About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Monday, July 30, 2012

NAMI NILIVYOSHIRIKI MECHI YA YANGA NA AZAM

Mmiliki wa mtandao wa www.stephanomango.blogspot.com , Stephano Mango akiwa kwenye uwanja wa Taifa kabla ya mechi kati ya Yanga na Azam
Mgombea Uwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Ruvuma (FARU) Golden Sanga akiwa na Dickson kwenye uwanja wa Taifa wakishuhudia mechi kati ya Yanga na Azam
Mgombea Uwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Ruvuma (FARU) Golden Sanga akiwa na Dickson kwenye uwanja wa Taifa kushuhudia mechi kati ya Yanga na Azam
Mgombea Uwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Ruvuma (FARU) Golden Sanga akiwa na Dickson kwenye uwanja wa Taifa kushuhudia mechi kati ya Yanga na Azam
 Mgombea Uwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Ruvuma (FARU) Golden Sanga akifurahia ushindi wa Yanga kutwaa kombe la Kagame nje ya uwanja wa Taifa

 
Wachezaji wa Yanga wakishangilia huku wakiwa na Kombe la Kagame, baada ya kutawazwa tena kuwa wafalme wa michuano ya soka ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kwa kuibwaga Azam FC mabao 2-0.
Kocha Mkuu wa Yanga, Tom akiungana na wachezaji kushangilia ubingwa huo

Mashabiki wakiungana na wachezaji wa Yanga kushangilia ubingwa huo
Mmiliki wa Blogu ya Michuzi, Muhidini Michuzi akiendelea kuchukua matukio
Ubao ulivyokuwa unaonekana baada fainali hiyo kumaliziki


Mshambuliaji wa yanga Said Bahanunzi akimtoka beki wa Azam FC Agrey Morris wakati wa mchezo wao wa Fainali ya Kagame Cup uliomalizika hivi punde kwenye uwanja wataifa jijini Dar es Salaam ambapo Yanga wameibuka na Ushindi wa mabao 2-0, huku Bahanuzi akipachika bao kwenye dakika za nyongeza za mwamuzi.
Mshambuliaji wa Yanga Hamis Kiiza Akimtoka Beki wa Azam Fc Jabir Azizi kabla ya kupachika bao la kwanza kwenye mchezo huo.
Mashabiki wa Yanga wakijimwayamwaya kwenye uwanja wa Taifa leo baada ya Said Bahanuzi kupachika bao la pili.
Wachezaji nao waliburudika kimtindo baada ya kupata ushindi.

Friday, July 27, 2012

SANGA ONE ALONGA KUHUSU KUGOMBEA NAFASI YA UWENYEKITI WA CCM WILAYA YA SONGEA

             Diwani Mstaafu wa Kata ya Bombambili Golden Sanga( Sanga One)

Na Stephano Mango, Songea
KADA wa Chama cha Mapinduzi(Ccm) Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Golden Sanga (Sanga One) ametangaza nia ya kugombea Uwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Songea katika uchaguzi ambao unatarajiwa kufanyika mapema mwezi Septemba mwaka huu
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa ya Majimaji Songea Golden Sanga alisema kuwa ameamua kugombea nafasi hiyo ili kuweza kurudisha heshima ya Chama cha Mapinduzi mjini hapa
Sanga alisema kuwa kila kukicha mvuto wa Ccm miongoni mwa jamii umekuwa ukipungua kutokana na matendo maovu yasiyokuwa ya kimaadili yanayofanywa na Viongozi wa chama hicho ambayo yamekuwa yakiwakatisha tamaa wananchi na wanachama wa chama hicho
Alieleza kuwa kutokana na hali hiyo kumesababisha kata 6 kati ya 21 kuchukuliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na Urais wa mwaka 2010
Alieleza zaidi kuwa amejipanga kikamilifu kwa kushirikiana na viongozi wenzake watakaochaguliwa kushika nafasi mbalimbali ndani ya chama katika uchaguzi unaoendelea kufanyika mwaka huu ili kuweza kukijenga chama na kuleta ushindi stahiki katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa 2015
Kwa mujibu wa taarifa ya Chama cha Mapinduzi Halmashauri ya Manispaa ya Songea kuwa wagombea wana haki ya kutangaza nia za kugombea nafasi wanazozitaka ndani ya chama ambapo kwa nafasi ya uwenyekiti wa Wilaya fomu zinatolewa agosti 1 na kurudishwa ndani ya siku mbili ambapo uchaguzi unatarajiwa kufanyika mapema septemba
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa waliotangaza nia hadi sasa ni Gerald Mhenga ambaye ni Katibu wa mipango na uchumi wa Ccm Wilaya ya Songea na Golden Sanga ambaye amewahi kushika nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho ikiwemo udiwani wa kata ya Bombambili katika halmashauri hiyo
MWISHO

