About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Thursday, April 26, 2012

SHEREHE ZA UZINDUZI WA SONGEA GLOBAL NETWORK ZILIVYOFANA KATIKA UKUMBI WA AGOPAL

Katibu Mtendaji wa Songea Global Network John Kasembo akizungumza na mmoja wa wanachama wa mtandao huo

Kushoto ni Mtaalamu na mmiliki wa Kampuni ya kufunga Aluminium Songea Wailes Sebastian akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Elimark Eng.Co. Ltd Emanuel Nehemia Chapa

Mwenyekiti wa Songea Global Network Sakina Jamal akiwa na Mhasibu wa Mtandao huo Rehema Ayub wakati wa halfa ya uzinduzi wa mtandao huo
Miongoni mwa wanachama wa mtandao huo

Miongoni mwa wanachama wa Songea Global Network ambao walikuwa wanakamati wa chakula wakisubiri kuhudumia msosi

Mwenyekiti wa Songea Global Network Sakina Jamal akifungua mziki na mmoja wa wanachama wa Songea Global Network


Sasa ni kusaka lumba kwenda mbele na yeyote anayetaka kucheza kiduku ruksa

Mpaka kielewekeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

Mtandao wa Songea Global Network uwe chachu ya maendeleo
NA STEPHANO MANGO,SONGEA
WAHENGA walishanasihi kwamba, “Moyo usiokuwa na shukrani hukausha mema yote.” Hii inamaanisha kuwa tutakuwa wezi wa fadhila  kama hatutamshukuru sana Mwenyezi Mungu mwingi wa fadhili, rehema na mapendo kwa kutujalia sote uhai na afya na kutujalia nafasi hii adimu na adhimu ya kuandika na kusoma makala haya.
Nawashukuru wasomaji wote wa gazeti hili makini kwa kuendelea kulisoma na kutoa maoni yenu kwa mwandishi binafsi na wakati mwingine kwa viongozi wa Bodi ya Uhariri ili kuweza kuboresha kazi husika kwa lengo la kukidhi mahitaji ya wasomaji
Aprili 21 mwaka huu, nilialikwa kuhudhuria uzinduzi wa Mtandao wa Songea Global Network katika viwanja vya Hotel ya Agopal ambapo mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu ambaye aliwakilishwa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Seligius Ngahi.
Tukio hilo la kihistoria la uzinduzi wa mtandao lilihudhuriwa na watu wa kada mbalimbali lilikuwa ni mwanzo mpya wa wanachama wake kuifikia ndoto ya kuanzishwa kwake kwani walitaka, wakatakana na sasa hawana budi kuendeleza mipango waliojiwekea ili kuweza kuleta mafanikio waliokusudia toka awali wakati wanapanda mbegu ya kuanzisha mtandao huo.
Mtandao huo kama vilivyo vikundi vingine au chama chochote, una viongozi wake wakuu kwa maana ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mtendaji, Mhasibu na Kamati ya Utendaji, ambao watahakikisha malengo ya kuanzishwa kwa mtandao yanafikiwa kwa kushirikiana na wanachama wa mtandao huo.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mwenyekiti wa Songea Global Network (SGN) Sakina Jamal alisema kuwa malengo la kuanzisha mtandao huo ni kwanza, kusaidiana na kujaliana kwa shida mbalimbali mfano. Misiba, dharura.shida ni sehemu ya maisha ya binadamu.
Jamal alisema kuwa pili, kufahamiana na kupanua mtandao katika dunia hii ya utadawazi ambapo watu wanatafuta kuungana na kushirikiana katika maisha ya kila siku ,kwasababu ujifungia ni kuukumbatia umaskini wa mawazo na fikra.
Alisema tatu, kuwezeshana na kujengana kimawazo, kiushauri na kiuchumi, nne, kufunguliana  fursa za kusaidiana kadri ya utaalamu na kazi ya kila mmoja na tano, baadaye kuwa na SACCOS itakayotuwezesha kiuchumi: kuweka akiba, kukopa.
Alieleza zaidi kuwa hadi tunazindua rasmi mtandao unajumla ya wanachama 20 wakiwamo watu wa fani mbalimbali: wajenzi, mainjinia, mafundi, wahasibu, wanafunzi,madaktari, wajasiriamali, wafanyakazi wengine wa serikali.
Alisema ni mseto ulioiva wa wanachama wenye nia ya kushikamana na kutimiza ndoto ya mafanikio, udugu, ushirikiano na utajiri kwani tumedhamiria kuwa mbegu imara itakayoweza kutoa matunda stahiki katika siku za usoni kama tulivyojiwekea malengo, pia tunawakaribisha wanachama wapya kujiunga katika mtandao ili uwe na nguvu kubwa ,hivyo kwa yoyote yule anayetaka na kukubaliana na malengo tuliyojiwekea tunamkaribisha.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Songea Global Network John Kasembo akielezea historia ya kuanzishwa kwa mtandao huo wakati wa hafla ya uzinduzi huo alisema kuwa ,mtandao ulianza kama wazo la kukutana na kufanya hafla ya kuuaga mwaka 2011.
Kasembo alisema kuwa baada ya kukaa tukasema hapana, tulitajirishe wazo letu kwa kuanzisha mtandao utakao tuunganisha wote hata baada ya sherehe kama umoja wenye nia ya kusaidiana wakati wa shida na raha, kushauriana na kujengeana uwezo ili sote tufanikiwe.
Alisema baada ya majadiliano mapana na ya kina, tulikubaliana sote tuanzishe mtandao au umoja huo tukaupa jina la Songea Global Network (SGN) ambapo leo ndio siku tuliyokubaliana ya kupanda mbegu imara na safi ya mtandao huu ili umee na kuwa faida kwetu sisi wanachama na kuutangaza mkoa wetu wa Ruvuma kupitia mtandao wetu huu.
Alifafanua kuwa tulichagua jina hili SGN kwa sababu lina dhima ya kuunganisha watu wa kada mbalimbali bila kubagua umri, kazi, kabila, jinsia, rangi, dini wala itikadi. Anayekubali malengo yetu na kuwajibika kuchangia dira yetu, huyo ni mwanachama mzuri kwetu.
