Afisa Kazi Mkoa wa Ruvuma Oddo Egino Hekela akizungumzia mapitio ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2005 wakati wa mdahalo
Hakimu Mkazi Elizabeth Misano akizungumza wakati wa mdahalo
Mwenyekiti wa Mtandao wa Sonngo Siwajibu Gama akifafanua hoja mbalimbali katika mdahalo
Washiriki wa mdahalo huo wakiendelea kusikiliza hoja mbalimbali katika mdahalo huo uliofanyika jana kwenye ukumbi wa mikutano wa kanisa la Bombambili
Thursday, December 29, 2011
MDAHALO WA WAZI KUHUSU UCHAMBUZI NA MAPITIO YA KATIBA YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977
MWANDAAJI: SONGEA NETWORK OF NON – GOVERNMENTAL ORGANIZATIONS (SONNGO)
MADA: MAPITIO YA KATIBA YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977 ILIYOFANYIWA MAREKEBISHO 2005
MTOA MADA: ODDO EGINO HEKELA
AFISA KAZI RUVUMA , NA MKURUGENZI WA KAMPUNI YA KAZI BUREAU SERVICES CO.LTD
P.O. BOX 1050, SONGEA
TEL: 0784 332 378/ 0655 332 378/0755 094 862
E- MAIL: odo.egino@yahoo.com
MADA: MAPITIO YA KATIBA YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977 KAMA ILIVYOFANYIWA MAREKEBISHO 2005.
1.0 UTANGULIZI
1.0 MAANA YA KATIBA
Katiba ni sheria mama ya nchi inayotoa au kuweka Utawala na eneo la utawala, madaraka ya viongozi na mgawanyo wa majukumu katika miimili yote mitatu ya Serikali yaani Bunge, Mahakama na watendaji wa Serikali (Parliament, Judiciary and Executives).
2.0 KATIBA YA KUDUMU (1977) KAMA ILIVYOFANYIWA MAREKEBISHO 2005.
Katiba hii ilipatikana kupitia tume ya Rais yenye wajumbe 20 yaani 10 kutoka Bara na 10 kutoka Visiwani (Zanzibar ). Katiba hii iliitwa Katiba ya kudumu. Kabla ya kuandaliwa Katiba hii tume hii ilianza kuandika Katiba ya CCM baada ya kuunganisha vyanma vya TANU na ASP tarehe 5/2/1977. Katiba iliweka misingi mikuu ya madaraka na majukumu
i. Mfumo wa chama kimoja
ii. Uraisi wenye nguvu zaidi na
iii. Mfumo wa Serikali mbili.
Katiba ya kudumu ilipitishwa na Rais na baadae aliteua Bunge la kawaida kujigeuza kuwa Bunge la Katiba na kupitisha Katiba ndani ya masaa matatu tu. Katiba hii imefanyiwa marekebisho mengi kufuatia mahitaji ya Taifa kwa nyakati mbalimbali hadi 2005. Mabadiliko makubwa ni yale ya kuruhusu tena uwepo wa vyama vingi na uanzishwaji wa tume ya uchaguzi ya Taifa (NEC), ongezeko la viti maalum na uwiano wao (2005).
3.0 SERIKALI YA WATU
Katika sehemu ya pili ya Katiba, Ibara ya 8 (1) ya Katiba ya mwaka 1977, na marekebisho ya 2005, inasema;
· Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii. Wananchi ndio msingi wa mamlaka yote.
· Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi.
· Lengo kuu la Serikali ni ustawi wa wananchi.
· Serikali itawajibika kwa wananchi.
· Wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao .
Sheria iliyoundwa kutoa maelekezo ni sheria ya Serikali na watu ya 1984 na. 15.
Swali ni je?
Uwanja wa demokrasia umepanuliwa na kuwapa wananchi madaraka ya kuweka Serikali kama wapendavyo? Na nini kifanyike?
