingama, Kihulu na Litui Wilayani nyasa Mkoa Ruvuma na wananchi wa vijiji vya kipingu, ngelenge, msungu na mbongo Wilayani Ludewa Mkoa wa Iringa wameilalamikia serikali kupitia wizara ya ujenzi hapa nchini kwa kuchukua uamuzi wa kuing’oa injini 1 kati ya injini 2  zilizokuwa zikitumika kwenye pantoni ambayo ilikuwa ikiwasaidia wananchi wa vijiji hivyo kuvuka kwenye mto Ruhuhu na kuiamishia kwenye pantoni iliyoko mto Ifakara Kilombelo Mkoani Morogoro
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mtandao wa www.stephano,mango.blogspot.com  huko katika kijiji cha Lituhi wameonesha kusikitishwa kwa kiasi kikubwa pale Meneja wa wakala wa ufundi na umeme Mkoani Ruvuma (TEMESA) pamoja na timu yake kufika ghafla kwenye kijiji hicho na kwenda kuingoa injini moja iliyokuwa ikitumika kwenye pantoni iliyoko mto Ruhuhu ambayo kwa sasa imesimamishwa .
Benadi Komba mkazi wa kijiji cha Lituhi ameelaza kuwa kwa muda mrefu wananchi wavijiji vilivopo kandokando ya ziwa nyasa walikuwa na kero kubwa ya usafiri kwenye ziwa nyasa pamoja na kivuko cha mto Ruhuhu ambako kwa miaka iliyopita wananchi wa vijiji hivyo walikuwa wakivuka mto Ruhuhu kwa kutumia mitumbwi huku wakiofia maisha yao na wengine kupoteza maisha.
Amesema kuwa kufuatia kilio hicho walichokuwa nacho kwa muda mrefu kupita kwa Mbunge wa jimbo la mbinga magharibi Kapteni mstaafu John Komba serikali ilisikia kilio hicho kisha ilileta pantoni ambayo imekuwa ikiwasaidia kuvuka mto huo kwa urahisi zaidi lakini ameshangazwa na kitendo cha wakala wa ufundi wa umeme Mkoni Ruvuma (TEMESA) kufika Lituhi na kuingoa injini iliyokuwa kwenya pantoni ambayo ilikuwa ikiwasaidia kwa urahisi kutoka Lituhi kwenda vijiji vya ngerenge, Ilele, Msungu, Mbongo na Kipingu Wilayani Ludewa Mkoani Iringa ambako kunahuduma muhimu za kilimo na biashara.
Sebasiani Inju mkazi wa kijiji cha kihuru ameiomba serikali kupitia wizara ya ujenzi kuchukua hatua za haraka kuirudisha injini hiyo iliyochukuliwa kwenye pantoni iliyoko kwenye mto Ruhuhu kwa madai kuwa imepelekwa Ifakara, Kilombelo Mkoani Morogoro ambako injini 1 ya pantoni ilikuwa imeharibika.
 Kwa upande wake Afisa mtendaji wa kijiji cha Lituhi Joseph Chawala amesema kuwa kwa muda mrefu kanisa katoliki Jimbo la Mbinga limekuwa likitoa huduma ya afya nzuri kwa wakazi wa vijiji vilivyo kandokando ya ziwa nyasa kupitia kituo chake cha afya ambacho kipo lituhi ambacho kimekuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa vijiji mbalimbali vya wilaya ya nyasa mkoani Ruvuma na wilaya ya Rudewa Mkoani Iringa ambapo alihoji ni kwanini serikali ilishindwa kutambua umuhimu wa maeneo hayo kwani kuna wananchi wengine kutoka wilaya wanapoumwa wanakuja kupata matibabu lituhi kupitia kivuko cha pantoni iliyoko mto ruhuhu .
