About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Saturday, October 15, 2011

WADAU WA HABARI WAKIWA KWENYE MATUKIO TOFAUTI TOFAUTI WAKATI WA MKUTANO WAO

Wadau wa Habari Mkoani Ruvuma wakiwa kwenye picha ya pamoja
Mmiliki wa Mtandao huu wa www.stephanomango.blogspot.com, wa kwanza mstari wa mbele akiwa kwenye picha ya pamoja ya Wadau wa habari mkoani Ruvuma na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu wa tatu(mwenye suti nyeusi)mara baada ya kuufungua mkutano wa wadau wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa CWT

Mwandishi wa Habari wa TBC mkoani Ruvuma Gerson Msigwa akitoa mada wakati wa mkutano wa wadau wa habari mkoani Ruvuma
Wadau waliohudhuria mkutano huo wakiendelea kusikiliza kwa umakini mkutano huo


MKUTANO WA WADAU WAFUNGULIWA RASMI NA MKUU WA MKOA WA RUVUMA SAID MWAMBUNGU

     
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akifungua mkutano wa wadau wa habari mkoani Ruvuma,Kulia ni Mwenyekiti wa Ruvuma Press Club,Kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt Daniel Malekela
Mjumbe wa Kamati ya Maadili ya Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Ruvuma Judith Mwenda akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi baada ya kufungua mkutano huo wa wadau

WAANDISHI WA HABARI WAENDELEA NA MKUTANO NA WADAU WA HABARI MKOANI RUVUMA

 Mwenyekiti wa Ruvuma Press Club Endrew Kuchonjoma akimkaribisha mgeni rasmi ili aweze kufungua mkutano wa wadau na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Chama cha Walimu Tanzania Tawi la Ruvuma,wa kwanza toka kulia ni Augustine Mbunda Mwasisi wa Chama cha Waandishi Mkoa wa Ruvuma,Dkt Daniel Malekela Mganga Mkuu wa Mkoa,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu,Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Charles Mhagama
 Katibu  Mkuu wa Ruvuma Press Club Andrew Chatwanga na Mweka Hazina wa Ruvuma Press Club Joyce Joliga
 Waandishi wa Habari wakiendelea kufuatilia majadiliano katika mkutano huo
 Wadau wa Habari wakiendelea kusikiliza majadiliano yaliyokuwa yanaendelea kwenye mkutano huo
Cresencia Kapinga Mwandishi wa Gazeti la Majira akiendelea kufanya kazi yake kwa Ueledi mkubwa

WAANDISHI WATAKIWA KUTUNZA AMANI NA MSHIKAMANO MIONGONI MWA WANANCHI

Na Steven Augustino,Songea.

WAANDISHI wa habari nchini wameaaswa kufanya kazi zao kwa kufuata misingi ya taaluma ya habari ili kulinda amani ya taifa letu.

Hayo yalisemwa na mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambugu wakati alipokuwa akifungua mkutano maalumu wa Wadau wa habari  mkoani Ruvuma uliofanyika kwenye ukumbi wa chama cha walimu mjini Songea.

Mwambungu alisema waandishi wa habari ni kioo cha jamii hivyo hawana budi kufanya kazi zao kwa moyo wenye uzalendo na sio kuandika habari zenye kuchochea maovu.

“Ndugu zangu waadishi tusimame katika maadili, mtihani uliopo ni namna ya kuzingatia maadili yanayoambatana na taaluma yenu hivyo fanyeni kazi kwa uaminifu”,alisema Mwambungu

Alisema kwa ujumla vyombo vyote vya habari vinaongozwa na kanuni zilizowekwa, lengo lake la kwanza ni kuhakikisha umma unapata habari zilizo sahihi hivyo msipotoshe umma mkasababisha mahafa makubwa

Kadhalika alieleza kuwa ni vyema waandishi wajitambue kuwa wao ni nani katika jamii hivyo ni vyema wajiwekee utaratibu mzuri wa kufanya kazi katika taaluma yao ili wasiweze kuingiliwa na watu wengine.

