About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Thursday, December 29, 2011

MDAHALO WA WANANCHI NA VIONGOZI MBALIMBALI JIMBO LA SONGEA MJINI KUHUSU MAPITIO YA KATIBA UKUMBI WA KANISA LA BOMBAMBILI WAMALIZIKA NA SASA NI ZAMU YA JIMBO LA PERAMIHO





 Katibu wa Sonngo Mathew Ngarimanayo akizungumza katika mdahalo

 Mwanaharakati na Mwandishi wa Habari mkongwe Juma Nyumayo akifafanua jambo wakati wa mdahalo huo
 Mwanaharakati Fatuma Misango kulia na Ifigenia Mbawala wakifuatilia mdahalo huo
Mwenyekiti wa Mtandao wa Sonngo Siwajibu Gama akiwa na Katibu wa Mtandao huo Mathew Ngarimanayo
SONGEA NETWORK OF NON – GOVERNMENTAL ORGANIZATIONS
(SONNGO)
SLP. 791 SONGEA – RUVUMA TANZANIA
Simu Na:025- 2600877, Simu ya kiganjani: 0754-533032, 0752 - 202117
Baruapepe: sonngosongea @yahoo.Com
Ofisi – Barabara ya Sokoine Jengo la CCM Mkoa

                 
HISTORIA YA KATIBA TANZANIA
 NA MICHAKATO YA UANDIKAJI WAKE


1.0.   MAANA YA KATIBA
Wanazuoni, wanaharakati, wadau, wabia wa maendeleo na wananchi mbalimbali wanaielezea Katiba kwa mitazamo tofauti kutokana na mandhari na matumizi yake katika jamii.  Hata hivyo makundi yote hayo wanaielezea Katiba kuwa ni:-

·        Waraka wa Kisiasa, Kiutawala na Kisheria ambao unawawezesha wananchi kujitambua kama Taifa, unaelezea mgawanyo wa madaraka na majukumu ya vyombo mbalimbali vya dola na kuongoza shughuli zote kisheria ambao ndio chimbuko la sheria zote nchini.

·        Pia Katiba ni muafaka wa Kitaifa na ni mkataba kati ya viongozi na wananchi.

2.0.         MISINGI NA SIFA YA KATIBA.
                                                          i.            Katiba lazima iwezeshe wananchi kuridhiana kitaifa.
                                                       ii.            Wananchi kuwa na nguvu ya kumiliki Katiba yao.
                                                     iii.            Katiba kuwa ya kipekee kutokana na historia ya nchi hisika.
                                                     iv.            Katiba kuwa na nguvu ya kisheria inayozingatia haki za binadamu, haitoi mwanya wa ubaguzi wala upendeleo wa aina yoyote.
                                                       v.            Katiba lazima itoe maono na mwelekeo wa Taifa.
                                                     vi.            Katiba lazima iweke bayana masuala ya msingi ya kitaifa na mustakabali wake.

3.0.         KATIBA ZILIZOTANGULIA TANGU UHURU
Tangu Tanganyika na Zanzibar zipate Uhuru na kuungana kumekuwa na Katiba 5 za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba kadhaa za Zanzibar.  Kwa upande wa Zanzibar tunagusia kwa muhtasari Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na marekebisho ya 10 ya Katiba hiyo ya mwaka 2010.

Katiba zilizotangulia tangu Uhuru ni hizi:-

3.1.         KATIBA YA UHURU (1961)
·        Katiba hii iliundwa kwa lengo la kuipatia Tanganyika Uhuru wake toka kwa Waingereza, ndio maana ikaitwa Katiba ya Uhuru.
·        Katiba hii iliundwa Uingereza na kuileta Tanganyika.
·        Katika uandikaji wake Katiba hii haikushirikisha wananchi wa Tanganyika.
·        Katiba hii ilimtambua Waziri Mkuu ambaye hakuwa na madaraka makubwa kwani yeye alikuwa anasimamia masuala ya serikali bungeni tu.
·        Malkia wa Uingereza bado alikuwa na madaraka makubwa kwani maamuzi mengi yalikuwa yanamtegemea Malkia.
·        Katiba hii haikutambua haki za binadamu.
·        Hata hivyo baadhi ya mambo mazuri yaliyokuwamo katika Katiba ya Uhuru ni kwamba:-
                                                         i.            Katiba ilitoa Uhuru wa Mahakama.
                                                       ii.            Baraza la Mawaziri na Waziri mmoja walikuwa wanawajibika kwa Bunge.

3.2.         KATIBA YA JAMUHURI (1962)
·      Katiba hii iliitwa Katiba ya Jamuhuri kwa sababu ndiyo iliyoanzisha mfumo wa Urais.
·      Mchakato wa kuiandika kwake haukushirikisha wananchi.
·      Bunge la wabunge 71 wa TANU walijigeuza kuwa Bunge la Katiba na kuipitisha Katiba hii.
·      Katiba hii ilimtambua Rais kuwa mkuu wa Nchi na kiongozi wa serikali.
·      Baraza la mawaziri na Waziri mmoja mmoja sasa walikuwa wanawajibika kwa Rais.
·      Rais wan chi alikuwa na nguvu nyingi sana.
·      Sheria nyingi zilitungwa chini ya Katiba hii na nyingi zilikuwa kandamizi.

3.3.         KATIBA YA MUUNGANO (1964)
·        Katiba hii iliundwa baada ya Tanganyika na Zanzibar kuungana na kuwa nchi moja. 
·        Katiba hii ilisimamia mambo 11 ya Muungano na mambo ya Serikali ya Tanganyika.
·        Katiba hii iliweka muundo wan chi wa serikali mbili (Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar)
·        Katiba hii ilimtambua Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano na mjumbe wa baraza la mawaziri.
·        Katiba hii ilianzishwa kwa tamko la Rais na kuridhiwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la wawakilishi Zanzibar.
·        Katiba hii ilikuwa ya muda ya Muungano na ilikusudiwa kutumika kwa muda wa mwaka mmoja tu.
·        Katiba hii iliweka utaratibu wa wa kuandaa Katiba ya kudumu ya Muungano kwa kuunda tume ya Katiba na bunge la Katiba ili kuhakikisha ushiriki wa wananchi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

3.4.         KATIBA YA MPITO (1965)
·        Katiba hii iliitwa ya mpito.
·        Katiba hii ndio iliyoitambua nchi kuwa ni ya chama kimoja tu cha siasa (TANU kwa upande wa Tanganyika na ASP kwa upande wa Zanzibar).
·        Katiba hii ndiyo iliyotamka rasmi chama kushika hatamu kuu ya TANU (NEC) ilikuwa na nguvu zaidi kuliko bunge au hata Katiba yenyewe.
·        Katiba hii ilipitishwa kama sheria ya kawaida inavyopitishwa bungeni.
·        Katiba ya TANU ilikuwa sehemu ya Katiba ya Muungano.
·        Katiba hii iliongeza mambo ya Muungano.
·        Utata wa Uhuru wa Muungano (autonomy) kuwa nchi ulionekaka dhahiri.
·        Tume ya Rais ya Katiba ya kukusanya maoni kwa wananchi iliundwa.

