Mhashamu Askofu Mkuu Norbert Mtega
Na Gideon Mwakanosya,Songea
WAUMINI wa Makanisa ndugu katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wanatarajia kufanya tamasha kubwa la uimbaji la Jubilei ya miaka 50 ya uhuru wa Taifa la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Oktoba 29 Mwaka huu ambapo mgeni rasmi kwenye tamasha hilo ni Waziri wa Habari utamaduni na michezo Dr. Emmanuel Nchimbi.
Akizungumza na mtandao wa www.stephanomango.blogspot.com jana ofisini kwake Katibu wa umoja wa Makanisa ndugu katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mackie Mguhi amesema kuwa tamasha hilo ambalo linatarajiwa kuhuzuliwa na mamia ya waumini wa Makanisa ndugu wakiwemo Askofu Mkuu wa Kanisa katoliki jimbo kuu la Songea Norbert Mtega, Askofu wa dayosisi wa Ruvuma kanisa la Angelikana Dr. Martenius Kapinga, Mkuu wa kanisa la kiinjili la kiliteli Tanzania (KKKT) Mchungaji Nashoni kikalawa Pamoja na mkuu wa mkoa wa Ruvuma Saidi Mwambungu Mguhi ameyataja Makanisa yanayeunda umoja huo ambao umeandaa tamasha kubwa ni kanisa katoliki Parokia za Songea,Mjimwema na Bombambili kanisa la kinjili la kiluteli Tanzania (KKKT) Usharika na Songea mjini na Msamala kanisa la Anglikana Songea Mjini pamoja na kanisa la Moraviani Tanzania ushirika wa Songea.
Ameeleza zaidi kuwa Tamasha hilo litafanyika siku ya jumamosi oktoba 29 mwaka huu katika uwanja wa michezo wa mpira wa miguu wa Majimaji ambalo litatanguliwa na maandamano makubwa ya waumini wa Makanisa ndugu yatakayoanzia katika kanisa la Luthelani Songea Mjini hadi uwanja wa Majimaji.
Amesema kuwa lengo la tamasha hilo ni kuonyesha furaha kubwa kwa waumini wa Makanisa ndugu katika manispaa ya Songea kwa jubilee ya nchi ya Tanzania Kwa vitendo pili kuendelea kumshukuru mungu na kumuomba kwa upendo ,Amani na uvumilivu aliyo ijalia nchi ya Tanzania pamoja na viongozi na wananchi kwa ujumla .
Amebainisha zaidi kuwa katika tamasha hilo pia litaudhuliwa na wanafunzi wa chuo cha elimu ya Taifa Songea , Shule ya wasichana na Wavulana Songea na kwaya zaidi ya ishirini zimesibitisha kushiriki kwenye tamasha hili na viongozi wa makanisa hayo wanatarajiwa kuongoza ibada ya maalumu ya kuiombea amani kwa mwenyezi mungu kwani Tanzania toka ipate uhuru hawajawai kupata misuko suko ya aina yoyote tofauti na nchi zingine zikiwemo baadhi ya nchi zilizo pakana na Tanzania ambazo wananchi wake wakipata shida kutokana na vita.