Na, Augustino Chindiye Tunduru
MCHIMBAJI wa madini ya Vito katika eneo la machimbo yaliyopo Namba 8 katika Mto Muhuwesi Wilayani Tunduru Kessi Mtolela ( Mpogolo)amefariki dunia baada ya kuangukiwa na kifusi cha udongo.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa marehemu aliangukiwa na kifusi hicho wakati akifuatilia madini hayo katika eneo hilo baada ya kuvutiwa na udongo ulio onekana kuingia kwa ndani ya kifusi hicho.
Walisema akiwa katika harakati hizo ghafla udongo uliokuwa juu yake ulikatika na kumuangukia kwa kumfunika mwili mzima na kupoteza maisha yake papo hapo.
Mganga kutoka katika Hospitali ya Serikali ya Wilaya ya Tunduru
Dkt.Jeshi Daraja aliyeufanyia uchunguzi mwili wa marehemu Mpogoro alisema kuwa kifo hicho kilitokana na mkandamizo mkubwa na udongo huo na kukosa hewa kwa muda mrefu.
Akizingumzia tukio hilo afisa madini makazi wa Wilaya hiyo
Fredriki Mwanjisi mbali na kukiri kuwepo kwake aliwatahadharisha
wachimbaji hao wadogo wadogo kufanya kazi zao kwa uangalifu ili
kujikinga na matukio ya aina hiyo ambayo yamekuwa yakisababisha vifo na vilema vya maisha.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Michael kamuhanda
alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kueleza kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi wa kifo hicho.
Mwisho