About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Thursday, March 29, 2012

WAKULIMA WA KOROSHO TUNDURU BADO HAWAJALIPWA MADAI YAO LICHA YA SERIKALI KUTOA AGIZO

       Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Madaha
Na Augustino Chindiye, Tunduru

WAKATI kukiwa na maelekezo kutoka Serikani kuwa mabenki yatoe fedha zitakazotumika kuwalipa malipo ya pili, pamoja na kulipia korosho ilizo kopwa kutoka kwa wakulima wa zao hilo wakulima wa wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma malipo hayo bado hayajaanza  kutolewa.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Chama kikuu cha Ushirika wa wakulima wilayani Tunduru (TAMCU) Imani Kalembo alipotakiwa kuzungumzia utekelezaji wa agizo hilo kutoka serikalini.

Akifafanuaa taarifa hiyo Bw. Kalembo alisema kuwa malipo hayo yameendelea kukwama kutokana na majibu ya viongozi wa Benki ya NMB tawi la Tunduru waliodai kuwa bado hawajapokea maelekezo kutoka makao yao makuu juu ya kuanza kutoa fedha hizo zitakazotumika wakati wa malipo hayo.

Katika taarifa hiyo Kalembo alisema kuwa jumla ya tani 4800 zimekwama katika maghala na kusababisha malipo kwa wakulima wa Korosho wilayani humo kushindwa kutolewa ni sehemu ya tani 7000 zilizozalishwa Msimu wa mwaka 2011/2012.

Alisema katika msimu huu Wilaya hiyo ilibahatika kuuza katika mnada mmoja tu kati ya minada 9. ambapo iliuza tani kama 1100 na kwamba hayo ilitokana na wanunuzi wakubwa kukataa kununua korosho hizo kwa bei ya shilingi 1480 kwa kilo moja  waliyoitaka wakulima hao wakiwa wanashinikiza wanunue kwa chini ya shilingi 1400.

Kufuatia hali hiyo baadhi ya vyama vya msingi vya ushirika vya wakulima wa wilaya hiyo vimepata changamoto ya baadhi ya wakulima wake kuondoa korosho maghalani na kuanza kuuza korosho zao kwa walanguzi ambao hutumia kipimo halamu kiitwacho KANGOMBA yaani bakuli linalobeba kilo 2 linanunuliwa kwa shilingi 600.

Akizungumzia hali hiyo Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Madaha pamoja na kuipongeza serikali kwa kutoa tamko hilo alisema kuwa ofisi ya kwa kushirikiana na uongozi wa Mkoa huo zikiwa ni juhudi zaa kuhakikisha kuwa malipo hayo yatolewe kwa haraka.
Mwisho

MKURUGENZI WA WILAYA YA NAMTUMBO MKOANI RUVUMA ATISHIWA KUUAWA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda
Na Stephano Mango, Songea
JESHI la Polisi mkoani Ruvuma linawasaka watu wasiofahamika wanaodaiwa kumtishia kumuua Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Mussa Zungiza(56) ambaye inadaiwa kuwa alitumiwa ujumbe wa maandishi kwenye simu yake ya mkononi akitishiwa kuuawa  .
Akizungumza na www.stephanomango.blogspot.com  jana mchana ofisini kwake Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Michael Kamhanda alisema kuwa tukio hilo lilitokea machi 25 mwaka huu majira ya saa za mchana huko katika wilaya ya Namtumbo .
Kamanda Kamhanda alieleza zaidi kuwa inadaiwa mnamo siku tofauti za mwezi machi mwaka huu huko katika wilaya ya Namtumbo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri  ya wilaya hiyo Zungiza alipokea ujumbe wa maandishi kupitia kwenye simu yake ya mkononi akitishiwa kuuawa. 
Alibainisha zaidi kuwa kwenye simu hiyo ya mkononi ujumbe huo ulitoka  katika namba  mbalimbali za simu,ambapo ujumbe wa kwanza ulitumwa machi 14 mwaka huu  majira ya saa 1:46 asubuhi na ujumbe wa pili ulitumwa  mach 14 mwaka huu majira ya saa 4:08 usiku .
Alieleza zaidi kuwa ujumbe huo ulieleza kuwa siku yoyote Zungiza atauawa kwa njia ya aina yoyote na kutoeleza chanzo au sababu ya kutaka kumuuwa ,jambo ambalo lilimpa hofu kubwa juu ya maisha yake .
Kamanda Kamhanda alisema kuwa Mkurugenzi Mtendaji huyo Zungiza  baada ya kupokea ujumbe huo kupitia kwenye simu yake ya mkononi  hatua ya kwanza alichukua ya kuwasiliana na kamati ya ulinzi ya wilaya hiyo na kisha alitoa taarifa juu ya ujumbe huo aliotumiwa wa vitisho katika kituo cha polisi cha wilaya ya Namtumbo ambako lilifunguliwa jalada la uchunguzi .
Hata hivyo kamanda Kamhanda alisema kuwa jeshi la polisi mkoani Ruvuma  linaendelea na upelelezi zaidi wa kina kuhusiana na tukio hilo ili kuwabaini watu waliohusika kumwandikia ujumbe kupitia simu yake ya mkononi ambao ulimtishia kumuuwa Zungiza.
 MWISHO

