About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Saturday, September 3, 2011

HAYA NDIYO MTANDAO HUU ULIVYOSHUHUDIA PILIKAPIKA ZA MAHAFALI YA AINA YAKE YA SHULE YA MSINGI MKOMBOZI ILIYOPO KATA YA BOMBAMBILI,MANISPAA YA SONGEA ILIYOFANYIKA JANA KATIKA VIWANJA VYA SHULE HIYO NA BAADAE KWENYE UKUMBI WA CHAMA CHA WALIMU MKOA WA RUVUMA

 Mzee Samwel Mapunda akimpongeza Mgeni Rasmi Juma Nyumayo mara baada ya kumaliza kuwahutubia katika sherehe za mahafali katika shule ya Msingi Mkombozi na kuwapatia msaada wa mifuko kumi ya Saruji(Cement) na wazazi kuahidi kubebelea mchanga kwa ajili ya kusakafia darasa la Awali shuleni hapo
 Kushoto Padre Chinguku akiwaonyesha,Gideon Mwakanosya,Mwandishi Mkongwe wa Magazeti ya Nipashe na guardian na Mjumbe wa Bodi ya Swacco(katikati)kulia ni mzee Samwel Mapunda namna watoto walivyopendeza katika mahafali hiyo
 Kulia ni Gideon Mwakanosya akisalimiana na Mjapani ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja kutokana na pilikapilika za kufanikisha mahafali hiyo,pembeni ni wanafunzi wakiwa na hamu ya kuendelea kusherehekea mahafali hayo
 Viongozi mbalimbali wakiwa na Mgeni Rasmi Nyumayo katika darasa linalodaiwa kuwa ni la Awali ambalo halijasakafiwa na mgeni Rasmi kutoa mifuko kumi ya Saruji na wazazi kuahidi kutoa mchanga wa kusakafia darasa hilo kwa lengo la kutaka watoto wao wakombolewe na elimu itolewayo Shuleni hapo
 Watoto wakitafakari kwa umakini hatima ya elimu yao mara baada ya kupewa Saruji na mchanga utakaotumika kuondoa vumbi katika darasa lao
 Watoto wakitamani kucheza kiduku kutokana na furaha kubwa waliyonayo baada ya kusikia kuwa darasa lao litakuwa katika hali stahiki kwa kuendelea kupatiwa elimu kusudiwa
 Viongozi wa Serikali ya Kata ya Bombambili wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mgeni rasmi nje ya darasa la Awali ambalo linatarajiwa kukarabatiwa hivi punde
 Wa kwanza kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mkombozi Imelda Mbawala akiwa kwenye picha ya pamoja na Mgeni Rasmi na familia ya Kazimguru
 Sherehe ikifunguliwa kwa mbwembwe zote kwenye ukumbi wa Chama cha Walimu Mkoa wa Ruvuma,ikiongozwa na Mgeni Rasmi Nyumayo,kushoto ni Diwani wa kata ya Bombambili Kenny Moto akisaidiwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Mjimwema Twalik Mpakasini wa kwanza kushoto
 Mwalimu Mstaafu Agnes Nkoma aliyeanza kazi mwaka 1972 na kustaafu utumishi wa UMMA,mei mwaka huu 2011 akipokea zawadi ya utumishi uliotukuka kutoka kwa Mgeni Rasmi Nyumayo katika Mahafali ya Shule ya Mkombozi ambapo amestaafu akiwa Mwalimu Mkuu katika Shule hiyo
 Mwalimu Bibi(Notbuluga Mapunda)akimshukuru kwa utumishi wake Mwalimu Agnes Nkoma na kumtakia maisha mema ya kustaafu utumishi wa UMMA
 Sherehe yoyote duniani haiwezi kufanikiwa bila kuwepo mziki au burudani,sasa kazi ipo Dj MKongwe ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Bombambili akionyesha umahiri wake wa kusugua Cd na kuchezesha pini za uhakika kwa wazee na vijana(Masharobaro)
 Wahitimu wa darasa la Saba katika Shule ya Msingi Mkombozi wakimng'ang'ania Mgeni Rasmi Nyumayo kucheza muziki wa kisasa bila kufahamu kuwa mwenzao alikuwa kijana wa zamani na sasa akitaka kutikisa kichwa na kisigino chini lazima achezewe nyimbo za zamani kama vile Ottu Jazz Band,Sikinde na zingine za aina hiyo bila kusahau TWISTI
 Hapo sasa Mgeni Rasmi akiwa na Wazee wenzake akisakata rumba katika mahafali ya aina yake huku akitamani kuvua koti la suti ili aweze kumudu vizuri rumba hilo
Ukosikia kipindi maalumu ndio hicho cha kuongeza vocha ya tumbo ili uweze kupata nguvu za kufanya jambo na uwezo kamilifu wa kufikiri,kwa kweli sherehe hiyo ilikuwa ni ya aina yake kufanyika mjini hapa,tuwashukuru wote waliowezesha mtandao huu wa http://www.stephanomango.blogspot.com/ kufika shuleni hapo na ukumbi ili kuweza kuwaletea wasomaji na wadau wa mtandao huo taarifa na burudani
 Mzee Samwel Mapunda na Mkewe Mwalimu Notbuluga Mapunda(Mwalimu Bibi) hawakubaki nyuma katika Mahafali hayo kwa kumsindikiza mjukuu wao Dickson Mapunda kushikana mkono na Mgeni Rasmi Nyumayo na kupokea uthibitisho wa kuhitimu elimu ya Msingi darasa la Saba mwaka huu 2011
 Hapa sasa ni kucheza Kiduku kwenda mbele kwa wahitimu wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Mkombozi ikiwa ni furaha ya kuhitimu na kukabidhiwa cheti na Mgeni Rasmi Nyumayo kwa kudumu katika darasa la kwanza hadi la saba mwaka huu
 Usiposhuhudia Mahafali haya unaweza kujilaumu kwa kukosa raha na maneno ya busara na hekima kutoka kwa Mgeni rasmi Nyumayo na hapa ni watoto ambao urefu wake ni wa mashaka wakiwa wanatafuta uwezo wa kuona kinachoendelea
 Wageni waalikwa,walimu na wanafunzi wakiwa wanafuatilia mahafali hayo kwa umakini mkubwa
 Mgeni Rasmi Juma Nyumayo ambaye ni Mwanaharakati wa masuala ya haki za binadamu akimpa msaada wa fedha ya kununulia Uniformu Mwanafunzi wa darasa la tano Agnes Magagura baada ya kusikia kuwa anashindwa kuendelea na Shule kwa kukosa Uniformu na kuguswa kutoa msaada huo
Mwalimu Mkuu Mstaafu wa Shule ya Mkombozi Agnes Nkoma akishangiliwa na Wanafunzi wake alipokuwa anawaaga na kwenda kuanza maisha mapya ya URAIANI kwa kuwa amestaafu utumishi wa Umma


