About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Friday, March 16, 2012

RC ENG, MANYANYA AWATIMUA WAKURUNGENZI WA HALMASHAURI ZA MKOA WA RUKWA KIKAONI

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ENG, Stella Manyanya(Mb)
Na Stephano Mango, Rukwa
MKUU wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya, aliwafukuza kwenye mkutano wakurugenzi wote wa halmashauri za mkoa huo kwa kushindwa kutoa maelezo ya kina kuhusu madai ya fedha za walimu.
Manyanya alilazimika kufanya hivyo jana wakati wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) alichokuwa mwenyekiti wake ambapo alipewa taarifa za walimu kutolipwa zaidi ya sh milioni 6.5 wanazoidai Halmashauri ya Sumbawanga Mjini.
Akieleza madai ya walimu hao Ofisa Tawala Msaidizi mkoani hapa David Kilonzo alisema walimu hawajalipwa kwa muda mrefu sasa hususan waliotoka nje ya mkoa huo kwa ushawishi wa mfuko wa kuboresha mazingiara ya watumishi.
Baada ya maelezo ya ofisa tawala huyo, mkuu wa mkoa alichukizwa na kuwatoa nje ya kikao hadi watakapopata majibu sahihi ni jinsi gani watawalipa walimu hao.
Alisema mara ya mwisho niliwaeleza kuwa sihitaji kusikia tena suala hilo likijirudia kwenye kikao cha RCC na niliwaagiza wakurugenzi wote kuhakikisha mnawalipa walimu lakini hii leo mnakuja na porojo hizo hizo sasa natamka kuwa siwahitaji humu ndani tokeni nyote na mkirejea mniambie namna mtakavyowalipa walimu hao haraka
Alisema serikali inabebeshwa lawama kwa sababu ya uzembe wa baadhi ya watendaji wake na kwamba inashangaza kuona katika malipo yenu na hata posho zenu mnavyohangaika ili mjilipe haraka lakini madai ya walimu yanachukua muda mrefu huku mkiwazungusha mara nenda mara rudi!
“Mkifanya kazi kwa kufuata taratibu na kuwajibika mtakuwa rafiki zangu lakini kama kuna mtu anapuuza maelekezo yanayotolewa kamwe sitamvumilia na tutamshughulikia kwa mujibu wa kanuni na sheria zilizopo.” Alisema Mhandisi Manyanya
Hata hivyo baada ya dakika 45 wakurugenzi hao walirejea kwenye kikao hicho wakidai watahakikisha walimu hao wanalipwa madeni yao katika kipindi cha mwezi mmoja kuanzia sasa.

Thursday, March 15, 2012

RC MANYANYA AWAPONGEZA MADAKTARI WA RUKWA KWENYE KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA MKOA

Na, Stephano Mango, Rukwa
MKUU wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya amewapongeza Madaktari  na wauguzi wote nchini  ambao walifanya kazi zao kwa umakini mkubwa na uadilifu katika kipindi chote cha mgomo wa kwanza na wa pili ulioitishwa na chama cha Madaktari Tanzania (MAT) na kumalizika hivi karibuni
Akizungumza jana kwenye kikao cha Kamati ya mkoa wa Rukwa kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa huo alisema kuwa Madaktari na wauguzi wa Rukwa wametujari na kutuheshimu sana
Mhandisi Manyanya alisema kuwa wanataaluma hao wamejari uhai wa watanzania wenzao kwa kudiriki kufanya kazi yao ya kuwatibu wagonjwa na kutoa huduma stahiki za kiafya bila kinyongo wakati wenzao wakiwa kwenye mgomo
Alisema kuwa kitendo chao cha kuwajali  wananchi katika kipindi hicho kigumu hivyo , mkoa unajipanga ili kuona namna bora ya kuwapongeza Madaktari na wauguzi wa mkoa wa Rukwa kwa heshima na utu waliouonyesha katika wakati huo na sasa ambapo mgomo nchi nzima umemalizika
Alieleza kuwa wakati wa mgomo maeneo mengine huduma zilisitishwa na kupelekea watu wengi kupata usumbufu, ulemavu wa maisha, vifo na madhara mengine mengi hali ambayo imelitia doa Taifa hili ambalo linajali misingi ya haki za binadamu
"Watanzania tunapaswa tuimarishe maadili ya kazi zetu na kujali utu wa binadamu kwani inasikitika Madaktari na wauguzi wanashindwa kuwahudumia wagonjwa na badala yake wanaendekeza mgomo wenye maslahi binafsi huku wakiwaacha wagonjwa wakifa kwasababu ya kushindwa kumaliza madai yao kwa njia ya kukaa mezani"alisema Mhandisi Manyanya
Alifafanua zaidi kuwa haki ya kuishi ni haki kubwa kuliko zote na kwamba hakuna mtu mwenye mamlaka ya kuondoa uhai wa mwenzake kwa sababu yoyote ile kwani mwenye uwezo na mamlaka hayo ni mwenyezi mungu peke yake ni vema kazi yake tukamuachia yeye
Aliesema kuwa mkoa wa Rukwa unampongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kumaliza mgomo huo wa Madaktari nchini na kuahidi kutekeleza baadhi ya madai yao  hilo ndilo jambao ambalo watanzania wengi walikuwa wanarisubiri kutokana na kuchoka kwa madhara yaliyokuwa yanajitokeza kutokana na mgomo huo ,hivyo Madaktari wale waliogoma warejee kazini na kuendelea na kazi wakati madai yao yanafanyiwa kazi na Serikali
MWISHO

KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA RUKWA CHAMALIZIKA KWA KUWEKA MIKAKATI MBALIMBALI YA MAAZIMIO

 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akitoa hotuba ya ufunguzi wa kikao cha RCC

HOTUBA YA UFUNGUZI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA INJINIA STELLA MANYANYA KWENYE KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA (RCC) TAREHE 14/ 03/ 2012

Mhe. Mwenyekiti wa CCM, Ndugu H. Matete,
Katibu Tawala wa Mkoa, Ndugu Salum M. Chima,
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa,
Waheshimiwa, Wakuu wa Wilaya,
Bibi Joyce Mgana,
na Dr.
Rajabu Lutengwe,
Wah. Wabunge,
Meya, na Wenyeviti wa Halmashauri zote za Mkoa wa Rukwa,
Wakurugenzi,
Wakuu wote wa Idara,
Wageni Waalikwa,
Mabibi na Mabwana.
Rukwa Ruka!, Sumbawanga Ng’ara!
·        Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuweka hai.
·        Pili napenda kuwakaribisha katika Kikao hiki, na poleni kwa safari kwa wale mliotoka mbali.
Nachukua pia nafasi hii kuwakaribisha watumishi wageni wote waliohamia katika Mkoa wetu katika kipindi cha kuanzia Oktoba mpaka leo.  Ni imani yangu kuwa wataungana na viongozi, pamoja na watumishi wenzao kuhakikisha kuwa Rukwa inaruka na Katavi inaimarika zaidi.

Waheshimiwa wajumbe,
Nichukue pia nafasi hii kwanza kuwashukuru sana ninyi Wajumbe kwa niaba ya wananchi wote kwa jinsi tulivyoshirikiana katika matukio yote makuu na ya muhimu katika Mkoa wetu wa Rukwa na Katavi.  Naishukuru sana Kamati yangu ya Ulinzi na Usalama, Chama cha CCM na Vyama vya Siasa, Wakuu wa Idara mbalimbali, Watumishi wote, Wafanyabiashara, Wawekezaji na Wananchi wote kwa ujumla, kwa kufanikisha shughuli hizo kwa umakini mkubwa.
Shughuli kuu zilizofanyika ni pamoja na:-
1.      Kongamano la Uwekezaji la Ukanda wa Ziwa Tanganyika ambalo lilifanyika tarehe 17/10/2012 mjini Mpanda, Kongamano hilo lilifunguliwa na Mgeni wetu rasmi Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.  Waliohudhuria wengine ni pamoja na Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda Mbunge wetu, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mary Nagu, Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji katika Ofisi ya Rais, Mabalozi 34 kutoka nchi mbalimbali, Wakuu wa Mikoa 3 kutoka Kigoma, Mheshimiwa Issa Machibya, ambaye pia alikuwa muandaaji wa Kongamano, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mheshimiwa Fatma Mwase, na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Joseph Simbakalia, pia Wadau mbalimbali wa makampuni na mashirika ya umma, na kwa namna ya pekee wananchi wenyewe.
Kwa upande wa Vyama vya Siasa, Chama Tawala CCM chini ya Mwenyekiti wake wa Mkoa Ndugu H. Matete walishiriki, pamoja na Chama cha Chadema.
2.      Mapokezi ya Mwenge yalifanyika kwa ufanisi mkubwa.
3.      Tulifanya Tamasha la Wana Rukwa na Katavi kuanzia tarehe 25 – 27/11/2011 katika kijiji cha Makumbusho Jijini Dar es Salaam. 
Tamasha hilo lilifana sana, hivyo napenda kuwapongezeni wote mlioshiriki katika kuandaa tamasha hilo, wakiwemo wazee wa mila, Viongozi wa Serikali pamoja na Wafanyabiashara wetu, na nimtaje ndugu Sumri kwa kutuweka vizuri kiusafiri

