About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Thursday, September 15, 2011

MAJAMBAZI WAPORA MILIONI 5 NA KUJERUHI WAFANYABIASHARA WATATU NA KISHA KUTOKOMEA KUSIKOJULIKANA

                                   Na Gideon Mwakanosya, Songea
 
MFANYABIASHA mmoja Habiba Kazembe (45) mkazi wa Mtaa wa Muungano uliopo Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma amevamiwa na kundi la watu wanaosaidikiwa kuwa ni majambazi na kuporwa fedha taslimu shilingi milioni 5 akiwa amelala chumbani kwenye nyumba ya kulala wageni ya Mataya iliyopo katika kijiji cha Lusewa Wilayani Namtumbo na wafanya biashara wengine watatu wamejeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi na majambazi hayo ambayo yalitoroka na kutokomea kusiko julikana.
 
Walio jeruhiwa kwa kupigwa na risasi wametajwa kuwa ni Edga Kayombo mfanya biashara Mkazi wa Eneo la Lizaboni Manispaa ya Songea, Michael Komba mfanya biashara ambaye ni Mkazi wa Mahenge Songea Mjini na Muhudumu wa nyumba ya kulala wageni wa nyumba ya Mataya Mariamu Azizi .
 
Habari zilizopatikana mjini hapa ambazo zimethibitishwa na Majeruhi zimeeleza kuwa tukio hilo  limetokea  September 15 majira ya saa za usiku huko katika Kijiji cha Lusewa kilichopo Wilayani Namtumbo ambako inadaiwa majambazi ambao idadi yao haikuweza kufahamika mara moja wakiwa na silaha aina ya SAR na SMG walivamia nyumba ya kulala wageni  kisha waliwajeruhi watu watatu kwa kuwapiga na risasi watu watatu sehemu mbalimbali za miili yao na kumpora mfanyabiashara mmoja shilingi milioni tano nakutokomea nazo.
 
Mmoja wa majeruhi Edga Kayombo ameuambia mtandao huu wa http://www.stephanomango.blogspot.com/  jana mchana kuwa yeye amejeruhiwa kwa  kupigwa risasi mkono wa  kushoto  akiwa amelala kwenye gari ambalo lilikuwa nje ya nyumba ya kulala wageni baada yakukosa vyumba .
 
Amefafanua  kuwa  kundi hilo la watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi walivamia nyumba hiyo ya kulala wageni saa 9 usiku yeye akiwa kwenye gari ghafla alisikia  mlio  wa  risasi  zikipigwa ndani  ya nyumba  ya kulala  wageni .
 
Amesema  kuwa  baada ya  kusikia  milio  ya risasi  aliondoka  na  kwenda ndani ya nyumba ya kulala wageni ambako walikuwa wamelala  wafanyabiashara  wenzake   lakini akiwa anatoka  kwenye  gari  hilo  alikutana na watu watatu  wakitokea kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni wakiwa na siraha wameshika  mikononi ambapo mmoja kati yao alimpiga risasi kwenye mkono wa kushoto.
 
Ameeleza zaidi  kuwa  majambazi hao baadaye waliondoka na kutokomea kusikojulikana na  yeye alianza kupiga kelele kwa ishara ya kuomba msaada ambapo majirani walifika kwenye eneo la tukio kisha waliwachukua majeruhi hadi kituo cha polisi cha lusewa ambako walipatiwa hati ya matibabu ambako walikimbizwa kwenda hospitali ya serikali ya Mkoa kwa matibabu zaidi.
 
Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Mkoa Songea Dkt Benedict Ngaiza ameiambia nipashe kuwa majeruhi hao walipokelewa majira ya saa 5 na nusu asubuhi ambapo alibainisha kuwa Kayombo amepigwa risasi kwenye kiganja cha mkono wa kushoto, Komba amepigwa risasi kwenye makalio na Mariam Azizi amepigwa risasi sehemu za siri chini ya kinena na kwamba mpaka sasa risasi moja bado ipo kwenye paja lake wanafanya jitihada ya kuondoa risasi hiyo mwilini.
 
Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP)  George Chiposi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo amedai kuwa limetokea majira ya saa 9 usiku huko katika Kijiji cha Lusewa Wilayani Namtumbo kwenye nyumba ya kulala wageni ya Mataya ambako kundi la Majambazi wakiwa na siraha zinazosadikiwa kuwa ni SAR  na SMG waliingia kwenye nyumba ya kulala wageni ya mataya na kupiga risasi na baadaye walifanikiwa kuvamia chumba cha mfanyabiashara mmoja habiba kayombo ambaye alidaiwa kuwa alitokea Tunduru kuja kufanya biashara kwenye mnada na walimpora fedha tasilimu shilingi milioni tano na baadaye walimjeruhi kwa kumpiga makofi na wapangaji wengine walijeruhiwa kwa kupigwa risasi.
 
Chiposi amesema kuwa watuhumiwa hao baada ya kupora fedha za mfanyabiashara huyo walikimbia na kutokomea kusiko julikana na polisi inaendelea kuwasaka majambazi hao ambao mpaka sasa bado hawajafahamika.
 
MWISHO

WANAHARAKATI WAKUTANA NA KUJADILIANA KUHUSU HAKI ZA BINADAMU NA USAWA WA KIJINSIA KATIKA KUMILIKI RASILIMALI ZA NCHI ZA UKANDA WA AFRIKA

Akifungua tamasha hilo la 10 la jinsia Profesa Dzodzi Tsikata wa chuo kikuu cha Ghana alisema kuwa tatizo la ukosefu wa ajira katika soko la Dunia na hasa kwa vijana waliohitimu chuo kikuu ni miongoni mwa sababu ziliopelekea kuibuka kwa migogoro mingi katika nchi za Afrika,ingawa kimsingi vurugu hizo pia zinachangiwa kwa kiasi kikubwa na mapungufu ya Demokrasia na utawala bora miongoni mwa nchi za kiarabu.
 
Profesa Tsikata alisema katika siku za hivi karibuni kumeibuka kile kinachoitwa wimbi la migogoro kwa nchi za Kiarabu ambalo kwa kiasi kikubwa limechangiwa na hali duni ya maisha ya watu kutokana na ukosefu wa ajira kwa vijana na wahitimu wa vyuo, japo kimsingi limechangiwa kwa kiasi kikubwa na mapungufu ya kidemokrasia na utawala bora miongoni mwa nchi za Kiarabu.
 
Alisema kwa upande wa Afrika, takwimu za ukosefu wa ajira kwa nchi nyingi ukiondoa Afrika Kusini, kuongezeka kwa ajira katika sekta isiyo rasmi, imetoa kisingizio cha kushindwa kwa serikali za nchi hizo katika utekelezaji wa programu za mabadiliko ya kisera na kiuchumi, na zaidi kushindwa huko kunadhihirishwa na machafuko ya kisiasa yaliyotokea wakati wa chaguzi za Kenya, Nigeria, Ivory Coast na Guinea, na misukosuko ya kiuchumi katika nchi za Swaziland na Malawi hivi karibuni.
 
‘ Kutokana na hali hii Tamasha hili ni fursa muhimu ya kutafakari na kujadili kwa pamoja hali ya maisha endelevu katika Afrika, na mapambano ya harakati za usawa wa kijinsia na pia kutafuta mbinu mbadala zitakazohamasisha upatikanaji wa maisha endelevu na bora na kutoa fursa sawa za maendeleo kwa walio wengi....badala ya mtindo wa sasa wa wachache kupata...’’ alisema Profesa Tsikata.
 
Alisema kwamba umuhimu wa haki za ardhi, ajira na maisha endelevu kwa wanawake na wanaume katika nchi za Afrika zilizoko Kusini mwa Sahara unatokana na ukweli kwamba shughuli nyingi za maendeleo zinategemea kilimo ambacho si cha kisasa kutokana na kutumia zana duni na hivyo kufanya uhitaji mkubwa wa ajira.
 
‘Kadhalika utagundua kwamba zaidi ya kilimo, ardhi ina wigo mpana wa matumizi kwa ajili ya shughuli za maisha endelevu,nyumba za kuishi na kupangisha, kama mojawapo ya chanzo cha ajira, teknolojia na pembejeo, dawa zitokanazo na mimea, upatikanaji wa mafuta, ukuzaji wa rasilimali kwa njia asilia kama vile matunda ambayo huvunwa kwa ajili ya biashara...’’ anasema Profesa Tsikata na kuongeza kuwa.
 
