Friday, April 20, 2012
ADAIWA KUJINYONGA KWA SABABU ZA WIVU WA KIMAPENZI
KAMANDA WA POLISI MKOA WA RUVUMA MICHAEL KAMHANDA
Na Augustino Chindiye, Tunduru
MSONGO wa mawazo uliotokana na wivu wa kimapenzi umesababisha kifo cha Mkazi wa Mtaa wa Kasuguru Mjini Tunduru aliyefahamika kwa jina la Said Issa (43) aliyefariki dunia baada ya kujinyonga.
Taarifa za tukio hilo zinaeleza kuwa kabla ya kukumbwa na umauti Marehemu Issa alitoweka na kupotelea kusiko julikana March 31 Mwaka huu kabla ya mwili wake kuokotwa April 16 mwaka huu ukiwa vipande vipande kutokana na kuharibika vibaya.
Taarifa hiyo iliendelea kufafanua kuwa kutokana na mwili wake kuharibika vibaya ambapo mashuhuda hao walikuta baadhi ya viungo vikiwa vimetawanywa katika maeneo tofauti huku vingine vikiwa vimeanza kuliwa na wanyama na kufanikiwa kumzika akiwa hana kichwa
Akizungumzia mkasa huo mdogo wa marehemu Isaa Matumla alisema kuwa marehemu kaka yake huyo alianza kuchanganyikiwa siku chache baada ya kuachwa na Mkewe ambaye alidaiwa kuchukua uamuzi huo kwa lengo la kupumzika maisha ya shida waliyo kuwa wakiishi kwa muda mrefu kutokana na mumewe huyo kutokuwa na uwezo kifedha.
Alisema kufuatia mkasa huo Marehemu alionesha kuchanganyikiwa kiakili na kuwa mlevi wa kupindukia hatimaye akaamua kuchukua uamuzi huo wa kukatisha maisha yake kwa kujinyonga akiwa mafichoni katika msitu ulozunguka mashamba ya Shule ya Sekondari Tunduru.
Mganga aliyeufanyia uchunguzi mwili wa Marehemu Issa Dkt. Joseph Ng`ombo alidai kuwa chanzo cha kifo hicho kilisababishwa na tukio la kujifunga kamba shingoni na kujining`iniza juu ya mti kabla ya mwili wake kuanguka chini na kuharibika vibaya.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Mchael Kamuhanda mbali ya kuthibitisha kuwepo kwa tukio hilo alisema kuwa polisi bado wanaendelea na uchunguzi wa kifo hicho.
Mwisho
Thursday, April 19, 2012
GARI NA PIKIPIKI ZAGONGANA NA KUSABABISHA KIFO WILAYANI MBINGA
KAMANDA WA POLISI MKOA WA RUVUMA MICHAEL KAMHANDA
NA DUSTAN NDUNGURU ,SONGEA.
MTU mmoja mkazi wa Mbinga mjini mkoani Ruvuma amefariki dunia na mwingine kujeruhiwa vibaya baada ya gari na pikipiki kugongana katika kijiji cha Makatani.
Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Maiko Kamuhanda alisema kuwa ajali hiyo imetokea aprili 16 mwaka huu majira ya saa 11.45 katika barabara itokayo Mbinga mjini kuelekea Mpepo.
Kamuhanda alisema kuwa pikipiki aina ya Honda XLR yenye namba za usajili T941 AGJ iliyokuwa ikiendeshwa na Naftari Tweve akiwa amembeba airia mmoja aliyetajwa kwa jina la Yacob Ndunguru imehusika na ajali hiyo.
Alisema kuwa pikipiki hiyo iligongana uso kwa uso na gari aina ya 110 T779 BUU iliyokuwa ikiendeshwa na Saulo Mapunda na kusababisha kifo cha dereva wa pikipiki Naftari Tweve ambaye alifariki baada ya kufikishwa katika hospitali ya wilaya ya Mbinga.
Kamanda huyo alimtaja majeruhi kuwa ni Yacob Ndunguru ambaye alipanda pikipiki na kwamba amelazwa katika hospitali hiyo na hjali yake bado ni mbaya.
MWISHO.
Tuesday, April 17, 2012
MADIWANI WALILIA ONGEZEKO LA POSHO KUTOKANA NA UGUMU WA MAISHA
Na Augustino Chindiye,Tunduru
MADIWANI wa halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma wameibuka na kulilia nyongeza ya
maslahi yao likiwemo ongezeko fidia,nauli na posho za vikao.
Hayo ni miongoni mwa mambo yaliyo ibuka katika kikao cha kawaida cha Baraza la halmashauri hiyo lililo keti katika ukumbi wa Klasta Mjini hapa.
Huku akishangiliwa na Madiwani wenzie katika kikao hicho Diwani wa kata ya Marumba Msenga Said Msenga alisikika akilalama na kuiomba Serikali kutambua na kuona umuhimu wa kuwaongezea mafao pamoja na posho wakati wa vikao.
“Umefika wakati wa Serikali kutuona sisi tunao wawakilisha wananchi ngazi hiyo ya kata maeneo yaliyopo vijijini fedha tunazopata zote zinaishia njiani kutokana na gharama za usafiri na za maisha kuwa juu “ alisema Msenga
Katika taarifa hiyo Diwani huyo alitolea mfano wa madiwani hao kulipwa nauli ya Shilingi 3500 kwa madiwani wanaotoka vijijini lakini wakati huo hali halisi wao hutozwa kati ya shilingi 7,000 na 8,000 kutokana na hali ya maisha kupanda.
Diwani huyo ambaye alionekana wazi kuungwa mkono na madiwani wenzakealifikia hatua ya kupendelezwa kuwa posho zao ziongezeke hadi kufikia shilingi Milioni 3 kutoka Shilingi 120,000 ambazo wamekuwa wakilipwa hivi sasa kwa mwezi.
Mambo mengine yaliyo ibuka katika kikao hicho ni lawama za madiwani hao kwa Serikali wakiituhumu kuchelewesha fedha hali ambayo imepelekea miradi mingi kukwama na kusababisha kero kwa wananchi.
