Wednesday, September 11, 2013
Saturday, August 3, 2013
ENG, STELLA MANYANYA AMETHIBITISHA UONGOZI WAKE RUKWA
Na, Stephano Mango, Songea
SIKU za hivi karibuni nimebahatika kufuatilia mambo mawili huko Mkoani Rukwa ambayo leo nakusudia kuwajuza wasomaji wa andiko la Ukanda wa Uranium popote pale mlipo kwani naamini bila kueleza nitakuwa sijawatendekea haki wasomaji na wapenzi wa Viongozi ambao wanafanya vyema kwenye Serikali hii ya awamu ya nne
Mambo hayo ni uandikaji wa kitabu cha Sumbawanga Ng’ara na uanzishaji wa Makumbusho ya Mkoa wa Rukwa iliyopo ndani ya jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambaye kwa sasa ni Mhandisi Stella Martin Manyanya(MB)
Nimebahatika kutembelea Mkoa huo na kuona Makumbusho hayo pamoja na kukisoma kitabu hicho kizuri cha Sumbawanga Ng’ara ambacho kimeandikwa na Mkuu wa Mkoa huo
Licha ya mambo mazuri mengi ambayo yanapaswa kuelezwa kwa wananchi ili waweze kubadili mwenendo wao katika uendeshaji wa jamii zinazotuzunguka , leo mie nakusudia kueleza haya mawili ya kuhifadhi mazingira na kumbukumbu za maeneo yetu
Viongozi wengi nchini wanapenda kufanya vitu vya muda mfupi ambavyo vina maslahi kwao na havionekani kwenye jamii pana wala havishikiki na kusababisha kutokikidhi dhana ya Uongozi kwa maslahi ya Umma
Naamini kuwa sifa za kiongozi bora ni miongoni na kuwa kiongozi wa vitendo na sio madaraka, kuwa na uwezo wa kushawishi watu ili kufanikisha jambo bora kwa manufaa ya watu na kuleta matokeo yanayotarajiwa
Uongozi ni mchakato wa kujua njia, kuonyesha njia, kutembea katika njia hiyo ili kufikia lengo kusudiwa mahali na wakati husika, uongozi ni kipaji na taaluma, ingawa wahenga wanasema kuwa “Kiongozi mzuri ni yule asiyependa kuwa kiongozi , lakini kutokana na uzembe wa viongozi waliopo, anashawishika na kuamua kuwa kiongozi”
Licha ya kuwa uongozi ni utumishi lakini sio ubwana na pia uongozi ni vitendo na sio madaraka, hivyo uongozi unahitaji nia thabiti na moyo wa kujitolea kwa kutumia taaluma na kipaji ulichonacho
Na katika maisha ya binadamu miongoni mwa mambo muhimu ni utamaduni na mazingira ambayo yanamzunguka katika kuimarisha uhai wake, na ndio maana mie leo nakusudia kuzungumzia kitabu cha Sumbawanga Ng’ara na uanzishaji wa Makumbusho katika Mkoa wa Rukwa
Leo nakusudia kumpa ushindi wa kiuongozi Mhandisi Stella Martin Manyanya kuwa ni kiongozi ambaye ameweza kukidhi malengo ya yeye kuwa Mkuu wa Mkoa wa kwanza Mwanamke Mkoani Rukwa na hasa kwa mambo ambaye ameyafanya katika mkoa huo katika Nyanja zote
Ni mengi mno aliyoyafanya lakini kama nilivyosema kuwa kwa leo nayazungumzia hayo mawili na nikipata muda mwingine nitayazungumzia mengine ambayo nayo yanafaida kwa wananchi na mustakabali wan chi yetu
Mhandisi Manyanya amethubutu kuwa ni Mkuu wa Mkoa wa kwanza kuandika kitabu cha mazingira katika eneo lake na pia amekuwa wa kwanza kuanzisha Makumbusho katika Mkoa wake tangu wakuu wa mikoa wapya katika awamu zote mbili za Uongozi wa Rais Jakaya Kikwete walipoteuliwa
Katika hali ya kumpongeza Mkuu huyo Manyanya mzaliwa wa Mkoa wa Ruvuma, Wilaya mpya ya Nyasa katika Kata ya Kihagara nayazungumzia mambo hayo mawili aliyoyaasisi katika Mkoa wa Rukwa toka alipoteuliwa mwaka 2011 ambayo matokeo yake tumeyaona
Kitendo chake cha kuandika kitabu cha Sumbawanga Ng’ara kimefufua na kuanzisha moyo mpya wa uhifadhi mazingira kwa wadau mbalimba , pamoja na kupendesha mji kwani ukienda katika mitaa ya Sumbawanga usiku imekuwa kama mchana. Hii ni kutokana na ushirikishwajiu wa wadau mbalimbali katika uhifadhi wa mazingira kama vile Vodacom, Tigo, na wengine
Katika mambo yalioredheshwa kwenye cha Sumbawanga Ngara kwani uchafuzi uliopo unaoendana na kusambaa kwa taka ngumu umeleta athari kubwa kwa viumbe hai ikiwemo binadamu, wanyama wanyonyeshao na wasionyonyesha, wadudu ambao wengine ni muhimu katika maendeleo chanya ya ardhi,
Kuongezeka kwa mmomonyoko wa ardhi unaosababisha vina vya maji kupungua katika maziwa kama Rukwa na Tanganyika na kukauka kwa baadhi ya mito , Utiririshaji wa maji taka yenye viashiria vya sumu au sumu kamili vinavyotokana na mabaki ya bidhaa za viwandani zimekuwa na athari kwa viumbe hai waishio nchi kavu na majini na kusababisha kupungua kwa wanyama na baadhi ya aina za samaki, na wengine kubadilisha hata ladha yao ya asili.
Kwa ujumla wake uharibifu huo umechangia kwa kiwango kikubwa mabadiliko ya tabia nchi hususan, hali ya hewa katika baadhi ya maeneo, na hivyo kubadili uzuri wa asili na kupoteza baadhi ya vivutio.