Thursday, July 26, 2012

URAIS WAMTESA ZITTO KABWE

<>
<>
<>



<>
<>
<>
Asema ana uwezo,uadilifu kuwa Amiri Jeshi Mkuu
Na Edson Kamukara
HARAKATI za kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka 2015 umeanza kuwatesa viongozi wa vyama vya siasa ambapo safari hii, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA (Bara), Zitto Kabwe, amesema kama akiandikiwa kuwa rais hakuna wa kumzuia.
Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini alijitapa kuwa kama urais upo, utakuja tu, kwani ana uwezo, uadilifu na uzalendo wa kuwa Amiri Jeshi Mkuu.
Zitto ameibuka na kuzungumzia sakata la urais ikiwa ni siku moja tu imepita baada ya wabunge wenzake kulalamika na kukanusha taarifa za kumpigia debe kwa ajili ya urais mwaka 2015.
Wabunge hao, Halima Mdee (Kawe) na Joshua Nassari (Arumeru Mashariki), waliandika barua za kulalamikia habari iliyochapishwa na gazeti moja la kila siku (si Tanzania Daima), wakidai liliwalisha maneno kuwa walimpigia debe Zitto wakiwa mkoani Kigoma kwamba anapaswa kuwa rais mwaka 2015.
Akichangia mjadala wa hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya Wizara ya Mawasilaino, Sayansi na Teknolojia jana mjini hapa, Zitto alitumia muda mfupi kufafanua sakata hilo lililozagaa kwenye vyombo kadhaa vya habari na kwenye mitandao ya kijamii.
“Tamasha letu la wasanii la Kigoma limeleta maneno maneno…lakini napenda kusema kuwa urais kama upo utakuja tu. Sina mashaka hata kidogo kwamba uwezo, uadilifu na uzalendo wa kuwa Amiri Jeshi Mkuu ninao,” alisema Zitto na kushangiliwa na wabunge wenzake.
Mjadala huo ulichukua sura mpya kwenye mitandao ya kijamii juzi ambapo baadhi ya watu walionekana kumlaumu Zitto, wakimhusisha na habari hiyo kuwa aliitengeneza mwenyewe kama sehemu ya kujiandalia mazingira hayo.
Zitto ambaye amekuwa akiandamwa mara kadhaa na wanasiasa ndani na nje ya chama chake, baadhi wakimtuhumu kuwa mamluki na wengine wakimwelezea kuwa ni mwanasiasa mwenye malengo makubwa hapo baadaye, alifafanua zaidi suala hilo kwenye taarifa yake kwa kusema:
“Katika gazeti la Mwananchi la tarehe 23 Julai 2012, kulikuwa na habari yenye kusomeka: ‘Wabunge wamsafishia Zitto njia ya urais 2015?. Habari hii imeleta mjadala mara baada ya kutoka na kusomwa. Mjadala umekuzwa zaidi baada ya wabunge, Halima Mdee na Joshua Nassari kukanusha maneno waliyonukuliwa kusema. Napenda kusema masuala yafuatayo:
“Moja, waheshimiwa wabunge Halima Mdee, Joshua Nassari, Kangi Lugola, Esther Bulaya, Deo Filikunjombe, Raya Ibrahim, Amina Mwidau na David Kafulila walihudhuria tamasha la vijana wa Kigoma All Stars kwa kualikwa na Mratibu wa kundi hilo, Mwasiti Almasi.
“Wabunge wengine walialikwa lakini hawakutokea wakiwamo Joseph Mbilinyi, David Silinde, Amos Makala, Vicky Kamata na Peter Serukamba. Wabunge hawa hawakualikwa na mimi na wala sikufanya mazungumzo nao yoyote ya awali au kuwaambia au kukubaliana nini cha kuzungumza au hapana. Tamasha lilikuwa la muziki na halikuhusika kabisa na siasa.
“Waheshimiwa wote walipewa nafasi ya kusalimia na wote walizungumza. Wabunge waliozungumza kwa muda mrefu kidogo ni ndugu Halima Mdee, Joshua Nassari, Deo Filikunjombe na Kangi Lugola.
“Hotuba za wabunge wote zilirekodiwa kwenye video neno kwa neno na video hizo zitawekwa wazi kwenye blogu yangu kama sehemu ya documentary ya tamasha lile la kihistoria.
“Pili, sikuhusika kwa namna yoyote ile na kuandikwa kwa habari hii iliyozusha mjadala. Wala sikujua kama habari hii ingeandikwa, maana katika ziara ile sikuita mwandishi hata mmoja, maana nilitaka liwe tukio la Kigoma tu.
“Kama mwandishi kaandika mambo ambayo wabunge hawa hawakuyasema basi itaonekana kwenye video hizo. Wabunge wenyewe wanajua kwenye nafsi zao nini walichosema Kigoma na kipi kiliwasukuma kusema waliyoyasema. Nisingependa kuhusishwa kwa njia yoyote ile na matamshi yao, habari iliyowanukuu na hata makanusho yao. Maana mwisho wa siku ukweli ndio utasimama.
“Suala la urais lisitupotezee muda kwani kuna mambo mengi sana ya kujadili kuhusu nchi yetu. Taharuki ambazo watu wanazipata masuala ya urais yanapotajwa zinashangaza sana.
“Chama changu bado hakijatangaza rasmi mchakato wa kupata mgombea urais. Hivi sasa chama hakina mgombea urais mpaka hapo mchakato utakapotangazwa, ambapo wanachama wataruhusiwa kuomba kupeperusha bendera ya chama. Mwanachama wa chama chetu atakaye kubalika na jamii na wajumbe wa mkutano wa uteuzi ndiye atakuwa mgombea wetu. Kwa sasa hayupo na hivyo tusipoteze muda kujadili jambo hili.
“Mzee Thabiti Kombo alituachia usia tunapokuwa tunazungumza. Alisema ‘weka akiba’ si akiba ya fedha, bali ya akiba ya maneno. Tuweke akiba ya maneno. Tusimalize yote.”
Hata hivyo akizungumza na gazeti hili mjini hapa jana mara baada ya Bunge kuahirishwa kwa ajili ya mapumziko ya mchana, Zitto alikanusha tuhuma hizo zinazomhusisha kuandaa habari hiyo akisema ni matusi kwa tasnia ya habari, hivyo kuvitaka vyombo vya habari kutowaendekeza wanasiasa wanaotukana waandishi na vyombo vyao.
“Ni upuuzi kudhani kwamba mimi naweza kuandaa habari kwenye gazeti hilo…nimeshangaa na wewe unaweza kuniuliza jambo hili…unaliamini?” alihoji Zitto.
Kuhusu habari hiyo inayolalamikiwa na wabunge wenzake kuwa ilipotoshwa, alisema kwamba haoni ubaya kwenye habari husika akidai hata hivyo mengi yaliachwa kuliko kuongezwa chumvi. “Hakuna aliyenukuliwa kwa ambalo hakusema. Tamasha zima limerekodiwa kwenye video”.
Kwa muda sasa kumekuwepo na mjadala juu za Zitto kuhusu kauli yake kwamba anautaka urais, jambo liliotafsiriwa kuwa ni mikakati ya kutaka kukivuruga chama chake kwa kikigawa kimakundi lakini Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, amekuwa akisema kila wakati kuwa ajenda yao kwa wakati huu si kujadili nani anafaa kugombea urais 2015 badala yake wanajikita kutatua kero za wananchi.

Chanzo Tanzania Daima

Tuesday, July 24, 2012

MWANAFUNZI AFA MAJI KATIKA LAMBO LA KUNYWESHEA NG’OMBE

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki
Na Steven Augustino, Tunduru
MWANAFUNZI wa Darasa la nne katika Shule ya Msingi Majimaji Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma aliyefahamika kwa jina la Rehema Salum (12) amefariki dunia baada ya kutumbukia katika lambo la kunyweshea ng’ombe.

Mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa marehemu alikubwa na mkasa huo wakati akijaribu kuogelea katika lambo hilo lililochimbwa na Idara ya magereza kwa ajili ya kunywesha Ng,ombe wa Gereza la Mifungo la Kilimo la Majimaji lililopo kijijini hapo.

Wakifafanua taarifa hiyo mashuhuda hao walidai kuwa katika tukio hilo marehemu alikuwa ameongozana na kundi la watoto wenzake kwa nia ya kwenda kuoga katika lambo hilo kama ambavyo hufanya siku zote na kwamba kilichotokea ni bahati mbaya iliyotokana na yeye kuogelea eneo
lenye kina kirefu.