Akifafanua kero hiyo Mtoaji wa kero hiyo Makamu mwenyekiti wa halamashauri ya Wilaya hiyo Diwani wa kata ya Nakayaya Charles Haule alisema kuwa pamoja na kukiweka chama tawala katika wakati mgumu katika chaguzi zijazo.
Alima pamoja na hali hiyo pia hivi sasa asilimia kubwa ya wananchi imeonekana kukatishwa tamaa na utendaji wa viongozi waliopo madarakani kutokana na kushindwa kusimamia maendeleo na kufanya miundombinu hasa ya barabara kushindwa kupitika wakati wote wa mwaka.
Hata hivyo Haule alitumia nafasi hiyo kuwataka madiwani wenzake kuendelea kutoa hamasa kwa wananchi ili waongeze juhudi za kushiriki katika shughuli za kimaendeleo tofauti na sasa ambapo wamekuwa wakigoma kufanya kazi hizo wakiamini kuwan miradi yote imekuwa ikitengewa fedha za kutosha kutekeleza miradi hiyo kwa asilimia 100.
Awali akiongea katika kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya hiyo alikiri kuwepo mrundikano wa mirani viporo hali iliyoonesha kuwepo kwa tatizo la ucheleweshwaji wa fedha za miradi kutoka Serikali kuu.
Mwisho
MADIWANI wa halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma wameibuka na kulilia nyongeza ya
maslahi yao likiwemo ongezeko fidia,nauli na posho za vikao.
Hayo ni miongoni mwa mambo yaliyo ibuka katika kikao cha kawaida cha Baraza la halmashauri hiyo lililo keti katika ukumbi wa Klasta Mjini hapa.
Huku akishangiliwa na Madiwani wenzie katika kikao hicho Diwani wa kata ya Marumba Msenga Said Msenga alisikika akilalama na kuiomba Serikali kutambua na kuona umuhimu wa kuwaongezea mafao pamoja na posho wakati wa vikao.
“Umefika wakati wa Serikali kutuona sisi tunao wawakilisha wananchi ngazi hiyo ya kata maeneo yaliyopo vijijini fedha tunazopata zote zinaishia njiani kutokana na gharama za usafiri na za maisha kuwa juu “ alisema Msenga
Katika taarifa hiyo Diwani huyo alitolea mfano wa madiwani hao kulipwa nauli ya Shilingi 3500 kwa madiwani wanaotoka vijijini lakini wakati huo hali halisi wao hutozwa kati ya shilingi 7,000 na 8,000 kutokana na hali ya maisha kupanda.
Diwani huyo ambaye alionekana wazi kuungwa mkono na madiwani wenzakealifikia hatua ya kupendelezwa kuwa posho zao ziongezeke hadi kufikia shilingi Milioni 3 kutoka Shilingi 120,000 ambazo wamekuwa wakilipwa hivi sasa kwa mwezi.
Mambo mengine yaliyo ibuka katika kikao hicho ni lawama za madiwani hao kwa Serikali wakiituhumu kuchelewesha fedha hali ambayo imepelekea miradi mingi kukwama na kusababisha kero kwa wananchi.
Akifafanua kero hiyo Mtoaji wa kero hiyo Makamu mwenyekiti wa halamashauri ya Wilaya hiyo Diwani wa kata ya Nakayaya Charles Haule alisema kuwa pamoja na kukiweka chama tawala katika wakati mgumu katika chaguzi zijazo.
Alima pamoja na hali hiyo pia hivi sasa asilimia kubwa ya wananchi imeonekana kukatishwa tamaa na utendaji wa viongozi waliopo madarakani kutokana na kushindwa kusimamia maendeleo na kufanya miundombinu hasa ya barabara kushindwa kupitika wakati wote wa mwaka.
Hata hivyo Haule alitumia nafasi hiyo kuwataka madiwani wenzake kuendelea kutoa hamasa kwa wananchi ili waongeze juhudi za kushiriki katika shughuli za kimaendeleo tofauti na sasa ambapo wamekuwa wakigoma kufanya kazi hizo wakiamini kuwan miradi yote imekuwa ikitengewa fedha za kutosha kutekeleza miradi hiyo kwa asilimia 100.
Awali akiongea katika kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya hiyo alikiri kuwepo mrundikano wa mirani viporo hali iliyoonesha kuwepo kwa tatizo la ucheleweshwaji wa fedha za miradi kutoka Serikali kuu.