3.1 UJENZI WA UJAMAA NA KUJITEGEMEA
Ibara ya 9 ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania 2005 inatoa msingi huu kwa kutamka uelekeo wa nchi ni wa ujamaa na kujitegemea. Kwa hiyo sera na shughuli zote za Serikali zielekeze nguvu katika ujenzi huo.
Mambo yaliyowekewa mkazo na Katiba hii ni:
· Utu na haki za binadamu.
· Utawala wa sheria.
· Utajiri wa Taifa unakuwa kwa manufaa ya umma.
· Ulinganifu na ushirikishwaji wa wananchi katika maendeleo ya nchi.
· Kazi kama shughuli halali.
· Heshima ya binadamu inahifadhiwa.
· Hakuna ubaguzi wa rangi, jinsi, kabila, dini wala hali ya mtu.
· Dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa, uonevu na upendeleo zinaondolewa nchini.
· Utajiri wa Taifa unanufaisha umma.
· Hakuna ulimbikizaji wa mali .
· Demokrasia inatawala zaidi.
Swali ni je?
1. Tunauhitaji wa kuendelea na msingi wa ujamaa na kujitegemea? Kama ndio kwa uelekeo gani?
2. mali asili ya nchi imewekewa misingi ya umiliki kwa faida ya umma?
4.0 SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO
Ibara ya 34 (1) inasema kutakuwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ambayo itakuwa na mamlaka ya mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya muungano, na pia juu ya mambo mengine yote yahusuyo Tanzania Bara.
Swali ni je?
Hakuna uwezekano wa kuwa na Serikali tatu yaani Tanganyika , Zanzibari na Muungano?
4.1 MADARAKA YA RAIS
Ibara ya 33 (2) ya Katiba 1977 na marekebisho ya 2005, inasema Rais atakuwa Mkuu wa Nchi, kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu. Rais anapewa madaraka yafuatayo na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania .
Upana wa Madaraka ya Rais
· Mamlaka ya kuanzisha na kufuta nafasi za madaraka ya namna mbalimbali katika utumishi wa umma. Ibara ya 36(1) ya katiba 1977,iliyorekebishwa 2005
· Kuwateua watu kushika nafasi za madaraka. Ibara ya 36 (2) ya Katiba 1977, iliyorekebishwa 2005.
· Madaraka ya kuwapandisha vyeo au kuwafukuza kazi Ibara 26 (3) ya Katiba 1977, 2005.
· Kudhibiti nidhamu katika watumishi wa Serikali Ibara ya 36 (4) 2005.
· Hatalazimika kufuata ushauri atakaopewa na mtu yeyote , isipokuwa tu pale anapotakiwa na Katiba hii au sheria nyingine Ibara ya 37 (1) ya Katiba 2005.
· Madaraka ya kutangaza vita, Ibara ya 44 (1) ya Katiba 2005, inatoa madaraka kwa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania .
· Uwezo wa kutoa msamaha kwa mtu yeyote aliyepatikana na hatia mbele za mahakama kwa kosa lolote bila ya masharti au kwa masharti Ibara ya 45 (1) (a) (b) 2005.
· Kuibadilisha adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa kosa lolote iwe adhabu tahalifu Ibara ya 45 (1) (c), 2005.
· Kufuta adhabu yoyote au sehemu ya adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa ajili ya kosa lolote au kuhozi (kuchukua) kitu cha mtu mwenye hatia ambacho vinginevyo kingechukuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano Ibara ya 45 (d) ya Katiba 2005.
Swali ni je?
Akitoa upendeleo wowote nani atakuwa na jukumu la kuuliza au kupinga katika madaraka makubwa kiasi hicho?
4.2 UTEUZI WA MAWAZIRI
Katiba inampa madaraka hayo Rais ya kuteua mawaziri wake wa kusaidia Serikali yake. Ibara ya 55 (1) ya Katiba 1977, iliyorekebishwa ,2005.
Ibara ya 55(4) ya katiba 1977, iliyorekebishwa 2005 inasema; Mawaziri na manaibu mawaziri wote Katiba inataka watokane na Wabunge waliounda Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
Swali ni je?
