Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda
Na Gideon Mwakanosya,Songea
LUKAS Bajuta (35)mkazi wa Kijiji cha Milonji kilichopo katika kata ya Lusewa Wilayani Namtumbo mkoa wa Ruvuma amenusurika kufa baada ya kujeruhiwi na Simba kwa kung’atwa sehemu ya makalio upande wa kulia wakati akijaribu kuwaokoa ng’ombe wake waliokuwa kwenye zizi waliotaka kuliwa na samba huyo
Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda alisema kuwa tukio hilo lilitokea Disemba 12 mwaka huu majira ya saa 10:30 jioni huko katika kijiji cha Milonji
Kamuhanda alisema kuwa inadaiwa siku ya tukio Bajuta mwenye asili ya kabila la Mang’ati akiwa nyumbani kwake ghafla alimuona simba akiwa katikakati ya ng’ombe wake waliokuwa kwenye zizi ambalo liko jilani na nyumba anayoishi
Alisema kuwa Bajuta baada ya kumuona simba huyo alichukua mkuki na kuelekea kwenye eneo la ziziz la ng’ombe wake ambako alipofika jilani inadaiwa samba alimuona kisha aliruka toka ndani ya zizi hadi nje alikosimama Bajuta
Alifafanua kuwa Bajuta baada ya kuona hivyo aliamua kulala chini ambapo samba akaja kumlalia kwa juu na kuanza kumkata sehemu ya upande wa kulia wa makalio yake na kumsababishia maumivu makali ambayo yalimfanya apoteze fahamu
Alieleza zaidi kuwa wakati Bajuta anavamiwa na simba watu waliokuwa jilani na eneo hilo wakiwemo na watu wa kabila lake la wamang’ati walifika eneo hilo na kuanza kumshambulia samba huyo kwa kumpiga na mikuki ambapo baadaye samba huyo alikimbia na kutokomea kusiko julikana
Alibainisha zaidi kuwa baada ya samba huyo kuondoka kwenye eneo la tukio wanakijiji wenzake walimchukua Bajuta na kumpeleka kwenye Kituo cha Afya cha Lusewa kwa matibabu ambako kwa sasa hivi amelazwa na hali yake inaendelea vizuri
MWISHO