About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Saturday, November 19, 2011

NBC WATAMBA KUIFUNGA CRDB KATIKA MECHI YA KIRAFIKI INAYOCHEZWA LEO ASUBUHI KWENYE UWANJA WA MAJIMAJI

 Nahodha wa timu ya NBC Emmanuel Ntobi akitamba kuwashushia mvua ya magori watani wao wa jadi CRDB
 Kikosi cha timu ya NBC kinachopambana na CRDB leo asubuhi
 Nembo ya NBC ikiwa imewekwa kwenye uwanja wa Majimaji na kumaanisha kuwa ushindi ni lazima
 Kikosi cha timu ya CRDB kinachopambana na NBC leo kwenye uwanja wa Majimaji kikiwa kimetulia na kukwepa kutoa aina yoyote ya tambo na kusubiri dakika tisini uwanjani ndipo watasema jambo
Nahodha wa timu ya NBC Emmanuel Ntobi akitafakari jambo na mke wake Bi Sara kabla ya mechi kuanza katika uwanja wa Majimaji

MUASISI WA VURUGU NA MISA YA PILI KANISA LA ANGLIKANA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIEZI 12

            Askofu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya  Ruvuma Dk.Maternus Kapinga

NaThomas Lipuka,Songea.
MUASISI na kiongozi wa wakristo wa dhehebu la misa ya pili  wilayani Mbinga mkoani Ruvuma Joseph Lombola amehukumiwa kifungo cha miezi 12 kwa kosa la kufanya vurugu katika kanisa la Anglikana la Kristo Mfalme mjini Mbinga.
Lombola ambaye pia ni katibu wa Tume ya Utumishi ya Walimu (TSD) wilayani Mbinga ametiwa hatiani pamoja na  Martin Mawala aliyeachishwa upadre wa kanisa Anglikana kwa kutomtii Askofu wa Dayosisi ya Ruvuma.
Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Mbinga Frank Mahimbali akitoa hukumu alisema ameridhika na upande wa mashitaka kuwa washitakiwa bila uhalali walifanya vurugu wakati ibada ikiendeshwa na padre  Andrew Nkomola wa kanisa la Kristo Mfalme mjini Mbinga.
Kutokana na hali hiyo ,mahakama iliwatia hatiani hivi karibuni na kuwahukumu kifungo cha nje  cha miezi 12 kila mmoja na kwamba katika kipindi hicho  hawatakiwi kufanya kosa la aina yoyote.
Awali mwendesha mashtaka wa polisi Inspekta Isaya alidai washitakiwa  hao walitenda makosa hayo Agosti 16 ,2009 katika kanisa hilo ambapo washitakiwa waliingia kanisani na kwenda madhabahuni kisha waliondoa vitambaa,kutupa vitabu  vitakatifu na sakramenti takatifu jambo ambalo lilisababisha vurugu kutoka kwa waumini.
Habari   zaidi kutoka ndani ya kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma zinadai kuwa  Lombola ambaye hivi sasa anatumikia kifungo cha mwaka mmoja ndiye kiongozi wa kikundi cha kidini  kinachojiita Wakristo wa Misa ya Pili(SECT) ambacho kinaendesha shughuli zake mkoani Ruvuma bila uhalali wa  kisheria kwa kuwa hakina usajiri wowote.
Dhana ya Misa ya Pili  imetokana na ibada ya waumini ambao wamejitenga na  uaskofu wa kanisa la Anglikana hivyo hawana Askofu na bado walijiita waanglikana, wakalazimisha kufanya ibada zao katika makanisa ya uaskofu wa Ruvuma kwa kuvamia  makanisa na kujiita waumini wa misa ya pili.
Askofu wa kanisa Anglikana Dayosisi ya Ruvuma Dk.Maternus Kapinga  amesema amani ya kanisa hilo itaimarika zaidi baada ya kufungwa kwa muasisi wa SECT  ambaye alikuwa ni muhimili wa kikundi  cha Wakristo wa Misa ya Pili  ambao kazi yao kubwa ni  kulaghai,kuposha,kuharibu kanisa la Mungu na kuvuruga uongozi wa Askofu wa Ruvuma.
Kwa mujibu wa Askofu Kapinga waasisi,viongozi na wafadhili wakuu wa SECT ni wanasiasa,watu walioshindwa huduma takatifu  na watu wanaowania vyeo na mali katika kanisa hilo ambao wamejiengua kutoka katika kanisa hilo kwa madai  ya kutotaka kumtii Askofu wa Ruvuma wa awamu ya tatu.
Uchunguzi uliofanyika ndani ya Dayosisi hiyo  umebaini kuwa kikundi ambacho kinamkataa Askofu  na kujiita wakristo wa dhehebu la Misa ya pili ndani ya kanisa hilo ni wale wenye roho inayoongozwa na ukabila, chuki,  ulaghai, tamaa, wizi,  upinzani, uzushi, kiburi,ukengeufu na faraka.
“Lengo kuu la kikundi hicho ni kumwaga damu isiyo na hatia hasa wakidhamiria kumuondoa Askofu wa Ruvuma kutoa huduma takatifu aliyoitiwa na Mungu,mbinu kuu ambayo wanaitumia ili kutekeleza lengo hilo ni kupotosha na kutowaambia watu ukweli’’,alisema mkristo  ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini.
Mkristo huyo anabainisha zaidi kuwa kikundi hicho kinawashawishi watu wawafuate katika kumkataa Askofu wa Ruvuma na kwamba walifanikiwa kuanzisha vikundi katika maeneo ya Mbinga,Songea,Chiulu,Liuli na Puulu, vikundi ambavyo hivi sasa vyote vimekufa na wakristo wametubu na wamerudi kwa Askofu wa kanisa la Mungu.
Viongozi wa SECT ili kutimiza azima yao ya kulivuruga kanisa ,waliamua kuwa ajiri makasisi waliosimamishwa ili wawe viongozi wao wa kiroho.
Makasisi hao walisimamishwa kutoa huduma takatifu katika kanisa hilo baada ya kufanya makosa mabaya yakiwemo kuvunja ndoa, kutokutii mamlaka ya Mungu na kuishi na  vimada.
Askofu Dk.Kapinga anasema waumini wa dhehebu la Misa ya Pili   wamekuwa wakiigiza ibada zao kanisani na kwamba lengo lao halikuwa kumuabudu Mungu bali ni kuleta fujo ili ulimwengu useme Dayosisi ya Ruvuma ni yenye ni migogoro.
“Watu waliozuiwa kutoa huduma ya ukasisi katika kanisa hilo ,walikaidi amri hii ya Mungu na mamlaka halali ya kanisa,watu hao wakijua kuwa hawana mamlaka ya kasisi,lakini waliwadanganya watu  na serikali kwa kuwaibia malipo,mathalani kwa kufungisha ndoa bila kulipia kibali cha kufungisha ndoa’’,alifafanua Askofu Dk.Kapinga.
Kikundi cha  cha dhehebu la Misa ya pili kilijitokeza hadharani Desemba mwaka 2007  na hadi mwaka 2010 kikundi hicho kilikuwa kimemalizika na Dayosisi  ya Ruvuma kuwa katika hali ya amani na utulivu kutokana na juhudi zilizozaa matunda kwa ushirikiano baina ya waumini,uongozi wa kanisa  na viongozi wa serikali katika ngazi mbalimbali mkoani Ruvuma.
Takwimu  toka ofisi ya Askofu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma zinaonesha kuwa hadi kufikia Oktoba 31  mwaka huu kanisa hilo lina jumla ya waumini 41,000 ambapo dhehebu la Misa ya Pili lina waumini wasiozidi 50(hamsini)

WASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUKUTWA NA PURI 54 ZA BANGI KATA YA MSHANGANO

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda

Na Gideon Mwakanosya, Songea

JESHI la Polisi Mkoani Ruvuma linawashikilia watu watano wakikabiliwa na tuhuma za kukutwa na puri 54 za bangi ambayo ilikuwa ikiuzwa kwenye eneo la Mshangano katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda amesema kuwa tukio hilo lilitokea jana majira ya saa tatu asubuhi huko katika eneo la Mshangano Manispaa ya Songea ambako askari wakiwa doria walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao wakiuza wengine wakinunua bangi.

Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Kessy Mwegela (28) na  Jordan Juma (19) wote wakazi wa bombambili,wengine ni John Kanjoroka (26)  na Joseph Moyo wote wakazi wa eneo la Mshangano Manispaa ya Songea.

Amesema kuwa watuhumiwa hao baada ya kuona askari Polisi wakiwa wamewazunguka walitafuta njia ya kutaka kukimbia lakini Polisi walifanikiwa kuwatia mbaroni wakiwa na puri 54 kwenye mfuko wa Rambo na nyingine zilikuwa kwenye mifuko yao ya suruali walizokuwa wamevaa.

Amefafanua kuwa watuhumiwa hao kati yao ni wauzaji maarufu wa bangi katika Manispaa ya Songea na wengine ni wavutaji ambao walikuwa wamefika kwenye eneo hilo kwaajili ya kununua bangi.

Kamanda kamuhanda amesema kuwa polisi bado inaendelea kufanya upelelezi zaidi wa tukio hilo na kwamba utakapokamilika watuhumiwa watafikishwa Mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili.