| ||
|
Thursday, May 17, 2012
RC ENG, MANYANYA AKEMEA MAUAJI YA KISHIRIKINA RUKWA
Wednesday, May 16, 2012
Yeah: Sasa ni Undava Undava tu! [WANAFUNZI WAASI, MKUU WA SHULE ANUSURIKA KUUAWA)
Yeah: Sasa ni Undava Undava tu! [WANAFUNZI WAASI, MKUU WA SHULE ANUSURIKA KUUAWA) LOL
MKUU WA SHULE ANUSURIKA KUUAWA
Katika tukio lingine, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Muhoro iliyopo Wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani, ameponea chupuchupu kuuawa na wanafunzi baada ya kukimbilia porini akikwepa kipigo kutoka kwa wanafunzi wapatao 400.
...
Vurugu hizo zilitokea jana asubuhi baada ya wanafunzi hao kuasi na kuzingira shule kabla ya kufunga barabara itokayo Dar es Salaa kwenda Mtwara na kusababisha abiria kukwama kwa muda.
Kwa mujibu wa shuhuda mmoja, wanafunzi hao walikuwa wanamtuhumu mwalimu wao aliyejulikana kwa jina moja la Mwita, kuwa anawalisha ugali na maharage kila siku pamoja na kushindwa kuwapa tisheti za shule licha ya kuwa wamezilipia.
Wanafunzi hao pia wanamtuhumu mwalimu huyo kwa kushindwa kuandaa mikakati ya kuwawezesha kushiriki katika michezo ya shule pamoja na kushindwa kuwapatia vitambulisho vya shule.
Shuhuda huyo alisema mwalimu huyo baada ya kuona wanafunzi wameasi na kuanza kuzingira eneo la shule, alikimbilia porini kukwepa kipigo.
Kutokana na vurugu hizo, wanafunzi wawili walijeruhiwa na hali zao ni mbaya, huku wengine 12 wakiwa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi katika wilayani Rufiji.
Taarifa kutoka eneo la tukio zilisema kuwa, baada ya abiria ambao magari yao yalizuiwa kupita walishuka na kuanza kushirikiana na polisi kuwaondoa wanafunzi hao barabarani.
Mapambano hayo yalikuwa makali baada ya wanafunzi kuanza kuchukua mawe kutoka barabarani na kuanza kuwapiga abiria, ambapo baada ya kuzidiwa walikimbilia vijijini kujificha.
Vurugu hizo zilisababisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza, kufika eneo la tukio na kufanya kikao cha dharura jana jioni, ambapo aliahidi kushughulikia kero za wanafunzi hao haraka na kuzipatia ufumbuzi.
Mahiza akizungumza na NIPASHE jana jioni alithibitisha kwenda eneo la shule hiyo kutafuta suluhu ya vurugu hizo.
Mahiza alisema vurugu hizo zilimalizika na kwamba ameuagiza uongozi wa wilaya na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya kushughulikia madai ya wanafunzi hao.
Hata hivyo, Mahiza alisema wanafunzi hao walikuwa na hoja, lakini hawakuwa na sababu ya kufanya vurugu na kufunga barabara.
“Hawa wanafunzi kufunga barabara na mgogoro wao na uongozi wa shule kuna uhusiano gani kama siyo ukorofi wa wanafunzi?” alihoji.
Alisema wanafunzi wanane wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano ili kubaini vinara walioanzisha vurugu hizo.
Imeandikwa na Emmanuel Lengwa, Rungwe; Ashton Balaigwa, Ulanga na Richard Makore, Dar.
CHANZO: NIPASHE

WAMILIKI WA MASHINE WAMSHUKIA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI
Na Stephano Mango, Songea
WAMILIKI wa mashine za kukoboa na kusaga nafaka katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wamemshukia Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kwa kitendo chake cha kukaa kimya wakati wananchi wanateseka kwa kukosa nishati ya umeme kwa muda mrefu
Wakizungumza na waandishi wa habari jana wamiliki hao walisema kuwa kitendo cha waziri huyo kukaa kimya kinaashiria kushindwa kwake kazi toka mapema kwani haiwezekani wananchi wanateseka bila kuwa na nishati ya umeme na kusababisha gharama za maisha kupanda
Walisema kuwa kitendo cha shirika la umeme mkoani humu kushindwa kutoa huduma hiyo kwa wakati mbali ya kusababisha usumbufu kwao pia kimekuwa kikiwakosesha mapato ambayo wanayatumia kulipa kodi kwenye mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) kutokana na hasara zinazosababishwa na ukosefu wa umeme
Mkurugenzi wa kampuni ya Mtazamo Enterpress, Julius Mlawa akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kiwanda cha kampuni hiyo kinachojishughulisha na ukoboaji nafaka, usagaji na uuzaji wa unga alisema kuwa wananchi wa Manispaa ya Songea wanapaswa kuokolewa kutokana na mgao mkubwa na usio na kikomo wa umeme unaoendelea kuwakabili
Mlawa alisema kuwa mashine za kusaga nafaka ambazo zipo katika baadhi ya maeneo ya Manispaa hiyo zimeshindwa kutoa huduma kwa muda muafaka na kusababisha wananchi walio wengi kulazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma nje ya Manispaa ambako kuna mashine za kusaga nafaka zinazotumia mafuta ya Dizeli na kusababisha bei ya huduma hiyo kupanda mara mbili ikilinganishwa na awali
Alisema kuwa bei ya unga wa mahindi ambayo hapo awali ilikuwa ni shilingi 500 kwa kilo hivi sasa kilo moja ya unga wa mahindi ni shilingi 1200 na bei ya mchele kwa miezi iliyopita kabla ya tatizo la umeme halijaanza kujitokeza kama ilivyo sasa ilikuwa ni shilingi 1000 kwa kilo lakini hivi sasa kilo moja ya mchele ni kati 1800 hadi 2000.
