About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Wednesday, March 14, 2012

KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA RUKWA CHAMALIZIKA NA KUAINISHA MAAZIMIO MBALIMBALI

Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akitoa hotuba ya ufunguzi. 
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Dkt. Rajab Rutengwe kulia akiteta na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Joyce Mgana wakati kikao hicho kikiwa kinaendelea
Wajumbe wa kikao hicho wakiendelea kusikiliza kwa umakini hoja mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa kwenye kikao hicho
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Rukwa Florian Kabaka akiwasilisha taarifa ya Idara yake kwenye kikao hicho 
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Dkt. Rajab Rutengwe akizungumza kwenye kikao hicho, kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Joyce Mgana.

KWA PICHA ZAIDI

WATATU WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA MAUAJI

Na,Augustino Chindiye Tunduru

WATU watatu wamefikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma kwa  tuhuma za kumuua kwa kukusudia marehemu Said Ally Kaunya.

Walioshitakiwa kwa tuhuma hizo katika Shauri hilo la mauaji namba 3/2012 ni Rajab Kalanje Namdoa (82), Asha Rajab (44) na Yasin Mohamed (52) ambao wamedaiwa kuwa  walifanya kosa hilo kwa kukusudia,

Akiwasomea shauri hilo Mwendesha mashtaka Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Asp Alfred Kasoro alisema kuwa kwa pamoja watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Machi 8 mwaka huu katika kijiji cha Nalwale kilichopo katika Kata ya Nandembo wilayani humo.

Kutokana na Shauri hili linalowa kabiliwa watuhumiwa hao kuwa nje ya uwezo wa kusikilizwa na mahakama hiyo,  watuhumiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote.

Hata hivyo  hakimu wa mahakama hiyo  Goefre Mhini aliwaamuru kwenda Lumande hadi Machi 26 mwaka huu wakati shauri hilo litakapo somwa tena.

Kwa mujibu wa Taarifa za tukio la mauaji hayo yalitokea kwa sababu ya kugombea mashamba katika kijiji cha Nalwale katika Kata ya Nandembo ambapo Mtuhumiwa namba moja  amedaiwa kufanya tukio hilo ili kumaliza ugomvi huo.

Kwa mujibu wa taarifa hizo marehemu alidaiwa kuvamia shamba la mtuhumiwa namba moja nakuanza kulilima miaka 8 iliyopita ambapo katika kipindi chote hicho kesi ilikuwa ikiendelea katika hatua mbalimbali na kwamba kabla ya kifo hicho marehemu alikuwa ametoka kushinda kesi hiyo katika mahakama ya Ardhi ya Mkoa iliyopo katika manispaa ya Songea.

Mwisho.

MBUNGE WA VITIMAALU MKOA WA RUVUMA, MNEC NA MKUU WA MKOA WA RUKWA MHANDISI STELLA MANYANYA AWA MBUNGE WA KWANZA KUTEMBELEA JENGO LA POLISI WANAWAKE LINALOJENGWA NA WANAHARAKATI NA KUAHIDI KUTOA MILIONI 1

 Kutoka kushoto ni Katibu wa UWT Mkoa wa Ruvuma Mariam Yusuph, Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Hamza Temba, Mwanaharakati wa TGNP Kanda ya Kusini na Mhariri Msaidizi wa Tujifunze Kanda ya Kusini Juma Nyumayo, Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Ruvuma, Mnec na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya, Mwanaharakati wa TGNP Kanda ya Kusini, Mwandishi wa Star Tv/ Redio Free na Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa jengo la Polisi wanawake mkoa wa Ruvuma Adam Nindi, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Fadhiri Chacha 
 Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Ruvuma Kuruthum Mhagama, Katibu wa UWT Mkoa wa Ruvuma Mariam Yusuph, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mnec na Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Stella Manyanya akiwa na wajumbe wengine wa Baraza la Uwt mkoa wa Ruvuma wakitembelea jengo maalum la kusikiliza matatizo ya wanawake (Dawati la Jinsia) lilopo karibu na kituo kikuu cha Polisi Mjini Songea
 Mwanaharakati wa TGNP Kanda ya Kusini na Mhariri Msaidizi wa Tujifunze Kanda ya Kusini Juma Nyumayo akitoa maelezo ya awali ya jengo hilo kwa viongozi wa Jumuiya ya UWT Mkoa wa Ruvuma walipotembelea jengo hilo wakiongozwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mnec na Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Stella Manyanya
 Mwanaharakati wa TGNP Kanda ya Kusini, Mwandishi wa Star Tv/ Redio Free na Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa jengo la Polisi wanawake mkoa wa Ruvuma Adam Nindi akitoa maelezo ya ujenzi wa jengo hilo