Alieleza zaidi kuwa leo tunavyopanda rasmi mbegu ya mtandao wetu (SGN), tunatumia fursa hii kukumbushana wanamtandao masharti ya kufanikiwa ili tuendelee mbele zaidi kufikia malengo na ndoto yetu ni kujitoa kweli,kupenda kweli mtandao,kuwa na ndoto na kutoa michango ya dhati bila kuchoka
Alisema kuwa ni kweli kuja pamoja ni mwanzo. Kufanya kazi pamoja ni umoja. Kudumu katika umoja ni maendeleo. Kuunganisha vipaji vyetu ni kuwa timu moja. Hatimaye kustahimili pamoja ni ushindi wa mtandao wetu huu.
Alieleza zaidi kuwa wanachama tukikaribisha upendo wa kweli tutafanikiwa katika malengo yetu na kutajirisha mtandao wetu kwa maendeleo ya mkoa wa Ruvuma, hivyo tunawajibika kutafakari na kuchukue hatua.
Alisema inapendeza, inakubalika, inawezekana na inahitajika kuwa na mtandao imara usiokatika network na kufanikiwa kweli. Ni kweli wahenga wa Ghana walishatuasa kwa methali yao kuwa, “Unaweza kumlaumu mtu kwa kukuangusha chini lakini ujilaumu mwenyewe kwa kukataa kunyanyuka.”
“Naomba wanamtandao tulioamua kuanzisha kwa hiari mtandao huu tusikalie kumlaumu mtu au kujilaumu wenyewe na badala yake tudhamirie na kuwa na bidii ya kunyanyuka leo na kuendeleza ndoto na mtandao wetu. Bila shaka linaloonekana haliwezekani litawezekana, milima isiyokweeka itakweeka na miti isiyopandika itapandika”alisema Kasembo.
Alisema kuwa tumuombe Mungu ili idumu, iote na ifanikiwe mbegu ya SGN ambapo sote tuchangie maendeleo yetu na ya taifa letu la Tanzania. Karibuni sote tufurahie jambo hili adhimu na tuchangie kila mmoja kwa nafasi na uwezo wake, kiushauri na kirasilimali aliyonayo kwa  mafanikio ya SGN.
Alisema kuwa wanachama tushikane mikono tuanze safari yetu kwa hatua ya kwanza leo, kwani hata Waswahili wanasema, “Safari ya maili elfu huanzia na hatua moja.” Na hakika ni kweli.  Tumethubutu kubuni na kuanzisha mtandao, tumeweza kuanzisha mtandao huu na sasa tunanuia kusonga mbele na mtandao tuliouanzisha.
Naye mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu  katika hotuba yake iliyosomwa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Seligius Ngahi alisema leo nashuhudia ndoto ikizaa jambo la uhalisia nayo ni Songea Global Network, nawapongeza sana kwa ndoto yenu, juhudi, nia na dhamira ya kuanzisha na kuendeleza mtandao wenu huu wenye malengo mliyojipangia ninyi wenyewe
Mwambungu alisema kuwa Chama au kikundi chochote cha watu hujengwa na mambo makuu matatu. Kwanza ni mahudhurio ya watu au wanachama, katiba na michango ya wanachama (rasilimali, ushauri, muda, fedha na nguvu).
Alifafanua kuwa kama mwanzo wa chama chenu napenda niwaombe tokea mwanzo kuwa kama mnanuia kweli ustawi, mafanikio na maendeleo ya mtandao wenu basi jibidisheni nyote kuhudhuria vikao bila kuchoka wala kudharau kwani mtu mmoja una thamani kwa mtandao huu.
Alisema tena jitahidini kuunda na kuwa na katiba imara itakayokuwa dira na mwongozo wa kufikia mafanikio ya malengo mliyojiwekea. Na Zaidi jalini na kujitoa sadaka nguvu, akili, utashi, rasilimali muda na michango yenu ya hali na mali katika kujenga, kukuza na kustawisha mtandao wenu. Haya kwenu ni ya msingi na ya kuzingatia kati ya mengi kama mnataka kuwa na mtandao imara na wenye nguvu.
“Nami najiunga rasmi katika mtandao pia naunga mkono jitihada mlizozianzisha kwa kutoa sh,300,000 ili ziwe chachu yaw engine kujitoa kwa lengo la kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake”alisema Mwambungu
Alieleza zaidi kuwa natambua kuwa mtandao ili uendelee mbele kuwa wenye nguvu, wenye mafanikio na watu wengi inapaswa kuutangaza, kuulinda, kuukuza, kuustawisha, kujivunia na kuufurahia. Tumieni fursa hii kufanya yale yote mtakayoona yanausaidia mtandao wenu kustawi na zaidi epukeni yale yote yanaweza kuvunja na kudhoofisha mtandao kama ubinafsi, dharau, chuki, fitina na majungu. Haya ni sumu kwenu!
Alisema kuwa leo mmeitangazia Songea, Ruvuma, Tanzania na dunia kuwa mna ndoto kubwa ya mafanikio. Kwa kawaida kuanzisha kazi ni rahisi kuliko kuiendeleza na kuimalizia. Mmeanza kwa kishindo, sasa msirudi nyuma. Daima kwenda mbele kwa kasi na viwango ili ndoto yeni itimie. Inawezekana, timizeni wajibu wenu.
Hakika wanamtandao wamethubutu,kubuni na kuanzisha mtandao, wameweza kuanzisha mtandao huu na sasa wanahitaji kusonga mbele ili uweze kuwa msaada wa ushauri, msaada wa kiuwezeshaji na msaada wa rasilimali watu wenye upeo na ndoto kwa mkoa wetu wa Ruvuma
Kuzaa si kazi, kazi ni kulea. Leeni mtandao huu uwe taa ya kutoa giza la umasikini na uwe chumvi ya kuleta ladha kwa mafanikio yenu na mkoa wa Ruvuma. Kama wengine waliweza kwanini nyie mshindwe?Hapana, kataeni msamiati wa kushindwa na siku zote neno msamiati wa kwanza uwe ni USHINDI DAIMA. Heri na mafanikio kwenu na Hongereni sana.Nyie mbele sisi nyuma
Mwandish wa Makala
Anapatikana 0715-335051
www.stephanomango.blogspot.com



