Kushoto ni Mwandishi wa Radio Maria Songea,Julius Konala,Mwandishi wa Gazeti la Majira Crecensia Kapinga
Mtaalamu wa ICT wa Asasi ya Sonngo Boniface Bundala akifuatilia Mdahalo wa wananchi wa Jimbo la Songea unaofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Ualimu Songea
Washiriki wakiendelea kufuatilia Mdahalo huo
Wa kwanza kutoka kushoto Dereva wa Sonngo Bucard Mkuwa (Maarufu kwa jina la SHILINGI) wa pili ni Mtoa huduma wa watoto HBC wa Asasi ya Roa na Mwanaharakati na Mtaalamu wa Zana za Kilimo Wilaya ya Songea Venas Komba,wa tatu ni Mkurugenzi wa Asasi Rumed David Kakoyo
Wa kwanza kutoka kulia ni Katibu Muhtasi (Msaidizi wa Ofisi) wa Sonngo Sophia Limbuya akizungumza jambo na Mtaalum wa ICT wa Asasi ya Sonngo Boniface Bundala
Friday, January 27, 2012
WANANCHI JIMBO LA SONGEA MJINI WAANZA MDAHALO WA WAZI WENYE LENGO LA KUPATA TASWIRA YA UWAJIBIKAJI WA VIONGOZI KWA WANANCHI WAO
| Kutoka kushoto Afisa Kazi Ruvuma Oddo Hekela,Diwani wa Kata ya Matarawe James Makane,Diwani wa Viti maalum Genfrida Haule |
ABAKWA NA WATU WATANO NA KUMSABABISHIA KIFO
Na Gideon Mwakanosya,Songea
JESHI la Polisi mkoani Ruvuma linawasaka watu watano wasiofahamika wakazi wa eneo la Lilambo Manispaa ya Songea kwa tuhuma za kuvamia na kuingia ndani ya nyumba kisha kumbaka Mwanamke mwenye umri wa miaka 20 kwa kupokezana wakati akiwa amelala na kumsababishia Kifo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma Michael Kamuhanda alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa nne usiku kata ya Lilambo nje kidogo ya mji wa Songea.
Amesema,Inadaiwa siku ya tukio majira ya saa nne usiku watuhumiwa hao walifanya kitendo hicho cha kinyama na kumsababishia maumivu makali sehemu nyeti marehemu ambaye hata hivyo jina lake limehifadhiwa .
Ameeleza zaidi kuwa watuhumiwa hao inadaiwa baada ya kumfanyia kitendo cha unyama mwanamke huyo walimchukua toka nyumbani kwake na kwenda kumtupa nje ya nyumba kwenye shamba la migomba ambapo watu waliokuwa wakipita kwenye eneo hilo walishituka kuona mwili wa marehemu ukiwa umelazwa katika shamba hilo.
Amefafanua zaidi kuwa mara baada ya wananchi wa kata hiyo kuona mwili huo walitoa taarifa kwa viongozi wa serikali ya kata ambao ndio waliotoa taarifa kwenye kituo kikuu cha polisi cha Songea , na kuwa askari polisi wakiwa wameongozana na daktari walifika katika eneo la tukio na kuuchukua kwa ajili ya uchunguzi zaidi ambapo waligundua kuwa sehemu zake za siri zinamchubuko.
Kamanda Kamuhand amesema kuwa wakati Polisi wanaendelea kuwasaka watuhumiwa bado inaendelea kufanya uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo.
Mwisho.
Wednesday, January 25, 2012
WAZAZI WAKIWA KUFUATILIA MAENDELEO YA ELIMU YA MTOTO WA KIKE
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Madaha
Na Augustino Chindiye,Tunduru
SERIKALI imewataka Wazazi na Walezi kusimamia na kufuatilia kwa karibu maendeleo ya Watoto wao hasa wa kike zikiwa ni juhudi za kuhakikisha kuwa watoto hao wanafanya vizuri katika masomo yao na kujiletea maendeleo yao.
Wito huo umetolewa kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma
Madaha na kaimu Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Manfred Hyera wakati akiongea na Wadau wa elimu waliohudhuria katika mafunzo
ya uzinduzi wa Mradi wa Usimamizi na Utetezi wa Haki ya Mtoto wa kike kupata elimu yaliyofanyika katika ukumbi wa Skyway mjini hapa.
Alisema ili kufanikisha hali hiyo serikali imejipanga kutoa elimu kwa kuwaomba wazazi na walezi kuchangia chakula ili kufanikisha watoto wao kuanza kupata chakula mashuleni kama kivutio kwa wanafunzi kupenda masomo.
Akizungumzia mila na destuli za makabila ya Wayao alisema kuwa tayari serikali imeunda kikosi kazi cha kuonana na viongozi wa mila, makungwi na manyakanga kuwaelimisha juu ya utoaji wa elimu kwa watoto wa kike kupenda masomo tofauti na sasa ambapo kundi hilo limekuwa likifundishwa kukabiliana na maisha ya ndoa hali iliyo sababisha kuwepo kwa matukio mengi ya ndoa za utotoni wakiwa shuleni.
Wakiongea kwa nyakaka tofauti baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo Hadija Hasan na Amina Mwajesa katika maoni yao juu ya kinachosababisha elimu kushuka Wilayani humo walidai kuwa Kipato duni cha akina mama ambao mara nyingi ndio wamekuwa wakiachiwa jukumu la kutunza Watoto wa kike .
Kuhusu mila na desturi za makabila hayo washiriki hao waliiomba
Serikali kuchukua hatua za makusudi kusimamia na kutokomeza mila hizo hasa mafunzo mabaya ambayo hutolewa wakati wa jando na unyago pamoja na kuwataka akina mama kuacha tabia za kutunza siri za watoto wao wa kike.
Akisoma risala ya mafunzo hayo Mwakilishi kutoka shirika lisilokuwa la kiserikali la TUFAE Educcation Aids Trust linalo ratibu mafunzo hayo Hakimu Kilowa alisema kuwa mafunzo hayo yamefuatia majibu mabaya baada ya utafiti uliofanywa na shirika hilo mwaka 2007 hadi 2010 juu ya maendeleo ya elimu kwa mtoto wa kike wilayani humo.
Kilowa alisema katika utafiti huo uliofanyika katika Tarafa za
Muhuwesi,Namasakata,Ligoma,Nandembo,Mlingoti Mashariki na Mlingoti Magharibi zilibainisha kuwapo kwa kundi kubwa la watoto wa kike waliopata mimba pamoja na kikwazo cha uelewa mdogo wa jamii juu ya SERA ya Elimu,Haki ya mtoto wa kike kupata Elimu,Mila zilizopitwa na wakati.
Alisema Takwimu hizo zilifafanua kuwa katika kipindi cha Mwaka
2007-2010 jumla ya waliotarajiwa kuandikishwa shule ni watoto wa kike 17,386, walioandikishwa ni 14,692 ambao ni Sawa na asilimia 85.49% na waliosajiliwa ni 13,411,waliofanya mitihani wa kumaliza darasa la saba walikuwa 13,097 ambao ni sawa na asilimia 97.65%, huku kukiwa na anguko la watoto 314 ambao waliacha shule kwa sababu mbalimbali ikiwemo kupata mimba wakiwa shuleni pamoja na utoro.
Awali akitoa ufafanuzi wa mafunzo hayo Meneje wa Mradi wa shirika hilo John Nginga katika maelezo yake alisema kuwa lengo la mradi huo ni kuhakikisha kuwa mtoto wa kike anapata elimu kuanzia darasa la awali, elimu ya msingi, sekondari hadi Chuo Kikuu.
Mafunzo hayo ya siku 15 yanayofadhiliwa na Shirika la The Foundation for Civi Society (FCS) la Jijini Dar Es Salaam yatahusisha wadau 180 kutoka katika makundi ya Walemavu,walimu, wazee,Viongozi wa Vyama vya Siasa, Dini,Watendaji Kata na Vijiji kutoka katika Kata Sita hizo kwa ajili ya kupeana mbinu na kubainisha changamoto zinazotokana na vikwazo vya Mtoto wa kike kupata Elimu badala ya kuwa ozesha wakiwa
wadogo.
Mwisho.
SERIKALI imewataka Wazazi na Walezi kusimamia na kufuatilia kwa karibu maendeleo ya Watoto wao hasa wa kike zikiwa ni juhudi za kuhakikisha kuwa watoto hao wanafanya vizuri katika masomo yao na kujiletea maendeleo yao.
Wito huo umetolewa kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma
Madaha na kaimu Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Manfred Hyera wakati akiongea na Wadau wa elimu waliohudhuria katika mafunzo
ya uzinduzi wa Mradi wa Usimamizi na Utetezi wa Haki ya Mtoto wa kike kupata elimu yaliyofanyika katika ukumbi wa Skyway mjini hapa.
Alisema ili kufanikisha hali hiyo serikali imejipanga kutoa elimu kwa kuwaomba wazazi na walezi kuchangia chakula ili kufanikisha watoto wao kuanza kupata chakula mashuleni kama kivutio kwa wanafunzi kupenda masomo.
Akizungumzia mila na destuli za makabila ya Wayao alisema kuwa tayari serikali imeunda kikosi kazi cha kuonana na viongozi wa mila, makungwi na manyakanga kuwaelimisha juu ya utoaji wa elimu kwa watoto wa kike kupenda masomo tofauti na sasa ambapo kundi hilo limekuwa likifundishwa kukabiliana na maisha ya ndoa hali iliyo sababisha kuwepo kwa matukio mengi ya ndoa za utotoni wakiwa shuleni.
