About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Saturday, June 30, 2012

MAHAKAMA YAPELEKA KILIO KWENYE FAMILIA

Na Steven Augustino, Tunduru
MAHAKAMA kuu Tanzania Kanda ya Songea imepeleka kilio katika familia ya Shaibu Zuberi Kipande baada ya kumhukumu  kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia katika kosa la kuua kwa kukusudia kinyume na kifungu cha 196 cha Kanuni ya Adhabu, sura ya 16 kama ilivyofanyiwa mapitio mwaka 2002.

Kipande alihukumiwa adhabu hiyo baada ya Mahakama hiyo kumtia hatiani katika kosa kubwa la kuua kwa kukusudia, shauri Namba 7/2012 lililofunguliwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Songea na kusikilizwa katika kikao cha Mahakama Kuu kilichofanyika katika Mahakama ya Wilaya ya Tunduru. Bwana Kipande alishtakiwa kwa kosa la kumuua Hamisi Henyeka kwa kumnyonga na kumvunja shingo tukio lililotokea katika kijiji cha Nakapanya Wilayani Tunduru Januari 28/2010 na kwamba kutokana na mazingira hayo alistahili kupata adhabu hiyo kutokana na unyama alioufanya.

Sambamba na familia hiyo kuonja makali kutokana na machungu hayo ya kutenganishwa na ndugu yao huyo ambaye hata kaburi lake hawataliona,familia mbili ambazo ndugu zao walikuwa katika hamaki kutokana na kusubilia kutolewa kwa amri na Mahakama hiyo kutokana na tuhuma za aina hiyo Adhabu iliyotolewa ikawafuta machozi ya kutengana na ndugu zao muda mrefu baada ya Mahakama hiyo kuwaona hawana hatia na kuwaachia huru taarifa ambayo ililishitua Jeshi la polisi kutokana na vijana hao kudaiwa kuifahamu vyema yazi hiyo wawapo mitaani.

Aidha katika Mahakama hiyo pia familia nyingine tano (5) za wafungwa waliokuwa wakitumikia vifungo tofauti baada ya kupatikana na hatia katika makosa ya wizi wa kutumia silaha nazo zikanufaika na Rufaa walizokata baada ya mahakama hiyo kutengua adhabu za vifungo hivyo huku mahakama hiyo ikibainisha kuwa sababu za kuachiliwa huru kwao kunatokana na kilichodaiwa kuwa ni udhaifu wa ushahidi pamoja na kutozingatiwa kwa vifungu sahihi wakati wa kufungua mashtaka.

Akifafanua adhabu hizo Hakimu Mkuu Mwenye mamlaka ya Ki JAJI Mhesh. Wilifred Peter Dyansobera alisema kuwa mahakama hiyo imetoa adhabu ya kunyogwa hadi kufa baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi wanne waliongozwa kutoa ushahidi wao mahakamni na Mwanasheria mwandamizi wa Serikali Mkoani Ruvuma  Maurice
Mwamwenda.

Alisema mbali na kuzingatia rai ya upande wa utetezi iliyotolewa na Wakili Msomi wa kujitegemea  Dickson Ndunguru alitoa maoni kuwa adhabu anayostahili mstakiwa ni kunyongwa na kwa kuwa hakuna adhabu mbadala kwa mujibu wa kosa la mauaji ya makusudi aliomba Mahakama iandae nyaraka zinazostahili ili mshtakiwa aweze kukata rufaa.

Upande wa Jamhuri ukiongozwa na mwanasheria wa Serikari Wilbroad Ndunguru alihitimisha kwa kutoa maoni kwa kuiomba Mahakama hiyo izingatie kifungu cha 196 cha Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 juzuu ya 2002 katika kutoa adhabu kwa mshtakiwa.

Aidha Hakimu Mkuu mwenye  mamlaka ya Jaji,Mhesh. Dyansobera baada ya kumtia hatiani mshtakiwa na kutoa adhabu ya kunyongwa hadi kufa alihitimisha hukumu hiyo kwa kuutalifu upande wa utetezi kuwa njia ipo wazi endapo watahitaji kukata Rufaa na kuongeza kuwa Mahakama yake ipo tayari kutoa nakala ya hati ya hukumu na mwenendo wa shauri hilo mapema iwezekanavyo baada ya kukamilika kwa taratibu za kisheria.

Kwa mujibu wa adhabu zilizotolewa na Mahakama hiyo walionufaika kwa kuachiwa huru kutokana na udhaifu wa ushahidi wa tuhuma zilizo kuwa zikiwakabili ni pamoja na Salum Rashid Chibama aliyekuwa anatuhumiwa kwa tuhuma za mauaji ya bila kukusudia katika shauri la mauaji namba 6/2012 ambapo alidaiwa kuchoma nyumba moto na kusababisha kifo cha Mtoto Shadrack Hasani ambalo kiini chake ni tukio la fumanizi lililotokea katika
kijiji cha Muhuwesi Januari 4/2011.

Aidha Gotad Rufunda aliyekuwa anatuhumiwa katika Shauli la mauaji namba 4/2012 la tuhuma za kumuua marehemu Emmanuel Nyoni, Katika tukio lililo tokea Wilayani Namtumbo Tarehe 28/06/2008 aliachiwa huru baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kumwunganisha na
shtaka la mauaji.

Walionufaika na Rufaa zao kwa kuachiwa huru ni pamoja na Hasan Rajabu ,Kiwembe Kampose na Hamad Wajika Jamshid waliokuwa wanatumikia kifungo cha miaka 30 kila mmoja baaya ya Mahakama ya Wilaya ya Tunduru kuwatia hatiani kwa kosa la Wizi wa kutumia Silaha kinyume cha sheria namba 294 (A) kanuni ya Adhabu kama ilivyofanyiwa mapitio mwaka 2002 ambapo ilidaiwa kuwa kwa pamoja waliiba kwa kutumia silaha na baada ya kuiba walimtishia kumchoma Kisu askari (mstaafu) wa Jeshi la wananchi  Abbas Husein katika tukio lililotokea February 13/2011.

Kesi nyingine iliyotolewa maamuzi ya aina hiyo ni ya Rufaa namba 4A/2012 wakata rufaa wakiwa ni  Alex Steven Chipasula, Lazack Ally Jaza na Rashid Kamwana walikuwa wanatumikia kifungo cha miaka 11 kila mmoja wao baada ya Mahakama ya Wilaya hiyo kuwatia hatiani katika makosa mawili likiwemo la kuvunja na kuiba Seti ya TV na deki vyote
vikiwa na thamani ya Shilingi 900,000 mali ya Afisa utumishi wa halmashauri ya Wilaya hiyo  Christina Kumwenda katika tukio lililo tokea usiku wa manane agosti 19/2011.

