About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Thursday, June 14, 2012

MAGUFURI AITWA MAHAKAMANI


 
Na Mustapha Kapalata, Nzega

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Tabora, jana ilipokea ombi la upande wa walalamikaji la kumtaka Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli ili afike mahakamani hapo Juni 19, mwaka huu, kujibu tuhuma zinazomkabili.

Hatua hiyo ni mwendelezo wa kusikiliza maelezo ya mashahidi kwenye kesi ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi Mbunge wa Igunga, Dk. Dalaly Kafumu (CCM).

Shauri hilo lilifunguliwa na mlalamikaji, Joseph Kashindye, aliyekuwa mgombea ubunge wa CHADEMA dhidi ya Dk. Kafumu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na msimamizi wa uchaguzi.

Mapema, Wakili Kayaga Kamaliza anayewakilisha upande wa Dk. Kafumu aliiomba mahakama hiyo itoe hati ya kumtaka Waziri Magufuli afike mahakamani hapo kupitia Ofisi za Bunge Dodoma.

Dk. Magufuli ni mmoja kati ya mashahidi muhimu wanaotegemewa katika kesi hiyo kwa upande wa utetezi.

Wakati akitoa maombi hayo, pande zote mbili za walalamikaji na serikali, hazikuwa na hoja za kupinga kufuatia wito huo kwa Waziri Magufuli.

Tuhuma zinazomkabili Magufuli ni pamoja na kutoa ahadi za ujenzi wa daraja la Mbuntu ambalo ni moja ya changamoto jimboni humo, kutao ahadi za kugawa mahindi ya njaa kwa wananchi wa jimbo hilo, na viapo kwa baadhi ya ahadi alizokuwa akizitoa katika majukwaa ya kumnadi Kafumu kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa Igunga.

Jaji Mery Shangali, akitoa uamuzi juu ya hati hiyo alisema kuwa, mahakama imekubali ombi hilo la kuituma kwa Waziri Magufuli ili afike mahakamani hapo tarehe hiyo kutoa ushahidi wake.

Wakati huo huo, Profesa Abdallah Safari anayemtetea Kashindye, aliiomba mahakama hiyo iahirishe shauri hilo kufuatia mazishi ya muasisi wa CHADEMA, Bob Makani, yaliyofanyika jana mkoani Shinyanga, akidai ni lazima naye ahudhurie kama mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho.

Jaji Shangali alikubali, na hivyo kuihairisha kesi hiyo hadi leo ambapo itaendelea kusikilizwa, huku mashahidi zaidi ya 43 wakiwa wametoa ushahidi wao, 20 wakiwa ni upande wa mlalamikaji na 20 kwa upande wa utetezi pamoja na Magufuli na washtakiwa wengine wawili.

Tuesday, June 12, 2012

Rais Kikwete amwapisha RAS wa Mkoa wa Ruvuma na apokea Vitabu vya Hadithi za Kikwere

 

Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Ruvuma Bwana Hassan Mpapi Bendeyeko akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili TATAKI Dkt.Aldin Mutembei akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kitabu cha kwanza cha fasihi simulizi ya jamii ya Wakwere ikulu jijini Dar es Salaam leo. Kulia anayeshuhudia ni Mkuu wa Idara ya historia katika chuo kikuu cha Dar es Salaam Profesa Kapepwa Tambila. Dkt. Mutembei ambaye pia ni mchapishaji na msimamizi wa tafiti za Tamaduni lugha na fasihi za makabila ya Tanzania alikabidhi pia kamusi Asisi ya Kiingereza-Kiswahili na Kiarabu. (picha na Freddy Maro).

Saturday, June 9, 2012

WASAMALIA WAOMBWA KUTOA MSAADA WA MATIBABU KWA MTOTO FAHAHATI

Na Steven Augustino, Tunduru

WASAMALIA  nchini wameombwa kutoa msaada wa hali na mali ili kusaidia matibabu ya Mtoto Fahahati Rajab anayetakiwa kufanyiwa upasuaji wa kuwekewa sehemu ya kutolea haja kubwa na matundu ya masikio.
Ombi hilo limetolewa na wazazi wa Mtoto huyo Bwana na Bibi Rajab Idd wakidai kuwa hali hiyo imetokana na familia yao kutokuwa na uwezo wa kughalamia matibabu hayo yanayotarajiwa kufanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Walisema Mtoto huyo aliyezaliwa akiwa hana sehemu ya kutolea haja kubwa na matundu katika masikio July 4 2011 katika Hospitali ya Missioni ya Mbesa Wilayani humo ambako  awali watalamu wake
waliahidi kutoa msaada wa matibabu lakini kadili siku zilipo enda waliwajibu kuwa wameshindwa na kuwaomba wampeleke muhimbili.

Walisema mtoto huyo ambaye ni mzao wao wa kwanza kwa sasa ana umri wa miezi 11 hula na  hujisaidia kupitia mdomoni hali ambayo imekuwa ikiwawia vigumu watu wangine kumsaidia kutokana na kuona kinyaa.

Walisema kuwa atakaye guswa na hali hiyo anaombwa kutoa msaada wake autume kwa njia ya M-pesa kupitia namba 
0758168501
inayo mirikiwa na Baba Mzazi wa Mtoto huyo  Rajab Idd ili kuwawezesha kusafiri hadi jijini Dar es Salaam na kughalimia matibabu hayo.

Akizungumzia tukio hilo Mganga Mkuu wa Hospitali ya Serikali ya Wilaya Tunduru Dkt.Alex Kazula alisema kuwa hospitali yake ina andaa utaratibu wa kumpeleka Mtoto huyo katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili.

Mwisho

JERRY MURO:NARUDI TBC..JUMAPILI HIINITAFANYA HAYA...

 

Mtangazaji/Mwandishi wa habari ambae alisimama kufanya kazi kwa miezi kutokana na kesi ya kuomba rushwa, kesi ambayo baadae alitangazwa kushinda, ametangaza kituo chake cha kazi baada ya wengi kutomuona kwa muda TBC alikokua akifanya kazi.

Jerry amesema anarudi kufanya kazi TBC na jumapili hii saa tatu na nusu usiku ndio kipindi chake cha kwanza kitaanza kuonekana ambapo kitakua kinaingia kwenye siasa, afya, Uchumi na mengine.

Jerry amethibitisha kwamba wakati alipokua kimya baada ya kushinda kesi kuna vituo vingi vya TV Tanzania ambavyo vilitaka kufanya kazi na yeye lakini alishindwa kwa sababu vituo vingi sasa hivi vinafanya kazi kwa makundi ya kisiasa, vingine vimeegemea upande mmoja ndio maana akaamua atumikie kwanza wananchi.
“Sio kwamba TBC ndio mwisho wangu lakini ni sehemu ambayo naweza kukaa na kuangalia nakwenda wapi nafanya nini sehemu gani, kila kitu lazima kiwe na mwanzo kwa hiyo hilo kwangu ni mwanzo tu lakini kama nafasi nzuri zitajitokeza basi zitapewa nafasi” – Jerry Muro

Friday, June 8, 2012

UJIO WA FILAMU YA ADELAHIDA NI NGUZO MUHIMU KATIKA KUINUA TASNIA YA FILAMU MKOANI RUVUMA

 

Kaa tayari kwa Filamu ya Adelahida iliyotayarishwa na Mtayarishaji anayechipukia Shukrani K.Faraji.
 
Ni ndugu wa mapacha watatu Ade,Lah na Ida wanakuja kukutana tena baada ya kupoteana kwa muda wa miaka ishirini.
 
Kujua kilichosababisha utakiona ndani ya Filamu hii kwani ipo mitaani.
 
Ni filamu iliyotengenezwa kwenye mazingira ya asili katikati ya Misitu ya maeneo ya milima ya Matogoro-Songea.
 
Filamu hiyo itazinduliwa rasmi katika Ukumbi wa Songea Club Tarehe 1,7,2012 majira ya alasiri

MWAKYEMBE ALIPUKA TENA NA AANIKA MADUDU YALIYOMNG'OA MKURUGENZI ATC



Na Nasra Abdallah

WAZIRI wa Uchukuzi, Dk. Harison Mwakyembe, ameendelea kuwasha moto ndani ya Shirika la Ndege (ATCL) ambapo jana aliweka bayana sababu kadhaa za kutengua uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Paul Chizi.