Wakiongea kwa nyakaka tofauti baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo Hadija Hasan na Amina Mwajesa katika maoni yao juu ya kinachosababisha elimu kushuka Wilayani humo walidai kuwa Kipato duni cha akina mama ambao mara nyingi ndio wamekuwa wakiachiwa jukumu la kutunza Watoto wa kike .
Kuhusu mila na desturi za makabila hayo washiriki hao waliiomba
Serikali kuchukua hatua za makusudi kusimamia na kutokomeza mila hizo hasa mafunzo mabaya ambayo hutolewa wakati wa jando na unyago pamoja na kuwataka akina mama kuacha tabia za kutunza siri za watoto wao wa kike.
Akisoma risala ya mafunzo hayo Mwakilishi kutoka shirika lisilokuwa la kiserikali la TUFAE Educcation Aids Trust linalo ratibu mafunzo hayo Hakimu Kilowa alisema kuwa mafunzo hayo yamefuatia majibu mabaya baada ya utafiti uliofanywa na shirika hilo mwaka 2007 hadi 2010 juu ya maendeleo ya elimu kwa mtoto wa kike wilayani humo.
Kilowa alisema katika utafiti huo uliofanyika katika Tarafa za
Muhuwesi,Namasakata,Ligoma,Nandembo,Mlingoti Mashariki na Mlingoti Magharibi zilibainisha kuwapo kwa kundi kubwa la watoto wa kike waliopata mimba pamoja na kikwazo cha uelewa mdogo wa jamii juu ya SERA ya Elimu,Haki ya mtoto wa kike kupata Elimu,Mila zilizopitwa na wakati.
Alisema Takwimu hizo zilifafanua kuwa katika kipindi cha Mwaka
2007-2010 jumla ya waliotarajiwa kuandikishwa shule ni watoto wa kike 17,386, walioandikishwa ni 14,692 ambao ni Sawa na asilimia 85.49% na waliosajiliwa ni 13,411,waliofanya mitihani wa kumaliza darasa la saba walikuwa 13,097 ambao ni sawa na asilimia 97.65%, huku kukiwa na anguko la watoto 314 ambao waliacha shule kwa sababu mbalimbali ikiwemo kupata mimba wakiwa shuleni pamoja na utoro.
Awali akitoa ufafanuzi wa mafunzo hayo Meneje wa Mradi wa shirika hilo John Nginga katika maelezo yake alisema kuwa lengo la mradi huo ni kuhakikisha kuwa mtoto wa kike anapata elimu kuanzia darasa la awali, elimu ya msingi, sekondari hadi Chuo Kikuu.
Mafunzo hayo ya siku 15 yanayofadhiliwa na Shirika la The Foundation for Civi Society (FCS) la Jijini Dar Es Salaam yatahusisha wadau 180 kutoka katika makundi ya Walemavu,walimu, wazee,Viongozi wa Vyama vya Siasa, Dini,Watendaji Kata na Vijiji kutoka katika Kata Sita hizo kwa ajili ya kupeana mbinu na kubainisha changamoto zinazotokana na vikwazo vya Mtoto wa kike kupata Elimu badala ya kuwa ozesha wakiwa
wadogo.
Mwisho.
Tuesday, January 24, 2012
WASAFIRISHAJI WA MIZIGO WAULALAMIKIA UONGOZI WA MANISPAA SONGEA
Na Stephano Mango,Songea
WASAFIRISHAJI wa mizigo wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wameulalamikia uongozi wa Manispaa hiyo kwa kitendo cha kuwazuia kuingia na magari ya mizigo katikati ya mji wafanyabiashara wachache huku wengine wakiingia na magari ya mizigo bila kuchukuliwa hatua yoyote
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari jana mjini hapa,wasafirishaji hao ambao waliomba majina yao yahifadhiwe,walisema kuwa kitendo kinachofanywa na Uongozi wa Manispaa ni cha uonevu kwa sababu wamewazuia kuingia na magari katikati ya mji bila kuwatengea maeneo mengine yenye miundombinu mizuri ya maji,choo,ofisi na umeme
Walisema kuwa wasafirishaji wengi wana ofisi zao katikati ya mji ambazo zinahuduma zote muhimu ambapo uwepo wake unawasaidia wateja wao kuweza kuchukua mizigo yao kwa urahisi na kwa bei ndogo hivyo uwepo wa ofisi mbali kinawaletea usumbufu wananchi ambao ni wateja muhimu kwao
Walieleza kuwa pamoja na kupokea maelekezo ya Viongozi wa Manispaa kuwa magari yanayotakiwa kuingia mjini yasizidi tani 10 lakini kuna baadhi ya magari yanaingia na hayachukuliwi hatua yoyote na maagizo ya Viongozi hao yanabadilika kila wanavyoamua bila kujali usumbufu unaojitokeza kwani awali walituambia gari za tani 10 ndizo zinazopaswa kuingia mjini lakini baada ya wiki moja kwisha wanatuambia gari za 9 ndizo zinapaswa kuingia mjini
Walisema kuwa kutokana na usumbufu huo Wasafirishaji wanalazimika kupandisha bei ya kusafirisha mizigo na kusababisha wananchi kupandishiwa bei ya bidhaa kwani kila inachokifanya Serikali dhidi ya wafanyabiasha mwisho wa siku gharama hizo zote zinapaswa kulipwa na mwananchi mnyonge na kusababisha gharama za maisha kupanda sana
Walieleza zaidi kuwa miji mingine yote nchini gari zinaingia mwisho gari za tani 10 ili kuweza kulinda barabara za ndani ya mji na kupunguza msongamano katikati ya mji lakini hapa tunashangaa kuambiwa kuwa gari zinazotakiwa kuingia mjini mwisho za tani 9 tena ziingie usiku wakati gari hizo hazipo
Walifafanua kuwa wameelekezwa kuanzia disemba 31 mwaka 2011 walitakiwa kutoingia kwenye barabara za mjini badala yake waishie na kushusha mizigo kwenye uwanja wa nanenane na sio vinginevyo wakati eneo hilo ni uwanja uwezi kujenga choo,hakuna huduma ya umeme,ofisi za wasafirishaji ,maji,chakula hivyo wametupatia wakati mgumu sana wa kuitunza mizigo ya watu na utunzaji wa mazingira
Walisema kuwa maagizo ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea yamejaa utata hata wanaopaswa kusimamia maagizo yake wamekuwa wakishindwa kuyazuia magari yote kuingia katikati ya mji na ndio maana magari mengine yamekuwa yakipita bila maelezo yoyote kutokana na udhaifu wa viongozi hao
Awali kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa Nachoa Zakaria,Afisa Biashara wa Manispaa hiyo Kelvin Challe aliwaandikia barua tarehe 12 Disemba,2011 wasafirishaji yenye kumb,na,SO/MC/T.10/14/11 kuhusu kusitisha kuingia magari ya mizigo yanayozidi tani 10 ndani ya barabara za Manispaa kuanzia Disemba 31,2011
Baada ya agizo hilo kuhojiwa na Wasafirishaji kutokana na kugubikwa na utata Uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea tarehe 9 Januari 2011, iliwaandikia tena wasafirishaji barua na kusaini na Kelvin Challe yenye Kumb.Na.SO/MC/T.10/14/11/17 yenye kichwa cha habari Ufafanuzi wa kina juu ya zoezi la kusitisha kuingiza magari ya mizigo kuanzia tani 10 ndani ya barabara za Manispaa Songea Kuanzia tarehe 31/12/2011
Sehemu ya barua hiyo inasema…..magari yanayoruhusiwa ni magari yenye uzito wa kuanzia tani 9 tu.Magari yenye uzito zaidi ya tani 9 yanatakiwa kushusha mizigo katika uwanja wa nanenane,hivyo unatakiwa kuzingatia na kutekeleza maamuzi hayo
Jitihada za kumpata Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea aweze kujibu malalamiko ya wasafirishaji Nachoa Zakaria ziligonga mwamba baada ya kuambiwa na mhudumu wa Ofisi yake kuwa yupo kwenye vikao ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na alipotafutwa kwenye simu yake ya kiganjani,simu iliita bila kupokelewa
MWISHO
Monday, January 23, 2012
WASHAURIWA KUTOJITOA KWENYE TAASISI ZA FEDHA WAKATI WA MTIKISIKO WA KIUCHUMI WA VYAMA HIVYO
Na Stephano Mango,Songea
WANACHAMA wa Chama Cha ushirika cha Akiba na Mikopo cha walimu Songea Manispaaa wameshauriwa kuacha tabia ya kujitoa uanachama kutokana na kukosa uvumilivu baada ya mikopo yao kuchelewa kutolewa kwa wakati au wanapokosa mikopo na badala yake wametakiwa kuwa wavumilivu.
Wito huo umetolewa jana na Meneja mikopo wa benki ya NMB tawi la Songea Derick Fidelis wakati akifungua mkutano mkuu wa 14 wa wanachama wa chama hicho uliofanyika kwenye ukumbi wa Songea Club.
Amesema,Wanachama wanapaswa kuwa wavumilivu na si kukimbilia kujitoa pindi mikopo waliyoomba kutoipata kwa wakati na badala yake wajue kuwa matatizo hayo ni ya kawaida hivyo wasikate tamaa wala kukimbia matatizo.
“Walimu tunapaswa kuwa wavumilivu tuache tabia ya kujitoa uanachama pindi tunapokosa mikopo au kucheleweshewa mikopo , tuwe wavumilivu matatizo ni jambo la kawaida ,nyinyi ni wadau wa kubwa wa NMB ili benki iendelee tunawategemea sana kwani mapato mengi ambayo yanaingia benki yanatokana na michango ya walimu,na mikopo mingi tunawakopesha walimu,”alisema Derick.