3.5.         KATIBA YA KUDUMU (1977)
·        Katiba hii iliitwa Katiba ya kudumu.
·        Katiba hii ilikuwa ya Tano.
·        Uandikaji wa Katiba hii haukushirikisha wananchi.
·        Katiba hii ilipatikana kupitia tume ya Rais yenye wajumbe 20 (10     
     toka  Tanzania bara na 10 toka Tanzania Zanzibar).
·        Tume hii ya Rais iliongozwa na Sheikh Thabita Kombo na Katibu wa tume alikuwa ndugu Pius Msekwa.
·        Kabla ya kuandika Katiba ya kudumu, tume hii ilianza kuandika Katiba ya CCM baada ya kuunganisha vyama vya TANU na ASP tarehe 5/2/1077.
·        Katiba ya kudumu ilijikita katika misingi mikuu mitatu yaani:-
                                                       i.            Urais wenye nguvu zaidi.
                                                     ii.            Mfumo wa chama kimoja.
                                                  iii.            Mfumo wa serikali mbili.

·        Katiba ya kudumu ilipitishwa kwa Rais kuliteua Bunge la kawaida kujigeuza kuwa bunge la Katiba na kupitisha Katiba ndani ya masaa matatu tu.

4.0.         MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 1977
·        Katiba ya kudumu ya mwaka 1977 imefanyiwa mabadiliko 14 na kwa kiasi kikubwa mabadiliko hayo yamewakwepa wananchi, isipokuwa mabadiliko ya mwaka 1984 ambayo yaliwashirikisha wananchi.
·        Badala ya NEC kufanya maamuzi ilianzisha mjadala wa mwaka mmoja wa wananchi na kuiagiza serikali kutekeleza.
·        Baadhi ya mapendekezo ya wananchi yalikuwa ni:-
                                                                   i.            Hati ya haki za binadamu.
                                                                 ii.            Kujitawala kwa Zanzibar ambayo haikuwemo kwenye mapendekezo ya chama.
·        Mwaka 1991 Rais mstaafu Hassan Mwinyi aliteua tume ya   
                          kuangalia hali ya kisiasa nchini.  Tume hii iliongozwa na                                      
                          marehemu Jaji Francis Nyalali.
·        Tume hii pamoja na mambo mengine ilipendekeza kufutwa kwa sheria kadhaa kandamizi na kufanyia mabadiliko Katiba ya Muungano nay a Zanzibar.
·        Mwaka 1988 iliundwa tume nyingine iliyoongozwa na Jaji Robert Kisanga ambayo nayo pia ilitoa mapendekezo yake mengi kuhusiana na masuala ya kisiasa nchini.

4.1.         MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 1979.
·        Mabadiliko haya yalilenga kuanzisha mahakama ya Rufaa nchini yaani kwa Muungano na Zanzibar.

4.2.         MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 1980
·        Mwaka 1980 Katiba ya kudumu ya mwka 1977 ilifanyiwa mabadiliko mara mbili kwa malengo tofauti tofauti:-
                                                             i.      Mabadiliko yalifanywa kwa lengo la kuimarisha Muungano
     kwa kujibu masuala ya Zanzibar.
4.3.         ii. Kuweka mfumo wa uchaguzi wa Rais wa Zanzibar.
·        Kuweka mfumo wa Serikali ya Zanzibar.
·        Kuweka muundo wa Baraza la wawakilishi Zanzibar.
4.4.         MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 1982
·        Mabadiliko haya yalilenga uteuzi wa wakuu wa mikoa ingawa hayakuweka uwajibikaji wa wakuu wa mikoa na Wilaya.

4.5.         MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 1984
·        Mabadiliko haya yalilenga kuingiza masuala ya haki za binadamu kwenye Katiba ya nchi.

4.6.         MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 1990
          Mwaka 1990 Katiba ya kudumu ilifanyiwa mabadiliko mara mbili kwa lengo la :-
·        Kuanzisha Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995.

4.7.                                 Kuweka utaratibu wa kupata mgombea mmoja wa Urais kwa Zanzibar.

4.8.         MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 1992
          Mwaka 1992 yalifanyika mabadiliko ya Katiba mara mbili kwa malengo ya :-
·        Kufuta mfumo wa chama kimoja nchini.
·        Kuanzisha mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini.
·        Kubadilisha mfumo wa bunge la Jamuhuri ya Muungano na kuanzisha viti maalum vya wanawake kufikia 15% na viti 5 toka baraza la wawakilishi.
·        Yalianzisha uandikishaji wa vyama vya siasa na uteuzi wa wagombea kupitia vyama vya siasa.


4.9.         Miezi sita baadae baada ya kufanyika kwa mabadiliko ya nane ya Katiba
          yalifanyika mabadiliko mengine yaliyolenga:-
·        Kubadilisha utaratibu wa uchaguzi wa Rais.
·        Nguvu ya Bunge ya kumuondoa Rais madarakani kwa kupiga kura ya kutokuwa na imani naye iliwekwa.
·        Ilianzisha nafasi ya Waziri Mkuu na uwezo wa Bunge wa kumuondoa madarakani kwa kupiga kura ya kutokuwa na imani naye.
·        Masharti ya Rais kulivunja Bunge yaliwekwa.

4.10.    MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 1993
·        Mabadiliko hayo yalifanywa kwa lengo la kuzifanya chaguzi za Madiwani, Wabunge na Rais kufanyika kwa pamoja.
·        Mabadiliko hayo pia yaliipa nguvu “Tume y Taifa ya Uchaguzi” kisimamia chaguzi za Madiwani, Wabunge na Rais.