Rufaa ya mwisho iliyotolewa maamuzi hayo na Mahakama hiyo ni Namba 7/2011 iliyokatwa na  Said Hamidu Manyiru ambaye alihukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 6 na Mahakama ya Wilaya baada ya kumtia hatiani kwa kosa la wizi wa pikipiki yenye namba za Usajiri T 772 EAD
mali ya Erasmo Damian iliyokuwa ameegeshwa katika yadi ya Idara ya Ujenzi Wilayani humo ambapo maelezo ya shauri hilo yalidai kuwa, Manyiru alibambwa na walinzi wa idara hiyo akitaka kuondoka na Pikipiki hiyo Mei 16/2011.

Wakizungumzia adhabu hizo Mwanasheria msomi wa Serikali  Wilbroad Ndunguru mbali na kukiri Jamhuri kufanya vibaya katika kesi hizo alisema kuwa kuanguka huko kumetokana na mapungufu ya kiushahidi ulioandaliwa na kutolewa Mahakamani huku Wakili wa kujitegemea .
Dickson Ndunguru alidai kutoridhishwa na adhabu ya kunyogwa hadi kufa
iliyotolewa dhidi ya mteja wake nikubwa mno na akaahidi kukata rufaa.

Upande wa Zuberi Kipande ambaye ni Baba mzazi wa mtuhumiwa aliyehukumiwa adhabu ya Kifo cha kunyongwa alipotakiwa kuzungumzia adhabu hiyo aliongea kwa uchungu kuwa kitendo cha kutenganishwa na mpendwa wao huku wakiwa hawajui mwili wake utazikwa wapi baada ya adhabu hiyo kutekelezwa kimewauma sana.
Mwisho

Wednesday, June 27, 2012

WAKULIMA WA KOROSHO WALILIA MADAWA YA KUUA VISUMBUFU


Na Steven Augustino, Tunduru
WAKULIMA wa Korosho Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma wameiomba Serikali kuwa na msukumo na kuhakisha Madawa ya Pembejeo za bei ya ruzuku ambayo hutumika kwa ajili ya Kupulizia na kuua visumbufu katika mikorosho yao yanafika kwa wakati.
Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya wakulima hao walisema kuwa malalamiko hayo yametokana na kuwepo kwa taarifa za kutatanisha juu ya ujio wake huku mikorosho yao ikiwa katika hali ya kuhitaji kupuliziwa baada ya kuchanua
Mtua issa,Kawanga Abdala na Milanzi Athuiman ni miongoni mwa wakulima waliopaza sauti zao na kuongeza kuwa endapo madawa hayo yataendelea kucheleweshwa kuna hatari ya wakulima hao kuanguka kimavuno msimu huu wa mwaka 2012/2013.

Walisema hali hiyo inatokana na wakulima wengi kushindwa kumudu bei ya Shilingi 45,000/= kwa mfuko wa kilo 25 za madawa hayo kutoka kwa wafanyabiashara walanguzi tofauti na bei ya ruzuku ambayo mfuko huo ulipangwa kuuzwa kwa Shilingi 12,000.
Akizungumzia hali hiyo Afisa Kilimo wa Wilaya hiyo Chiza Marando alisema kuwa tayari ofisi yake imekwisha kabidhi kazi hiyo kwa Mzabuni aliyeteuliwa kusimamia usambazaji wa madawa ya ruzuku ya y a asilimia 50% kutoka Serikalini yakiwemo ya viuatilifu vya kudhibiti visumbufu vya wadudu katika Mikorosho ya wakulima hao tangu mei 29 mwaka huu.

Marando aliendelea kufafanua kuwa uteuzi huo ulifanyka katika kikao kilichofanyika mei 8 mwaka huu baada ya kamati inayosimamia zao hilo kuridhika na sifa zilizohitajika kati ya Wazabuni Wanne (4)
wakiwemo Halima Luambano, Mohamed kionjo na Alli Chimwa.

Alisema katika mkataba huo unaomruhusu Namhala kusambaza pembejeo hizo unaonesha kuwa jumla ya Madawa yenye thamani ya shilingi 144,294,600/= yamepangwa kusambazwa kwa Wakulima wa wilaya hiyo zikiwemo Kilo 234,194 za Sulphur ya Unga madawa ya maji lita 6183 zikiwemo lita 2,108 za Mupavil,Lita 1,171 za duduali, lita 1,405 za Faipro na lita 234 za dawa aina ya Rav.
Upande wa Mzabuni huyo aliyeteuliwa na Kamati inayosimamia usambazaji wa Pembejeo za Ruzuku kwa Wakulima wa Korosho Wilayani Tundudru Mkoani Ruvuma Zuberi Rashid Namahala alipo takiwa kuzungumzia maendeleo ya mradi huo alianza kwa kuulalamikia uongozi wa Mfuko unaosimamia
ukuzaji wa zao hilo kwa urasimu na ucheleweshaji wa Madawa ya mgao uliyopangwa kupelekwa kwa wakulima wa Wilaya hiyo.
Aidha katika taarifa hiyo Namahala alidai kuanza kupoteza imani na uongozi wa mfuko huo ambao tayari amekwisha walipa fedha hizo tangu Mei 29 mwaka huu kupia katika akaunti namba 0150237061700 inayomilikiwa na mfuko huo katika Mabenki ya CRDB tawi la Mtwara na toka wakati huo hajakabidhiwa hata mfuko mmoja wa madawa hayo kitendo alicho kitilia mashaka kuwa huenda wanapanga mambo ya kufanyia utapeli wa fedha hizo.
Alisema kufuati hali hiyo ofisi yake ina andaa utaratibu wa kutafuta mwanasheria ili amsaidie kuangali utaratibu wa kukatisha mkataba huo na kudai arudishiwe fedha zake kwa madai kuwa ucheleweshaji huo utamfanya ashindwe kumudu kulipia mkopo wake benki na kumsababishia hasara.
Akiongea kwa njia ya Simu Mwenyekiti wa mfuko wa kuendeleza uzarishaji wa Korosho Tanzania Athumani Nkinde mbali na kukiri kupokelewa kwa fedha za mzabuni huyo, alisema kuwa chanzo cha kuchelewa kwa madawa hayo kunatokana na kuangushwa na Mzabuni aliyeteuliwa na Mfuko huo
kampuni ya Export Treding iliyo pewa kazi ya kusambaza Tani 5000 ambayo hadi wanakatisha mkataba Mei 4 mwaka huu ilikuwa imemudu
kuingiza tani 800 tu.
Alisema baada ya kukatishwa kwa mkataba huo Mfuko ulimteua wakala mwingine kampuni ya HAMAS (T) LTD katika kikao kilicho keti Mei 31 mwaka huu na kuahidiwa kuletewa madawa hayo mwishoni mwa mwezi huu.