AKAMATWA NA POLISI BAADA YA KUMZIKA MWANAE KICHANGA MAMA AKIWA HAI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda

NA GIDEON MWAKANOSYA ,SONGEA
JESHI la polisi mkoani Ruvuma limemtia mbaroni Anna Mhenga (25) mkazi wa Bombambili katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa tuhuma za kumtupa mtoto wake mwenye umri wa siku moja  kwenye eneo la msitu wa milima ya Chandamali ambako alichimba shimo na kumfukia .
Habari zilizopatikana jana mjini Songea ambazo zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Michael Kamhanda zilisema kuwa tukio hilo lilitokea machi 24 mwaka huu majira ya saa za mchana huko katika eneo la msitu wa Chandamali uliopo katika Manispaa ya Songea.
Kamanda Kamhanda alisema inadaiwa kuwa siku hiyo ya tukio Anna alijifungua mtoto wa jinsia ya kike kisha aliondoka eneo la nyumbani kwake na alielekea kwenye eneo la msitu mkubwa wa miti wa Chandamali ambako aliamua kuchimba shimo na kukifukia kichanga alichotoka kujifungua .
Alifafanua kuwa inadaiwa kuwa Anna alijifungua mtoto huyo akiwa na ujauzito wa miezi 7 kisha alifikia uamuzi wa kumtupa mtoto wake kwa kumfukia  jambo ambalo liliwafanya majirani wamshitukie ambapo mmoja kati yao ambaye ndiye raia mwema alitoa taarifa katika kituo kikuu cha Polisi cha Songea.
Alieleza zaidi kuwa Polisi baada ya kupata taarifa ya tukio hilo walifanikiwa kumkamata Anna ambapo katika mahojiano ya awali mtuhumiwa alikataa kuhusika na tukio hilo na baada ya upelelezi zaidi wa Polisi alikiri kuwa ni kweli alikuwa na ujauzito .
Alifafanua zaidi kuwa machi 26 mwaka huu majira ya saa za asubuhi  mtuhumiwa Anna alipelekwa kwenye Hospitali ya Serikali ya mkoa Songea kupimwa ambako ilibainika kuwa mazingira yote yalionyesha kuwa mtuhumiwa alitokakujifungua .
Alieleza zaidi kuwa Polisi baadaye waliendelea kumhoji na alikubali kuwa ni kweli alijifungua mtoto wa jinsia ya kike ambaye alidai kuwa amemzika kwenye msitu mkubwa wa miti uliopo eneo la Chandamali .
Kamanda Kamhanda alibainisha zaidi kuwa inadaiwa mtuhumiwa baadaye aliwapeleka askari Polisi kwenye msitu wa Chandamali ambako aliwaonyesha mahali alipomfukia mtoto huyo ambapo walichukua jukumu la kufukua eneo hilo na kukuta maiti ya kichanga ikiwa ndani ya shimo.
Alisema kuwa maiti ya kichanga huyo baadaye ilichukuliwa na kupelekwa kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kilichopo katika hospitali ya Serikali ya mkoa Songea na Polisi bado inaendelea kufanya uchunguzi kuhusiana na tukio hilo .
MWISHO