About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Sunday, October 23, 2011

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA LEVINA ADAKWA,AKUTWA NA VITU VYA MAREHEMU

Na Gideon Mwakanosya, Songea
 
JESHI la Polisi mkoani Ruvuma limemtia mbaroni Thomas Jilala (22) mkazi wa Mwanza kwa tuhuma za kumuua anayedaiwa kuwa mpenzi wake Levina Kihwili (26) mkazi wa Mfaranyaki katika Manispaa ya Songea ambaye alikutwa akiwa amekufa kwa kunyongwa shingo katika nyumba ya kulala wageni ya Mikumi mjini hapa
 
Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Polisi, Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma, Inspekta Paulo Mashimbi alisema tukio hilo lilitokea Octoba 22 mwaka huu majira ya saa 2 asubuhi huko kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni chumba namba Kumi.
 
Insekta Mashimbi alisema kuwa ililetwa taarifa katika kituo kikuu cha polisi mjini Songea kuwa katika nyumba ya kulala wageni ya Mikumi chumba namba Kumi kilichokuwa kikitumika na watu wawili alikutwa mwanamke akiwa amefariki dunia huku mwanaume aliyekuwa naye akiwa amekimbia.
 
Alisema mnamo octoba 23 mwaka huu majira ya saa Sita usiku mtuhumiwa anayedaiwa kufanya mauaji hayo Jilala ambaya anadaiwa alikuwa Mpenzi wa marehemu alikamatwa akiwa anatoroka kuelekea barabara ya Songea-Tunduru maeneo ya Namtumbo.
 
Alieleza kuwa mtuhumiwa Jilala baada ya kukamatwa alikutwa na baadhi ya vitu vya marehemu ikiwemo Saa aliyokuwa ameivaa kabla ya kuuawa pamoja na simu Mbili za mkononi vyote vikiwa ni mali ya marehemu.
 
Alifafanua kuwa mtuhumiwa pia alikutwa na vifaa vingine vilivyoibiwa kwenye ofisi aliyokuwa akifanyia kazi marehemu usiku wa kuamkia siku ya tukio hilo la mauaji.
 
Hata hivyo vyanzo vya habari vimeeleza kuwa Jilala kabla hajafanya kitendo hicho cha kinyama alikuwa akionekana mara kwa mara katika Ofisi ya marehemu ijulikanayo kwa jina la Mpenda Production kwa madai kuwa amekuja kutengeneza kadi za harusi ya kaka yake.
 
Aidha Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limesema linaendelea na uchunguzi dhidi ya tukio hilo na kwamba baada ya uchunguzi huo kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu shitaka la mauaji linalomkabili.
 
Mganga mkuu mfawidhi wa hospitali ya mkoa mjini Songea, Dkt. Benedict Ngaiza alipohojiwa na waandishi wa habari ofisini kwake amethibitisha kuuawa kwa Levina na kwamba uchunguzi unaonesha kwamba alivunjika shingo baada kupigwa na kitu kizito.
 
Wakati huo huo Jeshi la Polisi linawatafuta watu wasiofahamika kwa tuhuma za kumuua mtu mmoja wa Kiume ambaye jina lake halijapatikana kwa kumchoma moto na mwili wake kuharibika vibaya.
 
Insekta Mashimba alisema tukio hilo lilitokea octoba 23 mwaka huu majira ya saa 12 asubuhi katika eneo la shule ya Msingi ya Bombambili mjini Songea ambako inahisiwa kuwa marehemu huyo alikuwa ni kibaka.
Mwisho.  

KIJANA ASIYEFAHAMIKA JINA LAKE AKUTWA AMEKUFA BAADA YA KUCHOMWA MOTO NA WATU WASIOFAHAMIKA KATIKA UWANJA WA BOMBAMBILI USIKU WA KUAMKIA LEO

 Mwili wa Marehemu ukiwa kwenye gari la Polisi nje ya Chumba cha kuhifadhia Maiti katika Hospital ya Mkoa Songea



 Mwili wa Marehemu ukishushwa kwenye gari la Polisi ukiingizwa kwenye chumba cha kuhifadhi Maiti katika Hospital ya Mkoa wa Songea
 Mwili wa Marehemu ukiingizwa kwenye chumba cha kuhifadhia Maiti kwa ajili ya kukamilisha taratibu kabla ya mazishi
Watu waliojitokeza kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospital ya Mkoa Songea wakiwa na nyuso za huzuni baada ya kuuona mwili wa marehemu
Mtandao huu wa www.stephanomango.blogspot.com una laani vikali vitendo vya kujichukulia sheria mikononi kwa kuondoa haki muhimu ya binadamu ya kuishi kwani tunapaswa kutambua kuwa mwenye mamlaka ya kuondoa uhai wa binadamu ni Mwenyezi Mungu pekee,Binadamu tusinyang'anye mamlaka ya Mwenyezi Mungu