WAKULIMA WALALAMIKIA KUTOZWA USHURU WA MAZAO TOKA SHAMBANI



                             
MKUU WA WILAYA YA TUNDURU JUMA MADAHA
Na Augustino Chindiye, Tunduru


WAKATI wakulima wa mazao ya Chakula Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wakilalamikia
kutozwa ushuru mkubwa kupitia vizuizi vilivyo wekwa na Wakala aliyeshinda zabuni ya kukusanya ushuru wa mazao ameahidi kuto msaidia mtumishi yeyote atakaye bainika kukiuka maelekezo yake.

Pamoja na kuitolewa kwa kauli hiyo Meneja wa kampuni ya StetyBussiness inayo kusanya ushuru huo katika halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Rashid Akbal aliwafananisha watumishi hao na mafisadi ambao wamekuwa wakiichafulia kasi ya Utendaji Serikali ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Kampuni yangu inafanya kazi kulingana na maelekezo tuliyosaini katika Mkataba na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya hiyo” alisema Akbal na akatumia nafasi hiyo kuwaomba wakulima watakao fanyiwa vitendo viovu na watumishi hao kutoa taarifa zenye ushahidi kwake ili waweze kuwawajibisha.


Akbal ambaye alikuwa akijibu swali la kwanini kampuni yake inatoza ushuru hadi wakulima wa kawaida wanaobeba kuanzia debe mbili aliendelea kueleza kuwa maelekezo yaliyotolewa kwa wafanyakazi wa
kampuni hiyo ni kutoza wafanyabiashara wanaonunua mazao ya wakulima tu na si kuwatoza hadi wakulima wanao rudisha mazao yao kutoka shambani.

Akizungumzia hali hiyo Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya hiyo Mary Ding`ohi mbali na kukiri kupokea malalamiko mengi juu ya tozo hizo alisema kuwa ofisi yake ina andaa utaratibu wa kumwita mzabuni huyo na kumpatia maelekezo upya zikiwa ni juhudi za kuondoa kero hiyo.


Alisema katika maelekezo ya awali mzabuni huyo alielekezwa kukusanya kiwango kisicho zidi asilimiaa 5% kutoka kwa wafanyabishara hao wa mazao ya Chakula na kwamba mkataba huo pia uliwaondoa katika tozo hiyo wakulima wanaorudisha mazao yao kutoka shambani baada ya kuyavuna.


Akizungumzia kero hiyo katibu wa Umoja wa Chama Cha wauzaji na wanunuzi wa mazao ya wakulima (WAMANATU) Wilayani Tunduru Athuman Milanzi alisema kuwa katika uchunguzi wao wamebaini kuwa kero hiyo inasababishwa na Mzabuni huyo kulazimisha kukusanya tozo hiyo kwa zaidi ya asilimia 5 iliyo kubaliwa katika mkataba wao.


Mwisho