Mganga aliyeufanyia uchunguzi mwili wa marehemu Rehema, Dkt. Mosses Mwahasunga alidai kuwa chanzo cha kifo hicho ni kukosa hewa kulikosababishwa na kunywa maji mengi.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki mbali na kukiri kuwepo kwake alidai kuwa polisi wanaendelea na uchuinguzi tukio hilo.
Mwisho

Monday, July 23, 2012

MAVETERANI WA SIMBA WACHAPWA BAO MOJA NA MAVETERANI WA YANGA

 Maveterani wa Yanga wakiwa katika uwanja wa mazoezi ili kuweza kujiweka sawa katika mechi na Maveterani wa Simba

Mechi ambayo ilimalizika kwa kuichapa Simba bao 1 katika dakika ya 13 ya kipindi cha pili na mchezaji Kelvin Haule



 Wachezaji wa Maveterani wa SIMBA wakifanya mazoezi ili kuweza kuleta upinzani wa dhati katika mechi yake na YANGA




                     Mdhamini wa Mechi hiyo Golden Sanga (Sanga Transport) ambaye ni VETERANI WA YANGA
 Mdhamini wa Mechi hiyo Paskary Msigwa (Top One Inn) ambaye ni VETERANI WA SIMBA
 Mohamend Mchele (kushoto) akiwa na watazamaji wengine katika mechi hiyo
 wa kwanza toka kushoto ni Godfey Mvula, Peter Mhina na Amasha wakiwa na watazamaji wengine
 Washabiki wa Simba wakionyesha manjonjo yao katika uwanja wa Sokoine ambao mechi hiyo ilikuwa inachezwa jana
 Wachezaji wa Yanga Gerson Msigwa na Kabisama wakishusha pumzi wakati wa mapumziko
Methew Msigwa akiwa na wachezaji wenzake wakitafakari namna ya kuwafunga wapinzani wao wakati wa mapumziko ya kipindi cha kwanza

MKUTANO WA CCM MJINI KIGOMA

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala wa Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI,) Aggrey Mwanri akihutubia, kwenye mkutano wa CCM uliofanyika, jana , Julai 22, 2012, kwenye Uwanja wa Community Centre, Mwanga mjini Kigoma.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akihutubia, kwenye mkutano wa CCM uliofanyika, jana , Julai 22, 2012, kwenye Uwanja wa Community Centre, Mwanga mjini Kigoma.

Waziri wa Nchi Ofsi ya Rais, Mahusiano, Steven Wasira akihutubia kwenye mkutano wa CCM uliofanyika, jana , Julai 22, 2012, kwenye Uwanja wa Community Centre, Mwanga mjini Kigoma.
Mamia ya wananchi waliofurika kwenye mkutano wa CCM katika Uwanja wa Community Centre, Mwanga mkoani Kigoma

Wazee kwenye mkutano wa CCM, Uwanjwa wa Community Cetre Mwanga Kigoma

Viongozi mbalimbali wa CCM waliohudhuria katika mkutano huo

AUAWA KWA TUHUMA ZA KUIBA KANISANI


Na Augustino Chindiye, Tunduru

WANANCHI wenye hasira wamempiga na kumuua kazi wa mtaa wa Kadewele mjini Tunduru mkoani Ruvuma aliyefahamika kwa jina la Nasoro Hashim (18) baada ya kutuhumiwa kuingia na kuiba katika nyumba ya Paroko wa Kanisa kuu lililopo katika Jimbo la Tunduru/ Masasi.

Mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa katika mkasa huo marehemu Hashim alikutwa na kidhibiti cha simu tatu za mkononi mali za viongozi wa Kanisa hilo.

Walisema katika tukio hilo marehemu alishtukiwa baada ya kuonekana wakati akitoka katika nyumba hiyo na Sista mmoja ambaye hawakutaja jina lake ambapo baada ya kugundua hali hiyo alipiga kelele za kuomba msaada na kulifanya kundi hilo kujitokeza.

Walisema baada ya kipigo hicho marehemu alikimbizwa katika hospitali ya serikali ya Wilaya kwa matibabu ambapo alifariki baada ya muda mfupi.

Mganga aliye ufanyia uchunguzi mwili wa marehemu Hashim Dkt. Jeshi Daraja alisema kuwa chanzo cha kifo hicho ni kutokwa na damu nyingi kuliko sababishwa na kupasuka kwa fuvu la kichwa kulikotokana na kupigwa na kitu kizito.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki, mbali na kukiri kuwepo kwa tukio hilo alisema kuwa Polisi wanaendelea na uchunguzi ili sheria iweze kufuata mkondo wake kwa waliohusika na tukio hilko.

Aidha kamanda Nsimeki alitumia nafasi hiyo kuwataka wananchi wa Mkoa huo kuachana na tabia za kuchukua sheria mikononi.
Mwisho

Sunday, July 22, 2012

WANANCHI WAPATA MASHAKA NA MKANDARASI WA UJENZI WA LAMI NAMTUMBO HADI TUNDURU

Na Steven Augustino, Tunduru SERIKALI imeombwa kuichukulia hatua kampuni ya progressive Constraction  iliyopewa kazi ya kujenga kwa kiwango cha Lami Barabara ya Tunduru hadi Namtumbo Mkoani Ruvuma zikiwa ni juhudi za Serikali kuiunganisha mikoa ya Kusini kwenye mtandao wa barabara za kiwango cha Lami.

Hayo yamesemwa na baadhi ya wananchi waliotakiwa kutoa maoni yao juu ya maendeleo ya Ujenzi wa Barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 180 wenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni. 180.66 ambazo ilipewa kampuni hiyo kwa makubaliano ya kuikamirisha katika kipindi cha miezi 27 inayoishia mwezi july 2013.

Wakifafanua maelezo yao walidai kuwa Mradi huo ambao hadi sasa umetimiza miezi 16 iliyopita kampuni hiyo bado haijakamirisha hata ujenzi wa kambi zao hali inayo onesha wazi kutokuwepo kwa matumaini ya mradi huo kukamirisha ujenzi wake hata ikipewa miaka 10 zaidi wakiwa na maana kuwa kampuni hiyo haina uwezo kwani hata vyombo haina.

Goerge Mrope, Fatu Alli, Mohamed Said na Adam Mkwanda ni miongoni mwa wananchi waliotoa maoni hayo na kudai kuwa endapo serikali haitachukua hatua za kuuokoa mradi huo na kuufanya ukamilike kwa wakati kuna hatari ya Chama tawala CCM kufanya vibaya katika matokeo ya uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015 ambapo wapigakura hawatakuwa tayari kusikiliza la mtu na badala yake itakuwa ni kukisulubu tu.

Nao Madiwani Athuman Nkinde, Msenga Said na Mchungaji Wiliam Mazuguni katika maoni yao walionesha mashaka ya kuanguka kwa chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi huo kutatokana na wananchi wengi kuwa na uelewa hasa wakati huu ambao vyama vya siasa vya Chadema na CUF vinaendelea kujijenga na kuanza kuimung`unyua na kuwateka wanachi wa mikoa ya kusini ambako kumekuwa ni ngome kubwa ya CCM toka nchi hii ipate Uhuru.

Walisema ili kuokoa hali hiyo hatua madhubuti zinatakiwa kuchukuliwa na kufanyika kwa kazi ya ziada kwa dalili za kushindikana kukamilika kwa barabara hiyo katika kipindi kilicho pangwa zinaonekana kugonga ukuta kutokana na kampuni hiyo kuonekana kuifanya kazi hiyo kwa mwendo wa Kinyonga huku ikiwa imebakia miezi 11 ya kuikabidhi huku wakibainisha kuwa chanzo cha kuichelewa kukamirika kwa mradi huo ni uchakachuaji uliofanywa viongozi wa Wizara ya Ujenzi kutokana na kutoa kazi zote kwa mkandarasi mmoja badala ya kila kipande kupewa kampuni tofauti.