Mfano ni kuhama kwa wanyama na ndege katika maeneo yao ya asili, kukauka kwa maporomoko ya maji na kadhalika.Uharibifu unaoendana na taka umesababisha miji ya maeneo ya Mkoa huo kuwa michafu na isiyovutia, milipuko ya magonjwa kama kuhara na kipindupindu, magonjwa ya ngozi kama upele, kudumaa kwaafya, kimsingi watu kuwa na afya hafifu na vifo. Matumizi ya dawa yamekuwa ya kiongezeka, gharama kubwa kwa ajili ya kutoa huduma za afya, kushuka kwa kipato kutokana na kupoteza nguvu kazi, au kuwa na nguvu kazi hafifu na kwa ujumla wake kuongezeka kwa umaskini uliokithiri hasa katika miji
Kitabu hicho ambacho kimezinduliwa na Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda (Mb kinatoa mwongozo wa kufanikisha Mpango wa Sumbawanga Ng’ara kwa faida ya watanzania wote nchini
Ni muhimu kukisoma na kukielewa kwa faida ya vizazi vilivyopo na vijacho kwani malengo yake ni kuona kuwa jamii ina ishi katika mazingira safi na salama , kwani hakuna maisha katika mazingira machafu na yenye viashiria vya hatari katika pumzi ya binadamu, leo ukifika Rukwa unakutana na mabadiliko mengi katika uhifadhi wa mazingira
Jambo jingine ambalo nimekusudia kulisema leo ni juhudi za Manyanya kuanzisha makumbusho katika Mkoa wa Rukwa Kwani Makumbusho ni sehemu ambayo watu wanaweza kujifunza namna ya uhifadhi bora wa mazingira kwa kuangalia watu wa kale walivyoweza kunufaika na mazingira yaliyowazunguka na mali asili zilizokuwepo kwa kupata dawa za miti shamba,chakula na vitoweo
Kupitia Makumbusho wananchi wanaweza kujifunza wajibu wao kwa nchi yao na jamii nzima inayowazunguka kwa kuangalia Mashujaa wa kale waliojitoa kwa moyo kupigana kwa ajili ya uhuru wa nchi,ulinzi na usalama wa mali zao
Uwepo wa Makumbusho ni jambo la kujivunia kwani yanaweza kutumika kujenga amani katika jamii ya watu wanaoishi kama ndugu na marafiki kwa kuangalia maisha ya watu wa kale walivyoishi kwa kushirikiana katika mambo yaliyokuwa yanawahusu wao na jamaa zao
Pia ni sehemu ambayo huwakutanisha watu wa mataifa mbalimbali wanaokuja kuzitembelea na kujifunza historia na tamaduni zetu hivyo kuifanya dunia kuwa mahali padogo kwani vitu wanavyojifunza hupelekwa nchi za mbali na kujulikana kwa watu wa mataifa mbalimbali
Nakufanya kuwa kiungo cha mabadiliko na maendeleo ya Taifa kwani kupitia Makumbusho watu wanaweza kujifunza umuhimu wa mabadiliko na umuhimu wa kila mmoja kujiletea maendeleo kwa kuangalia namna mwanadamu alivyopitia hatua mbalimbali za mabadiliko mpaka kufikia hatua tuliyopo hivi sasa
Kukuza amani na kuchangia kwa ufanisi zaidi katika kujenga amani Dunia, Makumbusho yanaweza kuandaa midahalo, kuonesha filamu, jitihada za utafiti, matembezi, mikutano ya amani na maonyesho ya utalii
Ni sehemu ambayo huvuta watalii,hukuza sayansi,hushangaza/kustaajabisha,kuelimisha,kuburudisha na hutia chachu ya uwajibikaji kwani ndani yake yana kumbukumbu zilizohifadhiwa hivyo makumbusho ni historia inayoishi
Uwepo wa Makumbusho ni wasaa wa kutafakari sisi wenyewe maisha yetu hivyo tunapaswa kuweka juhudi za kutunza makumbusho zilizopo na zinazoendelewa kujengwa
Suala la kutunza Makumbusho ni tete kulibinafsisha kwani linabeba utamaduni na utambulisho wa Taifa au jamii husika, hivyo zinawezwa kutunzwa na mtu binafsi kwa maendeleo yake, taasisi au Taifa lakini kuwepo kwenye taasisi ya umma ni kufanya uhai uendelee kuwepo
Mchango wa Tanzania kwenye tamaduni za nchi za Ulaya ni mdogo mno na hajulikani vyema, japo tumeshuhudia watu wa mataifa mbalimbali wamekuja kujifunza tamaduni, ingawa kila siku tunaendelea kutothamini utamaduni wetu kwa kuendelea kuiga tamaduni za nje bila sababu za msingi
Utamaduni wa jamii za Watanzania unastahili kukuzwa,kutangazwa na kusimamia ili nasi tuweze kuchangia utamaduni wetu kwenye mataifa mengine na ustaarabu wa ulimwengu, hivyo utambulisho binafsi na wa pamoja, kati ya kumbukumbu na historia
Makumbusho ni benki ya kumbukumbu licha ya kuwa ni sehemu ya kuelimishana na kuburudisha, pia makumbusho ni kumbukumbu ya fikra, kazi,maisha,mtazamo wa matukio ya watu mbalimbali, Viongozi na wananchi wengi leo, kuna kila kila sababu ya wananchi kutembelea na kuikuza Makumbusho yao kwa maslahi ya vijazi vilivyopo na vijavyo
Leo wakazi wengi wa Rukwa wanatembelea Makumbusho hayo kwa kasi kwani yamekuwa ya kwanza kuanzishwa katika mkoa huo licha ya kuwa ni Makumbusho ya kipekee katika mikoa yote nchini
Nimalizie makala yangu kwa kusema tunawajibika kuwaiga na kuwaenzi viongozi wenye nia ya dhati ya kusukuma guruduma la maisha ya jamii mbele, wakiwa hai au wakitangulia mbele ya mwenyezi Mungu
Mtazamo wangu na wako ndio unaotengeneza uhai wa Makumbusho na mazingira ya taifa letu, hivyo tuamue kuwa chombo cha mabadiliko kwa kuwaelimisha na kuwahamasisha umuhimu wa utamaduni, mazingira na makumbusho kwani utambulisho una uwezo mkubwa wa kuakisi maendeleo kusudiwa
Kama Mhandisi Stella Manyanya alivyomnukuu Mwandishi wa Marekani Hellen Keller alisema kwamba, “Peke yetu tunafanya machache, pamoja tunafanya mengi.” Tukijitoa sote kufanya kazi kwa bidii, ufahamu na maarifa hata yale yanayoonekana hayawezekani yatawezekana na hata yale yanayoonekana magumu yatakuwa mepesi
Maandishi haya yatuongezee nguvu ya kuanza safari yetu ya kuhakikisha kuwa Sumbawanga ina Ng’ara na Halmashauri nyingine za Rukwa zifuate na maeneo mengine nchini nayo yanapaswa kuiga kwa nguvu kubwa
Hakika siwezi kukuzuia kusoma maandishi yenye tija kwako, kwa maana ya kuwa siwezi kuzuia sikio lako kusikia lakini naweza kuzuia mdomo wako usiseme, nami kwa uhakika naweza kuzuia mkono wangu usiandike zaidi lakini siwezi kukuzuia wewe kusoma uthubutu wa kiuongozi wa Mhandisi Manyanya kwani ameonyesha njia na wengine wanapaswa kujipanga na kuonyesha uongozi tarajiwa kwa faida ya wananchi wanaowaongoza na Taifa kiujumla, na hakika uongozi hauna jinsi
Mwandishi wa Makala haya
Anapatikana, 0715-335051
Barua pepe;stephano12mango@yahoo.com
www.stephanomango.blogspot.com
Tuesday, July 30, 2013
DC NALICHO AWATIMUA WAVAMIZI MSITU WA SHAMBA LA BIBI
Na Steven Augustino, Tunduru
MWENYEKITI wa kamati ya Ulinzi ya Wilaya ya Tunduru, Mkuu wa Wilaya hiyo Mkoani Ruvuma Chande Nalicho ametoa wiki moja kwa Wakulima na Wafugaji wa jamii ya Kisukuma kuondoka katika eneo la hifadhi ya msitu wa Shamba la Bibi vinginevyo hatua kali za Kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Dc, Nalicho alitoa maagizo hayo baada ya kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo kufanya ziara ya kushtukiza katika msitu huo na kujionea hali halisi ya uhalibifu wa vyanzo vya maji, mabwawa na misitu iliyopo katika hifadhi hiyo inayo unganisha Vijiji vya Nangunguru, Majala na Mkalekawana katika Tarafa ya Nampungu kata ya Nandenbo Wilayani humo.
