About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Friday, September 2, 2011

WACHAWI WAKUTANA KUPANGA KUMUUA MGANGA WA JADI

                            Frola Ndembo maarufu kwa jina la Binti Ndembo akionyesha miliki yake ambayo inaonekana kuwa tishio kwa waganga wenzake na watu wananao daiwa kuwa ni WACHAWI
 Na Joseph Mwambije,Songea
WATU wanaosadikiwa kuwa wachawi wanadaiwa kufanya vikao viwili usiku vya kumuua Mganga mmoja maarufu Mkoani Ruvuma aitwaye Frola Ndembo ambaye hulisaidia jeshi la Polisi kukamata wahalifu wanaokuja kwake kujizindika.
Wachawi hao watatu akiwemo akiwemo binti wa miaka tisa walinaswa na Mganga huyo anayefanyia shughuli zake kwenye kijiji cha Namabengo Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma na kujisalimisha huku wakieleza jinsi shughuli za ushirikina ziavyofanyika.
Mwandishi wa habari hizi wa mtandao wa http://www.stephanomango.blogspot.com/ ,Joseph Mwambije alishuhudia mtoto huyo Loveness Mapunda(jina linahifadhiwa)akijieleza kwenye eneo maaalumu kwa Mganga huyo ambalo huitwa Uwanja wa dhambi ambalo Mshirikina hueleza jinsi anavyofanya ushirikina na kutubu kwenye umati mkubwa wa watu unaokuwa umemzunguka.
Akijieleza katika eneo hilo mtoto huyo ambaye ana maendeleo mazuri darasani alisema uchawi alipewa na Bibi yake ambaye alikuwa pamoja naye kwa mganga huyo alisema yeye na Bibi yake huyo walihudhuria  vikao viwili vya Wachawi vya kumuua Mganga huyo lakini hawakuchangia hoja yoyote.
Akisimulia huku akitoa machozi katika Uwanja wa dhambi alisema Bibi yake amemtia muhuri mama yake mzazi kwa ajili ya kumla Krismas ya mwaka huu na kwamba amemuweka yai sehemu za siri jambo linalomfanya aumwe ugonjwa usiojulikana.
Alisema sababu za kufanya kikao hicho ni kutokana na Mganga huyo kuwaumbuanakuwasumbua jambo linalowafanya kushindwakula nyama za watu kwa raha.
 Alijieleza kuwa yeye ni mchawi na huwa anakwenda makaburini usiku na Bibi yake na kwamba alipewa uchawi bila kujijua hivyo anapenda Mganga huyo amuondoe uchawi.
 Kwa upande wake Mganga huyo maarufu kwa jina la Binti Ndembo alijigamba kwamba Wachawi hawawezi kumuua bali atakufa Mungu atakapopenda na kwamba ataendelea kuwaumbua wachawi na Majambazi na wezi.

WALIMU WA UFUNDI WATAKIWA KUWAJENGEA UWEZO WA KUJITEGEMEA WANAFUNZI

                                                     Na Joseph Mwambije,Songea
KAIMU Mkurugenzi wa  VETA Kanda ya Nyanda za juu kusini Susan Magani amewataka wahitimu wa kozi ya CBET kutokuwa na muda wa mchezo kwenye kazi yao ya Ualimu wa Ufundi  kwa kuwa inamjengea mtu ujuzi katika maisha yake
Aliitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati akifunga kozi ya kufundisha kwa kutumia mfumo mpya wa Compitance based education and training(CBET) iliyofanyika Peramiho na kushirikisha walimu 36 wa vyuo vya ufundi toka  Mikoa ya Ruvuma na Iringa.
Magani alisema kuwa kazi hiyo ni kazi nzito na muhimu kama zilivyo kazi nyingine hivyo ni vyema walimu wanaofundisha vyuo vya ufundi wakatambua jukumu lao la kuwajengea watu ujuzi wa kwenda  kujitegemea.
‘Walimu mnaofundisha vyuo vya ufundi mnapaswa kujijua kuwa nyinyi ni watu muhimu mnaohusika katika kumjengea mtu ujuzi wa kujitafutia maisha hivyo mnapaswa kujiendeleza kielimu kwa  kuwa kuna mabadiliko ya kiuchumi’alisema Magani.
Pia aliwataka walimu wa vyuo vya ufundi kuwa wajasiriamali ili waweze kupambana na makali ya maisha  ya sasa ambayo yanaendelea kupanda kila siku na kuwa  wajasiriamali wa vitendo na kwamba kwa hali hiyo hata wanafunzi wao wanaweza kuiga ujasiriamali toka kwao.
Alisema kuwa walimu hao waliohitimu mafunzo ya kufundisha  kwa kutumia mfumo huo mpya watakuwa na nafasi nzuri ya kuwaeleza wanafunzi watakaokuja kusoma kwenye vyuo vyao.
Akijibu risala ya wahitimu hao ilyotaka walimu wa ufundi toka taasisi za dini na binafsi kuongezewa mishahara,walimu kupata mafuzo ya kopyuta na kiingereza na kufungua maduka ya vitabu vya ufundi alisema maombi yao yatafanyiwa kazi.
Kaimu Mkurugenzi huyo wa VETA alisema  suala la upatikanaji wa vitabu wataliingiza kwenye mpango kazi wa miaka mitano na maoni yao yatapelekwa kwenye ngazi za juu kwa ajili ya hatua zaidi
MWISHO