Kwa mujibu wa maelekezo ya Mikataba ya Barabara hiyo ilyogawanywa katika vipande vitatu, kipande cha Tunduru Matemanga Kilometa 58.70 Shilingi Bilioni. 63.41 kilipangwa kukabidhiwa mwezi July 2013, Matemanga Kilimasera kilometa 68.20 chenye thamani ya Shilingi Bilioni. 64.02 kilipanwa kukabidhiwa mwezi Mei 2013 na Kilimasera Namtumbo Kilometa 60.70 Chenye thamani ya Shilingi Bilioni.53.23 kilipangwa kukamilika mwezi march 2013.

Wakizungumzia hali hiyo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Bakari Nalicho na Meneja wa wakala wa Barabara TANROADs Mkoa wa Ruvuma Eng. Abraham Kisimbo waliungana na wananchi hao kwa madai ya kutoridhishwa wala kufurahishwa na maendeleo ya Mradi huo na kuongeza kuwa serikali inajitahidi kwa kutumia nguvu zao zote kubanana na kusukumana kukabiri vitendo vya Mkandarasi wa kampuni hiyo na kuhakikisha kuwa barabara hiyo inajengwa.

Aidha Mwambungu aliwapongeza wakandarasi wanaojenga Bara bara za Songea/ Namtumbo kilometa 67.00 utakao ghalimu Shilingi Bilioni.62.88 na Peramiho/Mbinga kilometa 78.00 wenye thamani ya shilingi Bilioni.79.81 kuwa inaendelea vizuri na akaongeza kwa kuonesha mashaka ya mdororo wa ujenzi wa Barabara ya Tunduru/ Namtumbo kuwa huenda mradi huo ukapitwa na miradi mipya ya Barabara za Tunduru Mtambaswala Kilometa 202.5, Shilingi Bilioni.240.858 na Mbinga /Mbambabey kilometa 66.00 utakao ghalimu shilingi Bilioni.2.90.

Wakati hayo yakiendelea taarifa zilizovuja kutoka kwa wakaguzi wa Barabara hiyo waliotembelea Wilayani Tunduru July 12 mwaka huu zinadai kuwa kampuni hiyo hadi sasa imefanya kazi kwa asilimia 1 tu toka ikabidhiwe kazi hizo katika kipindi hicho cha miezi 16 iliyopita

MWISHO

Friday, July 20, 2012

MAVETERANI WA SIMBA NA YANGA SONGEA DIMBANI JULAI 22

Mdhamini  mkuu wa mechi ya Simba na Yanga Gorden Sanga (Sanga One) akizungumza na waandishi wa habari

Na Stephano Mango, Songea
MAVETERANI wa Simba na Yanga wa Kata ya Bombambili Halmashauri ya Manispaa ya Songea wameanza mazoezi kwa ajiri ya mechi ya kirafiki ambayo wanatarajia kucheza Julai 22 mwaka huu yenye lengo la kuboresha mahusiano ya kijadi
Akizungumza na waandishi wa habari jana Mdhamini mkuu wa mechi hiyo Gorden Sanga (Sanga One) alisema kuwa mavetani wamekuwa wakikutana vijiweni na kufanya ushabiki wa timu hizo ambazo zina mashabiki wengi bila nao kushiriki kucheza katika maeneo yao
Sanga alisema kuwa tayari wachezaji wa timu zote mbili wamesha sajiriwa kutoka katika pande zote za Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa ajiri ya mechi hiyo yenye ushindani mkubwa na majigambo ya pande zote mbili
Alisema kuwa kamati ya maandalizi imejipanga kikamilifu kwa mechi hiyo ambapo zawadi za mfungaji bora, mchezaji bora na kipa bora zimeandaliwa na zitatolewa siku hiyo kwa lengo la kuthamini mechi hiyo na kanuni bora za michezo
Alieleza kuwa siku ya mechi ulinzi utakuwa wakutosha ili kuweza kudhibiti vitendo vya fujo na uhalifu wowote ule ambao unaweza kutokea kutokana na Maveterani hao kutambiana sana kutokana na hamu ya mechi hiyo itakayofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Sokoine mjini hapa
Alifafanua kuwa mechi hiyo inadhaminiwa na wapenzi wa michezo mjini Songea ambao ni Sanga One Transport, Top One Inn Hotel na Redio Jogoo na kwamba amewataka washabiki wa michezo kujitokeza kwa wingi katika mechi, pia amewaasa wachezaji kucheza kwa amani na upendo mkubwa na mashabiki kushangilia bila kuleta vurugu kwani michezo ni amani
MWISHO


Tuesday, July 17, 2012

MKURUGENZI MTENDAJI WA KAMPUNI YA CARGO STARS DIONIS MALINZI AWEZESHA UPATIKANAJI WA MILIONI 18

Na Stephano Mango, Songea
VIONGOZI wa dini na Wanakwaya nchini wametakiwa kumwomba Mungu kwa njia ya nyimbo na sala ili aweze kuwajalia viongozi wa Serikali nguvu za kumkataa shetani na mambo yake yote na awape busara na hekima katika kuliongoza Taifa kwa maendeleo ya wananchi
Wito huo umetolewa jana na Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo la Songea Dkt Norbert Mtega wakati akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Cargo Stars  Dionis Malinzi kwenye harambee ya uzinduzi wa Kanda ya Shetani Ameshindwa iliyoimbwa na kwaya ya Mt.Paulo Mtume Parokia ya Songea Mjini
Mtega alisema kuwa imeanza kujengeka tabia miongoni mwa viongozi wa Serikali kutoa maneno ambayo yanasababisha kuwepo kwa migawanyiko ya kiutendaji na kifikra miongoni mwa jamii kuhusu umoja na muungano wetu kama taifa