Alisema anatoa siku Saba kwa watu wote waliovamia msitu huo wa hifadhi kuondoka kwani haiwezekani watu waendelee kuishi wanavyo penda na kuharibu mazingira katika vyanzo vya maji na hifadhi ya misitu kana kwamba serikali haipo
Mkuu huyo aliwataka Watendaji Kata ,Vijiji kwa kushirikiana na Maafisa Tarafa Wilayani humo kutekeleza majukumu yao ikiwemo kuwaelekeza wafugaji kufuata taratibu za kuonana na viongozi wa Vijiji husika, kufanya mikutano inayo wahusisha wananchi katika maamuzi ya kuwapokea wafugaji hao ili kuyaondoa maeneo yao katika migogoro ya aina hiyo.
“Kwavile mifugo ni muhimu kwetu na endapo itatumika vizuri na kwa kuzingatia kanuni, miongozo na maelekezo yanayotolewa na Serikali italeta manufaa kwa Wananchi wetu” alisema Dc, Nalicho na kuongeza kuwa mtindo wa kuishi kwa uhasama kati ya wafugaji na wakulima hauwezi kuwa na tija.
Awali akiongea katika ziara hiyo Afisa misitu wa Wilaya la Tunduru Rashid Mtotela alimweleza Dc, Nalicho kuwa Wakulima na wafugaji hao walivamia msitu huo mwaka 2006 /2007 na kuendelea kujiimarisha kila mwaka baada ya kubaini kutokuwepo kwa vikwazo vyovyote kutoka Serikalini.
Alisema hifadhi hiyo ambayo awali ilikuwa imeunganishwa na Hifadhi ya Taifa (Selous) tangu mwaka 1974 na baadae kuunda hifadhi shirikishi mwaka 2007 kupitia mradi wa Jont participatory Forest Menegement (JPFM) liyounganisha Vijiji vya Nangunguru, Mkalekawana na Majala kila Kijiji kimekuwa kikikwepa majukumu yake ya kulinda hifadhi hiyo hali ambayo imechangia kuendelea kuhalibika kwa mazingira hayo.
Wakiongea kwaniaba ya Wananchi wa Vijiji hivyo Mwenyekiti wa Kijiji cha Nangunguru Bw.Said Rashid Mkwekwele, Mtendaji wa Kijiji hicho Zainabu Twaha na Afisa Tarafa wa Nampungu Joshua John wakawashushia lawama baadhi ya wakuu wa Idara katika halmashauri ya Wilaya hiyo kuwa umekuwa na kigugumizi katika ufuatiliaji na uchukuzi wa maamuzi juu ya migogoro hiyo.

Friday, July 26, 2013
WAFANYABIASHARA SOKO KUU SONGEA WAPINGA MPANGO WA MANISPAA
Na Stephano Mango, Songea
WAFANYABIASHARA katika Soko Kuu la Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wamepinga ongezeko la pango kwa asilimia 100 na tangazo la Zabuni la ukodishaji wa Vibanda hivyo lililotolewa na Halmashauri hiyo hivi karibuni
Akitoa maazimio ya kikao cha Umoja wa Wafanyabiashara Masoko ya Manispaa ya Songea(UWABIMASO) kilichofanyika jana mjini hapa kwenye ukumbi wa Saccos ya Walimu Songea Vijijini Mwenyekiti wa Uwabimaso Karim Matumla alisema kuwa wafanyabiashara wamepinga kwa nguvu zote mpango wa kifisadi ulioletwa na viongozi wabovu wa Halmashauri hiyo wa kuongeza kiwango cha kodi kwa asilimia 100 na tangazo la Zabuni
Matumla alisema kuwa mipango ya Halmashauri kuhusu Masoko yake haina ushirikishwaji wa pamoja kutoka pande zote mbili kwa maana Wafanyabiashara(Uwabimaso) na Halmashauri hiyo hali inayosababisha migogoro mara kwa mara
Alisema kuwa kwa muda mfupi tumepokea barua mbili zenye malengo tofauti ndani ya kipindi cha mwezi mmoja jambo ambalo linaleta mashaka sana katika dhamira za viongozi wa Halmashauri hiyo yenye mipango dhalimu
Alisema kuwa kitendo cha Mkurugenzi kutoheshimu wala kutimiza makubaliano yetu yaliyomtaka kuondoa kero zinazowapata wafanyabiashara katika Masoko ya Halmashauri ni kitendo cha dharau kwa wafanyabiashara ambao wanachangia pato la Halmashauri
“ Tulimtaka Mkurugenzi katika vikao vyetu kuondoa mashimo na kuboresha mifereji na miundombinu mingine ndani ya Masoko, wauza matunda watafutiwe eneo maalumu la biashara yao kwani kwa sasa wanazuia mizigo kuingia ndani na wateja wanapata kero ya kuhudumiwa, unyanyasaji unaofanywa na Afisa Masoko uachwe na pia tulimuomba atukutanishe na Viongozi wa Halmashauri ili tutoe maoni yetu, lakini yeye amekaidi”alisema Matumla
Alisema kuwa mei 22 mwaka huu Halmashauri ilileta barua Uwabimaso ikitoa taarifa ya ongezeko la kodi ya pango kwa asilimia 80 kulingana na ukubwa wa chumba cha biashara kuanzia julai 1 mwaka huu, kabla hatujaanza kuitekeleza, julai 9 mwaka huu wanaleta barua na wanatangaza Zabuni ya ukodishaji wa vibanda hivyo, baada ya Uwabimaso kupinga ongezeko la pango la asilimia 80
Alieleza kuwa kumekuwepo na mgongano wa kimaagizo kutoka katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kitendo ambacho kinaibua maswali mengi, hivyo Uwabimaso imeamua kwenda kwa Mwanasheria ili aweke zuio la mpango wa upandishaji wa Kodi na Utangazaji wa Zabuni yenye lengo la kuwaondoa wafanyabiashara wote wa maduka katika soko hilo
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Zakaria Nachoa alisema kuwa Halmashauri imekusudia kuongeza mapato yake kupitia miradi yake, hivyo mfanyabiashara ambaye hataki kuendana na utaratibu aache kibanda ili mfanyabiashara mwingine achukue
MWISHO
Saturday, July 6, 2013
AMINA CHIFUPA HUYU HAPA, AWASUMBUA VIJANA
AMINA CHIFUPA AKIWA KATIKA POZI ENZI ZA UHAI WAKE
Na; Stephano Mango, Songea
JUNI 26 mwaka 2007 Tanzania hususani jamii ya vijana ilikumbwa na msiba mzito wa kuondokewa na Mwanaharakati wa Vijana,mpendwa wetu Amina Chifupa Mpakanjia.
Hadi anafariki dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi katika hospitari ya Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) ya Lugalo alikokuwa amelazwa akiugua homa kali na kisukali alikuwa ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia tiketi ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UV-CCM)
Amina Chifupa amefariki akiwa na umri wa miaka 26 ya kuzaliwa kwake, tarehe aliyofariki ni siku ya upingaji wa madawa ya kulevya Dunia ambayo yeye ndie alikuwa miongoni mwa Vijana ambao wanapinga matumizi ya madawa hayo
Kimsingi msiba ule ulikuwa ni pigo kubwa sana kwa wanajamii wote na hasa vijana tulio katika mapambano ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazotukabili katika maisha yetu.
Mazishi ya mwanadada huyo chipukizi na jasiri katika kuwakomboa Vijana na makundi mengine yaliyopembezoni yalifanyika katika kijiji cha Lupembe,wilayani Njombe katika mkoa wa Iringa zamani.