Alifafanua kuwa bei hizo zinaendele kupanda siku hadi siku kutokana na TANESCO kushindwa kutoa huduma ya umeme kwenye maeneo ya manzese, Mfaranyaki , Bombambili, Majengo, Lizaboni Mjimwema na Msamala ambako ndiko kuna mashine nyingi zinazo saga nafaka na badala yake umekuwa ukiwashwa kwa mgao ambao ratiba yake haufahamiki kwa wamiliki wa mashine hizo.
Alisema kuwa katika kiwanda chake kuna wafanyakazi zaidi 30 ambao wanashinda kiwanda wakisubiri umeme ili waweze kufanya kazi bila mafanikio huku wakilipwa posho zao za kila siku bila kufanya kazi jambo linalosababisha hasara kubwa
Alieleza zaidi kuwa kutokana na ukosefu wa umeme ambao umekithiri katika manispaa ya Songea wafanyabiashara wengi wanashindwa kurejesha mikopo waliyokopa kwenye taasisi za fedha jambo ambalo ni hatari kwa biashara zao na jamii ambayo inanufaika na biashara hizo
Alisema kuwa kutokana na hali hiyo huenda akalazimika kusitisha kwa muda kutoa huduma ya usagaji na ukoboaji wa nafaka kama hali hiyo ya ukosefu wa umeme wa uhakika haitafanyiwa kazi na shirika hilo la umeme mkoani humu kwa sababu mbali ya kukosa mapato lakini imekuwa ni usumbufu kwa wananchi ambao wanahitaji huduma hiyo.
Kwa upande wake Meneja wa shirika la umeme mkoa wa Ruvuma Mhandisi Monika Kebara alikiri kuwepo kwa tatizo hilo na alisema hivi sasa huduma hiyo ya umeme inatolewa kwa mgawo kwa sababu uwezo wa ufuaji wa umeme umepungua sana kutokana na kuharibika kwa mitambo ya kuzalisha umeme iliyopo Kibulang’oma mjini hapa.
Kebara alisema kituo hicho kina mashine saba za kuzalisha umeme lakini kwa hivi sasa ni mashine tatu ndizo zinazofanya kazi hiyo kwa kutoa Megawati 2.6 wakati mahitaji ni Megawati 5 hasa ikizingatiwa kuwa katika mji wa Songea shirika hilo lina wateja elfu kumi na mbili hivyo bado umeme utaendea kutolewa kwa mgao lakini maeneo muhimu kama hospitali, ofisi za serikali na kambi za jeshi umeme utaendelea kutoleawa kama kawaida
MWISHO
Friday, May 11, 2012
WAANDISHI WAASWA KURIPOTI KIKAMILIFU ADHA YA UMEME MANISPAA YA SONGEA
MAHINDI YAKIWA KWENYE KIWANDA CHA MTAZAMO KWA AJIRI YA KUSUBIRI UMEME ILI YAKOBOLEWE NA YASAGWE
Na Stephano Mango, Songea
WAANDISHI wa Habari mkoani Ruvuma wametakiwa kutumia taaluma yao kikamilifu katika kuwaokoa wananchi wanaoteseka kutoka na adha wanazozipata kutokana na mgawo mkubwa wa umeme usiokuwa na kikomo unaoendelea kuwakabili katika Halmashauri ya Manspaa ya Songea
Wito huo umetolewa jana na Mkurugenzi wa kampuni ya Mtazamo Enterpress, Julius Mlawa wakati akizungumza na waandishi wa habari jana waliotembelea kiwanda cha kampuni hiyo kinachojishughulisha na ukoboaji nafaka, usagaji na uuzaji wa unga
Mlawa alisema kuwa waandishi wa habari ndio jukwaa la wananchi wanyonge ambao sauti zao hazisikiki vizuri kusemea licha ya kuendelea kuteseka na adha ya mgao mkubwa wa umeme unaowasababishia kupanda kwa gharama za maisha
Alisema kuwa mashine za kusaga nafaka ambazo zipo katika baadhi ya maeneo ya Manispaa hiyo zimeshindwa kutoa huduma kwa muda muafaka na kusababisha wananchi walio wengi kulazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma nje ya Manispaa ambako kuna mashine za kusaga nafaka zinazotumia mafuta ya Dizeli na kusababisha bei ya huduma hiyo kupanda mara mbili ikilinganishwa na awali
Alieleza kuwa kitendo cha shirika la umeme mkoani humu kushindwa kutoa huduma hiyo kwa wakati mbali ya kusababisha usumbufu kwao lakini kimekuwa kikiwakosesha mapato ambayo wanayatumia kulipa kodi kwenye mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) kutokana na hasara zinazosababishwa na ukosefu wa umeme
Alifafanua zaidi katika kiwanda chake kuna wafanyakazi zaidi 30 ambao wanashinda kiwanda wakisubiri umeme ili waweze kufanya kazi bila mafanikio huku wakilipwa posho zao za kila siku bila kufanya kazi jambo linalosababisha hasara kubwa
Alieleza zaidi kuwa kutokana na ukosefu wa umeme ambao umekithiri katika manispaa ya Songea wafanyabiashara wengi wanashindwa kurejesha mikopo waliyokopa kwenye taasisi za fedha jambo ambalo ni hatari kwa biashara zao na jamii ambayo inanufaika na biashara hizo
Alisema kuwa kutokana na hali hiyo huenda akalazimika kusitisha kwa muda kutoa huduma ya usagaji na ukoboaji wa nafaka kama hali hiyo ya ukosefu wa umeme wa uhakika haitafanyiwa kazi na shirika hilo la umeme mkoani humu kwa sababu mbali ya kukosa mapato lakini imekuwa ni usumbufu kwa wananchi ambao wanahitaji huduma hiyo.
