About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Friday, May 11, 2012

WAANDISHI WAASWA KURIPOTI KIKAMILIFU ADHA YA UMEME MANISPAA YA SONGEA

                            
MAHINDI YAKIWA KWENYE KIWANDA CHA MTAZAMO KWA AJIRI YA KUSUBIRI UMEME ILI YAKOBOLEWE NA YASAGWE 




Na Stephano Mango, Songea
WAANDISHI wa Habari mkoani Ruvuma wametakiwa kutumia taaluma yao kikamilifu katika kuwaokoa wananchi wanaoteseka kutoka na adha wanazozipata kutokana na mgawo mkubwa wa umeme usiokuwa na kikomo unaoendelea kuwakabili katika Halmashauri ya Manspaa ya Songea
Wito huo umetolewa jana na Mkurugenzi wa kampuni ya Mtazamo Enterpress, Julius Mlawa wakati akizungumza na waandishi wa habari jana waliotembelea kiwanda cha kampuni hiyo kinachojishughulisha na ukoboaji nafaka, usagaji na uuzaji wa unga
Mlawa alisema kuwa waandishi wa habari ndio jukwaa la wananchi wanyonge ambao sauti zao hazisikiki vizuri kusemea licha ya kuendelea kuteseka na adha ya mgao mkubwa wa umeme unaowasababishia kupanda kwa gharama za maisha
Alisema kuwa mashine za kusaga nafaka ambazo zipo katika baadhi ya maeneo ya Manispaa hiyo zimeshindwa kutoa huduma kwa muda muafaka na kusababisha wananchi walio wengi kulazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma nje ya Manispaa ambako kuna mashine za kusaga nafaka zinazotumia mafuta ya Dizeli na kusababisha bei ya huduma hiyo kupanda mara mbili ikilinganishwa na awali
Alieleza kuwa kitendo cha shirika la umeme mkoani humu kushindwa kutoa huduma hiyo kwa wakati mbali ya kusababisha usumbufu kwao lakini kimekuwa kikiwakosesha mapato ambayo wanayatumia kulipa kodi kwenye mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) kutokana na hasara zinazosababishwa na ukosefu wa umeme
Alifafanua zaidi katika kiwanda chake kuna wafanyakazi zaidi 30 ambao wanashinda kiwanda wakisubiri umeme ili waweze kufanya kazi bila mafanikio huku wakilipwa posho zao za kila siku bila kufanya kazi jambo linalosababisha hasara kubwa
Alieleza zaidi kuwa kutokana na ukosefu wa umeme ambao umekithiri katika manispaa ya Songea wafanyabiashara wengi wanashindwa kurejesha mikopo waliyokopa kwenye taasisi za fedha jambo ambalo ni hatari kwa biashara zao na jamii ambayo inanufaika na biashara hizo
Alisema kuwa kutokana na hali hiyo huenda akalazimika kusitisha kwa muda kutoa huduma ya usagaji na ukoboaji wa nafaka kama hali hiyo ya ukosefu wa umeme wa uhakika haitafanyiwa kazi na shirika hilo la umeme mkoani humu kwa sababu mbali ya kukosa mapato lakini imekuwa ni usumbufu kwa wananchi ambao wanahitaji huduma hiyo.
Kwa upande wake Meneja wa shirika la umeme mkoa wa Ruvuma Mhandisi Monika Kebara alikiri kuwepo kwa tatizo hilo na alisema hivi sasa huduma hiyo ya umeme inatolewa kwa mgawo kwa sababu uwezo wa ufuaji wa umeme umepungua sana kutokana na kuharibika kwa mitambo ya kuzalisha umeme iliyopo Kibulang’oma mjini hapa.
Kebara alisema kituo hicho kina mashine saba za kuzalisha umeme lakini kwa hivi sasa ni mashine tatu ndizo zinazofanya kazi hiyo kwa kutoa Megawati 2.6 wakati mahitaji ni Megawati 5 hasa ikizingatiwa kuwa katika mji wa Songea shirika hilo lina wateja elfu kumi na mbili.
Alisema kuwa tayari jopo la mafundi kutoka Jijini Dar es Salaam limefika kwa ajiri ya ukarabati mkubwa wa mitambo hiyo na kwamba mwishoni mwa mwezi mei kutakuwa na umeme wa uhakika
MWISHO

KAGASHEKI:SIKUBALI KUNYONGWA

                           .MAIGE AKIRI KUPONZWA NA WATENDAJI



Na Asha Bani, Dar
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, amesema hatokubali kuhukumiwa kufa kwa kunyongwa au kupigwa risasi kwa sababu ya madudu yatakayofanywa na watendaji wa wizara hiyo.

Kagasheki alisema wizara hiyo imechafuka kwa kiasi kikubwa na tuhuma za ubadhirifu wa hali ya juu umewafanya hata wabunge kupendekeza mtumishi wa serikali atakayebainika kuhujumu mali za nchi kuuawa kwa kunyongwa.

Akizungumza katika makabidhiano baina yake na aliyekuwa akishikilia wizara hiyo, Ezekiel Maige, waziri huyo mpya alisema wizara hiyo ina sura mbaya kwa nje kutokana na tuhuma za ufisadi wa kutisha unaofanywa na baadhi ya watendaji wake jambo lililosababisha katika kipindi cha utawala wa Rais Jakaya Kikwete kuongozwa na mawaziri watano.

Wizara hiyo imeongozwa na mawaziri Anthony Diallo, Prof. Jumanne Maghembe, Shamsa Mwangunga, Ezekiel Maige na sasa Kagasheki mwenyewe.

“Katika Bunge lililopita mbunge mmoja alitaka mawaziri wabadhirifu wanyongwe au wapigwe risasi mimi sitaki kufikia huko nitawanyonga wafanyakazi wabadhirifu kabla ya kunyongwa mimi; nasema hili kwa nia njema kabisa na sio kutisha watu,” alisema Kagasheki.

Alisema kutokana na uozo huo, wizara hiyo imebadilishwa jina na kuitwa ‘mali ya siri kubwa’ jambo ambalo si zuri kwa kuwa kila kitu kinatakiwa kufanyika kwa uwazi kwa maendeleo ya taifa.

Waziri huyo pia alisema Wizara ya Maliasili na Utalii inatakiwa kuchangia pato kubwa la taifa kupita wizara nyingine yoyote hata ile ya Nishati na Madini isingeweza kufikia lakini kwa sasa inachangia pato la taifa kwa asilimia 18 tu.

“Mimi nataka kufanya kazi kwa kushirikiana na sio kwa ugomvi: waziri haelewani na naibu wake; vurugu tupu. Hii inaondoa ufanisi katika kazi na kama naibu waziri na waziri wanashindwa kuelewana itasababisha hata watendaji wa ngazi ya chini kushindwa kuelewana pia,” alisema Kagasheki.

Alisema atafanya kazi kwa kuangalia pia changamoto mbalimbali katika sekta za wizara hiyo, ikiwa ni pamoja na kuangalia sekta ya wanyapori, misitu na sera nzima ya utalii na changamoto nyingine ikiwemo ya upungufu wa watumishi na kufuatilia kwa kina yanayozungumzwa katika hifadhi ya Ngorongoro.

Naye Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Lazaro Nyalandu, alisema kwa kushirikiana watahakikisha pato la wizara hiyo linakuwa kwa kasi, watalii wanaongezeka kwa kuutangaza utalii ndani na nje ya nchi.

Aidha alimtaka kila mfanyakazi wa wizara hiyo kufanya kazi kwa moyo mmoja na kuhakikisha kuwa anaongeza uzalishaji wake.
Akikabidhi ofisi aliyekuwa waziri, Ezekiel Maige, aliwatahadharisha mawaziri hao kuwa macho kwa vile anajua aliondolewa kutokana na makosa ya baadhi ya watendaji wake wa chini.