Alifafanua kuwa kuna watu wamekuwa wakiingilia taaluma hiyo ni vyema wachukuliwe hatua zinazostahili pale wanapobainika kuvamia tasnia hiyo kwa nia mbaya ya kuchafua sifa ya wanahabari.

Vilevile alisema kuwa habari zinazoandikwa  zizingatie utamaduni wa kujenga taifa iliziweze kulinda amani, kukosoa maovu katika jamii na kuepusha kuchochea chuki na uhasama miongoni mwa watanzania na akaongeza kuwa endapo hatutazingatia haya gharama yake baadaye ni kubwa.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoani Ruvuma Bw. Andrew Kuchonjoma aliwataka waandishi wa habari kuacha malumbano yasiyo ya lazima miongoni mwao.
MWISHO.  

WAANDISHI WA HABARI KUJADILIANA NA WADAU WA HABARI MKOANI RUVUMA LEO

                            Katibu wa Ruvuma Press Club Andrew Chatwanga
Baadhi ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma wakiwa na Waziri wa Habari,Utamaduni na Michezo Dkt Emmanuel Nchimbi
Na Stephano Mango,Songea
CHAMA cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma kinatarajia kuanza mkutano wa Wadau wa Habari mkoani Ruvuma ulioandaliwa na chama hicho unaotarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Chama Cha Walimu Tanzania tawi la Ruvuma(CWT)
Akizungumza kabla ya mkutano huo wa Wadau kuanza Katibu wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma Andrew Chatwanga alisema kuwa mkutano huo ambao utafunguliwa na Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu una lengo la kujadili mafanikio na changamoto zinazoikabili sekta ya Habari mkoa wa Ruvuma
Chatwanga alisema kuwa washiriki watapata fursa ya kuelezwa historia fupi ya Chama cha Waandishi wa habari mkoa wa Ruvuma,Utaratibu wa Wadau  kuwapata Waandishi wa Habari,Kuelewa majukumu ya Chama cha Waandishi wa Habari kwa maendeleo ya mkoa wa Ruvuma,Kusuluhisha migogoro baina ya Waandishi wa Habari na Wadau
Alifafanua kuwa mkutano huo ni muhimu sana kwani utawezesha kurahisisha upatikanaji wa habari na ujenzi wa uandishi wenye ueledi kwa maendeleo ya wananchi wote kwa ujumla

CHAMA KUTOA HUDUMA ZA USHAURI NASAHA KWA WANACHAMA WAKE KUTOKANA NA VIKOMBE KUDUNDA WILAYANI TUNDURU

Na, Augustino Chindiye Tunduru

CHAMA cha Wanaoishi na Virusi vinavyo sababisha Ukimwi na Ukimwi cha Tunduru Affected Society TAAs+ Tawi la Tunduru mkoani Ruvuma limeanza kutoa huduma ya Ushauri nasaha kwa Wateja wake zikiwa ni juhudi za taasisi yao kuwanusuru wanachama wake wasikate tamaa na kuwafanya wapoteze maisha haraka baada ya kugundulika kuwa na ugonjwa huo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Chama hicho Issa Kadabadi na kuongea kuwa maamuzi hayo yamechukuliwa kufuatia kuwepo kwa wimbi kubwa la Waganga wa Tiba asili wanaotoa tiba mbadala ya VIKOMBE kwa Watu wanaoishi na VVU na UKIMWI hali ilipelekea baadhi ya wanachama wake kupoteza maisha.

Alisema hadi sasa Chama chake kimepoteza wanachama watano baada ya kuibuika kwa watoa vikombe hao ambao wengi wao wamekuwa wakiwadanganya kwa kuwazuia kuendelea kunywa dawa zao ambazo hutolewa Hospitali za ARVs hali iliyo usukuma uongozi wa Taasisi hiyo kuanzisha darasa hilo katika kitengo cha darasa la kutolea elimu ya ushauri nasaha kilichopo katika Hospitali ya serikali ya Wilaya ya Tunduru.