4.11.    MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 1994
·        Mabadiliko hayo yalikuja kutokana na mapendekezo ya Tume Paul Boman.
·        Mabadiliko hayo ndiyo yaliyomtambua mgombea mwenza wa Urais wa Jamuhuri ya Muungano ambaye angekuwa Makamu wa Rais.
·        Mabadiliko hayo ndiyo yaliyofuta Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano.
·        Mabadiliko hayo yaliendelea kumtambua Rais wa Zanzibar kuwa mjumbe katika baraza la mawaziri la Jamuhuri ya Muungano.

4.12.    MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 1995
·        Mabadiliko haya yalifanyika mwaka 1995 kabla ya kuvunja bunge.
·        Mabadiliko haya yalifanywa kwa lengo la :-
                                                       i.            Kumtaka Rais wa Jamuhuri ya Muungano na Makamu wake, Waziri Mkuu na Rais wa Zanzibar kula kiapo cha kuulinda Muungano.
                                                     ii.            Mabadiliko haya pia yaliweka ukomo wa muda wa Urais wa kukaa madarakani kuwa ni awamu mbili za miaka mitano mitano.

4.13.    MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 2000
·        Mabadiliko haya yalifanywa baada ya uchaguzi wa kwanza kwa mfumo wa vyama vingi na baada ya kuwasilishwa kwa ripoti ya Jaji Robert Kisanga.
·        Mabadiliko hayo yalilenga:-
                                                       i.            Ilifafanua kura za ushindi wa Rais sio lazima awe ameshinda kwa 51% na zaidi bali Rais atatangazwa kuwa mshindi kwa uwingi wa kura.
                                                     ii.            Mabadiliko haya yalimpa uwezo Rais wa kuteua watu 10 kuwa wabunge wa Jamuhuri ya Muungano.
                                                  iii.            Mabadiliko hayo pia yaliongeza idadi ya viti maalum vya wanawake toka 15% hadi 20%.

4.14.    MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 2005
·        Mabadiliko haya yalifanywa kwa lengo la:-
                                                       i.      Kuongeza idadi ya viti maalum vya wanawake toka 20% hadi 30% .
                                                     ii.      Uhuru wa kuabudu.
                                                  iii.      Uhuru wa kushiriki na watu wengine katika kujieleza.
                                                  iv.      Utaratibu wa kuteua wabunge wa viti maalum kwa wanawake kutegemea na uwiano wa ushindi katika uchaguzi.

5.0.         KATIBA YA ZANZIBAR YA MWAKA 1984
·        Mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 yaliyofanyika mwaka 2010 yameleta maswali mengi kwa Watanzania kwani kwa kiasi kikubwa yamegusa sana masuala ya Muungano, hivyo tunaweza kusema Muungano umetikisika kwani:-
                                                 i.            Yameitambua Zanzibar kama nchi na mipaka yake, bendera na vikosi vyake.
                                               ii.            Yamempa nguvu Rais wa Zanzibar  kuigawa Zanzibar kama Wilaya na mikoa kinyume na ilivyokuwa awali ambapo walikuwa wanashauriana na Rais wa Jamuhuri ya Muungano.
                                            iii.            Yamempa nguvu Rais wa Zanzibar ya kuteua wakuu wa mikoa na Wilaya.
                                            iv.            Yameipa Zanzibar Mahakama ya Rufaa ambalo lilikuwa suala la Muunano hapo awali.
                                               v.            Yameongeza idadi ya viti maalum vya wanawake na kuwa 40% ambapo Muungano ni 30%.
                                            vi.            Yamemtaja Rais wa Zanzibar kuwa ni mkuu wan chi.
                                          vii.            Yameanzisha makamu wawili wa Rais ambapo Katiba ya Jamuhuri ya Muungano haiwatambui.  Katiba ya Jamuhuri ya Muungano inawatambua Rais wa Zanzibar na Waziri Kiongozi.
                                       viii.            Yameweka wigo wa baraza la wawakilishi kutochezea na kubadilisha Katiba ya Zanzibar na hasa sehemu inayohusu tamko la haki za binadamu na ibara ya kwanza nay a pili mpaka kura ya maoni ipigwe.

6.0.         KWA NINI KATIBA MPYA SASA
·        Watanzania wengi wanajiuliza swali hili, kwa nini Katiba mpya sasa?  Lakini jambo la maana zaidi ni pale tunapowaona watanzania wanajibu swali hili ingawa kwa mtazamo tofauti tofauti.
·        Hizi nitakazozitaja hapa chini ni sababu chache zinazitajwa na watanzania walio wengi kuwa ndizo sababu hasa zinazopeleka Taifa kwenye utungaji wa Katiba mpya.  Sababu nhizo ni pamoja na:-
                                           i.            Katiba za awali hazikushirikisha wananchi hivyo Katiba hizo hazikutokana na matakwa ya wananchi.
                                         ii.            Katiba ya mwaka 1977 imefanyiwa mabadiliko mengi (14) hivyo ni dhahiri imepoteza sifa za kuitwa Katiba ya kudumu.
                                      iii.            Marekebisho ya 10 ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
                                      iv.            Mfumo wa kisasa nchini wa vyama vingi vya siasa, kwani Katiba iliyopo ilitungwa kipindi cha mfumo wa chama kimoja cha siasa.
                                         v.            Kuweka sawa swala nyeti na muhimu la Muungano maana kuna mkanganyiko kati ya serikali na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali ya Zanzibar, suala hili linatakiwa liwekwe vyema katika Katiba mpya.

7.0.         MCHAKATO WA KUTUNGA KATIBA MPYA
Kuna njia mbalimbali za kutunga/kuandika katiba mpya nchini, lakini wanazuoni na wananchi walio wengi wanapendekeza njia/mchakato ufuatao kama nitakavyoeleza hapo baadae.

·        Nchi yoyote inaingia kwenye machafuko ya kivita kwa kuwa wananchi wake wanakosa jukwaa la kujadili na kukubaliana namna bora na inayofaa ya kufanya michakato mbalimbali inayohusu maamuzi wan nchi zao na namna bora ya kutumia rasilimali zao, hioy ikiwa ni pamoja na suala hili tunalozungumzia la uandikaji/utungaji wa Katiba mpya.

·        Wananchi kama Taifa ni muhimu na ni vema wakubaliane namna mchakato wa kuandika Katiba mpya utakavyokuwa.