Maige alidai kuwa katika wakati wake wa utendaji, alijitahidi sana kutumia akili na nguvu zake nyingi kuimarisha wizara hiyo, na kukiri kuwa kuna tuhuma za baadhi ya wafanyakazi wanaojihusisha na biashara za utalii.

Alidai kuwa baadhi ya wafanyakazi, akiwemo mtumishi mmoja mwandamizi ambaye kesi yake iko mahakamani, wamejitumbukiza katika biashara hizo, na kumtaka Kagasheni kupambana nalo.

Maige alidai wizara hiyo katika kutekeleza majukumu yake inakabiliwa na upungufu wa watumishi, ujangili, uvujaji wa mapato, ukosefu wa vitendea kazi na uchakavu wa miundombinu.

Nyingine ni utoroshwaji wa wanyamapori hai kupitia uwanja wa ndege wa Kilimanjaro, ambapo wizara ilisitisha biashara ya wanyapori hai sambamba na kuunda tume mbalimbali za kufanya uchunguzi kwa maofisa walioshiriki.

Waziri Maige aliahidi kushirikiana nao bega kwa bega katika kuendeleza yale aliyoanza kuyafanyia kazi ikiwa ni pamoja na suala la uchimbaji urani katika pori la akiba la Selous.

Tuesday, May 8, 2012

SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI MKOANI RUVUMA ILIVYOFANA KATIKA MATUKIO MBALIMBALI

Timu ya waandishi wa mtandao huu, inaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kwa kutokuwa jamvini siku zaidi ya 3 na hasa kwa kutokuwajuza habari za mkoa wa Ruvuma na mikoa jilani na hasa siku ya uhuru wa vyombo vya habari mei 3 mwaka huu kutokana na sababu za kiufundi ambazo zilikuwa nje ya uwezo wetu, na sasa tumerudi tena jamvini kwa kasi kubwa yenye kukidhi ladha ya kitasnia,Tunawashukuru sana wadau wa mtandao huu wa www.stephanomango.blogspot.com, kwa kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi uliokuwa unalengo la kujua tatizo letu na kutupa pole, Asanteni sana, BY UTAWALA
 Mjumbe wa Bodi ya Muunganiko wa Vyama vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Mhariri Msaidizi wa Kanda ya Kusini(Tujifunze) na Mhandishi wa Habari wa Uhuru Fm, Juma Nyumayo akitoa mada ya mchango wa vyombo vya habari katika jamii katika mdahalo ulioandaliwa na Kituo cha Redio Jogoo Fm siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani Mei 3
 Mwandishi wa Serikali za Mitaa Tanzania mkoani Ruvuma(ALAT) Mwakilishi wa Vyombo vya IPP MEDIA(Nipashe,Guardian,Redio One na Itv) Nathan Mtega akizungumza katika Studio ya Kituo cha Redio Jogoo kuhusu umuhimu wa waandishi wa habari katika maendeleo ya Jamii, katikati ni Muongozaji wa kipindi hicho Isabela Nchama,wa kwanza kulia ni Aden Mbelle ambaye alikuwa ni msimamizi wa kipindi hicho
 Mwandishi wa Habari wa Tanzania Daima, Dira ya Mtanzania, Changamoto,Mitandao mbalimbali ya Kijamii na mmiliki wa mtandao wa www.stephanomango.blogspot.com, Stephano Mango akitoa mada ya umuhimu wa vyombo vya habari katika kukuza Demokrasia nchini, kulia ni Msimamizi wa kipindi Aden Mbelle
 Kutoka kushoto ni mwongozaji wa kipindi hicho kilichorushwa hewani moja kwa moja na kituo cha Redio Jogoo Fm, Isabela Nshana na Aden Mbelle ambaye alikuwa msimamizi wa matangazo hayo siku ya uhuru wa vyombo vya habari mei 3 mwaka huu
 Mtangazaji wa Redio Jogoo Innocent akifanya mahojiano na Mwandishi Juma Nyumayo katika Studio ya Redio hiyo siku ya Uhuru wa vyombo vya habari
 Mtangazaji wa Redio Jogoo Innocent akifanya mahojiano na Mwandishi Nathan Mtega katika Studio ya Redio hiyo siku ya Uhuru wa vyombo vya habari mei 3, katikati ni Mwandishi Juma Nyumayo
 Mwandishi Nathan Mtega akisaini kitabu katika Studio ya Redio Jogoo Fm ikiwa ni ishara ya kumaliza kipindi kilichorushwa moja kwa moja na Redio hiyo, kushoto ni Mtangazaji wa kituo hicho Isabela Nshama siku ya uhuru wa vyombo vya habari mei 3 mwaka 2012
 Mwandishi Juma Nyumayo akiteta jambo na Mtangazaji wa Redio Jogoo Fm Aden Mbelle baada ya kumaliza mdaharo wa umuhimu wa vyombo vya habari katika muktadha wa uchumi, siasa na utamaduni

MUDA WA TAFRIJA KATIKA UKUMBI WA SONGEA CLUB MAMBO YALIKUWA HIVI............
 Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho Jenista Mhagama mbaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu kuwa mgeni rasmi katika tafrija ya jioni ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari mkoani Ruvuma, kushoni ni Katibu Mtendaji wa Chama cha waandishi wa habari moani Ruvuma Andrwe Chatwanga, wapili kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Ruvuma Press Club Andrwe Kuchonjoma wakiimba wimbo wa kuisifu na kuipenda TANZANIA
 Katibu Msaidizi wa Ruvuma Press Club, Mozes Julius Konala na Mwandishi wa Tanzania Daima kushoto, kulia ni Mwekahazina Msaidizi  na Mwandishi wa Channel Ten mkoani Ruvuma Emmanuel Msigwa wakiimba wimbo wa kuipenda TANZANIA
 Waandishi wa habari kutoka kulia ni Jofrey Nilai Redio Maria na Mjumbe wa Kamati wa Ruvuma Press Club, Mwakilishi wa IPP MEDIA mkoani Ruvuma Nathan Mtega na Anna wakiimba wimbo huo

 Mwandishi wa Jambo Leo Thomas Lipuka Komba akitoa maombi kwa niaba ya dhehebu la kikristo katika tafrija hiyo
 Naye akitoa maombi kwa niaba ya dhehebu la kiislam




















Monday, May 7, 2012

CUF WATEMA CHECHE WILAYANI TUNDURU

Na Steven Augustino, Tunduru

WAKULIMA wa Mpunga Wilayani Tunduru wametakiwa kuukataa kuuza mpunga wao kupitia mfumo wa Stakabadha gharani na kugoma kulipa ushuru kulingana na maelekezo yaliyotolewa na Halmashauri ya wilaya hiyo .
Pamoja na wito huo wakulima wa mazao hayo pia wamehimizwa kuwa na mshikamano wa kugomeaa tozo za ushuru ambao umedaiwa kutozwa na Halmashauri ya Wilaya hiyo hata kwa wakulima wanao ingiza mazao yao kutoka shambani.

Wito huo ulitolewa hivi karibuni na Viongozi waandamizi wa Chama cha wananchi CUF wa Wilaya ya Tunduru kwa ushirikiano wa viongozi wa chama hicho kutoka Mkoani Mtwara wakati wakiongea na wananchi katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya baraza la Idd mjini hapa.