Aidha, Meneja mikopo ameahidi kuwa benki hiyo itaendelea kuboresha huduma zaidi ili kufanikisha malengo ambayo wateja wao wakiwemo walimu wanahitaji , ameishauri bodi ya chama hicho kukaa na kuomba mkopo ili kuweza kumalizia jengo lao ili kuinua uchumi wa chama hicho.
Akitoa salamu wakati wa mkutano huo Mwenyekiti wa chama hicho Martin Challe amewataka wanachama hao kuendelea kuwa wajasili na kutokubali kuyumbishwa au kushawishiwa kujitoa uanachama na watu ambao wasiopenda na ustawi na maendeleo ya chama hicho.
“Tayari kunawachama ambao wamejitoa ukiuliza wanadai kuwa kwa sababu uchumi wa chama siyo mzuri na kuchelewa kupata mikopo waliporudi kuomba tena uanachama nasi tumewakataa kwani walikimbia baada ya kuona tumeyumba,”alisema.
Mwisho.
Sunday, January 22, 2012
WATAKIWA KUWAPIMA WABUNGE WAO KWA USHIRIKISHAJI WA WANANCHI
Afisa Kazi Ruvuma Oddo Hekela
Na Stephano Mango,Songea
WANANCHI wametakiwa kuwapima Wabunge na Madiwani wao ili kuweza kubaini ubora wao katika ushirikishaji wa wananchi katika eneo lake la uongozi katika kuleta maendeleo ya nchi kwa kutumia dhana shirikishi
Wito huo umetolewa jana na Afisa Kazi Ruvuma Oddo Hekela kwenye mdahalo wa wazi wenye lengo la kupata taswira ya uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi wao ulioitishwa na Mtandao wa Asasi za Kiraia Wilaya ya Songea(Sonngo)kwa ufadhiri wa Shirika la The Foundation For Civil Society
Hekela alisema kuwa Mbunge na Diwani wote ni wawakilishi katika eneo lao la kazi ambao wamebeba jukumu la kuhamasisha wananchi katika kutekeleza majukumu ya maendeleo hivyo ushirikishwaji bora ndio maendeleo bora
Alisema kuwa ili kupima ubora wa Mbunge na Diwani lazima upime uwezo wa ushirikishwaji wa wananchi katika eneo lake ili kuweza kuleta maendeleo ya nchi kwani wote ni wawakilishi wa wananchi katika Serikali ya watu hivyo wajibu wao unafanana
Alieleza kuwa miongoni mwa majukumu ya Mbunge akiwa jimboni ni kukaa ofisini na kuhudumia wananchi kwa kusikiliza hoja zao ili aweze kuzitatua au kuzipeleka sehemu husika kwa hatua zaidi,kufanya ziara kwa wananchi ili kuweza kujua mikakati ya maendeleo,kufuatilia utekelezaji wa miradi ya kitaifa jimboni kwake inayotekelezwa na Serikali kuu kusikiliza maoni ya wananchi kuhusiana na utekelezaji wa miradi hiyo
Alieleza zaidi kuwa majukumu yake mingine akiwa jimboni ni pamoja na kusimamia utekelezaji wa sera mbalimbali kwa kutoa tafsiri ya sera zenyewe ili wananchi wazielewe,kutoa elimu na kuwahamasisha wananchi ushiriki wao katika miradi ya maendeleo
Kwa upande wake Katibu wa Mtandao wa Sonngo Mathew Ngarimanayo alisema kuwa Viongozi wanapaswa kutimiza wajibu wao kikamilifu katika kuhakikisha Sera mbalimbali zinawanufaisha wananchi ili kuweza kupunguza umaskini wa kipato unaowakabili na kuweza kuchangia pato la Taifa
Ngarimanayo alieleza kuwa ni jambo la aibu kuona Mbunge anazunguka mjini huku wapiga kura wake wanahangaika kutokana na sera mbalimbali kutokuwa wazi na wakati mwingine kushindwa kumnufaisha mwananchi kutokana na kuwa katika mazingira magumu ya upatikanaji wake na zimewekwa katika lugha ambayo mwananchi mnyonge hawawezi kuielewa
MWISHO
WAZIRI MAGHEMBE ATAKIWA KUTEMBELEA MIKOA INAYOZALISHA MAZAO YA CHAKULA
Ukiwaona kwa mara ya kwanza unaweza kusema ni vijana wa familia moja(Baba mmoja) lakini hawa sio ndugu ila ni Wanaharakati wakubwa wa Haki za Binadamu katika Mkoa wa Ruvuma
Picha hii walipiga nje ya ukumbi wa mdahalo uliofanyika katika Wilaya ya Songea,Jimbo la Peramiho,Kata ya Mtyangimbole mara baada ya kumalizika kwa mdahalo huo ikiwa ni furaha ya kumalizika kwa mdahalo huo kwa upendo na amani
Hawa vijana wana vyeo vingi sana katika jamii,lakini kwa eneo hili na madhumuni ya picha hii kila mmoja atakuwa na cheo kimoja kilichowakutanisha hapo
Kutoka kushoto ni Katibu wa Mtandao wa Asasi za Kiraia Wilaya ya Songea (Sonngo) Mathew Ngarimanayo,wa kwanza kulia na Afisa Habari wa Mtandao wa Asasi za Kiraia Wilaya ya Songea(Sonngo) Andrew Chatwanga
Mmiliki wa Mtandao huu,Stephano Mango akiendelea kuhabarisha umma katika mdahalo huo,wa pili toka kulia ni Mwanafunzi wa Chuo cha Ustawi na maendeleo ya Jamii Rungemba Mariana Nyoni,wa tatu ni Msaidizi wa Ofisi ya Sonngo Sophia Limbuya
Picha hii walipiga nje ya ukumbi wa mdahalo uliofanyika katika Wilaya ya Songea,Jimbo la Peramiho,Kata ya Mtyangimbole mara baada ya kumalizika kwa mdahalo huo ikiwa ni furaha ya kumalizika kwa mdahalo huo kwa upendo na amani
Hawa vijana wana vyeo vingi sana katika jamii,lakini kwa eneo hili na madhumuni ya picha hii kila mmoja atakuwa na cheo kimoja kilichowakutanisha hapo
Kutoka kushoto ni Katibu wa Mtandao wa Asasi za Kiraia Wilaya ya Songea (Sonngo) Mathew Ngarimanayo,wa kwanza kulia na Afisa Habari wa Mtandao wa Asasi za Kiraia Wilaya ya Songea(Sonngo) Andrew Chatwanga
Mmiliki wa Mtandao huu,Stephano Mango akiendelea kuhabarisha umma katika mdahalo huo,wa pili toka kulia ni Mwanafunzi wa Chuo cha Ustawi na maendeleo ya Jamii Rungemba Mariana Nyoni,wa tatu ni Msaidizi wa Ofisi ya Sonngo Sophia Limbuya
Na Stephano Mango,Songea
WANANCHI wa kata ya Mtyangimbole wilaya ya Songea mkoani Ruvuma wamemtaka Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika Profesa Jumanne Maghembe kuona umuhimu wa kutembelea mikoa inayozalisha mazao ya chakula ili kuweza kutatua changamoto zinazowakabili katika msimu huu wa kilimo ili kuweza kupunguza uhaba wa chakula nchini
Wito huo umetolewa jana na Diwani wa Kata ya Mtyangimbole Meckezedeck Mwella kwenye mdahalo wa wazi wenye lengo la kupata taswira ya uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi wao ulioitishwa na Mtandao wa Asasi za Kiraia Wilaya ya Songea(SONNGO kwa ufadhiri wa Shirika la The Foundation For Civil Society
Mwella alisema kuwa Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa mitano inayoongoza kwa uzalishaji wa mazao ya chakula kama mahindi,mihogo lakini wananchi wake wamekuwa wakiendelea kukwamisha na mipango mbalimbali ya Serikali yenye malengo ya kuinua kilimo
Alisema kuwa wananchi wengi wamekuwa wakilalamikia mfumo mbovu wa ugawaji wa pembejeo za ruzuku zinazotolewa na Serikali kwa lengo la kuwainua wakulima kutokana na urasimu mkubwa unaojitokeza kuanzia ngazi ya mtaa hadi Wilaya na kusababisha kero kubwa kwa wakulima hao
Alieleza kuwa siku zote mkulima hana likizo kwani kwa kipindi chote cha mwaka yeye anahangaika na shughuli za kilimo lakini amekuwa ni maskini wa kutupwa kutokana na uzembe toka kwa viongozi wa Serikali ambao wamekosa huruma dhidi ya wakulima kwa kuwanyonya haki zao mbalimbali
Alieleza zaidi kuwa kitendo cha Serikali kushindwa kununua mahindi toka kwa mkulima msimu wa 2011/2012 na kusababisha mahindi hayo kuanza kuota yakiwa kwenye magunia maeneo mbalimbali ya maghala ni cha uonevu mkubwa kwani wakulima wengi wamekata tamaa kutokana na madeni mbalimbali yanayowakabili kutokana na uzalishaji walioufanya katika msimu uliopita
“Wakulima walitegemea kuwa msimu wa uuzaji wa mahindi wangeweza kupata fedha kwa ajili ya kuandaa msimu mwingine wa kilimo,kulipia karo za watoto,kupata mahitaji muhimu ya kibinadamu,na kulipia huduma mbalimbali za kijamii lakini imeshindikana kutokana na mipango mibovu ya Serikali kuhusu kumkomboa mkulima kwenye upatikanaji wa masoko ya uhakika wa mazao hayo”alisema Mwella
Akizungumza kwenye Mdahalo huo Katibu wa Sonngo Mathew Ngarimanayo alisema kuwa Viongozi wanapaswa kutimiza wajibu wao kikamilifu katika kuhakikisha Sera za kilimo,ushirika na masoko zinawanufaisha wakulima ili kuweza kupunguza umaskini wa kipato unaowakabili na kuweza kuchangia pato la Taifa