Katika maombolezo ya Mbunge huyo ilithibitika pasipo na shaka hata chembe kwamba alikuwa anakubalika na watu wengi na ni mtu wa watu ,na kwa kweli ujasiri aliouonyesha katika kipindi kifupi alichofanya kazi akiwa Mbunge,kilithibitisha kuwa jamii ilimkubali.
Pamoja na umri wake mdogo (26) akiwa Mbunge wa Viti Maalum na aliyekaa Bungeni kwa kipindi cha miezi kumi na nane (18),habari za msiba wake na namna watu walivyouomboleza ni mambo yaliyoonyesha dhahiri njia bora inayowafaa wabunge na viongozi wetu kutimiza wajibu wao
Kujitokeza kwa watu wenye hadhi ya juu kabisa kitaifa na kimataifa katika mazishi yake na wingi wa wananchi wa kada mbalimbali nyumbani kwa baba yake Mikocheni na huko Njombe ambako yalifanyika mazishi yake, ni ushahidi unatuonesha kuwa dada huyu alikuwa mpiganaji wa kweli katika mambo mazito ambapo kifo chake kilipaswa kuguswa na wengi hususani vijana.
Ingawa imekuwa ni desturi kwetu kuwaenzi watu waliokufa hata wakati mwingine kwa wale ambao hawastahili sifa tunazowapa, lakini kwa Amina hali hiyo ni tofauti kabisa, kwani kila sifa ambayo amekuwa akipewa imekuwa ni sehemu ya mambo ya msingi aliyoyafanya na wananchi wakasikia au kushuhudia kwa macho yao
Hakika kifo cha Amina Chifupa kiliibua mambo mengi sana , wapo waliohusisha kifo chake na siasa kwa kuwa alitamani kuwa kiongozi wa juu katika umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UV-CCM).
Wapo waliofananisha kifo chake na cha Horace Kolimba ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa CCM ambapo aliwaambia wenzake waziwazi kuwa “CCM haina dira wala mwelekeo” lakini hawakumwelewa, na wakamwita Dodoma ajieleze kwenye kikao maalumu, alipowapatia maelezo, ghafla tukasikia Kolimba amefariki dunia.
Wengine walithubutu kukifananisha kifo cha Amina Chifupa na cha Ipyana Malecele ambaye alikuwa ni mtoto wa kiongozi na Mbunge mkongwe hapa nchini John Malecele.
Ingawa mzee Malecele na mwenzake Hamis Chifupa walikana waziwazi kuwatuhumu Binadamu wenzetu kwamba ndio waliofanya vitendo vya kigaidi na kijasusi na kusababisha vifo kwa vijana hao
Ni katika mazingira tofauti walitoa kauli zao na kuwaasa watanzania waamini kuwa vifo hivyo vilitokana na mipango ya Mungu na kuwaomba watanzania wasihusishe vifo vya watoto wao na harakati za kisiasa.
Hata hivyo wapo waliohusisha kifo hicho na harakati zake za kupinga na kutaka kuwataja hadharani wauzaji na vigogo wa madawa ya kulevya hapa nchini, ndiyo maana wakasema kwa kuwa alihaidi kuwataja vigogo hao siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani ambapo kimsingi inaadhimishwa Duniani kote Juni 26 ndiyo maana wakawahi kumwondoa mapema kabla hajasema kitu siku husika.
Lakini kuna baadhi ya watu wamefananisha kifo chake na cha Princess Diana wa Uingereza. Kwa sababu Diana alikufa katika umri mdogo wa miaka 36 na alipendwa na watu wengi na wenye nyadhifa mbalimbali
Diana na Amina maisha yao yalikatishwa ghafla na kuwaacha watu wakiwahitaji katika kuchangia maendeleo katika jamii zao na kutufanya tudondoshe machozi katika kuwaomboleza.
Hata hivyo watanzania wasingeweza kufanya makosa pale wanafananisha kifo cha Amina na cha Ipyana, kijana mdogo ambaye kama alivyokuwa Amina alikuwa ameanza harakati za kuwania uongozi wa juu ndani ya UVCCM, wote wawili walikutwa na janga na baadaye walipotea katika mazingira yenye utata na kigugumizi wakiwa wanahitajika katika harakati husika.
Lakini kimsingi katika kumkumbuka Amina chifupa tunapaswa kutambua kuwa kila nafsi katika ulimwengu huu itaonja mauti, ingawa kila mja kabla hajaumbwa, mwenyezi mungu alimjua na kumtaka atimize wajibu wake kama kiumbe hai.
Natambua na kuamini kila mtu ana sababu zake za kuumbwa na kuwekwa katika ulimwengu na ana wajibu stahiki ambao amelazimika kuja kuutimiza hapa Duniani.
Hii haimaanishi kila mmoja wetu kutimiza wajibu wake kikamilifu, ingawa wajibu huo tumepewa na muumba wetu kuja kuutimiza kwa kutumia utashi wetu ulio kamilifu.
Kwa muda mfupi alioishi Amina Chifupa alipokuwa Bungeni amedhihirisha jinsi alivyotimiza wajibu wake, ameweza kuwa chachu kwa kuibua mambo mazito ambayo yalitoa cheche kali na kuzua mijadala mikali ndani na nje ya Bunge la tisa.
Akiwa kijana mtanzania na kwa kuzingatia majukumu yake aliweza kutimiza wajibu wake ipasavyo kama Mbunge na Mwakilishi wa Vijana, ni ukweli uliowazi kuwa tunapaswa kuziendeleza juhudi alizoziacha .
Naamini alipokuwa Bungeni hoja alizoibua na jinsi zilivyokuwa na hamasa na kuweza kufufua matumaini ya wengi na kukuza hadhi ya vijana wenye nia ya dhati katika kupigania nchi yao , ndiyo kilichonifanya niendelee kumkumbuka na kumuenzi daima leo akiwa ametimiza miaka 6 toka atutoke
Hicho ndicho haswa kilichofanya kifo chake kumshtua kila mtu bila kujali rika awe aliyekuwa anamfahamu vizuri marehemu aula. Kwa sababu ni miongoni mwa waheshimiwa waliokuwa na nia thabiti ya kurejesha hadhi ya Bunge na kufanya litimize wajibu wake.
Kwani alitambua kuwa cheo ni dhamana na kwamba uheshimiwa aliopewa ulikuwa unamaanisha utumishi kwa wananchi na kuzingatia kundi alilopaswa kulitumikia kikamilifu ambalo ndilo lililompa dhamana (Vijana).
Kwa nguvu zake zote aliamua kutoa mchango wake ili kuwezesha vita dhidi ya madawa ya kulevya ishinde, kwa kuwa madawa ya kulevya yanaangamiza vijana wengi wa nchi hii ambao yeye alikuwa na wajibu wa moja kwa moja wa kuwatetea.
Sina hakika kama kuna mtanzania mwenye akili timamu anaweza kubisha kwamba Amina Chifupa alikuwa nuru ya matumaini kwa vijana na harakati zetu za kujiletea maendeleo.
Ni ukweli kuwa Taifa lolote Duniani haliwezi kuwa imara kiuchumi ,kisiasa, kiutamaduni na kijamii katika mapambano dhidi ya umaskini, ujinga na maradhi bila kundi kubwa la vijana kulitengenezea mazingara ya kujikomboa.
Katika ulimwengu asilimia kubwa ni vijana na ndio viongozi wa leo na kesho na nguvu yao inategemewa sana katika jamii zetu.
