About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Wednesday, January 18, 2012

WANACHAMA WA SACCOS YA WATUMISHI WA MANISPAA YA SONGEA KUNUFAIKA NA MKOPO WA FEDHA ZA UJENZI WA NYUMBA

Na Augustino Chindiye, Songea

ZAIDI ya Wanachama 300 wa Cha akiba na Mikopo(SACCOS) cha Watumishi wa Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wanatarajia kunufaika mpango maalumu wa kukopeshwa fedha za kuwawezesha kujenga nyumba zikiwa ni juhudi za chama hicho kuwakwamua na umasikini wanachama wake.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa chama hicho Sky Mpange wakati
akiongea katika mkutano wa 19 wa mwaka wa chama hicho uliofanyika katika ukumbi wa Songea Club mjini hapa.

Akifafanua taarifa hiyo Mpange alisema kuwa kupitia mpango maalumu wa kutoa mikopo ya ujenzi wa nyumba kwa wanachama wake kwa riba nafuu zaidi utawawezesha watumishi hao kumiliki nyumba zao wenyewe baadala ya sasa ambapo wengi wa wanachama hao wamekuwa wakiishi katika nyumba za kupanga hali ambayo huwafanya na kutozwa fedha nyingi na kuwafanya washindwe kufanya hivyo kutokana na gharama kubwa za vifaa vya ujenzi
wa nyumba hizo.

Alisema kufutia hali hiyo chama hicho kimelazimika kuanza kutoa mikopo ya Shilingi Milioni Nane kwa kila mwanachama ili kufanikisha ujenzi huo kwa wanachama wake kutokana na wengi wao kushindwa kumudu gharama za ujenzi huo hivyo kushindwa kuendeleza maisha yao kiuchumi kwa kulipa fedha nyingi kwenye nyumba za kupanga.

Mpange aliendelea kueleza kuwa ili kufanikisha Mkakati huo Chama
hicho kuwawezesha wanachama wake huku kukiwa na maelekezo kuwa kila mwezi mwanachama wao atatakiwa kukatwa asilimia 10 ya mkopo wa nyumba wa shilingi Milioni Nane kwa kwa mwezi.

Aidha,Mpange alibainisha kuwa pamoja na juhudi hizo kuoneshwa na
uongozi wa Chama hicho lakini mwitikio wa wanachama kukopa mkopo huo umekuwa mdogo na kuongeza kuwa tangu Mpango wa mkopo huo uanze kutolewa miaka miwili iliyopita ni wanachama Wanne tu waliojitokeza kukopa.

Awali akifungua mkutano huo Meneja wa SONAMCU Songea Bw.Salum Mbuyu aliwahimiza wanachama hao kukopa mkopo wa nyumba ili kujiletea maendeleo yakiwemo ya kupangisha nyumba zao ili kujiongezea kipato tofauti na mikopo midogo ambayo mwisho wake fedha hizo huishia katika matumizi ya starehe.

Aidha, Chama hicho kimefanikiwa kutoa mikopo mingine zaidi ya shilingi milioni 300 kwa wanachama wake 330 katika kipindi cha mwaka jana na kwamba mwaka huu Saccos hiyo inatarajia kutoa mkopo wa shilingi milioni 400 kwa wanachama hao.
MWISHO