Alisema kuwa anapotokea mtu na kusema kuwa tusiliombee taifa, tusiimbe wimbo wa taifa au Tanzania igawanyike ni ishara ya nguvu za shetani kwasababu kazi yake kubwa ni kutia chuki miongoni mwa binadamu ili wachukiane na watengane na kuharibu tunu ya umoja wetu
Alifafanua kuwa umoja na muungano wetu kama taifa ni ishara ya maendeleo kwani kitendo cha kukaribisha migawanyiko husababisha amani kutoweka miongoni mwa jamii na ndio maana leo taifa linaanza kunuka damu kutokana na vitendo vya kikatili na mauaji yanayoendelea kutokea katika jamii zetu
“ Taifa limekumbwa na mambo ya kishetani sana kwani vitendo vya watu kuvamiwa, kutekwa, kuteswa, kujeruhiwa, kuuawa vinashamiri kwa kasi kubwa kutokana na wananchi kukosa imani na vyombo vya dola, jambo ambalo linaendelea kuathiri jamii zetu” alisema Mtega
Alisema Shetani akishindwa viongozi wetu watakuwa wakweli katika kuliongoza taifa na hapo ndipo amani, haki, uhuru wa kweli utapatikana na usawa wa binadamu na maendeleo yatasonga mbele
Kwa upande wake  mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Cargo Stars Dionis Malinzi akitoa salamu zake kwenye harambee hiyo alisema kuwa kwaya zote zinapaswa kutunga nyimbo nzuri za kumtukuza mungu na kumkataa shetani ili upatikane wokovu wa kweli
Malinzi alisema kuwa kanda inayozinduliwa katika harambee hii inaitwa Shetani Ameshindwa ni njia nzuri ya kuimarika katika utume na imani za jamii ya watanzania
Kwa upande wake Mwenyeketi wa Kamati ya uzinduzi wa kanda hiyo Jumanne Nyingo alisema kuwa michango iliyopatikana ambayo imeletwa na mgeni rasmi kutoka kwake binafsi, kwa marafiki zake na michango iliyopatikana kutokana na ushawishi wake itasaidia mambo mengi sana katika kwaya hiyo kwa kununua vifaa mbalimbali
Nyingo alisema kuwa Mgeni rasmi Dionis Malinzi alitoa mchango wa shilingi milioni 16, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma alitoa shilingi laki tatu, ahadi milioni 1.6 na michango mingine ambapo jumla yake ni shilingi milioni 18.7 kwa ajiri ya kwaya, pia mgeni rasmi alitoa shilingi milioni 30 kwa ajiri ya Kanisa katoliki la Songea mjini
MWISHO

Monday, July 16, 2012

SANGA ONE AGOMBEA UWENYEKITI WA CCM HALMASHAURI YA MANISPAA YA SONGEA NA UWENYEKITI WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU MKOA WA RUVUMA (FARU)

Diwani Mstaafu wa Kata ya Bombambili na Mwenyekiti  Mstaafu wa Chama cha Mpira wa miguu Halmashauri ya Manispaa ya Songea (Songea Mjini)SUFA Gorden Sanga (Sanga One) akizungumza jambo wakati wa ufungaji wa mashindano ya Sanga One Cup, kulia ni aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda ambaye kwa sasa ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa

SANGA ONE ni mdau mkubwa wa michezo mkoa wa Ruvuma na Mwanasiasa mwenye hekima, busara na ueledi mkubwa

MTANDAO HUU, www.stephanomango.blogspot.com, utaendelea kuwajulisha kila kinachoendelea kuhusu kampeni husika

Uchaguzi unaweza kufanyika mwezi wa 9, 2012 wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Ruvuma( FARU)

Uchaguzi Ccm fomu zinatolewa mwezi wa 8 tarehe 2,2012


Sunday, July 15, 2012

UZINDUZI WA WIMBO WA SHETANI AMESHINDWA YA KWAYA YA MTAKATIFU PAULO MTUME PAROKIA YA SONGEA MJINI WAFANA

 Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya uzinduzi wa ALBAMU ya SHETANI AMESHINDWA, Diwani wa Kata ya Litisha Jumann Nyingo akimkaribisha mgeni rasmi katika sherehe iliyofanyika leo mchana katika ukumbi wa Centenary
Kiongozi wa wanakaya akisoma risala kwa niaba ya wanakwaya ya mtakatifu Paulo