Naye Gaitani Ngatunga mkazi wa kijiji cha kipingu wilayani Rudewa ameeleza kuwa wananchi wa vijiji vya ngerere,ilela isungu na mbongo walikuwa wakitegemea kwa kiasi kikubwa kwenda wilayani nyasa kupata huduma ya matibabu pale wanapoumwa hasa ikizingatiwa maeneo ya kandokando ya ziwa nyasa wanasumbuliwa sana na homa ya Malaria .
Ngatunga amemwomba mbunge wa jimbo la Rudewa Deo Filikunjombe na Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi Kapteni John Komba kuchukua hatua za haraka za kuishawishi Wizara ya ujenzi kurudisha injini hiyo
Mbunge wa jimbo magharibi keptani mstaafu komba ameiambia nipashe  kuwa ofisi yake imepokea malalamiko kwamba TEMESA Ruvuma wamengoa injini 1 iliyopo mto ruhuhu na kuipeleka Ifakara kilombelo ambako kuna pantoni inayowasaidia wananchi kama pantoni inavyowasaidia wilaya ya nyasa na Ludewa jambo ambalo limeñaza kuleta hofu kunbe wananchi wa jimbo lake pamoja na wananchi wa Ludewa sio wananchi wa Tanzania.
Akizungumzia hilo Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi Kapteni John Komba alisema ameshangwazwa sana na kitendo cha TEMESA Ruvuma cha kuondoa injini 1 kwenye pantoni iliyokuwa inawasaidia wapiga kura wangu kwenda Rudewa kwa shughuri zao kwa kufika Lituhi kwa kutumia pantoni iliyopo mto Ruhuhu kuja kupata mahitaji yao na wengine kuja kupata matibabu ya afya katika kituo cha Lituhi
Ameeleza zaidi kuwa kero hiyo ya kuondolewa injini kwenye pantoni mto Ruhuhu iliyokuwa ikiwasaidi wapiga kura wake anatarajia kuifikisha kwenye kikao cha Bunge mjini Dodoma kinachotarajia kufanyika mapema januari mwaka ujao, kwani kitendo cha TEMESA kuamisha injini kwenye pantoni mto Ruhuhu na kuipeleka kwenye pantoni nyingine iliyopo Ifakara Kilombelo ni usaliti mkubwa na imeonekana kuwa na lengo baya  kwa wananchi wa mwambao mwa Ziwa Nyasa
Akizungumza na mtandao wa www.stephanomango.blogspot.com ofisini kwake Meneja wa wakala wa ufundi na umeme Mkoa Ruvuma (TEMESA)  Mhandisi Afred Ngwani amesema kuwa agizo la kuiondoa injini hiyo kwenye pantoni iliyoko mto Ruhuhu lilikuwa limetoka kwa Katibu mkuu wa wizara ya ujenzi Bw. Mlango ambaye alimwagiza aiondoe haraka iwezekanavyo baada ya kuona pantoni iliyoko mto Ruhuhu imesimama kutokana na kina cha maji kupungua na kujaa mchanga .
Mhandisi Ngwani amesema sababu kubwa ya kuhamisha injini hiyo kwenye  kivuko cha mto Ruhuhu kwenda kwenye pantoni ya kivuko cha Ifakara kilombelo kiliharibika na kushindwa kuvuka mto huo ambacho kinadaiwa kuwa kina umuhimu mkubwa huko kwani kinawavusha watu zaidi ya 1000 kwa kila siku na Magari kati ya 200 hadi 400 kwa siku tofauti na kivuko cha mto Ruhuhu ambacho kilikuwa kinawavusha watu wachache na Magari kati ya 4 hadi 6 kwa wiki.
Mwisho.