Kwa upande wake Meneja wa shirika la umeme mkoa wa Ruvuma Mhandisi Monika Kebara alikiri kuwepo kwa tatizo hilo na alisema hivi sasa huduma hiyo ya umeme inatolewa kwa mgawo kwa sababu uwezo wa ufuaji wa umeme umepungua sana kutokana na kuharibika kwa mitambo ya kuzalisha umeme iliyopo Kibulang’oma mjini hapa.
Kebara alisema kituo hicho kina mashine saba za kuzalisha umeme lakini kwa hivi sasa ni mashine tatu ndizo zinazofanya kazi hiyo kwa kutoa Megawati 2.6 wakati mahitaji ni Megawati 5 hasa ikizingatiwa kuwa katika mji wa Songea shirika hilo lina wateja elfu kumi na mbili.
Alisema kuwa tayari jopo la mafundi kutoka Jijini Dar es Salaam limefika kwa ajiri ya ukarabati mkubwa wa mitambo hiyo na kwamba mwishoni mwa mwezi mei kutakuwa na umeme wa uhakika
MWISHO
KAGASHEKI:SIKUBALI KUNYONGWA
.MAIGE AKIRI KUPONZWA NA WATENDAJI
| ||
|
Tuesday, May 8, 2012
SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI MKOANI RUVUMA ILIVYOFANA KATIKA MATUKIO MBALIMBALI
Timu ya waandishi wa mtandao huu, inaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kwa kutokuwa jamvini siku zaidi ya 3 na hasa kwa kutokuwajuza habari za mkoa wa Ruvuma na mikoa jilani na hasa siku ya uhuru wa vyombo vya habari mei 3 mwaka huu kutokana na sababu za kiufundi ambazo zilikuwa nje ya uwezo wetu, na sasa tumerudi tena jamvini kwa kasi kubwa yenye kukidhi ladha ya kitasnia,Tunawashukuru sana wadau wa mtandao huu wa www.stephanomango.blogspot.com, kwa kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi uliokuwa unalengo la kujua tatizo letu na kutupa pole, Asanteni sana, BY UTAWALA
Mjumbe wa Bodi ya Muunganiko wa Vyama vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Mhariri Msaidizi wa Kanda ya Kusini(Tujifunze) na Mhandishi wa Habari wa Uhuru Fm, Juma Nyumayo akitoa mada ya mchango wa vyombo vya habari katika jamii katika mdahalo ulioandaliwa na Kituo cha Redio Jogoo Fm siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani Mei 3
Mwandishi wa Serikali za Mitaa Tanzania mkoani Ruvuma(ALAT) Mwakilishi wa Vyombo vya IPP MEDIA(Nipashe,Guardian,Redio One na Itv) Nathan Mtega akizungumza katika Studio ya Kituo cha Redio Jogoo kuhusu umuhimu wa waandishi wa habari katika maendeleo ya Jamii, katikati ni Muongozaji wa kipindi hicho Isabela Nchama,wa kwanza kulia ni Aden Mbelle ambaye alikuwa ni msimamizi wa kipindi hicho
Mwandishi wa Habari wa Tanzania Daima, Dira ya Mtanzania, Changamoto,Mitandao mbalimbali ya Kijamii na mmiliki wa mtandao wa www.stephanomango.blogspot.com, Stephano Mango akitoa mada ya umuhimu wa vyombo vya habari katika kukuza Demokrasia nchini, kulia ni Msimamizi wa kipindi Aden Mbelle
Kutoka kushoto ni mwongozaji wa kipindi hicho kilichorushwa hewani moja kwa moja na kituo cha Redio Jogoo Fm, Isabela Nshana na Aden Mbelle ambaye alikuwa msimamizi wa matangazo hayo siku ya uhuru wa vyombo vya habari mei 3 mwaka huu
Mtangazaji wa Redio Jogoo Innocent akifanya mahojiano na Mwandishi Juma Nyumayo katika Studio ya Redio hiyo siku ya Uhuru wa vyombo vya habari
Mtangazaji wa Redio Jogoo Innocent akifanya mahojiano na Mwandishi Nathan Mtega katika Studio ya Redio hiyo siku ya Uhuru wa vyombo vya habari mei 3, katikati ni Mwandishi Juma Nyumayo
Mwandishi Nathan Mtega akisaini kitabu katika Studio ya Redio Jogoo Fm ikiwa ni ishara ya kumaliza kipindi kilichorushwa moja kwa moja na Redio hiyo, kushoto ni Mtangazaji wa kituo hicho Isabela Nshama siku ya uhuru wa vyombo vya habari mei 3 mwaka 2012
Mwandishi Juma Nyumayo akiteta jambo na Mtangazaji wa Redio Jogoo Fm Aden Mbelle baada ya kumaliza mdaharo wa umuhimu wa vyombo vya habari katika muktadha wa uchumi, siasa na utamaduni
MUDA WA TAFRIJA KATIKA UKUMBI WA SONGEA CLUB MAMBO YALIKUWA HIVI............
Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho Jenista Mhagama mbaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu kuwa mgeni rasmi katika tafrija ya jioni ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari mkoani Ruvuma, kushoni ni Katibu Mtendaji wa Chama cha waandishi wa habari moani Ruvuma Andrwe Chatwanga, wapili kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Ruvuma Press Club Andrwe Kuchonjoma wakiimba wimbo wa kuisifu na kuipenda TANZANIA
Katibu Msaidizi wa Ruvuma Press Club, Mozes Julius Konala na Mwandishi wa Tanzania Daima kushoto, kulia ni Mwekahazina Msaidizi na Mwandishi wa Channel Ten mkoani Ruvuma Emmanuel Msigwa wakiimba wimbo wa kuipenda TANZANIA
Waandishi wa habari kutoka kulia ni Jofrey Nilai Redio Maria na Mjumbe wa Kamati wa Ruvuma Press Club, Mwakilishi wa IPP MEDIA mkoani Ruvuma Nathan Mtega na Anna wakiimba wimbo huo
Mwandishi wa Jambo Leo Thomas Lipuka Komba akitoa maombi kwa niaba ya dhehebu la kikristo katika tafrija hiyo
Naye akitoa maombi kwa niaba ya dhehebu la kiislam

Monday, May 7, 2012
CUF WATEMA CHECHE WILAYANI TUNDURU
Na Steven Augustino, Tunduru
WAKULIMA wa Mpunga Wilayani Tunduru wametakiwa kuukataa kuuza mpunga wao kupitia mfumo wa Stakabadha gharani na kugoma kulipa ushuru kulingana na maelekezo yaliyotolewa na Halmashauri ya wilaya hiyo .
Pamoja na wito huo wakulima wa mazao hayo pia wamehimizwa kuwa na mshikamano wa kugomeaa tozo za ushuru ambao umedaiwa kutozwa na Halmashauri ya Wilaya hiyo hata kwa wakulima wanao ingiza mazao yao kutoka shambani.
Wito huo ulitolewa hivi karibuni na Viongozi waandamizi wa Chama cha wananchi CUF wa Wilaya ya Tunduru kwa ushirikiano wa viongozi wa chama hicho kutoka Mkoani Mtwara wakati wakiongea na wananchi katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya baraza la Idd mjini hapa.
Akifafanua hotuba hiyo Mgeni rasmi katika mkutano huo Mwenyekiti wa Chama cha wananchi Cuf Wilaya ya Tandahimba na Mgombea wa Ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 Katani Mohamed alisema kuwa ukosefu wa wataalamu wabunifu na uvivu wa kujituma kwa viongozi katika halmshauri hiyo ndiko kuliko wasukuma kuandaa utaratibu huo huku
wakifahamu wazi kuwa mpango huo unalenga kuwaibia wakulima hao.
wakifahamu wazi kuwa mpango huo unalenga kuwaibia wakulima hao.
Huku akishangiliwa na maelfu ya wananchi waliojitokeza katika mkutano huo Katani aliwahimiza kudai haki zao bila kuogopa jambo lolote kwani vitendo hivyo vya unyonyaji ni hatari kwa ustawi wa jamii
Katani aliendelea kueleza kuwa kinachowafanya viongozi hao kufikia hatua hiyo ya kuchukua maamuzi bila kuwashirikisha wananchi kinatokana na wanatunduru wenyewe kulala usingizi wa pono na akatumia nafasi hiyo kuwataka waamke kudai haki zao vinginevyo watajikuta wameuzwa katika maeneo yao.
Alisema wakati viongopzi hao wakifikilia kuingiza zao hilo katika mfumo huo viongozi hao bado wameendelea kuwa kero katika utoaji wa msaada kwa wakulima wakorosho ambao pia waliingizwa katika mkenge huo bila kuwepo kwa makubaliano.
Akizungumzia tozo kwa wakulima wa mpunga alisema ingawa viongozi hao wanafahamu maelekezo na miongozo ya tozo hizo iko wazi kuwa anayetakiwa kulipa ushuru ni mtu yeyote au mfanyabiashara anayeondoka na shehene ya chakula kutoka ndani ya wilaya husika.
Wakitoa salamu kutoka mkoani Mtwara Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Cuf Taifa Reherma Mautuka, Katibu wa Cuf Wilaya ya Tandahimba Shaban Namaneha,Katibu wa Cuf Mtwara Mjini Said Mdoya na Mkurugenzi wa haki za binadamu Wilaya ya Tandahimba Alfonce Andrew walisema kuwa mikikimikiki ambayo imekuwa ikijitokeza katika Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara imetokana na kuchoshwa na vitendo vya unyanyasaji kutoka kwa viongozi wao.
Awali akimkaribisha msemaji mkuu katika mkutano huo mwenyekiti wa CUF
Wilayani humo Abdalah Mtalika alidai kuwa kitendo cha kuwatoza wakulima Ushuru huo wakati wakiingiza mazao yao kutoka Shambani ni cha uonevu kwavile wakazi wote wa mji huo hulima vijijini.
Mwisho
Saturday, May 5, 2012
Monday, April 30, 2012
WANACHAMA WA SACCOS YA WALIMU TUNDURU WALIDHIA ONGEZEKO LA MAKATO
Na Steven Augustino, Tunduru
WAJUMBE wa Mkutano mkuu wa chama cha Ushirika cha akiba na Mikopo cha Walimu wa Wilaya ya Tunduru kimeridhia kuongeza makato yao na kufikia Shilingi 30,000 kutoka Shilingi 15,000 walizo kuwa wakikatwa awali zikiwa ni juhudi za kutunisha mfuko kwa kutumia uwezo wa ndani.
Walisema kulingana na taratibu na sheria zinazosimamia ushirika pamoja na kuweka utaratibu wa kujiunga na chama husika pamoja na kuwekwa kwa mikakati yake pia kuwe na utaratibu wa kuwaruhusu wanachama kuchangia fedha kulingana na mahitahi tu.
