MWENYEKITI WA CHADEMA RUVUMA AMTIMULIA VUMBI DKT NCHIMBI
MAMIA YA WAKAZI WAKIMSIKILIZA MTANGA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE KATIKA KATA YA LIZABONI
Na Stephano Mango, Songea
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
mkoa wa Ruvuma Joseph Lusius Fuime
ametangaza nia ya kugombea Ubunge kwa
tiketi ya Chama hicho katika Jimbo la uchaguzi la Songea mjini ifikapo mwaka
2015 katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu
Fuime ambaye Diwani
wa Kata ya Mjini katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea akitangaza nia hiyo jana ya kutaka kugombea jimbo ambalo kwa
sasalinaongozwa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt Emmanuel
Nchimbi kwenye mkutano wa hazara uliofanyika
kwenye viwanja vya Soko kuu la Songea Mjini alisema kuwa ametafakari kwa muda
mrefu pia ameombwa na makundi mbalimbali ya jamii ya Songea kuchukua fomu ya
kugombea kiti hicho
Alisema kuwa baada ya kutafakari ameamua kwa dhati
kusikiliza kilio cha makundi hayo na kugombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA ili kwa pamoja kuweza kuondoa kero mbalimbali
ambazo zinawasumbua wakazi hao
“Naomba niwaondoe hofu wanachama wenzangu ndani ya Chadema
kuwa kutangaza kwangu nia ya kutaka kugombea
Ubunge hakuna maana kuwa wanachama wengine wanaotaka kugombea washindwe
kutangaza nia ya kuwania nafasi hiyo”
Alisema kuwa wanachama ndio wenyewe mamlaka ya kumchagua mgombea mwenye kujua
matatizo ya wakazi wa Manispaa ya Songea na mbinu ya kushirikiana na wananchi
hao kuweza kuyatatua kwa maslahi mapana ya ustawi wa jamii hiyo, pia
atakayeweza kupambana na mgombea wa Ubunge kwa tiketi ya ccm.
Alieleza zaidi kuwa baada ya kufikia uamuzi huo kabla ya
kutangaza nia aliamua kukaa na wazee wote wa Songea Mjini ambao wote kwa pamoja
wameonyesha ushirikiano mkubwa na wamemwakikishia kuwa mwaka 2015 wakati wa
uchaguzi watamuunga mkono kama walivyomuomba
Fuime ambaye pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Ccm
katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea alijigamba na kuwaeleza wakazi wa Songea
kuwa yeye ndiye anayefaa kupambana na Mbunge wa Songea Mjini kwa tiketi ya Ccm Dkt Emmanuel Nchimbi.
Alifafanua zaidi kuwa Chadema imejipanga kwa dhati kutotoa
nafasi tena ya uongozi kwenye Jimbo la uchaguzi la Songea Mjini kuchukuliwa na
Ccm ambalo lina kata 21 na kati ya hizo 8 zinaongozwa na Madiwani wa Chama cha
Chadema na kwamba mwaka 2015 kata zilizobaki zitanyang’anywa na Chadema.
Aliongeza kusema kuwa dawa ya kupambana na manyang’au waliomo
ndani ya Ccm ni kujipanga na kuwabana kwa kutowapa nafasi ya aina yeyote kuanzia
sasa na mpaka ifikapo 2015 kwani hivi sasa miradi mbalimbali katika Halmashauri
ya Manispa ya Songea imekuwa ikijengwa chini ya viwango ambapo alitoa mfano
kuwa miundombinu ya barabara, ujenzi wa vyumba vya madarasa na ofisi zimekuwa
zikijengwa chini ya viwango huku manyang’au wa Ccm wakineemeka.
Alisema kuwa Wananchi wa Songea ambao wamekuwa wakikabiliwa
na shida mbalimbali kutokana na ombwe la uongozi unaotokana na mfumo mbovu wa
Ccm wana kila sababu ya kuunga mkono wazo lake la kuwania kiti cha Ubunge ili
kuweza kufanikisha ustawi bora wa maisha ya wakazi wote kwa ushirikiano
Awali katika vipindi viwili vya uchaguzi mkuu vilivyopita
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kilikuwa kinamnadi Wakiri wa kujitegemea Edson
Osward Mbogoro kugombea nafasi hiyo ambapo alikuwa akibwagwa na Mgombea wa
Ccm Dkt Emmanuel Nchimbi ambaye ndiye Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini
hadi sasa.
MWISHO