HABARI KAMILI INAFUATA

KUTEKWA,KUTESWA KWA ULIMBOKA LAZIMA MTU AWAJIBISHWE

 
       Na Padri Privatus Karugendo

HATA kama tumetangaziwa kwamba aliyemteka na kumtesa Dk. Stephen Ulimboka alitoka nje ya nchi, imetajwa Kenya, ina maana itawaponya baadhi ya watu hapa nchini kuwajibika kwa tukio hilo?
Vyovyote vile ni lazima mtu au watu wawajibishwe! Uzembe unajionyesha wazi wazi. Bila kuziba ufa huu, tutalazimishwa kujenga ukuta!
Kama kikundi cha watu wabaya kutoka nje wanaweza kuingia ndani ya nchi bila kutambuliwa na kutekeleza kazi yao na kuondoka bila ya kukamatwa, mpaka wao waamue kwenda kanisani kuungama, ulinzi wa taifa letu si uko mashakani?
Zamu hii ametekwa Ulimboka, je kesho watu hawa wakiingia na mabomu na kuyatega sehemu mbali mbali si itakuwa hatari kwa taifa letu? Je polisi wanaotiliwa shaka kushiriki sakata zima la kumteka na kumtesa Ulimboka, wataweza kukwepa kuwajibika kwa vile mhusika mkuu amejitokeza?
Kwa maelezo ya Kamanda Kova, si kwamba mtu huyu (Aliyemteka na kumtesa Ulimboka) amekamatwa na Polisi, bali mtu mwenyewe alikwenda kanisani kuungama na “Mchungaji” akafanya kazi ya usalama wa taifa. Hadi hapo Polisi, hawawezi kukwepa kuwajibika! Wanashindwa kufanya kazi yao ya upelelezi hadi wasaidiwe na “Mchungaji”?
Ni bahati mbaya kwamba Kamanda Kova, hakutaja kanisa ambalo mtu huyo alikwenda kuungama. Tungependa kulijua kanisa hilo na mchungaji huyo. Tujuavyo sisi ni kwamba maungamo ni “siri” kati ya anayeungama na anayeungamisha.
Na kamwe, hata kama ni chini ya tishio la kupoteza maisha, mchungaji au padri, anakatazwa kutoa siri ya maungamo. Kutoa siri ya maungamo ni dhambi ya mauti na haina msamaha popote labda kwa Mungu Mwenyewe.
“Usiri” huu wa maungamo ndo uliwajengea watu imani ya kuendelea kukumbatia mfumo huu wa kutubu dhambi.
Mtu anataja dhambi zake, anasafishwa na kuendelea na maisha. Nje ya imani, huu ni mfumo mbaya kabisa; mtu anaweza kuendelea kutenda dhambi na kuwanyanyasa wengine kwa vile anajua kuna “mchungaji” wa kusafisha dhambi zake.
Ni mfumo wa mtu kuufungua mdomo wake (kusema yote machafu) na kuufunga mdomo wa “mchungaji”. Kama wachungaji na mapadri wangejenga utamaduni wa kuzitangaza siri za maungamo, basi mfumo huu ungekufa zamani sana.
Sasa huyu “mchungaji” aliyeamua kutoa siri za maungamo, na kuamua kufanya kazi na polisi ni nani? Huyu amesoma chuo gani cha teolojia? Au ni uchungaji wa kujipachika? Mchungaji mchana na usiku ni Polisi? Sijasema alichokifanya ni kibaya kwa taifa letu; sijasema amekosea kushiriki kazi ya ulinzi na usalama wa taifa letu; sijasema amekosea kumfichua huyu mtu aliyetenda unyama wa kumteka na kumtesa Dk. Ulimboka.
Sote tumechukia na kuguswa na tukio hili na tungependa kumfahamu aliyetenda hivi na ni kwa nini? Hoja hapa ni namna mchungaji huyu alivyoshiriki.
Mchungaji huyu anataka tuamini kwamba makanisa ni usalama wa taifa? Kwamba makanisa yanafanya kazi na serikali? Waislamu wamekuwa wakipiga kelele nyingi kwamba serikali inapendelea wakristu na kwamba makanisa yamekuwa yakifanya kazi kwa karibu sana na serikali ya Tanzania.
Tumekuwa tukilipinga jambo hili kwa nguvu zote, lakini sasa baada ya Kamanda Kova, kutangaza kwamba mtu aliyemteka na kumtesa Ulimboka, ameibukia kanisani kwa njia ya maungamo, ni lazima tushawishike kwamba madai ya Waislamu yana ukweli fulani? Je, mchungaji huyu ametoa hili la Ulimboka tu, au anatoa mengine? Ushawishi huu wa kanisa kufanya kazi kwa karibu na polisi, unaishia hapo au unaendelea? Je “Mchungaji” huyu anashirikiana na polisi tu au ushawishi wake unaendelea kwenye idara nyingine za serikali? Tuna haki ya kujua, maana kama Kamanda Kova, ameamua kulifichua hili ni lazima aliweke wazi! Vinginevyo ni kuleta vurugu na kuvuruga amani ya watanzania.
Inawezekana kabisa kwa kutaka kujikosha, Polisi wanatuingiza kwenye matatizo mengine makubwa: Tutaanza kuhoji umakini wa polisi wetu, tutaanza kuhoji kwa nguvu zote uhusiano wa serikali na kanisa na wenye imani zao wataanza kuhoji uadilifu wa wachungaji na mapadri juu ya siri za kitubio.
Lakini pia kuna hili tatizo kubwa la kufunika mambo ambayo kesho na keshokutwa yatafumuka na kuliingiza taifa kwenye majanga makubwa.
Kwa kumkamata mtuhumiwa huyo kutoka Kenya, na kama alivyoeleza Kamanda Kova kwamba atafunguliwa kesi; suala la Ulimboka, litakuwa halijadiliwi tena, kwani tutaambiwa kwamba liko mahakamani. Utamaduni wa mahakama zetu, kesi inaweza kwenda zaidi ya miaka mitatu; suala kama hili la Ulimboka, ambalo limegusa hisia za watu wengi na zaidi vijana wa nchi hii, kulifunika na kuzuia mjadala kwa kisingizio cha kesi kuwa mahakamani ni kuchokoza mzinga wa nyuki.
Na kuna tatizo jingine la kuleta mahusiano mabaya kati ya nchi na nchi. Tunaweza kuanza kuinyoshea Kenya kidole kwa kutuingizia makundi ya majambazi ya kuwateka na kuwatesa. Hata Kenya, wanaweza kuja juu kwa kuitumia nchi yao kuficha madhambi ya baadhi ya watu wetu.
Utamaduni huu wa kuitumia Mahakama kama kinga ya maovu, umeanza hivi karibuni nchi yetu ilipotumbukia kwenye dimbwi la mambo ya ovyo kama vile ufisadi na uporaji wa rasilimali za taifa. Hadi sasa mambo mengi yamefunikwa kwa kisingizio cha kesi kuwa mahakamani. Serikali inaposhikwa pabaya inakimbilia mahakamani. Suala likishafikishwa mahakamani, halijadiliwi tena bungeni, kwenye jamii na kwenye vyombo vya habari.
Njia pekee ya kuwanyamazisha watu, kuwazuia watu kutetea haki zao za msingi ni kukimbilia mahakamani. Ile dhana nzima ya Mahakama kama chombo cha kutetea na kutoa haki sawa kwa kila mwananchi imeanza kupotea. Kinachojitokeza ni Mahakama kugeuka kuwa chombo kandamizi na kulinda maslahi ya wakubwa, serikali na watu wenye fedha.
Mbali na kutumia maungamo kumfichua mtu aliyemteka na kumtesa Dk. Ulimboka, na mpango mzima wa kutaka kuitumia mahakama kuzuia mjadala juu ya sakata hili, kuna jambo jingine la kushangaza:
Katika hali ya kawaida, tulitegemea mtu aliyetoka nje ya nchi kuja kutekeleza kazi ya “Mauaji”, angetoroka na kurudi nchini kwao mara baada ya kumaliza kazi yake. Sasa huyu “Mtu wa Ulimboka”, baada ya kazi yake, ambayo aliifanya na kuimaliza bila kukamatwa, akaendelea kuishi Tanzania, bila wasi wasi wowote na bila Polisi kutambua, mpaka Roho wa Bwana alipomwingia akaamua kwenda kanisani kwa mchungaji kuungama?
Na je, aliungama kwa lengo la kusafishwa dhambi zake ili aendelee kutenda dhambi nyingine? Ili aendelee kuwateka na kuwatesa watu wengine? Au aliungama kwa kuchukia dhambi aliyoifanya? Na kama ni hivyo si angejisalimisha moja kwa moja kwa polisi na kwa kufuata mantiki, angejisalimisha nyumbani kwao Kenya.
Kilio cha madaktari na watetezi wa haki za binadamu ni kwamba suala la kutekwa na kuteswa kwa Ulimboka liundiwe tume huru. Tume ambayo badala ya kukimbilia kanisani na nje ya nchi na mahakamani itachunguza kiini cha tukio lenyewe hapa hapa nchini. Kwa vile suala hili linaelekea kuwagusa watu wengi na kuibua dalili za kutoaminiana na kulituhumu moja kwa moja Jeshi la Polisi, hekima pekee ni kuliundia tume huru. Vinginevyo tutaendelea kusikia “hadithi” ambazo hazitatusaidia kuleta maelewano.
Vyovyote vile kwa suala la Kutekwa na kuteswa kwa Dk. Ulimboka, ni lazima mtu awajibishwe, vinginevyo ni kuendelea kuwalazimisha watu kujichukulia sheria mkononi!

Friday, July 13, 2012

ALAT RUVUMA YAWEKA AZIMIO LA KILIMO CHA MAZAO MBADALA

Na Steven Agustino,Tunduru

KIKAO cha jumuiya za serikali za mitaa (ALAT) mkoa wa Ruvuma kimeazimia kuanzisha na kuendeleza kilimo cha mazao mbadala katika mkoa wa Ruvuma ambayo ni pamoja na korosho,karanga,mihogo na kahawa badala ya kuendeleza zaidi kilimo cha mahindi pekee.

Azimio hilo limepitishwa na wajumbe wa jumuiya hiyo katika mkutano mkuu uliofanyika wilayani Tunduru ambao ulitanguliwa na ziara ya mafunzo kwa wajumbe kutembelea kituo cha utafiti wa kilimo cha Naliendele kilichopo mkoani Mtwara zikiwa ni juhudi za wajumbe hao
kupata ufahamu zaidi wa shughuli za uzalishaji bora wa zao la korosho.