 Viongozi wa Jumuiya ya UWT Mkoa wa Ruvuma walipotembelea jengo hilo wakiongozwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mnec na Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Stella Manyanya wakisikiliza maelezo ya jengo hilo
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mnec na Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Stella Manyanya akizungumza kwa furaha baada ya kutembelea ujenzi wa jengo hilo ambalo linapaswa kuigwa na mikoa mingine ambapo aliahidi kutoa milioni 1 kuchangia ujenzi huo na kushauri kuwa mara litakapo kamilika licha ya kutoa ushauri wa kisheria, ujinsia pia kiwe kioo cha maendeleo kwa wanawake kwa kutumia sheria watakazojifunza kupitia dawati hilo
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mnec na Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Stella Manyanya akiondoka eneo hilo baada ya kukamilisha kazi yake ya kukagua jengo la dawati la jinsia(mtandao wa Polisi Wanawake)

TAARIFA YA KAMATI YA MAUAJI MKOA WA RUVUMA YATOLEWA NA RC MWAMBUNGU

MKUU WA MKOA WA RUVUMA SAID MWAMBUNGU

WAANDISHI WA HABARI WAKITAFUTA PICHA YA MNATO WAKATI MKUU WA MKOA WA RUVUMA SAID MWAMBUNGU AKITOA TAARIFA YA KAMATI
Na Gideon Mwakanosya ,Songea.
KAMATI iliyoundwa na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu kuchunguza chanzo cha mauaji ya watu waliouwawa kuhusiana na imani za kishirikina na kusababisha vurugu za watu kuandamana na iliyopolekea mauaji ya watu wawili imekamilika.

Kamati hiyo iliyoundwa na watu wanane ikiongozwa na katibu tawala msaidizi miundombinu Severin Tossi ili Serikali iweze kuchukuwa hatua na kuhakikisha mambo kama hayo hayatokei tena

Akitoa taarifa hiyo Mwambungu alisema kuwa wale wote waliotuhumiwa kwenye mauaji hayo wamefikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Hata hivyo alisema kuwa kamati hiyo imeshindwa kuthibitisha uvumi wa watu kumi na nne waliouwawa kwa kuhusishwa na imani za kishirikina na kwamba tabia ya watu kueneza uvumi wa uongo ni mbaya sana kwani inagharama kubwa kwa wananchi na kuongeza kuwa kamati hiyo imefatilia na kupata taarifa kuwa hakuna mtu yoyote aliyenyofolewa viungo vya siri .

“Naomba nitoe rai kwenu kuwa tabia hii ya uenezaji wa uvumi ni mbaya sana kwa sababu inagharama kubwa sana kwa wananchi ambao wanashindwa kufanya kazi zao za kila siku katika ujenzi wa Taifa.”alisema Mwambungu.

Amesema,tayari elimu kwa wananchi imeshatolewa na wananchi wameanza kufanya kazi ya ulinzi shirikishi kwa kushirikiana na polisi kata ambapo kazi ya ulinzi na kwamba  mitaa yote ya Manispaa ulinzi umeimalishwa.