·        Baadhi ya njia/mchakato wa kuandika Katiba ambao unapendekezwa na wanazuoni na wananchi mbalimbali mchakato ambao unatoa fursa kwa wananchi wote kushirikikatika hatua zote za uandikaji wa Katiba mpya ni huu

                                                          i.            Mijadala ya awali ya Katiba.
·        Hii ni hatua ya awali kabisa ambapo wananchi wanapata fursa ya kuibua, kujadili na kukubaliana mambo ambayo wanataka yazingatiwe katika Katiba mpya.  Hili laweza kufanyika katika mikutano ya vijiji, kata na mikusanyiko ya ibada.

                                                       ii.            Mkutano Mkuu wa kitaifa.
·        Mkutano huu utajadili mambo yaliyoibuka katika majadiliano ya makundi, kuyachambua na kuyapanga katika mafungu mambo yanayojadilika, kwa mfano mambo yanayohusu haki za binadamu, rasilimali za nchi, mgawanyiko wa madaraka na
masuala ya kubishaniwa (contentious issues).  Mkutano huu unatakiwa uhusishe uwakilishi mpana wa makundi mbalimbali ya wananchi.

Inashauriwa wajumbe wa mkutano huu wachaguliwe na wananchi kama sheria itakavyoelekezwa kwa lengo la kujenga muafaka wa kitaifa kuhusu masuala muhimu.

                                                     iii.            Tume ya wataalamu wa Katiba (Constitutional commission)
·        Hii ni hatua ambapo tume ya wataalamu wa Katiba na sheria itateuliwa.  Kazi ya tume itakuwa ni kuratibu maoni ya wananchi na kuyaweka katika waraka maalum na kuhamasisha wananchi.

·        Tume hii ya wataalamu wa Katiba na sheria inapendekezwa iteuliwe na Rais na kuthibitishwa na Bunge la Jamuhuri ya Muungano ambalo litawawakilisha wananchi.

·        Tume hii inapendekezwa kuwa na wataalam wa kada mbalimbali na izingatie usawa wa kijinsia.

                                                  iv.                  Mjadala wa waraka maalum wa Katiba.
·        Matokeo ya kazi ya tume ya wataalam yatawekwa katika waraka maalum wa Katiba kwa ajili ya mjadala mpana zaidi wa wananchi juu ya yaliyomo.

                                                     v.                  Bunge maalum la Katiba (constituent Assembly)
·        Rasimu ya Katiba ikishaandaliwa ipelekwe mbele ya Bunge maalum la Katiba.

·        Bunge hili maalum la Katiba liundwe kwa utaratibu maalum tofauti na bunge lililopo la Jamuhuri ya Muungano.


·        Bunge hili maalum la Katiba liwakilishe makundi mbalimbali kama vile wanawake, wanaume, walemavu, wakulima, wafanyakazi, wafanyabiashara, vyama vya wafanyakazi, asasi za kiraia, madhehebu ya dini mbalimbali na kadharika.

·        Kazi kubwa ya bunge hili ni kupitia na kuridhia rasimu ya Katiba iliyoandaliwa.
·        Bunge maalum la Katiba litakoma mara tu baada ya kuridhia rasimu hiyo ya Katiba.

                                            vi.      Kura ya maamuzi (Referundum)
·              Baada ya rasimu ya Katiba kuridhiwa na Bunge maalum la Katiba, hatua ya mwisho katika kupata katiba mpya ni kwa wananchi kushiriki kwa njia ya kura ya maamuzi.

·              Kura hii itapigwa nchi nzima na wananchi wote wenye na sifa za kupiga kura watapiga kura.


·              Endapo kura za ndio kwa Katiba zitazidi zile za hapana Katiba itakubalika na kuanza kutumika/kufanya kazi.


AHSANTE SANA KWA KUNISIKILIZA NA KARIBU KWA MAJADILIANO.

MDAHALO WA KATIBA WAENDELEA

 Afisa Kazi Mkoa wa Ruvuma Oddo Egino Hekela akizungumzia mapitio ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2005 wakati wa mdahalo
 Hakimu Mkazi Elizabeth Misano akizungumza wakati wa mdahalo
 Mwenyekiti wa Mtandao wa Sonngo Siwajibu Gama akifafanua hoja mbalimbali katika mdahalo

Washiriki wa mdahalo huo wakiendelea kusikiliza hoja mbalimbali katika mdahalo huo uliofanyika jana kwenye ukumbi wa mikutano wa kanisa la Bombambili

MDAHALO WA WAZI KUHUSU UCHAMBUZI NA MAPITIO YA KATIBA YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977



MWANDAAJI:  SONGEA NETWORK OF NON – GOVERNMENTAL         ORGANIZATIONS (SONNGO)


MADA:  MAPITIO YA KATIBA YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977 ILIYOFANYIWA MAREKEBISHO 2005





MTOA MADA:  ODDO EGINO HEKELA
                            AFISA KAZI RUVUMA, NA MKURUGENZI WA KAMPUNI YA KAZI BUREAU SERVICES CO.LTD
                            P.O.
BOX 1050
, SONGEA
                            TEL: 0784 332 378/ 0655 332 378/0755 094 862
                             E- MAIL: odo.egino@yahoo.com


MADA:  MAPITIO YA KATIBA YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977 KAMA ILIVYOFANYIWA MAREKEBISHO 2005.

1.0    UTANGULIZI
Ili kupitia Katiba yote na kuielewa tunahitaji darasa la wiki na zaidi kujenga uelewa.  Lakini kwa matakwa ya mdahalo  tunagusa maeneo muhimu ya Katiba yetu ili tuone mapungufu yake na kuelekeza maoni yetu katika maeneo hayo.  Maeneo hayo ni  Maana ya Katiba,Aina ya katiba iliyopo, Serikali ya watu, Madaraka ya Rais, Uteizi wa mawaziri, Madaraka ya Bunge, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari, Uhuru wa Mahakama, Haki za binadamu na Serikali za mitaa.

1.0    MAANA YA KATIBA
Katiba ni sheria mama ya nchi inayotoa au kuweka Utawala na eneo la utawala, madaraka ya viongozi na mgawanyo wa majukumu katika miimili yote mitatu ya Serikali yaani Bunge, Mahakama na watendaji wa Serikali (Parliament, Judiciary and Executives).