Sambamba na kuthibitishwa kwa maapendekezo hayo wajumbe hao walipitisha bajeti ya mapato na matumizi ya shilingi Milioni 66,819,220 na kutumia jumla ya Shilingi 45,857,840 katika mwaka wa
fedha wa 2012 kukiwa na ongezeko la asilimia 78 % ikilinganishwa na bajeti ya shilingi milioni 52,666,000. zilizotumika mwaka uliopita wa mwaka 2011.
fedha wa 2012 kukiwa na ongezeko la asilimia 78 % ikilinganishwa na bajeti ya shilingi milioni 52,666,000. zilizotumika mwaka uliopita wa mwaka 2011.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na Kaimu meneja wa chama hicho Mwl.Hassan Isaya alisema kuwa kati ya Fedha hizo shilingi 36,675,000 zinatarajiwa kukusanywa kutoka katika vyanzo vya ndani , misaada na Ruzuku kutoka kwa wahisani wamepanga kuingiza jumla ya shilingi 800,000, na Tshs 27,851,220 zitatokana na faida ya mkopo wa CRDB.
Katika taarifa hiyo pia Mwl. Isaya alieleza kuwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2011/2012 chama hicho kiliweza kukopesha jumla ya shilingi Milioni 95,970,325 kwa wanachama wake
Mwl. Juma Ado akisoma taarifa zilizotokana na mrejesho wa mikutano mbalimbali alidai kuwa uzoefu unaonesha kuwa pamoja na kuwepo kwa upungufu wa wanchama katika chama hicho pia udogo wa makato ya Tsh 15,000 wanayo katwa wanachama wake ni kikwazo kingine kinacho kwamisha
maendeleo ndani ya chama chao.
maendeleo ndani ya chama chao.
Aidha Mwl ,Ado katika taarifa hiyo alitolea mfano hatua za maendeleo zilizopigwa na vyama vya kuweka na kukopa vya UTWANGO SACCOS iliyopo katika Mkoa mpya wa Njombe na NEWALA SACCOS Mkoani
Mtwara ambazo zimemudu kujenga vitega uchumi vya kujenga Nyumba za kulala wageni kupitia mfumo wa mbinu za uhamasishaji na kupeana majukumu ili miradi hiyo iwe vyanzo mbadala
vya kutunisha .
Mtwara ambazo zimemudu kujenga vitega uchumi vya kujenga Nyumba za kulala wageni kupitia mfumo wa mbinu za uhamasishaji na kupeana majukumu ili miradi hiyo iwe vyanzo mbadala
vya kutunisha .
Pamoja na kutolewa kwa mapendekezo hayo wito ukatolewa kwa Viongozi wa chama hicho kuongeza juhudi za utoaji wa elimu kwa wanachama wapya pamoja na kumpelekea salamu mwajiri wao kuwa siku atakayo chelewesha makato yao kupeleka katika chama hicho wapo tayari kufanya maandamano
zikiwa ni juhudi za kuongeza mapato ya ndani ili kujiletea maendeleo.
zikiwa ni juhudi za kuongeza mapato ya ndani ili kujiletea maendeleo.
Awali akifungua mkutano huo Mkuu wa 12 wa mwaka wa wanachama wa umoja huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Klasta, Afisa elimu ya Shule za Msingi Wilayani humo Mwl. Rashid Mandoa alitumia nafasi hiyo kuwahimiza wanachama hao kukopa kwa busara na kulipa kwa busara mikopo hiyo.
Wakitoa nasaha kwa nyakati tofauti katika mkutano huo Afisa Ushirika wa Wilaya hiyo Jalia Msangi na Katibu wa chama cha Walimu Wilaya ya Tunduru Mwl. Lazaro Saulo waliwahimiza wanachama hao kuwa waumini wa chama hicho kwa kukubali kwa hiari zao kuongeza makato kulingana na malengo ya kila mwanachama na kujiletea maendeleo kulingana na mahitaji yao.
Walisema kulingana na taratibu na sheria zinazosimamia ushirika pamoja na kuweka utaratibu wa kujiunga na chama husika pamoja na kuwekwa kwa mikakati yake pia kuwe na utaratibu wa kuwaruhusu wanachama kuchangia fedha kulingana na mahitahi tu.
Akifunga Mkutano huo Mwenyekiti wa umoja huo Mwl. Hassan Nakoma pamoja na kuwahimiza wanachama hao kuendelea kuwashawishi wanachama wapya kujiunga na umoja huo pia aliwataarifu wanachama hao kuwa ujenzi wa Ofisi ya chama hicho umepangwa kupitia uwezo wao wa ndani baada ya mfadhiri wao Daimu Mpakate kushindwa kutimiza masherti ya umoja huo
Mwisho
Mwisho
Saturday, April 28, 2012
WAWILI WAFA PAPO HAPO NA WATATU WAJERUHIWA VIBAYA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda
Na Gideon Mwakanosya, Songea
WATU wawili wamefariki dunia na wengine watatu akiwemo dereva wa gari hilo wamejeruhiwa vibaya mkoani Ruvuma baada ya kugongwa na gari katika eneo la Mahenge katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea baadaya ya kugongwa na gari la Jeshi la wananchi (JWTZ) la Makao makuu ya brigedi Chandamali
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Michael kamuhanda amesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saaa mbili na nusu asubuhi huko kwenye barabara ya Songea na Namtumbo ambapo aliwataja waliokufa kuwa ni Stumai Moyo (20) na Tabia Bilali (23) wote wakazi wa eneo la Mahenge wa Songea mjini na walio jeruhiwa vibaya ni Amina Moyo (2) na Issa Moyo (65) wote wakazi wa Mahenge ambao baada ya kutokea ajali hiyo walikimbizwa katika Hospitali ya mkoa ambako wamelazwa
Alifafanua zaidi kuwa gari hiyo Landlover Discova yenye namba za usajili 1513 JW 97 iliyosababisha ajali na kuuwa watu wawili papohapo na wengine wawili kujeruhiwa vibaya.