Ngarimanayo alisema kuwa katika kipindi hiki cha msimu wa kilimo Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika, maafisa kilimo wa ngazi zote wanapaswa wawatembelea wakulima kwenye maeneo yao ili kuweza kubaini vikwazo mbalimbali wanavyokutana navyo wakulima katika msimu wa kilimo badala ya kukaa ofisini wakisubiri taarifa potofu toka kwa wasaidizi wao
Alieleza kuwa ni jambo la aibu kuona Mbunge anazunguka mjini huku wapiga kura wake wanahangaika na kilimo kwa kutumia dhana duni zisizokidhi viwango vya uzalishaji wa mazao kwa wengi bila kusaidiwa na wataalamu wa kilimo na kusababisha uzalishaji kupungua kutokana na kutumia pembejeo duni
Awali Mwenyekiti wa mtandao wa Asasi zisizokuwa za Kiserikali Wilaya ya Songea (Sonngo)Siwajibu Gama akifungua mdahalo huo alisema kuwa lengo la mdahalo huo ni kuwawezesha wananchi kutambua wajibu wao na kuelewa wajibu wa viongozi wao ili waweze kukaa pamoja,kupanga na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa pamoja
MWISHO
MDAHALO WA WAZI KUHUSU KUIMARISHA MAHUSIANO KATI YA WABUNGE NA WANANCHI WAO WAMALIZIKA
Viongozi wa Asasi ya Sonngo na Viongozi wa Serikali wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea wakiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mdahalo huo mara baada ya kumalizika
Saturday, January 21, 2012
SONNGO WAWAKUTANISHA WANANCHI WA MTYANGIMBOLE KWENYE MDAHALO WA WAZI KUHUSU KUIMARISHA MAHUSIANO KATI YA WABUNGE NA WANANCHI WAO
Kutoka kulia ni Afisa Maendeleo ya Jamii,Halmashauri ya Wilaya ya Songea Bashiru Mgwassa,Diwani wa Kata ya Mtyangimbole Meckezedeck Mwella, Mwenyekiti wa Sonngo Siwajibu Gama,Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mwl,Mwingira,Makamu Mwenyekiti wa Sonngo Ifigenia Mbawala,wa kwanza kutoka kushoni ni Katibu wa Sonngo Mathew Ngarimanayo
Washiriki wa mdahalo huo wakisikiliza kwa makini mada zilizokuwa zinatolewa na wataalamu wa masuala ya uwajibikaji wa wa viongozi kwa wananchi wake
Waandishi wa Habari wakiendelea kunasa matukio mbalimbali kwenye mdahalo huo,kutoka kushoto ni Mpiga picha Mpenda Mvula,Fundi Mitambo Boniface Bundala,Mwandishi wa Star Tv na Radio Free Africa Adam Nindi
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Sonngo Jongo Haule
Mwendesha ratiba katika Mdahalo huo MC Juma Nyumayo akitoa muongozo kwa washiriki
Dj Ras akirekebisha mitambo ili washiriki wa mdahalo waendelee na libeneke husika
Viongozi wa Asasi ya Sonno wakiwa kwenye dawati la usajiri wa washiriki wa mdahalo huo
Mzee Said Ramadhan akichangia hoja katika mdahalo huo
Washiriki wa mdahalo huo wakisikiliza kwa makini mada zilizokuwa zinatolewa na wataalamu wa masuala ya uwajibikaji wa wa viongozi kwa wananchi wake
Waandishi wa Habari wakiendelea kunasa matukio mbalimbali kwenye mdahalo huo,kutoka kushoto ni Mpiga picha Mpenda Mvula,Fundi Mitambo Boniface Bundala,Mwandishi wa Star Tv na Radio Free Africa Adam Nindi
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Sonngo Jongo Haule
Mwendesha ratiba katika Mdahalo huo MC Juma Nyumayo akitoa muongozo kwa washiriki
Dj Ras akirekebisha mitambo ili washiriki wa mdahalo waendelee na libeneke husika
Viongozi wa Asasi ya Sonno wakiwa kwenye dawati la usajiri wa washiriki wa mdahalo huo
Mzee Said Ramadhan akichangia hoja katika mdahalo huo
APANDISHWA KIZIMBANI KWA KOSA LA KUMBAKA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA TATU
Na Gideon Mwakanosya,Songea
MTU mmoja mkazi wa mtaa wa Ruvuma katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi mkoani humo kwa
tuhuma ya kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha tatu.
Ilidaiwa Mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka Wakili wa Serikali Shaban Mwegole mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Jenifer Changani
kuwa mnamo kati ya Januari na Mei mwaka jana, mshtakiwa Sababu Iddi(18) ambaye ni mkazi wa mtaa huo alitenda kosa hilo.
Mwendesha mashtaka huyo aliendelea kudai kuwa mwanafunzi huyo anasoma shule ya sekondari Ruvuma ambapo mshtakiwa ameonekana kutenda kosa hilo huku akijua kwamba ni kosa kisheria kufanya mapenzi na mwanafunzi jambo ambalo lilisababisha kukatisha masomo.
Kadhalika wakati kesi hiyo ikiendelea mahakamani hapo Hakimu mkazi wa Mahakama ya mkoa wa Ruvuma Shangani alisema mshtakiwa ana kesi ya kujibu kutokana na shtaka linalomkabili na kwamba anapaswa kuleta utetezi wake mahakamani.
Hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 14 mwaka huu itakapoletwa mahakamani kwa ajili ya kuanza kusikiliza utetezi wa mshtakiwa na kwamba mshtakiwa amerudishwa mahabusu kutokana na kukosa
mdhamini.
tuhuma ya kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha tatu.
Ilidaiwa Mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka Wakili wa Serikali Shaban Mwegole mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Jenifer Changani
kuwa mnamo kati ya Januari na Mei mwaka jana, mshtakiwa Sababu Iddi(18) ambaye ni mkazi wa mtaa huo alitenda kosa hilo.
Mwendesha mashtaka huyo aliendelea kudai kuwa mwanafunzi huyo anasoma shule ya sekondari Ruvuma ambapo mshtakiwa ameonekana kutenda kosa hilo huku akijua kwamba ni kosa kisheria kufanya mapenzi na mwanafunzi jambo ambalo lilisababisha kukatisha masomo.
Kadhalika wakati kesi hiyo ikiendelea mahakamani hapo Hakimu mkazi wa Mahakama ya mkoa wa Ruvuma Shangani alisema mshtakiwa ana kesi ya kujibu kutokana na shtaka linalomkabili na kwamba anapaswa kuleta utetezi wake mahakamani.
Hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 14 mwaka huu itakapoletwa mahakamani kwa ajili ya kuanza kusikiliza utetezi wa mshtakiwa na kwamba mshtakiwa amerudishwa mahabusu kutokana na kukosa
mdhamini.
MWISHO.
VILABU MANISPAA YA SONGEA KUANZA KUCHUKUA FOMU USHIRIKI LIGI YA SANGA ONE
Mwenyekiti wa SUFA Golden Sanga, Maarufu kwa jina la Sanga One
Diwani Mstaafu na Mdau wa Michezo Golden Sanga(Sanga One) akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ligi ambayo inatarajia kuanza hivi karibuni mjini hapa
Na Stephano Mango,Songea
CHAMA cha mpira wa miguu katika Manispaa ya Songea(SUFA) kimezitaka vilabu kujitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Sanga One Cup ambayo yamepangwa kufanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Sokoine katika Manispaa hiyo.
Akizungumza mjini hapa jana, Katibu msaidizi wa SUFA, Godfrey Mvula alisema kuwa mashindano hayo yatahusisha vilabu vyote ndani ya Manispaa hiyo ambavyo vina usajili wa kudumu kutoka kwa msajili wa vyama vya michezo nchini na vile visivyokuwa na usajili huo.
Mvula alisema mashindano hayo yatadhaminiwa na mmoja wa wadau wa soka na pia Mwenyekiti wa SUFA katika Manispaa hiyo, Golden Sanga maarufu kwa jina la Sanga One yenye lengo la kusaka vipaji vipya na kuviibua ili kuwafanya wachezaji hao kuwa tegemeo na hazina kwa Manispaa mkoa na Taifa kwa ujumla.
Alisema mashindano hayo yatakuwa chachu na mbinu ambayo itasaidia SUFA kuwapata wachezaji wenye vipaji na wanaojituma wawapo uwanjani badala ya kuwatafuta kwa kuwateua kupitia kwenye mashindano ya ligi ya wilaya au mkoa na kuishia kutafuta maslahi yao binafsi badala ya mpira uliomweka hapo.
Alieleza kuwa bingwa wa mashindano hayo ataondoka na kitita cha fedha taslimu Sh. 200,000/=, wa pili atazawadiwa fedha Sh. 100,000/= na mshindi wa tatu ataambulia fedha Sh.70,000/=, mchezaji bora atazawadiwa fedha taaslim Sh.20,000/= na timu itakayoonyesha nidhamu ya ndani na nje ya uwanja watapata fedha Sh.20,000/=.
Alisema gharama ya uchukuaji wa fomu imepangwa kulipia Sh.10,000/= ambayo itapenda kushiriki mashindano hayo na zitarejeshwa fomu hizo Januari 26 mwaka huu saa 10:30 jioni kwenye ofisi za SUFA alidai mchezaji atakaye bainika amesajiliwa na timu zaidi ya moja jina lake litaondolewa kushiriki mashindano hayo.