Akifafanua hotuba hiyo Mgeni rasmi katika mkutano huo Mwenyekiti wa Chama cha wananchi Cuf  Wilaya ya Tandahimba na Mgombea wa Ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010  Katani Mohamed alisema kuwa ukosefu wa wataalamu wabunifu na uvivu wa kujituma kwa viongozi katika halmshauri hiyo ndiko kuliko wasukuma kuandaa utaratibu huo huku
wakifahamu wazi kuwa mpango huo unalenga kuwaibia wakulima hao.

Huku akishangiliwa na maelfu ya wananchi waliojitokeza katika mkutano huo Katani aliwahimiza kudai haki zao bila kuogopa jambo lolote kwani vitendo hivyo vya unyonyaji ni hatari kwa ustawi wa jamii

Katani aliendelea kueleza kuwa kinachowafanya viongozi hao kufikia hatua hiyo ya kuchukua maamuzi bila kuwashirikisha wananchi kinatokana na wanatunduru wenyewe kulala usingizi wa pono na akatumia nafasi hiyo kuwataka waamke kudai haki zao vinginevyo watajikuta wameuzwa katika maeneo yao.

Alisema wakati viongopzi hao wakifikilia kuingiza zao hilo katika mfumo huo viongozi hao bado wameendelea kuwa kero katika utoaji wa msaada kwa wakulima wakorosho ambao pia waliingizwa katika mkenge huo bila kuwepo kwa makubaliano.

Akizungumzia tozo kwa wakulima wa mpunga alisema ingawa viongozi hao wanafahamu maelekezo na miongozo ya tozo hizo iko wazi kuwa anayetakiwa kulipa ushuru ni mtu yeyote au mfanyabiashara anayeondoka na shehene ya chakula kutoka ndani ya wilaya husika.

Wakitoa salamu kutoka mkoani Mtwara Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Cuf Taifa Reherma Mautuka, Katibu wa Cuf Wilaya ya Tandahimba Shaban Namaneha,Katibu wa Cuf  Mtwara Mjini Said Mdoya na Mkurugenzi wa haki za binadamu Wilaya ya Tandahimba Alfonce Andrew walisema kuwa mikikimikiki ambayo imekuwa ikijitokeza katika Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara imetokana na kuchoshwa na vitendo vya unyanyasaji kutoka kwa viongozi wao.

Awali akimkaribisha msemaji mkuu katika mkutano huo mwenyekiti wa CUF
Wilayani humo Abdalah Mtalika alidai kuwa kitendo cha kuwatoza wakulima Ushuru huo wakati wakiingiza mazao yao kutoka Shambani ni cha uonevu kwavile wakazi wote wa mji huo hulima vijijini.
Mwisho

Monday, April 30, 2012

WANACHAMA WA SACCOS YA WALIMU TUNDURU WALIDHIA ONGEZEKO LA MAKATO

Na Steven Augustino, Tunduru
WAJUMBE wa Mkutano mkuu wa chama cha Ushirika cha akiba na  Mikopo cha Walimu wa Wilaya ya Tunduru kimeridhia kuongeza makato yao na kufikia Shilingi 30,000 kutoka Shilingi 15,000 walizo kuwa wakikatwa awali zikiwa ni juhudi za kutunisha mfuko  kwa kutumia uwezo wa ndani.
Sambamba na kuthibitishwa kwa maapendekezo hayo wajumbe hao walipitisha bajeti ya mapato na matumizi ya shilingi Milioni 66,819,220 na kutumia jumla ya Shilingi 45,857,840 katika mwaka wa
fedha wa 2012 kukiwa na ongezeko la asilimia 78 % ikilinganishwa na bajeti ya shilingi milioni 52,666,000.  zilizotumika mwaka uliopita wa mwaka 2011.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na Kaimu meneja wa  chama hicho Mwl.Hassan Isaya alisema kuwa kati ya Fedha hizo  shilingi 36,675,000 zinatarajiwa kukusanywa kutoka katika vyanzo vya ndani , misaada na Ruzuku kutoka kwa wahisani wamepanga kuingiza jumla ya shilingi 800,000, na Tshs 27,851,220 zitatokana na faida ya mkopo wa CRDB.
Katika taarifa hiyo pia Mwl. Isaya  alieleza kuwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2011/2012 chama hicho kiliweza  kukopesha jumla ya shilingi Milioni 95,970,325  kwa wanachama wake
 
Mwl. Juma Ado akisoma taarifa zilizotokana na mrejesho wa mikutano mbalimbali alidai kuwa uzoefu unaonesha kuwa pamoja na kuwepo kwa upungufu wa wanchama katika chama hicho pia udogo wa makato ya Tsh 15,000 wanayo katwa wanachama wake ni kikwazo kingine kinacho kwamisha
maendeleo ndani ya chama chao.
Aidha Mwl ,Ado katika taarifa hiyo alitolea mfano hatua za maendeleo zilizopigwa na vyama vya kuweka na kukopa vya UTWANGO SACCOS iliyopo katika Mkoa mpya wa Njombe na NEWALA SACCOS  Mkoani
Mtwara  ambazo zimemudu kujenga vitega uchumi vya kujenga  Nyumba  za kulala wageni kupitia mfumo wa  mbinu za uhamasishaji na kupeana majukumu ili miradi hiyo iwe vyanzo mbadala
vya kutunisha .
Pamoja na kutolewa kwa mapendekezo hayo wito ukatolewa kwa Viongozi wa chama hicho kuongeza juhudi za utoaji wa elimu kwa wanachama wapya pamoja na kumpelekea salamu mwajiri wao kuwa siku atakayo chelewesha makato yao kupeleka katika chama hicho wapo tayari kufanya maandamano
zikiwa ni juhudi za kuongeza mapato ya ndani ili kujiletea maendeleo.
 
Awali akifungua mkutano huo Mkuu wa 12 wa mwaka wa wanachama wa umoja huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Klasta, Afisa elimu ya Shule za Msingi Wilayani humo Mwl. Rashid Mandoa alitumia nafasi hiyo kuwahimiza wanachama hao kukopa kwa busara na kulipa kwa busara mikopo hiyo.
Wakitoa nasaha kwa nyakati tofauti katika mkutano huo Afisa Ushirika wa Wilaya hiyo Jalia Msangi na Katibu wa chama cha Walimu Wilaya ya Tunduru Mwl. Lazaro Saulo waliwahimiza wanachama hao kuwa waumini wa chama hicho kwa kukubali kwa hiari zao kuongeza makato kulingana na malengo ya kila mwanachama na kujiletea maendeleo kulingana na mahitaji yao.

Walisema kulingana na taratibu na sheria zinazosimamia ushirika pamoja na kuweka utaratibu wa kujiunga na chama husika pamoja na kuwekwa kwa mikakati yake pia kuwe na utaratibu wa kuwaruhusu wanachama kuchangia fedha kulingana na mahitahi tu.
Akifunga Mkutano huo Mwenyekiti wa umoja huo Mwl. Hassan Nakoma pamoja na kuwahimiza wanachama hao kuendelea kuwashawishi wanachama wapya kujiunga na umoja huo pia aliwataarifu wanachama hao kuwa ujenzi wa Ofisi ya chama hicho umepangwa kupitia uwezo wao wa ndani baada ya mfadhiri wao Daimu Mpakate kushindwa kutimiza masherti ya umoja huo
Mwisho

