Marehemu Mohamed Mnyachi enzi za uhai wake(Picha kwa hisani ya Familia yake)
Na Agustino Chindiye,Tunduru
Mtandao huu unatoa pole kwa Familia ya Marehemu Mnyachi na inaungana na watanzania wote katika majonzi hayo;Tunaamini kuwa Marehemu Mnyachi ameacha pengo kubwa ambalo halitazibika lakini mchango wake umeonekana dhahili katika kuchangia harakati za ukombozi wa Taifa hili kutoka nikononi mwa Mafisadi na wabadhilifu nchini
Marehemu Mnyachi ametangulia mbele za haki nasi tunamfuata lakini aliweza kutimiza wajibu wake kikamilifu enzi za uhai wake,uliobaki ni wetu,wakati tunaendelea kumkumbuka tutafakari kwa umakini fikra zake ili ziweze kutusaidia katika ujenzi wa pamoja wa taifa tunalolihitaji
Bwana alitoa na Bwana ametwaa,Jina lake lihimidiwe
Saturday, September 17, 2011
MAHAFARI YA KIDATO CHA NNE SHULE ZA WILAYANI TUNDURU YATUMIKA KUKUSANYA FEDHA YA KUBORESHA MIUNDOMBINU KATIKA SHULE ZILIZOPO MJINI HUMO
Na Steven Augustino,Tunduru
MAHAFARI ya kuwaaga wanafunzi wanaomaliza kidato cha Nne katika Shule za Sekondari za Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma yametumika kufanya harambee za kuchangisha fedha kutoka kwa wazazi na walezi wa wanafunzi wanaosoma katika shule hizo ili ziweze kusaidia utengenezaji wa miundombinu mbalimbali .
Hali hiyo imetokana na Shule nyingi za Sekondari katika Wilaya hiyo kukabiliwa na uhaba mkubwa wa vifaa mbalimbali pamoja na kutokuwepo kwa miundombinu ya maji, uchakavu wa vyumba vya madarasa pamoja na upungufu wa thamani yakiwemo madawati, meza na viti vya kukalia wanafunzi.
Akizungumzia hali hiyo katika mahafari yaliyofanyika katika Shule za Sekondari za Masonya na Mataka afisa elimu wa Shule za Sekondari wa Wilaya ya Tunduru Mwl. Ally Mtamila alisema kuwa mpango huo umebuniwa kufuatia tabia za ukaidi na ugumu wa kuchangia maendeleo kupitia michango ambayo imekuwa ikiombwa na Shule kutoka kwa wazazi na walezi hao.
Alisema baada ya kupatikana kwa fedha hizo zitasaidia kuanzia kutatua matatizo yanayozikabiri yakiwemo ya kujenga, kufanya ukarabati au kufanya malipo ya kuanzia kutengenezea vitanda kwa shule za Hostel au kununulia mbao ambazo zitatumika kutengenezea meza na madawati zikiwa ni juhudi za kupunguza adha mbali mbali zinazo ikabili idara hiyo wakati huohuo pia idara hiyo ikijitahidi kuomba uwezeshwaji kutoka halmashauri ya Wilaya hiyo.
Akizungumzia michango ya Shilingi 456,440 iliyopatikana kupitia harambe hiyo iliyofanyika katika Shule za Sekondari zilizopo mjini Tunduru ambazo ni Frenkweston, Mataka na Masonya wakati wa mahafari hayo, Mtamila alisema kuwa huo ni mwanzo mzuri na kwamba endapo utamaduni huo utaendelezwa kuna uwezekano wa Wilaya hiyo kupiga hatua kubwa za kimaendeleo katika nyanja hiyo ya elemu.
Aidha Mwl. Mtamila aliendelea kueleza kuwa idara yake yenye shule 19 inakabiriwa na upungufu wa walimu 130 kati ya mahitaji ya walimu 289 wengi wao wakiwa ni walimu wa masomo ya Sayansi hali inayotishia wanafunzi hao kufanya vibaya katika mitihani ya masomo hayo ambapo jumla ya wanafunzi 1200 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya sekondari mwaka huu.
Akiongea kwa nyakati tofauti wakati wa kufunga mahafari hayo pamoja na mambo mengine Mwl. Ally Mtamila aliwakumbusha wazazi na walezi wa wanafunzi waliomaliza darasa la saba kufanya maandalizi ili watoto wote watakao chaguliwa wajiunge kwa wakati na kuanza masomo ya sekondari.
