About


Karibu ujiunge na chuo cha kisasa cha Easy Tech.Computer kwa mafanikio yako,Walimu waliobobea katika fani hiyo wanapatikana chuoni hapo

elimak

elimak

Pages - Menu

Friday, March 2, 2012

WANANCHI WA KIHAGARA WAIOMBA WIZARA YA AFYA IWASAIDIA KUJENGA KITUO CHA AFYA

Na Gideoni Mwakonosya , Songea
WANANCHI wa kata ya Kihagara Wilayani Nyasa Mkoa wa Ruvuma wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuona umuhimu wa kuwasaidia shughuli za ujenzi wa kituo cha afya ambapo kwa awamu ya awali wamefyatua tofari za kutosha na ambazo zimesha chomwa na eneo linalotarajia kujengwa kituo hicho tayari mawe na mchanga wa kujengea ulishapelekwa.
Akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara Kaimu Afisa Mtendaji wa kata ya Kihagara Jackobo Yela alisema kuwa januari mwaka jana ajenda ya ujenzi wa kituo cha afya cha kata ya Kihagara ilipitishwa katika kikao cha Kamati ya Maendeleo ya Kata hiyo na kuadhimia kufyatua tofari na kuzichoma haraka iwezekanavyo .
Alieleza zaidi kuwa tofari 375,000 zilifyatuliwa na kuchomwa kati ya tofari 500,000 zilikuwa zikihitajika na Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga iliombwa na ikaridhia kuanza ujenzi wa kituo mara moja kwa kuchimba msingi na kupeleka Tani 210 za mawe na Tani 112 za mchanga kwenye eneo hilo.
 Alisema kuwa wananchi wa vijiji vya Tumbi, Ngehe, Mango, Songambele  na Kihagara wameiomba Serikali uwezekano wa kuwasaidia ujenzi wa kituo hicho kwani wakazi wa maeneo hayo wamekuwa wakitegemea kupata matibabu katika Hospitari za Liuli, Litembo na Mbinga mjini amabako ni mbali sasa na kata hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi Kapteni John Komba baada ya kupata taarifa hiyo aliamua kutoa fedha milioni tatu ili kusaidia ujezi wa kituo hicho ambacho alieleza kuwa ujenzi wa kituo hicho ukikamilia utakuwa ni msaada mkubwa kwa wakazi wa maeneo ya mwambao wa Ziwa Nyasa .
Aliwahimiza wananchi wa Kata hiyo kuhakikisha kuwa shughuli za ujenzi wa kiutuo hicho zinakamilika haraka iwezekanavyo ili kuondokana na tatizo lililopo la kwenda mbali kupata matibabu jambo ambalo limekuwa ni kero kubwa.
Mwisho.