Saturday, April 28, 2012

WAWILI WAFA PAPO HAPO NA WATATU WAJERUHIWA VIBAYA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda
Na Gideon Mwakanosya, Songea
WATU  wawili wamefariki dunia na wengine watatu akiwemo dereva wa gari hilo  wamejeruhiwa vibaya mkoani Ruvuma baada ya kugongwa na gari katika  eneo la Mahenge katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea baadaya ya kugongwa na gari la Jeshi la wananchi (JWTZ)  la Makao makuu ya brigedi Chandamali
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Michael  kamuhanda amesema kuwa tukio hilo limetokea  majira ya saaa mbili na nusu asubuhi huko kwenye barabara ya Songea na Namtumbo ambapo aliwataja waliokufa kuwa ni Stumai Moyo (20) na Tabia Bilali (23) wote wakazi wa eneo la Mahenge wa Songea mjini na walio jeruhiwa vibaya ni Amina Moyo (2) na Issa Moyo (65) wote wakazi wa Mahenge ambao baada ya kutokea ajali hiyo walikimbizwa katika Hospitali ya mkoa ambako wamelazwa
 Alifafanua zaidi  kuwa gari hiyo Landlover Discova yenye namba za usajili 1513 JW 97  iliyosababisha ajali na kuuwa watu wawili papohapo na wengine wawili kujeruhiwa vibaya.
 Alieleza zaidi kuwa gari hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na  MT 97812 SGT Kelvin Muhagama ilikuwa ikitoka Makao makuu ya Brigedi Chandamali na kuelekea Songea mjini  
 Kamanda Kamuhanda alibainisha zaidi kuwa chanzo cha ajari hiyo ni mwendo kasi ambao ilimsababisha dereva wa gari hilo kushindwa kumudu usukani
Naye Mganga mfawidhi wa Hospitali ya mkoa songea  Dr. Mathayo Chanangula amethibitisha kupokea maiti za watu wawili ambazo kwa sasa zimehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali hiyo  na majeruhi  watatu ambao wawili kati yao wamelazwa kwenye wodi za majeruhi na majeruhi mmoja ambaye ni mtoto wa umri wa mika 2 Amina Moyo amekimbizwa katika Hospitali ya Mision ya Peramiho kwa matibabu zaidi baada ya Hospitali hiyo kukosa mashine ya Ex –ray kwani imeonekana kuwa Amina ameumia kichwani ambako kunahitaji kupata vipimo vya Ex –ray ambapo kwa sasa hivi huduma hiyo inapatikana katika Hospitali ya Mision ya Peramiho
Dr. Chanangula alifafanua zaidi kuwa kwa muda mrefu hospitali ya mkoa songea haina kabisa huduma ya Ex –ray tangu mashine hiyo ilipo haribika na kwamba kwa hivi sasa wanasubiri mafundi kutoka ufiripino waje kitengeneza jambo ambalo limeonekana kuwa kero kuwa kwa wakazi wa songea ambao wamefika kupatiwa huduma hiyo lakini wamekuwa wakielekezwa kwenda Hospitali ya Mision ya Peramiho ambayo iko umbali wa kilometa 25 toka Songea mjini
 Mwisho.  

WAKULIMA WA KOROSHO WAGOMA KUPOKE MALIPO NUSU NUSU YA FEDHA ZAO

MKUU WA WILAYA YA TUNDURU JUMA MADAHA
Na Steven Augustino ,Tunduru

BAADHI ya wakulima wa korosho katika vyama vya msingi vya wakulima wa zao hilo wamegoma kupokea fedha za malipo yao huku wakidai kuto kuwa na imani na maelekezo yanayotolewa na viongozi wao.

Mgomo huo umefuatia kuwepo kwa maelekezo kuwa mkulima anayedai Shilingi 1200 kwa malipo ya korosho hizo atatakiwa kupokea mkononi Shilingi 850  na makulima anayedai Shilingi 350 atatakiwa kupokea Shilingi 200 huku kukiwa na maelekezo kuwa fedha nyingine watalipwa baada ya kuwasili kwa fedha zingine.

Wakiongea kwa nyakati tofauti miongoni mwa wakulima hao Mahamudu Ponera wa chama cha Msingi Nakayaya mashariki na Maghreth Mingwe walisema kuwa kitendo cha viongozu hao kuyumbisha malipo hayo kinalenga kuendelea kuichafulia sifa Serikali.

Walisema msimamo wao wa kukataa kupokea fedha hizo unatokana na wakulima kuelezwa kuwa baada ya kupokea fedha hizo watatakiwa kuacha Stakabadhi za malipo hayo na kubakia wakiwa hawana vielelezo vyovyote vinavyo onesha kuwepo kwa madai mengine katika vyama hivyo.

Alipo takiwa kuzungumzia hali hiyo Meneja wa Chama Kikuu cha wakulima wa wa Wilaya ya Tunduru  Iman Kalembo alithibitisha kuwepo kwa hali hiyo na kwamba msimamo wakutoa malipo hayo umetokana na fedha zilizofika kuwa ni kidogo hivyo wao hawakuona mkulima wa kumuacha wakati wa malipo hayo na kusisitiza kuwa fedha zikifika wakulima wote watakamilishiwa malipo yao.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Madaha alipotakiwa kuzungumzia kero hiyo alidai kuwa hakubaliani na utekelezaji wa zoezi hilo na kuongeza kuwa msimamo wa Serikali ni kulipa fedha zote na siyo kidogo kidogo na kwamba kama kuna kosa lilifanyika na viongozi hao ni uzembe wa viongozi wenyewe.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Afisa Ushirika wa Wilaya ya Tunduru Msangi alisema kuwa malipo hayo yanatokana na Benki kutoa Tsh. 2,587,506,900 zimepangwa kughalimia malipo ya Kilo 1200 tu kati ya Kilo  7,367,689 zilizopokelewa katika maghala kati ya Kilo
7,570,000 zilizo zalishwa na akulima hao katika msimu wa mwaka 2011/2012.

 Msangi aliendelea kueleza kuwa mchanganuao wa malipo hayo unaonesha kuwa kiasi kingi ne cha Shilingi 119,759,340 zitalipwa awamu ya pili na kwamba hali hiyo inatokana na taratibu za malipo hayo kuchelewa kupelekwa Benki.

Alisema fedha hizo zinatokana na malipo ya kilo 560,101 ambapo kati yake kilo 53,347 zenye thamani ya Shilingi 64,016,400 ni korosho za daraja la kwanza na shilingi 55,742,940  zinatokana na kilo 506,754 za daraja la pili.

Mwisho

Thursday, April 26, 2012

SHEREHE ZA UZINDUZI WA SONGEA GLOBAL NETWORK ZILIVYOFANA KATIKA UKUMBI WA AGOPAL

Katibu Mtendaji wa Songea Global Network John Kasembo akizungumza na mmoja wa wanachama wa mtandao huo

Kushoto ni Mtaalamu na mmiliki wa Kampuni ya kufunga Aluminium Songea Wailes Sebastian akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Elimark Eng.Co. Ltd Emanuel Nehemia Chapa

Mwenyekiti wa Songea Global Network Sakina Jamal akiwa na Mhasibu wa Mtandao huo Rehema Ayub wakati wa halfa ya uzinduzi wa mtandao huo
Miongoni mwa wanachama wa mtandao huo

Miongoni mwa wanachama wa Songea Global Network ambao walikuwa wanakamati wa chakula wakisubiri kuhudumia msosi

Mwenyekiti wa Songea Global Network Sakina Jamal akifungua mziki na mmoja wa wanachama wa Songea Global Network


