Na Gideon Mwakanosya,Songea
DIWANI wa Kata ya mjini kupitia Chadema Joseph Fuime amelalamikia tatizo la kuzuka kwa Madanguro katika Manispaa ya Songea ambapo amewataka madiwani wenzie na viongozi kukemea vitendo hivyo kwani vinachoche ongezeko la maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi.
Akichangia hoja wakati wa kujadili taarifa ya hali ya maambukizi ya ukimwi katika manispaa ya Songea Diwani huyo amesema, katika siku za hivi karibuni kumezuka madangulo na wimbi la wasichana ambao wanafanya biashara za ngono katika manispaa hiyo tafauti na zamani hali ambayo inachangia kuongezeka kwa maambukidhi mapya ugonjwa wa ukimwi katika Manispaa hiyo.
Amesema, pamoja na mji kukuwa kwa kasi kumekuwa na ongezeko la madanguro,kumbi za starehe hivyo amewaomba viongozi wenzake washirikiane kukemea tabia ambazo zinaweza kuchochea ongezeko la ugonjwa wa ukimwi kwani vitendo vinavyofanywa ni hatari.
"Mh.Mwenyekiti naomba Madiwani wenzangu na Viongozi wenzangu tusaidiane kupiga vita madanguro kwani yameongezeka sana na yanahatarisha maisha yetu , tupige vita ili kuweza kupunguza maambukizi mapya ya ukimwi katika manispaa yetu ambayo kwa sasa imevamiwa na kumbi nyingi za starehe na madanguro,alisema Fuime.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Zacharia Nachoma , mewataka madiwani hao na jamii kwa ujumla kushirikiana kwa pamoja katika kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi ambao umeonekana kuwa tishio kwa wananchi wa Manispaa ya Songea.
Amesema,kwa kutambua tatizo hilo kila kata ina kamati za kudhibiti ukimwi hivyo zinahitajika jitihada kutoka pande zote ili kuweza kukomesha tatizo la madanguro pamoja na ugonjwa wa ukimwi katika manispaa hiyo.
MWISHO.