Sunday, December 18, 2011

GARI DOGO LAPATA AJARI ENEO LA KWA SWAI MAHENGE KATA YA MJINI MANISPAA YA SONGEA

 Gari likiwa mtaroni baada ya kuanguka kutokana na kugongana na pikipiki jana jioni ambapo dereva wa pikipiki ameumia vibaya sana

Mashuhuda wa ajari hiyo wakiendelea kusikitika eneo la tukio

Saturday, December 17, 2011

SIMBA AMRARUA MAKALIO MFUGAJI WA KIMANG'ATI BAADA YA KUINGIA KWENYE ZIZI LA NG'OMBE

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda
Na Gideon Mwakanosya,Songea
LUKAS Bajuta (35)mkazi wa Kijiji cha Milonji kilichopo katika kata ya Lusewa Wilayani Namtumbo mkoa wa Ruvuma amenusurika kufa baada ya kujeruhiwi na Simba kwa kung’atwa sehemu ya makalio upande wa kulia wakati akijaribu kuwaokoa ng’ombe wake waliokuwa kwenye zizi waliotaka kuliwa na samba huyo
Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda alisema kuwa tukio hilo lilitokea Disemba 12 mwaka huu majira ya saa 10:30 jioni huko katika kijiji cha Milonji
Kamuhanda alisema kuwa inadaiwa siku ya tukio Bajuta mwenye asili ya kabila la Mang’ati akiwa nyumbani kwake ghafla alimuona simba akiwa katikakati ya ng’ombe wake waliokuwa kwenye zizi ambalo liko jilani na nyumba anayoishi
Alisema kuwa Bajuta baada ya kumuona simba huyo alichukua mkuki na kuelekea kwenye eneo la ziziz la ng’ombe wake ambako alipofika jilani inadaiwa samba alimuona kisha aliruka toka ndani ya zizi hadi nje alikosimama Bajuta
Alifafanua kuwa Bajuta baada ya kuona hivyo aliamua kulala chini ambapo samba akaja kumlalia kwa juu na kuanza kumkata sehemu ya upande wa kulia wa makalio yake na kumsababishia maumivu makali ambayo yalimfanya apoteze fahamu
Alieleza zaidi kuwa wakati Bajuta anavamiwa na simba watu waliokuwa jilani na eneo hilo wakiwemo na watu wa kabila lake la wamang’ati walifika eneo hilo na kuanza kumshambulia samba huyo kwa kumpiga na mikuki ambapo baadaye samba huyo alikimbia na kutokomea kusiko julikana
Alibainisha zaidi kuwa baada ya samba huyo kuondoka kwenye eneo la tukio wanakijiji wenzake walimchukua Bajuta na kumpeleka kwenye Kituo cha Afya cha Lusewa kwa matibabu ambako kwa sasa hivi amelazwa na hali yake inaendelea vizuri
MWISHO