Sasa ni kusaka lumba kwenda mbele na yeyote anayetaka kucheza kiduku ruksa

Mpaka kielewekeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

Mtandao wa Songea Global Network uwe chachu ya maendeleo
NA STEPHANO MANGO,SONGEA
WAHENGA walishanasihi kwamba, “Moyo usiokuwa na shukrani hukausha mema yote.” Hii inamaanisha kuwa tutakuwa wezi wa fadhila  kama hatutamshukuru sana Mwenyezi Mungu mwingi wa fadhili, rehema na mapendo kwa kutujalia sote uhai na afya na kutujalia nafasi hii adimu na adhimu ya kuandika na kusoma makala haya.
Nawashukuru wasomaji wote wa gazeti hili makini kwa kuendelea kulisoma na kutoa maoni yenu kwa mwandishi binafsi na wakati mwingine kwa viongozi wa Bodi ya Uhariri ili kuweza kuboresha kazi husika kwa lengo la kukidhi mahitaji ya wasomaji
Aprili 21 mwaka huu, nilialikwa kuhudhuria uzinduzi wa Mtandao wa Songea Global Network katika viwanja vya Hotel ya Agopal ambapo mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu ambaye aliwakilishwa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Seligius Ngahi.
Tukio hilo la kihistoria la uzinduzi wa mtandao lilihudhuriwa na watu wa kada mbalimbali lilikuwa ni mwanzo mpya wa wanachama wake kuifikia ndoto ya kuanzishwa kwake kwani walitaka, wakatakana na sasa hawana budi kuendeleza mipango waliojiwekea ili kuweza kuleta mafanikio waliokusudia toka awali wakati wanapanda mbegu ya kuanzisha mtandao huo.
Mtandao huo kama vilivyo vikundi vingine au chama chochote, una viongozi wake wakuu kwa maana ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mtendaji, Mhasibu na Kamati ya Utendaji, ambao watahakikisha malengo ya kuanzishwa kwa mtandao yanafikiwa kwa kushirikiana na wanachama wa mtandao huo.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mwenyekiti wa Songea Global Network (SGN) Sakina Jamal alisema kuwa malengo la kuanzisha mtandao huo ni kwanza, kusaidiana na kujaliana kwa shida mbalimbali mfano. Misiba, dharura.shida ni sehemu ya maisha ya binadamu.
Jamal alisema kuwa pili, kufahamiana na kupanua mtandao katika dunia hii ya utadawazi ambapo watu wanatafuta kuungana na kushirikiana katika maisha ya kila siku ,kwasababu ujifungia ni kuukumbatia umaskini wa mawazo na fikra.
Alisema tatu, kuwezeshana na kujengana kimawazo, kiushauri na kiuchumi, nne, kufunguliana  fursa za kusaidiana kadri ya utaalamu na kazi ya kila mmoja na tano, baadaye kuwa na SACCOS itakayotuwezesha kiuchumi: kuweka akiba, kukopa.
Alieleza zaidi kuwa hadi tunazindua rasmi mtandao unajumla ya wanachama 20 wakiwamo watu wa fani mbalimbali: wajenzi, mainjinia, mafundi, wahasibu, wanafunzi,madaktari, wajasiriamali, wafanyakazi wengine wa serikali.
Alisema ni mseto ulioiva wa wanachama wenye nia ya kushikamana na kutimiza ndoto ya mafanikio, udugu, ushirikiano na utajiri kwani tumedhamiria kuwa mbegu imara itakayoweza kutoa matunda stahiki katika siku za usoni kama tulivyojiwekea malengo, pia tunawakaribisha wanachama wapya kujiunga katika mtandao ili uwe na nguvu kubwa ,hivyo kwa yoyote yule anayetaka na kukubaliana na malengo tuliyojiwekea tunamkaribisha.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Songea Global Network John Kasembo akielezea historia ya kuanzishwa kwa mtandao huo wakati wa hafla ya uzinduzi huo alisema kuwa ,mtandao ulianza kama wazo la kukutana na kufanya hafla ya kuuaga mwaka 2011.
Kasembo alisema kuwa baada ya kukaa tukasema hapana, tulitajirishe wazo letu kwa kuanzisha mtandao utakao tuunganisha wote hata baada ya sherehe kama umoja wenye nia ya kusaidiana wakati wa shida na raha, kushauriana na kujengeana uwezo ili sote tufanikiwe.
Alisema baada ya majadiliano mapana na ya kina, tulikubaliana sote tuanzishe mtandao au umoja huo tukaupa jina la Songea Global Network (SGN) ambapo leo ndio siku tuliyokubaliana ya kupanda mbegu imara na safi ya mtandao huu ili umee na kuwa faida kwetu sisi wanachama na kuutangaza mkoa wetu wa Ruvuma kupitia mtandao wetu huu.
Alifafanua kuwa tulichagua jina hili SGN kwa sababu lina dhima ya kuunganisha watu wa kada mbalimbali bila kubagua umri, kazi, kabila, jinsia, rangi, dini wala itikadi. Anayekubali malengo yetu na kuwajibika kuchangia dira yetu, huyo ni mwanachama mzuri kwetu.
Alieleza zaidi kuwa leo tunavyopanda rasmi mbegu ya mtandao wetu (SGN), tunatumia fursa hii kukumbushana wanamtandao masharti ya kufanikiwa ili tuendelee mbele zaidi kufikia malengo na ndoto yetu ni kujitoa kweli,kupenda kweli mtandao,kuwa na ndoto na kutoa michango ya dhati bila kuchoka
Alisema kuwa ni kweli kuja pamoja ni mwanzo. Kufanya kazi pamoja ni umoja. Kudumu katika umoja ni maendeleo. Kuunganisha vipaji vyetu ni kuwa timu moja. Hatimaye kustahimili pamoja ni ushindi wa mtandao wetu huu.
Alieleza zaidi kuwa wanachama tukikaribisha upendo wa kweli tutafanikiwa katika malengo yetu na kutajirisha mtandao wetu kwa maendeleo ya mkoa wa Ruvuma, hivyo tunawajibika kutafakari na kuchukue hatua.
Alisema inapendeza, inakubalika, inawezekana na inahitajika kuwa na mtandao imara usiokatika network na kufanikiwa kweli. Ni kweli wahenga wa Ghana walishatuasa kwa methali yao kuwa, “Unaweza kumlaumu mtu kwa kukuangusha chini lakini ujilaumu mwenyewe kwa kukataa kunyanyuka.”
“Naomba wanamtandao tulioamua kuanzisha kwa hiari mtandao huu tusikalie kumlaumu mtu au kujilaumu wenyewe na badala yake tudhamirie na kuwa na bidii ya kunyanyuka leo na kuendeleza ndoto na mtandao wetu. Bila shaka linaloonekana haliwezekani litawezekana, milima isiyokweeka itakweeka na miti isiyopandika itapandika”alisema Kasembo.
Alisema kuwa tumuombe Mungu ili idumu, iote na ifanikiwe mbegu ya SGN ambapo sote tuchangie maendeleo yetu na ya taifa letu la Tanzania. Karibuni sote tufurahie jambo hili adhimu na tuchangie kila mmoja kwa nafasi na uwezo wake, kiushauri na kirasilimali aliyonayo kwa  mafanikio ya SGN.
Alisema kuwa wanachama tushikane mikono tuanze safari yetu kwa hatua ya kwanza leo, kwani hata Waswahili wanasema, “Safari ya maili elfu huanzia na hatua moja.” Na hakika ni kweli.  Tumethubutu kubuni na kuanzisha mtandao, tumeweza kuanzisha mtandao huu na sasa tunanuia kusonga mbele na mtandao tuliouanzisha.
Naye mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu  katika hotuba yake iliyosomwa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Seligius Ngahi alisema leo nashuhudia ndoto ikizaa jambo la uhalisia nayo ni Songea Global Network, nawapongeza sana kwa ndoto yenu, juhudi, nia na dhamira ya kuanzisha na kuendeleza mtandao wenu huu wenye malengo mliyojipangia ninyi wenyewe
Mwambungu alisema kuwa Chama au kikundi chochote cha watu hujengwa na mambo makuu matatu. Kwanza ni mahudhurio ya watu au wanachama, katiba na michango ya wanachama (rasilimali, ushauri, muda, fedha na nguvu).
Alifafanua kuwa kama mwanzo wa chama chenu napenda niwaombe tokea mwanzo kuwa kama mnanuia kweli ustawi, mafanikio na maendeleo ya mtandao wenu basi jibidisheni nyote kuhudhuria vikao bila kuchoka wala kudharau kwani mtu mmoja una thamani kwa mtandao huu.
Alisema tena jitahidini kuunda na kuwa na katiba imara itakayokuwa dira na mwongozo wa kufikia mafanikio ya malengo mliyojiwekea. Na Zaidi jalini na kujitoa sadaka nguvu, akili, utashi, rasilimali muda na michango yenu ya hali na mali katika kujenga, kukuza na kustawisha mtandao wenu. Haya kwenu ni ya msingi na ya kuzingatia kati ya mengi kama mnataka kuwa na mtandao imara na wenye nguvu.
“Nami najiunga rasmi katika mtandao pia naunga mkono jitihada mlizozianzisha kwa kutoa sh,300,000 ili ziwe chachu yaw engine kujitoa kwa lengo la kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake”alisema Mwambungu
Alieleza zaidi kuwa natambua kuwa mtandao ili uendelee mbele kuwa wenye nguvu, wenye mafanikio na watu wengi inapaswa kuutangaza, kuulinda, kuukuza, kuustawisha, kujivunia na kuufurahia. Tumieni fursa hii kufanya yale yote mtakayoona yanausaidia mtandao wenu kustawi na zaidi epukeni yale yote yanaweza kuvunja na kudhoofisha mtandao kama ubinafsi, dharau, chuki, fitina na majungu. Haya ni sumu kwenu!
Alisema kuwa leo mmeitangazia Songea, Ruvuma, Tanzania na dunia kuwa mna ndoto kubwa ya mafanikio. Kwa kawaida kuanzisha kazi ni rahisi kuliko kuiendeleza na kuimalizia. Mmeanza kwa kishindo, sasa msirudi nyuma. Daima kwenda mbele kwa kasi na viwango ili ndoto yeni itimie. Inawezekana, timizeni wajibu wenu.
Hakika wanamtandao wamethubutu,kubuni na kuanzisha mtandao, wameweza kuanzisha mtandao huu na sasa wanahitaji kusonga mbele ili uweze kuwa msaada wa ushauri, msaada wa kiuwezeshaji na msaada wa rasilimali watu wenye upeo na ndoto kwa mkoa wetu wa Ruvuma
Kuzaa si kazi, kazi ni kulea. Leeni mtandao huu uwe taa ya kutoa giza la umasikini na uwe chumvi ya kuleta ladha kwa mafanikio yenu na mkoa wa Ruvuma. Kama wengine waliweza kwanini nyie mshindwe?Hapana, kataeni msamiati wa kushindwa na siku zote neno msamiati wa kwanza uwe ni USHINDI DAIMA. Heri na mafanikio kwenu na Hongereni sana.Nyie mbele sisi nyuma
Mwandish wa Makala
Anapatikana 0715-335051
www.stephanomango.blogspot.com