Aidha, nawashukuru na kuwapongeza sana Wana Rukwa na Katavi, waishio Dar es Salaam, chini ya Mwenyekiti Bibi Mwangaza Mwanisongole kwa kufanikisha tamasha hili kwa kiwango kikubwa.
Tamasha hili lilifunguliwa na Mheshimiwa Dkt Mohammed G. Bilal Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kufungwa na Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda (Mb) na Waziri Mkuu.
4.     Miaka 50 ya Uhuru tuliadhimisha mjini Namanyere katika Halmashauri ya Wilaya ya  Nkasi 9/12/2011.
5.     Tulipata Mgeni, ambaye ni Makamu wa Rais Dkt Mohammed Gharib Bilal kuanzia tarehe 18 – 24/2/2012 katika mikoa yetu ya Rukwa na Katavi.  Ziara yake ilikuwa ya mafanikio makubwa kutokana na ushirikiano mkubwa kati ya Chama Tawala na Serikali, Vyama vingine vya Siasa pamoja na wananchi wote waliohudhuria kwa wingi kwenye mikutano, kwa utulivu na heshima kubwa.  Nawashukuruni sana.
6.  Maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani yalifanyika tarehe 8/3/2012 Mjini Sumbawanga, na yalikuwa mazuri.
         Pamoja na taarifa hizo ili ngoma inoge kuna wenyewe, hivyo basi nawashukuru sana Waandishi wa habari wa Mkoa wangu wa Rukwa pia Katavi pamoja na rafiki zao wa vyombo mbalimbali kwa jinsi wanavyotuunga Mkono na kuisaidia serikali ya Mkoa wa Rukwa, na taifa kwa ujumla. Pia navishukuru vikundi vya ngoma.
Mambo mengine muhimu.
1.   Barabara zetu zinaendelea kujengwa vizuri kwa kiwango cha lami, japo katika zile tunazogharimia sisi wenyewe (Serikali ya Tanzania) zinakabiliwa na upungufu wa fedha kutokana na majukumu mbalimbali ya serikali ikiwemo umeme, madeni ya watumishi kama Madaktari, Walimu n.k.
2.   Mkoa umeanzisha mpango wa Sumbawanga Ng’ara tuuunge mkono pamoja na Halmashauri zote zing’are.
3.   Napenda kuwataarifu kuwa madaktari wetu wa Mkoa wa Rukwa pamoja na wauguzi wote wa Mkoa wetu kwa kweli hawakugoma kabisa katika migomo yote miwili.  Wametujali sana wana Rukwa, na wametupa heshima kubwa sana na wamethamini sana uhai na maisha yetu.  Mkoa utaangalia namna bora zaidi ya kuwapongeza. Lakini kwa kuanzia naomba niwapongeze wote katika Kikao hiki.
Kwa namna ya pekee nakiomba kikao hiki kiazimie pongezi kwa Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jinsi alivyoshughulikia mgomo huu wa madaktari na kwa kuridhia kutupatia Mkoa mpya wa Katavi baada ya Mkoa wetu kugawanywa.
Waheshimiwa wajumbe, kutokana na ukubwa wa jiografia na maumbile ya Mkoa wetu tunashauri kuwa serikali ione uwezekano wa kuongeza ukomo wa bajeti.  Na kwa vile Mkoa wa Rukwa umegawanywa, basi ni vema Mkoa wa Rukwa uendelee na ukomo wa zamani na Mkoa wa Katavi upewe ukomo mpya. 
Waheshimiwa wajumbe, katika kuandaa bajeti ya mwaka huu kama ilivyoelezwa na Katibu Tawala wetu ndugu Chima, Mkoa unaazimia kuweka kipaumbele katika kumaliza miradi iliyopo na kuwa na miradi michache ili ikamilike na kutoa matukio badala ya kuwa na miradi mingi isiyoisha.  Hali hiyo ni kuharibu fedha kidogo tunayopata bila kupata matukio mazuri.
Waheshimiwa wajumbe tunayo mengi ya kujadili, muda hautoshi, na naona hali ya RAS wetu kimfuko ni mbaya, lakini kikao hiki ni muhimu sana ikizingatia kuwa ni dira ya bajeti.  Naomba tuchangie kwa makini ili kuufanya mkoa wetu uruke.
Kikao kimefunguliwa

 Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho, Ignas Malocha Mbunge wa Jimbo la Kwela, Ally Kessy Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini, na Suleiman Kakoswe Mpanda Vijijini wakifuatilia kikao hicho.
 Baadhi ya wajumbe na wageni waalikwa wa kikao hicho wakisikiliza neno la ufunguzi wa kikao hicho likitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya (hayupo pichani).

Meneja wa Sido Mkoa wa Rukwa Martin Augustino Chang'a akiwa anafuatilia kwa umakini kikao hicho. Wengine ni baadhi ya wataalamu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa. 

Wednesday, March 14, 2012

KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA RUKWA CHAMALIZIKA NA KUAINISHA MAAZIMIO MBALIMBALI

Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akitoa hotuba ya ufunguzi. 
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Dkt. Rajab Rutengwe kulia akiteta na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Joyce Mgana wakati kikao hicho kikiwa kinaendelea
Wajumbe wa kikao hicho wakiendelea kusikiliza kwa umakini hoja mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa kwenye kikao hicho
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Rukwa Florian Kabaka akiwasilisha taarifa ya Idara yake kwenye kikao hicho 
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Dkt. Rajab Rutengwe akizungumza kwenye kikao hicho, kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Joyce Mgana.

KWA PICHA ZAIDI

WATATU WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA MAUAJI

Na,Augustino Chindiye Tunduru

WATU watatu wamefikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma kwa  tuhuma za kumuua kwa kukusudia marehemu Said Ally Kaunya.