Thursday, December 15, 2011

MATOKEO YA DARASA LA SABA MWAKA 2011 YATANGAZWA KWA MASIKITIKO MAKUBWA MKOANI RUVUMA

 Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Dkt Anselm Talimo akitangaza matokeo ya darasa la Saba mwaka 2011
Afisa Elimu wa Mkoa wa Ruvuma Paulina Mkonongo
Na Mwandishi Wetu,Songea
SERIKALI Mkoani Ruvuma imetangaza matokeo ya Mtihani wa kumaliza elimu ya Msingi mwaka 2011 ambapo wanafunzi 16,941 wamechaguliwa kuendelea na masomo kidato cha kwanza mwaka wa 2012 kati ya wanafunzi 36,718 waliofanya mtihani  mwaka huu.
Aidha walimu wakuu wa shule za msingi 7  zilizopo katika Wilaya za Mbinga na Tunduru wamevuliwa madaraka na walimu waliosimamia mtihani ya kumaliza elimu ya msingi katika shule hizo 7 wameondolewa dhamana ya kusimamia sensa ya Taifa na mitihani baada ya  baraza la mitihani la Taifa kubaini kuwa kulikuwa na udanganyifu wakati wa kufanya mtihani.
Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake Kaimu katibu tawala wa Mkoa wa Ruvuma Dr. Anselem Talimo amesema kuwa mkoa huo ulikuwa na watahiniwa wa mtihani wa kumaliza elimu ya msingi waliofanya mtihani walikuwa 36,718 kati yao wavulana walikuwa 17,772 na wasichana walikuwa 18,946 hivyo watahiniwa waliofanya mtihani ni sawa 97.2% ya wanafunzi 37,778 walio sajiliwa kufanya mtihani mwaka huu.
Dr. Talimo ameeleza kuwa idadi ya watahiniwa ni sawa na 85.0% ya wanafunzi 43,149 walioandikishwa darasa la kwanza mwaka 2005 ambapo asilimia hiyo ya waliofanya mtihani inaonesha wazi kuwa baadhi ya wanafunzi walikuwa watoro, walio acha shule na ujauzito.
Dr. Talimo amewahimiza walimu wakuu wa shule za msingi Mkoani Ruvuma kusimamia maudhulio ya wanafunzi shuleni kila siku ili kuongeza asilimia za wanao hitimu elimu ya msingi kama yalivyo malengo ya milenia kwa wote.
Kaimu katibu tawala wa Mkoa Ruvuma Dr. Talimo akitangaza matokeo hayo amefafanua kuwa watahiniwa waliofaulu mtihani  wa kumaliza elimu ya msingi mkoani humo mwaka huu ni 16,941 kati yao wasichana ni 8606 wa wavulana 8335 sawa asilimia 46.1 ya watahiniwa 36,718 waliofanya mtihani mwaka huu Mkoani Ruvuma.
Ameeleza zaidi kuwa kwa ujumla ufaulu huo ni wa chini sana kwa kuwa haujafikia asilimia 50 pia ni pungufu kwa asilimia 1.78 ikilinganishwa na mwaka 2009 ambapo matokeo hayo ni ya wastani ni matokeo ya kiwilaya alihalisi inaonyesha kuwa Halmashauri za wilaya ya Mbinga, Namtumbo na Tunduru zimeshuka ufaulu ikilinganishwa na mwaka 2010.
Amebainisha zaidi kuwa Halimashauri ya wilaya ya Mbinga inaufaulu wa asilimia 40.2 ambayo ni chini kwa asilimia 0.82 ikilinganishwa na ufaulu wa asilimia 41.02 wa mwaka 2010, Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo inaufaulu wa asilimia 50 ikilinganishwa na asilimia 53.89 ya mwaka 2010 ambayo ni pungufu kwa 3.89 na Halmashauri ya wilaya ya Tunduru inaufaulu wa asilimia 41.2 ambayo ni upunguvufu wa asilimia 10.56 ikilinganishwa na asilimia 51.86 ya mwaka 2010.
Ameongeza kuwa Halmashauli ya wilaya ya Songea vijijini inaufaulu wa asilimia 47 ambayo ni nyongeza kwa asilimia 7.58 ikilinganishwa na asilimia 39.42 ya mwaka 2010 hivyo Halmashauli hiyo ufaulu umepanda kidogo kuliko ufaulu wa matokeo ya mwaka jana na kwamba bado ufaulu huo uko chini ya asilimia 50 na Halmashauli ya Manispaa Songea inaufaulu wa asilimia 67.2 ambayo ni nyongeza kwa asilimia 2.46 ikilinganishwa na ufaulu wa 64.54 ya mwaka jana hivyo amewapongeza walimu wa shule za msingi na Maafisa Elimu wa Manispaa hiyo kwa kuwa na ufaulu wa asilimia zaidi ya 50 na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi hata hivyo walimu pamoja na Maafisa Elimu wa  Manispaa hivyo wanapaswa kujiwekea malengo zaidi na kusimamia malengo ikiwa pamoja na viongozi na waalimu wa shule za msingi mkoani humo kujipanga upya hali ya kushuka na kupanda matokeo ya mtihani ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara.
Aidha kaimu katibu tawala wa Mkoa wa Ruvuma Dr. Talimo ameeleza kuwa wanafunzi 163 wa shule za msingi 7 Mkoani Ruvuma wamefutiwa mtihani yao kufuatia kuwepo kwa udanganyifu ambao inadaiwa kuwa kati yao walikutwa na majibu ya mitihani wakiwa kwenye vyumba vya mithani na wengine walikuwa na mawasiliano na wasimamizi wa mithani hiyo.
Dr. Talimo ametaja shule ambazo walimu wakuu wameng’olewa madaraka kutokana na udanganyifu uliofanwywa na mtihani wa kumaliza elimu ya msingi katika wilaya ya Tunduru ni shule ya msingi Namapungwa ambako wanafunzi 59 wamefutiwa mtihani , shule ya msingi Mchekeni watahiniwa 23 kati ya 35 waliofanya mtihani wamefutiwa mtihani, shule ya msingi mchemba wanafunzi 2 wamefutiwa mtihani kati ya wanafunzi 30 waliofanya  mtihani na katika wilaya ya mbinga kwenye shule ya msingi ya mnazi mmoja baraza la mtihani Tanzania limefuta matokeo ya watahiniwa 18 kati ya watahiniwa 46.
Dr. Talimo amezitaja shule zingine wameondolewa madaraka kuwa ni shule ya msingi Rulala watahiniwa 10 wamefutiwa mtihani kati ya wahitimu 18 na wanafunzi 43 waliofanya mtihani kati ya watahiniwa 63 wamefutiwa mtihani .
Mwisho