2.0    KATIBA YA KUDUMU (1977) KAMA ILIVYOFANYIWA MAREKEBISHO 2005.
Katiba hii ilipatikana kupitia tume ya Rais yenye wajumbe 20 yaani 10 kutoka Bara na 10 kutoka Visiwani (Zanzibar).  Katiba hii iliitwa Katiba ya kudumu.  Kabla ya kuandaliwa Katiba hii tume hii ilianza kuandika Katiba ya CCM baada ya kuunganisha vyanma vya TANU na ASP tarehe 5/2/1977.  Katiba iliweka misingi mikuu ya madaraka na majukumu
                          i.            Mfumo wa chama kimoja
                        ii.            Uraisi wenye nguvu zaidi na
                     iii.            Mfumo wa Serikali mbili.

Katiba ya kudumu ilipitishwa  na Rais na baadae aliteua Bunge la kawaida kujigeuza kuwa Bunge la Katiba na kupitisha Katiba ndani ya masaa matatu tu.  Katiba hii imefanyiwa marekebisho mengi kufuatia mahitaji ya Taifa kwa nyakati mbalimbali hadi 2005.  Mabadiliko makubwa ni yale ya kuruhusu tena uwepo wa vyama vingi na uanzishwaji wa tume ya uchaguzi ya Taifa (NEC), ongezeko la viti maalum na uwiano wao (2005).

3.0    SERIKALI YA WATU
Katika sehemu ya pili ya Katiba, Ibara ya 8 (1) ya Katiba ya mwaka 1977, na marekebisho ya 2005, inasema;
·        Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii.  Wananchi ndio msingi wa mamlaka yote.
·        Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi.
·        Lengo kuu la Serikali ni ustawi wa wananchi.
·        Serikali itawajibika kwa wananchi.
·        Wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao.

       Sheria iliyoundwa kutoa maelekezo ni sheria ya Serikali na watu ya 1984 na. 15.

Swali ni je?
Uwanja wa demokrasia umepanuliwa na kuwapa wananchi madaraka ya kuweka Serikali kama wapendavyo? Na nini kifanyike?

3.1      UJENZI WA UJAMAA NA KUJITEGEMEA
Ibara ya 9 ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania 2005 inatoa msingi huu kwa kutamka uelekeo wa nchi ni wa ujamaa na kujitegemea.  Kwa hiyo sera na shughuli zote za Serikali zielekeze nguvu katika ujenzi huo.
       Mambo yaliyowekewa mkazo na Katiba hii ni:
·        Utu na haki za binadamu.
·        Utawala wa sheria.
·        Utajiri wa Taifa unakuwa kwa manufaa ya umma.
·        Ulinganifu na ushirikishwaji wa wananchi katika maendeleo ya nchi.
·        Kazi kama shughuli halali.
·        Heshima ya binadamu inahifadhiwa.
·        Hakuna ubaguzi wa rangi, jinsi, kabila, dini wala hali ya mtu.
·        Dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa, uonevu na upendeleo zinaondolewa nchini.
·        Utajiri wa Taifa unanufaisha umma.
·        Hakuna ulimbikizaji wa mali.

·        Demokrasia inatawala zaidi.

       Swali ni je?
1.     Tunauhitaji wa kuendelea na msingi wa ujamaa na kujitegemea? Kama ndio kwa uelekeo gani?
2.     mali asili ya nchi imewekewa misingi ya umiliki kwa faida ya umma?


4.0 SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO
       Ibara ya 34 (1) inasema kutakuwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ambayo itakuwa na mamlaka ya mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya muungano, na pia juu ya mambo mengine yote yahusuyo Tanzania Bara.

        Swali ni je?
        Hakuna uwezekano wa kuwa na Serikali tatu yaani Tanganyika, Zanzibari na Muungano?

4.1       MADARAKA YA RAIS
Ibara ya 33 (2) ya Katiba 1977 na marekebisho ya 2005, inasema Rais atakuwa Mkuu wa Nchi, kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu. Rais anapewa madaraka yafuatayo na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Upana wa Madaraka ya Rais
     
·        Mamlaka ya kuanzisha na kufuta nafasi za madaraka ya namna mbalimbali katika utumishi wa umma. Ibara ya 36(1) ya katiba 1977,iliyorekebishwa 2005
·        Kuwateua watu kushika nafasi za madaraka.  Ibara ya 36 (2) ya Katiba 1977, iliyorekebishwa 2005.
·        Madaraka ya kuwapandisha vyeo au kuwafukuza kazi Ibara 26 (3) ya Katiba 1977, 2005.
·        Kudhibiti nidhamu katika watumishi wa Serikali Ibara ya 36 (4) 2005.
·        Hatalazimika kufuata ushauri atakaopewa na mtu yeyote , isipokuwa tu pale anapotakiwa na Katiba hii au sheria nyingine Ibara ya 37 (1) ya Katiba 2005.
·        Madaraka ya kutangaza vita, Ibara ya 44 (1) ya Katiba 2005, inatoa madaraka kwa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
·        Uwezo wa kutoa msamaha kwa mtu yeyote aliyepatikana na  hatia mbele za mahakama kwa kosa lolote bila ya masharti au kwa masharti Ibara ya 45 (1) (a) (b) 2005.
·        Kuibadilisha adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa kosa lolote iwe adhabu tahalifu Ibara ya 45 (1) (c), 2005.
·        Kufuta adhabu yoyote au sehemu ya adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa ajili ya kosa lolote au kuhozi (kuchukua) kitu cha mtu mwenye hatia ambacho vinginevyo kingechukuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano Ibara ya 45 (d) ya Katiba 2005.

Swali ni je?
Akitoa upendeleo wowote nani atakuwa na jukumu la kuuliza au kupinga katika madaraka makubwa kiasi hicho?

4.2       UTEUZI WA MAWAZIRI
Katiba inampa madaraka hayo Rais ya kuteua mawaziri wake wa kusaidia Serikali yake.  Ibara ya 55 (1) ya Katiba  1977, iliyorekebishwa ,2005.

Ibara ya 55(4) ya katiba 1977, iliyorekebishwa 2005 inasema; Mawaziri na manaibu mawaziri wote Katiba inataka watokane na Wabunge waliounda Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Swali ni je?
Hakuna uwezekano wa kupata mawaziri wasio wabunge kwa mujibu wa Katiba?