MWISHO
Thursday, January 19, 2012
RAIS KIKWETE AMESHINDWA KUTULETEA MAISHA BORA WANANCHI TUTIMIZE WAJIBU WETU
Rais Jakaya Kikwete
Na,Stephano Mango,Songea
SINA hata chembe ya shaka kuwa,Rais Jakaya Kikwete ameshindwa kutimiza ahadi yake ya kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania na badala yake anaamua kuzungumzia maafa na majanga mbalimbali katika kuhararisha kushindwa kwake kuzikabili changamoto zinazomkabili za kutimiza ahadi yake kama alivyotuahidi
Mgombea wa nafasi ya Urais mwaka 2005 Jakaya Kikwete wakati wa kampeni alituahidi kutuletea maisha bora kila mtanzania kwa ari mpya,nguvu mpya na kasi mpya,ahadi hiyo alishindwa kuitimiza katika kipindi chake cha miaka mitano
Kushindwa kwake huko yeye pamoja na wenzake Serikali wakajikita katika kueleza majanga na maafa mbalimbali kuwa ndio kikwazo cha kushindwa kutimiza ahadi zao ingawa mpango wowote mkakati kabla na baada ya kutekelezwa lazima kuwe na faida na hasara
Kitendo chao cha kushindwa kufahamu hilo iwe kwa bahati mbaya au kwa makusudi toka mapema ni ishara iliyodhahiri kuwa wameamua kutuona mabwege nasi kutokana na ukondoo wetu wa kushindwa kuwachukulia hatua viongozi wanaoshindwa kutimiza ahadi zao nao wanajiziuka na kujinyakulia rasilimali zinazotuzunga kila kukicha
Wanafanya hayo wakishirikiana na wawekezaji uchwala ambao wanakuja nchini wakiwa maskini wa kutupwa lakini baada ya muda mfupi wanakuwa na ukwasi wa kutisha na kuwaletea jeuri wananchi na wakati mwingine wakiwaua kama wanyama huku viongozi wetu wakikaa kimya na kuendelea kutuhubiria kuwa nchi yetu ni maskini
Wakipata fursa ya kusema viongozi hao utasikia kuwa ugumu wa maisha unaowakabili watanzania ni kutokana na kutetereka kwa mfumo wa fedha wa kimataifa na kuanguka kwa masoko ya hisa katika mataifa yanayoendelea ndiko kunakosababisha makali ya maisha nchini kuongezeka kutokana na hilo ambalo linasababisha sekta zinazochangia pato la taifa kuporomoka
Hilo linatokana na nchi yetu kwa kiasi kikubwa kutegemea mauzo ya bidhaa za nje, ikiwemo na utalii ambapo kuporomoka huko kwa biashara ya nje ni dalili mbaya kwa ukuaji wa uchumi wa Taifa letu ambalo toka mwaka 2008 mpaka 2011 katika hotuba zake Rais Kikwete amekuwa akirudia mara kwa mara kuwa uchumi wa taifa unatarajia kukua kwa asilimia 7.
Ahadi ya maisha bora iliyeyuka mchana kweupe huku watanzania wakiwaona viongozi wao walivyojaa tongotongo za aibu kwenye macho yao lakini kwa kutuona watanzania ni mabwege wakati wa kampeni za mwaka 2010 wakatuletea utani mwingine chini ya kauli mbiu ya Ari zaidi,nguvu zaidi na kasi zaidi
Hali ya ukuaji wa uchumi na maendeleo ya watanzania katika kipindi cha utawala wa Rais Kikwete umedorora na viongozi wanashindwa kutoa mwanga stahiki wa kupambana chini ya kauli mbiu iliyowaingiza madarakani mwaka 2005 na 2010 badala yake wanatoa hutuba za kuaga mwaka bila kuonyesha utekelezaji wa ahadi na malengo stahiki
Viongozi kulalamikia majanga na maafa kuwa ndio kikwazo cha kushindwa kutengeneza mazingira ya kukua kwa uchumi na kuleta maendeleo ya uchumi unaonyesha dalili za wazi kuwa uongozi huo umeshindwa kukidhi matarajio ya wananchi wake na kwa mtu mwenye akili alipaswa kusema jambo ili kupisha watu wengine wenye mawazo chanya kuongoza bila kuweka porojo katika hotuba
Uchumi ndio dira ya kufikia maisha bora kwa kila mtanzania hivyo kushindwa kutathimini madhara ya uchumi usiokuwa imara kwa viwango stahiki kwa taifa na kwa wananchi kuna leta hofu ya kuiona kesho iliyosalama kwa watanzania
Katika muktadha huo nimesikitishwa na maneno ya Rais Kikwete wakati akitoa salamu za mwaka mpya wa 2012 na kuuaga mwaka 2011 alikuwa anatuambia watanzania hali ya kiuchumi ya Taifa letu maneno ambayo yanamaana iliyosawa na hotuba zake zilizopita
Alisikika akiwaambia watanzania kuwa kwa upande wa uchumi mwaka 2011 ulikuwa na changamoto nyingi ,kulikuwa na mchanganyiko wa ukame,uhaba mkubwa wa umeme,upungufu wa chakula kwenye baadhi ya maeneo nchini,kupanda kwa bei za mafuta na vyakula, kushuka kwa thamani ya shilingi,mfumuko wa bei kupanda na sasa mvua nyingi na athari zake
Rais Kikwete aliendelea kusema kuwa pamoja na changamoto hizo tunatarajia uchumi wetu utakuwa kwa asilimia 7 ingawaje wenzetu wa IMF wanakadiria kuwa utakuwa kwa asilimia 6.3,hata kwa kiwango hicho bado nchi yetu inabaki kuwa ni miongoni mwa nchi 20 duniani zinazoongoza kwa ukuaji wa uchumi,Ni dhahiri basi kuwa kama athari hizo zisingekuwepo hali ya uchumi wetu ingekuwa bora zaidi
Hayo ndio maneno ya Rais Kikwete wakati akiuaga mwaka wa 2011 na kuwatakia watanzania heri na fanaka kwa mwaka mpya wa 2012 wenye mashaka ya uchumi na mbinu hafifu za kukuza uchumi ili wananchi wawe na uhakika wa kuishi kesho
Serikali imekuwa na mipango mahututi kabisa ya kuimarisha uchumi wa nchi na kuongeza thamani ya shilingi imebaki ikiendelea kuwakamua kila kukicha wananchi kile kidogo walichonacho kwa kuwaongezea gharama za vyakula,maji,umeme na mahitaji mengine ya kimsingi ya kibinadamu huku ikiwa imeshindwa kutengeneza miundombinu stahiki ya upatikanaji wa maisha bora
Kwa sababu ukuaji wa uchumi unapimwa katika ongezeko la uzalishaji, uwekezaji, utalii, kudhibiti mfumuko wa bei na ongezeko la thamani ya fedha hivyo huwezi kupata maisha bora katika mazingira yanayo onyesha kuporomoka kwa uchumi na kushuka kwa thamani ya fedha
Hadi sasa tayari baadhi ya viashiria katika ukuaji wa uchumi vimekumbwa na dhoruba, kwa mfano thamani ya shilingi yetu inazidi kuporomoka na uzalishaji wetu unasuasua na kusababisha kile kidogo kinachozalishwa kuuzwa kwa gharama kubwa.
Kipimo kimojawapo muhimu katika kujua ubora wa mwelekeo wa uchumi wa nchi yoyote ile ni thamani ya fedha yake ambapo ikiwa thamani ya fedha ya nchi yoyote inapungua basi ujue uchumi wake upo hatarini, na unahitajika kuratibiwa upya na kutafuta mbinu bora za kuufufua.
Thamani ya fedha kwa nchi ni muhimu katika kukuza uchumi wake na kusababisha kuleta maisha bora kwa wananchi wake kwani inaeleweka kuwa ukuaji wa uchumi na maendeleo ya kiuchumi ni dhana mbili tofauti, ingawa kimsingi zinategemeana.
Tofauti yake ni kuwa maendeleo ya kiuchumi yanapimwa kwa viwango vya upatikanaji wa ubora katika huduma za kijamii kama vile, miundo mbinu,afya, elimu,makazi ya watu huduma za maji n.k.
Ambapo ukuaji wa uchumi unazingatia kiwango cha uzalishaji, thamani ya fedha,udhibiti wa mfumuko wa bei na mengineyo, lakini maendeleo ya kiuchumi yanapimwa katika upatikanaji wa huduma za ustawi kwa wananchi.
Katika mazingira ya kawaida ukuaji wa uchumi ukiratibiwa vizuri unaweza kusababisha maendeleo ya kiuchumi na hapo ndipo kunako wezesha upatikanaji wa maisha bora
Kimantiki nchi ambayo imeshindwa kulinda thamani ya fedha yake ni ndoto kuleta maisha bora kwa wananchi wake na haina sababu ya kujidanganya kuwa nchi hiyo inapiga hatua katika ukuaji wa uchumi lakini sio kusingizia majanga mbalimbali ndiyo yanayosababisha gharama za maisha kupanda.
Mara kadha viongozi wa serikali wamekuwa wakijivunia ukuaji wa uchumi lakini wamekuwa wakikiri waziwazi kuwa bado kuna tatizo katika maendeleo ya watu na kukimbilia kusifia maendeleo ya vitu .
Kitendo cha kuporomoka kwa thamani ya shilingi kwa kiasi kikubwa tunako kushuhudia hapa nchini kina ashiria dalili za hatari katika maisha ya watanzania hata kama wataendelea kutupandishia gharama za umeme,maji,afya na bidhaa.