Akizungumza na wafanyakazi wa shirika hilo katika karakana ya uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam, Mwakyembe alisema kamwe hawezi kufanya kazi na watendaji wabovu na kuwataka wale walioumizwa na maamuzi yake kuacha kazi mara moja.

Huku akionyesha kukasirika, waziri huyo aliapa kuendelea kufukuza watendaji wengine zaidi watakaobainika kwenda kinyume na sheria.
Akitaja sababu zilizomwondoa Chizi, alisema kuwa uteuzi wake haukuzingatia tarartibu za utumishi wa umma.

“Chizi katika ripoti yake ya uzoefu wa kazi inaonekana kuwa alishastaafu kwa mujibu wa sheria ambapo kwa wafanyakazi wa aina yake kuna taratibu za kuwaajiri, hivyo anatakiwa azifuate ili kuajiriwa tena,” alisema.

Mbali na hilo, sababu nyingine iliyomponza mkurugenzi huyo ni kuingia mkataba wa kukodi ndege bila ridhaa ya serikali wala wizara husika.
Hata hivyo, Dk. Mwakyembe alipotakiwa aeleze kwa nini mkurugenzi huyo alifanya hivyo, alisema anaogopa kusema kwani huenda akazidi kuibua mjadala zaidi katika taifa.

“Inasikitisha sana kuona kuwa ilifika mahali watu wakaona shirika ni mali yao na kufanya maamuzi vile wanavyotaka huku wakisahau kwamba wananchi wanaliangalia shirika hilo linavyouawa,” alisema.

Alisema kuwa serikali mbali na kutoridhia pia ukodishwaji huo haukufuata taratibu za manunuzi ya umma kwani ndege hiyo ilinunuliwa nchini Liberia ambako bidhaa zote chakavu ‘mikweche’ kama baiskeli, pikipiki na ndege zimekuwa zikipelekwa huko na nchi zilizoendelea.

Alieleza kukerwa na kitendo cha watendaji wa shirika hilo kujinunulia magari ya kifahari wakati serikali ilitoa fedha ili shirika lifufuke.

“Maana inashangaza iweje idara na kampuni ndogo zinaweza kujiendesha na kusimama zenyewe lakini ATCL imekuwa ikibebwa hadi leo pamoja na kuwa na wafanyakazi wazuri ambao wakienda kufanya kazi katika makampuni mengine wanafanya vizuri,” alihoji.

Alisema kuwa serikali inajua wako mawakala wa makampuni ya ndege binafsi, wanaodhani wataiua ATCL kumbe wanajiua wenyewe, na hivyo kuwaonya akisema kama bado wapo ni bora waondoke wenyewe kabla hajawaondosha.

Alisema yuko tayari kufikishwa mahakamani kwa ajili ya suala hilo kwani wanaofanya hivyo ni sawa na kuchezea sebuleni kwake.
Akifafanua zaidi madudu ndani ya ATCL,

 Mwakyembe alisema kuwa fedha za bima ya ndege iliyodondoka mkoani Kigoma takriban dola bilioni saba, tatu za awali zililipwa na iliagizwa ziingizwe katika akaunti ya Shirika Hodhi la Mashirika ya Umma(CHC) lakini watendaji wakafanya kinyume.

“Watendaji hao hawakufanya hivyo na kuamua kuziingiza katika akaunti ya ATCL, ambapo kati ya fedha hizo tumekuta dola bilioni mbili na dola bilioni moja zilizosalia hazijulikani zilipopelekwa,” aliongeza.

Waziri huyo aligusia pia hatua ya baadhi ya maafisa kwenda nchini China na kukaa huko takriban siku 45 kwa ajili ya kusimamia sare za wafanyakazi, jambo ambalo alidai ni ufujaji wa fedha za umma kwa kugharamia sare moja dola 49,900.

Kuhusu ajira ndani ya ATCL, Dk. Mwakyembe alisema kuna waajiriwa wengi waliokwishastaafu na pia ajira mpya zilitolewa bila kufuata tararibu ikiwemo kutangaza nafasi zilizopo ili wenye sifa washindane.

Alisema kuwa badala yake watu wamekuwa wakipeana ajira hizo kwa kufahamina na kuacha wale walio na sifa, jambo alilodai kuwa walikuwa wameamua kufukuza menejimenti yote, lakini wakahisi wangekosa kumbukumbu za urushwaji ndege.

“Baada ya kupitia baadhi ya mafaili ya watendaji hao tulikuta mwenye afadhali ni Kaimu Mkurugenzi huyu niliyemteua, Kapteni Lusajo Lazaro,” alisema.
Aliwaonya wanaozusha kuwa ametumia ukabila kumteua mkurugenzi huyo, akidai kuwa amebebwa na sifa pamoja na uwezo wake kiutendaji.

Waziri huyo alisema kuwa wameunda tume ambayo anaamini itakuja na majibu mazuri yatakayoliwezesha shirika hilo kusonga mbele.
Aliwataka wafanyakazi waliobaki, kuchapa kazi ili kumrahisishia pale anapoomba fedha serikalini aeleweke na kuongeza kwamba tayari wameshakabidhiwa sh bilioni 4.9 kutoka hazina kwa ajili ya matengenezo ya ndege.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Shirika hilo aliahidi kuyafanyia kazi yale yote waziri huyo aliyowaagiza, na kutimiza malengo ndani ya miezi mitatu waliyopewa.

Kwa niaba ya wanafanyakazi hao, Nelson Kalinga, alisema kusuasua kwa ATCL kumechangiwa na serikali kutowasikiliza wafanyakazi, kwani tangu awali walipinga kununuliwa kwa ndege hiyo ya Air Bus, ambapo waliandamana na kuandika barua wizarani lakini hawakusikilizwa.

Thursday, June 7, 2012

MBATIA ATAKIWA KUPIMA UENYEKITI WAKE


Na Asha Bani

CHAMA cha Sauti ya Umma (SAU), kimemshukia Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia, kikidai kuwa anatumiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Mwenyekiti wa SAU, Paul Kyara, alitoa kauli hiyo jana katika taarifa yake aliyoituma kwenye vyombo vya habari, akisema kuwa Mbatia anapaswa kuutafakari upya uenyekiti wake baada ya kukubali uteuzi wa Rais Jakaya Kikwete kuwa mbunge.

Kauli ya Kyara inakuja siku mbili baada ya Katibu Mwenezi wa NCCR Mageuzi, Moses Machali, kumtaka Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje (CHADEMA), kuomba radhi kutokana na matamshi yake kuwa uteuzi wa Mbatia ni dhahili anatumiwa na CCM.

Kyara alisema kauli ya Machali kama alitumwa na mwenyekiti wake, basi inalenga kuua upinzani na inaongeza ushahidi wa NCCR kutumiwa na CCM na pia kuharibu mahusiano mazuri yaliyowekwa baina ya chama hicho na CHADEMA hadi kufikia muafaka wa Mbatia kufuta kesi ya uchaguzi katika Jimbo la Kawe dhidi ya Halima Mdee.

“Kama Mbatia alifuta kesi hiyo bila hila ni bora akawa na hofu ya Mungu ili kuepuka vitisho na malumbano, ni vema akatazama upya athari za kukubali uteuzi wa Mwenyekiti wa CCM huku yeye akibakia kama Mwenyekiti wa NCCR,” alisema.
Kwa mujibu wa Kyara, hilo linaondoa uhuru wa kutoa mawazo ya kuipinga CCM na hata uwezekano wa wananchi kumwamini kama mpinzani wa kweli.

“Mimi ninamshauri Mbatia afikirie kuachia ngazi kwenye nafasi ya uenyekiti wa taifa kama ilivyokuwa kwa Juma Duni Haji alivyoondoka katika nafasi ya Naibu Katibu Mkuu CUF mara baada ya kuteuliwa kuingia kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa,” alisema Kyara.

Alisema endapo Mbatia atafumbia macho jambo hilo, yatamkuta kama yaliyomkuta Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad, ambaye ameendelea na nafasi yake ya ukatibu mkuu wa CUF na kushindwa kuikosoa serikali na kukipotezea mwelekeo chama chake.
“Mbatia na chama chake wanatakiwa kumpongeza Wenje kwa kueleza ukweli maana kuendelea kupingana naye ni kupambana na nguvu ya umma,” alisisitiza.

