About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Monday, February 13, 2012

WAANDISHI WA RUVUMA PRESS CLUB WAKUTANA KUJADILIANA MAREKEBISHO YA KATIBA YAO

Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Ruvuma Press Club Andrwe Kuchonjoma, Katibu wa Ruvuma Press Club (katikati) wakiendesha kikao cha mabadiliko ya katika katika ukumbi wa ushirika juzi
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Ruvuma Press Club wakijadiliana jambo, kutoka kulia ni Alpius Mchucha, wa pili Crecencia Kapinga, wa tatu Mpenda Mvula na wanne Julius Konala
Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Revocatus Kassimba akiwa na Mweka Hazina wa Ruvuma Press Club wakati wa kikao cha mabadiliko ya Katiba

Waandishi wa Habari wa Ruvuma Press Club wakiendelea kuchangia mabadiliko ya katiba yao

Kutoka kulia ni Christian Sikapundwa, Gideon Mwakanosya na Thomas Lipuka

Kutoka kushoto ni Judith Lugome, Adam Nindi, Gerson Msigwa, Mark Mapunda, Catherine Nyoni

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL KUFANYA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU NNE MKOANI RUVUMA


MKUU WA MKOA WA RUVUMA SAID THABIT MWAMBUNGU
Na Stephano Mango,Songea
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Mohamed Gharib Bilal anatarajia kufanya ziara ya  kikazi ya siku nne mkoani Ruvuma  kuanzia kesho  jumanne (leo) hadi  februari 17 mwaka huu siku ya ijumaa
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ukumbi wa Maliasili Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu alisema kuwa Makamu wa Rais Dkt Bilal atawasili uwanja wa ndege wa Songea majira ya saa tano asubuhi na kupokelewa na viongozi wa chama na Serikali mkoa wa Ruvuma ambapo ataveshwa skafu na kukagua vikundi vya ngoma uwanjani hapo
Mwambungu alisema kuwa akitoka uwanjani hapo, Dkt Bilal atapokea taarifa ya maendeleo ya Mkoa na taarifa ya Chama tawala mkoa katika ikulu ndogo mjini Songea ambapo pia siku hiyo atatembelea, kukagua na kupata taarifa ya kituo cha hifadhi ya chakula kisha kuweka jiwe la msingi ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Songea na kuwasalimu wananchi
Alisema siku ya jumatano Dkt Bilal ataelekea Wilaya ya Namtumbo ambako atapewa taarifa ya mradi wa Uranium wa Mkuju unaofanywa na Kampuni ya Mantra, atakagua eneo la mradi na kuzungumza na waananchi wa Likuyusekamaganga ambao wanazunguka eneo la mradi kisha kurudi mjini Songea kuzungumza na Halmashauri kuu ya Ccm Mkoa
Alieleza kuwa siku ya Alhamisi Makamu wa Rais Dkt Bilal ataelekea Wilaya ya Mbinga na kupokelewa na viongozi wa Wilaya Kitai Gerezani na kupewa taarifa ya maendeleo ya Wilaya na kukagua shamba la mbegu bora, kisha ataelekea kukagua na kupata taarifa ya mradi wa uchimbaji wa makaa ya mawe Ruanda na kuelekea Mbinga mjini kuzindua mashine za kuzalisha umeme
Alieleza zaidi kuwa siku ya ijumaa Makamu wa Rais Dkt Bilal atafanya majumuisho ya ziara yake Mkoa wa Ruvuma katika ukumbi wa Umati Wilayani Mbinga na kuondoka kuelekea uwanja wa ndege wa Songea ili kuagana na viongozi wa Chama na Serikali na kuondoka kuelekea Mkoa wa Rukwa kwa ajiri ya majukumu mengine
Aliwataka wakazi wa Mkoa wa Ruvuma kujitokeza kwa wingi kumpokea mgeni huyo kama ilivyo tamaduni za mkoa huo wa kuwapokea wageni kwa amani, upendo na ukalimu
MWISHO