‘Kwa sababu mada kuu katika tamasaha hili ni Jinsia,Demokrasia na Maendeleo,Ardhi,nguvu kazi,na maisha Endelevu,ni vyema tukatambua kwamba Ardhi imekuwa ikitumika pia kama mtaji wa nguvu ya kisiasa na hivyo kuwa kiini cha kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia katika umiliki wa rasilimali....na pia umuhimu wa mifumo ya uzalishaji mali katika Afrika na maisha endelevu sambamba na mahusiano yaliyopo katika jamii za Kiafrika kwani kuna uhusiano wa karibu kati ya kushindwa kwa mafanikio ya mapinduzi ya kilimo na umuhimu uliopo wa ardhi kwa maisha bora.....’’.
 
Kuhusu mapambano ya masuala ya umiliki wa Ardhi,Ajira yenye staha na maisha bora na endelevu yenye kuzingatia usawa na haki kijinsia Profesa Tsikata alisema harakati za upatikanaji wa maisha bora na endelevu katika Afrika zinafanyika katika ngazi za kaya, jamii, mahali pa kazi, katika ngazi ya ndani na nje ya nchi na katika ngazi ya kidunia kwa ujumla.
 
Aliongeza kuwa Mapambano hayo yanajumuisha jinsi ya kujikimu kimaisha, shughuli za kila siku za uzazi na uzalishaji mali, na yanachagizwa na tafiti, uchambuzi, harakati mbalimbali na uhamsishaji sambamba na ushawishi na utetezi wa sera aghalabu unaofanywa na asasi za kijamii
 
Alisema Mapambano ya Ukombozi wa wanawake wa Kiafrika kuhusiana na haki ya kiuchumi kwa kiasi kikubwa msingi wake ni madai ya ardhi, ajira yenye staha na maisha bora na endelevu kutoka kwa wananchi wenyewe.
 
Wakati ambapo mapambano haya, hasa katika uanaharakati, hayajapata msukumo wa kutosha kwenye mapambano yanayoendelea katika ngazi ya mashirika. Masuala nyeti katika ufeminist na mchango wa utalaamu vimekuwa na mchango mkubwa katika mapambano haya.
 
Awali akiwakaribisha washiriki katika Tamasha hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) Ussu Mallya alisema kuwa

Alisema kuwa katika maeneo ya vijijini kumekuwepo
na uporaji mkubwa wa ardhi kwa wanawake lakini cha kushangaza viongozi
wamekuwa hawana msaada wowote wa kuwasaidia na hata wanawake wenyewe
wamekuwa na nidhamu ya uwoga katika kuyazungumzia matatizo yao waziwazi mbele ya
viongozi badala yake wamekuwa wakibaki kuwa wanyonge

"Kilichopo hapa kwa sisi wanaharakati sasa tuliopo mijini inatubidi
tufike vijijini ambako ndiko wanawake wengi wapo na hawana msaada
wowote na hawaelewi nini kinachoendelea mbele yao, mwanamke anafikia
hatua anadai haki yake ya kimsingi lakini watendaji wa vijiji
wamekuwa msumari kwao kwa kuwandamiza hivyo sisi kama wanaharakati
tujifunge mkanda kufika vijijini kuwasaidia wanawake wenzetu"alisema.
 
Alisema kuwa wanawake wa vijijini wanapaswa kusaidiwa kwani walio
wengi hawaelewi hata hii katiba mpya wapo ili mradi na hata
ikiwezekana matamasha haya yanayofanyika miaka inayokuja ifike
wakati angalau yahamie ngazi za wilaya au kata ili wanawake waelewe
nini kinazungumziwa
 
Ni wazi kuwaTamasha hilo la mwaka 2011 ni fursa nyingine kwa wanaharakati kujadili na kubadilishana uzoefu kwa lengo la kuondoa unyanyasaji wa kijinsia na haki za binadamu nchini ili kuweza kuleta ustawi stahiki kwa wananchi wa tanzania na hasa zaidi katika harakati ya mapambano kwenye ngazi ya jamii na hasa wanawake walioko pembezoni,kuhakikisha kuwa wanapata haki na fursa sawa katika kufikia na kumiliki rasilimali katika ngazi zote hususani katika muktadha huu wa mtikisiko wa uchumi na fedha
 
Mwandishi anapatika
Simu 0755 335051
Baruapepe;stephano12mango@yahoo.com
 
wanawake katika nchi za afrika wanatakiwa kuacha uwoga na kuwa tayari kuwaeleza
ukweli viongozi wao juu ya matatizo ambayo yamekuwa hayapewi
kipaumbele na kutozungumziwa na kufanyiwa maamuzi stahiki na mamlaka husika

"Wanawake kwa kiasi kikubwa bado tumekuwa na woga na ule unafiki wa
kuwaogopa viongozi wetu pale tunapokuwa na matatizo tunashindwa
kueleza hali halisi ya matatizo yaliyopo kwa kuona kiongozi si mtu wa
kumwambia unaona kama mungu mtu wakati ni mtu wa kawaida
tu"alisema Mallya

TAMASHA LA JINSIA 2011 NI FURSA NYINGINE KWA WANAHARAKATI WA MASUALA YA JINSIA
 
Na Stephano Mango
WANAHARAKATI mbalimbali wa masuala ya jinsia na haki za binadamu nchini wameungana na wanaharakati wenzao wa kutoka nchi jilani zilizopo kwenye ukanda wa afrika katika Tamasha la 10 la Jinsia lenye mada kuu ya Jinsia,Demokrasia na Maendeleo ili kujadili kwa kina masuala ya ardhi,nguvu kazi na maisha endelevu chini ya muktadha wa mfumo dume na uchumi wa soko huria,ubeberu na uliberali mambo leo
 
Tamasha hilo ni muhimu hasa katika kipindi hiki cha miaka 50 ya uhuru ambapo kumekua na tishio la ongezeko la uporaji wa ardhi unaofanywa na wawekezaji wakubwa na kuwepo kwa vuguvugu la madai ya katiba mpya toka kwa wananchi
 
Ni Tamasha la aina yake lililofanyika kwenye viwanja vya mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 13-16 mwaka huu 2011 kwa kuzinduliwa na mada maalum iliyotolea na Mwanaharakati wa masuala ya ardhi kutoka Ghana profesa Dzodzi Tsilsata
 
Tamasha hilo la aina yake liliratibiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) kwa kushirikiana na mashirika wanachama wa Muungano wa Wanaharakati wanaotetea ukombozi wa wanawake kimapinduzi,usawa wa jinsia,demokrasia,maendeleo na haki za binadamu(FemAct)
 
Tamasha hilo lilikuwa na mada kuu ya "Jinsia,Demokrasia na Maendeleo:Ardhi,Nguvu kazi na Maisha Endelevu" na pia mada ndogondogo zilizowasilishwa na watu waliobobea ikiwemo mada ya Mapambano ya Wanawake Kwenye Ajira,Maisha Endelevu na Nguvukazi,Mapambano ya Wanaharakati Wanawake kwenye Njia za kujiajili/Kupata Ajira na Maisha Endelevu:Ardhi,Maji,Nafasi na Masoko
 
Mada nyingine ndogo iliyowasilishwa ni Mapambano ya Wanawake Wanaharakati kwenye Ujira,Mishahara na Mazingira ya Kazi,Ustawi na Usalama wa Kijamii na Kiuchumi,Mikakati ya Mapambano ya Ukombozi wa Wanawake Kuweza Kupata Fursa ya Kumiliki Ardhi,Nguvu Kazi na Maisha Endelevu
 
Lengo la tamasha hilo ni kutoa fursa kwa wanawake,wafeministi,wapigania haki za binadamu na jinsia,kutafakari na kubadilishana ujuzi na tarifa kwenye masuala ya kipaumbele kwenye mada pana jinsia,demokrasia na maendeleo
 
Kuimarisha vuguvugu la usawa wa jinsia,demokrasia na maendeleo kutokana na uzoefu na ujuzi wa wanaharakati,ikiwa ni pamoja na kusherehekea nguvu ya wanaharakati na kuimarisha ushirikiano katika kujenga vuguvugu la kutetea haki za kiuchumi na ukombozi wa wanawake katika ngazi na nyanja zote za jamii
 
Kuweka kumbukumbu na kubadilishana uzoefu katika harakati za kimapinduzi za kuleta mabadiliko chanya kwenye masuala ya jinsia,demokrasia na maendeleoa
Tamasha la mwaka huu limeunganisha watu kutoka katika nchi za Uganda,Zimbabwe,Burundi,Ghana,Afrika Kusini,Marekani,Kenya na Ufaransa na kufanikiwa kupata washiriki 2500 kutoka ngazi ya Wilaya na vijiji nchini kote
 
