Friday, January 30, 2015
NAPE NNAUYE AWATAKA WANANCHI KUENDELEA KUIAMINI CCM MWAKA 2015
NA, STEPHANO MANGO,SONGEA
WANANCHI Wametakiwa Kuendelea kukiamini Chama cha Mapinduzi (Ccm) Kuwa Ndicho Chama Pekee Kinachopaswa Kuendelea Kuwaongoza na kutatua Changamoto Zinazowakabili Kuliko Vyama Vingine Vya Siasa Kutokana na Uchanga Wake Pamoja na Sera Zao Kutokukidhi Matakwa ya Wananchi Katika Karne ya sasa
Hayo yalisema Jana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakati akiwahutubia Mamia ya Wakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Kwenye Mikutano yake Tofauti aliyoifanya Mjini hapa baada ya Maandamano Makubwa yaliyoanza Katika Ofisi ya Ccm Mkoa wa Ruvuma Hadi Kata ya Lizaboni na kufanikiwa kufungua matawi ya chama, miradi mbalimbali ya chama na kuwapatia kadi wanachama wapya
Nnauye Alisema Kuwa Vyama Vingi Vya Siasa Havina dhamira ya Kweli ya Kuwaletea Wananchi Maendeleo bali Vimekuwa vikipiga Kelele ili viwalaghai Wananchi wapate Uongozi ili wajinufaishe wenyewe binafsi na Vyama Vyao
Alisema kuwa Chama cha Mapinduzi kinatarajia Februari Mosi Mwaka Huu kufanya Sherehe ya Kumbukumbu ya Kuzaliwa kwake miaka 38 iliyopita katika Sherehe hizo chama kinajivunia utekelezaji wa ahadi zake na maendeleo makubwa yaliyopatikana kwa kipindi chote cha uwepo wake madarakani.
Alieleza kuwa CCM inaendelea kutekeleza ilani yake vizuri na wataendelea kuisimamia Serikali katika kutimiza ahadi za mwaka 2010 na kwamba maeneo machache yalienda kwa wapinzani kimakosa na kuahidi makosa hayatorudiwa tena katika uchaguzi wa mwaka huu
“ Naomba Niviambie vyama vya Upinzani kuwa kauli mbiu ya Mwaka Huu ya Maadhimisho ya Ccm ni Umoja ni Ushindi, Katiba yetu nchi yetu hivyo chama kimejipanga kuelimisha wananchi namna ya upigaji wa kura katika katiba mpya pia kurudisha maeneo yaliyochukuliwa na vyama vya upinzania katika uchaguzi wa mwaka 2010”.
Alisema kuwa wananchi wana imani kubwa na Ccm hivyo Wapinzani walipanga kwa muda wa miaka mitano na kwamba kodi yao imesha wanapaswa kuondoka kabla hawajafukuzwa na mwenye nyumba kwani havina sera na vimeshindwa kuja na sera mbadala ya kuleta maendeleo ya kiuchumi nchini
Alifafanua kuwa Mafanikio ya Ccm yametokana na Watendaji wa Serikali kuwa karibu na wananchi kwani kumesaidia kufanikisha maendeleo na kuondoa sintofahamu za wananchi wanaotaka kujua taarifa za maendeleo ya miradi au maeneo husika.
Alisema pia kila mtu kwenye utumishi wa serikali inabidi awajibike katika kufanikisha lengo na asiyeweza inabidi aachie ngazi kwani ni lazima tutangulize utumishi wa umma.
Pia aliwataka vijana kuacha kuingia kwenye makundi ya watu watakaowatumia kisiasa na kabla ya kuwashabiki viongozi fulani kuna umuhimu watafute historia za viongozi hao
MWISHO
MWANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA SONGEA AJINYONGA
NA STEPHANO MANGO,SONGEA
MWANAFUNZI wa Kidatao cha kwanza katika shule ya Sekondari ya msamala iliyopo manispaa ya Songea mkoani Ruvuma James Mbano (16) amekutwa chumbani kwake alikokuwa analala amejinyonga kwa kutumia kamba aina ya Katani kwa kuifunga kwenye kenchi za paa la nyumba ya Mjomba wake.