Wakati Rais Jakaya kikwete anaingia madarakani mwaka 2005, dola moja ya marekani ilikuwa inabadilishwa kwa sh 1,128,leo dola moja ya marekani inabadilishwa kwa sh 1,595 hii ikiwa ni ongezeko la sh 467 kwa dola moja kwa takribani miaka sita
Hali hii inaonyesha kuwa kwa miaka sita ya utawala wa Rais Kikwete fedha yetu imepungua thamani yake kwa mwendo wa kupaa ambapo kwa mwenendo huo maisha bora yaliyo ahidiwa yanabaki kuwa ndoto, jambo hili linathibitishwa na ukali wa maisha kwa watanzania walio wengi kuongezeka kila kukicha
Kwa sababu ukuaji wa kiuchumi unaweza kusababisha maendeleo ya kiuchumi hasa pale ongezeko la uzalishaji mali linapotumika katika kuboresha maisha ya jamii kwa kuhakikisha huduma za kijamii zinapatikana hususani afya, elimu,maji safi, uhakika wa lishe na mambo mengine yanayo husiana na ustawi wa jamii.
Kutokana na kuzama kwetu kiuchumi tunawajibika kila mmoja wetu kwa nafasi yake kutimiza wajibu wake katika kulinda rasilimali za nchi na kutumia kwa manufaa ya jamii pana ili tuweze kutengeneza ukuaji wa uchumi na maendeleo ya kiuchumi kisha tuyafikie maisha bora kwani viongozi wetu wametudanya
Kama tungekuwa makini katika matumizi ya mapato yetu tusingekuwa na haja ya kutembeza bakuli kuomba misaada katika kutekeleza baadhi ya miradi kwa sababu sehemu kubwa ya fedha tunayoiomba kwa ajili ya maendeleo yetu kutoka kwa wahisani tunayo hapa hapa nchini na inaweza kutuletea maisha bora endapo ikitumika ipasavyo
Kitendo cha kukaa vijiweni bila kufanya shughuli za kimaendeleo zitakazo sababisha ustawi wa kimaisha na mazingira stahiki katika jamii hakutawezesha maisha kuwa bora hivyo,kufanya kazi kwa maarifa na bidii kunapelekea kukua kwa maendeleo ya kiuchumi na ukuaji wa uchumi wenyewe na Serikali tuidai kuweka mazingira bora kwa wananchi wake ili waweze kufanikiwa katika adhima ya kujiletea maisha bora siyo kupewa maisha bora na wao kwa sera chakavu
Mwandishi wa Makala
Anapatikana 0715-335051
Wednesday, January 18, 2012
WANACHAMA WA SACCOS YA WATUMISHI WA MANISPAA YA SONGEA KUNUFAIKA NA MKOPO WA FEDHA ZA UJENZI WA NYUMBA
Na Augustino Chindiye, Songea
ZAIDI ya Wanachama 300 wa Cha akiba na Mikopo(SACCOS) cha Watumishi wa Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wanatarajia kunufaika mpango maalumu wa kukopeshwa fedha za kuwawezesha kujenga nyumba zikiwa ni juhudi za chama hicho kuwakwamua na umasikini wanachama wake.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa chama hicho Sky Mpange wakati
akiongea katika mkutano wa 19 wa mwaka wa chama hicho uliofanyika katika ukumbi wa Songea Club mjini hapa.
Akifafanua taarifa hiyo Mpange alisema kuwa kupitia mpango maalumu wa kutoa mikopo ya ujenzi wa nyumba kwa wanachama wake kwa riba nafuu zaidi utawawezesha watumishi hao kumiliki nyumba zao wenyewe baadala ya sasa ambapo wengi wa wanachama hao wamekuwa wakiishi katika nyumba za kupanga hali ambayo huwafanya na kutozwa fedha nyingi na kuwafanya washindwe kufanya hivyo kutokana na gharama kubwa za vifaa vya ujenzi
wa nyumba hizo.
Alisema kufutia hali hiyo chama hicho kimelazimika kuanza kutoa mikopo ya Shilingi Milioni Nane kwa kila mwanachama ili kufanikisha ujenzi huo kwa wanachama wake kutokana na wengi wao kushindwa kumudu gharama za ujenzi huo hivyo kushindwa kuendeleza maisha yao kiuchumi kwa kulipa fedha nyingi kwenye nyumba za kupanga.
Mpange aliendelea kueleza kuwa ili kufanikisha Mkakati huo Chama
hicho kuwawezesha wanachama wake huku kukiwa na maelekezo kuwa kila mwezi mwanachama wao atatakiwa kukatwa asilimia 10 ya mkopo wa nyumba wa shilingi Milioni Nane kwa kwa mwezi.
Aidha,Mpange alibainisha kuwa pamoja na juhudi hizo kuoneshwa na
uongozi wa Chama hicho lakini mwitikio wa wanachama kukopa mkopo huo umekuwa mdogo na kuongeza kuwa tangu Mpango wa mkopo huo uanze kutolewa miaka miwili iliyopita ni wanachama Wanne tu waliojitokeza kukopa.
Awali akifungua mkutano huo Meneja wa SONAMCU Songea Bw.Salum Mbuyu aliwahimiza wanachama hao kukopa mkopo wa nyumba ili kujiletea maendeleo yakiwemo ya kupangisha nyumba zao ili kujiongezea kipato tofauti na mikopo midogo ambayo mwisho wake fedha hizo huishia katika matumizi ya starehe.
Aidha, Chama hicho kimefanikiwa kutoa mikopo mingine zaidi ya shilingi milioni 300 kwa wanachama wake 330 katika kipindi cha mwaka jana na kwamba mwaka huu Saccos hiyo inatarajia kutoa mkopo wa shilingi milioni 400 kwa wanachama hao.
ZAIDI ya Wanachama 300 wa Cha akiba na Mikopo(SACCOS) cha Watumishi wa Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wanatarajia kunufaika mpango maalumu wa kukopeshwa fedha za kuwawezesha kujenga nyumba zikiwa ni juhudi za chama hicho kuwakwamua na umasikini wanachama wake.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa chama hicho Sky Mpange wakati
akiongea katika mkutano wa 19 wa mwaka wa chama hicho uliofanyika katika ukumbi wa Songea Club mjini hapa.
Akifafanua taarifa hiyo Mpange alisema kuwa kupitia mpango maalumu wa kutoa mikopo ya ujenzi wa nyumba kwa wanachama wake kwa riba nafuu zaidi utawawezesha watumishi hao kumiliki nyumba zao wenyewe baadala ya sasa ambapo wengi wa wanachama hao wamekuwa wakiishi katika nyumba za kupanga hali ambayo huwafanya na kutozwa fedha nyingi na kuwafanya washindwe kufanya hivyo kutokana na gharama kubwa za vifaa vya ujenzi
wa nyumba hizo.
Alisema kufutia hali hiyo chama hicho kimelazimika kuanza kutoa mikopo ya Shilingi Milioni Nane kwa kila mwanachama ili kufanikisha ujenzi huo kwa wanachama wake kutokana na wengi wao kushindwa kumudu gharama za ujenzi huo hivyo kushindwa kuendeleza maisha yao kiuchumi kwa kulipa fedha nyingi kwenye nyumba za kupanga.
Mpange aliendelea kueleza kuwa ili kufanikisha Mkakati huo Chama
hicho kuwawezesha wanachama wake huku kukiwa na maelekezo kuwa kila mwezi mwanachama wao atatakiwa kukatwa asilimia 10 ya mkopo wa nyumba wa shilingi Milioni Nane kwa kwa mwezi.
Aidha,Mpange alibainisha kuwa pamoja na juhudi hizo kuoneshwa na
uongozi wa Chama hicho lakini mwitikio wa wanachama kukopa mkopo huo umekuwa mdogo na kuongeza kuwa tangu Mpango wa mkopo huo uanze kutolewa miaka miwili iliyopita ni wanachama Wanne tu waliojitokeza kukopa.
Awali akifungua mkutano huo Meneja wa SONAMCU Songea Bw.Salum Mbuyu aliwahimiza wanachama hao kukopa mkopo wa nyumba ili kujiletea maendeleo yakiwemo ya kupangisha nyumba zao ili kujiongezea kipato tofauti na mikopo midogo ambayo mwisho wake fedha hizo huishia katika matumizi ya starehe.
Aidha, Chama hicho kimefanikiwa kutoa mikopo mingine zaidi ya shilingi milioni 300 kwa wanachama wake 330 katika kipindi cha mwaka jana na kwamba mwaka huu Saccos hiyo inatarajia kutoa mkopo wa shilingi milioni 400 kwa wanachama hao.
MWISHO
Saturday, January 14, 2012
WAKULIMA WA TUMBAKU WALALAMIKIA MBOLEA YENYE KIWANGO DUNI
Na Stephano Mango, Songea
WAKULIMA wa zao la tumbaku wa wilaya za Songea na Namtumbo mkoani Ruvuma wameulalamika uongozi wa chama kilele (APEX ) ya tumbaku na Chama Kikuu cha Ushirika cha Songea na Namtumbo ( SONAMCU) kwakuwaletea mbolea ambayo iko chini ya kiwango na kuwasababishia hasara kubwa wakulima wa zao hilo.
Wakizunguza na wandishi wa habari mjini Songea wakulima zaidi ya 20 ambao waliongozwa na Salum Brashi ambaye ni Mkulima toka Chama cha Ushirika cha Msingi cha Mnazini kilichapo Wilayani Namtumbo walisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2009/2010 na 2010/2011 wakulima wa zao hilo walipata hasara kubwa baada ya kutumia mbolea hiyo na kusabisha kuzalisha tumbaku isiyo kuwa na ubora.