Walioshitakiwa kwa tuhuma hizo katika Shauri hilo la mauaji namba 3/2012 ni Rajab Kalanje Namdoa (82), Asha Rajab (44) na Yasin Mohamed (52) ambao wamedaiwa kuwa  walifanya kosa hilo kwa kukusudia,

Akiwasomea shauri hilo Mwendesha mashtaka Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Asp Alfred Kasoro alisema kuwa kwa pamoja watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Machi 8 mwaka huu katika kijiji cha Nalwale kilichopo katika Kata ya Nandembo wilayani humo.

Kutokana na Shauri hili linalowa kabiliwa watuhumiwa hao kuwa nje ya uwezo wa kusikilizwa na mahakama hiyo,  watuhumiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote.

Hata hivyo  hakimu wa mahakama hiyo  Goefre Mhini aliwaamuru kwenda Lumande hadi Machi 26 mwaka huu wakati shauri hilo litakapo somwa tena.

Kwa mujibu wa Taarifa za tukio la mauaji hayo yalitokea kwa sababu ya kugombea mashamba katika kijiji cha Nalwale katika Kata ya Nandembo ambapo Mtuhumiwa namba moja  amedaiwa kufanya tukio hilo ili kumaliza ugomvi huo.

Kwa mujibu wa taarifa hizo marehemu alidaiwa kuvamia shamba la mtuhumiwa namba moja nakuanza kulilima miaka 8 iliyopita ambapo katika kipindi chote hicho kesi ilikuwa ikiendelea katika hatua mbalimbali na kwamba kabla ya kifo hicho marehemu alikuwa ametoka kushinda kesi hiyo katika mahakama ya Ardhi ya Mkoa iliyopo katika manispaa ya Songea.

Mwisho.

MBUNGE WA VITIMAALU MKOA WA RUVUMA, MNEC NA MKUU WA MKOA WA RUKWA MHANDISI STELLA MANYANYA AWA MBUNGE WA KWANZA KUTEMBELEA JENGO LA POLISI WANAWAKE LINALOJENGWA NA WANAHARAKATI NA KUAHIDI KUTOA MILIONI 1

 Kutoka kushoto ni Katibu wa UWT Mkoa wa Ruvuma Mariam Yusuph, Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Hamza Temba, Mwanaharakati wa TGNP Kanda ya Kusini na Mhariri Msaidizi wa Tujifunze Kanda ya Kusini Juma Nyumayo, Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Ruvuma, Mnec na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya, Mwanaharakati wa TGNP Kanda ya Kusini, Mwandishi wa Star Tv/ Redio Free na Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa jengo la Polisi wanawake mkoa wa Ruvuma Adam Nindi, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Fadhiri Chacha 
 Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Ruvuma Kuruthum Mhagama, Katibu wa UWT Mkoa wa Ruvuma Mariam Yusuph, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mnec na Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Stella Manyanya akiwa na wajumbe wengine wa Baraza la Uwt mkoa wa Ruvuma wakitembelea jengo maalum la kusikiliza matatizo ya wanawake (Dawati la Jinsia) lilopo karibu na kituo kikuu cha Polisi Mjini Songea
 Mwanaharakati wa TGNP Kanda ya Kusini na Mhariri Msaidizi wa Tujifunze Kanda ya Kusini Juma Nyumayo akitoa maelezo ya awali ya jengo hilo kwa viongozi wa Jumuiya ya UWT Mkoa wa Ruvuma walipotembelea jengo hilo wakiongozwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mnec na Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Stella Manyanya
 Mwanaharakati wa TGNP Kanda ya Kusini, Mwandishi wa Star Tv/ Redio Free na Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa jengo la Polisi wanawake mkoa wa Ruvuma Adam Nindi akitoa maelezo ya ujenzi wa jengo hilo

 Viongozi wa Jumuiya ya UWT Mkoa wa Ruvuma walipotembelea jengo hilo wakiongozwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mnec na Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Stella Manyanya wakisikiliza maelezo ya jengo hilo
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mnec na Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Stella Manyanya akizungumza kwa furaha baada ya kutembelea ujenzi wa jengo hilo ambalo linapaswa kuigwa na mikoa mingine ambapo aliahidi kutoa milioni 1 kuchangia ujenzi huo na kushauri kuwa mara litakapo kamilika licha ya kutoa ushauri wa kisheria, ujinsia pia kiwe kioo cha maendeleo kwa wanawake kwa kutumia sheria watakazojifunza kupitia dawati hilo
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mnec na Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Stella Manyanya akiondoka eneo hilo baada ya kukamilisha kazi yake ya kukagua jengo la dawati la jinsia(mtandao wa Polisi Wanawake)

TAARIFA YA KAMATI YA MAUAJI MKOA WA RUVUMA YATOLEWA NA RC MWAMBUNGU

MKUU WA MKOA WA RUVUMA SAID MWAMBUNGU

WAANDISHI WA HABARI WAKITAFUTA PICHA YA MNATO WAKATI MKUU WA MKOA WA RUVUMA SAID MWAMBUNGU AKITOA TAARIFA YA KAMATI
Na Gideon Mwakanosya ,Songea.
KAMATI iliyoundwa na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu kuchunguza chanzo cha mauaji ya watu waliouwawa kuhusiana na imani za kishirikina na kusababisha vurugu za watu kuandamana na iliyopolekea mauaji ya watu wawili imekamilika.

