About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Friday, December 9, 2011

TEMBO WAVAMIA KIJIJI TUNDURU NA KUWAJERUHI WATU WAWILI

Na Steven Agustino, Tunduru
WATU wawili wakazi wa kitongoji cha Chipweteka katika kata ya Mlingoti Mashariki Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma Mussa Zubery (36) na Chuma Ramji(25) wamelazwa wakiwa hoi bini taabani katika Hospitali ya Serikali ya Wilaya hiyo baada ya kujeruhiwa vibaya na kundi laTembo lililovamia kijiji chao.

Mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa majeruhi hao walipatwa na mkasa huo baada ya kuvamiwa na kundi la Tembo hao ambao wamekuwa wakizagaa hovyo katika eneo la kitongoji hicho na vijiji jirani wakati wakienda mashambani.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Goerge Chiwango alisema kuwa hali za wagonjwa ni mbaya na kwamba Hospitali yake inatarajia kuwapeleka katika Hospitali ya Missioni ya Ndanda kwa matibabu zaidi.

Dkt. Chiwangu aliendelea kueleza kuwa majeruhi Mussa Zubery aliumizwa vibaya katika Mguu wa kushoto ambao pamoja na kuvunjwa mara mbili na Tembo huyo pia nyama za paja lake ziliondolewa kabisa katika tukio hilo pamoja na kuvunjwa mkono wake wa kushoto.

Kuhusu hali ya majeruhi Chuma Ramji Dkt. Chiwango alisema kuwa hali yake ni mbaya pia kutokana na kuvunjwa mguu wa kulia na tembo hao hali inayo wasukuma kuwahamisha majeruhi hao wote na kuwapeleka katika Hospitali ya Missioni baada ya wataalamu wa  Hospitali yake kushindwa kuwahudumia.

Akizungumzia tukio hilo Kaimu wa kaimu Afisa maliasili wa Wilaya ya Tunduru Abdalah Mbanganike mbali na kukiri kuwepo kwake alisema kuwa tayari amekwisha peleka askari wenye silaha kwa ajili ya kuwasaka Tembo hao ili kuepusha matukio ya aina hiyo kwa wananchi wengine.

Aidha Mbanganike alitumia nafasi hiyo kuwaomba Wananchi wa Wilaya hiyo kutoa taarifa za matukio ya uharibifu wowote ambao umekuwa ukisababishwa na Wanyama ili waweze kupatiwa msaada kabla ya kupatwa na madhara.

Alisema idara yake inazo Bunduki na Risasi za kutosha pamoja na askari wenye ujuzi wa kutosha katika matumizi ya Silaha hizo wakati wa mapambano dhidi ya wanyama hao waharibifu.

 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma  Michael Kamuhanda amedhibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kueleza kuwa Jeshi la Polisi lipo tayali kwenda kutoa msaada katika idara hiyo endapo wataombwa kufanya hivyo.
Mwisho.

WAHITIMU WA VETA KUPEWA KIPAUMBELE CHA AJIRA KWENYE MGODI WA URANI

Mkurugenzi wa  Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Kanda ya Nyanda za juu kusini Monica Mbelle

Na Joseph Mwambije ,Songea
SERIKALI  Mkoani Ruvuma imesema itatoa kipaumbele  katika kutoa ajira  kwenye mgodi wa madini ya Urani  yanayotarajiwa kuanza  kuchimbwa hivi karibuni kwa Wahitimu wa Chuo cha mafunzo ya ufundi stadi(VETA) cha Songea Mkoani Ruvuma baada ya utafiti wa madini hayo kukamilika.
 
Msimamo huo wa Serikali  ulitolewa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu kwenye  Mahafali ya 26 ya VETA Songea kupitia hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo  Saveli Maketa  ambaye aliwataka Wazazi kuwapeleka  watoto wao katika Chuo hicho  na kusema kuwa ukisomea ufundi huwezi kukosa kazi.
 
‘Vyuo vya  mafunzo ya ufundi stadi vina umuhimu mkubwa katika kipindi hiki ambacho ajira zimekuwa zikitatiza lakini pamoja na kusumbua kwa ajira lakini ufundi umekuwa ukiwafanya watu wachomoze na kufanikiwa kimaisha’alisema.
 
Kutokana na umuhimu huo alisema Serikali imepanga kujenga Vyuo vya ufundi stadi kila Wilaya ili kutoa nafasi kwa vijana wengi zaidi kupata ujuzi  na kujiajiri na kwa kujiunga na Vyuo hivyo alisema wanaweza kupambana na umaskini.
 