Akifafanua taarifa hiyo Kadabadi alisema kuwa masomo ambayo hutolewa kwa ushauri wenye ushuhuda wa wanachama 12 ambao walipelekwa katika Kikombe kinachotolewa kwa Bibi Hadija Alli Omari wa Kijiji cha Misechela Wilayani humo baada ya kugundulika kwa tiba hiyo mbadala maarufu kwa jina la KIKOMBE ambao mbali na Bibi huyo kuwaeleza wakapime baada ya wiki mbili watakutwa hawana maambukizi ya ugonjwa huo hatari lakini baada ya kupimwa walikutwa wakiwa hawajapona “ yaani kikombe kimedunda”    
       
Wakati hayo yakiendelea taarifa kutoka ofisi ya Chama kinachosimamia usajiri wa Waganga na Wataalamu wa Tiba asili (CHAWATIATA) na kudhibitishwa na Katibu wa Chama hicho wa Wilaya ya Tunduru Sofia Mpinga zinaonesha kuwa jumla ya Waganga 37 wamesajiriwa na Chama hicho kwa ajili ya kutoa Tiba mbadala ya kikombe Wilayani humo hali inayo onesha kuwa huduma zinazotolewa na maafisa tabibu katika Hospitali, Zahanati na Vituo vya afya wilayani humo wameonekana kuzidiwa nguvu na waganga hao.

Akizungumzia hali hiyo pamoja na kukiri kuwepo kwa changamoto kubwa ya mfumuko watoaji wa tiba mbadala za Vikombe  Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Dkt. Alex Kazula  alisema kuwa Wilaya yake inakabiliwa na tatizo kubwa la maambukizi mapya ya VVU na Ukimwi.

Dkt. Kazula aliendelea kufafanua kuwa Takwimu zinaonesha kuwa Wilaya yake inakabiliwa na maambukizi ya Ugonjwa huo kwa asilimia 4.1% kwa wakazi wote wanakadiliwa kuwa ni zaidi ya Wananchi 200,000 wanaoishi Wilayani humo.

Alisema pamoja na takwimu hizo, taarifa za wagonjwa wapya zinaonesha kuwa watu 226 wakiwemo wanawake 121 na wanaume 105 waligundulika mwaka 2010 ikiwa ni sawa na asilimia 3.7% ya  watu 6079 walijitokeza kupima Virusi vya ukimwi kwa hiari na kati yao wanaume walikuwa 2408 na wanawake 3671.

WAKILI AITAKA MAHAKAMA IWAPIME AKILI WASHTAKIWA WA KESI ZA MAUAJI

Na Augustino Chindiye, Tunduru
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma imewaamuru watuhumiwa Wawili wa makosa ya mauaji ya kukusudia kwenda kufanyiwa uchunguzi wa akili katika Hospitali maalumu ya Mirembe inayotibu wagonjwa wa akili nchini.

Amri hiyo imetolewa na Jaji wa Mahakama kuu kanda ya Songea Mkoani Ruvuma Hamisa Kalombola katika vikao vya kusikiliza kesi za mauaji zinazoendelea katika Mahakama kuu Wilayani Tunduru baada ya kuridhishwa na hoja zilizotolewa na upande wa Utetezi unao ongozwa na Wakili wa Kujitegemea Sebastia Waryuba.

Walio amriwa kupelekwa Mirembe kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa akili zao ndipo kesi zao zije kuendelea katika vikao vijavyo ni  Susani Kapinga anaye kabiliwa na kesi ya mauaji namba 10/2011 ya kumuua Mtoto wake wa Miaka 10 marehemu Jafeti Njovu katika tukio lilitokea kijiji cha Kumbara Wilayani Namtumbo April 27 2010.

Mtuhumiwa mwingine aliyeamriwa kwande kupimwa akili kupitia kifungu namba 220 (1) cha mwenendo wa Mashtaka kinacho iruhusu mahakama hiyo kutoa amri ya watuhumiwa wanaodhaniwa kuwa ni Wagonjwa wa akili ni Salum Furahisha Masame anayekabiriwa na kesi ya mauji ya kukusudia Namba 4/2011 ya kuwaua Baba yake mzazi Marehemu Furahisha Masame na  Mama yake wa kambo marehemu Asumini Mohamed katika tukio lilitokea May 22/2010 katika kijiji cha Muhuwesi Wilayani Tunduru.