Kufuati hali hiyo Nkinde pamoja na mambo mengine aliwaomba radhi wakulima hao na akawataka kuwa wavumilivu wakati taratibu za ufuatiliaji wa madawa hayo zikiendelea na akatumia nafasi hiyo
kumuomba Namahala kwenda kuchukua madawa ya maji aliyodai kuwa tayari yapo kwa wingi iIi yasambazwe ili wakulima wapulizie mikorosho yao awamu ya kwanza huku akiahidi kuwa awamu itakayo fuata watapuliza dawa ya Sulpur ya unga waliyo izowea.

Nae Mbunge wa Jimbo la Tunduru kusini alhaji Mtutura Mtutura alipotakiwa kuzungumzia ucheleweshaji wa madawa hayo aliahidi kutoa taarifa sahihi baada ya kuwasiliana na Waziri mwenye dhamana.
Mwisho

Tuesday, June 26, 2012

VIONGOZI WATAKIWA KUWA WAKWELI KATIKA MAJUKUMU YAO

Na Steven Augustino,Tunduru
IMEBANISHWA kuwa tabia za uongo miongoni mwa jamii yetu ndiyo chanzo cha kukosekana kwa ukweli na utendaji mbovu wa viongozi na watendaji wa Serikali na kumesababisha hali mbaya ya upatikana wa huduma za Utawala na Uchumi.

Hayo yameainishwa na baadhi ya wakazi wa Jimbo la Tunduru Kusini Wilayani humo Mkoani Ruvuma wakati wakazi hao waliposhiriki  mdahalo uliojadili Utawala Bora na uwajibikaji wa Viongozi wa serikali kwa wananchi uliofanyika katika Ukumbi wa Klasta mjini hapa.

Kufuatia hali hiyo wananchi hao pia wamedai kuwa ili kuongeza ufanisi na uwajibikaji kwa watumishi serikali inapaswa kuunda mfumo utakaowawajibisha haraka viongozi wabovu badala ya kutumia muda mrefu wa kuendesha kesi

Wakizungumza kwenye mdaharo huo Selemani Kachonjo kutoka kijiji cha Lukumbule, Athuman Milanzi na Casiana Magogwa ambao ni miongoni mwa makundi ya Jamii yaliyokutanishwa na Mtandao wa Asasi za Kirai wilayani Tunduru (MATU) chini ya mwavuli wa The foundation for Civil Society, kilio chao kwa niaba ya wananchi wenzao ni kwamba watawala bado hawajawaangalia kwa jicho la Umakini wananchi wanaowatawala hususani waishio pembezoni mwa Nchini ikiwemo Wilaya yao.

Pamoja na mambo hayo wananchi hao wamelalamikia kero za kutotatuliwa kwa matatizo ya wakulima, kushamiri kwa rushwa na kile walichokiita kuwa chanzo chake ni uongo uliotawala katika shughuli zote za utoaji huduma za utawala kwa wananchi yaliyobainishwa na
Monica Mbogolo na Abdalah Mgwila.

Aidha katika ya maoni hayo pia Abdalah Kawanga na Issa Mtua kwa niaba ya wananchi wakaibua tatizo linalo wakabili wakulima wa zao la Korosho ambapo wananchi wanadai kuwa ukosefu wa uwajibikaji kwa watendaji wa serikali ndio uliosababisha mpaka leo wakose malipo yao ya pili ya Korosho walizo uza msimu uliopita.

Awali Mchokonozi wa mada katika mdahalo huo, Afisa Uchunguzi Mwandamizi wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa Mkoani Ruvuma (TAKUKURU) Hamis Kidulani na Mwenyekiti wa Mtandao wa asasi za Kiraia Wilayani Tunduru  John Nginga walisema kuwa ili kuyafikia maendeleo ya kuanza kufaidi maziwa na asali bila ubaguzi watanzania wanapaswa kujenga utamaduni wa kuzingatia sheria.

Akifungua mdaharo kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Tunduru  Afisa tawala wa Wilaya hiyo Maltin Mulwafu katika hutuba yake alisisitiza uwazi na uwajibikaji kwa viongozi na Wananchi wake na kuwataka wasikubali kuona misingi ya utawala bora inakiukwa.
Mwisho

Monday, June 25, 2012

Liveee Muda Huu: Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Nape Nauye awasili Jijini Mbeya na Kukutana na wanafunzi wa chuo cha TEKU, na kuwakabidhi kadi za Chama hicho

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nauye Muda mfupi baada ya kuwasili jijini Mbeya
Viongozi mbalimbali waliofika pamoja na wanafunzi wa Chuo cha TEKU wakiwa wanasililiza jambo kwa umakini
Wanafunzi wa TEKU wakiwa wanafurahi huku mkutano ukiendelea
Makada mbalimbali wa Chama Cha mapinduzi wakiwa katika mkutano huo

Shughuli zinaendelea Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nauye akiwa anacheza Muziki pamoja na wanafunzi wa TEKU muda huu

Sunday, June 24, 2012

MIAKA 15 JERA KWA KOSA LA KUUA BILA KUKUSUDIA


Na Augustino Chindiye, Tunduru
Mahakama kuu Tanzania kanda ya Songea Mkoani Ruvuma kupitia vikao vinavyofanyika Wilayani Tunduru imemhukumu Said Adam (25) kutumikia kifungo cha miaka 15 baada ya kupatikana na hatia ya kosa dogo la kuua bila kukusudia.

Hukumu hiyo ilitolewa baada ya Adam kukiri kwa hiari yake kufanya kosa hilo kinyume cha Sheria ya kanuni ya adhabu namba 195 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2002 ambapo alidaiwa kumuua
kikongwe marehemu Asha Ramadhani (63)ambaye kifo chake kilisababishwa
na tukio la kumbakwa.

Akitoa hukumu hiyo hakimu mkuu mwenye mamlaka ya Ki Jaji Wilifred Ndyansobera alisema kuwa pamoja na kuzingatia ungamo la mtuhumiwa huyo mahakama yake imemtia hatiani kwa kosa hilo na kwamba adhabu hiyo ni halali ukilinganisha na kosa alilolifanya.
   
Awali akimsomea shitaka Mwanasheria wa Serikali Wilibrod Ndunguru alidai mbele ya mahakama hiyo kuwa Said Adamu kwa kukusudia kinyume cha Sheria ya kanuni ya adhabu namba 196 sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 alimuua kikongwe huyo katika tukio la ubakaji na  kifo chake July 18/2011 katika tukio lililotokea katika kijiji cha Naleo Wilayani Namtumbo kosa ambalo mtuhumiwa kuyo alilikanusha kuto litenda.

