About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Monday, January 19, 2015

AFARIKI AKIFANYA MAPENZI SONGEA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela Akizungumza Jambo

NA,STEPHANO MANGO,SONGEA.

John Haule (35)Mkazi wa Lupapila Manispaa ya Songea amefariki Dunia ghafla wakati akifanya mapenzi nyumbani kwa mpenzi wake jina linahifadhiwa (winifrida Ndalama-35).

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela alisema kuwa tukio hilo limetokea Januari 17 mwaka huu majira ya saa 8 usiku huko katika kijiji cha Subira manispaa ya Songea.

Alisema kuwa siku ya tukio Haule alienda nyumbani kwa mpenzi wake majira ya saa 2 usiku akitokea hospitali ya misheni ya Peramiho ambako alikwenda kwaajiri ya kumuuguza mjomba wake na alipokuwa hospitali alimuaga mjomba wake kuwa amemkumbuka mtoto wake mdogo mwenye umri wa miezi  11.

Kamanda Msikhela alieleza zaidi kwa mjomba wake alimruhusu kurudi nyumbani lakini Haule akufika nyumbani kwake badala yake alipitiliza hadi nyumbani kwa mpenzi wake ambapo alipofika aliandaliwa chakula lakini marehemu alikataa chakula hicho kwa madai kuwa ameshakula alikotoka hivyo ilipofika majira ya saa 3 usiku waliingia chumbani kulala na kushiriki tendo la ndoa mpaka majira ya saa 5 usiku ambapo walipumzika huku wakijadili mahusiano yao.

Alisema kuwa ilipofika majira ya saa 8 usiku Haule ambaye ni marehemu alimuomba mpenzi wake warudie tena tendo la ndoa ambapo mpenzi wake alikataa akidai kuwa amechoka lakini baada ya kumlazimisha alikubali ndipo akiwa kwenye tendo hilo Haule alisikika akitoasauti ya kukoroma na kuanza kutetemeka jambo ambalo lilimshtua mpenzi wake huyo ambye alichukuwa jukumu la kwenda kuwaita majirani zake pamoja na mjumbe wa serikali ya mtaa Winney Mwingira ambaye naye alitoa taarifa katika kituo kikubwa cha polisi cha mjini Songea.

Kamanda Msikhela alieleza zaidi kuwa Polisi baada ya kupata taarifa walienda eneo la tukio wakiwa wameongozana na Dkt. Ambaye alithibitisha kuwa Haule ameshafariki Dunia na kwamba jeshi la polisi linamshikilia mwanamke huyo kwa upepelezi .
 
MWISHO.

NAPE AWAPIGA MKWARA WAGOMBEA URAIS 2015

 . Asema wanapoteza muda na pesa zao
>. Awataka wakumbuke salaam za mwaka mpya 2015 za CCM.
>. Ajivunia uzoefu wa CCM kudhibiti wasio waadilifu
>. Atamba CCM kufanya vizuri uchaguzi mkuu 2015.
>. Awataka Watanzania kuiombea nchi ipate kiongozi mwadilifu.
Na Mwandishi Wetu, Kibaha
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Ndg. Nape Nnauye amewaibukia tena wasaka urais ndani ya CCM na kudai kuwa Chama hicho hakitatoa mwanya kwa wanaosaka uteuzi huo kwa kununua wajumbe mbalimbali wa vikao husika.

Nape ameyasema hayo jana kwenye  mafunzo kwa wachungaji wote wa huduma ya Efatha nchini yaliyofanyika Kibaha mkoani Pwani. Nape alikuwa akitoa mada inayohusu nafasi ya CCM na uhusiano wa CCM katika jamii.


Pamoja na Nape ambaye aliwakilisha CCM kwenye mafunzo hayo walikuwepo watoa mada wengine kutoka vyama vingine vya upinzani nchini.


Akizungumzia mada ya nafasi na uhusiano wa CCM ndani ya jamii, Nape alisema historia ya Chama hicho ambayo haiwezi kwa vyovyote kufanana na ya chama chochote kilichopo au kijacho nchini ni moja ya sababu kubwa ya Watanzania kuendelea kukiamini Chama hicho. Aliongeza kuwa sababu kubwa ya pili ni misingi ambayo Chama hicho kinaiamini ambayo ndio imelifanya taifa la Tanzania kuwa taifa.