WAKULIMA WALALAMIKIA KUTOZWA USHURU WA MAZAO TOKA SHAMBANI



                             
MKUU WA WILAYA YA TUNDURU JUMA MADAHA
Na Augustino Chindiye, Tunduru


WAKATI wakulima wa mazao ya Chakula Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wakilalamikia
kutozwa ushuru mkubwa kupitia vizuizi vilivyo wekwa na Wakala aliyeshinda zabuni ya kukusanya ushuru wa mazao ameahidi kuto msaidia mtumishi yeyote atakaye bainika kukiuka maelekezo yake.

Pamoja na kuitolewa kwa kauli hiyo Meneja wa kampuni ya StetyBussiness inayo kusanya ushuru huo katika halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Rashid Akbal aliwafananisha watumishi hao na mafisadi ambao wamekuwa wakiichafulia kasi ya Utendaji Serikali ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Kampuni yangu inafanya kazi kulingana na maelekezo tuliyosaini katika Mkataba na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya hiyo” alisema Akbal na akatumia nafasi hiyo kuwaomba wakulima watakao fanyiwa vitendo viovu na watumishi hao kutoa taarifa zenye ushahidi kwake ili waweze kuwawajibisha.


Akbal ambaye alikuwa akijibu swali la kwanini kampuni yake inatoza ushuru hadi wakulima wa kawaida wanaobeba kuanzia debe mbili aliendelea kueleza kuwa maelekezo yaliyotolewa kwa wafanyakazi wa
kampuni hiyo ni kutoza wafanyabiashara wanaonunua mazao ya wakulima tu na si kuwatoza hadi wakulima wanao rudisha mazao yao kutoka shambani.

Akizungumzia hali hiyo Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya hiyo Mary Ding`ohi mbali na kukiri kupokea malalamiko mengi juu ya tozo hizo alisema kuwa ofisi yake ina andaa utaratibu wa kumwita mzabuni huyo na kumpatia maelekezo upya zikiwa ni juhudi za kuondoa kero hiyo.


Alisema katika maelekezo ya awali mzabuni huyo alielekezwa kukusanya kiwango kisicho zidi asilimiaa 5% kutoka kwa wafanyabishara hao wa mazao ya Chakula na kwamba mkataba huo pia uliwaondoa katika tozo hiyo wakulima wanaorudisha mazao yao kutoka shambani baada ya kuyavuna.


Akizungumzia kero hiyo katibu wa Umoja wa Chama Cha wauzaji na wanunuzi wa mazao ya wakulima (WAMANATU) Wilayani Tunduru Athuman Milanzi alisema kuwa katika uchunguzi wao wamebaini kuwa kero hiyo inasababishwa na Mzabuni huyo kulazimisha kukusanya tozo hiyo kwa zaidi ya asilimia 5 iliyo kubaliwa katika mkataba wao.


Mwisho

Tuesday, April 24, 2012

SONGEA GLOBAL NETWORK YAZINDURIWA NA MKUU WA MKOA WA RUVUMA SAID MWAMBUNGU

HOTUBA YA UFUNGUZI WA SONGEA GLOBAL NETWORK (SGN) KWENYE UKUMBI WA AGOPAL – SONGEA TAREHE 21/04/2012.
Mh. Mwenyekiti,
Mh. Katibu
Mh. Mhasibu
Ndugu Wanamtandao,
Ndugu Wageni waalikwa,
Mabibi kwa Mabwana.

ASALAAM ALYEIKUM! TUMSIFU YESU KRISTO!

Kwanza, Nampenda nianze kwa Kumshukuru Mungu kwa Baraka na Neema zake alizotujalia na kuweza kutufikisha hapa kwa ajili ya kufanya tukio muhimu la uzinduzi wa mtandao wenu huku tukiwa na afya njema na furaha.

Pili, naomba niwashukuru sana kwa kunialika kuja kuungana nanyi katika siku hii muhimu ya kuzindua mtandao wenu (Songea Global Network). Mmenipa heshima na kunionyesha upendo kwa mwaliko wenu. Asanteni sana!

Tatu, naomba nitumie fursa hii kuwapongeza sana kwa ndoto yenu, juhudi, nia na dhamira ya kuanzisha na kuendeleza mtandao wenu huu wenye malengo mliyojipangia ninyi wenyewe. Leo kweli nashuhudia ndoto ikizaa jambo la uhalisia nayo ni Songea Global Network, hongereni sana!