Mwisho
| Mratibu wa Mradi wa TOT juu ya uchanganuzi na uchambuzi wa sera ya maendeleo ya wanawake na Jinsia Wilaya ya Songea Samwel Chiwangu akieleza neno la utangulizi wakati wa mafunzo hayo jana |
| Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Charles Mhagama akifungua mafunzo hayo, kulia ni Katibu wa mafunzo Mathew Ngarimanayo na kushoto ni Mwenyekiti wa mafunzo Fatuma Misango |
| Washiriki wa mafunzo hayo wakiendelea kusikiliza mada mbalimbali kutoka kwa wawezeshaji |
| Washiriki wakiendelea na mafunzo |
WANANCHI WATAKIWA KUHESHIMU HAKI ZA BINADAMU
Na Stephano Mango,Songea
WANANCHI wametakiwa kuheshimu haki za binadamu kwa kuzingatia kanuni,taratibu na sheria ili kila mtu aweze kuishi kwa amani na upendo katika jamii yake na nchi kwa ujumla kuliko kujichukulia sheria mkononi na kusababisha kukatisha uhai wa mwenzio
Wito huo umetolewa jana na Mratibu wa mafunzo ya uchanganuzi na uchambuzi sera ya maendeleo ya wanawake na jinsia Wilaya ya Songea Samwel Chiwangu yaliyoitishwa na Asasi ya Ruwodefu ambayo yanayofanyika kwa siku tatu kwenye ukumbi wa Saccos kwa ufadhiri wa shirika la The Foundation For Civil Sociaty
Chiwangu alisema kuwa inasikitisha kusikia matukio ya ukatili wa kijinsia yakiendelea kushamiri kwa kasi kubwa mkoani Ruvuma tofauti na utamaduni uliozoeleka miongoni mwa wananchi wa jamii za mkoa huo hali ambayo inatishia ustawi wa jamii
Alisema kuwa taarifa ya vifo vya kujinyonga,kupigana,kuchinjana kutokanana na mahusiano ya kimapenzi na matatizo mengine ya kijamii vinashamiri kila siku hali ambayo inaonyesha mashaka makubwa kwa wananchi
“Wanaharakati tunapaswa tusikitike sana na taarifa hizo na tuchukue hatua kukomesha hali hiyo, kwani mtu unayempenda huwezi kumuua kwa sababu za kukunyima penzi au kumkuta mpenzi wako na mwanaume au na mwanamke mwingine hivyo kama kweli unampenda utamlinda na vishawishi vinavyoweza kupunguza upendo wake kwako na sio kumuua”alisema Chiwangu
Alisema kuwa haki ya kuishi ni haki kubwa kuliko zote na kwamba hakuna mtu mwenye mamlaka ya kuondoa uhai wa mwenzake kwa sababu yoyote ile kwani mwenye uwezo na mamlaka hayo ni mwenyezi mungu pekee yake ni vema kazi yake tukamuachia
Alisema kuwa jambo hilo halipaswi kuvumiliwa hata kidogo hivyo ni vema viongozi wa dini na wakijamii pamoja na Serikali kushirikiana kikamilifu kudhibiti jambo hilo kwani kabla vifo havijatokea kunakuwepo na dalili za kutokuwa na amani miongoni mwa wapenzi hao tujaribu kusuluhisha migogoro kwa taratibu za mila na desturi na kwamba ikishindikana basi sheria itumike kudhibiti vifo hivyo
Akifungua mafunzo hayo Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Charles Mhagama alisema kuwa wanawake nchini wanatakiwa kuacha uwoga wa kutoa taarifa za ukatili wa kijinsia kwenye vyombo vya habari ili kuweza kujenga mazingira ya kukomesha ukatili mbalimbali wa kijinsia uliokithili miongoni mwa jamii zinazotuzunguka
Mhagama alisema kuwa vyombo vya habari ni wadau muhimu sana katika harakati za ukombozi wa mwanamke wa kimapinduzi hasa wakati huu ambao taifa letu linaelekea kwenye miaka 50 ya uhuru ili kuweza kuzibaini changamoto mbalimbali za wanawake zilizokuwa zinawakabili wanawake miaka hiyo na sasa tuweke mikakati mingine ya kuzikabili changamoto za sasa
Awali Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Ruwodefu Hieromina Lugomi alisema kuwa mafunzo hayo yanalengo la kuwajengea uwezo wananchi kutambua fursa zilizomo ndani ya sera ya wanawake na jinsia ili waweze kunufaika nayo
Lugomi alisema kuwa watu wanaohudhuria mafunzo hayo kwa lengo la kupata elimu,kubadilishana mawazo na kuangalia maeneo muhimu yaliyopo kwenye sera hiyo na kuishawishi Serikali iyafanyie kazi maeneo hayo ni pamoja na vikundi vya wajasiriamali, viongozi wa dini, viongozi wa siasa,na vikundi vya wafanyabiashara
Alisema kuwa washiriki watapata fursa ya kujadili kwa upana haki za binadamu,madhumuni ya sera ya wanawake na jinsia, malengo ya sera, maana ya jinsia, usawa wa kijinsia,mgawanyo wa madaraka, umiliki wa rasilimali sheria ya ndoa na mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia
MWISHO
AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 30 KWA KOSA LA UBAKAJI
NA DUSTAN NDUNGURU, MBINGA.
MKAZI mmoja wa kijiji cha Kihuru wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma amehukumiwa na mahakama ya wilaya adhabu ya kifungo cha miaka 30 kwenda jela kwa kosa la kumbaka msichana wa miaka 15.
Akisoma hukumu hiyo hakimu mkazi katika mahakama ya wilaya ya Mbinga Joakim Mwakyolo alisema kuwa mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka kuwa Dickson Komba alitenda kosa hilo la ubakaji.
Mwakyolo alisema kuwa mahakama imemtia hatiani Komba na kuhukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka 30 kwenda jela ili liwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.
Mara baada ya kusomewa hukumu hiyo mshitakiwa alibubujikwa na machozi huku akiangua kilio mahakamani hapo na kuomba kwa sauti apunguziwe adhabu.
Awali mwendesha mashitaka wa polisi inspekta Mwamba alidai mahakamani hapo kuwa mshitakiwa Komba alitenda kosa la kumbaka msichana huyo akiwa anaenda dukani machi 5 mwaka jana majira vya saa 3 usiku.
Aliendelea kudai kuwa pamoja na kumfanyia kitendo hicho pia alimpora simu moja aina ya Nokia yenye thamani ya shilingi 130,000 na fedha tasilimu shilingi 15,000 mali ya Essau Dukila.
MWISHO.
Monday, April 16, 2012
MBUNGE APINGA KUPITISHA BAJETI LAKINI AZIDIWA KETE NA MADIWANI
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA TUNDURU EPHRAIM OLE NGUYAINE
Na Augustino Chindiye, Tunduru
BARAZA la Madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma limepitisha rasimu ya Mapngo wa bajeti ya mapato na matumizi ya Shilingi Bilioni 26.775 itakayotumika katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2012/2013 huku Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini Eng. Ramo makani na Diwani wa Kata ya Nakapanya Halifa Wadari wakidai kutoiunga mkono bajeti hiyo.
Sambana na Mbunge huyo kukwamisha Bajeti hiyo isipite pia akatoa kauli ya kushinikiza halmashauri hiyo kubadirisha matumizi ya Shilingi Milioni 300 zilizopangwa kutumika kujengea kilometa Tatu za Barabara kwa kiwango cha Lami iliyo pangwa kutekelezwa katika kipindi cha utekelezaji wa Bajeti hiyo zikiwa ni juhudi za halmashauri hiyo kuboresha mji huo akidai kuwa fedha hizo zipelekwe kujenga barabara za vumbi.