Baada ya mtuhumiwa huyo kukana kufanya kosa hiyo Wakiri wa Utetezi  Dickson Ndunguru aliiomba mahakama hiyo imsomee mteja wake kosa dogo la kuua bila kukusudia endapo upande wa Jamhuri haunge kuwa na pingamizi na ombi hilo na kukubaliwa na kumuomba mteja wake akiri baada ya upande wa Jamhuri kutokuwa na pingamizi katika Shauli namba 4/2012.

Baada ya mtuhumiwa huyo kukiri upande wa Jamhuri unao ongozwa na Wilbroad Ndunguru aliiomba mahakama hiyo impatie adhabu kali kwani kosa alilo litenda ni baya nani la kinyama.

Naye mwanasheri wa Utetezi  Dickson Ndunguru katika hoja zake aliiomba mahakama hiyo impatie adhabu ndogo kwasababu ni mkosaji wa mara ya kwanza,amekiri kosa hilo na kuondolea usumbufu mahakama pamoja na kuokoa muda na kwamba kosa hilo alilifanya kwa bahati mbaya na kujikuta akisuguana na Sheria.
Mwisho

Saturday, June 23, 2012

WANAWAKE WATAKIWA KUJIUNGA NA CHADEMA KWA UKOMBOZI


Na Stephano Mango, Songea
WANAWAKE nchini wametakiwa kuzisikiliza sera za Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema na kujiunga na chama hicho chenye malengo ya kuleta ukombozi kutoka mikononi mwa Chama cha Mapinduzi ambacho kimewanyonya watanzania kwa muda mrefu na kuwafanya maskini
Wito huo umetolewa jana na Katibu wa wanawake wa Chadema Jimbo la Songea Asia Ngonyani akiwahutubia mamia ya wananchi baada ya kufungua Tawi la Chadema na Ofisi ya Chama hicho mtaa wa Kuchile kata ya Seedfarm Halmashauri ya Manispaa ya Songea  kwenye ziara  yenye lengo la kuimarisha chama katika kata za pembezoni mwa mji
Ngonyani alisema kuwa Chama cha Mapinduzi kimekuwa kikiwatumia wanawake kwenye chaguzi mbalimbali na kuwavesha vilemba na vitenge ambavyo hata ukivaa vinaangaza na baada ya kumaliza uchaguzi na kuunda Serikali ambayo imekuwa ikikosa mipango na vipaumbele vya kuwakomboa wanawake kiuchumi na kijamii
Alieleza kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi imekuwa ikiwanyanyasa na kuwadhalilisha sana wanawake wanapokuwa kwenye biashara zao ndogondogo kwa kuwakamata na kuwanyang’anya vitu vyao kwa kutumia mgambo wa mji hali ambayo inaendelea kuwaondolea utu katika jamii
Alisema kuwa kwa muda mrefu Serikali imekuwa ikiwadanganya wakina mama kuwa huduma za kujifungua ni bure na matibabu ya mtoto wa chini ya miaka mitano ni bure wakati wakina mama wanalipia huduma hizo kwa fedha nyingi
Alifafanua kuwa licha ya wakina mama kulala wanne wanne kwenye kitanda kimoja na wengine kulala chini , basi ukitaka kufa au kupoteza mtoto katika vituo vya afya au Hospital za Serikali usiwe na fedha au umwambie muuguzi kuwa natakiwa kupata huduma za matibabu bure
Naye Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Ruvuma na Diwani wa Kata ya Mjini Joseph Fuime  akiwahutubia wananchi hao alisema kuwa Serikali imeshindwa kuwaheshimu watanzania kutokana na matendo yao katili dhidi ya wananchi kutokana na kuwapandishia gharama za maisha kila kukicha,kushindwa kutekeleza ahadi ya maisha bora kwa kila mtanzania,kuwatoza kodi nyingi huku wakishindwa kutoa huduma stahiki kulingana na kodi zinazotozwa kwa wananchi
“Ili kufanya mabadiliko katika nchi hii ni lazima wananchi waamue kuchukua hatua za kuzisikiliza sera za Chadema na kujiunga nacho ili kuweza kuleta ukombozi stahiki mara uchaguzi wa Serikali za Vijiji,Mitaa na katika uchaguzi mkuu wa Madiwani,Wabunge na Urais”alisema Fuime
Alisema kuwa leo tumefungua Ofisi ambayo imegharamiwa na baadhi ya wanachama wa Chadema katika kata yenu hivyo tumewaletea chama chenye uhai na matumaini kwa watanzania na ambacho kina dhamira ya kweli ya kuwakomboa watanzania
Alieleza kuwa hakuna anayelazimishwa kukipokea na kujiunga nacho hivyo kama mnataka kuendelea kukandamizwa na Serikali ya Ccm miaka 50 ijayo ya uhuru,mnahiyali ya kukipokea au kukikataa kwa faida yenu na vizazi vijavyo
MWISHO