Awali wakisomewa mashitaka hayo mbele ya Jaji Kalombola watuhumiwa hao kwa nyakati tofauti walikubali kufanya makosa hayo hali ambayo ilisababisha upande wa Utetezi unao ongozwa na Wakili Waryuba kujenga hoja ya wateja wake kupelekwa kupimwa akili akidai kuwa kitendo cha kukubali kwao kiurahisi wakati wakiwa wanafahamu kuwa adhabu ya makosa waliyo kubali ni kifungo cha maisha au kunyongwa hadi wafe kinamtia mashaka kuwa huenda wateja hao walifanya makosa hayo bila kujifahamu au ni wagonjwa wa akili.

Wakati wakili Wariyuba akijenga hoja ya wateja wake kwenda kufanyiwa uchunguzi wa akili katika Hospitali ya Mirembe iliyopo katika Manispaa ya Dodoma, upande wa Jamhuri wenye jukumu zito la kuthibitisha bila kutia mashaka juu ya tuhuma zinazo wakabili watuhumiwa hao unao ongozwa na Mwanasheria Msomi wa Serikali Hamimu Nkoleye ulionekana kukubali amri hiyo kwa shingo upande hasa kwa kesi inayomkabili mtuhumiwa Masame.

Katika ujenzi wa hoja za kisheria pamoja na mambo mengine, Nkoleye alikataa kuridhia kitendo cha Wakili wa Utetezi kutumia kifungu hicho dhidi ya mtuhumiwa Masame kwenda kufanyiwa uchunguzi huo kwa kudai kuwa wakili Waryuba anapingana na kifungu Namba 220 (1)  kwani kauli za mteja ambaye pamoja na kukubali mbele ya Jaji pia hapo awali alikubali kutekeleza mauaji hayo kituo cha Polisi na mbele ya mlinzi wa amani.

Alisema katika Maelezo hayo mtuhumiwa huyo anayetetewa na Waryuba alidai kuwa alichukua uamuzi huo wa kuwaua kwa kuwapondaponda na mwichi wa kutwangia baada ya kumshuhudia Marehemu baba yake huyo akiponda raha na kimada wakati mama yake mzazi anapata shida kiasi cha kukosa fedha za kujikimu na chakula.

“ Ingawa kifungu namba 220 (1) kinairuhusu Mahakama kutoa amri ya mtuhumiwa kwenda kupimwa akili, upande wa mashtaka uliiomba mahakama isitoe amri hiyo kwa Mtuhumiwa mauaji Namba 4/2011  Salum Masame kwani kitendo hicho kitachelewesha kesi hiyo bila sababu za msingi” alisema Nkoleye .

Akitoa amri hiyo Jaji Kalombola alisema kuwa pamoja na Mahakama kuzingatia hoja zote zilizotolewa na upande wa Utetezi na Jamhuri alidai kuwa ingawa kifungu namba 220 (1) kilichotumika na upande wa Utetezi kinatoa uhuru kwa mahakama kuridhia kutoa amri hiyo au kutotoa lakini kutokana na uhuru huo, mahakama imeona ni busara kutoa amri hiyo ili haki iweze kutendeka.

Jaji Kalombola anaendele kusikiliza kesi Nne (4) zinazoendelea katika Mahakama kuu Wilayani Tunduru ambapo kati yake kesi mbili ni za mauaji ya kukusudia zinatokea Wilayani Namtumbo na kesi Mbili ni matukio yaliyo tokea Wilayani Tunduru. 

