About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Thursday, December 29, 2011

MDAHALO WA WANANCHI NA VIONGOZI MBALIMBALI JIMBO LA SONGEA MJINI KUHUSU MAPITIO YA KATIBA UKUMBI WA KANISA LA BOMBAMBILI WAMALIZIKA NA SASA NI ZAMU YA JIMBO LA PERAMIHO





 Katibu wa Sonngo Mathew Ngarimanayo akizungumza katika mdahalo

 Mwanaharakati na Mwandishi wa Habari mkongwe Juma Nyumayo akifafanua jambo wakati wa mdahalo huo
 Mwanaharakati Fatuma Misango kulia na Ifigenia Mbawala wakifuatilia mdahalo huo
Mwenyekiti wa Mtandao wa Sonngo Siwajibu Gama akiwa na Katibu wa Mtandao huo Mathew Ngarimanayo
SONGEA NETWORK OF NON – GOVERNMENTAL ORGANIZATIONS
(SONNGO)
SLP. 791 SONGEA – RUVUMA TANZANIA
Simu Na:025- 2600877, Simu ya kiganjani: 0754-533032, 0752 - 202117
Baruapepe: sonngosongea @yahoo.Com
Ofisi – Barabara ya Sokoine Jengo la CCM Mkoa

                 
HISTORIA YA KATIBA TANZANIA
 NA MICHAKATO YA UANDIKAJI WAKE


1.0.   MAANA YA KATIBA
Wanazuoni, wanaharakati, wadau, wabia wa maendeleo na wananchi mbalimbali wanaielezea Katiba kwa mitazamo tofauti kutokana na mandhari na matumizi yake katika jamii.  Hata hivyo makundi yote hayo wanaielezea Katiba kuwa ni:-

·        Waraka wa Kisiasa, Kiutawala na Kisheria ambao unawawezesha wananchi kujitambua kama Taifa, unaelezea mgawanyo wa madaraka na majukumu ya vyombo mbalimbali vya dola na kuongoza shughuli zote kisheria ambao ndio chimbuko la sheria zote nchini.

·        Pia Katiba ni muafaka wa Kitaifa na ni mkataba kati ya viongozi na wananchi.

2.0.         MISINGI NA SIFA YA KATIBA.
                                                          i.            Katiba lazima iwezeshe wananchi kuridhiana kitaifa.
                                                       ii.            Wananchi kuwa na nguvu ya kumiliki Katiba yao.
                                                     iii.            Katiba kuwa ya kipekee kutokana na historia ya nchi hisika.
                                                     iv.            Katiba kuwa na nguvu ya kisheria inayozingatia haki za binadamu, haitoi mwanya wa ubaguzi wala upendeleo wa aina yoyote.
                                                       v.            Katiba lazima itoe maono na mwelekeo wa Taifa.
                                                     vi.            Katiba lazima iweke bayana masuala ya msingi ya kitaifa na mustakabali wake.

3.0.         KATIBA ZILIZOTANGULIA TANGU UHURU
Tangu Tanganyika na Zanzibar zipate Uhuru na kuungana kumekuwa na Katiba 5 za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba kadhaa za Zanzibar.  Kwa upande wa Zanzibar tunagusia kwa muhtasari Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na marekebisho ya 10 ya Katiba hiyo ya mwaka 2010.

Katiba zilizotangulia tangu Uhuru ni hizi:-

3.1.         KATIBA YA UHURU (1961)
·        Katiba hii iliundwa kwa lengo la kuipatia Tanganyika Uhuru wake toka kwa Waingereza, ndio maana ikaitwa Katiba ya Uhuru.
·        Katiba hii iliundwa Uingereza na kuileta Tanganyika.
·        Katika uandikaji wake Katiba hii haikushirikisha wananchi wa Tanganyika.
·        Katiba hii ilimtambua Waziri Mkuu ambaye hakuwa na madaraka makubwa kwani yeye alikuwa anasimamia masuala ya serikali bungeni tu.
·        Malkia wa Uingereza bado alikuwa na madaraka makubwa kwani maamuzi mengi yalikuwa yanamtegemea Malkia.
·        Katiba hii haikutambua haki za binadamu.
·        Hata hivyo baadhi ya mambo mazuri yaliyokuwamo katika Katiba ya Uhuru ni kwamba:-
                                                         i.            Katiba ilitoa Uhuru wa Mahakama.
                                                       ii.            Baraza la Mawaziri na Waziri mmoja walikuwa wanawajibika kwa Bunge.