Matukio hayo yameanza kushamiri mkoani Ruvuma ambapo sababu zinazotajwa hazifanani na adhabu zinazotolewa kwa mkosaji kwani anapouawa hawezi kujilekebisha kwani tunaamini kuwa lengo la kuwepo kwa adhabu ni kumrekebisha mkosaji

HOSPITAL YA WILAYA TUNDURU YAKABILIWA NA CHANGAMOTO LUKUKI NA KUSABABISHA KERO KWA WAGONJWA NA WAUGUZI


Na Augustino Chindiye,Tunduru
WAGANGA na wauguzi wa Wilaya ya Tunduru wameonywa kuacha tabia za ubabaishaji wakati wa utekelezaji wa majukumu na shughuli zao za kila siku na kwamba Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo hata husika katika utetezi wa mtumishi yeyote pindi sheria itakapotakiwa kufuata mkondo wake.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt. Alex kazula wakati akijibu swali juu ya kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya utendaji mbovu dhidi ya wataalamu wa idara hiyo huku kukiwa na taarifa za mgomo baridi kutoka kwa Madaktari,Maafisa Tabibu na Wauguzi wa Wilaya hiyo huku ofisi yake ikidai kuto kuwa na taarifa zozote juu ya kinacholalamikiwa na wataalamu hao.

Katika taarifa hiyo Dkt. Kazula alikiri kuwa hivi sasa Hospitali yake imegubikwa na wimbi kubwa la malalamiko mbalimbali kutoka kwa wagonjwa na watu wanaokwenda kuuguza wagonjwa katika Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati kuwa wataalamu wake hawawajibiki ipasavyo wanapokea fedha kutoka kwa wagonjwa na wamekuwa na majibu mabaya na wakati mwingine wamekuwa wakiwatukana wateja wao.

Dkt. Kazula aliendelea kueleza kuwa malalamiko mengine aliyoyapokea  ni pamoja na kushamiri kwa matukio ya  VIFO visivyo vya lazima ambavyo hutokea  kwa wagonjwa wanaoenda kutibiwa na kulazwa katika Hospitalini hali ambayo imekuwa ikizusha manung`uniko kutoka kwa wananchi kuwa Wataalamu hao wamekuwa hawajitumi katika kutekeleza wajibu wao wa kutoa tiba sahihi na kuokoa maisha ya wateja wao.

Alisema sambamba na malalamiko hayo pia ofisi yake inazo taarifa za malalamiko ya Waganga na Wauguzi hao kutoa huduma kwa upendeleo ambapo wagonjwa wasio na uwezo kifedha hawapatiwi huduma kabisa na kwamba ukiona Daktari au Muuguzi anahangaikia mgonjwa kwa nguvu zote ujue amepokea chochote (RUSHWA) kutoka kwa mgonjwa huyo.  

Kufuatia hali hiyo Dkt. Kazula amesema milango ipo wazi kwa wagonjwa na wauguzaji kwenda kutoa malalamiko na ushahidi dhidi ya watumishi hao ili atayebainika sheria ifuate mkondo wake ikiwa ni pamoja na mhusika kufukuzwa kazi.

Wakati hayo yakiendelea  baadhi ya wagonjwa na wauguzaji wa wagonjwa wanaolazwa katika hospitali ya Wilaya hiyo nao waliibua  malalamiko ya kuwepo kwa hali mbaya na harufu kali katika vyoo vilivyopo Hospitalini hapo.

Walisema kufuati hali hiyo wamekuwa wakilazimika kutoka nje hasa nyakati za usiku ili kupata hifadhi katika mapori yaliyopo eneo la uwanja wa Ndege uliofungwa baada ya kupoteza siza za kutua ndege.
Mwisho

WATUMIKIA KIFUNGO CHA MIAKA MITATU JELA KWA KOSA LA MAUAJI NA MWINGINE AACHIWA HURU

Na Augustino Chindiye, Tunduru

MAHAKAMA kuu Kanda ya Songea imewahukumu kifungo cha miaka mitatu kila mmoja mtu na dada yake baada ya kukiri na kupatikana na hatia ya kufanya kosa dogo la kuua bila kukusudia na kumuachilia huru mtoto wa miaka 14.