Nape alisema CCM ipo kila kona ya nchi na hivyo inamtandao mkubwa kuliko taasisi yeyote nchini, na hiyo ndio moja ya siri za uimara wa CCM.


Akizungumzia swala la maadili Nape alidai kuwa CCM ndio chama duniani chenye nyaraka nyingi na bora zinazozungumzia maadili ya viongozi. Pamoja na nyaraka hizo alisema mfumo wa uchujaji majina hasa kwa nafasi ya urais kupitia CCM hautoi nafasi kwa mgombea yeyote wa nafasi hiyo kupita kwa kununua uteuzi huo.


Alisema Nape kuwa wasaka urais wanaohangaika kutoa pesa zao kujaribu kununua uteuzi wa CCM wanapoteza muda na pesa zao kwani Chama hicho hakitawateua kugombea nafasi hiyo.


Nape akatumia nafasi hiyo kuwaomba wachungaji hao kukiombea Chama hicho na viongozi wake wawe na ujasiri wa kulisimamia hilo kwani kupitisha wagombea walionunua uteuzi huo ni kukaribisha laana kwa nchi.


" Nawahakikishia kuwa hakuna mnunua urais atakayepenya mchujo ndani ya CCM. Kuruhusu mtu wa namna hiyo kupenya ni kuleta laana kwa nchi yetu,hivyo viongozi wa dini tuombeeni tuwe na ujasiri wa kutosha kukataa laana hii" alisisitiza Nape.


Nape alisema mwanzoni mwa mwaka huu wa 2015 Katibu Mkuu wa CCM  Ndg. Kinana akitoa salaam za mwaka mpya za CCM mjini Tanga, aliwaambia Watanzania kuwa CCM imekuwa ikisimamia maadili kwa miaka yote lakini mwaka huu itaongeza ukali ili kuhakikisha nchi inapata viongozi waadilifu watakaoisaidia nchi kupiga hatua zaidi.


Anasema Nape hakuna atakayeingia madarakani kwa rushwa atakayeunda serikali itakayokusanya kodi. Bila kukusanya kodi hakuna namna nchi itapiga hatua ya maendeleo na huduma za kijamii zitadumaa na hivyo kusababisha maisha magumu na hiyo itakuwa laana kwa nchi.


Semina hiyo inayofanyika Kibaha mkoani Pwani itahitimishwa tarehe 24/01/2015 na imehusisha wachungaji wa huduma ya Efatha nchi nzima, na baadhi ya wachungaji kutoka nchini Kenya.

HABARI KAIKA PICHA
 MTUME na Nabii wa Kanisa la EFATHA Josephat Mwingira akimlaki kwa furaha, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alipowasili katika ukumbini, kutoa mada kuhusu nafasi ya CCM na uhusiano wa CCM katika jamii, kwnye semina ya wachungaji wa kanisa hilo wa ndani na nje ya Tanzania, inayoendelea Kibahaka mkoa wa Pwani. Watatu kulia ni Mama Eliakunda Mwingira.

WAPIGA KURA NAMTUMBO WATAKIWA KUMFANYIA TATHIMINI MBUNGE WAO




                                             MBUNGE WA JIMBO LA NAMTUMBO VITA KAWAWA

NA, STEPHANO MANGO,NAMTUMBO

WAPIGA KURA  wa Jimbo La Namtumbo Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Wametakiwa Kumfanyia Tathimini Mbunge wao  Vita Kawawa Waliomchagua  katika vipindi viwili Mfululizo Mwaka 2005 na Mwaka 2010 kama ametekeleza vyema Ilani ya Chama chake na Ahadi alizozitoa wakati anaomba kura katika Chaguzi mbili hizo