Mwambungu ameongeza kuwa, kwa sasa hali ya utulivu na usalama katika mkoa wa Ruvuma imerejea kama awali ambapo wananchi wanaendelea na shughuli zao za kila siku kama kawaida .

“Napenda kuwahakikishia wananchi wa mkoa wa Ruvuma na watu wanaoishi nje ya mkoa wa Ruvuma kuwa Songea ni salama na wananchi wanaendelea na shuguli zao kama kawaida, nawashukuru wananchi kwa ushirikiano mkubwa ambao wameutoa pia wanahabari kwa kusaidia kurejesha hali ya utulivu na amani ”alisema

Aidha, amewataka wananchi kuelewewa umuhimu wa kujilinda na kufata sheria ikiwa ni pamoja na kuacha hulka ya kujichukulia hatua mkononi ,ikiwa ni pamoja na kuacha kujihusisha na tabia za uvumi na hisia za kishirikina ili kuimarisha amani na utulivu.
MWISHO.

NYUMBA ZAIDI YA 300 ZABOMOLEWA NA MVUA WILAYANI TUNDURU

MKUU WA WILAYA YA TUNDURU JUMA MADAHA

Na Augustino Chindiye,Tunduru
ZAIDI ya Nyumba 300 zimeripotiwa kubomoka  katika Tarafa ya Mlingoti Wilaya ya  Tunduru Mkoani Ruvuma kufuatia mvua kubwa zinazo endelea kunyesha kwa takribani siku tatu sasa na kusababisha wakazi wa kaya hizo kukosa makazi.

Sambamba na tukio hilo pia. mvua hizo zimesababisha miundombinu ya barabara za kwenda vijijini  kujifunga kutokana na maji kujaa kiasi cha kutishia kubomoka  huku madaraja yakiwa hayapitiki kutokana na maji kufurika na maji kupita juu ya daraja .

Taarifa kutoka kwa madereva wanaofanya safari katika barabara kuu iendayo Songea zinasema kuwa maji yamejaa sana na kupita juu ya Daraja la Mto Masonya hali ambayo imesababisha magari yao kusitisha safari za kwenda na kuingia mjini Tunduru.

Adha nao madereva wanaofanya safari za kwenda katika vijiji vya Lukumbule,Mbesa  Nalasi Mchoteka nako hakufai kutokana na maji katika mto Msinjewe  kujaa sana na kutishia magari ya abiria kushindwa kupita huku taarifa kutoka katika Barabara iendeyo Masasi Mkoani Mtwara na Jijini Dar es salaam zikisema kuwa kikwazo kipo katika daraja la Mto Muhuwesi ambapo pia hapapitiki hali inayo onesha kuwa mji wa Tunduru hivi sasa upo kisiwani .

Akizungumzia maafa hayo Afisa Tarafa wa tarafa ya Milingoti  Manfred kahobera Hyera mbali na kukiri kuwepo kwa wimba la maafa hayo alisema kuwa hali katika mji wa Tunduru ni mbaya sana kiasi cha kutishia maisha ya wakazi wake.

Akifafanua taarifa hiyo Hyera alisema kuwa  hadi sasa amepokea taarifa kutoka kwa watendaji  kata tatu za miji huo Nanjoka zimeripotiwa kubomoka  nyumba 50, kata ya Masonya Nyuma 52 na majengo Nyuma 32 huku taarifa kutoka katika Tarafa ya Ligoma zikidai kuwa hali ni mbaya , chanzo cha matukio hayo kikidaiwa kuwa nyumba
hizo zilijengwa kwa tofari mbichi.

Juhudi za kupata taarifa za uharibifu ulisaabishwa na Mvua hiyo katika meneo mengine ya Wilaya hiyo zilishindikana kutokana na Kaimu Mkuu wa Wilaya hiyo  Martin Mulwafu kudaiwa kuwa yupo katika safari ya kufuatilia taarifa hizo vijjini.
Mwisho