Akitoa hukumu hiyo Jaji wa Kanda ya Songea Jaji Hamisa kalombola alisema kuwa adhabu hizo zimetolewa baada ya kuzingatia hoja zilizotolewa na upande wa Jamhuri uliokuwa ukiongozwa na Mwanasheria wa Serikali Hamimu Nkoleye aliyeiomba Mahakama hiyo iwahukumu kifungo cha maisha huku upande wa utetezi ulioongozwa na Wakili wa kujitegemea Sebastian Waryuba akiiomba Mahakama hiyo iwapatie adhabu ndogo wateja wake akidai kuwa kukubali kwao kumeipunguzia usumbufu Mahakama hiyo.

Kaka na dada waliohukumiwa kutumikia kifungo hicho cha miaka mitatu Jela ni Hashim Msusa Ibrahim na Mwanahawa Msusa Ibrahim waliokuwa wanakabiliwa na Shauli la mauaji namba 8/2011 la kumuua marehemu Halifa abdalah February 2/2010 wakiwa wanagombea mfuko tupu wa kubebea mahindi wa kiroba cha mbolea ambapo tukio hilo lililotokea katika kijiji cha Lijombo Wilayani Tunduru.

Shauli jingine lililotolewa maamuzi na kufikia maamuzi ya kumuachilia huru yaani (Anconditional Discharge) baada ya Mahakama hiyo kumtia hatiani kwa kosa dogo la kuua bila kukusudia ni Shauli Namba 2/2011 lililo kuwa likimkabili Mwamini Mwandope (14) aliye muua marehemu Salome Sanga baada ya kutokea ugomvi kati yao katika tukio lilitokea katika Kijiji cha Hanga Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma.

Jaji Hamisa kalombola aliendelea kueleza kuwa mahakama yake   imeamua kutoa adhabu hizo kwa kuzingatia kifungu cha Sheria Namba 119 kifungu kidogo (2a) na kifungu kidogo cha (4) vya sheria ya kanuni ya adhabu vinavyoipatia mamlaka Mahakama hiyo.
  
Awali kabla ya kutolewa kwa adhabu hizo watuhumiwa hao walitiwa hatiani na mahakama hiyo baada ya kukiri kufanya kosa dogo la kuua bila kukusudia  baadaya kusomewa kosa la kumuua bila kukusudia ambapo Mtoto aliye achiliwa huru alidaiwa kumuua marehemu Salome Sanga kwa kumchoma kisu baada ya kutokea ugomvi kati yao huku wanandugu Hashimu na Mwanahawa wakidaiwa kumuua kwa kumpiga na mangongo kichwani marehemu Halifa Abdala katika ugomvi wa kugombea mfuko tupu.

Jaji Kalombola alisema kuwa pamoja na mambo mengine Mahakama yake imeridhishwa na hoja zilizotolewa na Wakili wa Upande wa utetezi Sebastian Waryuba kwamba pamoja na mambo mengine kikiwemo kigezo cha kukubali kosa hilo mbele ya Jaji na kuiondolea Mahakama usumbufu mteja wake anastahili kupatiwa adhabu yenye unafuu chini ya kifungu cha 119 cha Sheria ya watoto namba 21ya mwaka 2009.

Awali katika ujenzi wa hoja za Utetezi kwa mteja huyo wakili msomi wa kujitegemea Sebastian  Waryuba alidai kuwa chini ya makosa hayo wateja wake wanapaswa kunufaika chini ya kifungu cha 119 cha sheria za kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyia mapitio mwaka 2002 ambapo wakati mtuhumiwa akitenda kosa hilo Agosti 28/2010 na huku akimwelezea Mtoto Mwamini Mwandope kuwa wakifanya kosa hilo alikuwa na umri wa miaka 13, na sasa  ana Mtoto mchanga mwenye umri wa miezi 6 ambaye alijifungua wakati akiwa mahabusu.

Alisema kipitia kifungu hicho mteja wake anastahili kupewa adhabu ya kifungo cha nje ama kutumikia adhabu ya kutumikia jamii huku Mwanasheria wa Serikali Hamimu Nkoleye akiiomba mahakama hiyo impatie adhabu ya kifungo cha maisha.
Mwisho