About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Friday, February 3, 2012

JOHN KASEMBO AWALETEA WATANZANIA KITABU CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA: TULIKOTOKA, TULIPO NA TUNAKOKWENDA

                                                KIPO MITAANI SASA
                        JOHN MTWALE KASEMBO

JINA LA KITABU: MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA: TULIKOTOKA, TULIPO NA TUNAKOKWENDA

MWANDISHI: JOHN MTWALE KASEMBO
Ni mzaliwa wa Mkoa wa Mwanza. Alisoma shule ya msingi Shamaliwa. Na baadaye masomo ya Sekondari kwenye Seminari za Nyegezi - Mwanza na Maua - Moshi. 

Ni mwezeshaji na mtoa mada wa mambo ya uongozi, dini, vijana, falsafa, ujasiriamali na amali za maisha. Ni mhitimu wa masomo ya falsafa na dini katika Chuo cha Mtakatifu Augustino Peramiho ambacho ni Chuo Kishiriki cha Chuo Kikuu cha Urbaniana, Roma.

Tena yeye ni mtafiti wa maendeleo ya Tanzania. Sasa anaendelea na masomo ya Shahada ya Kwanza ya Teolojia katika Chuo hicho hicho.

Kitabu hiki kimechapishwa na kampuni ya Kolbe printing press, Nairobi nchini Kenya.

Yaliyomo
Kutabaruku................................................................................................. 7
Salamu za Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ...................... 9
Shukrani..................................................................................................... 11
Dibaji.......................................................................................................... 15
Utangulizi................................................................................................... 17
Vifupisho................................................................................................... 23
Sehemu ya Kwanza
TANZANIA TULIKOTOKA
1. UKOLONI TANZANIA BARA........................................................... 27
2. HARAKATI ZA UKOMBOZI............................................................. 39
3. UHURU................................................................................................ 47
4. MAISHA BAADA YA UHURU......................................................... 57
Sehemu ya Pili
TANZANIA TULIPO
5. JUBILEI YA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA....... 69
6. JUBILEI NI KUANGALIA TUNU ZETU KAMA WATANZANIA. 78
7. JUBILEI NA CHANGAMOTO ZETU................................................ 86
Sehemu ya Tatu
TANZANIA TUNAKOKWENDA
8. JUBILEI NI KUANZA UPYA............................................................. 107
9. KANUNI YA TIBA MCHEPUO KWA MAENDELEO
YA TAIFA LETU..................................................................................... 133
TATHMINI NA MOTISHA..................................................................... 145
HITIMISHO.............................................................................................. 159
REJEA....................................................................................................... 169
PICHA YA JALADA LA KITABU NIMEIAMBATANISHA KAMA ATTACHMENT. UNAWEZA KUIDOWNLOAD NA KUIWEKA PIA.
MUHTASARI:
Ndugu Watanzania wenzangu, nimendika kitabu hiki kwa malengo matatu. Kwanza kitabu hiki kinalenga kupanua mawazo na mtazamo wetu Watanzania kuhusu dhana ya Jubilei ambayo sisi tunafanya kumbukumbu ya miaka 50 ya uhuru wetu yaani kujua kuwa nini tunatakiwa tufanye. Uelewa huu utakuwa wa msingi kwa kizazi kitakachofanya Jubilei ya miaka 75 au miaka 100 ijayo ya taifa letu. Tena, lengo la pili la kuandika kitabu hiki ni kutoa uelewa ambao utakuwa ni chagizo la mabadiliko, ukombozi na maendeleo kwa watu tulioamua kutafakari na kutenda kadiri ya ukweli kwa manufaa ya taifa letu katika kizazi hiki na kijacho wakati huu tunapofanya Jubilei ya miaka 50 ya uhuru wetu. Na zaidi, lengo langu la mwisho la kuandika kitabu hiki ni kuchukua wajibu kama Mtanzania wa kushirikisha mawazo yangu kwa  Watanzania wenzangu ili kuyatafuta maendeleo ya kweli ya taifa letu na zaidi sana ni kutoa mchango wangu katika sherehe hizi za taifa letu. Sikupenda sherehe kubwa kama hii ipite kama meli isiyoacha nyayo baharini.