Kamati hiyo iliyoundwa na watu wanane ikiongozwa na katibu tawala msaidizi miundombinu Severin Tossi ili Serikali iweze kuchukuwa hatua na kuhakikisha mambo kama hayo hayatokei tena

Akitoa taarifa hiyo Mwambungu alisema kuwa wale wote waliotuhumiwa kwenye mauaji hayo wamefikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Hata hivyo alisema kuwa kamati hiyo imeshindwa kuthibitisha uvumi wa watu kumi na nne waliouwawa kwa kuhusishwa na imani za kishirikina na kwamba tabia ya watu kueneza uvumi wa uongo ni mbaya sana kwani inagharama kubwa kwa wananchi na kuongeza kuwa kamati hiyo imefatilia na kupata taarifa kuwa hakuna mtu yoyote aliyenyofolewa viungo vya siri .

“Naomba nitoe rai kwenu kuwa tabia hii ya uenezaji wa uvumi ni mbaya sana kwa sababu inagharama kubwa sana kwa wananchi ambao wanashindwa kufanya kazi zao za kila siku katika ujenzi wa Taifa.”alisema Mwambungu.

Amesema,tayari elimu kwa wananchi imeshatolewa na wananchi wameanza kufanya kazi ya ulinzi shirikishi kwa kushirikiana na polisi kata ambapo kazi ya ulinzi na kwamba  mitaa yote ya Manispaa ulinzi umeimalishwa.

Mwambungu ameongeza kuwa, kwa sasa hali ya utulivu na usalama katika mkoa wa Ruvuma imerejea kama awali ambapo wananchi wanaendelea na shughuli zao za kila siku kama kawaida .

“Napenda kuwahakikishia wananchi wa mkoa wa Ruvuma na watu wanaoishi nje ya mkoa wa Ruvuma kuwa Songea ni salama na wananchi wanaendelea na shuguli zao kama kawaida, nawashukuru wananchi kwa ushirikiano mkubwa ambao wameutoa pia wanahabari kwa kusaidia kurejesha hali ya utulivu na amani ”alisema

Aidha, amewataka wananchi kuelewewa umuhimu wa kujilinda na kufata sheria ikiwa ni pamoja na kuacha hulka ya kujichukulia hatua mkononi ,ikiwa ni pamoja na kuacha kujihusisha na tabia za uvumi na hisia za kishirikina ili kuimarisha amani na utulivu.
MWISHO.

NYUMBA ZAIDI YA 300 ZABOMOLEWA NA MVUA WILAYANI TUNDURU

MKUU WA WILAYA YA TUNDURU JUMA MADAHA

Na Augustino Chindiye,Tunduru
ZAIDI ya Nyumba 300 zimeripotiwa kubomoka  katika Tarafa ya Mlingoti Wilaya ya  Tunduru Mkoani Ruvuma kufuatia mvua kubwa zinazo endelea kunyesha kwa takribani siku tatu sasa na kusababisha wakazi wa kaya hizo kukosa makazi.

Sambamba na tukio hilo pia. mvua hizo zimesababisha miundombinu ya barabara za kwenda vijijini  kujifunga kutokana na maji kujaa kiasi cha kutishia kubomoka  huku madaraja yakiwa hayapitiki kutokana na maji kufurika na maji kupita juu ya daraja .

Taarifa kutoka kwa madereva wanaofanya safari katika barabara kuu iendayo Songea zinasema kuwa maji yamejaa sana na kupita juu ya Daraja la Mto Masonya hali ambayo imesababisha magari yao kusitisha safari za kwenda na kuingia mjini Tunduru.

Adha nao madereva wanaofanya safari za kwenda katika vijiji vya Lukumbule,Mbesa  Nalasi Mchoteka nako hakufai kutokana na maji katika mto Msinjewe  kujaa sana na kutishia magari ya abiria kushindwa kupita huku taarifa kutoka katika Barabara iendeyo Masasi Mkoani Mtwara na Jijini Dar es salaam zikisema kuwa kikwazo kipo katika daraja la Mto Muhuwesi ambapo pia hapapitiki hali inayo onesha kuwa mji wa Tunduru hivi sasa upo kisiwani .

Akizungumzia maafa hayo Afisa Tarafa wa tarafa ya Milingoti  Manfred kahobera Hyera mbali na kukiri kuwepo kwa wimba la maafa hayo alisema kuwa hali katika mji wa Tunduru ni mbaya sana kiasi cha kutishia maisha ya wakazi wake.

Akifafanua taarifa hiyo Hyera alisema kuwa  hadi sasa amepokea taarifa kutoka kwa watendaji  kata tatu za miji huo Nanjoka zimeripotiwa kubomoka  nyumba 50, kata ya Masonya Nyuma 52 na majengo Nyuma 32 huku taarifa kutoka katika Tarafa ya Ligoma zikidai kuwa hali ni mbaya , chanzo cha matukio hayo kikidaiwa kuwa nyumba
hizo zilijengwa kwa tofari mbichi.

