About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Friday, April 20, 2012

ADAIWA KUJINYONGA KWA SABABU ZA WIVU WA KIMAPENZI


       KAMANDA WA POLISI MKOA WA RUVUMA MICHAEL KAMHANDA

Na Augustino Chindiye, Tunduru

MSONGO wa mawazo uliotokana na wivu wa kimapenzi umesababisha kifo cha Mkazi wa Mtaa wa Kasuguru Mjini Tunduru aliyefahamika kwa jina la Said Issa (43) aliyefariki dunia baada ya kujinyonga.

Taarifa za tukio hilo zinaeleza kuwa kabla ya kukumbwa na umauti Marehemu Issa alitoweka na kupotelea kusiko julikana March 31 Mwaka huu kabla ya mwili wake kuokotwa April 16 mwaka huu ukiwa vipande vipande kutokana na kuharibika vibaya.

Taarifa hiyo iliendelea kufafanua kuwa kutokana na mwili wake kuharibika vibaya ambapo mashuhuda hao walikuta baadhi ya viungo vikiwa vimetawanywa katika maeneo tofauti huku vingine vikiwa vimeanza kuliwa na wanyama na kufanikiwa kumzika akiwa hana kichwa

Akizungumzia mkasa huo mdogo wa marehemu Isaa Matumla alisema kuwa marehemu kaka yake huyo alianza kuchanganyikiwa siku chache baada ya kuachwa na Mkewe ambaye alidaiwa kuchukua uamuzi huo kwa lengo la kupumzika maisha ya shida waliyo kuwa wakiishi kwa muda mrefu kutokana na mumewe huyo kutokuwa na uwezo kifedha.

Alisema kufuatia mkasa huo Marehemu alionesha kuchanganyikiwa kiakili na kuwa mlevi wa kupindukia hatimaye akaamua kuchukua uamuzi huo wa kukatisha maisha yake kwa kujinyonga akiwa mafichoni katika msitu ulozunguka mashamba ya Shule ya Sekondari Tunduru.

Mganga aliyeufanyia uchunguzi mwili wa Marehemu Issa Dkt. Joseph Ng`ombo alidai kuwa chanzo cha kifo hicho kilisababishwa na tukio la kujifunga kamba shingoni na kujining`iniza juu ya mti kabla ya mwili wake kuanguka chini na kuharibika vibaya.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Mchael Kamuhanda mbali ya kuthibitisha kuwepo kwa tukio hilo alisema kuwa polisi bado wanaendelea na uchunguzi wa kifo hicho.

Mwisho