Alieleza zaidi kuwa gari hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na MT 97812 SGT Kelvin Muhagama ilikuwa ikitoka Makao makuu ya Brigedi Chandamali na kuelekea Songea mjini
Kamanda Kamuhanda alibainisha zaidi kuwa chanzo cha ajari hiyo ni mwendo kasi ambao ilimsababisha dereva wa gari hilo kushindwa kumudu usukani
Naye Mganga mfawidhi wa Hospitali ya mkoa songea Dr. Mathayo Chanangula amethibitisha kupokea maiti za watu wawili ambazo kwa sasa zimehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali hiyo na majeruhi watatu ambao wawili kati yao wamelazwa kwenye wodi za majeruhi na majeruhi mmoja ambaye ni mtoto wa umri wa mika 2 Amina Moyo amekimbizwa katika Hospitali ya Mision ya Peramiho kwa matibabu zaidi baada ya Hospitali hiyo kukosa mashine ya Ex –ray kwani imeonekana kuwa Amina ameumia kichwani ambako kunahitaji kupata vipimo vya Ex –ray ambapo kwa sasa hivi huduma hiyo inapatikana katika Hospitali ya Mision ya Peramiho
Dr. Chanangula alifafanua zaidi kuwa kwa muda mrefu hospitali ya mkoa songea haina kabisa huduma ya Ex –ray tangu mashine hiyo ilipo haribika na kwamba kwa hivi sasa wanasubiri mafundi kutoka ufiripino waje kitengeneza jambo ambalo limeonekana kuwa kero kuwa kwa wakazi wa songea ambao wamefika kupatiwa huduma hiyo lakini wamekuwa wakielekezwa kwenda Hospitali ya Mision ya Peramiho ambayo iko umbali wa kilometa 25 toka Songea mjini
Mwisho.
WAKULIMA WA KOROSHO WAGOMA KUPOKE MALIPO NUSU NUSU YA FEDHA ZAO
MKUU WA WILAYA YA TUNDURU JUMA MADAHA
Na Steven Augustino ,Tunduru
BAADHI ya wakulima wa korosho katika vyama vya msingi vya wakulima wa zao hilo wamegoma kupokea fedha za malipo yao huku wakidai kuto kuwa na imani na maelekezo yanayotolewa na viongozi wao.
Mgomo huo umefuatia kuwepo kwa maelekezo kuwa mkulima anayedai Shilingi 1200 kwa malipo ya korosho hizo atatakiwa kupokea mkononi Shilingi 850 na makulima anayedai Shilingi 350 atatakiwa kupokea Shilingi 200 huku kukiwa na maelekezo kuwa fedha nyingine watalipwa baada ya kuwasili kwa fedha zingine.
Wakiongea kwa nyakati tofauti miongoni mwa wakulima hao Mahamudu Ponera wa chama cha Msingi Nakayaya mashariki na Maghreth Mingwe walisema kuwa kitendo cha viongozu hao kuyumbisha malipo hayo kinalenga kuendelea kuichafulia sifa Serikali.
Walisema msimamo wao wa kukataa kupokea fedha hizo unatokana na wakulima kuelezwa kuwa baada ya kupokea fedha hizo watatakiwa kuacha Stakabadhi za malipo hayo na kubakia wakiwa hawana vielelezo vyovyote vinavyo onesha kuwepo kwa madai mengine katika vyama hivyo.
Alipo takiwa kuzungumzia hali hiyo Meneja wa Chama Kikuu cha wakulima wa wa Wilaya ya Tunduru Iman Kalembo alithibitisha kuwepo kwa hali hiyo na kwamba msimamo wakutoa malipo hayo umetokana na fedha zilizofika kuwa ni kidogo hivyo wao hawakuona mkulima wa kumuacha wakati wa malipo hayo na kusisitiza kuwa fedha zikifika wakulima wote watakamilishiwa malipo yao.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Madaha alipotakiwa kuzungumzia kero hiyo alidai kuwa hakubaliani na utekelezaji wa zoezi hilo na kuongeza kuwa msimamo wa Serikali ni kulipa fedha zote na siyo kidogo kidogo na kwamba kama kuna kosa lilifanyika na viongozi hao ni uzembe wa viongozi wenyewe.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Afisa Ushirika wa Wilaya ya Tunduru Msangi alisema kuwa malipo hayo yanatokana na Benki kutoa Tsh. 2,587,506,900 zimepangwa kughalimia malipo ya Kilo 1200 tu kati ya Kilo 7,367,689 zilizopokelewa katika maghala kati ya Kilo
7,570,000 zilizo zalishwa na akulima hao katika msimu wa mwaka 2011/2012.
Msangi aliendelea kueleza kuwa mchanganuao wa malipo hayo unaonesha kuwa kiasi kingi ne cha Shilingi 119,759,340 zitalipwa awamu ya pili na kwamba hali hiyo inatokana na taratibu za malipo hayo kuchelewa kupelekwa Benki.
Alisema fedha hizo zinatokana na malipo ya kilo 560,101 ambapo kati yake kilo 53,347 zenye thamani ya Shilingi 64,016,400 ni korosho za daraja la kwanza na shilingi 55,742,940 zinatokana na kilo 506,754 za daraja la pili.

Thursday, April 26, 2012
SHEREHE ZA UZINDUZI WA SONGEA GLOBAL NETWORK ZILIVYOFANA KATIKA UKUMBI WA AGOPAL
| Katibu Mtendaji wa Songea Global Network John Kasembo akizungumza na mmoja wa wanachama wa mtandao huo |
| Kushoto ni Mtaalamu na mmiliki wa Kampuni ya kufunga Aluminium Songea Wailes Sebastian akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Elimark Eng.Co. Ltd Emanuel Nehemia Chapa |
| Miongoni mwa wanachama wa mtandao huo |
| Miongoni mwa wanachama wa Songea Global Network ambao walikuwa wanakamati wa chakula wakisubiri kuhudumia msosi |
| Mwenyekiti wa Songea Global Network Sakina Jamal akifungua mziki na mmoja wa wanachama wa Songea Global Network |
| Sasa ni kusaka lumba kwenda mbele na yeyote anayetaka kucheza kiduku ruksa |
| Mpaka kielewekeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee |
Mtandao wa Songea Global Network uwe chachu ya maendeleo
NA STEPHANO MANGO,SONGEA
WAHENGA walishanasihi kwamba, “Moyo usiokuwa na shukrani hukausha mema yote.” Hii inamaanisha kuwa tutakuwa wezi wa fadhila kama hatutamshukuru sana Mwenyezi Mungu mwingi wa fadhili, rehema na mapendo kwa kutujalia sote uhai na afya na kutujalia nafasi hii adimu na adhimu ya kuandika na kusoma makala haya.