 

Wednesday, June 6, 2012

WAPIGAKURA WAHAMASISHWA KUMKATAA MBUNGE WA CCM MWAKA 2015

Na Steven Augustino, Tunduru.

CHAMA cha  Demokrasaia na Maendeleo (CHADEMA) kimewaomba wananchi wa Jimbo la Tunduru Kaskazini kumkataa kwa kuto mchagua Mbunge wa Jimbo hilo  Eng. Ramo Makani katika uchaguzi ujao.

Katika hotoba iliyotolewa na viongozi wandamizi wa  CHADEMA Wilayani Tunduru walidai kuwa kutochaguliwa kwa Mbunge huyo kunatokana na msimamo wake wa kukataa kujengwa kwa Barabara ya  lami katika Mji huo akishinikiza fedha hizo zikajenge barabara za vumbi vijijini.

Viongozi hao Mwiodadi Saidi (Mwenyekiti) , Nyenje Abbas (Katibu), Hadja Said  Mratibu wa Umoja wa akinamama  Wilayani humo na Ajonga Rajab Mwenyekiti wa Vijana wa Chama hicho Wilaya waliyasema hayo wakati wakiongea na wananchi katika Mkutano uliofanyika katika viwanja vya Baraza la Idd mjini hapa.

Wakifafanua hotuba zao viongozi hao walisema kuwa kitendo cha Mbunge huyo kukataa  kujengwa kwa kilometa tatu zilizo pangiwa Shilingi Milioni 300 kunalenga kuendelea kuudumaza mji wao hali ambayo walidai kuwa haitakiwi kukubalika .

Walisema Wilaya hiyo ambayo ilitangazwa kuwa Boma mwaka 1940 hadi sasa imeonekana kutopiga hatua za kimaendeleo kutokana na wananchi wake kuchagua viongozi wasio kuwa na huruma na Wilaya na wananchi wake kutoka CCM na kwamba sasa wanapaswa kubadilika kuchagua viongozi bora bila kujali chama .

Aidha viongozi hao pia walikemea tabia ya Mbunge huyo kuwatukana hadharani madiwanai wa halmashauri hiyo kuwa Umbumbu wao ndio unao wafanya washindwe kusimamia miradi na kuwafanya Watendaji wasio waaminifu kujinufaisha.

Walisema kitendo hicho kinaonesha kuwa Mbunge huyo ama hafahamu taratibu na sheria katika kuwatumikia wananchi na kuongeza kuwa tuhuma hizo alipaswa kuzisemea ndani na si kuropoka katika mikutano ya hadhara na kujidai kuwa yeye si miongoni mwa walioshindwa kusimamia miradi hiyo.

Mwisho

Tuesday, June 5, 2012

SANGA ONE AFANYA BIRTHDAY YA KUTIMIZA MIAKA 48 KWENYE HOTEL YA KIFAHALI YA TOP ONE INN

 Diwani Mstaafu wa Kata ya Bombambili Golden Sanga ,Maarufu kwa jina la Sanga One akiwa na Mwandishi wa Habari Mkongwe Gidion Mwakanosya wakiwa wakiwa wanakagua eneo ambalo sherehe ya Birthday itafanyika
Diwani Mstaafu wa Kata ya Bombambili Golden Sanga ,Maarufu kwa jina la Sanga One akiangalia mchezo wa Draft ambao ulichezwa kwa ajili ya kufurahia kutimizwa kwa miaka hiyo 48 ambapo pamoja na mambo mengine pia zawadi mbalimbali zilitolewa kwa mshindi wa kwanza hadi wa tatu

Monday, June 4, 2012

ISPEKTA CHACHA AHIMIZA USAWA WA KIJINSI KWA MAENDELEO ENDELEVU

Na Stephano Mango, Songea
WANANCHI wametakiwa kuheshimu usawa wa kijinsia katika mchakato mzima wa kuleta mabadiliko ya kijamii ,kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni ili kuleta maendeleo endelevu katika jamii zetu kwa kuzingatia uangalifu wa kisheria
Wito huo umetolewa leo na makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoani Ruvuma Ispekta Fadhira Chacha wakati akitoa mada kwenye mdahalo wa wazi ya Usawa wa Kijinsia kwa Maendeleo uliofanyika Kata ya Magagura Jimbo la Peramiho, Wilaya ya Songea ulioitishwa na Mtandao wa Asasi za Kiraia Wilaya ya Songea(Sonngo) kwa ufadhiri wa The Foundation For Civil Society
Ispekta Chacha alisema kuwa wanawake na wanaume ni mawakala wakuu wa maendeleo na sio wapokeaji wa maendeleo na mabadiliko ambayo yanaiwezesha jamii kuweza kupata mahitaji yake na kuboresha maisha kwa kuzingatia mgawanyo sawa wa rasilimali
Alisema kuwa ili kuleta maendeleo uchambuzi wa mahitaji ya wake kwa waume waweza kufanyika kwa uwepo majadiliano,kuthubutu,kutoa mrejesho,kulinganisha na kuchanganua ni vitu vipi vinavyotakiwa ili kuleta maendeleo sawa
Kwa upande wake Katibu wa Sonngo Mathew Ngarimanayo alieleza kwenye mdahalo huo kuwa vitendo vya ukatili vinavyoendelea kuathiri maisha ya watu wengi katika jamii zetu jambo ambalo husababisha madhara kimwili na kiakili
Ngarimanayo alisema kuwa ukatili wa kijinsia hudumaza maendeleo kwani waathirika hushindwa kufanya majukumu yao,kupoteza fedha,muda katika kutibu majeraha,ongezeko la walemavu na kutoweka kwa upendo
Awali akieleza maudhui ya mdahalo huo Mwenyekiti wa Sonngo Siwajibu Gama alisema kuwa lengo kubwa ni kuelimishana,kuhabarishana na kujengana uwezo wa kujiletea maendeleo kwa kuzingatia usawa wa kijinsia, hivyo elimu hiyo inapaswa iwe mbegu ya kuleta mbegu ambayo itazaa matunda stahiki katika jamii
MWISHO

NAPE NNAUYE AFANYA MAKAMUZI MAKUBWA KATIKA UWANJA WA MAJIMAJI JANA



Msafara wa pikipiki ukiongoza msafara wa  Nape kwenda Uwanja wa Maji Maji ambako alizungumza mambo mbalimbali yenye kuleta mustakabali mzuri wa CCM na Serikali.
Nape akishiriki kucheza ngoma baada ya kuwasili Uwanja wa MajiMaji .
Nape akisalimiana na wakazi wa mji wa Songea waliojitokeza katika viwanja vya majimaji kuja kumsikiliza katika mkutano wa hadhara pindi alipokuwa akiiingia kiwanjani.

Nape akipita kwenye kanga zilizotandikwa na kina mama waliovutiwa na hotuba yake



Nape akiagana na wananchi wa Songea waliojitokeza kwa wingi katika uwanja wa majimaji kuja kumsikiliza.
Nape akisisitiza jambo alipokuwa akihutubia mamia ya wakazi wa songea walipojitokeza kuja kumsikiliza katika uwanja wa majimaji.

Sunday, June 3, 2012

NAPE AANZA KAZI KWA KUZINDUA VITEGA UCHUMI VYA CCM WILAYA YA SONGEA NA MATAWI YA CHAMA

 Katibu wa halmashauri kuu ya CCM Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akifungua jengo lenye vibanda zaidi ya 60 ambavyo vimegharimu zaidi ya milioni 202 katika Halmashauri ya Manspaa ya Songea
 Shina la wakeleketwa Kata ya Mshangano ambalo limefunguliwa leo na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
 Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipandisha bendera ikiwa ni ishara ya kutambua Tawi hilo
 Wananchi na wanachama wa cha Mapinduzi wakiwa wamezunguka wakishuhudia uzinduzi wa Tawi hilo
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wananchi na wanachama wa chama cha Mapinduzi ambao walishuhudia uzinduzi wa Tawi hilo

