About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Monday, March 5, 2012

WALIMU WAMCHARUKIA MWAJIRI WAO WILAYANI TUNDURU

Mkurugenzi wa Halmashauri Wilaya yaTunduru
                 Efraim Ole Nguyaine

Na, Steven Augustino Tunduru

CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) Wilayani Tunduru kimesema kuwa hivi sasa kimeanza kukosa imani na utendaji kazi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshuri ya wilaya hiyo ambaye ndiyo mwajiri wa Wanachama wake.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Chama hicho Wilayani humo Mwl. Razalo Saulo wakati akiongea na Walimu walioandamana hadi katika ofisi za chama hicho kwa nia ya kukitaka chama hicho kimshinikize mwajiri huyo ili awalipe stahili zao hizo.

Alisema kitendo cha kuchelewa kulipwa kwa madeni hayo kinatokana na Mwajiri huyo kutoonesha nia ya wazi katika ufuatiliaji wa Madai ya Malipo yanayo tokana na Mishahara kutoka hazina huku madeni hayo yakiwa tayari yamekwisha hakikiwa huku kukiwa na taarifa kuwa Wilaya zote zimekwisha lipa madeni hayo.

Akifafanua taarifa hiyo Mwl. Saulo alisema kuwa hadi Chama hicho kinaanza kupoteza imani na Mwajiri huyo Wanachama wake ambao wamekuwa wanaishi maisha ya kubahatisha na kusumbuka kwa muda mrefu wakidai
jumla ya Shilingi Milioni 268,524,643/= kwa Walimu 378 kuanzia mwaka
2008/ 2011.

Mwl. Saulo aliendelea kueleza kuwa awali walimu hao walikuwa wanadai jumla ya Shilingi Milioni 390,879,514/= na kwamba toka walilipwa
Shilingi Milioni 122,354,871 zilizo tokana na Madeni ya Uhamisho,Likizo,Matibabu na Gharama za Masoni juhudi za ufuatiliaji na
upelekaji wa taarifa za madeni ya deni lililo bakia umekuwa ukilegalega hali inayo kitia mashaka chama.

Alisema hayo yamebainika kuwa kila anapo kwenda ofisini kwa ajili ya ufuatilia majibu huwa ni taarifa zote zimekwisha tumwa, huku kukiwa
hakuna maelekezo ya wala takwimu zinazo onesha kuwa madai hayo yametumwa lini na yalitumwa kwanani hali ambayo inaonesha kuwepo kwa ubabaishaji wa utendaji kazi.

Aidha katika taarifa hiyo pia Mwl. Saulo akabainisha kuwepo kwa changamoto Mbalimbali zikiwemo za wanachama wake kuzubaishwa kutokana na kupewa hamisho zinazo tokana na majungu na uonevu wa baadhi ya wakuu wa idara ambao wamekuwa wakitaka kuabudiwa na watumishi walio chini yao hali ambao imekuwa ikiendelea kuisababishia Serikali mzigo wa madeni yasiyo kuwa ya lazima.

Changamoto nyingine iliyo bainishwa na Katibu huyo ni pamaja na wanachama wake kukosa imani na watumishi wa idara inayo simamia na
kutunza nyaraka za watumishi ambao wanadaiwa kuwa wamekuwa na tabia ya kuchomoa baadhi ya taarifa na kufanya kurudiwa mara kwa mara zoezi la uhakiki.

Akijibu kero hiyo Mbele ya Walimu hao Kaimu Mkurugenzi wa Halmashuri ya Wilaya hiyo Mwl. Rashi Mandoa mbali na kukiri kuwepo kwa deni hilo alisema kuwa siyo kweli ofisi yake haishughuliki madai ya walimu wake.

Mwl Mandoa alliendelea kueleza kuwa  hivi sasa Mkurugenzi Mtendaji mwenyewe Efraim Ole Nguyaine yupo Jijini Dar es salaam kwa ajili yua ufutiliaji wa kina ili kulitatua kabisa tatizo hilo na
kuondokana na mgogoro na walimu hao.

Mwisho