Masuala yanayopewa kipaumbele katika tamasha la mwaka huu yalijengwa kutokana na ushiriki mpana na mawasiliano yaliyofanyika kati ya waandaaji na wanaharakati katika ngazi ya kijamii,kitaifa,kikanda na kimataifa
 
Akizungumzia Mwongozo wa muktadha wa Tamasha la Jinsia kwenye uzinduzi wa Tamasha la mwaka 2011,Mwenyekiti wa Tamasha la Jinsia Mary Rusimbi alisema kuwa Tamasha ni nafasi ya wazi kwa ajili ya watu binafsi,vikundi,mashirik na mitandao walio katika mapambano yanayofanana ili kubadilishana uzoefu,taarifa na kujengana uwezo
 
Rusimbi alisema kuwa wanaharakati hao hukutana na kusherehekea mafanikio na kuthamini changamoto zilizo mbele yao,ili kuchangia katika mijadala ya wazi kuhusu maendeleo,kujenga na kuimarisha mitandao na kupanga kwa pamoja kwa ajili ya kuleta mabadiliko ya kijamii kwa mtazamo wa ukombozi wa wanawake kimapinduzi
 
Alieleza zaidi kuwa tamasha la jinsia 2011 linafanyika wakati muhimu katika historia ya Tanzania na Afrika kwa ujumla kutokana na ongezeko kubwa tangu 2008 la ubadhilifu wa rasilimali za taifa kama vile ardhi,madini,maji,misitu na nyinginezo
 
Alisema kuwa ubadhilifu huo unaofanywa na mashirika ya uwekezaji ya kitaifa kwa kuungwa mkono na serikali za nchi za afrika na wahisani pia wakati huo huo mapambano dhidi ya unyonyaji yameongezeka kwani miaka 50 baada ya uhuru Tanzania bado haijaweza kujitegemea kiuchumi,kisiasa,kijamii,kijeshi,kidini na kiutamaduni
 
Alieleza kuwa Tanzania bado imetawaliwa na utegemezi mkubwa kwa nchi za magharibi kupitia makampuni makubwa ya kimataifa ya uwekezaji na kupelekea taasisi hizo kudhibiti kwa kiasi kikubwa sera zetu za kiuchumi
 
Alifafanua kuwa Serikali imekuwa ikitekeleza kwa niaba yao,sera za utandawazi kupitia sera za ulegezaji wa uchumi na uuzaji wa bidhaa nje ili kuweka mazingira wezeshi kwa makampuni ya kibepari badala ya wazalishaji wadogo wadogo
 
Alisema kuwa matokeo yake mapato ya serikali yanazidi kutegemea makampuni machache yanayouza nje bidhaa kama vile maua,mbogamboga,madini,utalii na viwanda ambapo wanawake ndio waathirika na unyonyonywa zaidi na mfumo uliopo kwani wengi wao ndio wazalishaji wadogowadogo iwe ni wakulima,wafugaji au wavuvi
 
Alisema kuwa wao ndio wanaonyonywa zaidi na kuporwa rasilimali kutokana na mwingiliano wa mifumo kandamizi ya kibeberu,kibepari na mfumo dume na kufanya wao kunufaika zaidi iwapo mifumo hii kandamizi ya kiuchumi itaondolewa
 

WASHIRIKI WA TAMASHA LA JINSIA 2011 WATAKA WAFANYAKAZI WA NDANI WATHAMINIWE KWA KUPEWA HAKI ZAO ZOTE

Na FATUMA KITIMA ,Dar es Salaam.
SERIKALI imetakiwa kuwajibika na kuchukua hatua pamoja na mipango endelevu kwa jamii hasa kwa wafanyakazi wa ndani ili kuweza kuwasaidia watoto hao kuondokana na ukatili uliokithiri.
Wakitoa changamoto hizo wanaharakati mbalimbali katika Tamasha la Jinsia ,Demokrasia na Maendeleo Tanzania (TGNP) katika viwanja vya Mabibo jijini Dar es Salaam, walisema kuwa kukosekana kwa mipango madhubuti iliyowekwa na Serikali ndiyo kumesababisha tatizo hilo lilipo kwa sasa.
Mwanaharakati Sophia Kimbereja kutoka Wilaya ya Newala mkoani Mtwara  alisema kuwa Serikali iangalie kwa kina zaidi watu wanaowafanya ukatili kwa watoto hao katika nyumba zao na  kuchukuliwa hatua za kisheria.
“Wanawake tushirikiane kwa pamoja katika kutokomeza ukatili kwa watoto kwani tukiamua tunaweza “alisema Bi. Kimbereja.
Alitoa mwito kwa Serikali kuchukua hatua kwa watu wanaoenda vijijini kuchukua watoto na kudai wanakwenda kufanya kazi za ndani kumbe wanawachukua kwa lengo la kuwatumikisha katika biashara za ukahaba.
Kwa upande wake Matesa Bandoma aliainisha kuwa katika tatizo hilo la ukatili ambalo limekithiri linawakumba familia za hali ya chini kwa kuwa watoto zao ndio wanafanya kazi wa ndani.
“ Sisi kama wazazi au wanawake inabidi tubadilike ili jamii zetu ziweze kuwa bora kwa maendeleo yetu na vizazi vijavyo kwani tusipofanya hivyo watoto wetu watatulaumu kwa kushindwa kutimiza wajibu wetu”alisema Bandoma
Bandoma aliongeza kuwa mbali na changamoto hiyo ya ukatili lakini  kuna idadi kubwa ya wafanyakazi wa ndani hawajui kusoma na kuandika .
mwisho

Wednesday, September 14, 2011

VIWANJA 6354 KWA SHUGHULI MBALIMBALI VYAPIMWA MPAKANI MWA TANZANIA NA MSUMBIJI

                                     Na Joseph Mwambije,Songea
HALMASHAURI ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma imepima jumla ya Viwanja 6354 katika eneo la mpakani mwa Tanzania na Msumbiji la Mkenda ili kulifanya eneo hilo kuwa Mji mdogo ulipangika kimipango miji  na kuwa Mji wa mfano wa mpakani Nchini
 
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Fanuel Ndemfoo wakati akizungumza na mwandishi wa mtandao wa http://www.stephanomango.blogspot.com/ mjini Songea Joseph Mwambije ofisini kwake alisema kuwa hiyo ni awamu ya pili ya upimaji viwanja katika eneo hilo lenye daraja kubwa la Mkenda linaloziunganisha Nchi hizo mbili na kwamba awamu ya kwanza ya upimaji ilifanywa Januari 2009/2010 ambapo viwanja 1000 vilipimwa.
 
Alisema  kuwa ni nafasi nzuri kwa Watanzania kujitokeza  kuwekeza katika eneo hilo badala ya kuwaachia wageni na kujenga Hoteli,Shule,nyumba za kulaa wageni na uwekezaji mwingine.
 
‘Lengo letu ni kuwa na Mji mdogo ulipangika vizuri na kuwa  Mji wa mfano Nchini kwa kuwa Miji mingi ya mipakani haijapimwa na baadhi yake ni Namanga na Tunduma hivyo tunategemea mpaka mwaka 2015 tutakuwa na Mji ulikamilika na unaovutia’alisema Kaimu Mkurugenzi huyo.
 
Kaimu Mkurugenzi huyo anabainisha kuwa katika Mji huo mdogo wenye wakazi 3000 viwanja vya makazi vilivyopimwa ni 4775,viwanja vya biashara ni 1074,maeneo ya Shule za  awali 36,maeneo ya wazi 80,maeneo ya masoko 16,maeneo ya Shule za msingi 10,maeneo ya umma ni 33 na maeneo ya Zahanati ni 13.
 
Viwanja vingine anasema kuwa ni  maeneo ya kuegesha magari (Parking) viwanja saba,Maeneo ya Kanisa na misikiti 18,maeneo ya makaburi viwanja 10,Maeneo  ya ujenzi wa nyumba za Serikali 10,Maeneo ya biashara ndogondogo viwanja 6 na maeneo ya viwanja vya michezo 13.
 
Anasema kuwa viwanja vingine ni maeneo ya  vituo vya mafuta 10,maeneo ya hoteli 31,maeneo ya Vituo vya polisi 7,maeneo ya mapumziko matano(5),maeneo ya mpira wa gofu 1,maeneo ya vituo vya afya mawili(2),maeneo ya Hospitali mawili,maeneo ya Mama lishe na Baba lishe moja na  maeneo ya majumuiko ya jamii mawili.
 
‘Kimsingi tumejipanga kuufanya mji hu kuwa wa kuvutia kama ilivyo miji mingine ya wenzetu iliyopo mpakani tuna viwanja vya maeneo ya masoko ya kisasa(Super market) mawili,maeneo ya maduka 9,maeneo ya  Ukumbi mawili na maeneo ya huduma za jamii 106’alisema Ndemfoo.
 