4.0    MADARAKA YA BUNGE
                          i.            Bunge letu linaundwa na sehemu mbili yaani Rais na Wabunge.  Kwa mujibu wa Ibara ya 62 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano 2005.  Kwa hiyo Bunge letu linapoteza uwezo wa kujitegemea ukilinganisha na Bunge la Uingereza na Marekani kwa kuwa shughuli zake zinawezeshwa na Rais wa Nchi.  Na maamuzi yake yanachujwa na Rais wa Nchi kwa mujibu wa Ibara ya 63 (1) Rais kama sehemu moja ya Bunge atatekeleza madaraka yote aliyokabidhiwa na Katiba hii kwa ajili hiyo.

Bunge letu lina uwezo wa kupendekeza kwa Rais kuhusu kumuondoa mtu au kumweka mtu madarakani kutokana na  utovu wa nidhamu au wizi uliotendeka katika kusimamia Serikali lakini siyo kumuondoa, au madaraka ya kumwondoa mtu kama huyo yapo kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Swali ni je?
Kwa kufanya hivyo hatuoni kwamba Bunge linapunguziwa uwezo kwa mujibu wa Ibara ya 63 (2) ya Katiba 1977, iliyorekebishwa, 2005?

                        ii.            Madaraka ya kutunga sheria katika Ibara ya 63 (3) (d) ya Katiba ya 2005, Bunge linapewa uwezo wa kutunga sheria ili ifanye kazi inahitaji mkono wa Rais na ridhaa yake. Baada ya Bunge kutunga sheria haiwezi kufanya kazi kama rais hajasaini na kuifanya kuwa sheria katika nchi.

Swali ni je?
                  Hilo linaweza kupunguza madaraka ya Bunge kutunga sheria?

                     iii.            Madaraka ya Bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania dhidi ya Serikali ya Zanzabar ni madogo sana Ibara ya 64 (3) (4) ya 2005.  Baraza la wawakilishi la Zanzibar ndilo lenye madaraka makubwa na maswala ya Zanzibar.

Swali ni je?
Baraza la wawakilishi katika serkali ya mapinduzi la Zanzibar haliwezikukinzana katika maamuzi na Bunge la muungano?

5.0    SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBARI
Katika sura ya nne ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, iliyorekebishwa ,2005 Ibara ya 102 (1) inataja kuwa kutakuwa na serikali ya Zanzibar itakayojulikana kama Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari na ambayo itakuwa na madaraka na mambo yasiyo ya Muungano kwa mujibu wa masharti ya Katiba yenyewe.

Swali ni je?
Kwa nini katika Katiba hakuna madaraka ya Serikali ya Tanganyika? Je kuna umuhimu wa kuanzisha Serikali hiyo?
Swali lingine ni je? Ni muhimu kuwa na Serikali za Majimbo ili kupunguza uwezekano wa kuwa na Serikali nyingine ya tatu yaani Tanganyika?

6.0 UHURU WA MAHAKAMA
       Sura ya tano ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, iliyorekebishwa,  2005 Ibara ya 107 (1) ya Katiba ya 1977,  2005 inaunda mamlaka ya kauli ya mwisho ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano kuwa ni Mahakama.

Ibara ya 107 (B) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inatamka kuwa Mahakama itakuwa huru katika utekelezaji wa shughuli zake kwa mujibu wa sheria na katiba za nchi.  Ambapo mwaka 2002 iliundwa sheria ya Uhuru wa Mahakama sheria namba 3 ya mwaka 2002.



Swali ni je?
Kweli Mahakama zetu zipo huru mbali na madaraka ya Rais wa nchi katika kutekeleza majukumu yake?

Ili kujibu swali hili lazima tuangalie maeneo yafuatayo
                         i.            Nani anamchagua Jaji Mkuu na Jaji Kiongozi?
                       ii.            Nani anachagua Majaji wa Mahakama Kuu?
                    iii.            Je anayewachagua anaweza kuwa chini ya maamuzi au hizo posti ziwe za ushindani kama walivyofanya Kenya?  Ibara ya 118 ya Katiba 1977, iliyorekebishwa, 2005.

7.0             HAKI ZA BINADAMU
                      i.            Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 14 – 24 ya katiba ya 1977, iliyorekebishwa mwaka 2005, inatoa haki za raia wa Tanzania.  Miongoni mwa ya haki hizo ni haki ya kuishi .
Swali ni je?
 wakati  Mahakama imepewa uwezo wa kutoa adhabu ya kifo.   Katiba inatoa haki ya kuishi je? Kunauwezekano wa kufuta adhabu ya kifo?
                   ii.            Katiba imetoa haki ya kumiliki mali kwa raia wa Tanzania lakini kuna baadhi ya mali huwezi kumiliki kama madini, mafuta na vito vya thamani kwa mujibu wa sheria ya Ardhi na madini.  Hivyo wakati upande mmoja unatoa upande mwingine unanyang’anya.

 Swali ni je?
 Ardhi na madini yaliyomilikiwa kiasili yawekewe dhamana ya fidia na umiliki kwa wanaokutwa katika eneo hilo? 
Ibara ya 8 ya katiba 1977, 2005 inasema Serikali inawekwa na wananchi kwa ajili ya rasilimali zao na lengo kuu ni ustawi wao.

8.0             MADARAKA YA SERIKALI ZA MITAA (LOCAL AUTHORITY)
Sura ya nne ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, iliyorekebishwa, 2005 inaunda serikali za mitaa na madaraka yake.  Ibara ya 145 (1) ya Katiba ya 2005, inatoa muundo wa Serikali ya Mitaa kila Mkoa, Wilaya, Miji, Kata ka Kijiji cha Tanzania.

Lengo la Serikali ya Mitaa ni ushirikishwaji wa madaraka katika maeneo yao hasa maamuzi ya maendeleo yao.

Swali ni je?
Kuna haja ya kuongeza madaraka hayo katika kukusanya mapato ya uzalishaji katika  maeneo yao? Mfano maeneo ambayo kuna  makaa ya mawe, dhahabu, chuma na madini mengine katika maeneo hayo asilimia ya kodi au mrahaba unabaki katika Serikali yao uelekezwe kwao ili kuleta mabadiliko katika eneo husika?

HITIMISHO
Tumejaribu kupitia maaeneo kadhaa ya Katiba yetu na kuona kama tunaweza kuyaangalia na kutolea mapendekezo bora zaidi.