Wednesday, December 14, 2011

JAY BLACK MSANII CHIPUKIZI ANAYEIBUKIA KWA KASI KWENYE MUZIKI WA BONGO FREVA

 Msanii wa muziki wa kizazi kipya James Damian Jay Black

JINA lake ni James Damian maarufu kwa jina la Jay black ni mwanamuziki wa muziki wa bongo fleva , alianza rasmi kujishughulisha na kazi hii mwaka 2006 ingawa hakufanikiwa kurekodi kama anavyoendelea kuongea na Mtandao wa www.stephanomango.blogspot.com
Msanii huyo James Damian anafafanua kuwa Mnamo mwaka 2008 alibahatika kuingia studio na kurekodi nyimbo iliyofahamika kwa jina la MAISHA kwenye Albam ambayo ilikuwa na nyimbo nne ambazo ni Mashamsham, na Maisha japo hazikubahatika kuvuma, na mnamo mwaka 2009 alikutana na Mr. T muandaaaji wa muziki studio ya Gita music  iliyopo songea mjini na kufanikiwa kurekodi nyimbo iliyokwenda kwa jina la WANGU DUU.

Amesema kuwa  2011 alifanikiwa kuitolea video nyimbo hiyo katika studio za Fm Production chini ya muandaaji Geofrey Mhagama wa Songea Mjini  na hapo ndipo mafanikio yalipoanza kuonekana kwani nyimbo imebahatika kuchezwa katika vituo tofauti tofauti vya redio na televisheni za hapa nchini.
Amebainisha zaidi kuwa hivi karibuni mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu anatarajia kuachia audio na video itakayofahamika kwa jina la ATUPELE BINTI MWAFRIKA iliyoandaliwa na Prodyuza Mr. T wa studio ya Gita records na baada ya hiyo itafuatiwa na nyimbo itakayoenda kwa jina la MAPENZI NA SHULE  ambayo hiyo nyimbo imejaribu kuongelea hali halisi inayowakuta wanafunzi na wanazuoni wanao ingia katika mapenzi wakiwa masomoni.
Amesema kuwa Shoo yake kubwa aliyowahi kuifanya na kuwavutia Wapenzi wengi wa Muziki wa Kizazi kipya  ni Miss Mbinga ilifanyika kwenye ukumbi wa Umoja wa Vijana (UVIKAMBI) uliopo Mbinga Mjini na Miss Ruvuma 2011 iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Songea Parokia ya Bombambili Mjini Songea.
Msanii huyo James Damian anaeleza kuwa  amejitokeza kwenye safu hii kuomba support kwa wadau mbalimbali hapa nchini waweze kumsaidia hasa kimawazo ili aweze kutoka hapa alipo hadi hatua nyingine ya kimuziki.
Amesema kuwa Elimu yake ya sekondari amemaliza mwaka 2007 katika shule ya sekondari ya St. Agrey Mbeya na mwaka 2009 alijiunga na chuo cha Maendeleo ya jamii kilichopo Mlale Wilaya ya Songea na amehitimu Elimu ngazi ya Cheti Mwaka huu kwa sasa yupo mtaani akiangalia upande wa pili wa maisha unaendaje kwani msaada wake mkubwa katika maisha yake ni mama yake mzazi Suzan Fussy ndio tegemeo lake ambaye Kabila lake ni Mndendeule Mzaliwa wa Kijiji cha Hanga Kilichopo Wilayani Namtumbo na baba yake Mzazi ni Damian whiter Mashale mzaliwa wa Rombo Mkoani Kilimanjaro ambapo amedai kuwa yeye mwenyewe James Damian alizaliwa Octoba 3.1988 katika Hospitali ya Serikali ya Mkoa wa Songea na ni mtoto wa Mwisho kati ya watoto watatu wa  familia yao .
Msanii huyo wa Kizazi kipya anamaliza kusema kuwa anapenda kuwaeleza Watanzania kuwa amani na upendo ndio nguzo imara katika maisha na usije ukamdharau mtu yeyote kwani hujui wapi mtakutana na usijeukamtendea ubaya mwenzako kwani tangu Dunia hii iumbwe na mwenyezi Mungu Milima iliyopo kwenye Dunia hii haijawahi kukutana lakini Binadamu wanaweza wakapotezana kwa muda mrefu lakini baadaye wanaweza wakakutana.
Kwa Wadau watakaoonyesha nia ya kutaka kumsaidia msanii huyo Mchanga wa Muziki wa Kizazi kipya aliyepo Mjini Songea kwa Mawasiliano simu na. 0657784199 email. jayblack4real@gmail.com .

