About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Tuesday, October 18, 2011

WANANCHI WAHOFIA AFYA ZAO KUTOKANA NA MAGHUBA MENGI KUZIDIWA UWEZO WA TAKATAKA

Na Thomas Komba,Songea
HALI ya usafi ambayo tulizoea kuiona katika Manispaa ya Songea  sasa imeanza kutoweka polepole hasa katika maeneo ya ghuba  za kuhifadhia takataka na mifereji ya maji katika baadhi ya barabara mjini hapa .
Uchunguzi wa kina ulifanywa  na mwandishi wa mtandao huu wa www.stephanomango.blogspot.com Thomas Komba amebaini kuwa kuna ghuba nne maeneo ya Mfaranyaki zimekuwa kero kwa wakazi ,pia ghuba hizo zina dalili zote za kuzalisha magonjwa ya kuambukiza  hasa kipindi  hiki tunapoelekea masika .
Baadhi ya wakazi wa eneo la makaburi ya wahindi mtaa wa Bikuli  wameulalamikia uongozi  wa serikali ya mtaa kupitia Mwenyekiti wao Laurent  Mbewe kuwa ghuba yao imezagaa takataka ambazo sasa zimekuwa ni karata kwa watoto wa  maeneo hayo .
Mkazi mmoja wa jirani kabisa na ghuba hilo Semeni Msafiri alisikika akisema “Sasa hii ni hatari mbona kipindupindu kitatuua kwani sasa ni wiki mbili (2) hazijazolewa  takataka mpaka  zinanuka ,Mvua zikija  hapatakalika “alimalizia Semeni
Wakazi wa eneo la Mkomi darajani nao wamelalamikia ghuba lao kwa kusema “Songea imeongoza kwa usafi mara tatu ,sasa kimetokea nini ,labda malumbano ya madiwani  yanapelekea hali hiyo”,eneo hilo ghuba lake limejaa na halijazolewa  muda mrefu .
Jambo la kusikitisha ni pale kituo cha Lizaboni pana kila aina biashara ya vyakula zikiwemo samaki na dagaa ,nyanya ,ndizi , na aina nyingine za matunda ,napo uchafu umejaa kwenye  ghuba hilo   kama kawaida ya ghuba zilizo tanguliwa kutajwa .
Mkazi mmoja wa  eneo la soko la Mfaranyaki alisikika akisema kuwa “Heri tupewe  kazi hiyo sisi na manispaa  itulipe kuliko hali hii.
Hali hii iko karibu maeneo  yote  ya katikati ya mji wa Songea ,ikiwemo  Bombambili ,Matarawe,Misufini ,Mahenge  ,Ruvuma na mtaa wa polisi kata ya mjini .
Katika kuelezea tatizo hilo wataalamu wa Afya  wamesema wanakumbana na changamoto  ya makisio pamoja uhaba na magari ya kuzolea takataka.
Aidha mvua iliyonyesha hivi karibuni mjini hapa ,tayari imeonyesha hali ya mji itakavyo kuwa mbaya barabara zake zisipo wekewa mifereji  ya maji  mapema  ,kwani kuna maeneo maji  yataingia kwenye makazi ya watu,mfano mzuri ni Majengo ,Mfaranyaki ,Makaburi ya wahindi ,Misufini ,Bombambili eneo la sokoni na eneo la Washingitone kuvukia  sekondari ya Muslimu,
Uchunguzi wa Jambo leo  unaendelea ili kubaini uongozi wa manispaa  Songea  unakalibiana vipi na  changamoto hizo .
Mwisho

UANDISHI WA HABARI NI TAALUMA KAMA ZILIVYO TAALUMA NYINGINE-MWAMBUNGU

Na Thomas Lipuka,Songea.
MKUU wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu amewaagiza waandishi wa habari ambao hawajajiunga na chama cha waandishi wa habari mkoani humo RPC  kujiunga mara moja ili kuwa na jukwaa la kuzungumzia matatizo yanayowakabili na kukuza taaluma yao.
Akifungua mkutano wa wadau wa habari uliyoandaliwa na RPC  na kufanyika hivi karibuni kwenye ukumbi wa Chama Cha Walimu Tanzania CWT mkoa wa Ruvuma
Mwambungu alisisitiza kuwa mwandishi wa habari ambaye hajajiunga na chama cha waandishi wa habari katika mkoa husika anajichelewesha katika kujenga umoja wa taaluma na ameshindwa kujitendea haki yeye mwenyewe.
Mwambungu alifafanua kuwa kazi ya uandishi wa habari ni ya kitaaluma kama zilivyo taaluma nyingine hivyo suala la maadili kwa wanahabari sharti lizingatiwe wakati wote  mwandishi anapofanya kazi yake.
“Maadili ya habari ndiyo yanayoongoza ,taaluma ya habari,maadili pia yanaongoza taaluma nyingine ,kwa mfano daktari hawezi kutoa siri ya mgonjwa kwa kusema mgonjwa wako atakufa leo au kesho’’,alisisitiza
Amewaasa waandishi wa habari kuacha tabia ya kuhatamia  au kuficha habari ambazo wananchi wangezipata,na kwamba  habari hiyo inaweza kutafuta mkondo mwingine wa kuwafikia wananchi.
Mwambungu aliwaagiza viongozi wa RPC kuweka vigezo vya kutambua nani aitwe mwandishi wa habari pamoja na sifa zake zikiwemo kiwango cha taaluma au elimu ya weledi huo.
Mwisho