Bajeti hiyo ambayo ilipita kwa madiwani kupiga kura baada ya Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Faridu Hamisi kubaini kuwepo kwa mkanganyiko huo imebainisha kuwa kati ya fedha hizo Shingi Bilioni 1.584 zitatokana na mapato ya ndani na shilingi Bilioni19.081zitatoka na Ruzuku kutoka serikali kuu.
Taarifa hiyo iliendelea kufafanua kuwa katika klipindi hicho pia halmashauri hiyo imepanga kutumia Jumla ya Shilingi bilioni 28,775,774,730 ambapo kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni 19,0861,316,160 zitatumia katika matumizi ya kawaida, mishahara Shilingi Bilioni 16,653,115,160.
Upande wa kifungu cha matumizi mengineyo bajeti hiyo imekipangia Shilingi Bilioni 2,428,201,000, fedha kwa ajili ya maendeleo zimepangwa ni Shilingi Bilioni 8,109,726,570 huku bajeti hiyo ikielezwa kuwa na ongezeko la asilimia 37 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2012/2012.
Wakichangia kwa nyakati tofauti katika kikao hicho ambacho kilionekana wazi kumshinda kukiendesha Mwenyekiti wake kutokana na kuruhusu wajumbe kuchangia zaidi ya mara moja na kukiuka miongozo ya vikao vya mabaraza katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Klasta mjini hapa watoa pingamizi la kuto unga mkono bajeti hiyo walidai kuwa maandali zi yake hayakuzingatia uwiano wa ugawaji wa miradi katika kata zote 24/
Akifafanua kauli ya ombi lake la kubadilishwa kwa matumizi ya fedha za barabara ya Lami Eng. Ramo alisema Mradi huo wa kujenga Kilometa Tatu ndani ya Mji wa Tunduru utakao ghalimu Shilingi Milioni 300 ni matumizi mabaya rasilimali kwani mradi huo hautakuwa na manufaa yoyote kwa madai kuwa fedha hizo zingewekwa katika mradi wa kutengeneza barabara vijjini kwa kiwango cha Changarawe halmashauri hiyo ingewawezesha wakulima wengi kusafirisha mazao yao na kuyapeleka katika masoko.
“Mimi kama mwakirishi wa wananchi wa Jimbo la Tunduru Kaskazini Siungi mkono Bajeti hii na msimamo wangu ni fedha hizo zibadilishiwe matumizi na kupelekwa kutengeneza barabara za Vijijini ziweze kuwasaidia wananchi wengi zaidi kuliko kutengeneza Barabara ya lami ambayo haitawanufaisha wengi na itajengwa katika kieneo kidogo “ alisema Eng. Ramo.
Aidha viongozi hao pia wakabainisha kuwa Bajeti hiyo imependelea na kupeleka miradi mingi zaidi upande wa Jimbo la Tunduru Kusini kutokana kupeleka miradi mingi zaidi ikilinganishwa na miradi iliyo ainishwa kutekelezwa katika Kata za Jimbo la Tunduru Kaskazini.
Pamoja na viongozi hao kutofautia na madiwani wenzao kutokana na ushindi walioupata kutokana na kupiga kura, Diwani wa kata ya Nandembo alitolea mfano kutokana na kilichodaiwa kupangiwa miradi mindi Anitha Komba aliinuka na kueleza wazi wazi kuwa kitendo kilichofanywa na mbunge huyo ni mbaguzi na hakiitakii maendeleo ya dhati wilaya yao.
Akijibu tuhuma hizo Mkurugenzi matendaji wa halmashauri ya Wilaya hiyo Ephraim Ole Nguyaine alimtaka Mbunge huyo kuheshimu kanuni na miongozo ya uendeshaji wa mabaraza akikataa kata kata kuwa hawezi kukubaliana na maelezo ya viongozi hao waliotaka bajeti hiyo ijadiliwe upya katika ukumbi huo.
Guyainne aliendelea kueleza kuwa kabla ya kukamilika kwa mchakato huo bajeti hiyo ilipitiwa na kamati husika na kuidadavua kwa mapana na marefu hivyo kitendo cha viongozi hao kutaka bajeti hiyo ijadiliwe upya inalenga kukiuka taratibu na miongozo iliyo wekwa na mamlaka husika.
Alifunga kikao hicho Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya hiyo diwani Faridu hamisi alissitiza kuwa halmashauri yake itasimamia kwa makini na kuhakikisha kuwa fedha hizo zinatumika kulingana na matumizi yaliyo elekezwa.
Mwisho
HALMASHAURI YA WILAYA YA MBINGA KUJENGA STENDI YA KISASA KWA BILIONI 1.5
MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBINGA ODDO MWISHO
NA DUSTAN NDUNGURU MBINGA.
HALMASHAURI ya wilaya ya mbinga mkoani Ruvuma,imetenga kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha mabasi na majengo mawili yatakayotumika kwa ajili ya maduka kwa wafanyabiashara wilayani humo.
Akizungumza wakati wa utiliaji saini kati ya halmashauri hiyo na mkandarasi aliyepewa kazi hiyo kampuni ya GNMS kutoka mkoani Iringa,mwenyekiti wa halmashauri hiyo Oddo Mwisho alisema licha ya kujenga eneo la kuegesha magari lakini kutakuwa na majengo mawili yatakayokuwa na maduka.
Alisema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kuongezeka kwa mahitaji ya wananchi wa wilaya hiyo hasa wale wenye vyombo vya moto ambao wamekuwa wakipata shida ya kuegesha magari yao pindi wanapotaka kuingia kituoni hapo,na mahitaji mengine yakiwemo ya maeneo ya kufanyia biashara.
Mwisho alisema mkataba wa ujenzi wa kituo hicho cha mabasi unalenga kuboresha huduma za usafiri,usafi na hata ulinzi kwani hapo mwanzo ilikuwa ni kazi ngumu kufanya vitu hiyo kutokana na eneo ilo lilivyo hasa baada ya kuongezeka kwa idadi ya magari.
