Na Steven Augustino, Tunduru
SERIKALI imehaidi kubadilisha mfumo wa usambazaji wa pembejeo za ruzuku zikiwa ni juhudi za kumsaidia mkulima wa chini na kuhakikisha kuwa huduma hizo haziwanufaishi wajanja wachache.
Hali hiyo imetokana na kubainika wazi kuwa mfumo wa sasa wa kusambaza pembejeo hizo kwa kutumia mfumo wa vocha umekuwa ukiwanufaisha Mawakala na baadhi ya viongozi na watendaji wa vijiji, Kata ambao hushirikiana na maafisa tarafa wasio waaminifu.
Hayo yamebainishwa jana na Viongozi waandamizi wanaosimamia mfuko wa Vocha za Ruzuku Taifa, Afisa Kilimo Wizara ya Kilimo na Chakula anayesimamia sehemu ya Pembejeo na Flora Kumalilwa na Mkufunzi Mkuu wa Kilimo Sehemu ya Pembejeo Stella Mtagwaba wakati wakiongea na kamati ya Usimamizi wa usambazaji wa Pembejo Wilayani Tunduru
katika kikao kilichofanyika katika Ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo.
Wakifafanua taarifa hiyo walisema kuwa utaratibu huo mpya ambao kwa sasa unafanyiwa kazi na wataalamu umetokana na idara hiyo kupokea mapendekezo megi kutoka kwa wadau wa Kilimo wakiitaka idara hiyo kufanya mabadiliko katika mfumo huo huku wakibainisha kuwa mfumo uliopo sasa wa kugawa Pembejeo kwa wakulima umekuwa hauna manufaa kwa
walengwa kutokana na kuwepo kwa mianya inayolenga kuwanufaisha wajanja wachache kwa kuuza vocha hizo kwa mawakala.
Sambamba na matarajio hayo ya kubadilisha mfumo huo pia viongozi hao walikiri kuwepo kwa mapungufu makubwa ya ucheleweshaji wa utengenezaji na usambazaji wa Vocha kwa wakulima,kuchelewesha fedha za usimamiaji wa usambazaji wa vocha hizo kwa wakulima na ukubwa wa bei ya vocha Changamoto ambazo walidai kuwa hivi sasa zinafanyiwa kazi kwa makini ili kuziondoa kabisa kero hizo kuanzia mzimu ujao.
Aidha katika taarifa yao pia pamoja na mambo mengine viongozi hao waliipongeza kamati ya kusimamia usambazaji wa Pembejeo Wilayani humo kwa kufanya kazi vizuri kuanzia ngazi ya uteuzi wa mawakala wa kusambaza pembejeo hizo na kwamba hali hiyo imetokana na baadhi ya
wakulima waliotembelea katika vijiji vya Nandembo, Nanguinguru, Lelolelo na Azimio.
Walisema katika mahojiano kati yao na wakulima hao pamoja na mambo mengine yakiwemo malalamiko ya ukubwa wa bei ya vocha hizo na ucheleweshaji wake wakulima wa maeneo hayo walikiri kupokea vocha hizo na kuzitumia kulingana na maelekezo kutoka kwa mabwana shamba na wakadai kupata mafanikio makubwa kwa kuvuna kati ya magunia 26 na 28 kutoka magunia kati ya magunia 4 na 8 kabla ya mfumo huo kwa ekari moja.
Wakichangia katika kikao hicho kwa nyakati tofauti Mbunge wa jimbo la Tunduru Kusini Alhaji Mtutura Mtutura, Afisa kilimo waWilaya Jalia Msangi na Afisa kilimo wa Wilaya hiyo Chiza Marando mbali na kuipongeza serikali kwa kubuni mfumo huo unaolemga kuwanufaisha wakulima hasa wasio na uwezo waliiomba Serikali kuendeleza juhudi hizo kwa kuanza kuwawezesha kwa kuwakopesha zana za Kilimo yakiwemo Matrekta zikiwa ni juhudi za kuwaongezea uwezo wakulima hao.
Mapendekezo mengine yaliyo tolewa na viongozi hao ni pamoja na kuiomba Serikali kufanya mikataba ya bei ya pembejeo hizo na Mawakala wakubwa mapema ili kuwadhibiti wasipandishe bei ya soka kwa pembejeo husika na kama ambaavyo wamekuwa wakifanya sasa na kusababisha mfumo huoo kuonekana hauna maana wala manufaa kwa walengwa kutokana na bei za Vocha na Ruzuku inayo tolewa na Serikali kutowiani kwa Asimia 50% kwa
50% na bei za soko la mbolea hizo.
Wakizungumzia mfumo wa vocha walidai kuwa pamoja na sifa ilizopata Wilaya yao katika usimamiaji wa ugawaji wa vocha za Ruzuku lakini wamekuwa wakipambana na changamoto mbalimbali zikiwemo za kuzushiwa kashfa kuwa mawakala wanaoteuliwa hupatikana kwa kutoa Rushwa.
Awali akifungua kikao hicho kaimu Afisa tawala wa Wilaya ya Tunduru, Afisa Tarafa wa Tarafa ya Mlingoti Manfredi Kahobera Hyera alieleza kuwa mambo ambayo huzingatiwa katika uteuzi wa Mawakala wa kusambaza Pembejeo za Kilimo kwa mfumo wa Vocha ni kuangalia na kuwachuja kwa makini baada ya kuwabaini Mawakala wasio waadilifu na wenye nia ya kuchakachua vocha bila kupeleka huduma kwa wanufaika.
Katika taarifa hiyo ya Kahobera aliwataja mawakala waliobainika kuchakachua vocha hizo kuwa ni Michael Mdete ambaye pamoja na kukosa duka la kuuzia Pembejeo hizo lakini alikosa sifa kutokanan na kesi zao zinazoendelea mahakamani baada ya kubainika kuchakachua kwa kugushi na kujipatia Vocha wakati akiwa hajatoa huduma husika kwa wakulima.
Mwisho