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mjini hapa Jana Afisa Elimu Mstaafu na Mfanyabiashara Ally Mbawala Alisema kuwa Mwaka huu ni Mwaka wa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani hivyo ni fursa Muhimu Sana kwa Wananchi kuchukua tafakari Stahiki ya utendaji Kazi wa Wawakilishi wao waliowachagua vipindi vilivyopita na Kuwahukumu katika sanduku la kura

Mbawala Alisema Kuwa Kipindi hiki sio cha kufanya mchezo ni kipindi cha kujitendea haki kwa Kuangalia utatuzi wa Changamoto zilizokuwepo kabla ya kumchagua Kiongozi husika hadi leo ili kujiridhisha utendaji kazi wake na kama anataka kugombea tena basi ahukumiwe kwa mujibu wa kipimo chake cha utendaji Kazi

Alisema kuwa Jimbo la Namtumbo lina Fursa Nyingi  sana za Kimaendeleo kwani kuna ardhi nzuri, Misitu, Madini , Mbuga za Wanyama na Maliasili zingine nyingi na wananchi wake ni wakulima wazuri wa mazao mbalimbali ya chakula , hivyo ni muhimu kupima kama rasilimali hizo zimeweza kusimamiwa na kutumika vizuri na kama zimewezesha kuinua maisha ya wakazi wa Jimbo hilo

Alieleza Kuwa Jimbo hilo ndilo ambalo lilikuwa Maarufu kwa Kilimo Cha Tumbaku na Mbunge wa Jimbo hilo alikuwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tumbaku Tanzania hivyo ni vyema  tukamtafakari kwa kina kama  ameweza kushiriki kikamilifu kufufua vyama vya Ushirika na kukuza zao hilo ambalo ndilo zao kubwa la kiuchumi kwa Wakazi wa Namtumbo

Alifafanua kuwa kabla ya uchaguzi ni muhimu sana Wapiga Kura wa Jimbo hilo wakawa na vipaumbele vyao vya Kimaendeleo ili waweze kutengeneza ajenda ya pamoja badala ya kusubiri ilani za Vyama au matakwa ya Mbunge ambayo kimsingi hayana tija katika maisha yao

“Mimi ni Mzaliwa wa Namtumbo lakini kila Siku Maisha ya Wakazi Wa Jimbo hili yanazidi kuwa magumu kwa sababu mbalimbali hali ambayo ina hatarisha amani na utulivu katika jamii kwani kundi la walionacho wanaendelea kunufaika huku kundi kubwa la wasio nacho wakiendelea kuhangaika”

Alieleza zaidi kuwa  hadi leo bado kuna Wakazi wa Jimbo hilo hawajafikiwa na huduma za Maji Safi Na Salama, Elimu,  Afya, Miundombinu, huduma za kiuchumi na Mawasiliano hali ambayo inaendelea kuwafanya wawe masikini zaidi
MWISHO



DKT NCHIMBI; WANACCM WAJIPANGA SHEREHE ZA MIAKA 38 YA CCM TAIFA



MWENYEKITI WA KAMATI YA MAANDALIZI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 38 YA CCM TAIFA DKT EMMANUEL NCHIMBI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI SONGEA

NA, STEPHANO MANGO, SONGEA

WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi Mkoani Ruvuma Wametakiwa kuendelea kujipanga Kikamilifu Katika Sherehe za Maadhimisho ya kutimiza miaka 38 ya kuzaliwa kwake ambayo yanatarajiwa kufanyika Katika Viwanja vya Majimaji Mjini Songea Februari 2 mwaka huu

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jana katika Viwanja vya Ccm Mkoa wa Ruvuma Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe hizo za Maadhimisho ya miaka 38 Ccm Dkt Emmanuel Nchimbi alisema kuwa Maadhimisho hayo ni Muhimu sana kwani yanalenga zaidi kukumbuka toka kuzaliwa kwake hadi hapa kilipo hivyo wanaccm hawana budi kuhakikisha wanajipanga vizuri kufanikisha maadhimisho hayo

Dkt Nchimbi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo La Songea Mjini alisema kuwa Wanaccm wanatakiwa kutumia fursa hiyo muhimu kujiimarisha kiuchumi na kiutalii kwani kuwepo kwa wageni wengi wakati wa Maadhimisho hayo kutachangia ununuzi wa bidhaa mbalimbali ambazo zinazalishwa na Wajasiliamali Mjini hapa