Wakulima hao walieleza zaidi kuwa hali hiyo ya kutumia mbolea ambayo ipo chini ya kiwango jambo ambalo wamekuwa wakitumia nguvu kubwa isiyo kuwa na tija katika uzalisha wa zao hilo na kuwafanya hali zao kuwa duni kimaisha na kuendelea kuwadhofisha kiuchumi .
Walifafanua kuwa mfano kwa kawaida mbolea aina ya NPK 20.10.10 ambayo ndio inayofaa kwa zao la tumbaku wao badala yake walileta mbolea aina ya NPK 1.2.10.10 na msimu wa 2010/2011 ililetwa mbolea aina 6.10.10 badala ya mbolea iliyozoeleka ya NPK 20.10.10.
Walisema kwakuwa mbolea hiyo iliyoletwa haikuwa na nitrogen 20 ndio maana tumbaku hiyo ilikosa nikotin (sumu) hivyo wameiomba Serikali kuchua hatua za haraka za kuwasiliana na Uongozi wa chama kilele (APEX) ya tumbaku na Chama Kikuu cha Ushirika cha Wilaya ya Songea na Namtumbo (SONAMCU) kuhakisha kuwa wanaleta mbolea inayofaa kwa zao hilo.
Aidha wakulima hao wameiomba Serikali ione umuhimu wa kuzuia mbolea ambayo kwa hivi sasa imeifadhiwa kwenye maghala ikisubili kusambazwa kwa wakulima wa zao la tumbaku wakihofia kuwa mbolea hiyo haina sifa kama iliyo letwa kwa misimu miwili ya kilimo iliyopita na badala yake ichukuliwe sampuli kwenda kupima kwenye maabara ya mkemia mkuu ,TBS na maabara nyingine zilipo hapa nchini ambazo zitaweza kubaini ukweli huo.
Kwa upande wake Meneja shughuli wa Chama Kilele (APEX) ya tumbaku yenye makao makuu mkoani Morogoro Samuel Jokeya akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Songea alisema kuwa wakulima wa tumbaku wa Wilaya ya Songea na Namtumbo wamekuwa na malalamiko kuwa Vyama APEX na SONAMCU vimekuwa wakileta mbolea kwa wakulima ambayo iko chini ya kiwango jambo hilo ambalo alidai siyo la kweli.
Jokeya alisema kuwa malalamiko ya wakulima wa zao la tumbaku kuwa haifai kwa matumizi ni gumu na halina udhibitisho kwani wakulima inawezekana hawazingatii kanuni bora za wataalum wa zao hilo na matumizi ya za duni za kilimo.na kwamba utatuzi wa jambo hili unafanyika huku akiwa ameshauri maabara zilizopo kupima vipimo vyote wanavyo pelekewa badala ya vichache nakuomba kupewa cheti kinachothibitisha ubora wa mbolea inayoletwa.
Alifafanua kuwa chama chake kinaleta mbolea kutokana na mahitaji yanayotolewa na Vyama vya Ushirika vya msingi na amedai kwamba endapo wanaona mbolea inayoletwa haiwafai SONAMCU inalo jukumu la kusitisha mahitaji ya wakulima na wakaagiza mbolea ambayo wanaona inawafaa kwa ajili ya zao hilo.
Alisema mpaka sasa tayari mbolea kwa ajili ya tumbaku ya mvuke (VFC ) imeletwa mifuko 7735, mbolea aina ya CAN imeletwa mifuko 1878 , UREA mifuko 16394 na mbolea ya moshi mifuko 2323 .
Naye mbunge wa Jimbo la Namtumbo Vita Kawawa alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusiana na malalamiko alikili kupokea kero hiyo kutoka kwa wapiga kura wake na ameeleza kuwa kila Chama cha Ushirika cha msingi kina wajibu wa kutafuta pembejeo na siyo kutegemea toka kwenye Vyama vikuu ambayo vimeoneka kuwa vinaleta mbolea ambayo haifai kwa matumizi ya kilimo cha tumbaku.
Kawawa ambaye pia ni Mwenekiti wa Bodi ya tumbaku nchini alieleza kuwa kama malalamiko yanaendelea kuwepo zaidi ya mbolea hiyo ni vyema Chama Kilele APEX ya tumbaku na SONAMCU wakatafuta njia mbadala ya kumaliza utata uliopo kati yao na wakulima wa zao hilo.
Hata hivyo jitihada za kuwapata Maafisa Kilimo wa Wilaya ya Namtumbo na Songea kutolea ufafanuzi juu ya tatizo hilo ziligonga mwamba baada ya kutopatikana kwenye simu zao za mikononi.
Mwisho.
Friday, January 13, 2012
WAWILI WAFARIKI KATIKA MATUKIO MAWILI TOFAUTI
Na,Gideon Mwakanosya, Songea
WATU wawili wamekutwa wakiwa wamekufa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali katika matukio mawili tofauti mkoani Ruvuma likiwemo mkazi mmoja Andrea Hyera (35) mkazi wa kijiji cha Litembo Wilayani Mbinga Mkoa wa Ruvuma amekutwa akiwa amekufa kwa kukatwakatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na watu wasio fahamika na mwili wake kutupwa kando ya Barabara itokayo Litembo kwenda Kijiji cha Mbungu.
Habari zilizopatikana mjini hapa ambazo zimethibitishwa na Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda zimesema kuwa tukio hilo lilitokea januari 10 mwaka huu majira ya saa 7: 00 mchana huko katika kijiji cha Mtambotambo kilichopo wilayani humo.
Kamanda Kamuhanda amefafanua kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio Hyera alikutwa ameuawa na watu wasio fahamika ambapo mwili wake ulikuwa na majeraha kichwani ambayo yanahashiria kuwa yanatokana na kukatwa na kitu chenye ncha kali.
Amebainisha zaidi kuwa inadaiwa mwili wa Hyera ulikutwa kandokando ya barabara na watu walio kuwa wakipita kwenye eneo hilo ambao ndio walio toa taarifa kwenye Serikali ya Kijiji hicho.
Amesema kuwa uongozi wa Serikali ya Kijiji baada ya kupata taarifa ya tukio hilo walikwenda kwenye eneo la tukio na baadaye taarifa ilitolewa Polisi kituo kidogo cha Litembo ambao waliwasiliana na Polisi wilaya ya Mbinga.
Ameeleza zaidi kuwa Askari Polisi wakiwa wameongozana na Mganga walikwenda kwenye eneo la tukio na kuukuta mwili wa Hyera ukiwa kandokando ya barabara itokayo Litembo kwenda Kijiji cha Mbungu huku ukiwa na majeraha kichwani ambayo yanadaiwa kuwa yalisababisha kukatwakatwa na kitu chenye ncha kali kichwani.
Hata hivyo Kamanda Kamuhanda amesema kuwa Polisi bado inaendelea kufanya upelelezi kuhusiana na tukio hilo na mara utakapo kamilika na kuwabaini watuhumiwa hatua za kisheria zitachukuliwa.
WAKATI HUO HUO ********* Mtu mmoja Oswadi Mgele (65) mkazi wa Kijiji cha Ugano kilichopo Kata ya Kambarage Wilayani mbinga amekutwa akiwa ameuawa na watu wasio fahamika huku mwili wake ukiwa na majeraha kichwani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea januari 10 mwaka huu majira ya saa 3:00 asubuhi huko katika Kijiji cha Ugano wilayani mbinga.
Amesema kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio watu walikuwa wakipita njia hafla walimwona mtu amelazwa kando ya barabara huku akiwa na majeraha kichwani ndipo waliutafuta uongozi wa serikali wa kijiji hicho kwa kuwajulisha kuwa kunamtu kauwawa na watu wasio fahamika na polisi walipewa taarifa kisha walifika kwenye eneo la tukio ambao walifuatana na daktari ambaye walisibitisha kweli Mgele ameshauwawa kwa kupigwa na kitu kichwani.
Kamanda kamuhanda amefafanua kuwa Mgele kabla ajauwawa inadaiwa kuwa alikuwa akituhumiwa kijijini hapo na wanakijiji wenzake kuwa ni mshirikina hivyo inahofiwa kuwa chanzo cha mauwaji kinahusishwa na imani za kishirikina hata hivyo polisi inaendelea kufanya uchunguzi na kuhusiana na tukio hilo.