Kitabu hiki kimegawanyika katika sehemu kuu tatu. Sehemu ya kwanza ni Tanzania - tulikotoka ambayo inaongelea masuala ya ukoloni, harakati za ukombozi, uhuru na maisha baada ya uhuru. Sehemu ya pili inaongelea Tanzania – tulipo inayozungumzia hali yetu leo kiuchumi, kisiasa na kijamii nikijadili changamoto zetu kama taifa na tunu zetu tulizonazo tangu uhuru mpaka sasa kama Watanzania na maana na umuhimu wa sherehe zetu za Jubilei ya miaka 50. Hatimaye, sehemu ya tatu, inazungumzia Tanzania – tunakokwenda (mwanzo mpya) ikijadili wapi tunakokwenda kama taifa yaani kuwa na mwanzo mpya na kuingalia kanuni ya tiba mchepuo kama nyenzo ya kutufikisha huko.  Kama yule mshairi na mtunzi wa vitabu wa Uingereza Robert Louis Stevenson alivyopata kusema kwamba, “Usipime siku yako kwa yale uliyovuna bali pima kwa yale uliyopanda.” Malengo hayo ndiyo yamenifanya nipande mbegu ya kitabu hiki kwa kuitakia mema nchi yangu kwa miaka 50 mingine.

Mwisho natabaruku kitabu hiki ni kwa heshima ya taifa langu Tanzania linalofanya Jubilei ya miaka 50 ya uhuru wake na kwa namna ya pekee Mama yangu mpendwa Christina Shija, baba yangu mpendwa marehemu Gabriel Kasembo, marehemu babu yangu Chifu Yohana Kilangabhana Kasembo, marehemu bibi yangu Agatha Mija Michael, Hayati Askofu Mkuu Anthony Mayala, Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Watanzania wote ninaochangia nao utaifa na nia njema ya kuitakia mema nchi yetu na zaidi wenye moyo wa dhati wa kujenga taifa la Tanzania lenye heshima, upendo, amani na maendeleo ya kweli na ya uhakika kwa kizazi hiki na kijacho! Nakutakieni usomaji mwema na mafanikio tele katika maadhimisho ya jubilei ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania huku tu tukifakari  uwepo, maisha na mustakabali wa taifa letu !

KWA KUAGIZA NAKALA YA KITABU HIKI ADIMU NA ADHIMU KWA TAIFA LETU, WASILIANA NA:

JOHN MTWALE KASEMBO
P.O BOX 22, PERAMIHO.
SIMU: 0755 417 074 / 0712 120 775

WANNE WAFA KATIKA MATUKIO MANNE TOFAUTI MKOANI RUVUMA

KAMANDA WA POLISI MKOA WA RUVUMA MICHAEL KAMUHANDA

Na Gideon Mwakanosya, Songea
WATU wanne wa Vijiji vya Litolongi na Minango  vilivyopo Kata ya Kigonsera Wilayani Mbinga na Mkaya kilichopo Kata ya Lituhi Wilayani Nyasa Mkoa wa Ruvuma  wamekufa katika Matukio matatu tofauti yakiwemo ya kupigwa na radi wakati mvua zikiwa zinaendelea kunyesha.
Wametajwa waliokufa kwa kupigwa na radi kuwa ni Manfred Komba (18) na Pascar Ndomba (33) wote wakazi wa Kijiji cha Minango Kata ya Kigonsera na mwingine ni Maria Kinunda (18) Mkazi wa Kijiji cha Litolongi Kata ya Kigonsera Wilayani humo na Martias Charle (52) Mkazi wa Kijiji cha Mkaya Kilichopo Kata ya Lituhi Wilaya mpya ya Nyasa ambaye alikutwa Porini akiwa amekufa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda alisema kuwa tukio la kwanza lilitokea January 27 Mwaka huu majira ya Saa 11 Jioni huko katika Kijiji cha Minango kilichopo Kata ya Kigonsera ambako Komba na Ndomba kabla ya kukutwa na mauti walikuwa shambani wakilima.
Alieleza zaidi kuwa wakiwa wanaendelea kulima Majira ya Saa 11 Jioni ghafla manyunyu ya mvua yalianza na baadaye Mvua kubwa iliongezeka huku ikiwa imeambatana na radi ndipo walipoamua kuacha kuendelea kulima kasha wakaanza kukimbilia kwenye kibanda kwa ajili ya kujificha mvua lakini kabla hawajafika kwenye kibanda hicho walipigwa na radi na kufa papohapo.
Kamuhanda alisema kuwa tukio jingine lilitokea January 27 mwaka huu Majira ya saa 12 Jioni huko katika Kijiji cha Litolongo Kata ya Kigonsera wilayani humo Maria alipigwa na radi na kufa papohapo wakati akikimbilia ndani ya Nyumba yake kujificha Mvua.
Alifafanua kuwa Maria mapema inadaiwa kuwa alikuwa akifanya shughuli zake nje ya nyumba yake na baadaye Mvua zilipoanza kunyesha ambazo ziliambatana na radi ndizo zilizosababisha kukatisha Maisha yake kwa kupigwa na radi na kufariki papo hapo.
Wakati huo huo  Matias Charle (52) Mkazi wa Kijiji cha Mkaya kilichopo Kata ya Lituhi Wilayani Nyasa ambaye anadaiwa kuwa alikuwa mgonjwa wa akili na ni mlemavu wa mikono na miguu alikutwa porini akiwa amekufa.
Alieleza zaidi kuwa Charle anadaiwa kuwa wakati wa uhai wake Oktoba mwaka jana alitoweka nyumbani kwake na kutokomea kusikojulikana na jitihada za kumtafuta zilifanywa bila kuwepo mafanikio na Juzi majira ya saa 9 alasiri alikutwa porini akiwa amekufa.
Mwisho.  