Juhudi za kupata taarifa za uharibifu ulisaabishwa na Mvua hiyo katika meneo mengine ya Wilaya hiyo zilishindikana kutokana na Kaimu Mkuu wa Wilaya hiyo  Martin Mulwafu kudaiwa kuwa yupo katika safari ya kufuatilia taarifa hizo vijjini.
Mwisho

Monday, March 12, 2012

MBUNGE WA VITIMAALU MKOA WA RUVUMA, MNEC NA MKUU WA MKOA WA RUKWA MHANDISI STELLA MANYANYA AHUDHURIA KIKAO CHA BARAZA LA UWT MKOA WA RUVUMA NA KUTOA SHILINGI 150000

Mbunge wa Vitimaalum mkoa wa Ruvuma,Mnec na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiwasalimia wajumbe wa Baraza la Uwt Mkoa wa Ruvuma katika kikao kilichofanyika juzi katika ukumbi wa CCM mkoa wa Ruvuma, wa kwanza kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu, wapili Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma Corneus Msuya, watatu ni Mwenyekiti wa Uwt Mkoa wa Ruvuma Kuruthum Mhagama
 Wajumbe wa Baraza la UWT Mkoa wa Ruvuma wakimpa zawadi na kumpongeza Mbunge wa Vitimaalum mkoa wa Ruvuma,Mnec na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya kwa kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi
 Mbunge wa Vitimaalum mkoa wa Ruvuma,Mnec na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiwashukuru Wajumbe wa Baraza la UWT mkoa wa Ruvuma kwa zawadi na pongezi walizozitoa kwake wakati wa kikao cha Baraza la Uwt mkoa wa Ruvuma kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM mkoa wa Ruvuma juzi
 Wajumbe wa kikao cha Baraza la UWT Mkoa wa Ruvuma wakicheza wimbo wa chama na Mbunge wa Vitimaalum mkoa wa Ruvuma,Mnec na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya ikiwa ni ishara ya kufurahi pamoja katika kuanza mwaka wa uchaguzi ndani ya chama

 Wajumbe wa kikao cha Baraza la UWT Mkoa wa Ruvuma wakisikiliza hoja mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa na Katibu wa UWT mkoa wa Ruvuma Mariam Yusuph hayupi pichani kwenye kikao hicho kilichofanyika juzi
 Wakwanza toka kushoni Katibu wa CCM Wilaya ya Songea Lidya Gunda, wapili Katibu wa CCM Wilaya ya Songea Mjini Alfonce Siwale, watatu ni Katibu wa UVCCM Mkoa wa Ruvuma Mwajuma Rashid, wanne Katibu wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Ruvuma Rajab Honde wakifuatilia kikao hicho
 Kamati ya utendaji wa UWT mkoa wa Ruvuma ambao ndio Sekretarieti ya kikao hicho wakiendelea na majukumu yao wakati kikao hicho kikiendelea
 Wajumbe wa kikao hicho wakiendelea na kikao hicho
 Wajumbe wa kikao cha Baraza la UWT Mkoa wa Ruvuma wakimkabidhi zawadi na kumpa pongezi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu kwa kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kushika Mkoa wa Ruvuma
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akiwashukuru wajumbe wa kikao cha Baraza la UWT Mkoa wa Ruvuma kwa kumpatia zawadi na kumkaribisha Ruvuma, wa kwanza kulia ni Mbunge wa Vitimaalum mkoa wa Ruvuma,Mnec na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya, wa kwanza kutoka kushoto ni Katibu wa UWT Mkoa wa Ruvuma Mariam Yusuph, wa pili ni Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Ruvuma Kuruthum Mhagama wapili Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Corneus Msuya
 Mbunge wa Vitimaalum mkoa wa Ruvuma,Mnec na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiwa na Katibu wa CCM mkoa wa Ruvuma Emmanuel Mteming'ombe wakati Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akiwashukuru wajumbe wa kikao hicho kwa kumpatia zawadi
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akimkabidhi Katibu wa UWT Mkoa wa Ruvuma Mariam Yusuph jumla ya shilingi 250000 ikiwa shilingi 150000 kutoka kwa Mbunge wa Vitimaalum mkoa wa Ruvuma,Mnec na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya na shilingi 100000 kutoka kwake

Saturday, March 10, 2012

SUFA WAANZA KUTOA FOMU ZA KUGOMBEA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI

                                                Katibu Msaidizi wa SUFA Godfrey Mvula
Na Gideon Mwakanosya, Songea

CHAMA cha mpira wa miguu Manispaa ya Songea(SUFA) kimeanza kutoa fomu za kuwania nafasi mbalimbali za  uongozi wa chama hicho, uchaguzi ambao umepangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.