Kuhusu fedha za mradi huo alisema kuwa fedha ziko tayari na kwamba kazi ya ujenzi inatarajiwa kuanza muda wowote kuanzia sasa ili hatimaye iweze kukamilika kwa wakati uliopangwa.
Alifafanua kuwa fedha za mradi huo zimepatikana kutoka mfuko wa kuzipatia ruzuku halmashauri, chini ya wizara ya serikali za mitaa(TAMISEMI)ambayo imetoa kiasi cha shilingi bilioni 1.3 na kiasi kilichobaki cha shilingi milioni 200 ni fedha za halmashauri yenyewe kutokana na mapato yake ya ndani.
Pia aliongeza kuwa halmashauri ya wilaya ya Mbinga imejipanga katika utekelezaji wa ahadi za chama cha mapinduzi(CCM) ilizotoa kwa wananchi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2010 kuwa itajenga kituo kipya cha mabasi na kuboresha baadhi ya maeneo muhimu yakiwemo hospitali zake zote,barabara za mitaa na huduma ya maji.
Juu ya mkakati wa kuongeza mapato ya halmashauri Mwisho alisema wamejipanga vizuri na hamashauri ya mbinga imeshaanza kuchukua hatua kwa kutenga eneo kwa ajili ya ujenzi wa mahoteli na imeshatuma baadhi ya wataalam wake kwenda mkoani Mbeya kuangalia michoro ya soko la kisasa la Mwanjelwa ili nao wajenge soko linaloweza kufafanana na ilo kwa lengo la kuboresha huduma kwa wananchi kuiongeza vitega uchumi kwa halmasghauri yao.
Naye mkurugenzi wa halmashauri hiyo Shaibu Nnunduma aliwaomba wananchi wa mbinga kutunza miradi hiyo ambayo ipo kwa faida yao na kuona kuona umuhimu wa kuitunza ili kufanikisha kazi iliyokusudiwa kwa ajili ya kuiletea halmashauri fedha nyingi zitakasaidia kuboresha hudunma za jamii katika wilaya hiyo.
Alisema miradi hiyo inagharimu kiasi kikubwa cha fedha ambazo ni za kwao hivyo kinachotakiwa ni kuhakikisha kuwa inatunzwa na kwamba wawe macho na watu wenye tabia ya kuhujumu.
MWISHO.
Akizungumza wakati wa utiliaji saini kati ya halmashauri hiyo na mkandarasi aliyepewa kazi hiyo kampuni ya GNMS kutoka mkoani Iringa,mwenyekiti wa halmashauri hiyo Oddo Mwisho alisema licha ya kujenga eneo la kuegesha magari lakini kutakuwa na majengo mawili yatakayokuwa na maduka.
Alisema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kuongezeka kwa mahitaji ya wananchi wa wilaya hiyo hasa wale wenye vyombo vya moto ambao wamekuwa wakipata shida ya kuegesha magari yao pindi wanapotaka kuingia kituoni hapo,na mahitaji mengine yakiwemo ya maeneo ya kufanyia biashara.
Mwisho alisema mkataba wa ujenzi wa kituo hicho cha mabasi unalenga kuboresha huduma za usafiri,usafi na hata ulinzi kwani hapo mwanzo ilikuwa ni kazi ngumu kufanya vitu hiyo kutokana na eneo ilo lilivyo hasa baada ya kuongezeka kwa idadi ya magari.
Kuhusu fedha za mradi huo alisema kuwa fedha ziko tayari na kwamba kazi ya ujenzi inatarajiwa kuanza muda wowote kuanzia sasa ili hatimaye iweze kukamilika kwa wakati uliopangwa.
Alifafanua kuwa fedha za mradi huo zimepatikana kutoka mfuko wa kuzipatia ruzuku halmashauri, chini ya wizara ya serikali za mitaa(TAMISEMI)ambayo imetoa kiasi cha shilingi bilioni 1.3 na kiasi kilichobaki cha shilingi milioni 200 ni fedha za halmashauri yenyewe kutokana na mapato yake ya ndani.
Pia aliongeza kuwa halmashauri ya wilaya ya Mbinga imejipanga katika utekelezaji wa ahadi za chama cha mapinduzi(CCM) ilizotoa kwa wananchi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2010 kuwa itajenga kituo kipya cha mabasi na kuboresha baadhi ya maeneo muhimu yakiwemo hospitali zake zote,barabara za mitaa na huduma ya maji.
Juu ya mkakati wa kuongeza mapato ya halmashauri Mwisho alisema wamejipanga vizuri na hamashauri ya mbinga imeshaanza kuchukua hatua kwa kutenga eneo kwa ajili ya ujenzi wa mahoteli na imeshatuma baadhi ya wataalam wake kwenda mkoani Mbeya kuangalia michoro ya soko la kisasa la Mwanjelwa ili nao wajenge soko linaloweza kufafanana na ilo kwa lengo la kuboresha huduma kwa wananchi kuiongeza vitega uchumi kwa halmasghauri yao.
Naye mkurugenzi wa halmashauri hiyo Shaibu Nnunduma aliwaomba wananchi wa mbinga kutunza miradi hiyo ambayo ipo kwa faida yao na kuona kuona umuhimu wa kuitunza ili kufanikisha kazi iliyokusudiwa kwa ajili ya kuiletea halmashauri fedha nyingi zitakasaidia kuboresha hudunma za jamii katika wilaya hiyo.
Alisema miradi hiyo inagharimu kiasi kikubwa cha fedha ambazo ni za kwao hivyo kinachotakiwa ni kuhakikisha kuwa inatunzwa na kwamba wawe macho na watu wenye tabia ya kuhujumu.
MWISHO.
