About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Wednesday, November 21, 2012

WAZIRI KAGASHEKI AWATIBULIA VUMBI WAWINDAJI HARAMU



Na Steven Augustino, Tunduru

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Balozi Hamisi Kagasheki ameadhimia kupeleka Bungeni maadhimio ya kubadilisha Sheria ili kuongeza adhabu kwa watuhumiwa wa makosa ya Jinai na uhujumu uchumi ambayo yamekuwa yakifanywa  na wawindaji haramu.

Hali hiyo imefuatia Serikali kubaini kushamiri kwa vitendo vya uhalifu wa ujangiri kufuatia Oparesheni maalumu iliyofanyika Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma na kufanikiwa kukamata mali zenye thamani ya Milioni 618.408

Akifafanua taarifa hiyo Waziri Kagasheki alisema kuwa kuanzi sasa serikali haitawavumilia na kuwaacha wajanja wachache wakiendelea kujinufaisha kupitia maliasili za taifa hili huku kukiwa na kundi kubwa wakibakia kuwa watazamaji huku akipendekeza kuwa adhabu za watuhumiwa
hao ziwe kati ya miaka 40 na 50 jela.

Aidha pamoja na kuwapongeza askari waliofanikisha kukamatwa kwa mali hizo Waziri Kagasheki alisema kuwa Oparesheni hizo ni endelevu na akatumia nafasi hiyo kuwaomba Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano utakaofanikisha kukamatwa kwa wahusika wengine waliokimbia.

Kwa mujibu wa taarifa za Oparesheni hiyo miongoni mwa mali zingine zilizo kamatwa katika Oparesheni hiyo ni pamoja na Bunduki zaidi ya 300 na Risasi 667 na Maganda ya Risasi 150 zilizobainika kumirikiwa kinyume cha taratibu.

Mali zingine zilizokamatwa katika Oparesheni hiyo iliyo anza Oktoba 20 mwaka huu ni pamoja na Gari moja aina ya Toyota, Piki piki 4 ambazo wahusika walivitelekeza na kuvikimbia baada ya kubainika kuwa vilikuwa vimehusika kubeba Nyala za serikali.

Adha katika msako huo pia Mbao 10,183 zenye thamani ya Shilingi Milioni 377,257,000 zilikamatwa huku asilimia 90% ya Mbao hizo ni za mti aina ya Mninga ambao namba 1 katika Soko la Dunia.

Akisoma Taarifa ya Oparesheni hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Oparesheni hiyo Samson Mkasla, Mtendaji wa Oparesheni hiyo Emmanuel Kandihabi alisema kuwepo kwa mafanikio makubwa kutokana ushiriliano mzuri kutoka kwa Viongozi wa Serikali na waanchi wa
Wilaya hiyo.

 Kandihabi aliendelea kueleza kuwa tayari Silaha zote zitahifadhiwa Polisi katika kipindi cha Miaka Miwili na kwamba Wamiliki hao ambao wamefungwa kifungo cha nje kwa muda wa Miaka miwili watatakiwa kuomba upya baada ya muda huo kwisha.

Akizungumzia taarifa za matukio hayo Kandiahabi alisema kuwa katika kipindi hicho walifanikiwa kukamata jumla ya waharifu 163 wakiwa na vielelezo vya Bunduki,Risasi,Meno ya tembo na Viboko,Mikia na Singa za Tembo vyote vikiwa na thamani ya Shilingi 2,241,147 /22.

Alisema katika kipindi hicho pia Majalada 123 yalifunguliwa katika Kituo cha Polisi Tunduru na tayari kesi 55 zimekwisha pelekwa Mahakamani ambapo kesi 43 zimekwisha tolewa hukumu kwa wahusika kufungwa kati ya kifungo cha miaka 10 na miaka 5 jela huku wengine wakitozwa faini.

Awali akisoma taarifa ya Wilaya hiyo kwa niaba Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Bw. Chande Nalicho Kaimu afisa Tawala wa Wilaya Manufred Hyera alisema kuwa katika kuthamini maendeleo ya idara hiyo tayari Wilaya hiyo imetenga kiasi cha Shilingi 38,875,097/71  na Halmashauri ya Wilaya hiyo  kwa ajili ya kutekeleza shughuli za maliasili katika kipindi cha mwaka 2012/2013.

Kikosi hicho kinacho shirikisha maafisa kutoka katika Majeshi ya Polisi, Jeshi la wananchi,Usalama wa Taifa, Pccb,Magereza na kuwashirikisha maafisa kutoka mamlaka ya Mapato TRA kinaongozwa na Kamanda Mstaafu wa Jeshi la Polisi Venance Tosi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kupitia hotuba iliyotolewa na Kamanda Tossi alisema kuwa oparesheni hiyo ni ya pili kufanyika na kueleza kuwa oparesheni kama hiyo ilifanyika mwezi Julai katika Wilaya ya Liwale Mkoani Lindi.

Mwisho