3.2.         KATIBA YA JAMUHURI (1962)
·      Katiba hii iliitwa Katiba ya Jamuhuri kwa sababu ndiyo iliyoanzisha mfumo wa Urais.
·      Mchakato wa kuiandika kwake haukushirikisha wananchi.
·      Bunge la wabunge 71 wa TANU walijigeuza kuwa Bunge la Katiba na kuipitisha Katiba hii.
·      Katiba hii ilimtambua Rais kuwa mkuu wa Nchi na kiongozi wa serikali.
·      Baraza la mawaziri na Waziri mmoja mmoja sasa walikuwa wanawajibika kwa Rais.
·      Rais wan chi alikuwa na nguvu nyingi sana.
·      Sheria nyingi zilitungwa chini ya Katiba hii na nyingi zilikuwa kandamizi.

3.3.         KATIBA YA MUUNGANO (1964)
·        Katiba hii iliundwa baada ya Tanganyika na Zanzibar kuungana na kuwa nchi moja. 
·        Katiba hii ilisimamia mambo 11 ya Muungano na mambo ya Serikali ya Tanganyika.
·        Katiba hii iliweka muundo wan chi wa serikali mbili (Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar)
·        Katiba hii ilimtambua Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano na mjumbe wa baraza la mawaziri.
·        Katiba hii ilianzishwa kwa tamko la Rais na kuridhiwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la wawakilishi Zanzibar.
·        Katiba hii ilikuwa ya muda ya Muungano na ilikusudiwa kutumika kwa muda wa mwaka mmoja tu.
·        Katiba hii iliweka utaratibu wa wa kuandaa Katiba ya kudumu ya Muungano kwa kuunda tume ya Katiba na bunge la Katiba ili kuhakikisha ushiriki wa wananchi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

3.4.         KATIBA YA MPITO (1965)
·        Katiba hii iliitwa ya mpito.
·        Katiba hii ndio iliyoitambua nchi kuwa ni ya chama kimoja tu cha siasa (TANU kwa upande wa Tanganyika na ASP kwa upande wa Zanzibar).
·        Katiba hii ndiyo iliyotamka rasmi chama kushika hatamu kuu ya TANU (NEC) ilikuwa na nguvu zaidi kuliko bunge au hata Katiba yenyewe.
·        Katiba hii ilipitishwa kama sheria ya kawaida inavyopitishwa bungeni.
·        Katiba ya TANU ilikuwa sehemu ya Katiba ya Muungano.
·        Katiba hii iliongeza mambo ya Muungano.
·        Utata wa Uhuru wa Muungano (autonomy) kuwa nchi ulionekaka dhahiri.
·        Tume ya Rais ya Katiba ya kukusanya maoni kwa wananchi iliundwa.

3.5.         KATIBA YA KUDUMU (1977)
·        Katiba hii iliitwa Katiba ya kudumu.
·        Katiba hii ilikuwa ya Tano.
·        Uandikaji wa Katiba hii haukushirikisha wananchi.
·        Katiba hii ilipatikana kupitia tume ya Rais yenye wajumbe 20 (10     
     toka  Tanzania bara na 10 toka Tanzania Zanzibar).
·        Tume hii ya Rais iliongozwa na Sheikh Thabita Kombo na Katibu wa tume alikuwa ndugu Pius Msekwa.
·        Kabla ya kuandika Katiba ya kudumu, tume hii ilianza kuandika Katiba ya CCM baada ya kuunganisha vyama vya TANU na ASP tarehe 5/2/1077.
·        Katiba ya kudumu ilijikita katika misingi mikuu mitatu yaani:-
                                                       i.            Urais wenye nguvu zaidi.
                                                     ii.            Mfumo wa chama kimoja.
                                                  iii.            Mfumo wa serikali mbili.

·        Katiba ya kudumu ilipitishwa kwa Rais kuliteua Bunge la kawaida kujigeuza kuwa bunge la Katiba na kupitisha Katiba ndani ya masaa matatu tu.

4.0.         MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 1977
·        Katiba ya kudumu ya mwaka 1977 imefanyiwa mabadiliko 14 na kwa kiasi kikubwa mabadiliko hayo yamewakwepa wananchi, isipokuwa mabadiliko ya mwaka 1984 ambayo yaliwashirikisha wananchi.
·        Badala ya NEC kufanya maamuzi ilianzisha mjadala wa mwaka mmoja wa wananchi na kuiagiza serikali kutekeleza.
·        Baadhi ya mapendekezo ya wananchi yalikuwa ni:-
                                                                   i.            Hati ya haki za binadamu.
                                                                 ii.            Kujitawala kwa Zanzibar ambayo haikuwemo kwenye mapendekezo ya chama.
·        Mwaka 1991 Rais mstaafu Hassan Mwinyi aliteua tume ya   
                          kuangalia hali ya kisiasa nchini.  Tume hii iliongozwa na                                      
                          marehemu Jaji Francis Nyalali.
·        Tume hii pamoja na mambo mengine ilipendekeza kufutwa kwa sheria kadhaa kandamizi na kufanyia mabadiliko Katiba ya Muungano nay a Zanzibar.
·        Mwaka 1988 iliundwa tume nyingine iliyoongozwa na Jaji Robert Kisanga ambayo nayo pia ilitoa mapendekezo yake mengi kuhusiana na masuala ya kisiasa nchini.