Hakuna uwezekano wa kupata mawaziri wasio wabunge kwa mujibu wa Katiba?
4.0 MADARAKA YA BUNGE
i. Bunge letu linaundwa na sehemu mbili yaani Rais na Wabunge. Kwa mujibu wa Ibara ya 62 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano 2005. Kwa hiyo Bunge letu linapoteza uwezo wa kujitegemea ukilinganisha na Bunge la Uingereza na Marekani kwa kuwa shughuli zake zinawezeshwa na Rais wa Nchi. Na maamuzi yake yanachujwa na Rais wa Nchi kwa mujibu wa Ibara ya 63 (1) Rais kama sehemu moja ya Bunge atatekeleza madaraka yote aliyokabidhiwa na Katiba hii kwa ajili hiyo.
Bunge letu lina uwezo wa kupendekeza kwa Rais kuhusu kumuondoa mtu au kumweka mtu madarakani kutokana na utovu wa nidhamu au wizi uliotendeka katika kusimamia Serikali lakini siyo kumuondoa, au madaraka ya kumwondoa mtu kama huyo yapo kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Swali ni je?
Kwa kufanya hivyo hatuoni kwamba Bunge linapunguziwa uwezo kwa mujibu wa Ibara ya 63 (2) ya Katiba 1977, iliyorekebishwa, 2005?
ii. Madaraka ya kutunga sheria katika Ibara ya 63 (3) (d) ya Katiba ya 2005, Bunge linapewa uwezo wa kutunga sheria ili ifanye kazi inahitaji mkono wa Rais na ridhaa yake. Baada ya Bunge kutunga sheria haiwezi kufanya kazi kama rais hajasaini na kuifanya kuwa sheria katika nchi.
Swali ni je?
iii. Madaraka ya Bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania dhidi ya Serikali ya Zanzabar ni madogo sana Ibara ya 64 (3) (4) ya 2005. Baraza la wawakilishi la Zanzibar ndilo lenye madaraka makubwa na maswala ya Zanzibar .
Swali ni je?
Baraza la wawakilishi katika serkali ya mapinduzi la Zanzibar haliwezikukinzana katika maamuzi na Bunge la muungano?
5.0 SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBARI
Katika sura ya nne ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, iliyorekebishwa ,2005 Ibara ya 102 (1) inataja kuwa kutakuwa na serikali ya Zanzibar itakayojulikana kama Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari na ambayo itakuwa na madaraka na mambo yasiyo ya Muungano kwa mujibu wa masharti ya Katiba yenyewe.
Swali ni je?
Kwa nini katika Katiba hakuna madaraka ya Serikali ya Tanganyika ? Je kuna umuhimu wa kuanzisha Serikali hiyo?
Swali lingine ni je? Ni muhimu kuwa na Serikali za Majimbo ili kupunguza uwezekano wa kuwa na Serikali nyingine ya tatu yaani Tanganyika ?
6.0 UHURU WA MAHAKAMA
Sura ya tano ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, iliyorekebishwa, 2005 Ibara ya 107 (1) ya Katiba ya 1977, 2005 inaunda mamlaka ya kauli ya mwisho ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano kuwa ni Mahakama.
Ibara ya 107 (B) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inatamka kuwa Mahakama itakuwa huru katika utekelezaji wa shughuli zake kwa mujibu wa sheria na katiba za nchi. Ambapo mwaka 2002 iliundwa sheria ya Uhuru wa Mahakama sheria namba 3 ya mwaka 2002.
Swali ni je?
Kweli Mahakama zetu zipo huru mbali na madaraka ya Rais wa nchi katika kutekeleza majukumu yake?
i. Nani anamchagua Jaji Mkuu na Jaji Kiongozi?
ii. Nani anachagua Majaji wa Mahakama Kuu?
iii. Je anayewachagua anaweza kuwa chini ya maamuzi au hizo posti ziwe za ushindani kama walivyofanya Kenya ? Ibara ya 118 ya Katiba 1977, iliyorekebishwa, 2005.