Kuhusu wahitimu wa kidato cha Nne Mtamila aliwataka kufanya maandalizi mazuri ili waweze kufanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya taifa ili waweze kuendelea na masoma ya juu na kwamba wasikubali kudanganyika na maisha ya uraiani ambayo mwisho wake unaweza kufupisha maisha yao.
Awali wakisoma risala katika shule hizo kwa niaba ya wanafunzi wanaoagwa,Omari Jeuri wa Masonya Sekondari na Ayubu Adhuman wa Mataka sekondari walisema kuwa kukosekana kwa huduma ya maji katika shule zao kunatishia kulipuka kwa homa za matumbo ukiwemo ugunjwa wa kipindupindu.
Wakizungumzia madhara ya ukosefu wa Miundombinu ukosefu wa Walimu wa masomo ya sayansi, meza na viti vinavyo zikabili shule zao wakuu wa shule za Masonya Mwl. Mohamedi Ngaunje na Mkuu wa Shule ya sekondari ya Mataka Mwl. Johnes Liombo walidai kuwa endapo matatizo hayo yataachiliwa yaendelee kuna hatari ya idadi kubwa ya wanafunzi kuendelea kufanya vibaya katika matokeo ya mitihani ya taifa na kuiweka Wilaya yao katika alama mbaya kila mwaka.
Mwisho.
MSAMA PROMOTIONS KUGAWA MAMILIONI KWA WALEMAVU NCHINI
NA MWANDISHI WETU
MKURUGENZI wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama amesema kuwa baada ya kupata mafanikio kwenye Tamasha la Pasaka,anatarajia kutoa baiskeli 50 za walemavu zenye thamani ya Sh. milioni 30.
Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Msama alisema kuwa fedha hizo alizoamua kuzielekeza kwa walemavu, zimetokana na mauzo mazuri ya DVD na VCD za tamasha la Pasaka lililofanyika mwaka huu, ambalo pia lilihudhuriwa na rais Jakaya Kikwete.
Alisema kuwa ameamua kufanya hivyo kutokana na kuguswa na matatizo ya watanzania wenzake hasa walemavu ambao wamekuwa wakitaabika kutafuta ridhiki, kutokana na kushindwa kutembea.
“Nimeona kuna haja ya kuwajali walemavu,nilichoamua ni kuwa ni vema hiki kidogo nilichokipata nimeona ni vema kama nitagawana nao,”alisema Msama.
Alisema kuwa tayari ameshaanza kazi ya kununua baiskeli hizo, ambazo zitakuwa ni za kisasa.
Baiskeli hizo atazigawa kwenye mikoa ya Lindi, Mtwara,Songea na Tabora, ambapo Tabora na Songea kila mkoa mmoja utapata baiskeli 10 huku Lindi na Mtwara kila mmoja utapata baiskeli 15.
Kwa upande mwingine aliongeza kuwa utaratibu huo utaendelea kila mwaka, kwani anaamini wapo watanzania wenye matatizo ambayo yanahitaji kusaidiwa na anaona kwa upande wake analojukumu la kuwasaidia.
Mwisho..