NAPE ACHARUKA UHAMISHAJI WA KIWANDA CHA TUMBAKU SONGEA

KATIBU wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na wananchi,wanachama na viongozi wa CCM Mkoa wa Ruvuma mara baada ya kupokelewa, kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Corneus Msuha, kulia ni Mwenyekiti wa CCM Halmashauri ya Manispaa ya Songea Hemed Dizumba
Na Stephano Mango, Songea
KATIBU wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ameitaka Serikali kurudisha Kiwanda cha kusindika tumbaku cha Songea Tobacco Processing Industry(SanTop) ambacho kimepelekwa mkoani Morogoro na kuwaacha wakazi wa Ruvuma wakilalamika kutokana na msaada mkubwa uliokuwepo wakati kiwanda hicho kikifanya kazi Songea
Wito huo ameutoa jana wakati akizungumza na mamia ya wananchi,wanachama na viongozi wa Chama cha Mapinduzi (Ccm) waliokusanyika kumpokea Kata ya Shule ya Tanga Wilayani Songea mkoani Ruvuma ambako yupo katika ziara ya siku mbili
Nnauye alisema kuwa kiwanda hicho kilijengwa miaka mingi iliyopita na kiliwezesha kutoa ajira za muda mfupi na mrefu kwa wakazi wa mkoani humo na kusababisha kuwepo kwa mzunguko mkubwa wa fedha na kukua kwa uchumi wa Ruvuma na wananchi wake.
Alisema kuwa wakulima wa zao hilo kwa muda wote huo walikuwa wakijivunia kuwepo kwa kiwanda hicho, hali iliyowafanya kuongeza juhudi katika uzalishaji wa tumbaku na kujipatia maisha bora kutokana na shughuli yao ya kilimo
“ Inasikitisha kusikia wajanja wachache kwa kushirikiana na wawekezaji, bila aibu waliamua kukihamisha kiwanda hicho na kupeleka Morogoro, ambapo hakuna hata mche mmoja wa tumbaku unaozalishwa huko,” alisema Nnauye
Alisema tangu kiwanda hicho kilipohamishwa kutoka mjini humo, uchumi wa mkoa na watu wake umeshuka na kusababisha mateso makali kwa wananchi kutokana na kunyang’anywa fursa yao ya kujipatia kipato na kupelekea majengo ya kiwanda hicho kuwa mahame ambayo popo wanajihifadhi na wadudu wengine katika umasikini
Aliwataka viongozi wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Ruvuma kushirikiana kikamilifu na Serikali ili kuweza kukirudisha haraka iwezekanavyo kiwanda hicho ambacho kilikuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma
Katibu huyo ameanza ziara ya siku mbili mkoani Ruvuma ambako atafanya mikutano ya hadhara na wananchi, vikao vya ndani,kufungua mashina na matawi ya chama hicho pamoja na kuweka mawe ya msingi miradi mbalimbali ya chama
MWISHO


NAPE NNAUYE APOKELEWA MKOANI RUVUMA KWA MBWEMBWE KUBWA


Msafara wa Katibu wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ukiingia kwenye Kata ya Mshangano Halmashauri ya Manispaa ya Songea
 
 Katibu wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiingia Songea kuanza ziara ya siku mbili mkoani Ruvuma akitokea Mkoani Iringa kabla hajaelekea Mkoani Njombe kesho baada ya kumaliza ziara yake mkoani Ruvuma
 Chipukizi wa Chama cha Mapinduzi wakimkaribisha Katibu wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi Itikadi na Uenezi Nape Nnauye Mkoani Ruvuma kwa kumvesha Skafu
 Katibu wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (kulia) akipita katikati ya gwaride maalumu la Chama cha Mapinduzi huku akisindikizwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Colneus Msuha
 Katibu wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na wananchi waliojitokeza kumpokea kabla ajaanza ziara yake rasmi

Katibu wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisaini kitabu cha wageni ikiwa ni ishara ya kuanza ziara yake rasmi kwenye mkoa wa Ruvuma, wa kwanza kutoka kushoto ni Katibu wa Itikadi na Uenezi Mkoa wa Ruvuma Genfrida Haule( katikati) ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Colneus Msuha

Friday, June 1, 2012

WALIMU WAOMBA KUTENGEWA MAENEO YA KUJENGA MAKAZI YAO

Na, Steven Augustino,Tunduru

HALMASHAURI ya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma imeombwa kuandaa utaratibu wa kutoa viwanja vya makazi kwa Watumishi wa Hamashauri hiyo kama kivutio na kuwafanya wasifikilie kuhama.

Ombi hilo lilitolewa na Walimu wa Shule ya Sekondari Tunduru Wilayani humo wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wanafamilia hao kufuatia Shule yao kufanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya  Kidato cha Sita mwaka 2012.

Akifafanua ombi hilo kwa niaba ya wanafamilia hao, Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Ausi Limia alisema kuwa endapo kutakua na utaratibu huo kuna uwezekano mkubwa kwa watumishi wanaopangiwa kufanya kazi katika halmashauri hiyo kushawishika na kufanya kazi na kusaidia kukuza mji huo haraka baaa ya kujenga nyumba zao.

Pamoja na Ushauri huo pia wanafamilia hao wakaanika Changamoto mbalimbali zinazoikwamisha Shule yao kupa hatua za kimaendeleo kwa haraka yakiwemo ya ukosefu wa Walimu wa masomo ya Sayansi, Uchakavu wa Majengo na Shule kutokuwa na gari dogo kwa ajili ya kutoa huduma kwa
wanafunzi wake pamoja na kutokuwa na watumishi wasio walimu.

Awali akisoma risala katika hafla hiyo Mwl. Limia pia akabainisha kuwa katika matokeo hayo mwaka huu Shule hiyo iliweza kufaulisha wanafunzi wote 155 waliosajiriwa kujiunga na kidato cha tano mwaka jana,

Mwl. Limia aliendelea kueleza kuwa kufuatia matokeo hayo Shule yake ilishika nafasi ya pili kimkoa kati ya Shule 9 na kushika nafasi ya 21 kitaifa kati ya Shule 326 ikiwa ni tofauti na matokeo ya mwaka 2011
ambapo shule hiyo ilifaulisha wanafunzi 111 kti ya wanafunzi 133 waosajiriwa waka 2010

Ajikibu Risala hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Chande Nalicho, Afisa Tarafa wa tarafa ya Milingoti Manfredi Hyera pamoja na mambo mengine aliahidi kuzifikisha kero hizo kwa wahusika kwa ajili ya
utatuzi.

Kuhusu ukosefu wa Watumishi wasio walimu Hyera aliwaasa wanafamilia hao kubuni miradi mbalimbali ikiwemo ya kilimo ili wawezesha kumudu kuwalipa watumishi hao.

Mwisho

Tuesday, May 29, 2012

WAZEE WILAYANI TUNDURU WALILIA MATIBABU BURE

Na Steven Augustino, Tunduru

WAKATI Serikali ikitamba kutoa matibabu bure kwa Wazee na  Watoto chini ya miaka mitano,Wazee Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma wamelalamikia kutozwa fedha pindi wanapoenda kupata huduma za
matibabu,

Hayo yalibainishwa na Shekhe Mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania ( Bakwata) Wilayani humo Alhaji Waziri Alli Chilakweche wakati akiongea na Viongozi wa madhehebu hayo na viongozi wa kimila  katika ibada maalumu ya Hitma ya kuwakumbuka marehemu na wanafamilia wa Mwenyekiti Mstaafu wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Ndawambeb Mugwa iliyofanyika katika Kijiji cha Muhuwesi.

Akifafanua katika hotuba hiyo alhaji Chilakweche alisema kuwa kinacho washangaza wazee hao ni kutotekelezwa kwa ahadi za Serikali katika utoaji wa huduma za matibabu hayo bure mbali na kuwepo kwa taarifa za wazi juuu ya haki kwa wazee hao kupata huduma hiyo bure,

Alisema kama kweli Serikali ilitoa maagizo na maelekezo hayo kwa moyo wote kwanini wanashindwa kusimamia utekelezaji wake? Alihoji Shekhe Chilakweche na kuongeza kuwa kinacho tatanisha ni vitendo vya waliopewa mamlaka kutotambua hata vitambulisho vya misamaha kwa wazee vilivyo tolewa katika ngazi na maeneo tofauti wakidai kuwa wakitaka huduma waende huko.

Alhaji Chilakweche aliendelea kufafanua kuwa endapo Serikali inawapenda wazee na kuthamini mchango wao inapaswa kuzingatia maelekezo hayo ili kuwaokoa wasife kwa kukosa dawa kutokana na kukosa fedha .