DKT MPONDA AWAHIMIZA WANANCHI KUZINGATIA USAFI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA NCHINI

Thomas Lipuka Songea
WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hadji Mponda  katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani mwaka huu Mkoani Ruvuma,ikiwa pia siku ya uzinduzi wa sherehe za miaka 50 ya uhuru kauli mbiu ya siku hiyo ya Mazingira ilikuwa tusimamie na kudumisha muungano ,tuhifadhi Mazingira.
Ambapo kauli mbiu halisi ya miaka 50 ya Uhuru ni kwamba Tumedhubutu,Tumeweza na Tunasonga mbele.
Katika siku hiyo Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii aliwakumbusha watu wa Mkoa wa Ruvuma na nchi nzima kuwa Wizara ya Afya imechukua juhudi kadhaa katika kufikia lengo la kuwa na hali bora ya Afya na usafi wa Mazingira nchini.
Dk.Mponda alizitaja baadhi ya hatua hizo ni pamoja na uandaaji wa sera ya usafi na Afya kwa Mazingira,ambayo alisema ipo katika hatua za mwisho za ukamilikaji.
 Hatua nyingine ni uandaaji wa sheria ya Afya ya Jamii ya mwaka 2009 na Sheria ya usajili wa Afya kwa Mazingira ya mwaka 2007 ambazo zinakazia usafi na Afya ya Mazingira nchini kote.
Alisema mpango mkakati wa Afya na usafi wa Mazingira wa mwaka 2008-2017 utatiliwa mkazo mikoa yote ikiwa ni pamoja na kuratibu zoezi la mashindano ya Afya na usafi wa Mazingira yanayoshirikisha Halmashauri zote nchini.
 Dk Mponda aliongeza kusema kwamba Halmashauri zimefanikiwa kujenga uwezo kote nchini kupitia mbinu shirikishi zinazohimiza na kuhamasisha mabadiliko ya tabia ili kuinua usafi nchini.
 Amesema ushirikishwaji wa jamii ni mbinu kuu katika kuhimiza usafi wa mbinu ya Afya ya Mazingira pia urejeshwaji wa mafunzo ya wasaidizi wa Afya ya mazingira ni muhimu ili kujenga uwezo wa Vijiji na Kata katika kusimamia usafi wa Afya na Mazingira ngazi ya Kijiji na Kata.
 Dk.Mponda amesisitiza kuwa mashindano ya usafi na Afya ya Mazingira katika Halmashauri hapa nchini yameongeza chachu ya ushirikishi wa sekta binafsi katika kutoa huduma za usafi pia kuongezeka kwa ukusanyaji taka ngumu na jamii kushiriki kwa kiasi kikubwa katika shughuli za utunzaji wa usafi wa Afya ya Mazingira na kuchangia huduma hiyo hatimaye kupunguza magonjwa ya mlipuko.
Halmashauri nchini zimepata changamoto katika bajeti zake ambazo kuna ongezeko la fedha ili kwenda sambamba na utoaji wa huduma ya kutunza usafi na Afya ya Mazingira katika maadhimisho hayo.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mheshimiwa Dkt Haji Mponda alizipongeza Halmashauri kwa ongezeko la bajeti ya usafi wa Mazingira katika mipango yao,uimarishaji wa huduma za uzoaji wa taka ngumu na maji taka.
Dkt Mponda alizisifu baadhi ya Halmashaurti ambazo zinaimarisha na ukarabati machinjio ili kuleta afya na usafi wa mazingira katika utoaji wa huduma hizo za machinjio hatimaye kuepuka magonjwa yasiyo na mpango.
Akizungumzia masuala ya Masoko ili kuleta usafi wa Mazingira na Afya kwa walaji Dkt Mponda alisisitiza ujenzi wa Masoko mapya,vyakula viwe katika hali ya usafi na haiba kwa mlaji,pia kuwepo kwa vyoo katika Masoko hayo ambavyo ni bora na safi wakati wote.
Dkt Mponda alisisitiza Halmashauri zote kujali na kuongeza ujenzi wa mifereji ya maji ya mvua ili kuepuka mkusanyiko wa taka wakati wa mvua,kwani miundombinu dhaifu haiwezi kudhibiti taka ngumu na maji taka.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii alisema zipo changamoto za mipango dhaifu na bajeti ndogo ya usafi wa Mazingira uhaba wa vitendea kazi,wataalamu wa Afya kasi ndogo ya mabadiliko ya jamii katika kulinda usafi na Afya kasi ndogo ya mabadiliko ya jamii katika kulinda usafi  na Afya ya mazingira pamoja na tabia ya jamii katika kulinda,kuboresha mazingira mambo ambayo yanafanyiwa kazi na Serikali pia jamii ipate elimu na kubadilisha tabia ya kupenda usafi na kuchukia uchafu.