Aliwataka wahitimu 52 kati yao wavulana 42 na wasichana 10 wa fani za aina mbalimbali waliosoma kwa miaka mitatu Chuoni hapo kwenda kutumia ujuzi walioupata kulijenga Taifa  na kujiunga kwenye Vikundi vya maendeleo na Vyama vya akiba vya kuweka na kukopa(SACCOS) ili waweze kupata mitaji ya kununulia vitendea kazi.
 
Alilisisitiza kuwa  wahitimu wa VETA na Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla watapatiwa kipaumbele kwenye ajira katika mgodi wa Urani uliopo Namtumbo Mkoani humo ambao utakuwa mmoja wa migodi mikubwa duniani na kwamba utafiti wa madini hayo umeshakamilika na yataanza kuchimbwa hivi karibuni.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa  Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Kanda ya Nyanda za juu kusini Monica Mbelle aliwataka wazazi kuachana na dhana potofu kwamba ufundi ni kwa wavulana tu na kuwapeleka watato wa kike Chuoni  hapo.
 
Aliwataka wahitimu kwenda kufanya kazi ya kusaidia  jamii na kwamba kwa kutokufanya hivyo watakuwa hawajalitendea haki taifa lao kwa kuwa Serikali imetumia gharama kubwa kutoa mafunzo hayo huku ikitoza pesa kidogo.
 
MWISHO

MAKAMANDA WA CHADEMA MJINI SONGEA WAMPONGEZA MBUNGE REGIA MTEMA NA KATIBU WA JIMBO LA KAWE POWEL MFINANGA KWA KUJA SONGEA NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI KATIKA MKUTANO WA NDANI NA WA HADHARA KATIKA MASUALA NYETI YA TAIFA IKIWEMO MABADILIKO YA KATIBA,MIAKA 50 YA UHURU,UFISADI NA UBADHILIFU WA MALI ZA UMMA

 Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Regia Mtema akizungumza na Kamanda wa chama hicho Ntobi Emmanuel kwenye viwanja vya Songea Girl kabla ya kuanza safari yake ya kurudi jijini Dar Es Salaam kwa majukumu mengine
 Katibu wa Chadema Jimbo la Kawe Powel Mfinanga akipokelewa na Kamanda Willy Nestori kwenye eneo maalumu la kuagana lililoandaliwa na makamanda wa chama hicho mjini Songea


 Katibu wa Chadema Jimbo la Kawe Powel Mfinanga,Mbunge Regia Mtema na Emmanuel Ntobi wakiendelea kuzungumza masuala ya taifa kwa maslahi ya watanzania kupitia CHADEMA
Hayo nayo yanaendelea kusumbua vichwa vya wadau mbalimbali wa masuala ya DINI,UTAMADUNI wa mwafrika,tuendelea kutafakari kwa kina uamuzi wa jamaa huyo alioweka bango hilo kwenye gari yake na kauli zinazoendelea kutolewa na wababe wa DUNIA,Je Baraka Obama ambaye ni Mwafrika mwenzetu ametusaliti au vipi?

WAANDISHI WA HABARI WA VYOMBO MBALIMBALI WAKIENDELEA KUPATA MLO KUTOKA KWA MAMA LISHE FULANI SIKU YA UHURU

Kutoka kushoto ni Julius Konala(Radio Maria)Joseph Mwambije aliyesimama(Majira) Emmanuel Msigwa(Chanel Ten)Nathan Mtega(Nipashe na Redio One) Alpius Mchucha ambaye ni Diwani wa Kata ya Suluti,Wilayani Namtumbo

MIAKA 50 INAYODAIWA KUWA NI YA UHURU CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WAZEE ZIMETATULIWA?