Hivyo ni jukumu lako kutoa mapendekezo ya maboresho kuhusu Katiba mpya katika maeneo hayo tuliyoyapitia.  Lakini pia  ufungwi     kupanua wigo wako wa uelewa wa Katiba kwa kutoa maoni eneo lingine zaidi.

Asante kwa kunisikiliza.


WAKUU WA MIKOA INAYOLIMA KOROSHO KUANDAMANA KUMUONA RAIS JAKAYA KIKWETE

Na,Steven Augustino Tunduru

WAKUU wa Mikoa inayolima Korosho  nchini wameahidi kupeleka kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete kero ya ubabaishaji wa bei ya soko la zao hilo ili aweze kulitafutia ufumbuzi wa kudumu zikiwa ni juhudi za kuwawezesha Wakulima kupata matunda ya jasho lao.

Hayao yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma  Saidi Mwambungu wakati akiongea na wadau wa maendeleo waliojitokeza katika kikao cha dharula cha kujadili hatima ya tukio la ubabaisshaji wa soko la Korosho ambalo msimu huu bei yake imeonesha kusuasua kilichofanyika katika ukumbi wa Boma la halmashauri ya Wilaya hiyo mjini hapa .

Sambamba na maamuzi hayo pia Mwambungu na kamati hiyo ikatoka na azimio la kutouza Korosho hizo kwa Makampuni hayo babaishaji vinginevyo wakubali kununua Korosho hizo kwa Bei itakayo kubalika na wakatumia nafasi hiyo kumuomba Meneja wa Benki ya Nmb Omari Mleche kuongeza mkopo kwa vyama vya msingi ili kuwezesha kununua Korosho zote kwa wakulima wakati juhudi za kutafuta Soko la uhakika zikiendelea.

Akifafanua taarifa hiyo Mwambungu alisema kuwa maamuzi hayo yamefikiwa na Wakuu wa Mikoa ya Lindi Ruvuma na Mtwara baada ya kubaini kuwerpo kwa ubabaishaji wa Soko hilo ulio oneshwa na Wanunuzi hao wakubwa Korosho katika Msimu huu hauwezi kufumbiwa macho na Serikali na kuwaacha Wakulima wakiteseka bila msaada wa Serikali yao. 

Awali wakitoa taarifa ya ubabaishaji wa Soko la Mazao hayo Meneja wa Chama Kikuu cha Wakulima wa Korosho TAMCU Ltd  Imani Kalembo na Mwenyekiti wa  Chama hicho Mahamudu Katomondo walisema kuwa  ubabaishaji huo umeonekana katika minada mitatu iliyopita ambapo Makampuni ya Abbas Eport Treding Co.Ltd na Olam Co. Ltd awali wote waliomba kununua chini ya Bei  ya Tsh. 1500 kwa kilo moja hali iliyo onesha kuwa makampuni hayo yana ajenda ya siri ya kutaka chama hicho kishindwe kuwalipa Wakulima wake malipo yao ya awamu ya pili.

Walisema kinacho watia mashaka zaidi viongozi hao na kuwafanya wabaini uwepo wa mchezo mchafu kutoa katika Makampuni hayo ni kitendo cha Makampuni hayo pekee kati ya Makampuni 70 ambayo yalijiandikisha na kuomba kununua Korosho hizo katika Msimu huu wa Mwaka 2011/2012,

Wakizungumzia taarifa ya ununuzi Korosho hizo kutoka kwa wakulima walisema kuwa hadi sasa vyama vya msingi vya ushirika vime kwisha kusanya jumla ya Kilo 4,554334 kati ya Kilo 7,000,000 zinazotarajiwa kununuliwa katika Mismu huu na chama chao.

 Wakitoa maoni yao wabunge wa Wilaya ya Tunduru  Eng. Ramo Makani na Alhaji Mtutura Mtutura waliiomba Serikali kutumia Fedha zilizo idhinishwa katika Bajeti iliyopita kwa ajili ya Matumizi ya dhalula ili zitumike kununula Korosho hizo kutoka kwa Wakulima zikiwa ni juhudi za kuwaondolea adha hiyo.

Nao Madiwani Kazembe said  wa kata ya Ligunga na Burhani Nakanje wa Kata ya Marumba mbali na kuutuhumu uongozi wa Kiwanda cha Kubangulia Korosho kinacho milikiwa na Kampni ya Korosho Africa Ltd kuto kuwa na msaada kwa wakulima wa Wilaya yao waliiomba Serikali kuwa na macho na Wanunuzi hao vinginevyo watawaangusha na kuwafanya wananchi kukosa imani na Serikali yao.

Wakijibu tuhuma za Kiwanda hicho kuto kuwa na msaada kwa Wakulima wa zao hilo msimamizi wa Kiwanda hicho Dinesh Poojali na Enginia wa Kiwanda hicho Sivan Edayath mbali na kutoa taarifa kuwa kiwanda chao kimefungwa kutokana na kuishiwa Korosho za kubangua walisema kuwa wao hawana maamuzi yoyoyte juu ya ununuzi wa korosho hizo kutoka katika vyama vya ushirika vya msingi vya Wakulima wa Tunduru. 

Mwisho

MTANDAO WA SONNGO WAWAKUTANISHA WANANCHI WA KADA TOFAUTI KATIKA MDAHALO WA KUJADILI KATIBA YA MWAKA 1977


 Mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi zisizo za Kiserikali Wilaya ya Songea Siwaji Gama akifungua mdahalo,wa kwanza kushoto ni Afisa Habari wa Sonngo Endrwe Chatwanga,wa kwanza kulia ni Boniface Bundala, wa pili kulia ni Katibu wa Sonngo Mathew Ngarimanayo
 Washiriki wa mdahalo huo wakiendelea kusikiliza hoja mbalimbali zinazoendelea kuwasilishwa na jopo la wataalamu wa sheria na katiba
 Waandishi wa Habari wakisikiliza majadiliano katika mdahalo huo,kutoka kushoto ni Catherine Nyoni (Tbc) Amon Mtega(Mtanzania) Gideon Mwakanosya(Nipashe) Joseph Mwambije(Majira)

Washiriki wakisikiliza kwa umakini mapitio na uchambuzi wa wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 Jimbo la Songea Mjini

Tuesday, December 27, 2011

WADAU WA MTANDAO HUU WAMWEMELEKA KWENYE KUMBUKIZI ZA KUZALIWA KWA MDAU MWENZAO WA MTANDAO EMMANUEL NTOBI

 Keki iliyotengenezwa kwa ubora wenye viwango stahiki maalumu kwa kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwa Emmanuel Ntobi