Friday, April 13, 2012
MKUU WA MKOA MWAMBUNGU UMENENA, NAKUUNGA MKONO KWANI NAMI NIMEWAHI KUANDIKA MAKALA HAYA
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya SongeaoCharles MhagamaHALI YA USAFI KATIKA MANISPAA YA SONGEA IMESHINDIKANA?Na Stephano Mango,SongeaHALI ya usafi ambayo tulizoea kuiona katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea ambayo ndiyo makao makuu ya mkoa wa Ruvuma sasa imeanza kutoweka polepole hasa katika maeneo ya ghuba za kuhifadhia takataka na mifereji ya maji katika baadhi ya barabara mjini hapa .Uchunguzi wa kina uliofanywa na Dira ya Mtanzania umebaini kuwa Manispaa ya Songea kuna ghuba nyingi ambazo zimekuwa kero kwa wakazi na kwamba ghuba hizo zina dalili zote za kuzalisha magonjwa ya kuambukiza hasa kipindi hiki tunapoelekea masika .Baadhi ya wakazi wa Manispaa hiyo wameulalamikia uongozi wa Halmashauri hiyo kwa kushindwa kujali afya za wananchi wake kwani pamoja na ghuba zao kujaa takataka na zingine kuanza kuzagaa na kusababisha watoto kuchezea hali inayoweza kupelekea hatari kwa ustawi wao.Kwa sasa hali ya Manispaa hiyo ilivyo haimvutii mtu kuja kupumzika au kufanya shughuli zozote za burudani kutokana na uchafuzi wa mazingira uliokithiri kwenye viunga vya mjini hapa.Hakuna bustani iliyotunzwa vizuri kwa kuvutia hata watalii kupumzika ukiachia wakazi wa mji wa Songea kutokana na mipango mibovu ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea ambayo inaonekana ndio chanzo cha uchafuzi wa mazingiraKwani imeshindwa kutenga maeneo ya kuweka bustani za kupumzika wakazi wa Manispaa hiyo wakati wa mchana au wa jioni tofauti na miji mingine ambayo inathamini maeneo hayo muhimu kwa wananchi wake.Hata bustani za miti,maua na mboga mboga zipo chache na hazionekani kiurahisi kutokana na mipango yake mibovu inayosabibisha hewa ya Manispaa kuwa nzito kutokana na uchafu wa mazingira unaoendelea kukithiriNi wazi kuwa swala la usafi wa mazingira katika Manispaa hiyo bado halijatiliwa mkazo kwani wananchi wanajitahidi kukusanya takataka pamoja lakini haziondolewi jambo hili linawakera na kuonekana wazi kuwa mamlaka husika haziwajibikiKwani ili wananchi wawe na afya njema na hatimaye waweze kumudu kazi zao vizuri kwa kutopata magonjwa ya mlipuko ni lazima usafi uzingatiwe katika maeneo wanamoishi.Kila mwaka kumekuwa na taarifa za watu kupatwa na ugonjwa wa kipindupindu kutokana na kushamiri kwa uchafu unaotupwa hovyo huku ikifahamika kuwa ni hatari kwa afya za binadamu.Licha ya kuzagaa kwa mifuko ya plastiki na makopo mitaani kutokana na kutupwa ovyo na watumiaji wake kutokana na kuzipuuza kanuni na sheria ndogo za Halmashauri au kutozijua kwa wananchi wengiUkipita katika mitaa ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea ni lazima utakutana na malundo ya takataka ambayo yameoza na kupelekea kutoa halufu mbaya kutokana na uzembe wa watendaji wa Manispaa hiyo.Hali hiyo pia ipo katika Masoko ya Manispaa hiyo kama vile Soko la Manzese,Mfaranyaki,Bombambili,Majengo na Soko kuu la Songea kwani kutokana na watendaji wake kutosimamia sheria na kanuni za usafi katika maeneo hayoKumepelekea wafanyabiashara kutupa taka ovyo na kusababisha harufu mbaya kutokana na kuoza kwa taka hizo ambazo nyingi huwa zile za majimaji ya nyanya,maembe,machungwa,maji yaliyooshewa utumbo wa nyama na vyakula vilivyolala.Ili suala la kuzagaa kwa uchafu katika maeneo ya Manispaa ya Songea libaki historia viongozi wa Serikali hiyo wanapaswa kuonyesha mfano wa kusafisha mazingira kwa vitendo.Endapo Serikali hiyo inataka ifanikiwe katika operesheni ya kuboresha usafi wa mazingira ni lazima waache kuzungumzia usafi maofisini na kwenye majukwaa na badala yake waonyeshe mfano kwa wananchi kwa wao kujumuika nao na kusafisha mazingira.Viongozi waonyeshe mfano kwa wananchi kwa sababu mfumo wa namna hii unafanyika duniani kote ili kuboresha mazingira ,kwani kwa wale viongozi wanaowaelimisha wananchi jukwaani baadae huwafuata katika maeneo yao na kujumuika pamoja katika kusafisha mazingira yao.Serikali inapaswa kubadilika kwa kuchukua suala la usafi wa mazingira kimatendo zaidi na si maneno mengi ambayo hayaleti mabadiliko yeyote katika suala zima la usafiIkiwa ni pamoja na kuzikabili changamoto nyingi zilizopo ikiwemo za vifaa vya kuzolea taka,uelewa mdogo wa elimu ya usafi wa mazingira kwa wananchi,ikiwa na kuziweka wazi kanuni na sheria ndogo za usafi wa mazingira.Ili wananchi waweze kutambua wajibu wao kikamilifu na umuhimu wa utunzaji wa mazingira yao kwa afya na ustawi wao kwani bila kufanya hivyo ufanisi wa jambo hilo unaweza usifikie viwango stahiki.Mwandishi anapatikana Simu 0755-335051 www.stephanomango.blogspot.com |
TANGAZO LA NAFASI YA KAZI LIMETOLEWA NA OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUVUMA
TANGAZO LA NAFASI YA KAZI