Aidha katika hotuba hiyo pia Alhaji Chilakweche akatumia nafasi hiyo kuwaagiza Mashekhe wa Misikiti yote Wilayani humo na viongozi wa kimila kutumia nafasi zao kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi na kuhakikisha wanahesabiwa katika zoezi la sensa iliyopangwa kufanyika Agosti 26 mwaka huu na kuhakikisha kuwa wanatoa maoni yao katika zoezi la kutafuta maoni ya kuandika katiba mpya.

Mwisho

Sunday, May 27, 2012

MWENGE WA UHURU KUANZA MBIO ZAKE RUVUMA


Kaimu Katibu Tawala Mkoa Ruvuma Severine Tossi Akizungumza na Waaandishi wa Habari jana
Na Stephano Chitete,Songea.

MWENGE wa uhuru unatarajiwa kuzindua ,kuweka mawe ya msingi,kukaguwa na kufunguwa miradi mbalimbali ya maendeleo ipatayo 51 yenye thamani ya jumla ya  sh.1,930,357,902 mkoani Ruvuma iliyojengwa kwa nguvu za wananchi na Serikali.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambu kaimu katibu tawala wa Mkoa wa huo Severine Tossi alisema mbio za mwenge mkoani humo zinatarajiwa kuanza mei 28 mwaka huu hadi juni 3 mwaka huu ambapo utakabidhiwa katika kijiji cha Lumesule kilichopo mkoani Mtwara.

Alisema kuwa miradi itakayozinduliwa iliyojengwa kwa nguvu za wananchi inagharimu sh.206,022,645,halmashauri za Wilaya na Manispaa sh.204,486,125, Serikali kuu sh.773,599,581,wadau wa Maendeleo sh.458,809,551 na ya watu binafsi sh.287,440,000.

Aidha amewataka wananchi wa Mkoa huo kujitokeza kwa wingi kuupokea na kuushangilia mwenge huo wa uhuru ili waweze kupata ujumbe wa mwenge wa mwaka huu usemao "Sensa ni msingi wa mipango ya maendeleo yetu" wenye kauli mbiu shiriki kuhesabiwa Agosti 26 mwaka huu.

Akizungumzia kuhusu maandalizi ya sensa alisema yamekamilika na kufafanuwa kuwa mkoa huu unatarafa 24,kata 140,vijiji 509 na mitaa 79 na kwamba maeneo ya kuhesabiwa watu yaliyotengwa yapo 3,024 na maeneo ya usimamizi yapo 816.

Alifafanuwa kuwa kwa sasa Mkoa unajumla ya wakazi 1,412,084 kwa mujibu wa Sensa ya mwaka 2002 sawa na asilimia ya 2.5 ya ongezeko la watu.

Kaimu katibu Tawala huyo alisema Mwenge huo utakimbizwa katika wilaya mpya ya Nyasa, Mbinga,Songea,Namtumbo,na Tunduru ambapo Juni 3 mwaka huu utakabidhiwa kwa uongozi wa Mkoa wa Mtwara.

MWISHO.

Friday, May 25, 2012

SERIKALI YAAHIDI KUBADILISHA MFUMO WA VOCHA ZA RUZUKU

Na Steven Augustino, Tunduru

SERIKALI imehaidi kubadilisha mfumo wa usambazaji wa pembejeo za ruzuku zikiwa ni juhudi za kumsaidia mkulima wa chini na kuhakikisha kuwa huduma hizo haziwanufaishi wajanja wachache.

Hali hiyo imetokana na kubainika wazi kuwa mfumo wa sasa wa kusambaza pembejeo hizo kwa kutumia mfumo wa vocha umekuwa ukiwanufaisha Mawakala na baadhi ya viongozi na watendaji wa vijiji, Kata ambao hushirikiana na maafisa tarafa  wasio waaminifu.

Hayo yamebainishwa jana  na Viongozi waandamizi wanaosimamia mfuko wa Vocha za Ruzuku Taifa, Afisa Kilimo Wizara ya Kilimo  na Chakula anayesimamia sehemu ya Pembejeo na Flora Kumalilwa  na Mkufunzi Mkuu wa Kilimo Sehemu ya Pembejeo  Stella Mtagwaba wakati wakiongea na kamati ya Usimamizi wa usambazaji wa Pembejo Wilayani Tunduru
katika kikao kilichofanyika katika Ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo.

Wakifafanua taarifa hiyo walisema kuwa utaratibu huo mpya ambao kwa sasa unafanyiwa kazi na wataalamu umetokana na idara hiyo kupokea mapendekezo megi kutoka kwa wadau wa Kilimo wakiitaka idara hiyo kufanya mabadiliko katika mfumo huo huku wakibainisha kuwa mfumo uliopo sasa wa kugawa Pembejeo kwa wakulima umekuwa hauna manufaa kwa
walengwa kutokana na kuwepo kwa mianya inayolenga kuwanufaisha wajanja wachache kwa kuuza vocha hizo kwa mawakala.

Sambamba na matarajio hayo ya kubadilisha mfumo huo pia viongozi hao walikiri kuwepo kwa mapungufu makubwa ya ucheleweshaji wa utengenezaji na usambazaji wa Vocha kwa wakulima,kuchelewesha fedha za usimamiaji wa usambazaji wa vocha hizo kwa wakulima na ukubwa wa  bei ya vocha Changamoto ambazo walidai kuwa hivi sasa zinafanyiwa kazi kwa makini ili kuziondoa kabisa kero hizo kuanzia mzimu ujao.

Aidha katika taarifa yao pia pamoja na mambo mengine viongozi hao waliipongeza kamati ya kusimamia usambazaji wa Pembejeo Wilayani humo kwa kufanya kazi vizuri kuanzia ngazi ya uteuzi wa mawakala wa kusambaza pembejeo hizo na kwamba hali hiyo imetokana na baadhi ya
wakulima waliotembelea katika vijiji vya Nandembo, Nanguinguru, Lelolelo na Azimio.

Walisema katika mahojiano kati yao na wakulima hao pamoja na mambo mengine yakiwemo malalamiko ya ukubwa wa bei ya vocha hizo na ucheleweshaji wake wakulima wa maeneo hayo walikiri kupokea vocha hizo na kuzitumia kulingana na maelekezo kutoka kwa mabwana shamba na wakadai kupata mafanikio makubwa kwa kuvuna kati ya magunia 26 na 28 kutoka magunia kati ya magunia 4 na 8 kabla ya mfumo huo kwa ekari moja.

Wakichangia katika kikao hicho kwa nyakati tofauti Mbunge wa jimbo la Tunduru Kusini Alhaji Mtutura Mtutura, Afisa kilimo waWilaya  Jalia Msangi na Afisa kilimo wa Wilaya hiyo  Chiza Marando mbali na kuipongeza serikali kwa kubuni mfumo huo unaolemga kuwanufaisha wakulima  hasa wasio na uwezo waliiomba Serikali kuendeleza juhudi hizo kwa kuanza kuwawezesha kwa kuwakopesha zana za Kilimo yakiwemo Matrekta zikiwa ni juhudi za kuwaongezea uwezo wakulima hao.

Mapendekezo mengine yaliyo tolewa na viongozi hao ni pamoja na kuiomba Serikali kufanya mikataba ya bei ya pembejeo hizo na Mawakala wakubwa mapema ili kuwadhibiti wasipandishe bei ya soka kwa pembejeo husika na kama ambaavyo wamekuwa wakifanya sasa na kusababisha  mfumo huoo kuonekana hauna maana wala manufaa kwa walengwa kutokana na bei za Vocha na Ruzuku inayo tolewa na Serikali kutowiani kwa Asimia 50% kwa
50% na bei za soko la mbolea hizo.

Wakizungumzia mfumo wa vocha walidai kuwa pamoja na sifa ilizopata Wilaya yao katika usimamiaji wa ugawaji wa vocha za Ruzuku lakini wamekuwa wakipambana na changamoto mbalimbali zikiwemo za kuzushiwa kashfa kuwa mawakala wanaoteuliwa hupatikana kwa kutoa Rushwa.

Awali akifungua kikao hicho kaimu Afisa tawala wa Wilaya ya Tunduru, Afisa Tarafa wa Tarafa ya Mlingoti  Manfredi Kahobera Hyera alieleza kuwa  mambo ambayo huzingatiwa katika uteuzi wa Mawakala wa kusambaza Pembejeo za Kilimo kwa mfumo wa Vocha ni kuangalia na kuwachuja kwa makini baada ya kuwabaini Mawakala wasio waadilifu na wenye nia ya kuchakachua vocha bila kupeleka huduma kwa wanufaika.