DIWANI WA CHADEMA AWARUSHIA KOMBORA NZITO WABUNGE WA MKOA WA RUVUMA
Na Gideon Mwakanosya,Songea CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) Mkoani Ruvuma kimewashushia shutuma nzito Wabunge wa Majimbo mbalimbali Mkoani Ruvuma,pamoja na wa Viti Maalumu kuwa wamekuwa ni mzigo kwa wananchi waliowachagua kwani wamekuwa wakishindwa kuwakilisha matatizo yaliyoko katika majimbo yao kikamilifu. Akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara kwenye Kata mpya ya Mjimwema kwenye kiwanja cha eneo la Shule ya Msingi Samora Mwenyekiti wa chama hicho Mkoani Ruvuma Joseph Fuime alisema kuwa wabunge wa Mkoani wa Ruvuma wanapokwenda kuhudhuria vikao vya bunge wanashindwa kabisa kuwakilisha matatizo yaliyoko kwenye Manispaa ya Songea ambayo kwa muda mrefu kwa nyakati za usiku kunakuwa ni giza totoro lakini Mbunge wa Jimbo hilo amekaa kimya. Fuime ambaye pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa CCM katika Manispaa ya Songea ameeleza kuwa wabunge wa majimbo yaliyoko Mkoani Ruvuma inaonyesha wazi kuwa wanapokwenda kwenye vikao vya bunge wanakimbilia posho na sio kwenda kama wawakilishi bungeni kama wanavyofanya wabunge wengine toka majimbo ya Mikoa mbalimbali. “Wananchi niwaambieni Songea kumekuwa na matatizo mengi yakiwemo ya vocha za pembejeo zilizo chakachuliwa na wakubwa pamoja na tatizo Kubwa la kutopatikana umeme kwa muda mrefu katika mji wa Songea lakini tangu kikao cha bajeti ya bunge kilivyoanza mpaka kimeisha Mbunge wa jimbo hilo Dkt Emmanuel Nchimbi amekaa kimya kwa kisingizio cha kudai yeye ni Waziri” alisema Fuime. Vilevile amewataadharisha Watanzania wakiwemo wananchi wa Moka wa Ruvuma kuwaogopa viongozi wachache wa Serikali ya Ccm ambao wamekuwa ni mafisadi wakubwa na wamegeuza Watanzania kuwa ni sehemu la shamba la bibi ambalo halina mwenyewe. Amesema kuwa viongozi hao wamekuwa wakiuchezea uchumi wa nchi bila uoga na hakuna hatua zinazochukuliwa juu yao zaidi kumekuwepo na danganya toto kwa watanzania kuwa Serikali ya Ccm imeamua kupambana na mafisadi wakati mafisadi wenyewe wanaendelea kucheza kwenye shamba la bibi bila uoga. Kwa upande wake Katibu wa Chadema jimbo la Songea Masumbuko Paulo ameeleza kuwa kwa kitendo alichokifanya Mbunge wa Jimbo la Mbinga Kapteni John Komba cha kuamua kumsaidia Mbunge wa Songea Mjini Dkt Nchimbi kumfikishia bungeni tatizo Kubwa la miundo mbinu mibovu katika Kituo kikuu cha mabasi Songea,kinastahili pongezi kwani hali halisi ya miundo mbinu ya Kituo hicho cha Mabasi ni mbaya lakini mwakilishi wa wakazi wa Songea mjini bungeni kwa kipindi chote cha bunge la bajeti alishindwa kabisa kuliweka wazi ili Serikali ijue ni namna gani kusaidia ukarabati kwenye Kituo hicho. MWISHO |
Tamasha la Jinsia 2011 TGNP Dar laweka mikakati kibao! ikiwemo kuhitaji mahakama ya wananchi,kuvipa nguvu vyombo vya habari nchini na vile vya ukanda wa afrika kuripoti habari za Jinsia na wanawake wa kimapinduzi
Mwenyekiti wa Kamati ya Mafunzo na Maadili ya Baraza la Habari Nchini(MCT) JUMA NYUMAYO akionyesha bango baada ya kuwasilisha mrejesho wa waandishi wa habari namna ya Wadau wa Habari wanavyonyanyaswa pindi wanapofuatilia habari mbalimbali wakati wa kufunga Tamasha la Jinsia la 10 lililofanyika katika viwanja vya TGNP -Mabibo kuanzia Septemba 13-16
Viongozi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania wakiwa wanafuatilia mrejesho kutoka kwa wawasilishaji mbalimbali wakati wa ufungaji wa Tamasha la 10 la Jinsia mwaka 2011
Wanahabari wa vyombo mbalimbali wakiendelea na majukumu yao kabla ya kumalizika kwa tamasha la 10 la Jinsia mwaka 2011
Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili na Mafunzo ya MCT akisisitiza jambo na Mwanaharakati Mzee Abdalah Ndege wakati wa kufunga Tamasha la 10 la Jinsia Tanzania
Viongozi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania wakiwa wanafuatilia mrejesho kutoka kwa wawasilishaji mbalimbali wakati wa ufungaji wa Tamasha la 10 la Jinsia mwaka 2011
Wanahabari wa vyombo mbalimbali wakiendelea na majukumu yao kabla ya kumalizika kwa tamasha la 10 la Jinsia mwaka 2011
Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili na Mafunzo ya MCT akisisitiza jambo na Mwanaharakati Mzee Abdalah Ndege wakati wa kufunga Tamasha la 10 la Jinsia Tanzania
Subscribe to:
Posts (Atom)