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Sehemu ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na wafadhili Walter Reed, wanatangaza nafasi za kazi kama ifuatavyo:-
1. PROGRAMME OFFICER: NAFASI MOJA (1)
Kazi za kufanya:
· Kusimamia na kuratibu shughuli za mpango wa Huduma kwa wanaoishi na Virusi vya UKIMWI kwa kushirikiana na Mratibu wa Kudhibiti maambukizi ya UKIMWI Mkoa (Tiba)
· Kutekeleza kazi nyingine kama atakavyoelekezwa na Msimamizi wa Huduma za Afya Mkoa
Sifa za kuingilia:
- Wenye shahada ya Udaktari (MD) au Stashahada ya Udaktari (AMO) ambaye amehitimu katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
- Asiwe mwajiriwa wa Serikali au Taasisi nyingine ya Serikali na Serikali za Mitaa ndani ya Mkoa.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 25/04/2012
2. AFISA UFUATILIAJI NA TATHMINI (MONITORING & EVALUATION OFFICER 1 NAFASI MOJA (1)
Kazi za kufanya:
· Kufuatilia na kutathmini maendeleo ya mradi kwa kushirikiana na Meneja wa Mradi
· Kuwezesha na kutoa ushauri na tafsiri ya Sera, Mipango, mikakati na miongozo kuhusu taarifa za Afya kwa mujibu wa miongozo ya Wizara ya Afya
· Kutekeleza kazi nyingine kama zitakavyoelekezwa na Meneja wa Mradi
Sifa za kuingilia:
- Wenye Shahada/Shahada ya Uzamili katika fani ya Mipango, Uchumi na Takwimu kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
- Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 25/04/2012
3. MHASIBU:
Kazi za kufanya:
· Kufanya kazi kwa kushirikiana na Meneja wa Mradi
· Kusimamia shughuli zote za Uhasibu katika Mradi
· Kudhibiti hati za malipo
· Kujibu hoja za Ukaguzi
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 25/04/2012
SIFA ZA KUINGILIA:
- Awe na Shahada au Stashahada ya Uhasibu kutoka kwenye vyuo vinavyotambuliwa na Serikali
4. WATUNZA KUMBUKUMBU NAFASI TANO (5)
Kazi za kufanya:
· Kufanya kazi kwa mujibu wa maelekezo ya Meneja wa Mradi
· Kuandaa na kutunza taarifa /kumbukumbu na nyaraka mbalimbali za Mradi
· Kukusanya na kuhifadhi taarifa mbalimbali za wagonjwa.
Sifa za kuingilia:
- Awe na Shahada au Stashahada, au cheti cha utunzaji wa kumbukumbu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 25/04/2012
Maombi yote yatumwe kwa:
Katibu Tawala wa Mkoa,
S.L.P. 74,
SONGEA.
AU
Mganga Mkuu wa Mkoa,
S.L.P. 5,
SONGEA.
Thursday, April 12, 2012
KLABU YA MAJIMAJI YAMPONGEZA RC MWAMBUNGU KWA KUNUSURU KIFO CHAKE
MKUU WA MKOA WA RUVUMA SAID MWAMBUNGU
NA STEPHANO MANGO,SONGEA
NA STEPHANO MANGO,SONGEA
UONGOZI wa klabu ya Majimaji ya Songea imetoa pongezi ya kumshukuru Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Said Thabit Mwambungu kwa kazi kubwa ya kuiwezesha timu hiyo kubakia ligi ya Daraja la kwanza kwa ngazi ya Taifa msimu huu.
Akizumgumza mjini hapa ,Katibu Msaidizi wa Wanalizombe hao, Zakaria Ndumbaro alisema kuwa uongozi wa Majimaji umeweza kumwandikia barua ya kumpongeza pamoja na kumshukuru juu ya mchango wa kifedha , fikra na busara zake ambazo ndizo zilizoiwezesha timu hiyo kubakia kucheza tena ligi hiyo msimu ujao.
Alisema kama siyo mkuu wa mkoa kuipiga jeki timu hiyo basi kulikuwa na uwezekano mkubwa wa kushuka daraja na kucheza ligi ya mkoa kitu ambacho kingekuwa fedheha kwa timu kama hiyo yenye historia ya soka hapa nchini.
Alisema katika kipindi chote cha ligi hiyo ya Daraja la kwanza kwa ngazi ya Taifa hatua ya makundi, licha ya kukabiliwa na tatizo la uongozi na kupelekea wanachama kuwaengua baadhi ya viongozi na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Mohamed Gayo kujihuzuru timu hiyo ilifikia hatua ya kuyumba na hata kutiliwa shaka kushiriki ligi hiyo.
Alisema kutokana na busara za mkuu huyo aliweza kuunganisha nguvu ya pamoja baina ya viongozi waliokuwepo madarakani, wanachama na wale walioenguliwa na kuwa kitu kimoja na kufanikiwa kucheza na kubakia katika hatua hiyo licha ya matatizo ambayo waliweza kukumbana nayo katika kipindi hicho cha ligi.
Alisema kutokana na matatizo yote hayo ambayo waliweza kukabiliana nayo, tayari uongozi wa timu hiyo umeanza kujipanga kuhakikisha na timu hiyo itaendeshwa kwa mtindo wa mfumo wa kibiashara na kuachana na mfumo wa sasa wa timu kuendeshwa na wanachama kwa kutegemea mifuko yao.
Alisema katika kuhakikisha heshima ya timu hiyo inarejea kama ilivyo katika miaka ya nyuma tayari amedai wameandaa mazingira mazuri ikiwemo ya kufanya mkutano wa pamoja kati ya wadau na wanachama mada kuu kuelezea changamoto zinazoikabili pamoja na maendeleo yake kwa kipindi cha miaka mitatu ya nyuma na malengo wanayokusudia kwa miaka ya mbele.
Pia, Ndumbaro alisema katika kikao chao walichokutana hivi karibuni wameweza kumsimamisha kazi Ofisa Habari wa Klabu ya Majimaji, Osama Ulaya kwa kile alichokidai amekuwa akifanyakazi kinyume na maadili ya kazi yake na kupelekea timu hiyo kwa kipindi chote kuingia katika malumbano yaliyochangia na kuwepo kwa uvumi na habari za uchochezi ambazo zilikuwa zikitolewa na Ofisa huyo.
MWISHO.