Katika taarifa hiyo ya  Kahobera aliwataja mawakala waliobainika kuchakachua vocha hizo kuwa ni Michael Mdete ambaye pamoja na kukosa duka la kuuzia Pembejeo hizo lakini alikosa sifa kutokanan na kesi zao zinazoendelea mahakamani baada ya kubainika kuchakachua kwa kugushi na kujipatia Vocha wakati akiwa hajatoa huduma husika kwa wakulima.

Mwisho

Thursday, May 24, 2012

WAGONJWA WAISHUKIA WIZARA YA AFYA UKOSEFU WA EX-RAY RUVUMA

Na Gideon Mwakanosya
BAADHI ya wakazi wa halmashauri ya manispaa ya Songea wameimba serikali kupitia wizara ya Afya na ustawi wa jamii kuona umuhimu wa kuifanyia matengenezo X-ray ya hospitali ya serikali ya mkoa wa Ruvuma ambayo imeshindwa kutoa hiyo kwa wagonjwa kwa muda mrefu na kusababisha wagonjwa wanaotakiwa kupata huduma hiyo kwenda kwenye hospitali ya Peramiho ambako ni mbali na Songea mjini.

Wakizungumza na NIPASHE kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi wa maeneo ya Mfaranyaki, Mjimwema, Ruhuwiko na Mshangano ambao waliomba majina yao yahifadhiwe walieleza kuwa kwa muda mrefu sana huduma ya X ray katika hospitali ya mkoa haipatikani na wanapokwenda hospitalini hapo kupata huduma wamekuwa wakishauriwa kwenda Hospitali ya misheni ya Peramiho ambako ndiko huduma hiyo kwa sasa inatolewa.

Wananchi hao walisema kuwa ni vyema serikali ikaangalia uwezekano wa kuitengeneza mashine hiyo ambayo hapo awali ilikuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa Songea na wagonjwa wanaotoka kwenye wilaya nyingine kama vile Mbinga, Natumbo, Tunduru na wilaya mpya ya Nyasa.

Walitoa mfano kuwa hivi karibuni katika eneo la Seedfarm kwenye barabara itokayo Songea kwenda Namtumbo gari la jeshi la wananchi liliwagonga watu wanne ambao walikuwa wakitembea kwa miguu na kusababisha watu wawili kufa papo hapo na wengine wawili walijeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika hospitali ya serikali ya mkoa ambako mmojakati yao baadae ililazimika kumpeleka Peramiho baada ya hospitali hiyo kukosa huduma ya X ray jambo ambalo limeonekana kuwa ni kero kubwa kwa wananchi wa Songea na maeneo mengine.

Kwa upande wake kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dr Benedict Ngaiza alipohojiwa na NIPASHE kuhusiana na malalamiko hayo alikirikuwa mashine ya x ray ya hospitali ya serikali ya mkoa wa Ruvuma bado ni mbovu tangu mwezi mmoja uliopita.

Dr Ngaiza ambaye pia ni mganga mfawidhi wa hospitali ya serikali ya mkoa Songea alisema kuwa pamoja na kwamba katika hospitali yake haukuna huduma hiyo ya x ray lakini wagonjwa wanaohitajihuduma hiyo hushauriwa kwenda kupta huduma hiyo kwenye hospitali ya misheni ya Peramiho licha ya kuwa nayo maashine ya hospitali hiyo inaubovu haifanyi kazi kwa kiwango kinachotakiwa.

Alisema kuwa changamoto baadhi ya huduma zinazohusisha huduma ya x ray katika hospitali ya mkoa zimesimamishwa kwa sasa. Hadi hapo wataalamu toka wizara ya afya na ustawi wa jamii watakapofika na kuja kuifanyia matengenezo.

Alieleza zaidi kuwa kwa mujibu wa taarifa toka wizara ya afya na ustawi wa jamii mafundi wanatarajiwa kusambazwa katika hospitali zote za serikali zenye mashine za x ray kwa ajili ya kuzifanyia matengenezo x ray hizo ikiwemo na x ray ya hospitali ya serikali mkoa Songea.

Alifafanua zaidi kuwa pamoja na matengenezo yanayotarajiwa kufanyika bado hali si nzuri kwani chumba cha x ray kinatarajiwa kufanyiwa urakabati mkubwa ambao utafanywa kwa muda wa zaidi ya miezi mitatu. Hivyo hata kama mashine hiyo itakapo tengenezwa bado huduma ya x ray itasimama hadi ukarabati wa chumba hicho utakapo kamilika.

TANI 5480 ZA KOROSHO ZILIZOKWAMA TUNDURU ZAPATA MNUNUZI

Na AUGUSTINO CHINDIYE, Tunduru
JUMLA ya tani 5480 za korosho za Wakulima wa Tunduru Mkoani Ruvuma zilizo kuwa zimekwama katika Vyama vya Msingi vya Wakulima vya Wilaya hiyo baada ya Serikali kutoa dhamana ya fedha za Kugharamia malipo kwa Wakulima husika zimepata mnunuzi.

Taarifa ya kupatikana kwa mteja wa Korosho hizo imetolewa na Meneja wa
Chama kikuu cha Wakulima wa TAMCU  Imani kalembo jana wakati akiongea na wajumbe na wadau wa taasisi hiyo Wilayani humo katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Chama hicho mjini hapa.

Akitoa taarifa hiyo Kalembo alisema kuwa Korosho hizo zenye thamani ya Shilingi Bilioni 8 zimenunuliwa na kampuni ya Pan- African Consulting And Exportng (P.A.C.E) kutoka Carfonia
Martekan ambayo imekubali kununua korosho hizo kwa bei ya Shilingi 1491 kwa kila kilo moja.

Kalembo aliendelea kueleza kuwa tayari kampuni hiyo imekwisha tiliana saini mkataba wa kununua Korosho hizo na kuzifanyia uchunguzi wa kuzikagua kwa kuzikata ili kubaini ubora wake na kuahidi kuzilipia kwa kuingiza fedha Benki ya Nmb  muda wowote wiki hii.

Alisema kufuatia hali hiyo Chama hicho kinajipanga kuangalia uwezekano na taratibu za kulipa madeni yote ya wakulima ili kuondokana na kero hiyo iliyochukua muda mrefu.

Kwa mujibu wa takwimu za uzalishaji wa wa zao hilo kutoka katika Chama Kikuu cha Ushirika wa Wakulima wa Korosho Wilayani Tunduru (TAMCU) zinaonesha kuwa katika msimu wa Mwaka 2011/2012 chama hicho kupitia vyama vya msingi umeongezeka na kufikia kilo 7,570,000 kutoka kilo kilo 4,135,042 zilizo zalishwa  mwaka 2010/2011.
Mwisho

Wednesday, May 23, 2012

BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA YA MBINGA LAANZA KIKAO CHAKE AMBAPO HOJA NA TAARIFA MBALIMBALI ZA KAMATI ZINAENDELEA KUTOLEWA

 Madiwani wakiwa wamesimama ikiwa ni ishara ya heshima wakati Mwenyekiti wa Halmashauri Oddo Mwisho, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Priska Haule na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Shaib Mnunduma wakiingia kwenye kikao hicho
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Oddo Mwisho (katikati) akifungua kikao, kulia ni Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mashariki Gaudence Kayombo na kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Shaib Nnunduma wakiingia kwenye kikao hicho
 Waandishi wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo wakiendelea kufuatilia hoja mbalimbali
 Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya fedha, mipango na uongozi Prisca Haule akiwasilisha taarifa ya kamati

 Madiwani wakiendelea kufuatilia hoja mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa katika kikao hicho kutoka kwa wajumbe
Wenyeviti wa kamati za kudumu za Madiwani wa Halmashauri hiyo wakiendelea kufuatilia taarifa zao kwa umakini

AZIMIO LA ARUSHA, MWAROBAINI PEKEE ULIOBAKI


 
Paschally Mayega
RAIS wangu Kikwete, nalilia Azimio la Arusha sasa kuliko wakati mwingine wowote! Kuachwa kwa baadhi ya mawaziri kumeibua mambo ya kuogofya ambayo yanaweza yakatupeleka kwenye mwisho wa aibu kubwa!