7.0 HAKI ZA BINADAMU
i. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 14 – 24 ya katiba ya 1977, iliyorekebishwa mwaka 2005, inatoa haki za raia wa Tanzania . Miongoni mwa ya haki hizo ni haki ya kuishi .
Swali ni je?
wakati Mahakama imepewa uwezo wa kutoa adhabu ya kifo. Katiba inatoa haki ya kuishi je? Kunauwezekano wa kufuta adhabu ya kifo?
ii. Katiba imetoa haki ya kumiliki mali kwa raia wa Tanzania lakini kuna baadhi ya mali huwezi kumiliki kama madini, mafuta na vito vya thamani kwa mujibu wa sheria ya Ardhi na madini. Hivyo wakati upande mmoja unatoa upande mwingine unanyang’anya.
Swali ni je?
Ardhi na madini yaliyomilikiwa kiasili yawekewe dhamana ya fidia na umiliki kwa wanaokutwa katika eneo hilo ?
Ibara ya 8 ya katiba 1977, 2005 inasema Serikali inawekwa na wananchi kwa ajili ya rasilimali zao na lengo kuu ni ustawi wao.
8.0 MADARAKA YA SERIKALI ZA MITAA (LOCAL AUTHORITY)
Sura ya nne ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, iliyorekebishwa, 2005 inaunda serikali za mitaa na madaraka yake. Ibara ya 145 (1) ya Katiba ya 2005, inatoa muundo wa Serikali ya Mitaa kila Mkoa, Wilaya, Miji, Kata ka Kijiji cha Tanzania .
Lengo la Serikali ya Mitaa ni ushirikishwaji wa madaraka katika maeneo yao hasa maamuzi ya maendeleo yao .
Swali ni je?
Kuna haja ya kuongeza madaraka hayo katika kukusanya mapato ya uzalishaji katika maeneo yao ? Mfano maeneo ambayo kuna makaa ya mawe, dhahabu, chuma na madini mengine katika maeneo hayo asilimia ya kodi au mrahaba unabaki katika Serikali yao uelekezwe kwao ili kuleta mabadiliko katika eneo husika?
HITIMISHO
Tumejaribu kupitia maaeneo kadhaa ya Katiba yetu na kuona kama tunaweza kuyaangalia na kutolea mapendekezo bora zaidi.
Hivyo ni jukumu lako kutoa mapendekezo ya maboresho kuhusu Katiba mpya katika maeneo hayo tuliyoyapitia. Lakini pia ufungwi kupanua wigo wako wa uelewa wa Katiba kwa kutoa maoni eneo lingine zaidi.
WAKUU WA MIKOA INAYOLIMA KOROSHO KUANDAMANA KUMUONA RAIS JAKAYA KIKWETE
Na,Steven Augustino Tunduru
WAKUU wa Mikoa inayolima Korosho nchini wameahidi kupeleka kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete kero ya ubabaishaji wa bei ya soko la zao hilo ili aweze kulitafutia ufumbuzi wa kudumu zikiwa ni juhudi za kuwawezesha Wakulima kupata matunda ya jasho lao.
Hayao yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Saidi Mwambungu wakati akiongea na wadau wa maendeleo waliojitokeza katika kikao cha dharula cha kujadili hatima ya tukio la ubabaisshaji wa soko la Korosho ambalo msimu huu bei yake imeonesha kusuasua kilichofanyika katika ukumbi wa Boma la halmashauri ya Wilaya hiyo mjini hapa .
Sambamba na maamuzi hayo pia Mwambungu na kamati hiyo ikatoka na azimio la kutouza Korosho hizo kwa Makampuni hayo babaishaji vinginevyo wakubali kununua Korosho hizo kwa Bei itakayo kubalika na wakatumia nafasi hiyo kumuomba Meneja wa Benki ya Nmb Omari Mleche kuongeza mkopo kwa vyama vya msingi ili kuwezesha kununua Korosho zote kwa wakulima wakati juhudi za kutafuta Soko la uhakika zikiendelea.