Monday, December 12, 2011

MTAMBO WA KUFULIA UMEME JUA POSTA YA MBINGA WATOKOMEA KUSIKOJULIKANA

Na Gideon Mwakanosya, Songea

MTAMBO wa kufulia umeme jua (Sola) uliokuwa umefungwa kwenye Ofisi ya Shirika la Posta Tanzania ya Wilayani Mbinga wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni nne Mkoa wa Ruvuma inahofiwa kuwa umeondolewa katika mazingira tatanishi kwa madai kuwa kigogo mmoja mwandamizi wa Shirika hilo ameuhitaji kwa matumizi yake binafsi.

Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Posta Mkoani Ruvuma ambao wameomba majina yao yahifadhiwe wameuambia mtandao wa www.stephanomango.blogspot.com kuwa Mtambo huo wa kufulia umeme jua ulikuwa umefungwa kwenye Ofisi za Shirika hilo iliyopo Mbinga Mjini ambao ulikuwa ukisaidia kwa kiasi kikubwa shughuli mbalimbali ofisini hapo zikiwemo za mawasiliano pamoja na matumizi mengine ya kazi za kila siku ofisini hapo.

Wamesema kuwa jambo la kushangaza ni kuwa Meneja wa Shirika hilo la Posta Mkoani Ruvuma Rochus Asenga  mwezi machi mwaka huu alikwenda Mbinga na kuung’oa mtambo huo ambao ulikuwa umefungwa kwenye ofisi za Posta Mbinga na kudai kuwa kwa vile Mbinga kuna Shirika la umeme Tanzania Tanesco mtambo huo unatarajiwa kuondolewa Mbinga na Kupelekwa Jijini Dar es Salaam ambako kuna kiongozi mmoja anauhitaji.

Wameeleza zaidi kuwa Mtambo huo wa kufulia umeme jua inadaiwa kuwa uliondolewa Mbinga bila kuwepo na maandishi ya aina yeyote na badala yake Asenga alieleza kwa mdomo kuwa Sola hiyo inahitajika mahali pengine Jijini Dar es Salaam kwa bosi wake.