Anafafanua kuwa viwanja vingine ni maseneo ya ujenzi wa Sekondari 12,maeneo ya ujenzi wa Chuo mawili,maeneo ya kutengenezea magari(gereji) mawili,maeneo ya michezo mawili,maeneo ya ujenzi wa majengio ya umma mawili na maeneo ya ujenzi wa nyumba za ibada mawili  na kufanya kuwa jumla viwanja 6354.
MWISHO.

Tuesday, September 13, 2011

WANAHARAKATI WAZIKEMEA SERIKALI ZA AFRIKA KWA UKANDAMIZAJI

 Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)  Ussu Mallya akielezea tamasha la jinsia 2011 linaloendelea kufanyika jijini Dar Es Salaam
 Waandishi wa habari wakiwa kwenye moja ya vikao kwa ajili ya maandalizi ya kulipoti habari mbalimbali
 Wanaharakati mbalimbali wakiwa wanafuatilia mada zinazowasilishwa na wadau mbalimbali wa haki za binadamu
 Wanahabari mbalimbali kutoka katika vyombo tofauti tofauti wakiendelea kuchapa kazi wakati wa tamasha la jinsia 2011 linaloendelea kufanyika katika viwanja vya TGNP Jijini Dar Es Salaam
 Kikundi cha ngoma ya asili kikitumbuiza wakati wa tamasha
 Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari wanawake nchini Ananilea Nkya akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mtandao wa jinsia tanzania TGNP ikiwa ni maandalizi ya kuhabarisha umma
WANAHARAKATI WAZIKEMEA SERIKALI ZA AFRIKA KWA UKANDAMIZAJI
 Na Stephano Mango,Dar Es Salaam
WANAHARAKATI nchini wamezitaka Serikali  za nchi barani Afrika, kuhakikisha rasilimali zinawanufaisha wananchi hususani wanawake na watoto wanaoishi pembezoni ili kuweza kupunguza matabaka ya wenye nacho na wasio kuwa nacho ili kuweza kujenga jamii iliyostaarabika

Mwanaharakati wa masuala ya ardhi nchini Ghana, Profesa Dzodzi Tsilsata, alisema jana alipokuwa akifungua Tamasha la Jinsia, linalofanyika katika viwanja vya TGNP, Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Tsilsata, miaka michache iliyopita kumekuwepo na ongezeko kubwa kati ya wenye nacho na wasinacho hali inayosababisha kuwepo na matukio mengi ya uvunjifu wa amani, kwa kuandamana, kugoma ama vurugu mbalimbali.

Alisema, Serikali badala ya kupunguza hali hiyo imekuwa ikizembea kuchukua hatua stahiki na badala yake inawaongezea makali ya maisha wananchi wake kwa kuwaachia viongozi wake wakifanya vitendo viovu vya ubadhilifu wa rasilimali za taifa.

Alisema kuwa, Afrika inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya kukubali sera mbovu kutoka katika mataifa ya magharibi na taasisi za fedha za kimataifa ambazo zimekuwa zikiwakandamiza wananchi wengi.

Naye Mwenyekiti wa tamasha hilo, Mary Rusimbi alisema kuwa Serikali za Afrika zimekuwa zikishindwa kutengeneza sera stahiki kwa wananchi wake na kupelekea hisia za kuwa na ukoloni mamboleo

Rusimbi alieleza kuwa Tanzania imetimiza miaka 50 baada ya uhuru lakini bado haijaweza kujitegemea kiuchumi,kisiasa,kidini,kijamii,kijeshi na kiutamaduni kwani imekuwa ikitawaliwa na utegemezi mkubwa kwa nchi za magharibi kupitia makampuni makubwa ya kimataifa ya uwekezaji
.
Alisema kuwa Serikali hutekeleza kwa niaba ya nchi za magharibi sera za utandawazi kupitia sera za ulegezaji wa uchumi na uuzaji wa bidhaa nje ili kuweka mazingira wezeshi kwa makampuni ya kibepari badala ya wazalishaji wadogowadogo

Alieleza kuwa matokeo yake mapato ya serikali yanazidi kutegemea makampuni machache yanayouza nje bidhaa kama vile madini,mbogamboga , maua,utalii na viwanda ambapo wanawake ndio wamekuwa waathirika wakubwa wa mifumo ya unyonyaji

Alifafanua zaidi kuwa kutokana na hali hiyo wanawake wengi waliopo pembezoni wamekuwa wakinyang’anywa rasilimali zao na kupewa watu wenye nguvu ya kiuchumi kutokana na mwingiliano wa mifumo kandamizi ya kibeberu na kibepari na mfumo dume unaowaacha wanawake wengi wakiwa mikono mitupu
mwisho

KAZI IMEANZA SASA BAADA YA KUTUA NANGA KATIKA VIWANJA VYA MTANDAO WA JINSIA TANZANIA ILI KUWEZA KUWALETEA HABARI MBALIMBALI ZINAZOENDELEA KUJILI KATIKA TAMASHA LA JINSIA 2011 LINALOENDELEA KUFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA TGNP-MABIBO JIJINI DAR ES SALAAM

 Mmiliki wa mtandao huu wa http://www.stephanomango.blogspot.com,ndugu/ Stephano Mango akiwa amefika katika ofisi za TGNP kwa lengo la kuwahabarisha wasomaji wa mtandao huu kinachoendelea kwenye tamasha la jinsia 2011 ambapo wanaharakati zaidi ya 2500 wanatarajia kushiriki
 Moja ya picha za kiuhanaharakati ikiwa imepamba moja ya kuta kwenye jengo la mtandao wa jinsia Tanzania,picha hiyo inawakilisha akina mama wajawazito wanavyopata tabu ya huduma bora wanapokuwa wajawazito,wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua

 Ukifika TGNP-Mabibo jijini Dar Es Salaam wakati huu wa tamasha utaona bango kubwa linalokupa maelekezo ya awali ya uwepo wa Tamasha hilo
Bango hili ndilo lililonipa ishara ya kuiona Ofisi ya TGNP ili niweze kukutana na wanaharakati wenzangu kwa lengo la kujiandaa kushiriki Tamasha la Jinsia la 2011 na kuweza kupata yanayoendelea kujili katika viwanja hivyo kwa ajili ya wasomaji

MENEJA WA SHIRIKA LA POSTA RUVUMA ADAIWA KUWANYANYASA WAFANYA KAZI WAKE

                                               Na Gideon Mwakanosya,Songea.

WAFANYAKAZI wa shirika la Posta Tanzania mkoani Ruvuma wameulalamikia uongozi wa shirika hilo mkoani humo kwa vitendo vya unyanyasaji kwa wafanyakazi likiwemo cha wafanyakazi wawili kusimamishwa na kufukuzwa kazi kwa madai kuwa wameiba fedha kiasi cha sh.10,620 mali ya shirika hilo.

Wafanyakazi hao ambao walitoa malalamiko yao kwa masharti ya kutotajwa majina kwa kuhofia ajira zao walisema kuwa unyanyasaji uliopo katika shirika hilo unaofanywa na Meneja wa Shirika hilo mkoani Ruvuma Rochus Assenga unawafanya wawe wanafanya kazi kwa hofu kubwa.

Walisema kuwa kitendo cha kuwasimamisha wafanyakazi wenzao na mmoja kumwachisha kazi kinaonesha wazi ukiukwaji wa haki za wafanyakazi kwani wafanyakazi hao mpaka sasa hakuna kosa lolote la msingi linaloweza kuwafanya wasimamishwe au kuachishwa kazi.

Mfanyakazi aliyesimamishwa kazi ametajwa kwa jina la Johnson Miyola na aliyeachishwa kazi Peter Sendama ambaye mpaka sasa barua ya kuachishwa kazi ajakabidhiwa ingawa amepewa taarifa hiyo ya kuachishwa kazi na meneja kwa mdomo na kutakiwa asiingie kwenye ofisi za shirika hilo wakati uongozi unamuandalia barua pamoja na mafao ya kuachishwa kazi.

Uchunguzi uliofanywa na waandishi wa habari umebaini kuwa licha ya kuwasimamisha kazi  na kumwachisha  mmoja tayari wafanyakazi hao walishapelekwa polisi na kufunguliwa kesi ya wizi namba SO\ IR\3962\2011 katika kituo kikuu cha Songea tangu Agosti 19 mwaka huu.