Akifafanua taarifa hiyo Mwambungu alisema kuwa maamuzi hayo yamefikiwa na Wakuu wa Mikoa ya Lindi Ruvuma na Mtwara baada ya kubaini kuwerpo kwa ubabaishaji wa Soko hilo ulio oneshwa na Wanunuzi hao wakubwa Korosho katika Msimu huu hauwezi kufumbiwa macho na Serikali na kuwaacha Wakulima wakiteseka bila msaada wa Serikali yao.
Awali wakitoa taarifa ya ubabaishaji wa Soko la Mazao hayo Meneja wa Chama Kikuu cha Wakulima wa Korosho TAMCU Ltd Imani Kalembo na Mwenyekiti wa Chama hicho Mahamudu Katomondo walisema kuwa ubabaishaji huo umeonekana katika minada mitatu iliyopita ambapo Makampuni ya Abbas Eport Treding Co.Ltd na Olam Co. Ltd awali wote waliomba kununua chini ya Bei ya Tsh. 1500 kwa kilo moja hali iliyo onesha kuwa makampuni hayo yana ajenda ya siri ya kutaka chama hicho kishindwe kuwalipa Wakulima wake malipo yao ya awamu ya pili.
Walisema kinacho watia mashaka zaidi viongozi hao na kuwafanya wabaini uwepo wa mchezo mchafu kutoa katika Makampuni hayo ni kitendo cha Makampuni hayo pekee kati ya Makampuni 70 ambayo yalijiandikisha na kuomba kununua Korosho hizo katika Msimu huu wa Mwaka 2011/2012,
Wakizungumzia taarifa ya ununuzi Korosho hizo kutoka kwa wakulima walisema kuwa hadi sasa vyama vya msingi vya ushirika vime kwisha kusanya jumla ya Kilo 4,554334 kati ya Kilo 7,000,000 zinazotarajiwa kununuliwa katika Mismu huu na chama chao.
Wakitoa maoni yao wabunge wa Wilaya ya Tunduru Eng. Ramo Makani na Alhaji Mtutura Mtutura waliiomba Serikali kutumia Fedha zilizo idhinishwa katika Bajeti iliyopita kwa ajili ya Matumizi ya dhalula ili zitumike kununula Korosho hizo kutoka kwa Wakulima zikiwa ni juhudi za kuwaondolea adha hiyo.
Nao Madiwani Kazembe said wa kata ya Ligunga na Burhani Nakanje wa Kata ya Marumba mbali na kuutuhumu uongozi wa Kiwanda cha Kubangulia Korosho kinacho milikiwa na Kampni ya Korosho Africa Ltd kuto kuwa na msaada kwa wakulima wa Wilaya yao waliiomba Serikali kuwa na macho na Wanunuzi hao vinginevyo watawaangusha na kuwafanya wananchi kukosa imani na Serikali yao.
Wakijibu tuhuma za Kiwanda hicho kuto kuwa na msaada kwa Wakulima wa zao hilo msimamizi wa Kiwanda hicho Dinesh Poojali na Enginia wa Kiwanda hicho Sivan Edayath mbali na kutoa taarifa kuwa kiwanda chao kimefungwa kutokana na kuishiwa Korosho za kubangua walisema kuwa wao hawana maamuzi yoyoyte juu ya ununuzi wa korosho hizo kutoka katika vyama vya ushirika vya msingi vya Wakulima wa Tunduru.