Akizungumza mjini hapa jana Katibu Msaidizi wa SUFA, Godfrey Mvula alisema kuwa pamoja na utoaji wa fomu za kugombea nafasi mbalimbali za  uongozi wa chama hicho, bado kamati ya utendaji wa SUFA kimepanga kuteua kamati ya kusimamia uchaguzi huo ambao utafanyika Machi 30 mwaka huu katika ukumbi ambao utakaopangwa.

Alisema wagombea wa nafasi hizo wanatakiwa wawe angalau na elimu sio chini ya kidato cha nne na awe mtu anayejihusika na soka kwa kuongoza vilabu  ili kujenga ufanisi na uelewa zaidi katika kufanikisha na changamoto ya maendeleo ya soka katika Manispaa hiyo.

Alisema wagombea wote watakaojitosa kuchukua fomu na kuzirejesha watafanyiwa usaili wao wa mwisho Machi 25 kabla ya kuingia katika uchaguzi wa kuwania nafasi hizo za uchaguzi ambao watakaa madarakani kwa muda wa miaka mitatu.

Alisema SUFA kwa sasa inaongozwa na Mwenyekiti wake Gorden Sanga na ina vilabu vya soka 35 ikiwemo Majimaji ambavyo vimesajili kupitia msajili wa vyama vya michezo na vilabu nchini.
  MWISHO

RC MANYANYA ASHUSHA PRESHA YA WANANCHI WA MDUNDUALO KUHUSU MAENEO YAO KUCHUKULIWA NA WACHIMBAJI WA MAKAA YA MAWE NGAKA WILAYANI MBINGA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya ambaye pia ni Mbunge wa Vitimaalu Mkoa wa Ruvuma akizungumza na wananchi wanaozunguka mgodi wa makaa ya mawe ya Ngaka Wilayani Mbinga kuhusu mgogoro wa wananchi na wawekezaji katika mgodi huo

Wananchi wanaozunguka mgodi wa uchimaji wa makaa ya mawe wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Stella Manyanya



WATU WAWILI WAMEFARIKI KATIKA MATUKIO MAWILI TOFAUTI WILAYANI TUNDURU

Na,Augustino Chindiye Tunduru

WATU wawili wamefariki dunia katika  matukio tofauti yaliyotokea wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma likiwemo tukio la kuuawa kwa kushambuliwa kwa mapanga kutoka na kilichodaiwa kuwa chanzo chake ni ugomvi wa kugombea eneo la kulima na mwingine kupigwa na radi.

Taarifa za tukio la Mauaji ya kugombea shamba lilitokea katika kijiji cha Nakawale katika Kata ya Nandembo ambapo Mtu aliyeuawa amefahamika kwa jina la Said Kaunya.

Akizungumzia tukio hilo mjomba wa marehemu Yusuph Mangalai alisema kuwa marehemu alikumbwa na maswahibu hayo usiku wa kuamkia machi 9 mwaka huu ambapo baada ya maharamia hao kutekeleza unyama huo waliuficha mwili wa marehemu kwa kuuzika pembeni mwa bwawa la maji
hali ambayo iliwapa wakati mgumu wanafamilia.

Hata hivyo Mangalai amewapongeza watu wote walioshiriki katika msako uliofanikisha kupatikana kwa mwili wa marehemu na kuuzika katika makaburi ya Njasi Mjini Tunduru.

Kwa mujibu wa taarifa hizo tukio la pili lililo husu kifo cha Mkulima kupigwa radi kilitokea katika kijiji cha Kangomba Wilayani humo ambapo aliye fariki dunia katika tukio hilo amefahamika kwa jina la Said Abubakari(43),

Akizungumzia tukio hilo Kaka wa marehemu Ally Hatibu alisema kuwa Marehemu alikumbwa na mkasa huo ulimpata wakati akipandikiza mihogo
shambani kwake.

Alisema katika tukio hilo marehemu aliunguzwa vibaya kuanzia chini ya mguu hadi kichwani upande wa kulia na kufariki papo hapo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa ruvuma Naftali Mantamba amethibitisha kuwepo kwa matukio hayo na kueleza kuwa polisi wanendelea na uchunguzi
ili sheria ifute mkondo wake.


Mwisho

WAKULIMA WA KOROSHO WILAYA YA TUNDURU WAENDELEA KULILIA SOKO LA ZAO LAO

MKUU WA WILAYA YA TUNDURU JUMA MADAHA

Na,Augustino Chindiye,Tunduru

WAKATI Serikali ikiwa imetoa tamko la kuwafutia Leseni Wanunuzi wa
Korosho nchini, Wakulima wa zao hilo Wilayani Tunduru  Mkoani Ruvuma
wamehoji hatima ya Soko la Korosho zao.

Hayo yalitokea katika kikao cha wadau wa Korosho kilichofanyika katika Ukumbi wa Chama Kikuu cha Wakulima (TAMCU) na kuwashirikisha Waandishi na Wenyeviti wa Vyama vya msingi vya wakulima wa zao hilo na wakaituhumu Serikali ya awamu ya nne kuwa imekuwa butu katika  kutoa maamuzi hali ambayo inawafanya Wanachi kukata tamaa juu ya utendaji wake.