Mfanyakazi mmoja aliyeachishwa kazi Sendama alipoulizwa na waandishi wa habari amekiri kuchishwa kazi kwa mdomo na kwamba barua ya kuachishwa kazi pamoja na mafao atapewa siku ya Ijumaa kwa mujibu wa maelezo aliyoyatoa meneja wa shirika hilo Assenga

Alisema ameshangazwa kuona atua kali zikichukuliwa dhidi yake ambapo awali tangu aanze kazi kwenye shirika hilo hajawi kupewa barua ya onyo au kalipio kali kabla mfanyakazi hajaachishwa kazi.

“ Sina kosa jingine ambalo meneja alishanionya mara tatu kwa kujaza fomu tatu ambazo mfanyakazi kabla hajaachishwa hujazwa na kabla ya hapo meneja hajawahi kunipa onyo wala fedha hizo anazodai nimeiba si kweli bali kulikuwa na tatizo la kiufundi lililojitokeza kwenye mtandao na kusababisha kumwandikia mteja risiti kwa mkono.”alisema Bw. Sendama.

Hata hivyo baadhi ya wafanyakazi wa shirika hilo tawi la Songea wameeleza kuwa tangu meneja huyo Assenga afike Mkoa wa Ruvuma baada ya meneja aliyekuwepo kustaafu amekuwa na tabia ya kuwanyanyasa na kudai kuwa yeye amuogopi mtu wa aina yeyote kwani ametokea makao makuu ya shirika hilo na kwamba Posta masta mkuu ni swaiba wake hivyo hawezi kumfanya kitu chochote na ni lazima amsikilize anachosema.

Naye Meneja wa shirika hilo mkoani Ruvuma  Assenga alipofuatwa na waandishi wa habari ofisini kwake kutaka atoe ufafanuzi juu ya malalamiko dhidi yake alidai kuwa yeye sio msemaji wa shirika na kuwataka waandishi wamtafute posta masta mkuu wa shirika hilo ndio msemaji na baadae alipoona waandishi wa habari wanaendelea kumuliza maswali aliondoka ofisini kwake na kuwaacha waandishi wa habari wakiduwaa kwenye jengo la shirika hilo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi wa shirika la posta Tanzania tawi la Songea Gisla Mhagama alipotafutwa na  waandishi wa habari ili ataoe ufafanuzi juu ya malalamiko ya wafanyakazi dhidi ya uongozi hakuweza kupatikana kwa njia ya simu kwa kuwa yuko safarini nje ya Mkoa.

Hata hivyo waandishi wa habari waliwatafuta viongozi wa chama hicho (COTWU) kanda ya Mbeya kwa njia ya simu ambapo walifanikiwa kumpata katibu wa chama hicho  Getrud Mlai na mwenyekiti wake Peter Songela walishangazwa kusikia kuwa wafanyakazi wa tawi la Songea wamekuwa na malalamiko mazito dhidi ya uongozi na walidai kuwa wao bado hawajapata malalamiko rasmi lakini wanafanya taratibu za kwenda Songea kwenda kusikiliza kilio cha wafanyakazi wiki ijayo.

Akizungumza kwa njia ya simu Posta masta mkuu wa shirika la Posta Tanzania Deos Mndeme alieleza kuwa ni kweli ofisi yake inataarifa kuwa kunawafanyakazi wawili wa shirika hilo ambao walipelekwa polisi wakituhumiwa kuwa ni wezi wameiba fedha sh.10,620 lakini hana taarifa ya aina yeyote kama wafanyakazi hao wamesimamishwa na kuachishwa kazi kwani maswala ya utawala yanamgawanyo na mambo ya utawala wa mikoani yanaishia mikoani yeye anashughulikia mambo makubwa.

Aidha mndemi alikanusha kauli ya meneja wa shirika hilo mkoani Ruvuma Assenga ya kusema kuwa yeye yuko jirani naye na ni swaiba yake jambo ambalo alidai kuwa linaleta mazingira ya kumchafua kwani yeye ni mtawala wa shirika na wafanyakzi wote bila kuwa na ubaguzi labda uhusianao huo katika yangu na yeye anaujuwa yeye na si vinginevyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma  Michael Kamuhanda alipoulizwa na waandishi wa habarí kuhusiana na wafanyakazi wawili wa shirika la posta kukamatwa na kuwekwa mahabusu kwa tuhuma za wizi wa sh. 10,620 za shirika hilo amekiri kushikiriwa kwa wafanyakzi hao lakini ameeleza kuwa jambo hilo liko kwenye upelelezi na bado halijathibitishwa kama wafanyakazi hao kama waliiba au la.

MWISHO.

Monday, September 12, 2011

MAELFU YA WAKAZI WA TUNDURU WAJITOKEZA KUMZIKA MWENYEKITI WA TLP TUNDURU RAJABU MNYACHI

                             Na  Steven  Auguastino, Tunduru
 
MAELFU ya wakazi wa mji wa Tunduru wamejitokeza kumzika aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labour Party (TLP) Wilaya ya Tunduru Rajab Mohamed Mnyachi aliyefariki Dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu na kulazwa katika hospitali ya serikali ya wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma.
 
Msemaji wa familia ya Marehemu Mnyachi Bw. Shaibu Namkumbe akizungumza na mtandao wa http://www.stephanomango.blogspot.com/ alisema kuwa marehemu Mnyachi alikuwa anasumbuliwa na  maradhi ya shinikizo la damu.
 
Akifafanua wasia wa marehemu mnyachi Bw. Namkumbe alisema kuwa kipindi cha uhai wake alijishikisha na alikuwa mkereketwa wa mageuzi kupitia vyama ya siasa pamoja na kugombea nyadhifa mbali mbali.
 
Alisema mwaka 1986 hadi 1999 marehemu  Mnyachi alikuwa mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi na aligombea katika kinyang`anyiro cha Ubunge wa jimbo la Tunduru akiwa anapambana na marehemu Juma jamardini Akukweti wa CCM katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995.
 
Taarifa hiyo iliendelea kueleza kuwa Mwaka 1999 marehemu alikihama chama cha NCCR Mageuzi na kujiunga na TLP ambako pia alichaguliwa kuwa mwenyekiti wake hadi umauti ulipo mkuta Septemba 9 mwaka huu.
 
Akiwa katika chama hicho pia marehemu alitoa hamasa kubwa na kukifanya chama hicho kupata wanachama wengi na kugombea katika vinyang`anyiro vya Ubunge katika chaguzi za mwaka 2000, 2005 na uchaguzi mdogo wa kuziba pengo la marehemu Akukweti mwaka 2007.
 
Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi wanaomfahamu Marehemu Mnyachi, katibu wa Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kusini Bw. Maulidi Kalambo (Yakanungu) na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Wilaya ya Tunduru Bw. Maurid Said mbali na kukiri kuwa Marehemu alikuwa mahiri katika medani za siasa na kuongeza kuwa sasa Tunduru imeishiwa watu wenye vipaji.
 
Katika maelezo yao viongozi hao walisema kuwa Marehemu mnyachi, marehemu  Mazee Rajab wa CUF pamoja na Simbili Makanyaga wa UDP aliyehamia jijini Dar es salaam baada ya kuchaguliwa kuwa katibu Mwenezi wa Chama hicho Taifa walikuwa ni hazina kubwa na kwamba sasa Wilaya ya Tunduru inategemea majaliwa ya mungu kupata vijana wenye kipaji na watakao kubalika katika kuleta changamoto za maendeleo vinginevyo CCM itaendelea kushika hatamu.
 
Mwisho.   

ASKARI WANYAPORI AKUTWA AMEUWA NA WATU WASIOFAHAMIKA

                                               Na Gideon Mwakanosya,Songea.
ASKARI wa idara  ya wanyamapori Nchini  Msumbiji  Babu Abdalah (35) amekutwa akiwa ameuwawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali sehemu za kifuani na watu wasiofahamika huko katika  kijiji cha Chikomo wilayani Tunduru Mkoa wa Ruvuma.
Akizungumza na Mtandao huu wa http://www.stephanomango.blogspot.com/ ofisini kwake jana kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda alisema kuwa tukio hilo limetokea Septemba 10 mwaka huu majira ya saa 9 alasiri huko katika kijiji cha Chikomo.
Alisema kuwa siku hiyo ya tukio inadaiwa kuwa afisa mtendaji  wa kijiji hicho Ally Mtukusye alipatiwa taarifa ya tukio hilo kasha aliwasiliana na polisi wa kituo kikuu cha Tunduru ambao walifika kwenye eneo la tukio wakiwa wameongozana na mganga ambaye ndiye aliyethibitisha kuwa askari huyo wa idara ya maliasili toka Nchi ya Msumbiji amekufa kutokana na kipigo.
Kamuhanda alisema kuwa  Askari huyo alikutwa akiwa na majeraha makubwa sehemu za usoni upande wa kushoto na kifuani upande wa kushoto ambayo  ndio yalimsababishia  kuvuja kwa damu nyingi atimaye kufariki dunia.
 Hata hivyo kamanda Kamuhanda alisema kuwa kufuatia tukio hilo hakuna aliyekamatwa au kutiliwa mashaka na chanzo bado kinaendelea kuchunguzwa.
MWISHO.