Emmanue Ntobi akijiandaa kuwasha baruti huku akishuhudiwa na Mpenzi wake Bi Sarah Mohamed




 Emmanuel Ntobi akimrisha keki ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwake mpenzi wake Bi, Sarah Mohamed
 Emmanuel Ntobi akimrisha keki Mr Ng'aida kwenye sherehe hiyo

 Mdau wa Mtandao huu Stephano Mango akipata keki tamu iliyoandaliwa kwa ajili ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Emmanuel Ntobi wakati wa sherehe hiyo ya aina yake iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Benki ya biashara ya NBC juzi usiku muda mfupi kabla Bwana wetu yesu Kristu ajazaliwa ndio maana Ntobi Emmanuel alibatizwa jina hilo likiwa na maana ya Bwana pamoja nasi 






Wadau mbalimbali wakiendelea kupata chakula na vinywaji vya aina mbalimbali kwenye sherehe hiyo iliyofana

MUUGUZI WA KIJIJI CHA MANGO AJINYONGA KUTOKANA NA WIVU WA KIMAPENZI

                                              
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda
Na Gideon Mwakanosya ,Songea
MUUGUZI wa Zahanati ya kijiji cha Mango kilichopo kata ya Kihagara wilayani Mbinga Bosco Nchimbi (29) amekutwa  kwenye kenchi ya chumba chake akiwa amekufa baada ya kujinyonga  kwa kujitundika  juu ya kenchi kwa kutumia kamba ya katani.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda amesema kuwa tukio hilo limetokea juzi majira ya saa kumi jioni  huko katika kijiji cha Mango , ambapo katekista wa kijiji cha Tumbi  Joseph Nchimbi ndiye aliyegundua   kuwepo kwa tukio la kujinyonga Nchimbi .
Amefafanua kuwa, Inadaiwa siku ya tukio kateksta Nchimbi alikuwa ameenda nyumbani kwa Marehemu  kwa ajili ya kumpa ushauri  baada ya kuwepo malumbano  kati yake na Mwanamke aliyezaa naye mtoto  anayedaiwa kuwa alikuwa akilalamikiwa kuwa ameanza kufanya ngono na wanaume wengine wakati mtoto wao bado ni mchanga.
Kamanda alieleza zaidi kuwa Katekista Nchimbi  baada ya kugundua  tukio hilo  alitoa taarifa kwa uongozi wa serikali ya kijiji cha Mango  ambao nao ulitoa taarifa polisi  na askari polisi walipofika katika eneo la tukio wakiwa wameongoozana na Mganga walikuta mwili wa marehemu  ukiwa unaninginia  .
Kamanda amesema,chanzo cha kujinyonga ni wivu wa mapenzi   kati yake na mwanamke aliyezaa naye ambaye wakati wote alikuwa akimuonya kuacha tabia ya kufanya mapenzi na wanaume ovyo kwani anamuaharibu mtoto  wao mchanga lakini mwanamke huyo aliendelea hali iliyosababisha apandwe na hasira na kuchukua huamuzi huo.
MWISHO.

Monday, December 26, 2011

Nawatakia Sikukuu njema za X-MASS,BOXING DAY,na MWAKA MPYA wa 2012 wenye Baraka na mafanikio makubwa


Nawasalimu wadau wote wa mtandao wa www.stephanomango.blogspot.comkwa kunipa ushirikiano wenu katika kipindi chote cha mwaka 2011

Nawatakia heri sana katika msimu huu wa mwishoni mwa mwaka 2011 na maandalizi mema ya mwaka mpya wa 2012





God is Love

Christmas is all about love

Christmas is thus about God and Love

Love is the key to peace among all mankind

Love is the key to peace and happiness within all creation

Love needs to be practiced - love needs to flow - love needs to make happy

Love starts with your partner, children and family and expands to all world

God bless all mankind

VIONGOZI NCHINI WATAKIWA KUWATUMIKIA WANANCHI ILI KULINDA AMANI YA NCHI

Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Songea Norbert Mtega
 
Na, Augustino Chindiye Tunduru

VIONGOZI wa kuchaguliwa na waliopewa mamlaka ya kulitumikia Taifa wameombwa kuitumikia Jamii kwa uadilifu ili kuendelea kudumisha amani na utulivu vinginevyo kuna hatari ya amani hiyo inayojivuniwa na taifa letu kutoweka.

Rai hiyo imetolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo la TUNDURU- Masasi Castory Msemwa wakati akiongea na waamini waliohudhulia katika Misa takatifu ya kukumbuka kuzaliwa Yesu Kristo ya Noeli iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Xavery mjini hapa.

Akifafanua taarifa hiyo kupitia Mahubiri hayo Askofu Msemwa alisema kuwa pamoja na Viongozi hao kufahamu hayo lakini wamekuwa walafi hali ambayo imekuwa ikiwasukuma kuwatesa Wananchi waliowapa nyadhifa hizo .

Alisema mbali na hali hiyo kuonekana wazi kwa Viongozi wa Serikali lakini pia matukio kama hayo yamekuwa yakiwakumba viongozi wa Dini ambapo wamekuwa wakipenda kujinufasha ili waendeelee kuongeza furaha mioyoni mwao kwa kujipangia marupurupu yao wenyewe bila kuwajali wengine na kuiacha jamii ikiteseka bila misaada yao.

Askofu Msemwa akatumia nafasi hiyo kuhimiza upendo miongoni mwetu na kueleza kuwa endapo upendo utaendelea kutoweka kuna hatari ya amani tunayo jivunia kumomonyoka na kuipeleka nchi yetu pabaya.

Katika hutuba hiyo pia Askofu Msemwa akaikumbusha jamii kuiga mwenendo wa mwasisi wa Taifa la Watanzania Mwenyeheri Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mtumishi wa Mungu Sister Bernadeta wa Jimbo la Perahimo ambaye amekuwa gumzo kubwa kutokana na watu wengi kwenda kuomba katika kaburi lake na kufanikiwa.

Alisema Sister Bernadeta alitangazwa hivi karibuni kuwa mtumishi wa Mungu ukiwa ni mchakato wa kufikia nafasi ya Mwenyeheri na kongeza kuwa mapendo ya kweli katika jamii yao ndiyo yaliyowafanya waendelee kukumbwa na jamii yao .

Mwisho