WASAFIRISHAJI RUVUMA WAIDAI SERIKALI ZAIDI YA MILIONI 375

Na Stephano Mango, Songea
WASAFIRISHAJI wa Mizigo mkoani Ruvuma wameitaka Serikali kupitia  Wizara ya Kilimo,Chakula na Ushirika kuona umuhimu wa kuwalipa deni la fedha zaidi ya milioni 375 wanazozidai kwenye kitengo cha Taifa cha kuhifadhi mahindi kilichopo mkoani Ruvuma (SGR) baada ya kufanya kazi ya kubebelea mahindi kutoka vijijini na kuyaleta kwenye hifadhi hiyo mwaka 2011
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wasafirishaji hao ambao wameomba majina yao yahifadhiwe walisema kuwa walikopwa kuyabebelea mahindi hayo kwa ahadi kuwa fedha zao wangelipwa mara baada ya kumaliza kubebelea na kuyaleta kwenye hifadhi lakini cha ajabu toka wamemaliza kuyaleta mahindi hayo ambayo tayari yameuzwa na Serikali hawajalipwa hali ambayo inaendelea kuwakatisha tamaa
Walisema kuwa wafanyabiashara wengine waliikodisha Serikali Magodauni ili wahifadhi mahindi hayo kwa sababu Magodauni ya kituo cha Hifadhi kilichopo mjini hapa hayakuwa na uwezo wa kuhifadhi mahindi yaliyokuwa yanabebelewa na wasafirishaji kutokana na uwingi wake, pia wapo wafanyabiashara ambao walikopwa mafuta lakini wote hawajalipwa
Walisema kuwa Wasafirishaji hao walijitahidi kwa uaminifu mkubwa kuyabebelea mahindi hayo kutoka kwenye maeneo ambayo miondombinu yake ni mibovu sana huku mafuta na vipuri vya magari vikipanda kila mara hivyo tumepata tabu sana na sasa biashara zetu zinayumba tunaiomba Serikali itulipe fedha zetu
Walieleza kuwa wafanyabiashara hao wana mikopo ya biashara Benki na wanalipa kodi mbalimbali zikiwemo za Mamlaka ya Mapato (TRA) na wanachangia michango mbalimbali ya maendeleo mkoani hapa lakini wanashangazwa na kitendo cha Serikali cha kutowathamini wasafirishaji hao kwa kuwacheleweshea fedha zao hali ambayo inasababisha kupungua kwa mzunguko wa fedha mkoani Ruvuma na kupungua kwa kasi ya ulipaji wa kodi kutokana na madeni wanayodaiwa
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) mkoani Ruvuma Mays Mkwembe alisema kuwa wafanyabiashara wengi ambao waliikopesha Serikali ili kuweza kufanikisha uletaji wa mahindi mjini wamekuwa wakihangaika sana katika shughuli zao kutokana na fedha nyingi kuidai Serikali
Mkwembe alisema kuwa ni vema Serikali ikawalipa wafanyabiashara haraka ili waweze kulipa kodi ambazo wanadaiwa katika msimu wa fedha wa 2011/2012 kwani bila kufanya hivyo hali ya mapato ya mkoa yatakuwa ni madogo sana kuliko ilivyopanga, ingawa pia wafanyabiashara wengi wanadaiwa riba kwenye taasisi za fedha kutokana na mikopo waliyoikopa
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Hassan Bendeyeko alikiri kuwa wafanyabiashara wanaidai Serikali kutokana na huduma waliyoitoa hivyo wasubiri kidogo kwani Serikali inaandaa utaratibu wa kuwalipa haki zao kama ambavyo makubaliano yalivyo kwani Serikali inatambua mchango wao katika harakati za kimaendeleo mkoani hapa na taifa kwa ujumla.
MWISHO

Friday, June 22, 2012

WAZEE WAIOMBA SERIKALI KUU KUISAIDIA WILAYA YA TUNDURU


Na Augustino Chindiye, Tunduru
WAZEE wa Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma wameiomba serikali kuu kuisaidia Wilaya yao kwa hali na mali ili iweze kupiga hatua za kimaendeleo.

Sambamba na ombi hilo wazee hao pia wamebainisha kero za ucheleweshaji wa pembejeo kwa ajili ya matumizi ya kilimo hali ambayo ilidaiwa kuwa ni miongoni mwa vikwazo vya wakazi wa wilaya hiyo kupata mavuno ya kuwatosheleza kwa chakula na biashara katika harakati za kujiongezea vipato.

Wazee hao walitoa ombi hilo wakati wakiongea na Mkuu wa Wilaya hiyo Chande Nalicho katika kikao cha kujitambulisha kwa wazee hao kilichofanyika katika ukumbi wa Boma Mjini hapa.

Ndawambe Salum, Ajulu Kalolo na Mapunda Chikambo ni miongoni mwa wazee waliotoa ombi hilo huku wakibainisha kuwa wakazi wa Wilaya hiyo ni wavivu na hawapendi kujituma na kwamba serikali isipotoa msukumo wa matumizi ya nguvu ya dola watabaki katika lindi la
umasikini wa kupindukia.

Wazee hao waliendelea kubainisha kuwa Wilaya hiyo iliyozaliwa na kutangazwa kuwa Boma mwaka 1941 sawa na Mji mkuu wa Nchi ya Kenya Nairobi imekuwa haipigi hatua za kimaendeleo kutokana na viongozi wake kuwa wapole na wasiopenda kutumia mabavu ya nguvu za dola.

Wakifafanua kero ya ucheleweshaji na ukubwa wa bei za pembejeo walisema kuwa wakulima wengi wamekuwa wakishindwa kumudu bei ya mbolea za ruzuku kutokanana kukosa kipato hali ambayo imekuwa ikiwanufaisha wajanja wachache wakiwemo watendaji wa vijiji ambao wamekuwa wakiziuza  haki za wazee hao baada ya kukosa fedha za kumudu kuchangia.

Kuhusu zao la Korosho ambalo ndio tegemeo kwa wakulima wengi wazee hao walidai kuwa hadi sasa Sulphur ya Ruzuku iliyotolewa na Serikali bado haijafika na ni kitendawili kisicho kuwa na mteguzi kutokana na kila kiongozi anaye hojiwa majibu yake huonekana kutotoa matumaini huku mikorosho yao ikiwa imefikia kuhitaji kupuliziwa.

Aidha wazee hao pia wakatumia nafasi hiyo kumuomba Mkuu wa Wilaya hiyo kuwa mkali katika usimamizi wa shughuli zote za kimaendeleo na kutoa msukumo wa kipekee katika elimu ili nao waweze kupiga hatua.

Akijibu hotuba hiyo pamoja na mambo mengine Dc, Nalicho kufuatilia kero zao akaahidi kuwa msimamizi mzuri wa maendeleo na kuiwezesha wilaya hiyo kupiga hatua za kimaendeleo.

Dc, Nalicho alimaliza kwa kuwataka wazee na wananchi wa Wilaya hiyo kutoa ushirikiano katikia utekelezaji wa miradi iliyopangwa kutekelezwa wilayani humo.
Mwisho

Thursday, June 21, 2012

UWEKEZAJI WA MABWAWA YA SAMAKI MJINI SONGEA UTAINUA UCHUMI WA SONGEA

 Mabwawa haya yanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo fensi ya uhakika, ulinzi na endapo changamoto hizo zikathitiwa kwa ukamilifu ingekuwa ni kichocheo kikubwa cha upatikanaji wa samaki kwa wingi na ukuaji wa uchumi mjini Songea kwani mabwawa haya ni makubwa sana na yanauwezo wa kulisha idadi ya watu wengi mjini hapa








NAPE ARUSHIWA KOMBORA MKOANI RUVUMA

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Ruvuma na Diwani wa Kata ya Mjini Manispaa ya Songea akiwahutubia wananchi wa Kata ya Mshangano kwenye eneo la Stendi ya Maroli (hawapo pichani) kwenye moja ya mikutano ya oparesheni vua gamba vaa gwanda inayoendelea mkoani Ruvuma
    Diwani wa Viti Maalumu wa Chadema Manispaa ya Songea Roda Komba
Kiongozi wa Chadema Kata ya Mjini Abdalah Komba akizungumza kwenye moja ya mikutano hiyo


