NA, STEPHANO MANGO,SONGEA
WANAHARAKATI wamelalamikia Kitendo cha Raia wa Nchi ya China
Zhouguang Zheng (27)maarufu kwa jina la
Dani Johnson Kumpiga na Kumsababishia Maumivu Makali Mfanyabiashara Maarufu Na
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabasi ya Kisiwa Sport, Kisiwa Kisiwa (40) na kumsababishia Kulazwa
Siku Mbili katika Hospital ya Serikali ya Mkoa wa Songea na Wengine wawili
walijeruhiwa katika Vurugu hizo
Wakizungumza kwa Nyakati Tofauti na Gazeti Hili jana
Walisema kuwa Kitendo hicho ni kibaya sana kwani kimekiuka Sheria za Uraia na
Uwekezaji, ingawa pia ni ukiukwaji mkubwa wa Haki za Binadamu na kinavuruga
amani na Utulivu Miongoni Mwa Jamii
Hamis Abdala Ally alisema kuwa kitendo cha Mwekezaji huyo wa Kampuni ya Mabasi ya NewForce
inayosafirisha Abiria kutoka Songea Kuelekea Jijini Dar Es Salaam kimevuka mipaka
yake ya Uwekezaji na Ukiukwaji mkubwa wa Sheria na Taratibu
Ally Alisema kuwa ni kosa sana Raia wa Kigeni kwenye Nchi ya
Watu kufanya Vurugu na Kusababisha Raia wa Nchi Husika kupata Maumivu Makali katika
Mwili wake , kwani kitendo hicho kinaweza Kusababisha chuki na amani kuvurugika
miongoni mwa Jamii
Alisema kuwa Tukio hilo linahatarisha uwekezaji wake, ushirikiano
uliojengeka kwa kipindi kirefu kwenye jamii husika kwani mahusiano ya Watu
yamepungua kutokana na Jambo hilo
“Tunalitaka Jeshi la Polisi Kutenda Haki Katika Jambo Hili
la Mchina Kufanya Vurugu na Kusababisha amani kutoweka Katika eneo la Stendi
Kuu ya Mabasi Songea kwa Zaidi ya Masaa sita na kuongezeka kwa Chuki Miongoni
mwa jamii ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Mabasi ya Super Feo na NewForce”Alisema
Ally
Alieleza kuwa Wananchi wa Songea hatuna utaratibu wa
kuwadhuru au kuwanyanyasa Raia wa Kigeni wawapo kwenye Shughuli zao lakini
Tumeshangazwa na Mchina Huyu ambaye ameanzisha Utamaduni Mpya wa Kuwajeruhi Wazawa
Mukhtar Simba Alisema kuwa Wanaruvuma ni watu Waungwana na
Wakarimu sana na kwenye Swala la
Uwekezaji Kuna Sheria na Taratibu ambazo zinamuongoza Mwekezaji
kufanya shughuli zake pia ana mipaka ya uwekezaji wake katika eneo husika
Simba Alisema Tunalaani na kushangaa Kumuona Mwekezaji Huyo
bado anaendelea Kutamba Mitaani huku Mwenzake akiendelea na Matibabu ambayo
yamesababishwa na Kipigo chake wakati sheria zipo wazi
Akizungumzia Tukio Hilo Mkurugenzi wa Kampuni ya Super Feo
Omari Msigwa Alisema kuwa Kitendo alichokifanya Mchina Siku hiyo Cha Kumpiga
Msaidizi wake Haruna Msigwa na Kisiwa Kisiwa na Kuifanya Stendi kuwa ni Uwanja
wa Vurugu kimemshtua Sana kwani Hakukitegemea katika Sekta ya Usafirishaji
Mkoani Ruvuma
Msigwa Alisema kuwa licha ya Jambo hilo kuwa ni Ukiukwaji
Mkubwa wa Haki za Binadamu na Sheria za Nchi Lakini pia kimeleta picha mbaya
sana Katika Sekta ya Usafirishaji kiujumla kwani Vurugu hizo zimetokea Mbele ya
Abiria ambao hawajawahi kuona wala kutarajia vurugu katika Stendi hiyo