Mwisho
MTANDAO WA SONNGO WAWAKUTANISHA WANANCHI WA KADA TOFAUTI KATIKA MDAHALO WA KUJADILI KATIBA YA MWAKA 1977
Mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi zisizo za Kiserikali Wilaya ya Songea Siwaji Gama akifungua mdahalo,wa kwanza kushoto ni Afisa Habari wa Sonngo Endrwe Chatwanga,wa kwanza kulia ni Boniface Bundala, wa pili kulia ni Katibu wa Sonngo Mathew Ngarimanayo
Washiriki wa mdahalo huo wakiendelea kusikiliza hoja mbalimbali zinazoendelea kuwasilishwa na jopo la wataalamu wa sheria na katiba
Waandishi wa Habari wakisikiliza majadiliano katika mdahalo huo,kutoka kushoto ni Catherine Nyoni (Tbc) Amon Mtega(Mtanzania) Gideon Mwakanosya(Nipashe) Joseph Mwambije(Majira)
Washiriki wakisikiliza kwa umakini mapitio na uchambuzi wa wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 Jimbo la Songea Mjini
Tuesday, December 27, 2011
WADAU WA MTANDAO HUU WAMWEMELEKA KWENYE KUMBUKIZI ZA KUZALIWA KWA MDAU MWENZAO WA MTANDAO EMMANUEL NTOBI
Keki iliyotengenezwa kwa ubora wenye viwango stahiki maalumu kwa kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwa Emmanuel Ntobi
Emmanuel Ntobi akimrisha keki ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwake mpenzi wake Bi, Sarah Mohamed
Emmanuel Ntobi akimrisha keki Mr Ng'aida kwenye sherehe hiyo
Mdau wa Mtandao huu Stephano Mango akipata keki tamu iliyoandaliwa kwa ajili ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Emmanuel Ntobi wakati wa sherehe hiyo ya aina yake iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Benki ya biashara ya NBC juzi usiku muda mfupi kabla Bwana wetu yesu Kristu ajazaliwa ndio maana Ntobi Emmanuel alibatizwa jina hilo likiwa na maana ya Bwana pamoja nasi
Wadau mbalimbali wakiendelea kupata chakula na vinywaji vya aina mbalimbali kwenye sherehe hiyo iliyofana
| Emmanue Ntobi akijiandaa kuwasha baruti huku akishuhudiwa na Mpenzi wake Bi Sarah Mohamed |
Emmanuel Ntobi akimrisha keki ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwake mpenzi wake Bi, Sarah Mohamed
Emmanuel Ntobi akimrisha keki Mr Ng'aida kwenye sherehe hiyo
Mdau wa Mtandao huu Stephano Mango akipata keki tamu iliyoandaliwa kwa ajili ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Emmanuel Ntobi wakati wa sherehe hiyo ya aina yake iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Benki ya biashara ya NBC juzi usiku muda mfupi kabla Bwana wetu yesu Kristu ajazaliwa ndio maana Ntobi Emmanuel alibatizwa jina hilo likiwa na maana ya Bwana pamoja nasi
Wadau mbalimbali wakiendelea kupata chakula na vinywaji vya aina mbalimbali kwenye sherehe hiyo iliyofana
MUUGUZI WA KIJIJI CHA MANGO AJINYONGA KUTOKANA NA WIVU WA KIMAPENZI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda
Na Gideon Mwakanosya ,Songea
MUUGUZI wa Zahanati ya kijiji cha Mango kilichopo kata ya Kihagara wilayani Mbinga Bosco Nchimbi (29) amekutwa kwenye kenchi ya chumba chake akiwa amekufa baada ya kujinyonga kwa kujitundika juu ya kenchi kwa kutumia kamba ya katani.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda amesema kuwa tukio hilo limetokea juzi majira ya saa kumi jioni huko katika kijiji cha Mango , ambapo katekista wa kijiji cha Tumbi Joseph Nchimbi ndiye aliyegundua kuwepo kwa tukio la kujinyonga Nchimbi .
Amefafanua kuwa, Inadaiwa siku ya tukio kateksta Nchimbi alikuwa ameenda nyumbani kwa Marehemu kwa ajili ya kumpa ushauri baada ya kuwepo malumbano kati yake na Mwanamke aliyezaa naye mtoto anayedaiwa kuwa alikuwa akilalamikiwa kuwa ameanza kufanya ngono na wanaume wengine wakati mtoto wao bado ni mchanga.