Na Mwandishi Wetu, Songea
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoani Ruvuma kimemtaka Katibu wa halmashauri kuu ya CCM Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kuacha kuwadanganya wananchi kwa kuwapa matumaini ambayo yanaendelea kuwatesa kwa sababu ya kuokoa chama ambacho kinaendelea kufa
Wito huo umetolewa jana kwenye mikutano miwili tofauti yenye lengo la kuwahamasisha wananchi kuvua Gamba na kuvaa Gwanda iliyofanyika kwenye Kata ya Msamala na Kata ya Seedfarm na Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Ruvuma ambaye pia Diwani wa Kata ya Mjini Joseph Fuime ambapo katika mikutano hiyo jumla ya watu 60 walijiunga na chama hicho,ambapo kati yao viongozi wanne wa Ccm kata ya Seedfarm walijivua gamba na kuvaa gwanda
Fuime alisema kuwa Chama cha Mapinduzi kimemtuma Nape azunguke nchi nzima na kuendelea kuwadanganya wananchi kwa kutoa maagizo kwa Serikali ambayo imeshindwa kuifikisha nchi kwenye ustawi stahiki miaka 50 tuka tupate uhuru
Alisema kuwa Serikali iliyopo madarakani inaongozwa na Ccm hivyo maneno ambayo anazunguka nchi nzima kuyaongea Nape ni kuwadanganya wananchi kwani alipaswa amwagize Rais Jakaya Kikwete kwenye vikao vyao vya chama na wananchi waone utekelezaji na sio kutoa maagizo ambayo mtekelezaji wake ameshindwa toka alivyokuwa Rais mwaka 2005
Alifafanua kuwa Serikali ya Ccm toka mwaka 2005 hadi sasa imeshindwa kuwakomboa wananchi kutokana na umaskini ambao unawakabili bali kila siku imekuwa ikiwanyang’anya uwezo wa kuyafikia maisha bora kwa kuwapandishia gharama za maisha kupitia mfumuko wa bei na wafanyabiashara wengi wamekuwa wakitoa huduma kwa Serikali na kuwacheleweshea malipo hali ambayo inaendeleza ugumu wa maisha
Alieleza kuwa baadhi ya wafanyabiashara walihifadhi mahindi ambayo yalinunuliwa na Serikali kwenye magodauni yao na wengine waliyasafirisha mahindi hayo kutoka Songea kuyapeleka Makambako na Dar Es Salaam lakini hawajalipwa hadi leo jambo ambalo linaendelea kuwafanya wananchi wa mkoa wa Ruvuma ambao una viwanda vichache kuishi katika maisha magumu
Naye Diwani wa Viti Maalumu wa Chadema Manispaa ya Songea Roda Komba alisema kuwa  Chadema ndicho chama chenye dhamira ya kweli ya kuwakomboa Watanzania wote katika lindi la umasikini, ujinga na maradhi hivyo wananchi kuweni makini sana na porojo za Chama cha Mapinduzi kwani hakina jambo jipya watakalowafanyia wananchi kwasababu kwa muda mrefu wamekuwa wakiwaongoza bila kuleta tija.
Komba alisema kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi imeshindwa kuwajali wananchi ,wakiwemo wazee kwa muda mrefu kwa kushindwa kuwapatia huduma stahiki za jamii na kuwasababishia kuona maisha ya uzeeni kama ni hatari ambayo inapaswa kuogopwa
Alisema kuwa katika nchi nyingine wazee wanaheshimika na wanapewa huduma za jamii bure ikiwemo matibabu na pensheni kwa wazee bila kujali kuwa ulifanya kazi serikali kwani mchango walioutoa katika ujenzi wa taifa walipokuwa vijana unatosha kuwaenzi wanapokuwa wazee
MWISHO



Thursday, June 14, 2012

MAGUFURI AITWA MAHAKAMANI


 
Na Mustapha Kapalata, Nzega

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Tabora, jana ilipokea ombi la upande wa walalamikaji la kumtaka Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli ili afike mahakamani hapo Juni 19, mwaka huu, kujibu tuhuma zinazomkabili.

Hatua hiyo ni mwendelezo wa kusikiliza maelezo ya mashahidi kwenye kesi ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi Mbunge wa Igunga, Dk. Dalaly Kafumu (CCM).

Shauri hilo lilifunguliwa na mlalamikaji, Joseph Kashindye, aliyekuwa mgombea ubunge wa CHADEMA dhidi ya Dk. Kafumu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na msimamizi wa uchaguzi.

Mapema, Wakili Kayaga Kamaliza anayewakilisha upande wa Dk. Kafumu aliiomba mahakama hiyo itoe hati ya kumtaka Waziri Magufuli afike mahakamani hapo kupitia Ofisi za Bunge Dodoma.

Dk. Magufuli ni mmoja kati ya mashahidi muhimu wanaotegemewa katika kesi hiyo kwa upande wa utetezi.

Wakati akitoa maombi hayo, pande zote mbili za walalamikaji na serikali, hazikuwa na hoja za kupinga kufuatia wito huo kwa Waziri Magufuli.

Tuhuma zinazomkabili Magufuli ni pamoja na kutoa ahadi za ujenzi wa daraja la Mbuntu ambalo ni moja ya changamoto jimboni humo, kutao ahadi za kugawa mahindi ya njaa kwa wananchi wa jimbo hilo, na viapo kwa baadhi ya ahadi alizokuwa akizitoa katika majukwaa ya kumnadi Kafumu kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa Igunga.

Jaji Mery Shangali, akitoa uamuzi juu ya hati hiyo alisema kuwa, mahakama imekubali ombi hilo la kuituma kwa Waziri Magufuli ili afike mahakamani hapo tarehe hiyo kutoa ushahidi wake.

Wakati huo huo, Profesa Abdallah Safari anayemtetea Kashindye, aliiomba mahakama hiyo iahirishe shauri hilo kufuatia mazishi ya muasisi wa CHADEMA, Bob Makani, yaliyofanyika jana mkoani Shinyanga, akidai ni lazima naye ahudhurie kama mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho.

Jaji Shangali alikubali, na hivyo kuihairisha kesi hiyo hadi leo ambapo itaendelea kusikilizwa, huku mashahidi zaidi ya 43 wakiwa wametoa ushahidi wao, 20 wakiwa ni upande wa mlalamikaji na 20 kwa upande wa utetezi pamoja na Magufuli na washtakiwa wengine wawili.

Tuesday, June 12, 2012

Rais Kikwete amwapisha RAS wa Mkoa wa Ruvuma na apokea Vitabu vya Hadithi za Kikwere

 

Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Ruvuma Bwana Hassan Mpapi Bendeyeko akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili TATAKI Dkt.Aldin Mutembei akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kitabu cha kwanza cha fasihi simulizi ya jamii ya Wakwere ikulu jijini Dar es Salaam leo. Kulia anayeshuhudia ni Mkuu wa Idara ya historia katika chuo kikuu cha Dar es Salaam Profesa Kapepwa Tambila. Dkt. Mutembei ambaye pia ni mchapishaji na msimamizi wa tafiti za Tamaduni lugha na fasihi za makabila ya Tanzania alikabidhi pia kamusi Asisi ya Kiingereza-Kiswahili na Kiarabu. (picha na Freddy Maro).