Ndio maana mwanaharakati wa Vijana marehemu Amina Chifupa alijikita zaidi katika kutukomboa katika changamoto mbalimbali zinazotukabili ili atuoneshe njia stahiki na katika ustawi imara.
Hakuna ubishi kuwa Vijana ndio tumaini pekee la Taifa letu, kwaniTaifa lisilokuwa na vijana wazalendo na walio tayari kutetea taifa lao kwa gharama yoyote. basi nashawishika kuamini taifa hilo limepoteza mwelekeo (dira) na lipo hatarini.
Katika harakati za kuwakomboa Vijana na kupinga maovu naamini Amina Chifupa amekufa kifo cha kishujaa na ametutangulia mbele ya haki baada ya kutimiza baadhi ya wajibu wake
Mashujaa wapo wengi ambao wameshafariki ila kimsingi kila shujaa ameondoka akiwa na sifa zilizomfanya atambulike na aheshimike katika jamii iliyokuwa inamzunguka.
Mara nyingi shujaa hufikia hatua hiyo kutokana na ujasiri wake, uwezo wa kufikiri, kubuni,busara na pengine kujitoa kafara katika kuokoa watu wengine ambao kimsingi wamepotea
Ushujaa haupatikani kirahisi, mara nyingi mtu ambaye anaveshwa cheo cha ushujaa ni lazima akumbwe na vizingiti vingi (Maadui)ili afikie lengo husika la ukombozi na zawadi
Mwanaharakati Amina Chifupa alipata mapito magumu sana kimaisha katika safari yake hapa duniani na uwanaharakati wake kiujumla..Ingawa kifo chake kimeacha gumzo kubwa katika fikra za vijana.
Mwanaharakati huyu alikuwa tayari kufa akiongozwa na nanga ya kijasiri ya kusema ukweli na uwekaji wa mambo mengi bayana kwa kuipenda nchi yake na hasa jamii ya Vijana kwa kuyavalia njuga mambo mazito ambayo kimsingi yanaharibu maisha ya vijana.
Alitumia muda mfupi ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuonyesha uwezo na ujasiri mkubwa, kuwa Vijana wa leo wakipewa majukumu mazito wanaweza kufanya vizuri na wanastahili kupata dhamana hiyo.
Ni dhahiri kuwa Amina ni shujaa kwa kuwa kifo chake ni kielelezo kwa Vijana kuwa wakati wote tupo tayari kufa kwa ajili ya kutetea nchi yetu na kupambana na ufisadi ambao unalenga kuipeleka nchi mahali pabaya na kuharibu malengo ya vijana na Taifa kiujumla
Ni wazi kuwa katika harakati za Amina Chifupa za kusema na kudhamiria kufichua maovu alikuwa akizungukwa na maadui wa ndani na nje na pengine wengi ni wale wa nchi za nje ambao nia yao kuitumia nchi hii kama dampo la kuzalisha vijana matahira kutokana na Dawa za kulevya.
Maadui hao nia yao ni kuhakikisha kizazi chote cha Vijana kama Amina Chifupa kinaathirika na dawa za kulevya ili nchi hii iweze kutawaliwa kirahisi baada ya kuziharibu bongo zote za Vijana makini na wasomi ambao wanashawishika kutumia dawa za kulevya.
Jambo muhimu kwa sasa ni wajibu wa kuiga na kuendeleza mapambano dhidi ya dhuruma na masuala yote aliyopigania Mwanasiasa huyu, viongozi wetu wanao wajibu wa kutumia fikra za Amina kwa kuwa bado zinaishi kusahihisha makosa wanayofanya ambayo wamekuwa wakiambiwa mara kadhaa na makundi mbalimbali ya jamii lakini kwa makusudi wanayapuuza.
Uwakilishi wa Amina Chifupa haukuishia kuchangia mijadala Bungeni tu, bali tulimsikia na kumwona akifanya shughuli nyingine mbalimbali za kijamii,kwani aliwatembelea vijana na watoto wenye matatizo mbalimbali na kuwafariji na kuwapa misaada mbalimbali
Hivyo Vijana ndio tunatakiwa kuwa mstari wa mbele kwa kumuenzi Amina Chifupa na kuhakikisha kuwa Nchi hii haiendi mrama, ni vyema tukadhihirisha kumuenzi Amina Chifupa kwa vitendo vyetu, kwa kuwa tumeachiwa changamoto nyingi tunapaswa kuzitatua na kuweka mambo sawa katika harakati zetu za kujikomboa
Pamoja na kumkumbuka Amina ni vyema Vijana na wanajamii tukajiuliza tumejifunza nini kutoka kwake? Nani mtetezi wa Vijana aliyebaki Bungeni? Ni Zitto Kabwe, Dk Emmanuel Nchimbi , Deo Filikunjombe, Livingston Lusinde, Joshua Nassari, John Mnyika, Ester Bulaya au Waziri Mwenye dhamana ya Vijana?
Ni kweli kuwa Amina Chifupa hatunae tena katika ulimwengu huu, amefariki dunia, amelala na hatutamwona tena katika maisha haya ,lakini kauli na fikra zake zipo na zitaishi milele na itakuwa pumzi katika kizazi hiki na kijacho.
Amina tunakukumbuka na kukuenzi kwa yale yote uliyotuachia na tutashirikiana vyema na Mzee Hamis Chifupa kutoa mchango wetu katika taasisi yako ya Amina Chifupa Foundation ambayo ipo chini ya Mkurungezi Mzee Hamis Chifupa na ni jambo jema kuwa taasisi yako tayari imesajiriwa na Serikali na enaendelea kutimiza wajibu wake wa kusajiriwa
Kama mwenyezi mungu alivyotoa ndivyo alivyotwaa, Vijana sote tulikupenda na tutaendeleza juhudi zako ulizoziacha , sisi kama waja hatuna budi kumshukuru kwa kila jambo Mwenyezi mungu atupe faraja na busara katika kukabiliana na changamoto zinazotukabili watanzania wote.
Mheshimiwa Amina Chifupa uiombee nchi yako ili mafisadi wasiendele kuwaua kila kukicha eti kwa sababu za harakati ambazo wewe uliziasisi na watanzania wengine wasio na hatia ambao wanakosa Raslimali stahiki kwa sababu mafisadi wamezimaliza maliasili hizo kwa kuibia. Tunatambua kuwa wewe mbele sisi nyuma. Mungu Baba aipumzishe Roho yako katika mahali pa faraja na amani , Ameni.
Mwandishi wa Makala hii
Anapatikana kwenye, www.stephanomango.blogspot.com
Simu namba,0755 -0715 -0784 ,33 50 51
Friday, July 5, 2013
LOWASSA ADAIWA KUCHEZA KALATA VIZURI KASHFA YA RISHMOND
Aliyekuwa kuwa Waziro Mkuu, Edward Lowassa akiteta jambo na aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa Samwel Sitta
WAZIRI Mkuu aliyejihudhuru Edward Lowassa mwaka 2006 kwa tuhuma za ufisadi kupitia kampuni ya kufua umeme Richmoind, sasa imebainika kuwa alitolewa mbuzi wa kafara baada ya mitambo hiyo kuzinduliwa na Rais wa Marekani Barck Obama ikiwa na jina la Symbion.
Kwanza waliosuka mpango wa kumchafua Lowassa walisema Richmond ni Kampuni ya mfukoni, na ni ya Lowassa, haina uwezo wa kuzalisha Umeme wala kufunga balbu.