Nawashukuru wasomaji wote wa gazeti hili makini kwa kuendelea kulisoma na kutoa maoni yenu kwa mwandishi binafsi na wakati mwingine kwa viongozi wa Bodi ya Uhariri ili kuweza kuboresha kazi husika kwa lengo la kukidhi mahitaji ya wasomaji
Aprili 21 mwaka huu, nilialikwa kuhudhuria uzinduzi wa Mtandao wa Songea Global Network katika viwanja vya Hotel ya Agopal ambapo mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu ambaye aliwakilishwa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Seligius Ngahi.
Tukio hilo la kihistoria la uzinduzi wa mtandao lilihudhuriwa na watu wa kada mbalimbali lilikuwa ni mwanzo mpya wa wanachama wake kuifikia ndoto ya kuanzishwa kwake kwani walitaka, wakatakana na sasa hawana budi kuendeleza mipango waliojiwekea ili kuweza kuleta mafanikio waliokusudia toka awali wakati wanapanda mbegu ya kuanzisha mtandao huo.
Mtandao huo kama vilivyo vikundi vingine au chama chochote, una viongozi wake wakuu kwa maana ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mtendaji, Mhasibu na Kamati ya Utendaji, ambao watahakikisha malengo ya kuanzishwa kwa mtandao yanafikiwa kwa kushirikiana na wanachama wa mtandao huo.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mwenyekiti wa Songea Global Network (SGN) Sakina Jamal alisema kuwa malengo la kuanzisha mtandao huo ni kwanza, kusaidiana na kujaliana kwa shida mbalimbali mfano. Misiba, dharura.shida ni sehemu ya maisha ya binadamu.
Jamal alisema kuwa pili, kufahamiana na kupanua mtandao katika dunia hii ya utadawazi ambapo watu wanatafuta kuungana na kushirikiana katika maisha ya kila siku ,kwasababu ujifungia ni kuukumbatia umaskini wa mawazo na fikra.
Alisema tatu, kuwezeshana na kujengana kimawazo, kiushauri na kiuchumi, nne, kufunguliana fursa za kusaidiana kadri ya utaalamu na kazi ya kila mmoja na tano, baadaye kuwa na SACCOS itakayotuwezesha kiuchumi: kuweka akiba, kukopa.
Alieleza zaidi kuwa hadi tunazindua rasmi mtandao unajumla ya wanachama 20 wakiwamo watu wa fani mbalimbali: wajenzi, mainjinia, mafundi, wahasibu, wanafunzi,madaktari, wajasiriamali, wafanyakazi wengine wa serikali.
Alisema ni mseto ulioiva wa wanachama wenye nia ya kushikamana na kutimiza ndoto ya mafanikio, udugu, ushirikiano na utajiri kwani tumedhamiria kuwa mbegu imara itakayoweza kutoa matunda stahiki katika siku za usoni kama tulivyojiwekea malengo, pia tunawakaribisha wanachama wapya kujiunga katika mtandao ili uwe na nguvu kubwa ,hivyo kwa yoyote yule anayetaka na kukubaliana na malengo tuliyojiwekea tunamkaribisha.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Songea Global Network John Kasembo akielezea historia ya kuanzishwa kwa mtandao huo wakati wa hafla ya uzinduzi huo alisema kuwa ,mtandao ulianza kama wazo la kukutana na kufanya hafla ya kuuaga mwaka 2011.
Kasembo alisema kuwa baada ya kukaa tukasema hapana, tulitajirishe wazo letu kwa kuanzisha mtandao utakao tuunganisha wote hata baada ya sherehe kama umoja wenye nia ya kusaidiana wakati wa shida na raha, kushauriana na kujengeana uwezo ili sote tufanikiwe.
Alisema baada ya majadiliano mapana na ya kina, tulikubaliana sote tuanzishe mtandao au umoja huo tukaupa jina la Songea Global Network (SGN) ambapo leo ndio siku tuliyokubaliana ya kupanda mbegu imara na safi ya mtandao huu ili umee na kuwa faida kwetu sisi wanachama na kuutangaza mkoa wetu wa Ruvuma kupitia mtandao wetu huu.
Alifafanua kuwa tulichagua jina hili SGN kwa sababu lina dhima ya kuunganisha watu wa kada mbalimbali bila kubagua umri, kazi, kabila, jinsia, rangi, dini wala itikadi. Anayekubali malengo yetu na kuwajibika kuchangia dira yetu, huyo ni mwanachama mzuri kwetu.
Alieleza zaidi kuwa leo tunavyopanda rasmi mbegu ya mtandao wetu (SGN), tunatumia fursa hii kukumbushana wanamtandao masharti ya kufanikiwa ili tuendelee mbele zaidi kufikia malengo na ndoto yetu ni kujitoa kweli,kupenda kweli mtandao,kuwa na ndoto na kutoa michango ya dhati bila kuchoka
Alisema kuwa ni kweli kuja pamoja ni mwanzo. Kufanya kazi pamoja ni umoja. Kudumu katika umoja ni maendeleo. Kuunganisha vipaji vyetu ni kuwa timu moja. Hatimaye kustahimili pamoja ni ushindi wa mtandao wetu huu.