Wawakirishi wa Wakulima kutoka Chama cha Msingi  Litungulu Mohamed
Matoto na Yasini Masiano wa Chichilimbe walisema kuchelewa kutolewa
kwa maamuzi kunako fanywa na Serikali kumewafanya viongozi wa vyama
vya msingi kuishi katika hofu ya kufanyiwa fujo na wakulima wao.

Awali akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa Chama kikuu cha Wakulima Wa
Korosho (TAMCU) Mohamed Katomondo mbali na kupongeza hatua zilizo
chukuliwa na Serikali kwa kunukuu kauli ya Makampuni hayo
kunyang`anjwa Leseni bila majadiliano iliyotolewa na Rais wa Jamuhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete na kuongeza kuwa katika
tamko hilo hakukuwa na kipengele wala maelekezo yaliyozungumzia hatima
ya Korosho za wakulima.

Aidha katika taarifa hiyo Katomondo alionesha mashaka ya kuendelewa
kwa zao hilo kutokana na wakulima wengi kukatishwa tamaa na utaratibu
wa mfimo wa Stakabadhi ghalani wakidai kuwa mfumo huo unanyonya nguvu
zao.

Akitoa taarifa ya mdororo wa Korosho hizo Meneja wa Chama Kikuu cha
Ushirika wa Wakulima wa Korosho Wilayani Tunduru (TAMCU)Imani
Kalembo alisema kuwa katika msimu wa Mwaka 2011/2012 chama hicho kupitia
vyama vya msingi vya wakulima takwimu zinaoneshja kuwa uzalishaji
umeongezeka kutoka kilo 4,135,042 za mwaka 2010/2011 hadi kilo 7,570,000.

Kalembo aliendelea kufafanua kuwa hadi kufikia Februari 29 mwaka huu
takwimu zinaonesha kuwa Korosho zilizopokelewa Maghalani ni Kilo
6,842,446 na kilo 641,230 zipo katika maghala ya watu binafsi na
zingine zipo nje ya ofisi za chama hicho na kilo 86,324 bado zipo
mikononi mwa wakulima huku takwimu hizo zikionesha kuwa ni kilo
1,890,384 tu ndizo zilizouzwa katika mnada mmoja kati ya minada tisa
iliyofanyika hali inayotishia chama hicho kushindwa kulipa malipo ya pili ya wakulima ambapo TAMCU inadaiwa Jumla ya Shilingi 2,441,870,350/= .

Taarifa hiyo iliendelea kueleza kuwa deni hilo limetokana na chama
hicho kununua jumla ya Kilo 6,976,821 ambazo Chama hicho kupitia vyama
vya msingi vimeweza kuzilipia kwa asilimia 70% pekee, sambamba na Deni
la Shilingi 608,260,000 zilizotokana na Mkopo wa  kilo 506,855 za Korosho za zilizo kopeshwa na wakulima kwa vyama vya Msingi.

Kalembo aliendelea kueleza kuwa wakati hayo yakiendelea Chama
hicho pia  kinakabiliwa na changamoto ya Chama kushindwa kununua jumla
ya kilo 86,324 zenye Dhamani ya Shilingi Milioni 17,264,800 ambazo
bado zipo mikononi mwa wakulima wa zao hilo hali inayo endelea
kuwakatisha tamaa ya kuendelea na kilimo hicho

Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni Mjini Songea Katibu
Mtendaji wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika Wilgisi Mbogoro,
alisema takwimu za Korosho zote zilizokwama baada ya wanunuzi
kutunisha misuli kuzinunua ni kilo 72,978,340 zenye thamani ya
shilingi Bilioni 113.7

Wakitoa salamu za Serikali Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Madaha namlajisi msaidizi wa vyama vya Ushirika Mkoani Ruvuma WatsonNganiwa walisema kuwa msimamo wa Serikali ni kuhakikisha kuwa Korosho zote zinanunuliwa kutoka kwa wakulima na wakatumia nafasi hiyo kuwaomba wakulima kuwa na subira wakati taratibu za mchakato wa kufanikisha hayo zikiendelea.
Mwisho

Friday, March 9, 2012

MKUU WA MKOA WA RUKWA MHANDISI STELLA MANYANYA AKUTANA NA MKUU WA MKOA WA RUVUMA SAID MWAMBUNGU KUJADILIANA MAENDELEO YA BARABARA ZA MIKOA HIYO NA VIONGOZI WA MCC

 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na kiongozi wa miradi ya MCC Mzee Mchomvu walipokutana kwenye kikao maalumu kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
 Wa kwanza kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu, wa pili Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya wakijadiliana maaendeleo ya barabara katika mikoa hiyo kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na Kiongozi wa Miradi ya MCC
 Wakuu wa Mikoa ya Rukwa Mhandisi Stella Manyanya na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu wakiagana na ujumbe wa viongozi wa MCC baada ya kumalizika kwa kikao chao maalum kilichofanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

Kiongozi wa miradi ya MCC Mzee Mchomvu akisalimiana na Viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Ruvuma baada ya kuzungumza na wakuu wa Mikoa ya Rukwa na Ruvuma