Alieleza kuwa Sheria ziko wazi za Uwekezaji na za Kijinai
hivyo ni Muhimu Mamlaka zinazohusika kuchukua Hatua Stahiki Katika Jambo hilo
kwani kutochukua hatua madhubuti kutasababisha ulipizaji wa Kisasi miongoni mwa
Jamii hizo
“Ili Kuepuka chuki hizo ni Vyema Mamlaka zinazohusika
Zikatenda Haki kwa Kila Mmoja aliyeenda Kinyume cha Sheria na Taratibu katika
Tukio hilo Kwani Kitendo cha Kumpendelea Mtu huku Ukweli wa Jambo ukiwa wazi
kitaanzisha utamaduni mbaya ambao utaleta athari nyingi baadaye” Alisema Msigwa
Alieleza zaidi kuwa Siku za Nyuma Kulikuwa na Kampuni Nyingi
za Usafirishaji Abiria kama Vile Sabco, Saibaba,Scandnavia,Ottawa, na
Nyinginezo lakini hakuna Siku Hata Moja Wafanyakazi wake au Wafanyakazi wa
Kampuni nyingine hizo Kupigana lakini leo Mwekezaji wa Kigeni Amempiga
Mwekezaji wa Ndani hali ambayo inazua Mashaka sana
Akizungumza na Gazeti hili Nyumbani Kwake Kisiwa Kisiwa alisema
kuwa Ni ukweli ulio wazi kuwa nimepigwa tena kipigo Kikali na Mchina hadi
kulazwa Siku Mbili kutokana na Maumivu Makali Katika Sehemu mbalimbali za Mwili
wangu
Kisiwa Alisema licha ya Kushonwa Nyuzi kumi na nne Mdomoni
kutokana na Kipigo bado mwili wangu haujatengamaa na maumivu makali bado
nayasikia na sijaanza kufanya kazi zangu za kila siku kama ilivyo ada
Alisema kuwa Mchina huyu amekosa Utu wala aibu Toka
anisababishie Maumivu katika Mwili wangu ameshindwa hata kunijulia hali bali
yeye amekuwa akiendelea na shughuli zake huku mie nikiendelea kuumwa
Kamanda Wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela alisema Tukio hilo lilitokea Januari 13 Majira
ya Saa 12:10 asubuhi katika eneo la Kituo Kikuu cha Mabasi Kilichopo Msamala Mjini hapa , ambako ilizuka Vurugu
kubwa baina ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Mabasi ya Usafirishaji Abiria ya New Force na Kampuni ya Super Feo wakigombaniana
ratiba ya kuondoa Mabasi yao kutoka Songea Kuelekea Jijini Dar Es Salaam
Msikhela Alisema kuwa Katika tukio hilo Watu watatu
wamejeruhiwa ambao ni Zhouguang Zheng (27) ambaye ni Raia wa China, Danford
Thomas (40) Mkazi wa Mfaranyaki na
Abdurabi Kisiwa ambaye pia ni Mkazi wa Mfaranyaki na Mmiliki wa Mabasi
ya Kisiwa Sports
Alieleza zaidi kuwa inadaiwa katika vurugu hizo vitu
mbalimbali vimepotea zikiwemo Simu mbili aina ya Tecno ambazo thamani yake bado
haijafahamika ambazo zilikuwa mali ya Kisiwa, simu moja ya IPhone 5s yenye
thamani ya milioni 1.5 pamoja na fedha taslim shilingi milioni nne zimeporwa na
watu wasiofahamika ambazo ni mali ya Zhouguang Zheng
Alisema kuwa kufuatia
tukio hilo watu 14 wamekamatwa na Kuhojiwa na Polisi kwa tuhuma za kujihusisha
katika vurugu hizo na wapo nje kwa dhamana na kwamba Jarada la Uchunguzi Limefunguliwa
na Kupewa namba SO/IR/ 189/015 Na kwamba upelelezi bado unaendelea kufanywa na
kwamba ukikamilika Jarada hilo litapelekwa Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali ili
kulifanyia kazi kabla halijaenda Mahakamani
MWISHO