Baadhi ya wananchi wa Jimbo la Moshi Vijijini wanasema mbunge wao hakutendewa haki kuachwa katika baraza la mawaziri.

Raymond Assenga, mmoja wa wananchi hao alisema, “Mwaka 2010 Chami alituunganisha, tukachanga zaidi ya milioni 50 kusaidia kampeni za Rais”.

Hili ndilo neno linalotakiwa litolewe ufafanuzi. Zilichangwa milioni 50 kama bei ya kuununua uwaziri? Uwaziri 2010 ulikuwa unauzwa? Hii ikithibitika, itakuwa ni kashfa kubwa!

Kama hivyo ndivyo, je, wale mawaziri wawili ambao nao walituhumiwa kama mbunge wao Cyril Chami lakini wao wamo watakuwa walichangia shilingi ngapi? Ukiifikiria sana hali hii damu inaweza ikakusimama mwilini, hebu tuifikirie kwa kibonzo hiki.

Uongozi wa Kampuni moja tajiri sana duniani, mabingwa wa kutengeza chapati walitaka kuweka tangazo la chapati zake katika sehemu litakakosikika dunia nzima.

Wakakusanya masanduku mengi yaliyojaa fedha nyingi wakampelekea Baba Mtakatifu, Papa, wakimwomba awaamuru Wakristu wote duniani, wanaposali sala ya Baba yetu uliye mbinguni, badala ya ile sentensi wanayosema, ‘utupatie leo mkate wetu wa kila siku’, waseme, ‘utupatie leo chapati yetu ya kila siku’.

Baba Mtakatifu alipozikataa hela nyingi kiasi kile, Jamaa walizimia. Eti walishindwa kuelewa ni kiasi gani cha fedha kampuni ya kutengeneza mikate ilimpatia Baba Mtakatifu mpaka akakubali mkate utangazwe katika sala ya Baba yetu.

Rais wangu sasa inanijia akilini, wakati Jumanne Maghembe akiwa waziri wa Elimu, wadau wa elimu walifanya kila waliloweza kumwambia kuwa mtindo wa kitabu kimoja cha kiada pamoja na kwamba ni kuua elimu nchini lakini huko ni kuchochea rushwa kubwa kabisa!

Alikuwa mbogo mtu huyu sijapata kuona mfano wake. Lakini ni kweli kulikuwa na minong’ono mitaani kuwa waziri aliagizwa kuandaa mazingira ya uchaguzi mkuu 2010.

Kama naye alichangia, atakuwa alichangia kiasi gani mpaka abakishwe? Natamani hii isiwe kweli! Inapofikia watu wanauza mpaka elimu ya nchi nzima, ni kipi wanakuwa wamebakisha cha kuutambulisha utu wao? Mavazi tu!

Kama watu walilipia uwaziri nani atakuwa na ubavu wa kuwaamuru mawaziri hao? Utajikuta unalazimika kuunda baraza la mawaziri kubwa kuliko mahitaji halisi ya nchi. Hili tumeliona mara zote! Kulipa fadhila!

Hawa ni mawaziri. Kuna wakuu wa mikoa na wilaya. Au ndiyo sababu uteuzi wa wakuu wa wilaya imechukua miaka miwili? Yawezekana pia ikawa ni sehemu ya sababu ya kuongeza mikoa na wilaya? Tuendako, siko!

Mwenyekiti wa chama cha wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Haruna Lipumba alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Aprili 24 mwaka huu alisema, “Tatizo la ubadhirifu haliwezi kwisha katika serikali ya awamu ya nne maana tatizo siyo watendaji wala mawaziri, ni Rais Kikwete mwenyewe…amekuwa ni mtu asiyekuwa na uamuzi.”

Alisema, “Haishangazi kuona mawaziri katika wizara moja hawaelewani. Kuna mawaziri wana nia njema na wanasimamia haki, lakini hata wakitoa mapendekezo yao yanapuuzwa.

Na wapo wanaotumia nafasi zao vibaya huku rais akiendelea kuwachekea.” Nadhani ufunuo wa hapo juu ulikuwa haujamfikia. Utamfanya nini mtu aliyejilipia?

Naye Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk. Willibrod Slaa akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya Sahara Aprili 22 mwaka huu jijini Mwanza alisema, ”Uozo uliofanywa na mawaziri umekuwa ukipata baraka zake, kama

Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri na amekuwa na kawaida ya kulinda ubovu wa mawaziri wake kutokana na udhaifu wake mwenyewe wa kiuongozi.” Maskini Mwalimu Nyerere hakujua kama Ikulu kuna biashara. Nyumba ya baba yangu itageuzwa pango la walanguzi!

Dk. Slaa aliendelea kusema, “Kikwete ndiye chanzo cha udhaifu wote serikalini unaosababisha matatizo makubwa kwa taifa na kwa wananchi”. Huenda rais wetu si dhaifu kiivyo ila ikawa ndiyo hitaji ya mazingira ya biashara iliyofanyika.

Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa hivi karibuni alikaririwa akisema, “Muundo na imani ya chama cha mapinduzi ni mzuri. Tatizo ni uongozi katika utendaji. Ni dhaifu mno katika kufanya maamuzi.

Mara nyingine yamefanyika maamuzi yasiyo sahihi na wakati mwingine maamuzi yakifanyika yanafanyika yakiwa yamechelewa mno kiasi cha kuyafanya yaonekane ni maamuzi yasiyo na maana yoyote”.

Kama hawataki kukosolewa, watatakaje kujirekebisha? Mtu huyu alishiriki kikamilifu kuwaletea Watanzania uongozi wa awamu ya nne, inawezekana vipi asiujue udhaifu wa waliokuwa washirika wake?

 Lakini Edward Lowassa, kama alivyo Abdulrahman Kinana lazima wajue kuwa wana deni kubwa kwa Watanzania kutokana na maisha magumu waliyonayo sasa ambayo ni matokeo ya uongozi walioupigania.

Ndugu Rais wakati wa kuja mwaka 2005 ulikuja na Edward, ilibidi wakati wa kuondoka uondoke na Edward vinginevyo wananchi wataamini maneno ya Dk. Slaa kuwa, “Ni kiongozi anayekwepa lawama na kubebeshwa mzigo wa uzembe wake kwa watu wengine”.

Mlianza vema kwa maagizo mfululizo yaliyokuwa yanatoka Dar es Salaam kwenda mikoani, wilayani hadi vijijini. Hakukuwa na mzaha. Hali hii ilipelekea pia mateso fulani kwa baadhi ya wananchi na hasa pale viongozi wa vijijini walipojaribu kukabiliana na kasi ya maagizo katika shughuli za maendeleo hasa ujenzi wa shule za kata. Watu walinyang’anywa mifugo yao na madhila mengine mengi.

Msingeweza kuepuka kufanya makosa kwa sababu nyinyi nanyi ni wanadamu, lakini mlijijengea heshima kwa wananchi kwasababu kila tulipoandika kukosoa utendaji wenu mlifuatilia na kuchunguza na ilipobidi mkasahihisha bila kusubiri mateso kwa watu wenu kuzidi.

Tofauti na sasa ambapo huwezi kuthibitisha kama wanasikia au hawasikii. Kama hawasomi haya tuandikayo ni kwa hasara yao wenyewe kwasababu wananchi wanasoma.

Richmond ni matokeo ya viongozi kutaka kufanya biashara. Haya ndiyo makatazo yaliyomo katika Azimio la Arusha. Baba waambie watu wako, ‘mnahofia nini’ na Edward Lowassa kuhusu Richmond?

Tofautianeni lakini tambueni kuwa siku ya hukumu wananchi watawahukumu pamoja!
Kutokana na mparaganyiko wenu wahuni wachache wametumia fedha na raslimali nyingi za nchi kwa kisingizio cha kupinga ufisadi na gamba!

Aliyeileta Richmond alitenda dhambi kubwa. Waliowabebesha watu wengine dhambi ya Richmond walitenda dhambi kubwa zaidi na ndiyo maana hawana amani katika vifua vyao siku zote.
Wasipotubu, itawawewesesha usiku na mchana mpaka siku yao ya hukumu itakapowafika!

CHADEMA wamesema watazingatia Ibara ya 8 ya katiba waende kwa wananchi ili ipigwe kura ya kutokuwa na imani na Rais. Nchi imekwama. Tutatokaje hapa tulipokwama? Baba hakuna tulichoachiwa hapa cha kuchagua.