Wednesday, April 11, 2012
WATANO WASHILIWA NA POLISI KWA KUKUTWA NA MBAO ZA POLINI KINYUME NA SHERIA
Na Stephano Mango, Songea
WATU watano wakiwemo askari watatu wa Idara ya Wanyama pori walioko kwenye Mbuga ya hifadhi ya Wanyama ya Taifa ya Serous Wilayani Namtumbo wanashikiliwa na Polisi Mkoani Ruvuma kwa tuhuma za kukutwa na mbao za mti pori 135 kinyume na sheria.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Michael Kamhanda alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 5 asubuhi huko katika Kijiji cha Likuyu Sekamaganga kilichopo kwenye eneo la Mbuga ya hifadhi ya Wanyama ya Taifa ya Serous Wilayani Namtumbo.
Aliwataja askari wa Wanyama pori wanaoshikiliwa na Polisi kuwa ni Godian Mataba (30),Michael Mrutu (29) na Fabian Paul (34) ambao wote ni askari wa Idara ya Wanyama pori kwenye Mbuga hiyo ya Wanyama.
Amewataja wengine kuwa ni Sebastian Matembo (30) na Juma Iddi (35) maarufu kwa jina la Kilaza wote wakazi Kijiji cha Likuyu Sekamaganga ambapo alieleza zaidi kuwa watuhumiwa hao wote walikamatwa wakiwa na mbao 135 ndani ya kambi ya hifadhi ya wanyamapori ya Mbuga ya Serous bila kuwa na kibali.
Alifafanua zaidi kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio Katibu wa Hifadhi ya Maliasili Abeid Nihuka akiwa na askari wa wanyama pori wa Mbuga ya Serous walifanya msako mkali wa kuwabaini watu wanaoharibu mazingira ya Mali asili kwenye hifadhi ya Mbuga hiyo.
Alisema kuwa askari hao wa wanyama pori wakiwa kwenye doria walifanikiwa kuzikuta mbao 95 zikiwa zimehifadhiwa ndani ya Kambi na mbao 40 zilikutwa nje ya eneo la Kambi kwa watuhumiwa wawili ambao ni Matembo na Iddi Wakazi wa Kijiji hicho.
Hata hivyo alieleza kuwa watuhumiwa wote watano wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kukutwa na mbao za miti pori kinyume na sheria na kwamba kwa hivi sasa Polisi inaendelea na Upelelezi zaidi na ukikamilika watafikishwa Mahakamani kujibu shtaka linalowakabili.
MWISHO
Tuesday, April 10, 2012
ASHIKILIWA NA POLISI KWA KUKUTWA NA KETE 225 ZA MADWA YA KULEVYA
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Michael Kamhanda
Na Gideon Mwakanosya, Songea
JESHI la Polisi Mkoani Ruvuma limemtia mbaroni Hamza Mnadi (27) mkazi wa Mtaa wa Kalanje Wilaya ya Tunduru kwa tuhuma za kukutwa akiwa amehifadhi madawa ya kulevya aina ya Cocaine na Heroine ambayo thamani yake bado haijafahamika
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamhanda alisema kuwa tukio hilo limetokea aprili 7 mwaka huu majira ya saa 11 jioni huko katika mtaa wa Kalanje mjini Tunduru
Alieleza kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio askari Polisi wakiwa doria walipewa taarifa toka kwa raia wema kuwa kuna mtu anafanya biashara ya madawa ya kulevya katika mtaa huo na kwamba tangu alipoanza biashara hiyo kumekuwa na watu wengi wamekuwa wakifika kwenye nyumba hiyo ya Mnadi kwa lengo la kununua madawa hayo
Alifafanua kuwa Askari hao baada ya kupata taarifa toka kwa raia wema walikwenda mpaka kwenye eneo la nyumba ya Mnadi ambako walifanikiwa kumkuta na baadae walipofanya upekuzi kwenye nyumba hiyo walimkuta akiwa na madawa ya kulevya ya Cocaine na Heroine yakiwa yamehifadhiwa kwenye paketi tisa
Alieleza zaidi kuwa madawa hayo ambayo yalikuwa yamehifadhiwa kwenye paketi 9 ambapo kila paketi kulikuwa kumehifadhiwa vipande 25 na kufanya jumla ya vipande 225 vya madawa hayo kwenye paketi zote 9 zilizokutwa ndani ya nyumba yake
Alisema kuwa kwa hivi sasa mtuhumiwa anashikiriwa na Polisi na upelelezi wa Polisi bado unaendelea na utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabilI
MWISHO
MBARONI KWA KUKUTWA NA BUNDUKI NA RISASI KINYUME CHA SHERIA
Na Gideon Mwakanosya, Songea
JESHI la Polisi Mkoani Ruvuma linamshikilia Lameck Ruben Halfan (38) mkazi wa eneo la Mtaa wa Aroma, Tabata Jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kukutwa akiwa na siraha aina ya Riffle na risasi zake mbili kinyume na sheria za nchi
Akizungumza na Kahama Fm jana Ofisi kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamhanda alisema kuwa tukio hilo lilitokea Aprili 9 mwaka huu majira ya saa 2 usiku huko katika kijiji cha Angalia kilichopo Wilaya ya Tunduru
Kamanda Kamhanda alisema kuwa siku hiyo ya tukio Askari waPolisi wakiwa kwenye doria ambao walikuwa wanashirikiana na Askari wa Wanyamapori wa Wilaya hiyo walimkamata Halfan akiwa na siraha yenye namba za usajiri 083972 ambayo ilikuwa na risasi mbili ambayo alikuwa ameifunga kwenye nguo zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye begi
Alifafanua zaidi kuwa mtuhumiwa huyo Halfan alikamatwa akiwa anatokea Kijiji cha Mwenge ambako inadaiwa kuwa anajishughulisha na shughuli za uwindaji haramu wa wanyamapori akielekea mjini Tunduru
Hata hivyo Polisi bado inaendelea kufanya upelelezi zaidi wa tukio hilo na kwamba utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma mashtaka yanayomkabili
MWISHO
Subscribe to:
Posts (Atom)