Mzee ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja ikiwa amebeba vikapu akiviuza kandokando ya Soko kuu mjini Songea

REGIA MTEMA ATEMA CHECHE KWENYE MKUTANO WA HADHARA MJINI SONGEA

Mbunge wa Viti Maalum Chadema Regia Mtema akiwahutubia mamia ya wakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma kwenye Viwanja vya Soko la Samaki la Zamani Mfaranyaki ambapo aliwataka wananchi kutambua umuhimu wa kudai Katiba Mpya kwa maendeleo ya Watanzania wote badala ya kuendelea kukabali ubakaji wa demokrasia unaoendelea kufanywa na Serikali katika harakati za mchakato wa kuandaa Mswada wa mabadiliko ya Katiba mpya 2011 uliosainiwa na Rais Kikwete hivi karibuni

Mtema alisema kuwa Katiba iliyopo imechoka na ndio imelifikisha Taifa hapa lilipo na kusababisha upatikanaji wa viongozi wabovu wenye kila aina ya uchafu ambao wamekuwa wakiwadharau wananchi wazi wazi na kuwatengenezea mazingira ya kuendelea kuwa maskini huku wao wakiishi peponi kwa kutumia kodi za wananchi

Alisema amewashangaa wabunge wa CCM kwa kitendo chao cha kuipuuza Katiba ambayo waliapa kuilinda kwa kuwanyima haki wananchi ya kujadili na kutoa maoni yao kuhusu Katiba Mpya ambayo inahitajika kwa ajili ya watanzania wote na sio ya Rais Kikwete na Chama chake

Amewataka wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wabunge wa Chadema kwa kuidai katiba mpya toka wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2011 hadi sasa wanapopinga sheria ya mabadiliko ya Katiba Mpya  yenye vipengele katili iliyopitishwa na Rais Kikwete hivi karibuni kwani vinamapungufu mengi ambayo yasiporekebishwa basi Katiba ijayo itakuwa mbovu kuliko iliopo sasa

Alisema kuwa Taifa linadai kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru ambao haueleweki katika vichwa vya watu na hauna mantiki yoyote kwani uhuru unaodaiwa wa miaka 50 ya Tanzania haupo kwasababu Tanganyika ilipata Uhuru Disemba 9,1961 ambapo Tanzania haikuwepo,sasa huo uhuru unaodaiwa upo wapi

Aliendelea kusema kuwa maadhimisho hayo yameghalimu mabilioni ya Shilingi kutokana na kodi za wananchi ambao wanaishi kwenye lindi la umaskini huku wakidhurumiwa haki zao na Serikali na kwamba amewataka wananchi kuipuuza Serikali ya CCM kwani ndio inayowamaliza watanzania kila siku

Alieleza kuwa Serikali inafanya sherehe hizo za uhuru hewa huku watanzania wanakufa kwa kukosa dawa katika vituo vya afya,wengine wanakufa kwa kukosa chakula,wengine kwa kupigwa mabumu na risasi na Serikali kwa lengo la kuwanyima haki muhimu za binadamu ikiwemo kujieleza,kupata malipo yao kutoka na kazi zao, kutaka maeneo ya kufanyia shughuli zao na mambo mengine kadha wa kadha


                Mamia ya wananchi wakisikiliza mkutano huo
 Wananchi wakiwa wamekaa juu ya kijiwe cha CCM huku wakiwa wamechoka wakisikiliza mapungufu ya Sheria ya kuandaa mchakato Katiba Mpya iliyosainiwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete kutoka kwa Mbunge Regia Mtema hayupo pichani
 Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Ruvuma ,Diwani wa Kata ya Mjini na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa CCM Joseph Fuime (kulia) akiwa na Katibu wa Chadema Jimbo la Kawe Powel Mfinanga (kushoto)wakimsikiliza Mbunge Regia Mtema hayupo pichani
 Viongozi wa Chadema wakionyesha ishara ya kuichinja CCM kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2014 na uchaguzi Mkuu mwaka 2015,wa kwanza kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Songea na Diwani wa Kata ya Majengo Idd Abdalal,Katibu wa Chadema Mkoa wa Ruvuma Dorphin Ghazia,Katibu wa Jimbo la Kawe Powel Mfinanga,Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Ruvuma na Diwani wa Kata ya Mjini na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa CCM Joseph Fuime,
 Mbunge wa Viti Maalum Chadema Regia Mtema akiendelea kutema cheche mjini Songea

 Katibu wa Jimbo la Kawe Powel Mfinanga akizungumza na mamia ya wananchi wa Songea katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho ambapo aliwataka wananchi kukiamini chama cha CHADEMA kwani ndio chama mbadala kitakachoweza kuwavusha wananchi toka hapa walipo kwenda mbali zaidi katika masuala ya jamii,miundombinu,afya,elimu,maji kwa kuzitumia vizuri rasilimali za taifa kwa maendeleo ya wote

