About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Monday, February 6, 2012

WATOTO YATIMA WANAOSOMA SEKONDARI TUNDURU WAKOSA CHAKULA


                            MKUU WA WILAYA YA TUNDURU JUMA MADAHA

Na,Augustino Chindiye Tunduru
ZAIDI ya Watoto yatima 3000 wanaosoma katika Shule za Sekondari na Msingi Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma wamelalamika kukosa huduma ya chakula ambacho hutolewa katika shule hizo kutokana na wao kutochangia fedha za kuchangia ili kuwawezesha kupata huduma hiyo.

Wakiongea kwa nyakati tofauti wanafunzi hao wamesema kuwa toka shule zifunguliwe mwanzoni mwa mwaka huu ambapo wanafunzi hao wamekuwa hawaruhusiwi kunywa uji wala chakula cha mchana kama ambavyo wanafunzi wenzao hupewa huduma hiyo.

Katika taarifa hiyo wanafunzi hao walisema kuwa hali hiyo mbali na kuonekana kuwa wanabaguliwa lakini kitendo hicho kimekuwa
kikiwakatisha tamaa ya kuendelea na masomo katika shule zao.

Aidha wanafunzi hao walidai kuwa kitendo hicho cha viongozi wa Shule kuwabagua kupata huduma hiyo pia kimewasababisha kuonekana kwa tabaka la Watoto hao wasio na Wazazi na walezi kunyanyaswa na wanafunzi wenzao hali inayotishia kulididimiza kundi hilo kitaaluma.

Alipotakiwa kuzungumzia hali hiyo Afisa Elimu Shule za Sekondari
Wilayani humo Ally Mtamila mbali na kukiri kuwepo kwa changa moto hiyo alisema kuwa ipo haja ya kuboreshwa kwa taarifa za Watoto hao hasa kwa wasio kuwa na Walezi wa kuwahudumia ili wanapo pangiwa Shule vigezo vyao viwawezeshe kupangwa katika Shule za Bweni ambazo chakula chao hutolewa na Serikali.

Upande wa afisa maendeleo ya jamii wa Wilaya hiyo Mary Ding`ohi alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo mbali na kukiri kuwepo kwa kero hiyo alisema kuwa tatizo hilo limetokana na kuchelewa kwa fedha za kuwaghalamia wanafunzi hao.

Alisema hata hivyo tayari idara yake imekwisha pokea kiasi cha Shiligi Milioni 35.763 ambazo kati yake Tsh. 15,976,000 zimepangwa kughalamia malipo ya Ada, kununua sare za Shule na Michango hiyo ya Chakula kwa Watoto 3215 wanaosoma katika Shule hizo.

Ding`ohi aliendelea kufafanua kuwa Fedha hizo ambazo kila
mwanafunzi yatima amepangiwa kulipiwa Tsh. 70,000 kwa mgawanyo wa Tsh.20,000 za Ada na Tsh.50,000 kama mchango wa chakula kwa mwaka mzima fedha hizo zimepangwa kulipwa kuanzia Wiki ijayo.

Mwisho