About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Monday, December 26, 2011

Nawatakia Sikukuu njema za X-MASS,BOXING DAY,na MWAKA MPYA wa 2012 wenye Baraka na mafanikio makubwa


Nawasalimu wadau wote wa mtandao wa www.stephanomango.blogspot.comkwa kunipa ushirikiano wenu katika kipindi chote cha mwaka 2011

Nawatakia heri sana katika msimu huu wa mwishoni mwa mwaka 2011 na maandalizi mema ya mwaka mpya wa 2012





God is Love

Christmas is all about love

Christmas is thus about God and Love

Love is the key to peace among all mankind

Love is the key to peace and happiness within all creation

Love needs to be practiced - love needs to flow - love needs to make happy

Love starts with your partner, children and family and expands to all world

God bless all mankind

VIONGOZI NCHINI WATAKIWA KUWATUMIKIA WANANCHI ILI KULINDA AMANI YA NCHI

Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Songea Norbert Mtega
 
Na, Augustino Chindiye Tunduru

VIONGOZI wa kuchaguliwa na waliopewa mamlaka ya kulitumikia Taifa wameombwa kuitumikia Jamii kwa uadilifu ili kuendelea kudumisha amani na utulivu vinginevyo kuna hatari ya amani hiyo inayojivuniwa na taifa letu kutoweka.

Rai hiyo imetolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo la TUNDURU- Masasi Castory Msemwa wakati akiongea na waamini waliohudhulia katika Misa takatifu ya kukumbuka kuzaliwa Yesu Kristo ya Noeli iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Xavery mjini hapa.

Akifafanua taarifa hiyo kupitia Mahubiri hayo Askofu Msemwa alisema kuwa pamoja na Viongozi hao kufahamu hayo lakini wamekuwa walafi hali ambayo imekuwa ikiwasukuma kuwatesa Wananchi waliowapa nyadhifa hizo .

Alisema mbali na hali hiyo kuonekana wazi kwa Viongozi wa Serikali lakini pia matukio kama hayo yamekuwa yakiwakumba viongozi wa Dini ambapo wamekuwa wakipenda kujinufasha ili waendeelee kuongeza furaha mioyoni mwao kwa kujipangia marupurupu yao wenyewe bila kuwajali wengine na kuiacha jamii ikiteseka bila misaada yao.

Askofu Msemwa akatumia nafasi hiyo kuhimiza upendo miongoni mwetu na kueleza kuwa endapo upendo utaendelea kutoweka kuna hatari ya amani tunayo jivunia kumomonyoka na kuipeleka nchi yetu pabaya.

Katika hutuba hiyo pia Askofu Msemwa akaikumbusha jamii kuiga mwenendo wa mwasisi wa Taifa la Watanzania Mwenyeheri Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mtumishi wa Mungu Sister Bernadeta wa Jimbo la Perahimo ambaye amekuwa gumzo kubwa kutokana na watu wengi kwenda kuomba katika kaburi lake na kufanikiwa.

Alisema Sister Bernadeta alitangazwa hivi karibuni kuwa mtumishi wa Mungu ukiwa ni mchakato wa kufikia nafasi ya Mwenyeheri na kongeza kuwa mapendo ya kweli katika jamii yao ndiyo yaliyowafanya waendelee kukumbwa na jamii yao .

Mwisho