Padre Chinguku ambaye ni Mlezi wa Kituo cha Kulea Watoto Waishio katika Mazingira Magumu SWACCO akiendesha maombi kabla ya Mgeni Rasmi ajaanza kuhutubia Wazazi,Wageni Waalikwa,Wanafunzi na Walimu wa Shule ya Msingi Mkombozi wakati wa Mahafali ya Darasa la Saba katika Shule hiyo



Mgeni Rasmi katika Mahafali ya kwanza ya darasa la saba toka Shule hiyo ianzishwe ,Mhariri Msaidi wa Magazeti ya Elimu na Tujifunze kanda ya Kusini Juma Nyumayo,ambaye alimwakilisha Mhariri Mkuu wa Magazeti hayo Christiani Sikapundwa akiwasalimu wanafunzi na wageni waalikwa kabla hajaanza kuwahutubia,Kushoto ni Diwani wa Kata ya Bombambili kupitia Chadema,Kenny Moto Mpangara,kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo,Immelda Mbawala 

                                
Mgeni Rasmi Juma Nyumayo akimkabidhi cheti cha kuhitimu Elimu ya Msingi Mwanafunzi Amina Kazimguru katika mahafali yaliyofanyika jana katika viwanja vya Shule hiyo mjini hapa






RAIA 11 WA PAKSTANI NA BANGRADESHI WAKAMATWA RUVUMA

                                                         Na Stephano Mango,Songea

JESHI la Polisi Mkoani Ruvuma linawashikilia watu 11 ambao ni raia wa nchi za Bangradeshi na Pakstani ambao wanadaiwa kuwa wamefukuzwa toka Msumbiji kwa kupigwa mijeredi na kunyang’anywa fedha pamoja na mali walizokuwa nazo na askari wa nchi hiyo.

Akizungumza na mtandao wa http://www.stephanomango.blogspot.com/ Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda amesema kuwa raia hao wa Pakstani na Bangladeshi wamekamatwa jana majira ya saa za asubuhi huko katika kijiji cha Magwamila kilichopo mpakani mwa Msumbiji na Tanzania.

Kamuhanda amewataja waliokamatwa ambao ni raia wa Bangladeshi kuwa ni Shahed Alzam (29), Amar Ahmed  (25),Gavan Halifa (40),Mhamed Parvas (23),shojal Meya (28) na Sohal Meya (28), Raia toka Pakstani waliokamatwa amewataja kuwa ni Hassan Bilar (20),Fawad Yasin (20),Mohamed Awadh (20),Aftal Hussein (24) na Hasad Ashar (45).

Amefafanua kuwa watu hao baada ya kukamatwa na kuhojiwa na polisi kwa kushirikiana na Idara ya uhamiaji Mkoani humo wamedai kuwa katikati ya mwezi uliopita waliondoka Pakstan wote kwa pamoja na walisafiri kwa ndege hadi Jijini Dar es Salaam ambako walitafuta usafiri wa basi hadi Mtwara mjini.

Ameeleza zaidi kuwa raia hao wa Nchi za Pakstani na Bangladeshi wakiwa Mtwara mjini walifanikiwa kupata usafiri kwa kutumia magari hadi Msumbiji lakini lengo lao kubwa ni kuelekea Afrika Kusini kutafuta maisha ambako wamedai kuwa waliambiwa na wenzao ambao wako Afrika kusini kuwa huko maisha ni mazuri.

Amebainisha zaidi kuwa watu hao wakiwa Msumbiji huku wakiwa wanatafuta namna ya kufika Afrika kusini walikamatwa na askari wa Msumbiji kisha walipelekwa mpakani mwa nchi hiyo na Tanzania huku wakiwa wanapigwa mijeredi na baadae wakawatelekeza kwenye Kijiji cha Magwamila ambako walikutwa wakiwa hawana kitu chochote.

Amesema kuwa raia hao wa Bangladeshi na Pakstani kwasasa wameondolewa Magwamila wapo katika Kituo kikuu cha Polisi cha Songea wakati wanafanya utaratibu wa kuwasiliana na idara ya uhamiaji ili iangalie ni namna gani wahamiaji hao haramu watawachukulia hatua .

MWISHO