Na Augustino Chindiye, Tunduru
SERIKALI kupitia mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) imeombwa kuyachukulia hatua za kisheria makampuni yanayotoa huduma za mawasiliano nchini yanayo wayumbisha wateja wake kwa kudai imewawekea fedha kwenye akaunti maalum wakati inawadanganya.
Ombi hilo limetolewa jana na wateja wa makampuni hayo kwa nyakati tofauti kufuatia kuwepo kwa wimbi kubwa la watumiaji wa mitandao hapa nchini kukumbwa na kiwewe cha kila mtumiaji wa mtandao wa simu za mikoni kujikuta wakiwa wameingiziwa kitita cha fedha wanazoshindwa kuzihamisha na kuzitumia.
Fedha hizo zinazodaiwa kumwangwa katika Simu hizo ili zikae hewani na watu wanaodhani kuwa ni “Mafisadi” zimeingizwa kwa watumiaji wa mitandao yote nchini na kuzificha katika akaunti iliyopewa jina la future banking MBanking ambapo kila mtumiaji wa Simu ameingiziwa Shilingi 800,000 /= kwa kila mtandao wa simu anaoutumia.
Hamis Seleman alisema kuwa pamoja na fedha hizo kinachowachanganya watumiaji wa mitandao hiyo mbali na fedha hizo kuonekana kuingizwa katika Simu zao ni fedha hizo
kutowezekana kwa kutolewa kwa njia yoyote kutokana na kuwekwa namba ya siri ( PIN ) hali iliyosababisha mlundikano wa watu kutoa vijijini kuja mijini ili kuona uwezekano wa kutoa fedha hizo ili wazitumie.
Seleman alisema kuwa kwa mujibu wa maelekezo watumiaji waliovumbua fedha hizo ziliko
fichwa, mtumiaji wa simu ya mtandao wowote anatakiwa kubonyeza alama ya *150*55# na kubonyeza alama ya Ok ili kuituma katika mtandao anaoutumia atapata ujumbe unao mwelekeza kuwa kuingia katika akaunti hiyo na kadili utakavyo endelea utapata ujumbe unao kueleza kuwa umeingiziwa kiasi hicho.
Wakati hayo yakiendelea baadhi ya makampuni ya simu hapa nchini yamekuwa yakituma ujumbe unao watahadharisha wateja wake kuwa hayata husika na utapeli wowote wa kifedha utakaofanyika kutoka na wateja wao kutumiwa Meseji hali inayoonesha kuwa huenda wamiliki wa mitandao hiyo wamezidiwa nguvu na watu hao wanaoingilia mitandao ya simu zao.
Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya Mawakala wa M-pesa, Airtel money na Tigo pesa walikiri kupata usumbufu mkubwa kutoka kwa wateja hao ambao kila mtumiaji wa simu kwa muda sasa wamekuwa wakienda kuomba kutolewa fedha hizo.
Mwisho.