4.1.         MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 1979.
·        Mabadiliko haya yalilenga kuanzisha mahakama ya Rufaa nchini yaani kwa Muungano na Zanzibar.

4.2.         MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 1980
·        Mwaka 1980 Katiba ya kudumu ya mwka 1977 ilifanyiwa mabadiliko mara mbili kwa malengo tofauti tofauti:-
                                                             i.      Mabadiliko yalifanywa kwa lengo la kuimarisha Muungano
     kwa kujibu masuala ya Zanzibar.
4.3.         ii. Kuweka mfumo wa uchaguzi wa Rais wa Zanzibar.
·        Kuweka mfumo wa Serikali ya Zanzibar.
·        Kuweka muundo wa Baraza la wawakilishi Zanzibar.
4.4.         MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 1982
·        Mabadiliko haya yalilenga uteuzi wa wakuu wa mikoa ingawa hayakuweka uwajibikaji wa wakuu wa mikoa na Wilaya.

4.5.         MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 1984
·        Mabadiliko haya yalilenga kuingiza masuala ya haki za binadamu kwenye Katiba ya nchi.

4.6.         MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 1990
          Mwaka 1990 Katiba ya kudumu ilifanyiwa mabadiliko mara mbili kwa lengo la :-
·        Kuanzisha Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995.

4.7.                                 Kuweka utaratibu wa kupata mgombea mmoja wa Urais kwa Zanzibar.

4.8.         MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 1992
          Mwaka 1992 yalifanyika mabadiliko ya Katiba mara mbili kwa malengo ya :-
·        Kufuta mfumo wa chama kimoja nchini.
·        Kuanzisha mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini.
·        Kubadilisha mfumo wa bunge la Jamuhuri ya Muungano na kuanzisha viti maalum vya wanawake kufikia 15% na viti 5 toka baraza la wawakilishi.
·        Yalianzisha uandikishaji wa vyama vya siasa na uteuzi wa wagombea kupitia vyama vya siasa.


4.9.         Miezi sita baadae baada ya kufanyika kwa mabadiliko ya nane ya Katiba
          yalifanyika mabadiliko mengine yaliyolenga:-
·        Kubadilisha utaratibu wa uchaguzi wa Rais.
·        Nguvu ya Bunge ya kumuondoa Rais madarakani kwa kupiga kura ya kutokuwa na imani naye iliwekwa.
·        Ilianzisha nafasi ya Waziri Mkuu na uwezo wa Bunge wa kumuondoa madarakani kwa kupiga kura ya kutokuwa na imani naye.
·        Masharti ya Rais kulivunja Bunge yaliwekwa.

4.10.    MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 1993
·        Mabadiliko hayo yalifanywa kwa lengo la kuzifanya chaguzi za Madiwani, Wabunge na Rais kufanyika kwa pamoja.
·        Mabadiliko hayo pia yaliipa nguvu “Tume y Taifa ya Uchaguzi” kisimamia chaguzi za Madiwani, Wabunge na Rais.

4.11.    MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 1994
·        Mabadiliko hayo yalikuja kutokana na mapendekezo ya Tume Paul Boman.
·        Mabadiliko hayo ndiyo yaliyomtambua mgombea mwenza wa Urais wa Jamuhuri ya Muungano ambaye angekuwa Makamu wa Rais.
·        Mabadiliko hayo ndiyo yaliyofuta Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano.
·        Mabadiliko hayo yaliendelea kumtambua Rais wa Zanzibar kuwa mjumbe katika baraza la mawaziri la Jamuhuri ya Muungano.

4.12.    MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 1995
·        Mabadiliko haya yalifanyika mwaka 1995 kabla ya kuvunja bunge.
·        Mabadiliko haya yalifanywa kwa lengo la :-
                                                       i.            Kumtaka Rais wa Jamuhuri ya Muungano na Makamu wake, Waziri Mkuu na Rais wa Zanzibar kula kiapo cha kuulinda Muungano.
                                                     ii.            Mabadiliko haya pia yaliweka ukomo wa muda wa Urais wa kukaa madarakani kuwa ni awamu mbili za miaka mitano mitano.