Akizungumza na www.stephanomango.blogspot.com Meneja wa Shirika hilo Mkoani Ruvuma Rochus Asenga kuhusiana na kuuhamisha mtambo wa kufulia umeme (Sola) katika mazingira tatanishi alisema kuwa yeye siyo msemaji wa Shirika la Posta Tanzania ila alikiri kuwa Mbinga kulikuwa na mtambo wa umeme jua (Sola) ambao  uliondolewa lakini kwasasa hawezi kusema lolote kwa vile yeye siyo msemaji wa Shirika hilo.

Naye Afisa Mwandamizi wa Shirika la Posta Tanzania Wilayani Mbinga  Mbutolwe Mwakitalima alipohojiwa na mtandao huu kwa njia ya simu kuhusiana na mtambo wa umeme jua uliokuwa umefungwa kwenye Ofisi yake kwaajili ya matumizi mbalimbali ambao unadaiwa kuondolewa katika Mazingira tatanishi na kupelekwa kusikojulikana alisema kuwa ni kweli Meneja wake wa Mkoa Asenga mwezi machi mwaka huu majira ya saa za kazi alifika Ofisini kwake na kudai kuwa mtambo huo anauondoa na kuupeleka Makao makuu ya Shirika hilo Mkoani Ruvuma ambako baadae wataangalia ni wapi wataupeleka ukaendelee kutumika.

Mwakitalima alifafanua kuwa kwasasa hivi hawezi kufahamu mtambo huo wa kufulia umeme upo wapi wala hana sababu yeyote ya msingi kuulizia kwa vile Bosi wake aliuchukua na Wafanyakazi wengine wa Shirika hilo wakiwepo ila aliuchukua bila kuandikiana.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania Kanda ya Mbeya inayohusisha Mikoa ya Rukwa,Mbeya,Iringa na Ruvuma ambaye alijitambulisha kwa jina moja la  Mlay aliuambia mtandao huu kwa njia ya simu kuwa Wafanyakazi wa Posta Songea kwa muda mrefu wamekuwa na malalamiko mengi kati yao na Menejimenti lakini suala la upotevu wa Sola iliyokuwa ikitumika Posta Mbinga Ofisi yake ilikuwa bado haijapata taarifa hizo lakini ameeleza kuwa atawasiliana na Menejimenti ya Mkoa huo ili afahamu zaidi juu ya taarifa ya Sola iliyokuwa imefungwa Mbinga kuwa imepelekwa wapi.

Hata hivyo www.stephanomango.blogspot.com  iliwasiliana na Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Deus Mndeme na kumtaka atoe ufafanuzi juu ya Mtambo wa kufulia umeme jua uliokuwa umefungwa kwenye Ofisi ya Mbinga alieleza kuwa yeye mpaka sasa hafahamu lolote isipokuwa anachojua kuwa kwenye Ofisi ya Posta hakuna Sola iliyokuwa imenunuliwa na Shirika na kwamba amekanusha vikali uvumi unaodai kuwa mtambo huo umechukuliwa na baadhi ya vigogo Jijini Dare s  Salaam kwa matumizi yao binafsi.

Mndeme amefafanua kuwa Shirika la Posta lina utaratibu maalumu ambao unafahamika kwa kila Mfanyakazi kuwa anapohamisha mali ya Shirika kutoka Ofisi fulani kwenda Ofisi nyingine ni lazima kuna taratibu zinazotakiwa kufanywa kwa kujaza fomu maalumu ambazo zinaonyesha mali hiyo inahamishwa na mahali inakopelekwa lakini kama utaratibu huo haukufuatwa basi hapo kuna utata.

Amesema kuwa kwa vile Shirika la Posta lina kitengo cha usalama hivyo suala hilo ataliwakilisha kwa Mkuu wa Idara ya usalama ili nao waweze  kulifanyia  kazi na kuweza kubaini mtambo huo wa umeme umehamishwa Mbinga na umepelekwa wapi au ni nani anayeutumia kwa hivi sasa na kwamba kama kweli kuna kigogo mmoja ameamua kuuchukua basi hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

MWISHO.