Alisema kuwa Kitendo cha Viongozi Wakubwa  wa Ccm Taifa katika Vikao Vyao kuridhia kuwa Maadhimisho hayo Kufanyika Songea ni cha Busara sana hivyo Tunawajibika kujiandaa vyema kuwapokea Wageni na kufanya mambo ambayo yanaendana na maudhui ya Maadhimisho hayo

Alieleza kuwa Mwaka huu ni Mwaka wa Uchaguzi ni lazima wanachama na wapenzi wa chama hicho kuelezea mafanikio yaliyopatika katika miaka 38 ya kuzaliwa kwa chama hicho makini na kikubwa cha siasa nchini ambacho kinaongoza nchi kwa zaidi ya miaka 50 sasa

Alifafanua kuwa  Mafanikio ambayo chama hicho na kwa namana inavyotatua changamoto za Wananchi wake ndio msingi wa Vyama vya Upinzani Nchini kukionea  wivu na hata kukieneza vibaya katika mikutano yao ya hadhara

Hata hivyo amewataka Viongozi wote wa Jumuiya za Chama hicho kuendelea kujipanga ili kufanikisha Maadhimisho hayo  Muhimu yatahudhuriwa na wageni mbalimbali toka nchi jirani pamoja na wegeni kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.
 MWISHO

RC MWAMBUNGU AWACHARUKIA WALIMU WAKUU RUVUMA




 MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu

NA, STEPHANO MANGO, SONGEA

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu amewataka Walimu wakuu wa Sule za Sekondari na Msingi za Serikali Mkoani Ruvuma kutomrudisha Nyumbani Mwanafunzi Yeyote Kwa Kosa la Kutokuwa na ada, michango au Sare za Shule badala yake Washirikiane na Mzazi kuweza kutatua tatizo husika

Akizungumza na www.stephanomango.blogspot.com  Ofisini Kwake alisema ni Marufuku kumfukuza Mwanafunzi Shule kwa kosa ambalo sio lake kwani anayewajibika kulipa Ada au Michango  husika ya Shule ni Mzazi na Sio Mwanafunzi

Mwambungu Alisema kuwa Mwanafunzi anasomeshwa na Mzazi au Mlezi wake kitendo cha Kumfukuza Shule kwa Kosa ambalo sio Lake ni kumnyanyasa na  kumnyima haki yake ya msingi ya kupata Elimu Bora na Kwa Wakati Stahiki

Alisema kuwa Jukumu kubwa la Walimu ni Kutoa Elimu Bora na Malezi mazuri kwa Watoto kwani wao pia ni Sehemu ya Wazazi kitendo cha kuwafukuza kinaleta picha mbaya kwani mara nyingi wanafunzi hao wanapofukuzwa  wamekuwa wakiranda randa mitaani hali inayoweza kusababisha wakapatavishawishi vya kuingia kwenye makundi mabovu ya uvutaji bangi na ngono zembe kabla ya wakati

Alifafanua kuwa Walimu wanachotakiwa kufanya ni kuwasiliana na Wazazi wa Wanafunzi husika  Kupitia Maafisa Watendaji wa Vijiji au Mitaa ili kubaini ni tatizo gani ambalo linalomfanya Asilipe Ada na Michango kwa Wakati

"Maafisa Elimu na Wakaguzi hakikisheni agizo hili linatekelezwa kikamilifu ili kuongeza kiwango cha ufaulu katika Mkoa wa Ruvuma na kwamba yeyote Atakaye bainika kuzembea kutekeleza Wajibu wake basi Sheria zitafuata juu yake", Alisema Mwambungu

Alieleza kuwa Juhudi za Ujenzi wa Maabara ikiwa ni Utekelezaji wa Agizo la Rais Jakaya Kikwete zinaendelea kwa kasi Kubwa na Ifikapo mwezi Mei Mwaka huu Zitakuwa Zimekamilika na Kuanza kutumika kadri ilivyopangwa
MWISHO