About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Friday, July 26, 2013

WAFANYABIASHARA SOKO KUU SONGEA WAPINGA MPANGO WA MANISPAA

Kulia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabiashara wa Masoko Manispaa ya Songea(UWABIMASO) Karim Matumla akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Uwabimaso Leonard Chiunga wakifuatilia hoja mbalimbali kutoka kwa wanachama wa Uwabimaso
Wanachama wa Uwabimaso wakifuatilia kwa makini kikao hicho chenye lengo la kupinga ongezeko la kodi la Vibanda vya Soko Kuu na Kupinga tangazo la Zabuni lililotangazwa hivi karibuni


   
Na Stephano Mango, Songea
          
WAFANYABIASHARA katika Soko Kuu la Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wamepinga ongezeko la pango kwa asilimia 100 na tangazo la Zabuni  la ukodishaji wa Vibanda hivyo lililotolewa na Halmashauri hiyo hivi karibuni
Akitoa maazimio ya kikao cha Umoja wa Wafanyabiashara Masoko ya Manispaa ya Songea(UWABIMASO) kilichofanyika jana mjini hapa  kwenye ukumbi wa Saccos ya Walimu Songea Vijijini Mwenyekiti wa Uwabimaso Karim Matumla alisema kuwa wafanyabiashara wamepinga kwa nguvu zote mpango wa kifisadi ulioletwa na viongozi wabovu wa  Halmashauri hiyo wa kuongeza kiwango cha kodi kwa asilimia 100 na tangazo la Zabuni
Matumla alisema kuwa mipango ya Halmashauri kuhusu Masoko yake haina ushirikishwaji wa pamoja kutoka pande zote mbili kwa maana Wafanyabiashara(Uwabimaso)  na Halmashauri hiyo hali inayosababisha migogoro mara kwa mara
Alisema kuwa kwa muda mfupi tumepokea barua mbili zenye malengo tofauti ndani ya kipindi cha mwezi mmoja jambo ambalo linaleta mashaka sana katika dhamira za viongozi wa Halmashauri hiyo yenye mipango dhalimu
Alisema kuwa kitendo cha Mkurugenzi kutoheshimu wala kutimiza makubaliano yetu yaliyomtaka kuondoa kero zinazowapata wafanyabiashara katika Masoko ya Halmashauri ni kitendo cha dharau kwa wafanyabiashara ambao wanachangia pato la Halmashauri
“ Tulimtaka Mkurugenzi katika vikao vyetu kuondoa mashimo na kuboresha mifereji na miundombinu mingine ndani ya Masoko, wauza matunda watafutiwe eneo maalumu la biashara yao kwani kwa sasa wanazuia mizigo kuingia ndani na wateja wanapata kero ya kuhudumiwa, unyanyasaji unaofanywa na Afisa Masoko uachwe na pia tulimuomba atukutanishe na Viongozi wa Halmashauri ili tutoe maoni yetu, lakini yeye amekaidi”alisema Matumla
Alisema kuwa mei 22 mwaka huu Halmashauri ilileta barua Uwabimaso ikitoa taarifa ya ongezeko la kodi ya pango kwa asilimia 80 kulingana na ukubwa wa chumba cha biashara kuanzia julai 1 mwaka huu, kabla hatujaanza kuitekeleza, julai 9 mwaka huu wanaleta barua na wanatangaza Zabuni ya ukodishaji wa vibanda hivyo, baada ya Uwabimaso kupinga ongezeko la pango la asilimia 80
Alieleza kuwa kumekuwepo na mgongano wa kimaagizo kutoka katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kitendo ambacho kinaibua maswali mengi, hivyo Uwabimaso imeamua kwenda kwa Mwanasheria ili aweke zuio la mpango wa upandishaji wa Kodi na Utangazaji wa Zabuni yenye lengo la kuwaondoa wafanyabiashara wote wa maduka katika soko hilo
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Zakaria Nachoa alisema kuwa Halmashauri imekusudia kuongeza mapato yake kupitia miradi yake, hivyo mfanyabiashara ambaye hataki kuendana na utaratibu aache kibanda ili mfanyabiashara mwingine achukue
MWISHO