Wakasema Dowans ni pacha na Richmond, Wapambe wachache wakasema Serikali isinunue Mitambo hiyo maana haifai, sasa ni Simbyon Power.
Mitambo hiyo hiyo ndiyo imezinduliwa juzi na Obama, je?amezindua mitambo mibovu isio na uwezo wa kuzalisha Umeme wala kufunga balbu? je Obama naye ni fisadi? au kwasababu akina fulani wakisema ndimi zao zinaaminika zaidi ya wengine?
Wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema kuwa Lowassa alikuwa anaona mbali sana na alikuwa sahihi, ila alihujumiwa kisiasa tu na wasioitakia Nchi yetu mema bali kwa maslahi yao maana mitambo hiyo wakati inazinduliwa mpaka Rais Jakaya Kikwete na vionmgozi wengine wa nchi walionekana wakipiga makofi!
Thursday, July 4, 2013
MAMBO 10 YA MUHTASARI WA ZIARA YA RAIS OBAMA BARANI AFRIKA
Ametusemea Waafrika wote. Hasa katika swala la kujenga viwanda hapa hapa Afrika ambavyo vitatoa ajira kwa vijana wetu. Africa tusikubali kudanganywa kwa kuuza malighafi kwenda nje na kuhamishia ajira nchi za nje.
Amekemea sana swala la uongozi mbaya, rushwa, upendeleo katika swala la ajira kuwa vinakwamisha maendeleo Afrika.
Yeye na Rais wa Afrika Kusini, wamezungumzia swala la ICC na Afrika. Walisema kama Afrika inafikira kuwa ICC inaionea, ni bora Afrika izungumze na ICC. Lakini Rais Obama alitoa angalizo kwa viongozi wa Afrika kwa makini na madai yao ndani ya ICC.
Hapa Afrika kusini, alizungumzia swala la uchafuzi wa anga na hatua ambazo Marekani inachukuwa kupungaza hatari hiyo. Pia alielezea hatua ambazo China, India na Japan wanachukuwa. Alishauri kila mtu, watu na nchi wote tuhusike na swala hii la uchafuzi wa anga na maeneo tunayo ishi.
Alizungumzia, idadi ya wanafunzi darasani. Alisikitika kusikia kuwa darasa moja Afrika lina wanafuzi 90, ambapo Marekani dalasa moja lina wanafunzi 25 hadi 35 ambao bado waonaona ni wengi. Alishauri kuwepo utalaamu wa kisasa wa kufundishia darasa vikundi vikundi.
Aliwapa changamoto vijana wote wa Afrika ya kusoma sana hasa masomo ya hesabu na ufundi, kuwa tayari kwa ajira za viwandani. Aliahidi kuwapa msaada wa elimu kwa swala hili.
Aliwaambia vijana kuwa tayari kuwania nafasi za juu serikalini na kuwajibisha serekali zao kwa njia za amani.
Alikanusha uvumi uliopo kuwa anataka kuweka kituo cha Jeshi Africa. Pia safari ya Afrika hakusababishwa na uhusiano wa China-Afrika.
Amesema Afrika itajengwa na Waafrika kwa faida ya Afrika wote, ila wao wako tayari kuchangia mawazo, utalaamu na soko.
Aliwajibu Wakenya kuwa ahadi ya kuwatembelea bado ipo pale pale, maana bado ana miaka 3 na miezi 6 ofisini.
Ahsante.
Samuel G Mossama
Pretoria
+27 782 372 288
Sunday, June 30, 2013
SANGA ONE AHUDHURIA KILELE CHA MASHINDANO YA ANSIGAR CUP PERAMIHO NA ANATARAJIA KUYAFUNGA LEO
Viongozi mbalimbali wakiimba wimbo wa Taifa ulioimbwa katika Mashindano hayo, wakwanza kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa FARU, Golden Sanga, wa pili Mfadhiri wa mashindano hayo kwa niaba ya Dkt Ansigary Stuffe, na watatu ni Mwandishi Mahili wa Michezo katika Redio ya Jogoo Onesmo Emeran
Miongoni mwa Timu shiriki ikiwajibika kuimba wimbo wa Taifa kabla ya kufunga mashindano hayo
Mr Kolumbani Lugendo ambaye ni Msimamizi wa MECHI aliyeonyesha mkono akimpa maelekezo ya awali Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa FARU Golden Sanga mwenye tai kabla hajazikagua timu shindani, wa kwanza kulia ni Katibu wa Mashindano Sixbert Komba, wa kwanza kulia ni Katibu wa SORUFA Iddfonsi Luoga, nyuma kabisa ni Ayubu Mvulla ambaye ni Mwenyekiti wa Mashindano hayo
Katika Fainali hiyo ya Ansigary Cup ambaye imefanyika mbele ya Mgeni Rasmi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Ruvuma Golden Sanga (SANGA ONE) Timu mbili zilichezwa katika Uwanja wa Ansigary hapa PERAMIHO na kuhudhuriwa na mamia ya wapenzi na mashabiki wa timu hizo
Fainali hiyo iliwakutanisha Kilangano B 9 wenye pointi na Litisha yenye pointi 6
Mashindano hayo yalianza kwenye ngazi ya Tarafa April 21 mwaka huu na kuzinduliwa rasmi na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimike na kuhitimishwa Juni 30 mwaka huu na Mwenyekiti Golden Sanga
Habari kamili za mashindano hayo zitaendelea kukujia kupitia Mtandao huu wa www.stephanomango.blogspot.com
Miongoni mwa Timu shiriki ikiwajibika kuimba wimbo wa Taifa kabla ya kufunga mashindano hayo
Mr Kolumbani Lugendo ambaye ni Msimamizi wa MECHI aliyeonyesha mkono akimpa maelekezo ya awali Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa FARU Golden Sanga mwenye tai kabla hajazikagua timu shindani, wa kwanza kulia ni Katibu wa Mashindano Sixbert Komba, wa kwanza kulia ni Katibu wa SORUFA Iddfonsi Luoga, nyuma kabisa ni Ayubu Mvulla ambaye ni Mwenyekiti wa Mashindano hayo
Mwenyekiti wa Faru Golden Sanga akiendelea kuzisalimia na kuzikagua timu kabla hazijaanza mashindano hayo
Fainali hiyo iliwakutanisha Kilangano B 9 wenye pointi na Litisha yenye pointi 6
Mashindano hayo yalianza kwenye ngazi ya Tarafa April 21 mwaka huu na kuzinduliwa rasmi na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimike na kuhitimishwa Juni 30 mwaka huu na Mwenyekiti Golden Sanga
Habari kamili za mashindano hayo zitaendelea kukujia kupitia Mtandao huu wa www.stephanomango.blogspot.com
Monday, June 24, 2013
MBUNGENI WA CCM AHOFIA TANZANIA KUWA NA RAIS "SHOGA"
Ali Keissy (CCM), MBUNGE wa Nkasi Kaskazini
Na, Mwandishi Wetu, Dodoma
MBUNGE wa Nkasi Kaskazini, Ali Keissy (CCM), amesema kuwa bila Watanzania kuwa makini na sheria mpya ya ndoa ijayo, huenda nchi ikapata rais, wabunge na madiwani wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja (mashoga).
Keissy alitoa kauli hiyo wakati akichangia mada katika mkutano wa siku tatu wa Chama cha Wabunge cha Kupambana na Ukimwi (TAPAC) uliomalizika jana mjini Dodoma.