Aidha wakiwa katika ziara hiyo ya mafunzo katika kituo hicho wajumbe hao pamoja na kujifunza namna ya uzalishaji bora wa korosho pia walielimishwa namna ya kulima kilimo bora cha karanga,Ufuta, na muhogo mazao ambayo yanastawi pia mkoani Ruvuma ambako kunalimwa mahindi kwa kiasi kikubwa na kahawa ambalo ni zao la biashara linalolimwa zaidi katika wilaya ya Mbinga nalo limewekewa mikakati zaidi ya kuhakikisha wilaya zote za mkoa wa Ruvuma zinalima.

Akizungumza wakati akitoa mafunzo hayo kwa wajumbe Afisa utafiti wa kilimo wa kituo cha Naliendele Ramadhan Bashiru alisema kuwa uamuzi wa wajumbe hao kutoka mkoani Ruvuma kufika katika kituo hicho kwa ajili ya kujifunza ni ishara kuwa wamedhamiria kuinua kiwango cha wakulima wa mkoa wa Ruvuma kwani watalima kilimo bora chenye tija kwao na taifa kwa ujumla.

 Bashiru aliwaeleza wajumbe hao kuwa mbali na kituo hicho kufanya utafiti wa mazao mbali mbali pia kimekuwa kikitoa mafunzo kwa wakulima kulingana na mahitaji yao ingawa wananchi wanaokizunguka kituo hicho bado hawajaonyesha mwamko chanya wa kutaka kujifunza kilimo bora na uzalishaji bora wa mazao mbali mbali ambayo ni rahisi kwa wakulima wadogo wadogo.

Aidha Bashiru alitoa wito kwa mikoa mingine kuiga mfano wa mkoa wa Ruvuma kufika kwenye kituo hicho kwa ajili ya kujifunza na kupata mbegu bora za mazao mbali mbali ili kutekeleza kauli mbiu ya kilimo kwa vitendo kwa sababu kilimo ndiyo uti wa mgongo wa taifa.

Awali akifungua mkutano huo  Mkuu wa Wilaya ya Tunduru  Bakari Nalicho pamoja na kutoa hamasa kwa viongozi wa Jumuiya hiyo kuhamasisha uzalishaji wa mazao hayo kwa wakulima wao pia aliwaomba viongozi wa Bodi ya Korosho na Mfuko unaosimamia uzalishaji wa zao hilo
kuhakikisha wanatafuta soko la uhakika na kuuza korosho zilizo kwama katika maghala ya vyama vya ushirika Wilayani humo pamoja na kujenga tabia ya kupeleka madawa ya kupulizi mikorosho ya wakulima kwa wakati.

Aidha DC, Nalicho aliwahamasisha wajumbe hao kupia halmashauri zao kuhamasisha wananchi kukopa matrekta yaliyoletwa Mkoani humo, kutoa elimu  juu ya ukusanyaji wa kodi kutoka kwa wafanyabiashara, kubuni mbinu mpya za ukusanyaji wa mapato kutoka katika vyazo visivyo wa kwaza wananchi na akatumia nafasi hiyo kuwakumbusha watendaji katika halmashauri hizo kusimamia mapato hayo ili yatumike katika uboreshaji wa maisha ya wananchi kupitia huduma muhimu za Maji,Afya, Elimu,Kilimo kwa maana ya Pembejeo na miradi ya ufugaji.

Akifunga mkutano huo Mwenyekiti wa ALAT mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho aliwataka wajumbe waliofika kwenye kituo hicho kuwa mabalozi kwa kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kuwatumia wataalamu wa kilimo waliopo katika halmashauri zao ili kuufanya mkoa wa Ruvuma kuwa na mazao mbali mbali ya biashara na chakula.

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Charles Mhagama alisema kuwa ziara hiyo ya wajumbe kwenye kituo hicho ni chachu kubwa ya kuufanya mkoa wa Ruvuma kuwa kioo cha uzalishaji wa mazao hayo ambayo yakizalishwa kwa kuzingatia utaalamu yatainua uchumi wa mkulima na taifa kwa ujumla.
Mwisho.

Thursday, July 12, 2012

WAFANYAKAZI WA TANESCO LAWAMANI TUNDURU

Na Steven Augustino, Tunduru

WAFANYAKAZI wa Shirika la ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma wametuhumiwa kuwa wahujumu na wachakachuaji wa kubwa na wauzaji wa mafuta ya kuendeshea mitambo ya umeme ya shirika hilo.

Hayo yamesemwa na baadhi ya  wakazi wa Mji wa Tunduru kufuatia kuwepo na kujengeka kwa mazoea ya watumishi wa Shirika hilo kuuza mafuta hayo huku viongozi wao wakiwa wanawakingia vifua kwa visingizio kuwa mafuta yaliyo uzwa ni miongoni mwa mafuta yaliyotumika yaani machafu.
Baadhi ya wananchi hao ambao waliomba wasitajwe majina yao gazetini walidai kuwa wamelazimika kutoa kilio chao cha kuiomba serikali iwasaidie kufuatilia kwa karibu suala hilo ili kuwaondolea adha hiyo.
Walisema kufuatia kukosekana kwa huduma hiyo kumesababisha kuwepo kwa ukubwa na gharama za maisha kutokana na bidhaa zote kupanda bei hasa vyakula ambako chanzo chake kimekuwa kikisababishwa na kuzimwa kwa Umeme mara kwa mara.

Aidha pamoja na mambo mengine zikiwemo kero tofauti zinazo sababishwa na uzimwaji wa huduma hiyo ukiwemo mdororo wa utoaji wa huduma katika huduma za Serikali Gazeti hili lilishuhudia kupanda kwa bei za unga na kufikia Shilingi 1500 kwa kilo moja kutoka Shikingi 600, mchele Tsh.2200 kutoka tsh.1500.

Alipotakiwa kuzungumzia kero hiyo Kaimu Meneja wa Tanesco Wilayani humo Bosco Milumbe mbali na kukiri kuwepo kwa hali ya kutatanisha juu ya upatikanaji wa nishati hiyo alisema kuwa chanzo ni ukosefu wa mafuta ya kuendeshea mitambo hiyo.

Alisema hata hivyo wao hawana mamlaka ya kulishughulikia na kwamba wao hupokea mafuta baada ya kuandaliwa na Makao makuu ya Shirika hilo yaliyopo Jijini Dar Es Salaam ambao ndio hufanywa shughuli zote za manunuzi ya mafuta
Kuhusu tuhuma za watumishi kuchakachua mafuta alisema kuwa madai hayo siyo ya kweli akianisha kuwa Shirika hilo hupokea lita 30,000 za mafuta kila gari linapo fika na kwamba matumizi ya mitambo yake kwa siku ni wastani wa lita 3500 hadi lita 3600 ambapo hutakiwa kutumika wastani wa siku 10 tu.