Saturday, June 9, 2012

WASAMALIA WAOMBWA KUTOA MSAADA WA MATIBABU KWA MTOTO FAHAHATI

Na Steven Augustino, Tunduru

WASAMALIA  nchini wameombwa kutoa msaada wa hali na mali ili kusaidia matibabu ya Mtoto Fahahati Rajab anayetakiwa kufanyiwa upasuaji wa kuwekewa sehemu ya kutolea haja kubwa na matundu ya masikio.
Ombi hilo limetolewa na wazazi wa Mtoto huyo Bwana na Bibi Rajab Idd wakidai kuwa hali hiyo imetokana na familia yao kutokuwa na uwezo wa kughalamia matibabu hayo yanayotarajiwa kufanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Walisema Mtoto huyo aliyezaliwa akiwa hana sehemu ya kutolea haja kubwa na matundu katika masikio July 4 2011 katika Hospitali ya Missioni ya Mbesa Wilayani humo ambako  awali watalamu wake
waliahidi kutoa msaada wa matibabu lakini kadili siku zilipo enda waliwajibu kuwa wameshindwa na kuwaomba wampeleke muhimbili.

Walisema mtoto huyo ambaye ni mzao wao wa kwanza kwa sasa ana umri wa miezi 11 hula na  hujisaidia kupitia mdomoni hali ambayo imekuwa ikiwawia vigumu watu wangine kumsaidia kutokana na kuona kinyaa.

Walisema kuwa atakaye guswa na hali hiyo anaombwa kutoa msaada wake autume kwa njia ya M-pesa kupitia namba 
0758168501
inayo mirikiwa na Baba Mzazi wa Mtoto huyo  Rajab Idd ili kuwawezesha kusafiri hadi jijini Dar es Salaam na kughalimia matibabu hayo.

Akizungumzia tukio hilo Mganga Mkuu wa Hospitali ya Serikali ya Wilaya Tunduru Dkt.Alex Kazula alisema kuwa hospitali yake ina andaa utaratibu wa kumpeleka Mtoto huyo katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili.

Mwisho

JERRY MURO:NARUDI TBC..JUMAPILI HIINITAFANYA HAYA...

 

Mtangazaji/Mwandishi wa habari ambae alisimama kufanya kazi kwa miezi kutokana na kesi ya kuomba rushwa, kesi ambayo baadae alitangazwa kushinda, ametangaza kituo chake cha kazi baada ya wengi kutomuona kwa muda TBC alikokua akifanya kazi.

Jerry amesema anarudi kufanya kazi TBC na jumapili hii saa tatu na nusu usiku ndio kipindi chake cha kwanza kitaanza kuonekana ambapo kitakua kinaingia kwenye siasa, afya, Uchumi na mengine.

Jerry amethibitisha kwamba wakati alipokua kimya baada ya kushinda kesi kuna vituo vingi vya TV Tanzania ambavyo vilitaka kufanya kazi na yeye lakini alishindwa kwa sababu vituo vingi sasa hivi vinafanya kazi kwa makundi ya kisiasa, vingine vimeegemea upande mmoja ndio maana akaamua atumikie kwanza wananchi.
“Sio kwamba TBC ndio mwisho wangu lakini ni sehemu ambayo naweza kukaa na kuangalia nakwenda wapi nafanya nini sehemu gani, kila kitu lazima kiwe na mwanzo kwa hiyo hilo kwangu ni mwanzo tu lakini kama nafasi nzuri zitajitokeza basi zitapewa nafasi”Jerry Muro

Friday, June 8, 2012

UJIO WA FILAMU YA ADELAHIDA NI NGUZO MUHIMU KATIKA KUINUA TASNIA YA FILAMU MKOANI RUVUMA

 

Kaa tayari kwa Filamu ya Adelahida iliyotayarishwa na Mtayarishaji anayechipukia Shukrani K.Faraji.
 
Ni ndugu wa mapacha watatu Ade,Lah na Ida wanakuja kukutana tena baada ya kupoteana kwa muda wa miaka ishirini.
 
Kujua kilichosababisha utakiona ndani ya Filamu hii kwani ipo mitaani.
 
Ni filamu iliyotengenezwa kwenye mazingira ya asili katikati ya Misitu ya maeneo ya milima ya Matogoro-Songea.
 
Filamu hiyo itazinduliwa rasmi katika Ukumbi wa Songea Club Tarehe 1,7,2012 majira ya alasiri

MWAKYEMBE ALIPUKA TENA NA AANIKA MADUDU YALIYOMNG'OA MKURUGENZI ATC



Na Nasra Abdallah

WAZIRI wa Uchukuzi, Dk. Harison Mwakyembe, ameendelea kuwasha moto ndani ya Shirika la Ndege (ATCL) ambapo jana aliweka bayana sababu kadhaa za kutengua uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Paul Chizi.

Akizungumza na wafanyakazi wa shirika hilo katika karakana ya uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam, Mwakyembe alisema kamwe hawezi kufanya kazi na watendaji wabovu na kuwataka wale walioumizwa na maamuzi yake kuacha kazi mara moja.

Huku akionyesha kukasirika, waziri huyo aliapa kuendelea kufukuza watendaji wengine zaidi watakaobainika kwenda kinyume na sheria.
Akitaja sababu zilizomwondoa Chizi, alisema kuwa uteuzi wake haukuzingatia tarartibu za utumishi wa umma.

“Chizi katika ripoti yake ya uzoefu wa kazi inaonekana kuwa alishastaafu kwa mujibu wa sheria ambapo kwa wafanyakazi wa aina yake kuna taratibu za kuwaajiri, hivyo anatakiwa azifuate ili kuajiriwa tena,” alisema.

Mbali na hilo, sababu nyingine iliyomponza mkurugenzi huyo ni kuingia mkataba wa kukodi ndege bila ridhaa ya serikali wala wizara husika.
Hata hivyo, Dk. Mwakyembe alipotakiwa aeleze kwa nini mkurugenzi huyo alifanya hivyo, alisema anaogopa kusema kwani huenda akazidi kuibua mjadala zaidi katika taifa.

“Inasikitisha sana kuona kuwa ilifika mahali watu wakaona shirika ni mali yao na kufanya maamuzi vile wanavyotaka huku wakisahau kwamba wananchi wanaliangalia shirika hilo linavyouawa,” alisema.

