About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Wednesday, April 11, 2012

WATANO WASHILIWA NA POLISI KWA KUKUTWA NA MBAO ZA POLINI KINYUME NA SHERIA

Na Stephano Mango, Songea
WATU watano wakiwemo askari watatu wa Idara ya Wanyama pori walioko kwenye Mbuga ya hifadhi ya Wanyama ya Taifa ya Serous Wilayani Namtumbo wanashikiliwa na Polisi Mkoani Ruvuma kwa tuhuma za kukutwa na mbao za mti pori 135 kinyume na sheria.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Michael Kamhanda alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 5 asubuhi huko katika Kijiji cha Likuyu Sekamaganga kilichopo kwenye eneo la Mbuga ya hifadhi ya Wanyama ya Taifa ya Serous Wilayani Namtumbo.
Aliwataja askari wa Wanyama pori wanaoshikiliwa na Polisi kuwa ni Godian Mataba (30),Michael Mrutu (29) na Fabian Paul (34) ambao wote ni askari wa Idara ya Wanyama pori kwenye Mbuga hiyo ya Wanyama.
Amewataja wengine kuwa ni Sebastian Matembo (30) na Juma Iddi (35) maarufu kwa jina la Kilaza wote wakazi Kijiji cha Likuyu Sekamaganga   ambapo alieleza zaidi kuwa watuhumiwa hao wote walikamatwa wakiwa na mbao 135 ndani ya kambi ya hifadhi ya wanyamapori ya Mbuga ya Serous bila kuwa na kibali.
Alifafanua zaidi kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio Katibu wa Hifadhi ya Maliasili Abeid Nihuka akiwa na askari wa wanyama pori wa Mbuga ya Serous walifanya msako mkali wa kuwabaini watu wanaoharibu mazingira ya Mali asili kwenye hifadhi ya Mbuga hiyo.
 Alisema kuwa askari hao wa wanyama pori wakiwa kwenye doria walifanikiwa kuzikuta mbao 95 zikiwa zimehifadhiwa ndani ya Kambi na mbao 40 zilikutwa nje ya eneo la Kambi kwa watuhumiwa wawili ambao ni Matembo na Iddi Wakazi wa Kijiji hicho.
 Hata hivyo alieleza kuwa watuhumiwa wote watano wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kukutwa na mbao za miti pori kinyume na sheria na kwamba kwa hivi sasa Polisi inaendelea na Upelelezi zaidi na ukikamilika watafikishwa Mahakamani kujibu shtaka linalowakabili.
 MWISHO