Kamanda alieleza zaidi kuwa Katekista Nchimbi baada ya kugundua tukio hilo alitoa taarifa kwa uongozi wa serikali ya kijiji cha Mango ambao nao ulitoa taarifa polisi na askari polisi walipofika katika eneo la tukio wakiwa wameongoozana na Mganga walikuta mwili wa marehemu ukiwa unaninginia .
Kamanda amesema,chanzo cha kujinyonga ni wivu wa mapenzi kati yake na mwanamke aliyezaa naye ambaye wakati wote alikuwa akimuonya kuacha tabia ya kufanya mapenzi na wanaume ovyo kwani anamuaharibu mtoto wao mchanga lakini mwanamke huyo aliendelea hali iliyosababisha apandwe na hasira na kuchukua huamuzi huo.
MWISHO.
Monday, December 26, 2011
Nawatakia Sikukuu njema za X-MASS,BOXING DAY,na MWAKA MPYA wa 2012 wenye Baraka na mafanikio makubwa
Nawasalimu wadau wote wa mtandao wa www.stephanomango.blogspot.comkwa kunipa ushirikiano wenu katika kipindi chote cha mwaka 2011
Nawatakia heri sana katika msimu huu wa mwishoni mwa mwaka 2011 na maandalizi mema ya mwaka mpya wa 2012
God is Love
Christmas is all about love
Christmas is thus about God and Love
Love is the key to peace among all mankind
Love is the key to peace and happiness within all creation
Love needs to be practiced - love needs to flow - love needs to make happy
Love starts with your partner, children and family and expands to all world
God bless all mankind
Christmas is all about love
Christmas is thus about God and Love
Love is the key to peace among all mankind
Love is the key to peace and happiness within all creation
Love needs to be practiced - love needs to flow - love needs to make happy
Love starts with your partner, children and family and expands to all world
God bless all mankind
VIONGOZI NCHINI WATAKIWA KUWATUMIKIA WANANCHI ILI KULINDA AMANI YA NCHI
Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Songea Norbert Mtega
Na, Augustino Chindiye Tunduru
VIONGOZI wa kuchaguliwa na waliopewa mamlaka ya kulitumikia Taifa wameombwa kuitumikia Jamii kwa uadilifu ili kuendelea kudumisha amani na utulivu vinginevyo kuna hatari ya amani hiyo inayojivuniwa na taifa letu kutoweka.
Rai hiyo imetolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo la TUNDURU- Masasi Castory Msemwa wakati akiongea na waamini waliohudhulia katika Misa takatifu ya kukumbuka kuzaliwa Yesu Kristo ya Noeli iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Xavery mjini hapa.
Akifafanua taarifa hiyo kupitia Mahubiri hayo Askofu Msemwa alisema kuwa pamoja na Viongozi hao kufahamu hayo lakini wamekuwa walafi hali ambayo imekuwa ikiwasukuma kuwatesa Wananchi waliowapa nyadhifa hizo .
Alisema mbali na hali hiyo kuonekana wazi kwa Viongozi wa Serikali lakini pia matukio kama hayo yamekuwa yakiwakumba viongozi wa Dini ambapo wamekuwa wakipenda kujinufasha ili waendeelee kuongeza furaha mioyoni mwao kwa kujipangia marupurupu yao wenyewe bila kuwajali wengine na kuiacha jamii ikiteseka bila misaada yao.
Askofu Msemwa akatumia nafasi hiyo kuhimiza upendo miongoni mwetu na kueleza kuwa endapo upendo utaendelea kutoweka kuna hatari ya amani tunayo jivunia kumomonyoka na kuipeleka nchi yetu pabaya.
Katika hutuba hiyo pia Askofu Msemwa akaikumbusha jamii kuiga mwenendo wa mwasisi wa Taifa la Watanzania Mwenyeheri Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mtumishi wa Mungu Sister Bernadeta wa Jimbo la Perahimo ambaye amekuwa gumzo kubwa kutokana na watu wengi kwenda kuomba katika kaburi lake na kufanikiwa.