Alisema CCM kwa kushirikiana na Rais Kikwete wameshindwa kuwafikisha watanzania kule waliko waahidi mara baada ya kushika dola mwaka 2005 na mwaka 2010 kwani akili zao zimefika mwisho wa kufikili na zimeganda na ndio maana hata wenyewe wametambua hilo kwa kuiga sera za CHADEMA na kushindwa kuzitekeleza kutokana na kuganda kwa akili zao

Alisema CCM haistahili kuendelea kuitawala Tanzania kutokana na kuwapeleka watanzania motoni kutokana na kusababisha gharama za maisha kupanda,thamani ya shilingi kushuka,kutokuwepo kwa elimu bora,miundombinu bora,huduma bora za maji,afya na mambo mengine

Alieleza zaidi kuwa Rais Kikwete amekuwa bingwa wa kutengeneza kashfa akiwa madaraka kwani yeye amekuwa Rais wa kwanza kupigwa mawe akiwa Mbeya,wa kwanza kudondoka jukwaani,wa kwanza kuwadanganya wananchi,wa kwanza kuvutwa mguu akiwa jukwaani na mtoto,wa kwanza kutukanwa na Uingereza,wa kwanza gari zake kuchakachuliwa mafuta,wa kwanza kukabidhi cheki ikiwa na maneno tofauti na talakimu,Rais wa kwanza kukabidhi gari kwenye halmashauri isiyostahili,wa kwanza kutoa ahadi nchi nzima akiwa kwenye Kampeni,wa kwanza kutumia fedha nyingi za Serikali kwa kusafiri nje,kufanya sherehe nyingi kwa kudi za watanzania,wa kwanza kusaini miswada ya gharama za uchaguzi na wa mabadiliko ya katiba mpya huku akijua mapungufu yaliyoko,wa kwanza kuwamwagia maji ya upupu wazee wa jumuiya ya Afrika Mashariki na wa kwanza kutoa matamko mengi yasiyo na utekelezaji,wa kwaza kwa kucheza kiduku kwa mbwembwe kwenye sherehe mbalimbali za Kitaifa na kijamii

"Rais ambaye kila kukicha anatengeneza rekodi mbaya za utendaji kama anavyofanya Kikwete astahili kuwa kiongozi hata wa familia yake kwani watoto wakishafahamu uwezo mdogo wa baba yao wa kiuongozi kamwe hawatamuheshimu,Urais ni taasisi nyeti kitaifa hivyo kuendelea kuwachagua watu walioganda akili watateketeza vizazi viliopo na vijavyo"alisema Mfinanga

Alisema kuwa Serikali ya Kikwete imedhihirisha kuganda kwa akili kwani kila mpango wanaoubuni ukiwemo wa ujenzi wa Sekondari za kata,kilimo kwanza imeferi licha ya kutumia fedha nyingi za wananchi na nguvu kazi,hivyo watanzania wanatakiwa kuendelea kujitokeza kwa wingi kwenye mikutano ya CHADEMA ili kujiandaa kuchukua nchi kwenye chaguzi zijazo


Katibu wa Jimbo la Kawe Powel Mfinanga akiendelea kuwashushia NONDO wananchi ili waweze kuanza harakati za kuiondoa CCM madarakani katika chaguzi zijazo kwa kutumia nguvu ya umma kwa ustawi wa Taifa la Tanzania ambalo limesimama kiuchumi,kiutamaduni,kijamii,kielimu,kiafya na huduma zingine muhimu

ASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMUUA MKEWE NA KUMTUNDIKA KWENYE MTI AKIDAI AMEJINYONGA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda
Na Mwandishi Wetu,Songea
JESHI la Polisi Mkoani Ruvuma linamsaka Omary Almasi Mkazi wa Kijiji cha Pacha nne kilichopo katika Kata ya Nakapanya Wilayani Tunduru kwa tuhuma za kumuua mke wake wakiwa shambani kisha kumtundika juu ya mti akisingizia kuwa mkewe amejinyonga.
Habari zilizopatikana jana mjini hapa ambazo zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Michael kamuhanda zimesema kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 1 mwaka huu majira ya saa 8.10 mchana huko katika Kijiji cha Pacha nne.
Kamuhanda amemtaja mwanamke aliyeuawa na mume wake kuwa ni Somoe Mastawi (48) Mkazi wa Kijiji cha Pacha nne Wilayani Tunduru.
Amefafanua kuwa inadaiwa siku hiyo kabla ya tukio hilo kutokea Omary na mke wake Somoe waliondoka nyumbani kwao na kuelekea shambani kulima shamba la Mahindi na baadae majira ya saa nane na dakika kumi katika hali ambayo siyo ya kawaida Somoe alianza kupata kipigo kutoka kwa mume wake na kumsababishia kifo.
Amesema kuwa mwanamke huyo Somoe aliuwawa na mume wake wakiwa Shambani na baada ya kumfanyia kitendo hicho cha kinyama mke wake alichukua kamba na kumfunga shingoni kisha alimtundika juu ya mti mrefu kwa kusingizia kuwa mwanamke huyo amejinyonga.
Kamanda Kamuhanda ameeleza zaidi kuwa Omary baada ya kugundua kuwa watu wameshafahamu kuwa kitendo hicho cha kinyama amekifanya alikimbia na kutokomea kusikojulikana na kwamba Polisi bado wanachunguza chanzo cha tukio hilo huku wakiendelea kumsaka mtuhumiwa.
 TUKIO LINGINE………………………………….
Na Mwandishi Wetu,Songea