Hata hivyo Milumbe alimaliza kwa kusema kuwa Shirika hilo limepanga kuwasha Umeme  kesho  kwa masaa mawili tu na kumaliza stoku ya mafuta lita 10.000 waliyokopa kutoka kwa mfanyabiashara binafsi kwa ajili ya kutoa nafasi kwa wakazi wa mji huo kusaga na kukoboa nafaka zao na kwamba baada ya hapo huduma hiyo haitapatikana klwa muda usiofahamika.
Juhudi za kumtafuta Meneja wa Tanesco Kanda ya Nyanda za juu Kusini Eng. Boniface Njombe ili kuzungumzia hatima ya nishati hiyo kwa wakazi wa wilaya hiyo  hazikufanikiwa kutokana na simu zake  kutopatikana
MWISHO

Tuesday, July 10, 2012

MADAKTARI; KUNA KIKOSI CHA KUMUUA ULIMBOKA


• Wasema Ulimboka alimtambua afisa aliyemteka

Na Irene Mark


BAADA ya kutekwa, kupigwa na kutelekezwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka, viongozi wa vyama vya madaktari wamedai maisha yao yako hatari hali iliyowalazimu kuomba ulinzi Umoja wa Mataifa na makundi mbalimbali ya kutetea haki za binadamu.
Madaktari hao wamesema hawana imani na maofisa wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete, wanaotishia usalama wa maisha yao kwa namna tofauti hasa baada ya tukio la Dk. Ulimboka la Juni 27 mwaka huu.
Barua ya madaktari hao kwenda kwa Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa hapa nchini ya Julai 7, 2012, madaktari wameeleza namna maofisa wa serikali wanavyotishia usalama wa maisha yao hao na kuwaeleza namna walivyowatuma wenzao Afrika Kusini kuhakikisha Dk. Ulimboka anapoteza maisha.
Pia barua hiyo yenye kumb. Na.MAT/UN/SU/01, imetumwa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Namala Mkopi, Shirika la Human Rights Watch na Amnesty International.
Taasisi nyingine zilizopelekewa nakala ya barua hiyo ambayo Tanzania Daima ina nakala yake ni Kituo cha Haki za Binaadam (LHRC), SIKIKA Tanzania, Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA).
“Hata hivyo, watu kutoka serikalini waliihakikishia MAT kwamba timu ya wasaidizi wao imeenda Afrika Kusini kuhakikisha Dk. Ulimboka anarudi nyumbani akiwa maiti.
“Kwa kuongezea hapo, viongozi wa MAT tunapokea vitisho kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwenye simu na wakati mwingine tunapigiwa simu na namba zisizopatikana tukitishiwa maisha,” ilieleza sehemu ya barua hiyo iliyosainiwa na Dk. Mkopi.
Aidha, barua hiyo imeuomba Umoja wa Mataifa kuwahakikishia madaktari usalama wa Dk. Ulimboka kwenye hospitali anayotibiwa na kuwalinda madaktari wengine hasa viongozi wa vyama na jumuiya ya madaktari.
Kadhalika barua hiyo imeuomba umoja huo kuushauri mfumo wa sheria za Tanzania kutokubali kutumika kwa faida za kisiasa na kulitaka Bunge kubaki na majukumu yake ya Kikatiba ya kuiwajibisha serikali kwa vifo vya watu kama matokeo ya mgomo unaoendelea.
Katika barua hiyo madaktari hao wameeleza namna Dk. Ulimboka alivyoteswa na watekaji hao kwa kung’olewa kucha, meno na kuumizwa sehemu mbalimbali za mwili wake huku akimtambua ACP Msangi kuwa miongoni mwa watekaji hao.
Walieleza namna polisi wa kituo cha Bunju walivyoshindwa kuwapa ushirikiano kwa haraka ili kumuwahisha majeruhi huyo kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili na jinsi walivyokuwa wakizuiwa na magari ya askari kwa lengo la kumchelewesha asipate huduma za kitabibu.
“Akiwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI), Dk. Ulimboka licha ya maumivu makali aliyokuwa nayo alimtambua ACP Msangi kuwa ni miongoni mwa waliomteka na kumtesa,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo na kubainisha kwamba ACP Msangi ni kiongozi wa tume iliyoundwa kuchunguza suala hilo.
Ikulu yasononesha viongozi wa dini
Baadhi ya viongozi wa dini waliojitolea kusuluhisha mgogoro baina ya madaktari na serikali, wameeleza kusononeshwa na jibu la Ikulu la kukataa kuonana nao huku wakibainisha kwamba jukumu lao kubwa ni kuhakikisha amani inatawala.
Akizungumza kwa niaba ya viongozi hao, Msemaji wa Kamati ya Vijana wa Baraza Kuu la Waislamu (Bakwata), Said Mwaipopo, alisema licha ya jibu hilo wanaendeleza juhudi za kuhakikisha mgogoro huo unamalizika kwa njia za amani.
“Hatukatishwi tamaa na jibu la Ikulu kazi yetu kubwa ni kuhakikisha amani inakuwepo… ndiyo maana jana tulikutana na viongozi wa madaktari tukawaeleza kwamba njia bora ya kufanya ni kuandika barua na kuieleza jamii kupitia vyombo vya habari kwamba wanaomba msamaha kwa Rais, wananchi na serikali.
“Kitu kinachotusikitisha vijana wale walikataa ushauri wetu tukagundua kwamba inawezekana nyuma yao kuna siasa zinaingia,” alisema Mwaipopo.
Akijibu suala hilo Katibu wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Edwin Chitage, alikiri kukutana na viongozi hao jana na kueleza kwamba walichokubaliana ni kusubiri barua rasmi kutoka Ikulu ikiwataka madaktari hao kuandika barua kuomba msamaha kwa Rais, Watanzania na serikali.
“Ni kweli lakini alichokisema Mwaipopo ni kwamba alipigiwa simu na watu waliodai kwamba wako Ikulu, hivyo wakawaambia viongozi hao wa dini watuambie madaktari tuandike barua ya kuomba msamaha.Tunaomba msamaha kwa nini,” alihoji.
Dk. Mkopi aliongeza kuwa madai yao hayajatekelezwa licha ya kuwepo kwa muda mrefu tangu mwaka 2005 na kwamba kama serikali haina dhamira ya kweli ya kumaliza mgogoro huo utaendelea hata baada ya miaka 10.
Kukutana na Dk. Mwinyi
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Dk. Godbless Chale alisema walipokea simu kutoka kwa Waziri mpya ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi ikiwataka kwenda kumweleza sababu za mgomo wao.
“Kweli Dk. Mwinyi alitupigia simu akatuita alisema hajui madai yetu hivyo twende tukamweleze hivi kwa akili ya kawaida kweli ofisi inakosa nyaraka za kumbukumbu?!! Tunaona hayupo ‘serious’.
“Kabla hajatuita wizara yake iliteua wajumbe watatu Naibu Katibu Mkuu, Naibu Mganga Mkuu Dk. Donald Mbando na Mkurugenzi wa Rasilimali tukaketi nao kuwaeleza siku chache baadaye waziri anasema hajui madai yetu hii tumeona ni ‘kamchezo’ wanataka kutufanyia,” alisema Dk. Godbless.