WANNE WASHIKILIWA NA POLISI RUVUMA KWA TUHUMA ZA MAUAJI WILAYANI TUNDURU

                                        Na Gideon Mwakanosya,Songea.
JESHI la Polisi mkoani Ruvuma linawashikilia watu wanne wakazi wa kijiji cha kitanda wilayani Tunduru kwa tuhuma za kumpiga na kitu chenye ncha kali sehemu mbambali za uso na kumsababishia kifo mwanamke mwenye umri wa miaka 60 mkazi wa kijiji hicho.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma  Michael Kamuhanda akizungumza na mwandishi wa mtandao wa http://www.stephanomango.blogspot.com/, Gideon Mwakanosya kutoka mjini Songea, alisema kuwa tukio hilo limetokea septemba 10 mwaka huu mwajira ya saa 2.00 usiku huko katika kijiji cha kitanda kilichopo wilayani Tunduru.
Kamuhanda amemtaja aliyeuwawa kuwa ni Mwanahawa Landi (60) mkazi wa kijiji hicho na amewataja wanaoshikiliwa na polisi kuhusiana na tuhuma za mauaji hayo kuwa ni Mohamed Saidi (25), Kassim Said (39), Said Baina (76) na Ally Said (37) wote wakazi wa kijiji cha kitanda.
Alifafanuwa zaidi  kuwa inadaiwa kuwa siku hiyo ya tukio Mohamed Issa (70) alitoa taarifa kwenye kituo cha polisi cha Tunduru kuwa Mwanahawa ameuwawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali usoni na ambayo yalimsababishia sura yake kuharibika kabisa na watu wasiofahamika.
Kamanda Kamuhanda alisema kuwa chanzo cha mauaji hayo bado kinachunguzwa lakini tayari watu wanne polisi imewatia mbaroni kwa mahojiano zaidi na kwamba uchunguzi utakapokamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma za mauaji.
MWISHO.

NIMESAFIRI KIKAZI WAPENZI WASOMAJI WA MTANDAO HUU

Stephano Mango
Mmiliki wa mtandao huu wa http://www.stephanomango.blogspot.com/, ambaye ni ndugu Stephano Mango amesafiri kikazi toka Songea mpaka Jijini Dar Es Salaam, ambapo ameungana na wanaharakati wengine nchini na nchi jilani kwa ajili ya kuhudhuria Tamasha la Jinsia Tanzania ambalo linaanza kufanyika kesho Septemba 13-16 mwaka huu 2011

Katika Tamasha hilo Mada mbalimbali zitawasilishwa na wanaharakati na wasomi waliobobea katika utetezi wa masuala ya jinsia na haki za binadam, kwa mwaka huu Mada itakuwa ni ,"Ardhi,Nguvu Kazi na Maisha Endelevu" chini ya Kampeni kubwa ya "Haki ya Uchumi:Rasilimali ziwanufaishe Wanawake Walioko Pembezoni.

Hivyo,ndugu wasomaji jiandaeni kupata habari mbalimbali kutoka katika tamasha hilo kwani mtandao huu wa http://www.stephanomango.blogspot.com,utakuwa/ makini kuwaletea wasomaji vitu murua kwa kukidhi kiu yako ya kupata matukio muhimu ya kiharakati

MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA NA UFANYAJI KAZI ZENYE UCHUMI MDORORO

Akina mama ambao majina yao hayakuweza kufahamika mara moja wakiwa wamebeba miwa kwa ajiri ya kwenda kuiuza ili kuweza kujipatia kipato cha kujikimu kutokana na ugumu wa maisha unaowakabili katika jamii zao na taifa kiujumla,wananchi wengi wanaoishi pembezoni wamekuwa wakiishi katika mazingira duni kutokana na kushindwa kufaidi mgawanyo wa rasilimali za nchi

Saturday, September 10, 2011

HAYA NDIYO YALIYOJILI KATIKA MAONYESHO YA NANE YA SIDO KANDA YA KUSINI YANAYOENDELEA KUFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA CCM WILAYANI MBINGA MKOANI RUVUMA

 Mkurugenzi mkuu wa SIDO Michael Raizer akimuonyesha Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Cyril Chami shughuli za uzalishaji wanazozifanya kwenye banda la Sido mara baada ya kuzindua maonyesho hayo jana kwenye viwanja vya CCM wilayani Mbinga
 Waziri wa Viwanda na biashara Dkt Cyril Chami akisalimiana na Meneja wa Benki ya NMB tawi la Mbinga Lugano Mwampeta mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya maonyesho mjini Mbinga
 Mgeni rasmi katika maonyesho ya nane ya Sido kanda ya kusini,Waziri wa viwanda na biashara Dkt Cyril Chami akizindua maonyesho hayo katika banda la SIDO kwenye viwanja vya CCM mbinga,wa kwanza kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mashariki Gaudence Kayombo.Maonyesho hayo yameanza septemba 9-12 na kushirikisha wajasiliamali 200 kutoka katika mikoa ya mbeya,Lindi,Mtwara,Iringa na Ruvuma
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt Christine Ishengoma(mwenye suti nyeusi) akikagua banda la wajasiliamali JKT Mlale kabla ya mgeni Rasmi ajatembelea banda hilo na kujionea shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo ya Serikali,wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa habari na Masoko Sido makao makuu Jannet Ninja
 Mkurugenzi wa habari na Masoko wa Sido Jannet Ninja akimuonyesha mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt. Christine Ishengoma (mwenye suti nyeusi)sehemu atakayoanza mgeni rasmi kukagua mara atakapowasili kwenye viwanja hivyo vya maonyesho,wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya MBINGA Kanali Mstaafu Edmund Mjengwa,wa kwanza kushoto Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT)wilaya ya Mbinga Lusiana Ndunguru
 Askari wa Skauti akimvesha skafu Mgeni rasmi Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Cyril Chami ikiwa ishara ya kumkaribisha katika viwanja vya maonyesho,wa kwanza kushoto ni Mbune wa jimbo la Mbinga Mashariki Gaudence Kayombo,wa pili ni Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Christine Ishengoma
 Mgeni rasmi akipata maelezo katika banda la muungano wa wajasiliamali vijijini(MUVI) alipotembea katika banda hilo jana
 Mgeni Rasmi akiangalia kwa umakini ingini ya mashine ya kusaga kutoka kwa wajasiliamali wa Mbeya alipotembelea banda hilo wakati wa maonyesho
 Mjasiliamali wa usindikaji na uuzaji wa vinywaji aina mbalimbali ikiwemo Mvinyo kutoka Seedfarm Songea chini ya Kampuni ya Jeim Product Magdalena Talimo akimuonyesha bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kampuni yake Mgeni Rasmi Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Cyril Chami alipotembelea banda la kampuni hiyo
 Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Kanali Mstaafu Edmund Mjengwa akiwa amepumzika kutokana na uchovu wa kuzunguka kukagua mabanda ya wajasiliamali na kupata kahawa katika banda la MCCCO
 Mwanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi Veta SONGEA akimpa maelekezo mgeni rasmi Dkt Chami ya namna mashine ya kusukia nywele inavyofanya kazi alipotembelea banda hilo
Viongozi mbalimbali wa serikali ya mkoa wa Ruvuma wakimsindikiza Mgeni rasmi waziri wa viwanda na biashara Dkt Cyril Chami kuelekea jukwaani na kuhutubia wajasiliamali waliopo kwenye viwanja vya CCM wilayani Mbinga
 Mgeni Rasmi Dkt Chami akiangalia kwa umakini kikundi cha ngoma ya chioda kinavyotumbuiza maonyesho hayo
Mgeni rasmi Dkt Chami akimpa maelezo Mkuu wa Wilaya ya Mbinga kanali Edmund Mjengwa mara baada ya kumaliza kukagua mabanda yote ya maonyesho(PICHA ZOTE NA STEPHANO MANGO)

                   WAZIRI Dkt CHAMI AZIANGUKIA TAASISI ZA FEDHA NCHINI
Na Stephano Mango,Songea
WAZIRI wa Viwanda na Biashara Dkt .Cyril Chami ameziangukia taasisi za fedha nchini kuona umuhimu wa kuweka masharti nafuu ya mikopo kwa wajasiliamali ili waweze kukopa fedha kulingana na michanganuo ya miradi yao kwa lengo la kukuza uchumi wa jamii na nchi kwa ujumla