Mbunge huyo aliwaomba viongozi wa dini kukemea kwa nguvu vitendo hivyo, pia alipinga hatua ya wazazi kuwapeleka watoto wao wadogo shule za bweni akidai kuwa huko ndiko wanakojifunza vitendo hivyo.
“Mnashindwa kulea watoto wenu, mnawapeleka shule za bweni wakiwa na miaka mitatu ili walelewe kizungu. Huko watapakwa mafuta ya KY na wataingiliwa,” alisema.
Keissy alitolea mfano mkutano mmoja uliofanyika jijini Dar es Salaam kuwa uliwashirikisha mashoga 400, jambo alilodai ni ishara kwamba wanaojihusisha na vitendo hivyo wanaongezeka, na hivyo kuitaka serikali kuwapiga marufuku.
Hata hivyo, baada ya mbunge huyo kuhitimisha mchango wake, mmoja wa vijana wanaojihusisha na mapenzi hayo ya jinsia moja, Abdilah Ally ambaye alikuwa amealikwa na TAPAC, alitetea kuwa jamii inapaswa kukubali kwamba matendo hayo yanafanyika.
“Tunatambua kuwa sheria haziruhusu vitendo hivi, lakini vipo na vinafanyika na tunapata maambukizi kwa kiwango kikubwa. Tunachokitaka tusinyanyapaliwe na jamii, bali tupewe huduma ya afya ya kujikinga na maambukizi.
“Mathalani mimi hapa nina wapenzi wanaume watatu ambao nashiriki nao mapenzi, sasa kama nimeathirika ina maana wote wale nao wamethirika,” alisema.
Akifunga mkutano huo, Naibu Waziri wa Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu, aliwasihi wanasiasa wasiwabague makundi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya ushoga, usagaji na matumizi ya dawa za kulevya.
Alisema kuwa makundi hayo yanakabiliwa na janga la maambukizi makubwa ya virusi vya ukimwi, hivyo wanahitaji kusaidiwa kuondoka katika makundi hayo badala ya kuwahukumu.
Mwalimu alifafanua kuwa miongoni mwa washiriki wa mkutano huo kutoka katika makundi hayo, alikuwa mtumiaji wa dawa za kulevya, lakini baada ya kupata msaada wa kiafya ameachana na vitendo hivyo na sasa anaendelea vizuri chini ya uangalizi.
Mkutano huo uliratibiwa na Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), kama wadau wakuu waliotoa mada mbalimbali kuhusu jinsi wanavyopambana kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi.
Katika hilo, Mwalimu alisema kuwa serikali dhamira yake ni kufikia maambukizi asilimia sifuri, hasa kwa kutoa msukumo mkubwa kwa makundi ya wanawake, vijana na watoto ambayo yana maambukizi zaidi.
Mbunge wa Chambani visiwani Zanzibar, Yusuf Salam Hussein (CUF), alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefanikiwa kupunguza maambukizi hayo kwa wanandoa kutokana na sheria ya kuwataka wapime ukimwi kabla ya kufunga ndoa.
CHANZO: TANZANIA DAIMA
TGNP WAFUNGA MITAMBO YA KISASA MOROGORO
Afisa Habari na Mawasiliano wa TGNP Lilian Kittunga akifundisha Program Maalum ya Kutumia mawasiliano miongoni mwa Vikundi vya Sauti ya Jamii Kituo cha Taarifa na Maarifa
Na, Mwandishi Wetu, Morogoro
MTANDAO wa Jinsia nchini (TGNP), umepanua mawasiliano kwa kutoa na kufunga mitambo ya kisasa ya mawasiliano kwenye vituo vya taarifa na maarifa ya jamii chini ya wanaharakati wa maendeleo katika mikoa mitano nchini.
Hayo yamebainishwa mwishoni mwa wiki wilayani Morogoro na Ofisa Programu ya Utetezi na Mawasiliano na Habari TGNP, Deogratius Temba wakati akikabidhi mtambo wa aina hiyo kwenye kituo cha wanaharakati Mkabarani.
Alisema dhamira ya wananchi kuwezeshwa mtambo huo ni kuzinduliwa mradi wa ‘Sauti ya Jamii’ ambapo hapo utaitwa 'Sauti ya Jamii Mkambarani', ili kuongeza nguvu ya pamoja katika mapambano ya mabadiliko chanya ya maendeleo kwa kuhabarishana.
“Kuanzishwa kwa ‘Sauti ya Jamii’ na kutolewa kwa mtambo huu ni matokeo ya changamoto zilizojitokeza kwenye matamasha na mafunzo yaliyotolewa kwa jamii na TGNP hivi karibuni,” alisema Temba.
Alisema malengo ya kituo ni kumwezesha mwanawake na jamii kujikwamua kifikra, kiuchumi, kisiasa na kumharakishia maendeleo kutoka katika mfumo dume unaomzunguka.
Akitoa nasaha juu ya uanaharakati bora, Diwani wa Kata ya Mkambarani, Daniel Shawa, aliwataka wanaharakati kufuata sheria, taratibu na kanuni zilizopo ili waheshimike na kuthaminiwa katika jamii wanayoitetea.
Mtambo huo ulioambatana na vifaa vya teknolojia ya kisasa ikiwemo kompyuta, ‘printer’ na chombo cha kuhifadhia vimetolewa Mkambarani wilayani Morogoro, Kisarawe mkoani Pwani, Kishapu mkoani Shinyanga, Songea na jijini Dar es Salaam.

Saturday, June 22, 2013
OFISI YA CCM YANUSURIKA KUCHOMWA MOTO KATIKA VURUGU ZA MADIWANI
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho
Na Stephano Mango, Songea.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Ruvuma kimelazimika kusitisha uchaguzi wa kura za maoni wa kumpata Mgombea Uenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Mbinga baada ya baadhi ya Madiwani kuilalamikia Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Ruvuma ambayo inadaiwa kuwa ilishinikizwa na kigogo mmoja wa CCM kukata jina la mmoja kati ya Madiwani walioomba kugombea nafasi hiyo na kusababisha kuwepo vurugu kubwa za kisiasa ambazo zimesabibisha jengo la CCM la wilaya kunusurika kuchomwa moto na watu wasio fahamika.
Habari zilizopatikana jana mjini hapa kutoka ndani ya Chama Cha Mapinduzi ambazo zimethibitishwa na Katibu wa Chama hicho Mkoa wa Ruvuma Velena Shumbusho zimesema kuwa uchaguzi wa kura za maoni wa kumpata Mgombea Uwenyekiti wa halmashauri hiyo umesitishwa mpaka hapo baadae tarehe itakapopangwa tena.
Shumbusho aliuambia Mtandao huu kwa njia ya simu kuwa uchaguzi huo umehairishwa mpaka CCM mkoa kupitia Kamati yake ya utendaji itakapopanga tena kwani hali ya kisiasa kwa sasa si shwari.
Alifafanua zaidi kuwa pamoja na kusitisha uchaguzi huo jengo la ofisi ya CCM la wilaya hiyo limenusurika kuchomwa moto na watu wasiofahamika jambo ambalo limesababisha wanachama wengi kushtushwa.