4.13.    MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 2000
·        Mabadiliko haya yalifanywa baada ya uchaguzi wa kwanza kwa mfumo wa vyama vingi na baada ya kuwasilishwa kwa ripoti ya Jaji Robert Kisanga.
·        Mabadiliko hayo yalilenga:-
                                                       i.            Ilifafanua kura za ushindi wa Rais sio lazima awe ameshinda kwa 51% na zaidi bali Rais atatangazwa kuwa mshindi kwa uwingi wa kura.
                                                     ii.            Mabadiliko haya yalimpa uwezo Rais wa kuteua watu 10 kuwa wabunge wa Jamuhuri ya Muungano.
                                                  iii.            Mabadiliko hayo pia yaliongeza idadi ya viti maalum vya wanawake toka 15% hadi 20%.

4.14.    MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 2005
·        Mabadiliko haya yalifanywa kwa lengo la:-
                                                       i.      Kuongeza idadi ya viti maalum vya wanawake toka 20% hadi 30% .
                                                     ii.      Uhuru wa kuabudu.
                                                  iii.      Uhuru wa kushiriki na watu wengine katika kujieleza.
                                                  iv.      Utaratibu wa kuteua wabunge wa viti maalum kwa wanawake kutegemea na uwiano wa ushindi katika uchaguzi.

5.0.         KATIBA YA ZANZIBAR YA MWAKA 1984
·        Mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 yaliyofanyika mwaka 2010 yameleta maswali mengi kwa Watanzania kwani kwa kiasi kikubwa yamegusa sana masuala ya Muungano, hivyo tunaweza kusema Muungano umetikisika kwani:-
                                                 i.            Yameitambua Zanzibar kama nchi na mipaka yake, bendera na vikosi vyake.
                                               ii.            Yamempa nguvu Rais wa Zanzibar  kuigawa Zanzibar kama Wilaya na mikoa kinyume na ilivyokuwa awali ambapo walikuwa wanashauriana na Rais wa Jamuhuri ya Muungano.
                                            iii.            Yamempa nguvu Rais wa Zanzibar ya kuteua wakuu wa mikoa na Wilaya.
                                            iv.            Yameipa Zanzibar Mahakama ya Rufaa ambalo lilikuwa suala la Muunano hapo awali.
                                               v.            Yameongeza idadi ya viti maalum vya wanawake na kuwa 40% ambapo Muungano ni 30%.
                                            vi.            Yamemtaja Rais wa Zanzibar kuwa ni mkuu wan chi.
                                          vii.            Yameanzisha makamu wawili wa Rais ambapo Katiba ya Jamuhuri ya Muungano haiwatambui.  Katiba ya Jamuhuri ya Muungano inawatambua Rais wa Zanzibar na Waziri Kiongozi.
                                       viii.            Yameweka wigo wa baraza la wawakilishi kutochezea na kubadilisha Katiba ya Zanzibar na hasa sehemu inayohusu tamko la haki za binadamu na ibara ya kwanza nay a pili mpaka kura ya maoni ipigwe.

6.0.         KWA NINI KATIBA MPYA SASA
·        Watanzania wengi wanajiuliza swali hili, kwa nini Katiba mpya sasa?  Lakini jambo la maana zaidi ni pale tunapowaona watanzania wanajibu swali hili ingawa kwa mtazamo tofauti tofauti.
·        Hizi nitakazozitaja hapa chini ni sababu chache zinazitajwa na watanzania walio wengi kuwa ndizo sababu hasa zinazopeleka Taifa kwenye utungaji wa Katiba mpya.  Sababu nhizo ni pamoja na:-
                                           i.            Katiba za awali hazikushirikisha wananchi hivyo Katiba hizo hazikutokana na matakwa ya wananchi.
                                         ii.            Katiba ya mwaka 1977 imefanyiwa mabadiliko mengi (14) hivyo ni dhahiri imepoteza sifa za kuitwa Katiba ya kudumu.
                                      iii.            Marekebisho ya 10 ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
                                      iv.            Mfumo wa kisasa nchini wa vyama vingi vya siasa, kwani Katiba iliyopo ilitungwa kipindi cha mfumo wa chama kimoja cha siasa.
                                         v.            Kuweka sawa swala nyeti na muhimu la Muungano maana kuna mkanganyiko kati ya serikali na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali ya Zanzibar, suala hili linatakiwa liwekwe vyema katika Katiba mpya.