Alisema kuwa serikali mbali na kutoridhia pia ukodishwaji huo haukufuata taratibu za manunuzi ya umma kwani ndege hiyo ilinunuliwa nchini Liberia ambako bidhaa zote chakavu ‘mikweche’ kama baiskeli, pikipiki na ndege zimekuwa zikipelekwa huko na nchi zilizoendelea.

Alieleza kukerwa na kitendo cha watendaji wa shirika hilo kujinunulia magari ya kifahari wakati serikali ilitoa fedha ili shirika lifufuke.

“Maana inashangaza iweje idara na kampuni ndogo zinaweza kujiendesha na kusimama zenyewe lakini ATCL imekuwa ikibebwa hadi leo pamoja na kuwa na wafanyakazi wazuri ambao wakienda kufanya kazi katika makampuni mengine wanafanya vizuri,” alihoji.

Alisema kuwa serikali inajua wako mawakala wa makampuni ya ndege binafsi, wanaodhani wataiua ATCL kumbe wanajiua wenyewe, na hivyo kuwaonya akisema kama bado wapo ni bora waondoke wenyewe kabla hajawaondosha.

Alisema yuko tayari kufikishwa mahakamani kwa ajili ya suala hilo kwani wanaofanya hivyo ni sawa na kuchezea sebuleni kwake.
Akifafanua zaidi madudu ndani ya ATCL,

 Mwakyembe alisema kuwa fedha za bima ya ndege iliyodondoka mkoani Kigoma takriban dola bilioni saba, tatu za awali zililipwa na iliagizwa ziingizwe katika akaunti ya Shirika Hodhi la Mashirika ya Umma(CHC) lakini watendaji wakafanya kinyume.

“Watendaji hao hawakufanya hivyo na kuamua kuziingiza katika akaunti ya ATCL, ambapo kati ya fedha hizo tumekuta dola bilioni mbili na dola bilioni moja zilizosalia hazijulikani zilipopelekwa,” aliongeza.

Waziri huyo aligusia pia hatua ya baadhi ya maafisa kwenda nchini China na kukaa huko takriban siku 45 kwa ajili ya kusimamia sare za wafanyakazi, jambo ambalo alidai ni ufujaji wa fedha za umma kwa kugharamia sare moja dola 49,900.

Kuhusu ajira ndani ya ATCL, Dk. Mwakyembe alisema kuna waajiriwa wengi waliokwishastaafu na pia ajira mpya zilitolewa bila kufuata tararibu ikiwemo kutangaza nafasi zilizopo ili wenye sifa washindane.

Alisema kuwa badala yake watu wamekuwa wakipeana ajira hizo kwa kufahamina na kuacha wale walio na sifa, jambo alilodai kuwa walikuwa wameamua kufukuza menejimenti yote, lakini wakahisi wangekosa kumbukumbu za urushwaji ndege.

“Baada ya kupitia baadhi ya mafaili ya watendaji hao tulikuta mwenye afadhali ni Kaimu Mkurugenzi huyu niliyemteua, Kapteni Lusajo Lazaro,” alisema.
Aliwaonya wanaozusha kuwa ametumia ukabila kumteua mkurugenzi huyo, akidai kuwa amebebwa na sifa pamoja na uwezo wake kiutendaji.

Waziri huyo alisema kuwa wameunda tume ambayo anaamini itakuja na majibu mazuri yatakayoliwezesha shirika hilo kusonga mbele.
Aliwataka wafanyakazi waliobaki, kuchapa kazi ili kumrahisishia pale anapoomba fedha serikalini aeleweke na kuongeza kwamba tayari wameshakabidhiwa sh bilioni 4.9 kutoka hazina kwa ajili ya matengenezo ya ndege.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Shirika hilo aliahidi kuyafanyia kazi yale yote waziri huyo aliyowaagiza, na kutimiza malengo ndani ya miezi mitatu waliyopewa.

Kwa niaba ya wanafanyakazi hao, Nelson Kalinga, alisema kusuasua kwa ATCL kumechangiwa na serikali kutowasikiliza wafanyakazi, kwani tangu awali walipinga kununuliwa kwa ndege hiyo ya Air Bus, ambapo waliandamana na kuandika barua wizarani lakini hawakusikilizwa.

Thursday, June 7, 2012

MBATIA ATAKIWA KUPIMA UENYEKITI WAKE


Na Asha Bani

CHAMA cha Sauti ya Umma (SAU), kimemshukia Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia, kikidai kuwa anatumiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Mwenyekiti wa SAU, Paul Kyara, alitoa kauli hiyo jana katika taarifa yake aliyoituma kwenye vyombo vya habari, akisema kuwa Mbatia anapaswa kuutafakari upya uenyekiti wake baada ya kukubali uteuzi wa Rais Jakaya Kikwete kuwa mbunge.

Kauli ya Kyara inakuja siku mbili baada ya Katibu Mwenezi wa NCCR Mageuzi, Moses Machali, kumtaka Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje (CHADEMA), kuomba radhi kutokana na matamshi yake kuwa uteuzi wa Mbatia ni dhahili anatumiwa na CCM.

Kyara alisema kauli ya Machali kama alitumwa na mwenyekiti wake, basi inalenga kuua upinzani na inaongeza ushahidi wa NCCR kutumiwa na CCM na pia kuharibu mahusiano mazuri yaliyowekwa baina ya chama hicho na CHADEMA hadi kufikia muafaka wa Mbatia kufuta kesi ya uchaguzi katika Jimbo la Kawe dhidi ya Halima Mdee.

“Kama Mbatia alifuta kesi hiyo bila hila ni bora akawa na hofu ya Mungu ili kuepuka vitisho na malumbano, ni vema akatazama upya athari za kukubali uteuzi wa Mwenyekiti wa CCM huku yeye akibakia kama Mwenyekiti wa NCCR,” alisema.
Kwa mujibu wa Kyara, hilo linaondoa uhuru wa kutoa mawazo ya kuipinga CCM na hata uwezekano wa wananchi kumwamini kama mpinzani wa kweli.

“Mimi ninamshauri Mbatia afikirie kuachia ngazi kwenye nafasi ya uenyekiti wa taifa kama ilivyokuwa kwa Juma Duni Haji alivyoondoka katika nafasi ya Naibu Katibu Mkuu CUF mara baada ya kuteuliwa kuingia kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa,” alisema Kyara.

Alisema endapo Mbatia atafumbia macho jambo hilo, yatamkuta kama yaliyomkuta Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad, ambaye ameendelea na nafasi yake ya ukatibu mkuu wa CUF na kushindwa kuikosoa serikali na kukipotezea mwelekeo chama chake.
“Mbatia na chama chake wanatakiwa kumpongeza Wenje kwa kueleza ukweli maana kuendelea kupingana naye ni kupambana na nguvu ya umma,” alisisitiza.