Habari zilizopatikana jana mjini Songea ambazo zimethibitishwa na kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Yahaya Athumani zimesema kuwa tukio hilo limetokea Janua 29 mwaka majira ya saa 1030 za jioni huko katika eneo la Mkuzo Ruwawasi kata ya Msamala manispaa ya Songea.
Alisema kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio James alikutwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya katani ambayo ilifungwa kwenye kenchi la paa katika chumba alichokuwa analala ambapo tukio hilo liligunduliwa na mjomba wake Castory Silvesta (37) ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi mfaranyaki.
Alieleza zaidi kuwa Mwalimu Silvesta baada ya kugundua tukio hilo alitoa taarifa katika kituo kikuu cha Polisi cha mjini Songea ambapo baadae timu ya askari wa idara ya upelelezi Mkoa wakiongozana na Dkt. Toka hospitali ya Mkoa Songea walikwenda eneo la tukio na kufanikiwa kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu na hakuwa na jerhaa sehemu yeyote ya mwili na kwamba chanzo cha kujinyonga mpaka sasa hakijafahamika na hakuna ujumbe wowote aliouacha marehemu.
MWISHO.
WAZEE SONGEA WAIOMBA SERIKALI WAPATIWE MATIBABU BURE
Wazee wakiwa kwenye tafakari ya changamoto zao
NA,
STEPHANO MANGO,SONGEA
WAZEE wa kata ya Misufini Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma
wameiomba serikali iweze kuangalia upya suala la kupata matibabu bure kwa
wazee wenye umri kaunzia 60 kwa kuiboresha kwa kuwa sasa imekuwa haionyeshi
kama matibabu hayo hutolewa bure kutokana na kushindwa kupata dawa na baadala
yake kuambiwa wakanunue kwenye maduka ya dawa yaliyoko nje yaeneo lahospitali.
Ombi hilo limetolewa jana na mwenyekiti wa mfuko wa maendeleo ya wazee Mfaranyaki [MMWM] ,Lawrence Mbewe wakati wa mdahalo uliofanyika kata ya Misufini mjini hapo ambao ulikuwa ukijadili changamoto mbalimbali zinazo wakabili wazee hasa katika upande wa upatikanaji wa matibabu bure ambayo ni sera iliyowekwa na serikali.
Akiongea kwenye mdahalo huo uliyofadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Foundation For Civil Society la mjini hapo ,Mbewe alisema kuwa licha ya kuwepo kwa sera inayowataka wazee kutibiwa bure lakini bado wanakabiliwa na changamoto za matibabu hayo ikiwemokushindwa kupata dawa na kuambiwa wakanunue kwenye maduka ya madawa.
Alisema kuwa kama wanakuwa wamepata bahati ya kupata dawa ,hupewa za kutuliza maumivu hasa Panadol na siyo dawa za kutibu ugonjwa wanaosumbuliwa nao jambo ambalo amedai kuwa baadhi ya wazee wengi kushindwa kutibiwa kwa kutokumdu gharama za dawa.
‘’Tunaiomba serikali iweze kuliangalia hili namna ya kutusaidia maana sasa hali ya wazee siyo nzuri maana unaweza ukapokelewa na daktari vizuri lakini unapozidi kuendelea kupata huduma ya matibabu unakuta unaambiwa dawa hakuna labda tukusaidie za kutuliza maumivu Panadol na dawa nyingine ukanunue kwenye maduka ya madawa”alisema mwenyekiti
,Mbewe.
Kwa upande wake afisa ustawi wa jamii Manispaa ya Songea ,Victor Nyenza akitolea ufafanuzi wa sera ya wazee kutibiwa bure kwenye mdahalo huo alisema sera hiyo ilianzishwa mwaka 2015 ya kuzitaka kila Halmashauri kuhakikisha wazee wanatibiwa bure

Nyenza alisema kuwa changamoto kubwa kwa sasa ni upungufu wa
madawa kwenye vituo vya afya na mahospitalini jambo ambalo hufanya wazee wengi
kuona hawatendewi haki katika sera inayowataka watibiwe bure.
MWISHO
Subscribe to:
Posts (Atom)