Kuiepusha nchi isiingie katika vurugu tulirejelee Azimio la Arusha ili tuanze upya! Nchi imevurugwa kupita maelezo.

Rais wangu nchi iko katika mchakato wa kuandika katiba mpya. Hili ni jambo jema sana. Lakini tunataka katiba mpya, ili iweje? Katiba mpya haiwezi kutuletea chakula wala maisha bora.

Katiba mpya itashusha bei ya vyakula? Bila uongozi makini, imara katiba mpya itafaa vipi? Swali hapa ni je, tunaye msimamizi imara wa kusimamia hiyo katiba mpya?

Katiba tuliyonayo ndiyo ileile aliyokuwa akiitumia Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati wa urais wake.

Ni katiba ileile aliyokuwa anaitumia Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin William Mkapa, Rais wa awamu ya tatu ukiacha marekebisho madogo madogo ya hapa na pale.

Imewezekanaje imekuwa mbovu kupindukia ghafla tu katika awamu ya nne?
Katiba hii hii na ubovu wake huu huu usingekuwa kero kubwa kwa nchi kama inavyoonekana sasa, kama Azimio la Arusha lingekuwapo.

Maadili na miiko ya uongozi viliyokuwa vimezingatiwa ndani ya Azimio ya Arusha visingeruhusu hali hii kufikia hapa.

Rais wangu ni mengi yamesemwa na kuandikwa juu ya Azimio la Arusha. Hata wakati fulani Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisikika akisema, “Kila ninapotembea mfukoni mwangu ninakuwa na vitabu viwili. Biblia Takatifu na Kijitabu cha Azimio la Arusha”.

Mwalimu Nyerere alilienzi Azimo la Arusha kama sala. Wakati akiwa madarakani Nyerere hakuchoka kulihubiri Azimio la Arusha kwa watu wake. Alifanana na mitume na manabii waliohubiri habari njema kwa mataifa.

 Nchi ilitulia. Upendo na mshikamano kati yetu vilistawi kiasi cha kutufanya tushindwe kutambua tofauti zetu.

Ndani ya Azimio la Arusha wote tulikuwa ndugu na tuliitana ndugu toka mkuu wa nchi mpaka mponda kokoto! Tukajivunia amani ya kweli ilikuwa imetamalaki nchi nzima hadi vifuani mwetu! Nje ya Azimio la Arusha tuna waheshimu wezi na mafisadi. Mungu atawalaani wote!

Nyerere alipong’atuka manyang’au wakalihujumu hata wakalifuta. Yeyote aliyeshiriki kuliua Azimio adhimu la Arusha, Jua la Mwenyezi Mungu limwakie na siku yake ya mwisho ikifika raha ya milele hataipata wala mwanga wa milele hautamwangazia!

Mwalimu alilia! Akiwa amesimama mbele ya mkungu uliokuwapo mbele ya nyumba yake alimtazama katibu mkuu ofisi ya rais, akageuza uso wake na kumwangalia kwa muda Waziri wa Nyumba na Maendeleo Mijini, Edward Lowassa, kisha akasema, “….na nyinyi wengine, mkilivunja Azimio la Arusha kabisa kabisa, mtakuja kupata taabu sana baadaye.”

Wakati huu ndiyo naelewa ni uchungu kiasi gani Mwalimu alikuwa nao moyoni mwake wakati akitamka maneno hayo! Aliiona Tanzania ya bila Azimio la Arusha! Aliwaona viongozi wetu wa bila Azimio la Arusha, kisha akaiona dhiki kuu itakayowashukia watu wake kwa kukosekana Azimio la Arusha! Akasema, “Mtakuja kupata taabu sana baadaye!”

Naye akisha kuyasema hayo aliondoka katika eneo la mkungu tulilokuwapo, akaingia ndani katika kiofisi chake cha pale nyumbani kwake, Msasani. Alikuwa mtu mzima lakini unamwona anaingia ndani akiwa amechoka kabisa si kwa uzee bali kwa kuwahurumia watu wake maskini ambao sasa nadhani aliwaona wamebaki yatima.

Baadhi ya watu waliitwa ndani wakaongee faragha na Mwalimu. Nami pia niliitwa. Mwalimu hakuwa na mengi ya kusema zaidi ya kulalamika tu, kitu ambacho kilinifanya nijue kuwa alikuwa anaumizwa sana na jinsi viongozi wa serikali walivyokuwa wakiongoza.

Naikumbuka siku ile kama vile ilikuwa jana. Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akitumia mkono wake wa kulia alimshika Edward Lowassa mkono wa kushoto maana walikuwa wamekaa sambamba, akamtamkia maneno mazito usoni mwake katika sentensi tatu! Maneno yale kutoka katika kinywa cha Mwalimu yaliniingia na kuninyong’oneza kabisa, utadhani nilikuwa naambiwa mimi!

Aliyoendelea kusema Mwalimu nilibaki nasikia tu lakini nilikuwa sielewi kitu tena mpaka tulipoondoka!

Ndugu Rais, acha mimi leo nilililie Azimio la Arusha! Siku nyingine Mwenyezi Mungu akipenda nitakwambia maneno ambayo Baba wa Taifa aliyomtamkia Edward Lowassa usoni pake!

Nayakumbuka maneno yale, nukta kwa mkato! Edward alimjibu Mwalimu kwa unyenyekevu mkubwa.

Nyakati zimepita na sasa zimetimia. Siku za majaribu zinawasonga Watanzania, wakumlilia hawamwoni.

Viongozi wetu ndio hawa wa kununua na kuuza uongozi. Mwalimu Nyerere aliwatabiria dhiki kuu watu wake baada ya yeye kuuondoka ulimwengu huu wa mateso!

Leo Watanzania wanaporwa kila kitu! Wamebaki kuchechemea kwa ugumu wa maisha huku viongozi wao na familia zao wakiwa katika ukwasi wa kutisha!

Wananchi wamefanywa kama kuku wa kienyeji. Wanaachwa wajilishe wenyewe, jioni warudi. Mpaka siku wanapotakiwa kuchinjwa ndipo wanatupiwa mtama kidogo! Kapelo, fulana, kanga na buku mpaka uchaguzi ujao!

Aliposikia viongozi wa Tanzania wanapokewa kwa shangwe duniani kwa uhodari wao wa kuuza ardhi, Mwanamwema Anney Anney alinitumia ujumbe uliosomeka: “Nilikaa Segerea miezi 5. Nikaendesha kesi mwaka mzima, nikashinda! Kisa nilisema Jakaya Mrisho Kikwete anauza ardhi yetu pamoja na utu wetu kwa Wazungu na Wahindi.

Leo (18-5-2012) BBC asubuhi wametangaza, Tanzania inaongoza kwa kasi ya kutisha kuuza ardhi kwa wageni katika ukanda wa Afrika Mashariki. Ni Mayega tu aliyenisemea nikiwa jela! Kosa langu lilikuwa ni nini?”

Mwanamwema Anney Anney endeleeni kuomboleza. Kilio cha wenye haki Mungu anasikia! Alisikia kilio chako ukiwa gerezani! Akasikia na sauti yetu tuliyomlilia, leo uko huru nao watesi wako wameandaliwa anguko la aibu!

Siku zimekaribia ambapo milango ya Magereza itafunguka na wote walioko nje bila kuwa na haki wataingia humo, nao wenye haki waliokuwa ndani watatoka, kwa maana mtetezi wetu yu hai!

Rais wangu, warudishie Watanzania Azimio lao la Arusha upate heri na miaka mingi hapa duniani. Nanyi wana wa nchi hii yawapasa kufahamu kuwa wakuwakomboa hakuna.

 Yawalazimu mjikomboe nyinyi wenyewe. Yeyote anayekuja kwetu kutaka kutuongoza aje na ahadi ya Azimio la Arusha.

Bila hivyo naye hatufai! Nchi yetu kwanza! Vyama vyote vya siasa na uzuri wa viongozi wake baadaye! Kuendelea kulialia tu na kulalamikalalamika bila

Azimio la Arusha katika nchi hii, ni sawa na kung’ang’ana kunyoosha kivuli cha mti uliopinda! Azimio la Arusha, ndiyo mwarobaini pekee uliobaki! Mwenyezi Mungu awabariki nyinyi wote!