WATU SITA MBARONI KWA UPORAJI WA KUTUMIA BARUTI

KAMANDA WA POLISI MKOA WA RUVUMA MICHAEL KAMUHANDA

Na Nathan Mtega,Songea  
 
JESHI la polisi mkoani Ruvuma linawashikilia watu sita wanaodaiwa kuwa ni majambazi ambao walivamia nyumba mbili za wafanyabiashara wa kijiji cha Mkongotema eneo la Madaba Songea vijijini na kufanikiwa kupora zaidi ya shilingi milioni 415600 baada ya kufyatua milipuko mara nne hewani na kusababisha sintofahamu miongoni mwa wananchi wa kijiji hicho.
 
 Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda amesena kuwa tukio hilo lilitokea Januari 31 mwaka huu majira ya 7:30 usiku ambapo aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Baraka Bedo(25) mkazi wa Morogoro,Salum Ahmad(45) mkazi wa Mtwara na Stanley Mtega(20) mkazi wa Ludewa mkoani Iringa.
 
Wengine ni Peter Mbilinyi(35) mkazi wa kijiji cha Mkongotema,Mfaume Rashid(30) mkazi wa kijiji cha Hanga ngadinda na James Mtewele(21) mkazi wa kijiji cha Magingo wilayani Songea vijijini.
 
Alifafanua kuwa inadaiwa kuwa siku hiyo ya tukio watu wasiofahamika wakiwa na milipuko na mapanga waliivamia nyumba mbili ikiwemo ya Remigius Ngunja na Egno Mgeni na kufanikiwa kupora fedha taslimu kiasi cha shilini milioni 4.156.000 kabla ya uvamizi huo watuhumiwa hao inadaiwa kuwa walifyatua milipuko minne hewani na kumjeruhi Reimigius  kwa mapanga kichwani na mgongoni.
 
Alisema kuwa baada ya Remigius kupigwa alianguka na kuzirai ndipo mke wake Octaviana Danda walimuamuru atoe fedha huku wakimtishia kumkata mikono kwa kutumia panga walilokuwa nalo ndipo mke huyo alichukua shilingi milioni tatu na kuwakabidhi watu hao pamoja na simu mbili za mkononi.
 
 Kamanda kamuhanda alieleza zaidi kuwa baadae watuhumiwa hao walikwenda kwenye nyumba nyingine ya Egno Mgeni na kumkuta mlinzi wake Avito Mbilinyi na kumuaru awaonyeshe mahali alipo tajiri kisha walifyatua milipuko mitatu hewani na baadae walimkuta mkewe Mgeni na kumuuliza aliko mumewe ambaye alikataa kuonyesha mumewe alipolala na baadae walifanikiwa kumuona ndani ya nyumba na kumuomba awaonyeshe mahali alipo tajiri na mmiliki wa nyumba hiyo.
 
Alibainisha zaidi kuwa mmiliki wa nyumba hiyo hayupo kisha wakaenda kumvamia mkewe na kumuamuru atoe fedha ndipo alipowakabidhi shilingi milioni 1.126.000 na kisha wakatokomea na kwenda kusikojulikana.
 
 Kamuhanda alieleza kuwa polisi walipata taarifa ya tukio hilo kwa njia ya simu na kwenda eneo la tukio na baadae walisimamisha gari lenye namba za usajili T435 BHT Coaster ya abiria inayofanya safari zake kati ya Madaba na Songea mkoani humu ambao walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wa ujambazi watatu ambao ni Edo,Ahmad na Mtega.
 
Ambao walikutwa na kitambaa chenye damu,nguo zilizolowa damu milipuko,betri simu ya mkononi aina ya Nokia,fedha taslimu kiasi cha shilingi 758.000 pamoja na milipuko ambayo ilikuwa imeandaliwa kwa kuweza kulipuka muda wowote.
 
Amesema kuwa watuhumiwa wote wanatarajia kufikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.
 
Mwisho.