Thursday, January 12, 2012
MFUMO DUME WAATHIRI MAENDELEO WILAYANI NAMTUMBO
Na Stephano Mango,Namtumbo
IMEBAINIKA kuwa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma inaukandamizaji mkubwa wa haki za wanawake na watoto kutokana na mfumo dume na kuwafanya wanawake wengi wasinufaike na kazi za uzalishaji mali wanazozifanya kila siku
Hayo yalibainishwa jana na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Saveri Maketa wakati akifungua mafunzo ya siku tano ya uwezeshaji wa uchanganuzi na uchambuzi wa sera ya maendeleo ya wanawake na jinsia yanayoendeshwa na Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake Ruvuma(Ruwodefu) kwa ufadhiri wa Shirika la The Foundation For Civil Society
Maketa alisema kuwa hali hiyo imewafanya wanawake wengi kubeba mzigo mkubwa wa kazi ya uzalishaji na kutunza familia kwa ujira kidogo na kuwafanya wanawake hao kurudi nyuma kimaendeleo na kuendeleza kuzifanya kaya nyingi kuwa maskini
Alisema kuwa ni wajibu wa Asasi za kiraia kushirikiana na Serikali kwa kuwatumia wataalamu mbalimbali wakiwemo wa sheria ili kuweza kuwajengea uwezo wananchi wa kutambua haki na wajibu wao katika jamii ili waweze kujiletea maendeleo kwa mgawanyo ulio sawa wa kipato kadiri ya faida walizozipata kifamilia
Baadhi ya viongozi wa dini ambao wanashiriki katika mafunzo hayo walisema kuwa mafunzo yamewafikia muda muafa kabisa kwani wanashuhudia ongezeko la kuvunjika kwa ndoa na kusababisha watoto na wazee wengi kuishi katika mazingira magumu kwa kukosa huduma muhimu kutoka kwa wazazi na wategemezi wao kinyume na sheria na wajibu wa jamii
Viongozi hao wamesema mara kwa kuisha kwa mafunzo hayo wana wajibu wa kutoa elimu hiyo kupitia mahubiri yao katika nyumba za ibada ili kurekebisha hali hiyo kulingana na sera ya wanawake,jinsia na watoto
Awali Mwenyekiti wa Asasi ya Ruwedefu Siwajibu Gama alisema kuwa mafunzo hayo ya siku tano yanashirikisha viongozi wa makundi mbalimbali zikiwemo taasisi za dini,asasi zisizo za kiserikali na wanawake wenyewe ambayo yana lenga kuandaa wawezeshaji watakaokwenda kuelimisha katika ngazi ya jamii Wilaya ya Namtumbo yenye kata 18
Gama alisema kuwa pamoja na kufundisha umuhimu wa usawa katika kuleta maendele,mada nyingine ni madhumuni ya sera ya jinsia,haki za binadamu,mgawanyo na umiliki wa rasilimali kati ya wanawake na wanaume na sheria ya ndoa
MWISHO
Tuesday, January 10, 2012
ASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUNYOFOA ROHO YA MWENZIE KWENYE UGOMVI WA POMBE ,TUKIO JINGINE MAMA ALIPUKIWA NA TAA YA KANDILI NA KUSABABISHA KUUNGUA KWA MWILI MZIMA
Na Gideon Mwakanosya,Songea
JESHI la Polisi Mkoani Ruvuma linamshikilia Manywele Abdalah Manywele (34)mkazi wa Kijiji cha Chiwana Mashambani kilichopo Kata ya Mbesa Wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma kwa tuhuma za kumpiga na kumsababishia kifo Bakari Mohamed(35) mkazi wa kijiji hicho wakati walipokuwa wakigombana kwenye kilabu cha pombe za kienyeji
Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda alisema kuwa tukio hilo limetokea januari 8 mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi huko katika kijiji cha Chiwana Mashambani
Kamuhanda amefafanua kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio watu hao wakiwa kwenye kilabu cha pombe za kienyeji huku wakiwa wanakunywa pombe ghafla ulitokea ugomvi ambao unadaiwa kuwa chanzo chake walikuwa wakigombania pombe na baadae wakiwa wanaendelea kupigana Mohamed alipigwa na kufa papo hapo
Alisema kuwa baada ya kutokea tukio hilo uongozi wa Serikali ya Kijiji hicho waliotoa taarifa kwenye kituo cha Polisi cha Tunduru na baadae Askari Polisi wakiwa wameongozana na Daktari walifika kwenye eneo la tukio na kumkuta Mohamed akiwa amesha kufa
Ameeleza zaidi kuwa Askari Polisi wakiwa kwenye eneo la tukio walifanya upelelezi wa awali na walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa ambaye alikiri kuwa walikuwa na ugomvi kati yake na Mohamed ambaye amefariki dunia
Hata hivyo Kamanda Kamuhanda amesema kuwa Polisi inaendelea kufanya upelelezi zaidi ili kuubaini ukweli wa tukio hilo na kwamba utakapo kamilika mtuhumiwa atafikishwa Mahakama kujibu shtaka litakalomkabili
MWISHO
TAA YA KANDILI YALIPUKA NA KUSABABISHA MAJERUHI WILAYANI MBINGA
Na,Gideon Mwakanosya,Songea
MWANAMKE mmoja Theresia Nombo(27) Mkazi wa Kijiji cha Burma wilaya ya Mbinga Mkoa wa Ruvuma amelazwa katika Hospital ya Misheni ya Litembo baada ya kuungua moto mwili mzima wakati alipokuwa anaongeza mafuta kwenye taa yake ambayo baadae taa hiyo ililipuka na kumuunguza mwili mzima
Kamanada wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda alisema kuwa tukio hilo lilitokea Januari 4 mwaka huu majira ya saa 3 usiku nyumbani kwake huko katika kijiji cha Burma
Kamanda Kamuhanda amebainisha zaidi kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio Nombo alikuwa amechukua taa yake na kuiwasha na muda mfupi aligundua kuwa taa hiyo haina mafuta
Alieleza zaidi kuwa Nombo baada ya kugundua taa yake haina mafuta alichukua chupa ambayo alikuwa amehifadhia mafuta ya taa kisha alikwenda hadi ilipotaa yake na kuongeza mafuta kwenye taa yake ya kandili ndipo ghafla kandili hiyo ilianza kulipuka na kupasua chemli na moto kuanza kuwaka na kumsababishia majeraha mwili mzima
Amesema kuwa baada ya kutokea tukio majirani walimchukua Nombo na kumkimbiza katika Hospital ya Litembo kwa ajili ya matibabu ambako amelazwa na hali yake bado ni mbaya sana
MWISHO
Sunday, January 8, 2012
BRUDA AFUNGWA MIAKA 37 KWA KOSA LA KUIIBIA ABASIA MILIONI 105
Na Gideon Mwakanosya,Songea
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Ruvuma imemuhukumu kutumikia kifungo cha miaka 37 na miezi 6 jela Mtawa(Bruda) Aidan Mhuwa wa Abasia ya Peramiho jela baada ya Mahakama hiyo kumtia hatiani kwa kosa la kuibia Abasia hiyo shilingi milioni 105 na kuamliwa kuresha fedha hizo baada ya kumaliza kutumikia kifungo chake.
Akisoma hukumu hiyo juzi kwa zaidi ya masaa matatu Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo Baptisa Mhelela alisema Mahakama hiyo imemtia hatiani Bruda huyo wa Shirika la watawa la Wabenediktine lililo chini ya Kanisa Katoliki jimbo kuu la Songea baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka mahakamani hapo na kwamba itakuwa ni fundisho kwa Watumishi wengine wa Mungu wanye tabia za kuyaibia makanisa.
Hakimu huyo alifafanua kuwa Bruda huyo alitiwa hatiani kwa makosa 14 ya kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu na kufungwa kila kosa miaka mitatu na kwamba adhabu hizo zote zinakwenda kwa pamoja hivyo Mshtakiwa atatumikia adhabu ya miaka mitatu jela na kutakiwa kurejesha Shilingi milioni 105 atakapomaliza kutumikia kifungo chake.
Baada ya hukumu hiyo kutolewa Mahakama hiyo ilizizima kwa huzuni na ndugu wa Mshtakiwa walionekana kuwa na simanzi huku Mshtakiwa akibubujikwa na machozi na mikono yake ikiwa imefungwa pingu akilelekea kwenda kuanza maisha mapya ya gerezani.Mshtakiwa huyo anadaiwa kuliibia Shirika hilo kati ya mwaka 2006 na mwaka 2007.
Katika kesi hiyo ya mwaka 2009 Hakimu Mhelela alisema kuwa katika mashtaka 72 yakiongozwa na shtaka la kuiba vifaa vya ujenzi wa Mradi wa jengo la Abasia ya hanga hiyo Mshtakiwa alishinda lakini alitiwa hatiani kwa kosa la kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.
Alisema kuwa Mshtakiwa huyo alitumia jina bandia la Joseph Nchemeka wakati akisimia Mradi wa jengo hilo na kufungua Akaunti NBC tawi la Ubungo jijini Dar es salaam yenye namba 02221111913 akidai kuwa mtu huyo ni Mkandarasi Mshauri na kwamba hiyo ndiyo akaunti yake wakati mtu huyo ni yeye mwenyewe.
Alisema kuwa ilibainika kuwa mtu huyo ni yeye mwenyewe baada ya kutumwa wakaguzi na kugundua hayupo mtu mwenye jina hilo kwenye orodha ya Wataalamu wa majengo na ndipo Viongozi wa Abasia walipofuatilia na kugundua wizi huo na kwamba ada za ushauri zililipwa kwa jina hilo bandia.
‘Mahakama ilijenga mashaka makubwa kwa nini Bruda Adani atumie jina bandia kufungua Akaunti badala ya jina la Abasia au kwa nini asitumia jina lake ili kundoa mashaka na katika kufuatilia kama hayo ni miongoni mwa majina ikaonekana hayo si majina yake kwa misngi hiyo basi Mahakama imemtia hatiani kwa kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu’alisema Hakimu huyo wakakati akisoma hukumu hiyo.
Kabla ya ya kutiwa hatiani Bruda huyo alijitetea kuwa anasumbuliwa na vidonda vya tumbo na kwamba ana ndugu wanaomtegemea hivyo aliomba mahakama impunguziwe adhabu na ndipo Hakimu Mhelela alieleza kuwa Bruda Aidan katika kosa la kwanza anaukumiwa katika kifungo cha miaka 6 jera, kosa la pili mahakama inampa adhabu ya kifungo cha miezi 12 jera na kosa la 3 hadi la 14 mshtakiwa atatumikia kifungo miaka 3 kila kosa lakini adhabu zote zitakwenda pamoja hivyo atatumikia kifungo kwa muda miaka 3.
MWISHO
Subscribe to:
Posts (Atom)

