About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Saturday, April 28, 2012

WAWILI WAFA PAPO HAPO NA WATATU WAJERUHIWA VIBAYA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda
Na Gideon Mwakanosya, Songea
WATU  wawili wamefariki dunia na wengine watatu akiwemo dereva wa gari hilo  wamejeruhiwa vibaya mkoani Ruvuma baada ya kugongwa na gari katika  eneo la Mahenge katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea baadaya ya kugongwa na gari la Jeshi la wananchi (JWTZ)  la Makao makuu ya brigedi Chandamali
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Michael  kamuhanda amesema kuwa tukio hilo limetokea  majira ya saaa mbili na nusu asubuhi huko kwenye barabara ya Songea na Namtumbo ambapo aliwataja waliokufa kuwa ni Stumai Moyo (20) na Tabia Bilali (23) wote wakazi wa eneo la Mahenge wa Songea mjini na walio jeruhiwa vibaya ni Amina Moyo (2) na Issa Moyo (65) wote wakazi wa Mahenge ambao baada ya kutokea ajali hiyo walikimbizwa katika Hospitali ya mkoa ambako wamelazwa
 Alifafanua zaidi  kuwa gari hiyo Landlover Discova yenye namba za usajili 1513 JW 97  iliyosababisha ajali na kuuwa watu wawili papohapo na wengine wawili kujeruhiwa vibaya.
 Alieleza zaidi kuwa gari hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na  MT 97812 SGT Kelvin Muhagama ilikuwa ikitoka Makao makuu ya Brigedi Chandamali na kuelekea Songea mjini  
 Kamanda Kamuhanda alibainisha zaidi kuwa chanzo cha ajari hiyo ni mwendo kasi ambao ilimsababisha dereva wa gari hilo kushindwa kumudu usukani
Naye Mganga mfawidhi wa Hospitali ya mkoa songea  Dr. Mathayo Chanangula amethibitisha kupokea maiti za watu wawili ambazo kwa sasa zimehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali hiyo  na majeruhi  watatu ambao wawili kati yao wamelazwa kwenye wodi za majeruhi na majeruhi mmoja ambaye ni mtoto wa umri wa mika 2 Amina Moyo amekimbizwa katika Hospitali ya Mision ya Peramiho kwa matibabu zaidi baada ya Hospitali hiyo kukosa mashine ya Ex –ray kwani imeonekana kuwa Amina ameumia kichwani ambako kunahitaji kupata vipimo vya Ex –ray ambapo kwa sasa hivi huduma hiyo inapatikana katika Hospitali ya Mision ya Peramiho
Dr. Chanangula alifafanua zaidi kuwa kwa muda mrefu hospitali ya mkoa songea haina kabisa huduma ya Ex –ray tangu mashine hiyo ilipo haribika na kwamba kwa hivi sasa wanasubiri mafundi kutoka ufiripino waje kitengeneza jambo ambalo limeonekana kuwa kero kuwa kwa wakazi wa songea ambao wamefika kupatiwa huduma hiyo lakini wamekuwa wakielekezwa kwenda Hospitali ya Mision ya Peramiho ambayo iko umbali wa kilometa 25 toka Songea mjini
 Mwisho.  

WAKULIMA WA KOROSHO WAGOMA KUPOKE MALIPO NUSU NUSU YA FEDHA ZAO

MKUU WA WILAYA YA TUNDURU JUMA MADAHA
Na Steven Augustino ,Tunduru

BAADHI ya wakulima wa korosho katika vyama vya msingi vya wakulima wa zao hilo wamegoma kupokea fedha za malipo yao huku wakidai kuto kuwa na imani na maelekezo yanayotolewa na viongozi wao.

Mgomo huo umefuatia kuwepo kwa maelekezo kuwa mkulima anayedai Shilingi 1200 kwa malipo ya korosho hizo atatakiwa kupokea mkononi Shilingi 850  na makulima anayedai Shilingi 350 atatakiwa kupokea Shilingi 200 huku kukiwa na maelekezo kuwa fedha nyingine watalipwa baada ya kuwasili kwa fedha zingine.

Wakiongea kwa nyakati tofauti miongoni mwa wakulima hao Mahamudu Ponera wa chama cha Msingi Nakayaya mashariki na Maghreth Mingwe walisema kuwa kitendo cha viongozu hao kuyumbisha malipo hayo kinalenga kuendelea kuichafulia sifa Serikali.

Walisema msimamo wao wa kukataa kupokea fedha hizo unatokana na wakulima kuelezwa kuwa baada ya kupokea fedha hizo watatakiwa kuacha Stakabadhi za malipo hayo na kubakia wakiwa hawana vielelezo vyovyote vinavyo onesha kuwepo kwa madai mengine katika vyama hivyo.

Alipo takiwa kuzungumzia hali hiyo Meneja wa Chama Kikuu cha wakulima wa wa Wilaya ya Tunduru  Iman Kalembo alithibitisha kuwepo kwa hali hiyo na kwamba msimamo wakutoa malipo hayo umetokana na fedha zilizofika kuwa ni kidogo hivyo wao hawakuona mkulima wa kumuacha wakati wa malipo hayo na kusisitiza kuwa fedha zikifika wakulima wote watakamilishiwa malipo yao.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Madaha alipotakiwa kuzungumzia kero hiyo alidai kuwa hakubaliani na utekelezaji wa zoezi hilo na kuongeza kuwa msimamo wa Serikali ni kulipa fedha zote na siyo kidogo kidogo na kwamba kama kuna kosa lilifanyika na viongozi hao ni uzembe wa viongozi wenyewe.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Afisa Ushirika wa Wilaya ya Tunduru Msangi alisema kuwa malipo hayo yanatokana na Benki kutoa Tsh. 2,587,506,900 zimepangwa kughalimia malipo ya Kilo 1200 tu kati ya Kilo  7,367,689 zilizopokelewa katika maghala kati ya Kilo
7,570,000 zilizo zalishwa na akulima hao katika msimu wa mwaka 2011/2012.

 Msangi aliendelea kueleza kuwa mchanganuao wa malipo hayo unaonesha kuwa kiasi kingi ne cha Shilingi 119,759,340 zitalipwa awamu ya pili na kwamba hali hiyo inatokana na taratibu za malipo hayo kuchelewa kupelekwa Benki.

Alisema fedha hizo zinatokana na malipo ya kilo 560,101 ambapo kati yake kilo 53,347 zenye thamani ya Shilingi 64,016,400 ni korosho za daraja la kwanza na shilingi 55,742,940  zinatokana na kilo 506,754 za daraja la pili.

Mwisho