Alisema Sister Bernadeta alitangazwa hivi karibuni kuwa mtumishi wa Mungu ukiwa ni mchakato wa kufikia nafasi ya Mwenyeheri na kongeza kuwa mapendo ya kweli katika jamii yao ndiyo yaliyowafanya waendelee kukumbwa na jamii yao .
Mwisho
Thursday, December 22, 2011
DIWANI MSTAAFU GOLDEN SANGA (SANGA ONE) ATOA MSAADA WA ELFU HAMSINI KWENYE KIKUNDI CHA SANAA CHA WAZALENDO KWA AJILI YA MAANDALIZI YA UZINDUZI WA FALAMU YAO YA MAJARIBU
Diwani Mstaafu wa Kata ya Bombambili Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma Golden Sanga maarufu kwa jina la Sanga One akimkabidhi shilingi elfu hamsini(50,000/=) Mwenyekiti wa kundi la sanaa la Wazalendo Abdalah Bin Ahmed kwa jina la kisanii Ramsh,katikati ni Mlezi wa kundi hilo Mama Ndimbo,wa kwanza kushoto ni Mhasibu wa kundi hilo Zainab Nungu kwa jina la kisanii Walda
Diwani Mstaafu Sanga One akizungumza na kundi la wasanii la Wazalendo mara baada ya kukabidhi msaada wa fedha kwa ajili ya maandalizi ya uzinduzi wa filamu mpya ya kundi hilo,Katikati Mlezi wa kundi hilo Mama Ndimbo,wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa kundi hilo Abdalah Bin Ahmed-Ramsh
Sanga One akiwa kwenye picha ya pamoja na wasanii wa kundi la Wazalendo mara baada ya kuzungumza nao hivi karibuni kwenye ukumbi wa Better Life Tanzania mjini Songea
Baadhi ya wasanii wa kundi la Wazalendo wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wao
Diwani Mstaafu Sanga One akizungumza na kundi la wasanii la Wazalendo mara baada ya kukabidhi msaada wa fedha kwa ajili ya maandalizi ya uzinduzi wa filamu mpya ya kundi hilo,Katikati Mlezi wa kundi hilo Mama Ndimbo,wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa kundi hilo Abdalah Bin Ahmed-Ramsh
Sanga One akiwa kwenye picha ya pamoja na wasanii wa kundi la Wazalendo mara baada ya kuzungumza nao hivi karibuni kwenye ukumbi wa Better Life Tanzania mjini Songea
Baadhi ya wasanii wa kundi la Wazalendo wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wao
KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI WA HALMASHAURI YA SONGEA CHAANZA ASUBUHI HII KATIKA JENGO LA MAENDELEO
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Beatrice Msomisi akiwasalimia wajumbe wa Baraza la Madiwani
Kutoka kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho Jenista Mhagama,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Beatrice Msomisi,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Songea Rajabu Mtiula,Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Andrwe Mhagama
Madiwani wa Halmashauri ya Songea wakiendelea na kikao chao kilichofanyika kwenye ukumbi wa jengo la Maendeleo(Mnara wa saa)
Wataalamu na wakuu wa idara mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea wakisikiliza kwa umakini hoja mbalimbali zinazoendelea kuwasilishwa kwenye kikao hicho
Kutoka kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho Jenista Mhagama,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Beatrice Msomisi,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Songea Rajabu Mtiula,Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Andrwe Mhagama
Madiwani wa Halmashauri ya Songea wakiendelea na kikao chao kilichofanyika kwenye ukumbi wa jengo la Maendeleo(Mnara wa saa)
Wataalamu na wakuu wa idara mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea wakisikiliza kwa umakini hoja mbalimbali zinazoendelea kuwasilishwa kwenye kikao hicho
Subscribe to:
Posts (Atom)