MADIWANI WATANO WAFUTIWA ADHABU YA KUFUKUZWA UANACHAMA SONGEA NA WATAKIWA KUCHAPA KAZI KAMA KAWAIDA

 Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma Emmanuel Mteming'ombe wa kwanza kushoto akitoa tamko la kuifuta adhabu ya kuwafukuza Madiwani watano wa Chama hicho Wilaya ya Songea Mjini,Henhit Ndimbo Katibu wa Mipango na Uchumi wa Chama hicho Mkoa(katikati) wa Kwanza kulia na Katibu wa Uwt Mkoa wa Ruvuma
Na Stephano Mango,Songea
KAMATI ya siasa ya Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi mkoa wa Ruvuma imeifuta adhabu iliyopendekezwa na kutolewa na Kamati ya siasa ya chama hicho Wilaya ya Songea Mjini ya kuwafukuza uanachama Madiwani wake wa tano kwa kile alichojiita ukosefu wa maadili walioufanya wakati wa uchaguzi wa kumpata Meya wa Manispaa ya Songea uliofanyika hivi karibuni
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi za chama hicho mkoa wa Ruvuma Katibu wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Ruvuma Emmanuel Mteming’ombe alisema kuwa kamati ya siasa ya mkoa baada ya kuyapitia maelezo yaliyotolewa na kamati ya siasa ya Wilaya ya kuwafukuza Madiwani hao na baada ya kupitia kwa umakini maelezo ya utetezi ya Madiwani waliofukuzwa uanachama na kamati ya siasa ya Wilaya kamati ya siasa ya mkoa imelitengua pendekezo la adhabu hiyo kutokana na kutokuwa na hatia
Mteming’ombe alisema kuwa Kamati ya siasa ya mkoa imewaruhusu madiwani wale watano kuendelea na uanachama na udiwani wao kama ilivyokuwa awali na kwamba chama hicho kimesikitishwa sana na vurugu zilizojitokeza katika mkutano wa Baraza la Madiwani wa kumchagua Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Septemba 23 mwaka huu
“Chama kinakemea na kulaani tabia hiyo ya kufanya vurugu katika vikao kwani tabia ya kufanya vurugu vikaoni ni kinyume kabisa na kanuni za vikao na kwamba sio tabia za viongozi wanaotokana na Ccm hivyo chama kimeamua kuandaa semina kwa Madiwani wote wanaotokana na Ccm ili kuwaelekeza na kuwaelimisha kwa lengo la kuwapatia weledi juu ya namna bora ya kusimamia na kufuatilia utekelezaji na utendaji mzuri wa kazi zao”alisema Mteming’ombe
Hivi karibuni Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Songea kilipendekeza kuwafukuza uanachama Madiwani wake watano kutokana na kuungana na Madiwani wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)kwa kumpigia mgombea pekee Diwani wa Kata ya Matogoro kura 14 za hapana na za ndiyo 12 katika uchaguzi wa Umeya wa Manispaa ya Songea
Hali hiyo ilisababisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea ambaye ndiye Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Songea Mjini Nachoa Zakaria kushindwa kuyatangaza matokeo hayo na kumpa Naibu Meya Mariam Dizumba ambaye naye alikuwa ni miongoni mwa wapiga kura kuyatangaza matokeo hayo kinyume kwa kusema kuwa Mhagama amepata kura 14 za ndiyo na za hapana 12 na kusababisha vurugu kubwa na mkutano kuvunjika kutokana na ukiukwaji huo wa kanuni wa makusudi
Kutokana na hali hiyo Ccm Wilaya ya Songea mjini ikapendekeza Madiwani watano akiwemo Faustine Mhagama wa Kata ya Mshangano,Kurabest Mgwasa wa Msamala,Christian Matembo wa Seed Farm,Victa Ngongi wa Ruvuma na Genifrida Haule wa Viti Maalum wafukuzwe uanachama kutokana na kukizalilisha chama kwa kumpigia kura za hapana Charles Mhagama
MWISHO