Alieleza zaidi kuwa wanachama tukikaribisha upendo wa kweli tutafanikiwa katika malengo yetu na kutajirisha mtandao wetu kwa maendeleo ya mkoa wa Ruvuma, hivyo tunawajibika kutafakari na kuchukue hatua.
Alisema inapendeza, inakubalika, inawezekana na inahitajika kuwa na mtandao imara usiokatika network na kufanikiwa kweli. Ni kweli wahenga wa Ghana walishatuasa kwa methali yao kuwa, “Unaweza kumlaumu mtu kwa kukuangusha chini lakini ujilaumu mwenyewe kwa kukataa kunyanyuka.”
“Naomba wanamtandao tulioamua kuanzisha kwa hiari mtandao huu tusikalie kumlaumu mtu au kujilaumu wenyewe na badala yake tudhamirie na kuwa na bidii ya kunyanyuka leo na kuendeleza ndoto na mtandao wetu. Bila shaka linaloonekana haliwezekani litawezekana, milima isiyokweeka itakweeka na miti isiyopandika itapandika”alisema Kasembo.
Alisema kuwa tumuombe Mungu ili idumu, iote na ifanikiwe mbegu ya SGN ambapo sote tuchangie maendeleo yetu na ya taifa letu la Tanzania. Karibuni sote tufurahie jambo hili adhimu na tuchangie kila mmoja kwa nafasi na uwezo wake, kiushauri na kirasilimali aliyonayo kwa mafanikio ya SGN.
Alisema kuwa wanachama tushikane mikono tuanze safari yetu kwa hatua ya kwanza leo, kwani hata Waswahili wanasema, “Safari ya maili elfu huanzia na hatua moja.” Na hakika ni kweli. Tumethubutu kubuni na kuanzisha mtandao, tumeweza kuanzisha mtandao huu na sasa tunanuia kusonga mbele na mtandao tuliouanzisha.
Naye mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu katika hotuba yake iliyosomwa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Seligius Ngahi alisema leo nashuhudia ndoto ikizaa jambo la uhalisia nayo ni Songea Global Network, nawapongeza sana kwa ndoto yenu, juhudi, nia na dhamira ya kuanzisha na kuendeleza mtandao wenu huu wenye malengo mliyojipangia ninyi wenyewe
Mwambungu alisema kuwa Chama au kikundi chochote cha watu hujengwa na mambo makuu matatu. Kwanza ni mahudhurio ya watu au wanachama, katiba na michango ya wanachama (rasilimali, ushauri, muda, fedha na nguvu).
Alifafanua kuwa kama mwanzo wa chama chenu napenda niwaombe tokea mwanzo kuwa kama mnanuia kweli ustawi, mafanikio na maendeleo ya mtandao wenu basi jibidisheni nyote kuhudhuria vikao bila kuchoka wala kudharau kwani mtu mmoja una thamani kwa mtandao huu.
Alisema tena jitahidini kuunda na kuwa na katiba imara itakayokuwa dira na mwongozo wa kufikia mafanikio ya malengo mliyojiwekea. Na Zaidi jalini na kujitoa sadaka nguvu, akili, utashi, rasilimali muda na michango yenu ya hali na mali katika kujenga, kukuza na kustawisha mtandao wenu. Haya kwenu ni ya msingi na ya kuzingatia kati ya mengi kama mnataka kuwa na mtandao imara na wenye nguvu.
“Nami najiunga rasmi katika mtandao pia naunga mkono jitihada mlizozianzisha kwa kutoa sh,300,000 ili ziwe chachu yaw engine kujitoa kwa lengo la kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake”alisema Mwambungu
Alieleza zaidi kuwa natambua kuwa mtandao ili uendelee mbele kuwa wenye nguvu, wenye mafanikio na watu wengi inapaswa kuutangaza, kuulinda, kuukuza, kuustawisha, kujivunia na kuufurahia. Tumieni fursa hii kufanya yale yote mtakayoona yanausaidia mtandao wenu kustawi na zaidi epukeni yale yote yanaweza kuvunja na kudhoofisha mtandao kama ubinafsi, dharau, chuki, fitina na majungu. Haya ni sumu kwenu!
Alisema kuwa leo mmeitangazia Songea, Ruvuma, Tanzania na dunia kuwa mna ndoto kubwa ya mafanikio. Kwa kawaida kuanzisha kazi ni rahisi kuliko kuiendeleza na kuimalizia. Mmeanza kwa kishindo, sasa msirudi nyuma. Daima kwenda mbele kwa kasi na viwango ili ndoto yeni itimie. Inawezekana, timizeni wajibu wenu.
Hakika wanamtandao wamethubutu,kubuni na kuanzisha mtandao, wameweza kuanzisha mtandao huu na sasa wanahitaji kusonga mbele ili uweze kuwa msaada wa ushauri, msaada wa kiuwezeshaji na msaada wa rasilimali watu wenye upeo na ndoto kwa mkoa wetu wa Ruvuma
Kuzaa si kazi, kazi ni kulea. Leeni mtandao huu uwe taa ya kutoa giza la umasikini na uwe chumvi ya kuleta ladha kwa mafanikio yenu na mkoa wa Ruvuma. Kama wengine waliweza kwanini nyie mshindwe?Hapana, kataeni msamiati wa kushindwa na siku zote neno msamiati wa kwanza uwe ni USHINDI DAIMA. Heri na mafanikio kwenu na Hongereni sana.Nyie mbele sisi nyuma
Mwandish wa Makala
Anapatikana 0715-335051
www.stephanomango.blogspot.com
Subscribe to:
Comments (Atom)