Wito huo aliutoa jana wakati akihutubia mamia ya wajasilimali waliojitokeza katika uzinduzi waa maonyesho ya nane ya Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo(Sido) kanda ya kusini yaliyofanyika katika viwanja vya Ccm Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma

Dkt Chami ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo alisema kuwa taasisi za fedha nchini zinatakiwa kubuni utaratibu wenye masharti nafuu wa kuwakopesha wajasilimali wadogo na wakati kwani uzoefu wan chi nyingi unaonyesha kuwa wajasiliamali wadogo na wakati ndio walipaji wazuri wa mikopo

“Natoa wito kwa taasisi hizo kushirikiana na Sido pamoja na vyombo vingine vya kuendeleza wajasiliamali wadogo na wakati ili ziweze kubuni mbinu muafaka za kuwakopesha wajasiliamali na kutoa elimu itakayowawezesha wajasiliamali kukopesheka’alisema Dkt Chami

Alisema kuwa wajasiliamali wanakabiliwa na changamoto nyingi katika shughuli zao ikiwemo changamoto ya kutokujua kusoma vipimo hasa kwa wale wanaojihusisha na ujasiliamali wa mazao ya kilimo na misitu kama vile uuzaji wa mahindi,maharage,viazi,alizeti,ufuta na asali wamekuwa wakipata hasara sana na kurudisha nyuma ukuaji wa uchumi kwa mjasiliamali hivyo aliwataka wakala wa vipimo kuendelea kutoa elimu ya vipimo kwa wazalishaji hao ili kuweza kuleta ustawi na maendeleo sawa kwa wananchi wote

Akizungumza kwenye uzinduzi huo Mkurugenzi Mkuu wa Sido Michael Raizer alisema kuwa lengo la maonyesho hayo ni kuwawezesha wananchi kufahamu bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na viwanda vidogo nchini ili ziweze kuwasaidia katika harakati zao za kukuza uchumi

Raizer alisema kuwa maendeleo ya sekta ya wazalishaji wadogo na wakati ni muhimu sana kwa ukuaji wa uchumi endelevu na kuondoa umaskini hivyo licha ya serikali kuandaa sera ya ununuzi 2004 bado sera hiyo haijasaidia wazalishaji wadogo kwani sera hiyo haizazingatia umuhimu wa kukuza soko la ndani hasa kukuza bidhaa zinazozalishwa na viwanda vidogo

Awali Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Christine Ishengoma akimkaribisha mgeni rasmi alisema kuwa wajasiliamali wa mikoa ya kanda ya kusini wanatakiwa kuandaa mikakati ya kutumia fursa za ukanda wa maendeleo wa mtwara ili kuweka kitovu cha bidhaa zinazozalishwa kutokana na rasilimali zilizopo kwenye maeneo yetu ili wageni watakapokuja waweze kuona kuwa mikoa hii inatumia kikamilifu rasilimali zilizopo kuanzisha na kuendesha viwanda,kuongeza ajira na kipato

Aidha Dkt Ishengoma aliwataka wajasiliamali kuongeza ubora wa bidhaa na kuzalisha bidhaa kwa wingi kwani bidhaa bora zinauzika kwa haraka hivyo ni muhimu kuelewa kuwa tatizo la bidhaa zetu na nchi za nje siyo kukosa soko bali ni uwezo mdogo wa uzalishaji na usiozingatia mahitaji ya soko husika na ubora wa bidhaa
MWISHO


Friday, September 9, 2011

WANAFAMILIA WAMETAKIWA KUBORESHA MAHUSIANO YA KUMILIKI ARDHI


                                            Na Juma Nyumayo, Dar es Salaam,

KUTOKANA na migogoro mingi inayoibuka katika ngazi ya kaya na familia hapa nchini hali inayopelekea kuwa na mahusiano mabaya katika kuzalisha na kumiliki mali, familia hizo zimetakiwa kujenga na kuboresha mahusiano yao kwa kufuata vigezo vya uwazi na upendo hatua kwa hatua kabla mali wanazozalisha hazijawatesa kwa  kuwagombanisha kwa kile kinachodaiwa nani mmiliki halali kati ya mwanamke na mwanamume.

Hilo ni moja ya azimio lililofikiwa na washiriki wa warsha ya Uchumi na Ukombozi wa mwanamke   kimapinduzi inayoendeshwa  na Chuo cha Mafunzo ya Jinsia cha  TGNP katika Ukumbi wa kitivo cha Uhandisi Chuo Kikuu cha dar es Salaam.

Katika hali ya kubaini tatizo kuu la wanandoa pia familia nyingi kusambaratika kutokana na migogoro ya nani amiliki mali, au kurithi wanawarsha hao wamechambua mbinu mbalimbali na kuja na mapendekezo ambayo huenda yakapunguza tatizo linalozikabili familia nyingi hapa nchini hasa kutokana na mfumo dume unaomtenga mwanamke kumiliki mali hasa zenye thamani.

Sheikh wa wilaya ya Liwale, Adam Mpelengana, alisema ni muhimu kwa wanaume wote kutambua kuwa wanawake ni wasaidizi wa mwanamume na ni jukumu la mwanamume kumpenda na kumfanyia haki anazostahili badala ya kumuachia kazi nyingi bila usaidizi.
"Mwanamke anatakiwa aenziwe apendwe kwa kila namna, haifai kuendekeza mila na desturi za kumtumikisha mwanamke,' alisisitiza Sheikh Mpelengana.

Awali Mchungaji wa KKT toka Shinyanga, Odorus Gyunda , alisema ni muhimu kubainisha wazi ukatili wanaofanyiwa wanawake ni kinyume cha mapenzi ya mungu.
"imeelezwa wazi kuwa Mwanaume ampende mke wake na mwanamke amtii mumewe," alisema na kubainisha kuwa hayo hayawezekani kama hakuna upendo na mawasiliano mema katika uzalishaji na taratibu zote za kuishi.

Hata hivyo wanawarsha hao wamependekeza kuwa ili kusiwe na migogoro katika matumizi ya fedha na umiliki wa mali ni vyema wenza wakashiriki kikamilifu maamuzi ya kupanga utafutaji wa fedha au mali hatua kwa hatua mapema.

jambo jingine lililoelezwa ni wanawake na wanaume kwenye kaya zinazotegemea  kilimo wajue mahitaji yao ya chakula mapema wakati wa kuandaa mashamba ili wasije uza chakula chote kwa tamaa ya fedha.

Wakijadili suala la kudhibiti matumizi na kuweka kumbukumbu za mapato katika ngazi ya kaya washiriki hao wamependekeza kuwe na daftari la pamoja la kuwekea kumbukumbu za mapato na matumizi katika kila hatua.

Aidha wamewaasa wanawake kuwa makini na mchango wa nguvu kazi zao katika kuhudumia familia pia kuzalisha mali katika kaya na kuhoji matumizi na shughuli za kila mmoja katika kaya husika.

Vilevile imeelezwa wazi kuwa usafi na kujali afya za wanafamilia ni mtaji mkubwa katika kuleta mahusiano mema katika kutumia muda na kumiliki mali za kaya.

Washiriki hao hawakuishia hapo, walisema hayo yatawezekana iwapo, kutatengwa walao siku moja katika wiki kuzungumzia masuala na maendeleo ya kaya husika kwa kuwahusisha mume, mke na watoto ili kaya ziendeshwe  kwa shughuli na bajeti zenye mtazamo wa kijinsia zaidi. 
MWISHO

Thursday, September 8, 2011

RAIA 11 WA PAKISTANI NA BANGLADESHI KURUDISHWA MAKWAO

RAIA 11 WA PAKISTANI NA BANGLADESHI KURUDISHWA MAKWAO
Na Stephano Mango ,Songea.

WATU kumi na moja ambao ni raia wa Pakstani na Bangladesh waliokuwa wamekamatwa katika kijiji cha Magwamila kilichopo wilayani Songea mkoani Ruvuma wakitokea Msumbiji ambako walifukuzwa na askari wa Nchi hiyo kwa kupigwa na mijeredi sehemu mbalimbali za miili yao na kujeruhiwa wanatarajiwa kurejeshwa kwenye Nchi zao kwa kupitia ofisi za balozi za Nchi hizo hapa nchini.

Afisa uhamiaji wa Mkoa wa Ruvuma Koku Rwebandiza akizungumza jana na mtandao huu wa http://www.stephanomango.blogspot.com/ amesema kuwa raia hao wa Pakistan na Bangladesh kwa sasa hivi wanafanyiwa taratibu za kuwarejesha kwani walipokamatwa huko katika kijiji cha Magwamila walikutwa wakiwa na hati za kusafiria ambazo zilionekana kuwa na utata.