7.0.         MCHAKATO WA KUTUNGA KATIBA MPYA
Kuna njia mbalimbali za kutunga/kuandika katiba mpya nchini, lakini wanazuoni na wananchi walio wengi wanapendekeza njia/mchakato ufuatao kama nitakavyoeleza hapo baadae.

·        Nchi yoyote inaingia kwenye machafuko ya kivita kwa kuwa wananchi wake wanakosa jukwaa la kujadili na kukubaliana namna bora na inayofaa ya kufanya michakato mbalimbali inayohusu maamuzi wan nchi zao na namna bora ya kutumia rasilimali zao, hioy ikiwa ni pamoja na suala hili tunalozungumzia la uandikaji/utungaji wa Katiba mpya.

·        Wananchi kama Taifa ni muhimu na ni vema wakubaliane namna mchakato wa kuandika Katiba mpya utakavyokuwa.

·        Baadhi ya njia/mchakato wa kuandika Katiba ambao unapendekezwa na wanazuoni na wananchi mbalimbali mchakato ambao unatoa fursa kwa wananchi wote kushirikikatika hatua zote za uandikaji wa Katiba mpya ni huu

                                                          i.            Mijadala ya awali ya Katiba.
·        Hii ni hatua ya awali kabisa ambapo wananchi wanapata fursa ya kuibua, kujadili na kukubaliana mambo ambayo wanataka yazingatiwe katika Katiba mpya.  Hili laweza kufanyika katika mikutano ya vijiji, kata na mikusanyiko ya ibada.

                                                       ii.            Mkutano Mkuu wa kitaifa.
·        Mkutano huu utajadili mambo yaliyoibuka katika majadiliano ya makundi, kuyachambua na kuyapanga katika mafungu mambo yanayojadilika, kwa mfano mambo yanayohusu haki za binadamu, rasilimali za nchi, mgawanyiko wa madaraka na
masuala ya kubishaniwa (contentious issues).  Mkutano huu unatakiwa uhusishe uwakilishi mpana wa makundi mbalimbali ya wananchi.

Inashauriwa wajumbe wa mkutano huu wachaguliwe na wananchi kama sheria itakavyoelekezwa kwa lengo la kujenga muafaka wa kitaifa kuhusu masuala muhimu.

                                                     iii.            Tume ya wataalamu wa Katiba (Constitutional commission)
·        Hii ni hatua ambapo tume ya wataalamu wa Katiba na sheria itateuliwa.  Kazi ya tume itakuwa ni kuratibu maoni ya wananchi na kuyaweka katika waraka maalum na kuhamasisha wananchi.

·        Tume hii ya wataalamu wa Katiba na sheria inapendekezwa iteuliwe na Rais na kuthibitishwa na Bunge la Jamuhuri ya Muungano ambalo litawawakilisha wananchi.

·        Tume hii inapendekezwa kuwa na wataalam wa kada mbalimbali na izingatie usawa wa kijinsia.

                                                  iv.                  Mjadala wa waraka maalum wa Katiba.
·        Matokeo ya kazi ya tume ya wataalam yatawekwa katika waraka maalum wa Katiba kwa ajili ya mjadala mpana zaidi wa wananchi juu ya yaliyomo.

                                                     v.                  Bunge maalum la Katiba (constituent Assembly)
·        Rasimu ya Katiba ikishaandaliwa ipelekwe mbele ya Bunge maalum la Katiba.

·        Bunge hili maalum la Katiba liundwe kwa utaratibu maalum tofauti na bunge lililopo la Jamuhuri ya Muungano.


·        Bunge hili maalum la Katiba liwakilishe makundi mbalimbali kama vile wanawake, wanaume, walemavu, wakulima, wafanyakazi, wafanyabiashara, vyama vya wafanyakazi, asasi za kiraia, madhehebu ya dini mbalimbali na kadharika.

·        Kazi kubwa ya bunge hili ni kupitia na kuridhia rasimu ya Katiba iliyoandaliwa.
·        Bunge maalum la Katiba litakoma mara tu baada ya kuridhia rasimu hiyo ya Katiba.

                                            vi.      Kura ya maamuzi (Referundum)
·              Baada ya rasimu ya Katiba kuridhiwa na Bunge maalum la Katiba, hatua ya mwisho katika kupata katiba mpya ni kwa wananchi kushiriki kwa njia ya kura ya maamuzi.

·              Kura hii itapigwa nchi nzima na wananchi wote wenye na sifa za kupiga kura watapiga kura.


·              Endapo kura za ndio kwa Katiba zitazidi zile za hapana Katiba itakubalika na kuanza kutumika/kufanya kazi.


AHSANTE SANA KWA KUNISIKILIZA NA KARIBU KWA MAJADILIANO.