Aliwataja Madiwani wa CCM waliojitokeza kugombea nafasi ya hiyo kuwa ni Alanusi Ngahi ambaye ni Diwani wa Kata ya Kipapa, Alani Mahai Diwani wa Kata ya Maguu na Nathaniel Charles Diwani wa Kata ya Matili ambapo kamati ya siasa ya mkoa ilipokaa ilirudisha majina mawili ya Mahai na Charles jambo ambalo limeonekana kuwa na mtafaruku mkubwa baada ya baadhi ya Madiwani kuilalamikia Kamati ya Siasa kwa nini imekata jina la Diwani Alanusi Ngahi na kwamba majina ya nafasi ya Makamu mwenyekiti majina yote matatu ya madiwani walioomba yalirudishwa ambao ni Winfrid Kapinga diwani wa kata ya Ngima, Agnesi Mahangula na Prisca haule ambao wote ni Madiwani wa viti maalumu (CCM) .
Alibainisha kuwa Kamati ya Siasa ya Mkoa chini ya Mwenyekiti wake Oddo Mwisho ilikaa siku nne zilizopita na kupendekeza majina mawili ya wagombea ndio yaliyoletwa kwenye kikao cha Kamati ya Siasa ( CCM) Wilaya ya Mbinga ambayo ililidhia uchaguzi huo ufanyike lakini hakuna kigogo yeyote aliyeshinikiza kukata jina la mgombea bali ni kamati yenyewe ilifikia uwamuzi huo.
Baadhi ya Madiwani wa Halmshauri ya Wilaya ya Mbinga ambao hawakutaka majina yao yatajwe waliuambia Mtandao huu kwa nyakati tofauti walisema kuwa matukio hayo yanasababishwa na viongozi wenyewe wa CCM wa ngazi ya Wilaya na Mkoa kwani inaonyesha wazi kuwa jina la mgombea Ngahi limekatwa kwa shinikizo la kigogo mmoja ambaye ndiye kiongozi mmoja wa CCM vilevile ni kiongozi wa ngazi ya juu wa Halmshauri ya Wilaya mpya ya Nyasa ambayo inatarajia kugawanywa kuwa Halmashauri mbili tofauti
Walisema kuwa tukio hilo linahofiwa kuwa limetokana na Kamati ya Siasa ya Mkoa kutorudisha jina la mgombea jambo ambalo limewafanya baadhi ya Madiwani wagomee uchaguzi lakini swala la kutaka kuchoma jengo la CCM linahitaji Polisi waingie ndani zaidi kufanya upelelezi ili kuwabaini waarifu wenye tabia chafu za kutaka kukichafua Chama Cha Mapinduzi
Kwa upande wake Katibu wa CCM wa Wilaya ya Mbinga Anastasia Amasi alisema kuwa tukio la kutaka kuchoma ofisi yake limetokea Juni 20 mwaka huu majira ya saa za usiku ambapo alidai kuwa yeye akiwa nyumbani kwake juzi majira ya saa za asubuhi alipata taarifa za tukio hilo na alieleza kuwa alipofika kwenye eneo la tukio aliona uharibifu uliofanyika.
Alieleza zaidi kuwa baadaye alitoa taarifa kwenye Kituo Kikuu cha Polisi cha Wilaya ya Mbinga na Askari Polisi walipofika kwenye eneo la tukio walichukua maelezo ya awali kwa ajili ya uchunguzi zaidi na kufafanua kuwa kwenye eneo la tukio yalikutwa masalia ya mafuta yanayodaiwa kuwa ni ya Petrol kwenye chupa yenye ujazo wa lita moja yaliyoletwa na waalifu waliotaka kufanya tukio hilo, lakini mlango mmoja na madirisha mawili pamoja na mapazia ya madirisha hayo yaliungua na moto.
Naye Mkuu wa kikosi cha Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Ruvuma Baraka Mvano alipohojiwa na www.stephanomango.blogspot.com kwa njia ya simu alikanusha kuwepo kwa tukio hilo na kudai kuwa ofisi yake haijapata taarifa ya aina yoyote ila anaendelea kufuatilia zaidi.
Hata hivyo Mtandao huu ulijitahidi kufanya mawasiliano ya kumpata Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki ili atoe ufafanuzi juu ya tukio hilo ziligonga mwamba baada ya kumpigia simu zaidi ya mara tatu ambayo ilikuwa haipokelewi na baadaye Mtandao huu ulilazimika kuwasiliana na Afisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Ruvuma aliyejitambulisha kwa jina moja la Malimi ambaye alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo alidai kuwa lilitokea Juni 20 mwaka huu majira ya usiku lakini hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa na Polisi inaendelea kufanya upelelezi zaidi ili kuwabaini watuhumiwa.

Friday, June 21, 2013
WATOTO WALILIA HAKI ZAO ZA KUISHI, KULINDWA NA KUHESHIMIWA
Na Gideon Mwakanosya ,Namtumbo
WATOTO wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wameiomba Serikali kukomesha vitendo vya ubakaji vinavyofanywa kwa watoto wadogo wilayani humo kwani tatizo hilo limeonesha kuwa kubwa ambapo katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu jumla ya watoto 14 walibakwa na kesi zao kuripotiwa katika kituo kikubwa cha Polisi cha Wilaya hiyo.
Wakisoma Risala ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu jana iliyofanyika Kiwilaya katika kijiji cha Hanga wilayani Namtumbo walisema kuwa pamoja na jitihada za Serikali na wadau mbalimbali za kukomesha vitendo vya unyanyasaji kwa watoto wadogo bado tatizo hilo ni kubwa kwa Wilaya ya Namtumbo.
Walieleza kuwa katika takwimu za miaka miwili iliyopita zinaonesha kuwa mwaka 2012 wanafunzi 16 waliacha shule kutokana na mimba na wanafunzi 151 kati ya hao wavulana 88 na wasichana 63 waliacha shule kwa utoro na mwaka 2013 wanafunzi 12 wa kike walipata ujauzito na kuacha shule huku wanafunzi 34 walikuwa watoro mwaka 2012 na mwaka 2013 wanafunzi 18 ambao waliripotiwa kuwa watoro.
Walisema kuwa tatizo la watoto kutumikishwa kazi za majumbani kama vile kazi za ndani na mashambani,kutumiwa na watu wazima kufanya biashara ndogo ndogo hata kama wanatakiwa kuwepo mashuleni bado limekuwa ni tatizo hivyo ni vyema kila mzazi akatambua kuwa kila mtoto ni wake na anahitaji malezi bora hasa kuwapatia elimu iliyo bora na itasaidia kupunguza tatizo la watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Kwa Upande wake mgeni rasmi wa maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu alisema kuwa kila wananchi wakiwemo wazazi na walezi wanawajibu wa kuhakikisha kuwa watoto wao hawatumikishwi kazi za hatari na kazi zinazowazidi umri ili kupunguza tatizo la watoto kukimbilia mitaani na kujiingiza katika mambo mabaya ikiwemo madawa ya kulevya.
Alisema kuwa kutowajibika kwa wazazi na walezi katika kulea familia kunasababisha mambo mengi yasiyofaa ndani ya jamii ikiwemo utoro,mimba kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari hivyo ni wajibu wa kila mzazi katika kuwafichua waharifu wanaowapa mimba wanafunzi ili vitendo hivyo vikomeshwe kabisa ndani ya Mkoa huo.
Aidha alisema kuwa wazazi na walezi watambue kuwa watoto wanahaki ya kulindwa, kukua,kuendelea kuishi na kushiriki kutoa mawazo ndani ya jamii lakini kuna baadhi ya wazazi a walezi watoto wanapohitaji huduma hupewa karipio kali na wakati mwingine kipigo pasipo sababu.
MWISHO.
Subscribe to:
Comments (Atom)