Chama au kikundi chochote cha watu hujengwa na mambo makuu matatu. Kwanza ni mahudhurio ya watu au wanachama, katiba na michango ya wanachama (rasilimali, ushauri, muda, fedha na nguvu). Kama mwanzo wa chama chenu napenda niwaombe tokea mwanzo kuwa kama mnanuia kweli ustawi, mafanikio na maendeleo ya mtandao wenu basi jibidisheni nyote kuhudhuria vikao bila kuchoka wala kudharau kwani mtu mmoja una thamani kwa mtandao huu. Tena jitahidini kuunda na kuwa na katiba imara itakayokuwa dira na mwongozo wa kufikia mafanikio ya malengo mliyojiwekea. Na Zaidi jalini mtandao wenu na kujitoa sadaka nguvu, akili, utashi, rasilimali muda na michango yenu ya hali na mali katika kujenga, kukuza na kustawisha. Haya kwenu ni ya msingi na ya kuzingatia kati ya mengi kama mnataka kuwa na mtandao imara na wenye nguvu.

Mmeunda mtandao kwa malengo mliyoyataja kama kusaidiana, kufahamiana, kujengeana uwezo na kushauriana n.k. Mie natambua kuwa mtandao ili uendelee mbele kuwa wenye nguvu, wenye mafanikio na watu wengi inapaswa kuutangaza, kuulinda, kuukuza, kuustawisha, kujivunia na kuufurahia. Tumieni fursa hii kufanya yale yote mtakayoona yanausaidia mtandao wenu kustawi na zaidi epukeni yale yote yanaweza kuvunja na kudhoofisha mtandao kama ubinafsi, dharau, chuki, fitina na majungu. Haya ni sumu kwenu!

Ntatolea lugha ya picha ya mtandao wenu. Mfano mtandao wa simu wa Vodacom unawauunganisha watu wenye line za Vodacom na wengine. Promotion zikitoka zinawapata wote na mtandao ukikatika hasara ni kwa wote. Vivyo nanyi, muwe na nia ya kuleta faida ya wote na kuepa yanayowaletea hasara wote. Hili limo ndani ya uwezo wenu.

Leo mmeitangazia Songea, Ruvuma, Tanzania na dunia kuwa mna ndoto kubwa ya mafanikio. Kwa kawaida kuanzisha kazi ni rahisi kuliko kuiendeleza na kuimalizia. Mmeanza kwa kishindo, sasa msirudi nyuma. Daima kwenda mbele kwa kasi na viwango ili ndoto yeni itimie. Inawezekana, timizeni wajibu wenu.

Naomba tuendelee kuchangia mtandao huu sisi sote tuliopo ili uweze kuwa msaada wa ushauri, msaada wa kiuwezeshaji na msaada wa rasilimali watu wenye upeo na ndoto kwa mkoa wetu wa Ruvuma. Kufanikiwa kwa Songea Global Network ni kufanikiwa kwa mkoa wa Ruvuma. Katika maisha mafanikio yanapimwa kuanzia mtu mmoja mmoja. Kama kikundi endeleeni kuutanganza vyema mkoa wetu wa Ruvuma. Mti hauwezi kujifanya kinyago mpaka umechongwa. Basi chongeni vyema mtandao wenu ili uzae matunda mema na bora sana.

Mimi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa natoa au Mkuu wa Mkoa ametoa kiasi cha Tsh 300, 000/= kuachangia umoja na mtandao huu wa wanasongea wenye nia njema ya kuwa kisima cha ushauri, uwezeshaji na watu wanaopenda kuitangaza Ruvuma kwa mafanikio katika yale wanayoyafanya. Naomba na wengine tuliopo hapa ambao hatujauchangia mtandao huu kila mmoja agusike na ajitolee hapa ili kuuchangia mtandao wetu kwani “Peke yetu tunafanya machache, pamoja tunafanya mengi,” alisema Hellen Keller, Mwanafasihi wa Marekani.

Mwisho, naomba niwatakie kila jema katika makuzi ya mtoto mliyemzaa leo Songea Global Network. Kuzaa si kazi, kazi ni kulea. Leeni mtandao huu uwe taa ya kutoa giza la umasikini na uwe chumvi ya kuleta ladha kwa mafanikio yenu na mkoa wa Ruvuma. Kama wengine waliweza kwanini nyie mshindwe?Hapana, kataeni msamiati wa kushindwa na siku zote neno msamiati wa kwanza uwe ni USHINDI DAIMA. Heri na mafanikio kwenu na Hongereni sana. Sasa natamka rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mhe. Said Mwambungu kuwa nimeuzindua rasmi mtandao wenu wa “SONGEA GLOBAL NETWORK.”

Mungu Ibariki Ruvuma,
Mungu Ibariki Songea Global Network
Asanteni kwa kunisikiliza.

RISALA YA WANAMTANDAO KWENYE UFUNGUZI WA SONGEA GLOBAL NETWORK (SGN) KWENYE UKUMBI WA AGOPAL – SONGEA TAREHE 21/04/2012.

Mh. Mgeni Rasmi,
Mh. Mwenyekiti,
Mh. Viongozi,
Ndugu Wanamtandao,
Ndugu Wageni waalikwa,
Mabibi kwa Mabwana.

HABARI ZA JIONI NYOTE!

Wahenga walishanasihi kwamba, “Moyo usiokuwa na shukrani hukausha mema yote.”  Tutakuwa wezi wa fadhila  kama hatutamshukuru sana Mwenyezi Mungu mwingi wa fadhili, rehema na mapendo kwa kutujalia sote uhai na afya na kutujalia nafasi hii adimu na adhimu ya kushiriki tukio hili la kihistoria uzinduzi wa mtandao wetu wa “SONGEA GLOBAL NETWORK.”

Tena, tusheheneze shukrani zetu nyingi kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mh. Said Thabit Mwambungu ambaye amebariki tukio hili liwepo kwa kumtuma mwakilishi wake Kaimu Afisa Tawala wa Mkoa wa Ruvuma ndugu… Seligius Ngahi …….kuja kuwa Mgeni wetu Rasmi. Naye akakubali kwa hiari na utayari. Asante sana ndugu kwa kukubali kuwa Mgeni Rasmi.

Hali kadhalika, tunawashukuru wale wote waliojitolea kufanikisha uanzishwaji wa mtandao huu. Wanamtandao wenyewe na wadau wageni waalikwa mabibi kwa mabwana. Asanteni sana. Tujipogeze pia wanamtandao kwa kufanikisha ndoto yetu leo walau ya kupanda mbegu ya Songea Global Network. Tulitaka na tukataka sana, tumefanikiwa sana leo kuanza rasmi safari yetu ya kuifisha ndoto yetu mbali.

Kila asubuhi Tanzania, swala huamka. Anajua kwamba ni lazima akimbie kwa kasi kuliko simba anayekimbia kwa kasi sana ama sivyo atauawa. Aidha, kila asubuhi simba huamka. Anajua kwamba ni lazima kumkimbiza swala anayekimbia polepole ama sivyo atakufa kwa njaa. Haijalishi kama wewe ni simba au swala…jua linapochomoza, ni vema kukimbia!
Nasi Wanamtandao wa kila kada tunaitwa leo, sasa na hapa tulipo tukimbie kwa kasi katika kuunganisha mtandao na kujiendeleza ama sivyo tutakufa kwa njaa au kuangamiza taifa letu!

Mhe, Mgeni Rasmi na Wageni waalikwa mabibi kwa mabwana,
Awali kabisa, Mtandao wetu ulianza kama wazo la kukutana na kufanya hafla ya kuuaga mwaka 2011. Lakini baada ya kukaa tukasema hapana, tulitajirishe wazo letu kwa kuanzisha mtandao utaotuunganisha wote hata baada ya sherehe kama umoja wenye nia ya kusaidiana wakati na shida na raha, kushauriana na kujengeana uwezo ili sote tufanikiwe. Baada ya majadiliano mapana na ya kina, tulikubaliana sote tuanzishe mtandao au umoja huo tukaupa jina la SONGEA GLOBAL NETWORK (SGN). Leo ndio siku tuliyokubaliana ya kupanda mbegu imara na safi ya mtandao huu ili umee na kuwa faida kwetu sisi wanachama na kuutangaza mkoa wetu wa Ruvuma kupitia mtandao wetu huu.