AFARIKI DUNIA BAADA YA KUDONDOKEWA NA KIFUSI KWEMYE SHIMO ALILOKUWA AMELALA
SELEMANI Yahaya  (30) Mkazi wa Mtaa wa Mkuzo Kata ya Mshangano katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoa wa Ruvuma amekutwa akiwa amekufa kwenye shimo alikokuwa akilala kila siku baada ya kufukiwa na kifusi cha mchanga wakati mvua zikiendelea kunyesha.
Akizungumza na Mtandao wa www.stephanomango.blogspot.com jana Ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda amesema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa za usiku huko katika Mtaa wa Mkuzo uliopo Kata ya  Mshangano.
Amefafanua kuwa siku hiyo ya tukio Said Yassin Mkazi wa eneo la Mtaa wa Mshangano akiwa anapita akitokea Mjini kuelekea nyumbani kwake aligundua kuwa kwenye shimo alilokuwa akilala Yahaya limefukiwa na kifusi kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha.
Alisema kuwa Yassin baadaye alikwenda kwa majirani na kuwajulisha kuwa shimo ambalo alikuwa akilitumia Yahaya  kwa kulala limebomolewa na mvua na wananchi walipofika kwenye eneo hilo waligundua kuwa Yahaya amefukiwa na kifusi .
Alieleza zaidi kuwa Uongozi wa Serikali ya Mtaa kwa kushirikiana na Wananchi wa eneo hilo walifanya jitihada za kutoa taarifa Polisi na baadaye walianza kazi ya kufukua shimo hilo na kumkuta Yahaya akiwa tayari amekwisha kufa.
Kamanda Kamuhanda amesema kuwa inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo marehemu wakati wa uhai wake alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa akili ambao ndio ulimsababishia kulala kwenye shimo hilo.
TUKIO LINGINE…………………………….
Na Mwandishi Wetu, Songea
MWANAMKE AFA BAADA YA KUPIGWA NA RADI AKITOKEA SHAMBANI KWAKE 
AMINA Mstafa (45) Mkazi wa Matarawe katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma amekufa papo hapo baada ya kupigwa na radi wakati akiwa njiani anatoka shambani huku akiwa amevaa shingoni simu yake ya mkononi iliyokuwa imefungwa kwa kamba.
Akizungumza na www.stephanomango.blogspot.com jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 8 mchana huko katika Kijiji cha Mrogoro kilichopo eneo la Peramiho Wilaya ya Songea Vijijini.
Kamuhanda amesema kuwa Amina kabla ya kukutwa na mauti alikuwa anatoka shambani kwake kulima shamba la  mahindi na alipofika njiani mvua zilizokuwa zimeambatana na radi zilianza kunyesha.
Ameeleza zaidi kuwa Amina akiwa anaendelea na safari yake ya kurudi nyumbani kwa mguu huku akiwa amevaa shingoni simu yake ya mkononi iliyokuwa imefungwa kwa kamba ghafla radi ilimpiga na kumsababishia kifo papo hapo.
Amefafanua kuwa baada ya radi kumpiga Amina na kumsababishia kifo watu waliokuwa njiani walikwenda eneo la tukio kisha walitoa taarifa kwa Serikali ya Kijiji na baadaye Polisi ambao walifika kwenye eneo la tukio wakiwa wameongozana na Mganga ambaye alithibitisha kuwa Amina tayari alishakufa muda mrefu kwa kupigwa na radi.
 MWISHO