Sunday, December 11, 2011

WAKATI WA UCHAGUZI MKUU WA URAIS,WABUNGE NA MADIWANI MWAKA 2010,MGOMBEA MMOJA WA CHAMA FULANI ALIZUNGUKA NCHI NZIMA NA KUWAAHIDI WATANZANIA KUWANUNULIA BAJAJ ZITAKAZOSAMBAZWA NCHI NZIMA VIJIJINI KWA AJIRI YA KUWABEBA AKINA MAMA WAJAWAZITO ILI KUPUNGUZA VIFO VINATOVYOTOKANA NA UZAZI,JE BAJAJ HIZI NDIZO ZILIZOAHIDIWA AU TUSUBIRI ZINGINE?



WATANZANIA WATAKIWA KUTUMIA BIDHAA ZINAZOTENGENEZWA NA WAHITIMU WA VETA NCHINI

Mkurugenzi wa VETA Kanda ya  Nyanda za juu kusini Monica Mbelle

Na Gideon Mwakanosya,Songea

WATANZANIA wametakiwa kutumia bidhaa za ndani zinazotokana na malighafi za hapa nchini badala ya kuendelea  kutumia bidhaa za China ambazo  asilimia kubwa ubora wake ni mdogo na zimekuwa zikahiribika baada ya muda mfupi na kuiletea hasara Serikali.
 
Ushauri huo ulitolewa mwishoni mwa wiki na  Mkurugenzi wa VETA Kanda ya  Nyanda za juu kusini Monica Mbelle wakati akizungumza kwenye Mahafali ya 26 ya Chuo cha Ufundi stadi Songea Mkoani Ruvuma .
 
Alisema kuwa katika miaka ya hivi karibuni Taifa limeshuhudia bidhaa nyingi zenye ubora mdogo zikitoka nje ya Nchi ukilinganisha na za hapa Nchini ambazo zimekuwa na ubora mkubwa lakini zimekuwa zikikosa soko kutokana na dhana potofu iliyojengeka miongoni mwa jamii na Serikali kwamba bidhaa bora ni zile zinazotoka ng’ambo.
 
‘Tumeshuhudia Ofisi zetu zikiwa zimejaa fenicha za kutoka nje ya Nchi ambazo baada ya mwaka mmoja zinakuwa zimeharibika na Serikali inaingia gharama nyingine kuagiza tena bidhaa hizo wakati tuna mafundi wetu wanaotengeneza bidhaa bora kuliko hizo’alisema na kuongeza kuwa
 
Inatakiwa jamii na Serikali kubadilika na kuwatumia mafundi waliohitimu VETA kwa kuwaunga mkono kwa kununua bidhaa zao zenye ubora wa hali ya juu tofauti na bidhaa za nje ambazo alidai zina ubora mdogo.
 
Alisema kwa sasa wanawatumia mafundi wao badala ya Wakandarasi kujenga Vyuo kila Wilaya ambapo wamekiteua Chuo cha Ufundi stadi Mpanda kufanya kazi hizo kwa Nyanda za juu kusini na kwa sasa wanajenga Chuo cha VETA Makete na baada ya kumaliza huko watakuja kujenga  madarasa Veta Songea baada ya wanafunzi kuwa wengi.
 
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi Songea  Gideon Ole Lairumbe alisema wamekuwa wakikabiliana na changamoto mbalimbali katika Chuo hicho zikiwemo wazazi kuleta wanafunzi wa darasa la saba wenye uwezo mdogo wa kuelewa masomo na ukosefu wa vitendea kazi.
 
Hata hivyo aliishukuru Mamlaka ya Mawasiliano Nchini(TCRA) kuwapa msaada wa Kompyuta nane zenye thamani ya Tsh milioni 3.5 ambazo zilikabidhiwa siku hiyo na  Afisa wa Mamlaka hiyo Deograsias Nyoni ili ziweze kusaidia kwenye mafunzo ya Kompyuta Chuoni hapo ambapo alisema kuwa elimu ya Kompyuta na mawasiliano ni muhimu katika dunia ya leo.
MWISHO