Rwebandiza alisema kuwa hati hizo za kusafiria ambazo walikutwa nazo watu hao ambao ni Raia wa Bangladesh na Pakstan hazioneshi ni lini waliingia Tanzania wakati wakitokea kwenye Nchi zao wala hazionyeshi ni lini waliondoka hapa Nchini na kuelekea Msumbiji ambako walikamatwa wakiwa katika eneo la Lichinga na askari wa Nchi ya Msumbiji.

Alisema kuwa kutokana na hali hiyo idara ya uhamiaji  mkoani Ruvuma imelazimika kuwarejesha raia hao kwenye balozi za Nchi zao ambazo ndizo zitakazoangalia ni namna gani zitawarudisha kwenye nchi zao.

Rwebandiza alisema kuwa raia hao kumi na moja wa nchi za pakistan na Bangaladesh walikamatwa mwanzoni mwa wiki huko katika kijiji cha magwamila kilichopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji ambapo inadaiwa walifukuzwa toka msumbiji kwa kupigwa mijeredi sehemu mbalimbali za miili yao na kunyang'anywa mali zao zote walizokuwa nazo pamoja na fedha na askari wa nchi ya Msumbiji kisha waliletwa hadi mpakani na kufukuziwa kijijini hapo huku wakiwa na majeraha.

Hata hivyo afisa uhamiaji Rwebandiza alisema kuwa raia hao baada ya kuwahoji walieleza kuwa wao walitoka Pakstan kwa pamoja kwa usafiri wa Ndege hadi Tanzania kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa jijini Dar es salaamu na baadae walitafuta usafiri wa basi hadi Mtwara ambako nako walifanikiwa kupata usafiri wa malori hadi wakafanikiwa kuvuka msumbiji ambako walinaswa na askari wa Nchi hiyo.

Raia hao ambao walikamatwa ni wapakistan watano ambao ni Hassan Bilali (20), Fawad Yassin (20), Mohamed Hawadhi(20),Haftari Hussein (24) na Hassad Hawadh (45) na raia toka Bangladesh waliokamatwa ni sita ambao ni Shahed Alzani (29) ,Amar Hamad (25),Garuan Khalifa(40),Mohamed Parvaz(35) ,Shajar Meya (28) na Sao Meya (28) .

MWISHO.

WANAHARAKATI WALALAMIKIA MIGOGORO YA ARDHI KUKWAMISHA MAENDELEO NCHINI

WALALAMIKIA MIGOGORO YA ARDHI KUKWAMISHA MAENDELEO

Na Juma Nyumayo, Dar es Salaam

MIGOGORO ya Ardhi inayoendelea katika mikoa mbalimbali nchini imetajwa kuwa ni kikwazo kikubwa cha maendeleo ya wanawake katika harakati zao za kujikwamua kiuchumi pia kuleta ukombozi wa mwanamke na maendeleo stahiki hapa nchini.

Hayo yameibuliwa na washiriki wa warsha inayoendelea katika Ukumbi wa Kitivo cha Uhandisi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati wa uwasilishaji wa mada ya mifumo na vikwazo vinavyozuia wanawake kujikwamua kiuchumi.

Akiwasilisha Mada hiyo, Mwezeshaji toka TGNP, Rehema Mwateba alisema ni vyema washiriki wakaeleza hali halisi ya umiliki wa ardhi na migogoro inayendelea kujitokeza hivi sasa ikilinganishwa na mifumo iliyopo katika kumkomboa mwanamke kimapinduzi.

Mshiriki mmojawapo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Morogoro,Kibena Kingo, ametolea mfano wa mapigano yanayoibuka mara kwa mara na yanayoendelea wilayani kwake kati ya wafugaji na wakulima, ambapo chanzo kikiwa ni matumizi ya Ardhi na kwamba mgogoro huo ni mkubwa.

Imeelezwa wafugaji hao wanaotokea mikoa ya kaskazini na kati wanalishia wanyama wao mazao ya wakulima bila kujali na hivyo kuwakwaza wananchi wenyeji ambao wengi wao ni wakulima wa mazao ya chakula.

"Mgogoro wa ardhi ni mkubwa na waathirika wakubwa ni wanawake na watoto, hata hivyo ni lazima hatua zichukuliwe ili kutatua migogoro hii kabla hayajatokea mauaji makubwa," alishauri Kingo.

Wakati kingo akielezea mgogoro wa ardhi Morogoro bado Mwezeshaji toka TGNP Darus Badi alipaza sauti yake na kuthibitisha kuwa mtandao huo una rekodi ya migogoro ipatayo 60 ya ardhi katika mkoa huo na kwamba kuna haja ya kulichukulia uzito tatizo hilo.

" Tuna migogoro tunayoijua kule Morogoro na tukiwa kama wanaharakati lazima tushirikiane kuchukua hatua," alisema Badi.

Naye Makamu Mwenyekiti wa halamashauri ya Mbinga Prisca haule alisema migogoro mingi ya ardhi huko Mbinga imeibuka kutokana na wakazi wa huko kutafuta maeneo ya kulima baada ya kuishiwa ardhi maeneo ya milimani.

"Kuna migogoro ya ardhi katika familia na nje ya familia kupigania ardhi ya kulima," alisema na kubainisha kuwa bado kuna mipango mibovu na sera isiyoeleweka katika umiliki wa ardhi.

Hata hivyo lawama azikuachwa kwa wawekezaji katika vitalu vya mbuga za wanyama hadi migodi ya madini kama ya Buzwagi, Geita hadi huko Namtumbo kwenye Urani( Uranium) ambako wananchi wa kawaida na hasa wanawake wanaona kama mchezo wa kuigiza wasijue kinachoendelea kwenye ardhi yao.

Lawama kibao zimeelekezwa pia kwa Mamlaka za vijiji na Miji kugawa ardhi kwa upendeleo na hasa kwa wale wanaotoa kitu kidogo kwaajili ya kupata viwanja vya makazi na kuwaacha kabisa wanawake nyuma.

Wakati wa Ufunguzi wa warsha hiyo, Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Jinsia ya TGNP, Dkt. Diana Mwiru, aliwaasa washiriki kujadili mada mbalimbali kwa lengo la kujenga uelewa na kusaidi jamii tunapoelekea kusherehekea tamasha la Jinsia na Mika 50 tangu Tanganyika kupata Uhuru wake.

Dkt. Mwiru,alisema, katika miaka 50 iliyopita wanawake wa nchi hii wameendelea kuachwa nyuma katika kumiliki na utoaji wa maamuzi juu ya rasilimali  ikiwa ni pamoja na ardhi.
Mwisho

WATATU WAJITOKEZA KUGOMBEA UDIWANI KATA YA MATIMILA WILAYA YA SONGEA

                                Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Songea Anna Mbogo

Na Gideon Mwakanosya,Songea.

WATU watatu wamejitokeza kuchukuwa fomu akiwemo katibu wa Mbunge wa Jimbo la Peramiho Menansi Komba za kuwania nafasi ya kiti cha udiwani kata ya Matimila Wilaya ya Songea vijijini Mkoa wa Ruvuma baada ya kuachwa wazi na aliyekuwa diwani wa kata hiyo Joseph Komba (CCM) kufariki dunia kwa ajari ya pikipiki.

Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu wa http://www.stephanomango.blogspot.com/ jana ofisini kwake Mkurugenzi wa uchaguzi jimbo la Peramiho Anna Mbogo amewataja waliochukuwa fomu kuwa ni Eliutelius Pili  wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Juma Gawaza wa chama cha wananchi CUF na Menansi Komba wa chama cha Mapinduzi(CCM).

Mbogo amesema kuwa hata hivyo mwisho wa kurudisha fomu hizo ni septemba 9 mwaka huu majira ya saa 10 jioni na kwamba kampeni zitaanza rasmi septemba 10 hadi Oktoba 1 mwaka huu majira ya sa 12 jioni.

Hata hivyo amewataka wananchi wa kata hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi ya udiwani siku ya oktoba 2 mwaka huu kwani kumekuwepo na mazoea ya kutojitokeza kwenye zoezi la upigaji kura hali inayopelekea udororaji wa demokrasia nchini.

Mkurugenzi wa uchaguzi wa jimbo hilo ambaye pia ni kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Songea  Mbogo amesema kuwa uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi ya kiti cha udiwani katika kata ya Matimila unatarajiwa kufanyika oktoba 2 mwaka huu kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo  Joseph Komba aliyefariki kwa ajari ya pikipiki wakati anaendesha kijijini hapo Machi 9 mwaka huu.