Tulichagua jina hili SGN kwa sababu na dhima ya kuunganisha watu wa kada mbalimbali bila kubagua umri, kazi, kabila, jinsia, rangi, dini wala itikadi. Anayekubali malengo yetu na kuwajibika kuchangia dira yetu, huyo ni mwanachama mzuri kwetu. Tunatumia fursa hii kuwaomba wanachama wengi wajiunge zaidi ili kuupa nguvu mtandao wetu. Tena hata wewe Mgeni Rasmi tunakuomba leo ujiandikishe kama mwanamtandao ili tuufanikishe mtandao wetu. Karibu sana!

Sisi wanamtandao tupo watu wa fani mbalimbali: wajenzi, mainjinia, mafundi, wahasibu, wanafunzi,madaktari, wajasiriamali, wafanyakazi wengine wa serikali, n.k. Ni mseto ulioiva wa wanachama wenye nia ya kushikamana na kutimiza ndoto ya mafanikio, udugu, ushirikiano na utajiri!

Mhe, Mgeni Rasmi na Wageni waalikwa mabibi kwa mabwana,
Tumeamua kuanzisha mtandao huu kwa MALENGO yafuatayo
Kwanza, kusaidiana na kujaliana kwa shida mbalimbali mfano. Misiba, dharura. Hata Bill Gates ana shida zake. Shida ni sehemu ya ubinadamu.
Pili, kufahamiana na kupanua mtandao katika dunia hii ya utadawazi ambapo watu wanatafuta kuungana na kushirikiana katika maisha ya kila siku. Kujifungia ni umaskini wa mawazo na fikra.
Tatu, kuwezeshana na kujengana kimawazo, kiushauri na kiuchumi.

Nne, kufunguliana  fursa za kusaidiana kadri ya utaalamu na kazi ya kila mmoja.

Tano, baadaye kuwa na SACCOS itakayotuwezesha kiuchumi: kuweka akiba, kukopa.

Mafanikio ya malengo haya yanawezekana kadri tutakavyoendelea kuisimamia ndoto yetu kwa dhati. Ipo hadithi ya siku moja ambapo:
Watu walimuona sungura kashika fimbo na anatembea kwa haraka sana. Wakamuuliza sungura unaenda wapi mbona hauko kawaida? Naye akajibu kuwa naenda kuumuua tembo.  Utaweza sungura? Naye akajibu ndiyo, nitajaribu!

Tuchukue wajibu wa kutekeleza mipango yetu kikamilifu na kutibu matatizo yetu wenyewe kwa ujasiri kwamba tunaweza kumuua tembo wa matatizo yanayotukabili katika kujiendeleza na kuujenga mtandao wetu. Yupo Mshairi maarufu wa Uskochi Robert Louis Stevenson aliyewahi kusema, “Usipime siku yako kwa yale uliyoyavuna bali kwa yale uliyoyapanda.” Malengo hayo yametufanya tuamue kupanda mbegu ya Songea Global Network ili baadaye tuvune mbegu ya mafanikio na utajiri wa ndoto yetu kwa maslahi ya wanachama na ustawi wa mkoa wetu wa Ruvuma ambao sisi ni wakazi.

Mhe, Mgeni Rasmi na Wageni waalikwa mabibi kwa mabwana,
Leo tunavyopanda rasmi mbegu ya mtandao wetu (SGN), tunatumia fursa hii kukumbushana wanamtandao masharti ya kufanikiwa ili tuendelee mbele zaidi kufikia malengo na ndoto yetu.
·         Kujitoa kweli
·         Kupenda kweli mtandao
·         Kuwa na ndoto
·         Kutoa michango ya dhati bila kuchoka

Ni kweli kuja pamoja ni mwanzo. Kufanya kazi pamoja ni umoja. Kudumu katika umoja ni maendeleo. Kuunganisha vipaji vyetu ni kuwa timu moja. Hatimaye kustahimili pamoja ni ushindi wa mtandao wetu huu.

Kuna Hadithi, Upendo, mafanikio na Utajiri : tukikaribisha upendo wa kweli tutafanikiwa katika malengo yetu na kutajirisha mtandao wetu kwa maendeleo ya mkoa wa Ruvuma. Tutafakari na tuchukue hatua.

Inapendeza, inakubalika, inawezekana na inahitajika kuwa na mtandao imara usiokatika network na kufanikiwa kweli. Ni kweli wahenga wa Ghana walishatuasa kwa methali yao kuwa, “Unaweza kumlaumu mtu kwa kukuangusha chini lakini ujilaumu mwenyewe kwa kukataa kunyanyuka.” Naomba wanamtandao tulioamua kuanzisha kwa hiari mtandao huu tusikalie kumlaumu mtu au kujilaumu wenyewe na badala yake tudhamirie na kuwa na bidii ya kunyanyuka leo na kuendeleza ndoto na mtandao wetu. Bila shaka linaloonekana haliwezekani litawezekana, milima isiyokweeka itakweeka na miti isiyopandika itapandika.

Tumuombe Mungu ili idumu, iote na ifanikiwe mbegu ya SGN ambapo sote tuchangie maendeleo yetu na ya taifa letu la Tanzania. Karibuni sote tufurahie jambo hili adhimu na tuchangie kila mmoja kwa nafasi na uwezo wake, kiushauri na kirasilimali aliyonayo kwa  mafanikio ya SGN. Tushikane mikono tuanze safari yetu kwa hatua ya kwanza leo, kwani hata Waswahili wanasema, “Safari ya maili elfu huanzia na hatua moja.” Na hakika ni kweli.  Tumethubutu kubuni na kuanzisha mtandao, tumeweza kuanzisha mtandao huu na sasa tunanuia kusonga mbele na mtandao tuliouanzisha.

SGN safi, safi sana, SGN juu, juu sana!

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Atubariki sote.
Asanteni sana kwa usikivu wenu wa makini!

Naomba kuwasilisha!

KWA NIABA YA WANAMTANDAO WA SONGEA GLOBAL NETWORK. Imeandaliwa na Kusomwa na JOHN M. KASEMBO: 0755 417 074 / 0712 120 775: jmkasembo@gmail.com


 Mgeni rasmi aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu, Seligius Ngahi akiteta jambo na Mwenyekiti wa Mtandao wa Songea Global Network Sakina Jamal wakati wa hafla ya uzinduzi wa mtandao huo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Agopal
 Katibu Mtendaji wa Songea Global Network John Kasembo akitafakari jambo wakati wa hafla hiyo
 Mhasibu wa Mtandao wa Songea Global Network Rehema Nasibu akiendelea na utaratibu stahiki katika hafla hiyo
 Wanakamati ambao pia ni wanachama wa Mtandao wa Songea Global Network wakiwa na Mwenyekiti wa Mtandao huo Sakina Jamal katika viwanja vya Agopal
 Wanachama wa Mtandao wa Songea Global Network wakijadiliana jambo wakati wa hafla hiyo

 Wanachama wa Mtandao wa Songea Global Network wakijadiliana jambo wakati wa hafla hiyo


 Wanachama wa Mtandao wa Songea Global Network wakijadiliana jambo wakati wa hafla hiyo


Wanachama wa Mtandao wa Songea Global Network wakijadiliana jambo wakati wa hafla hiyo